Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, April 23, 2015

NANI KAMA MAMA-64


‘Huyo mama ni nani, na anatokea wapi….?’ Akauliza shemeji mtu.

‘Huyu mama mnamfahamu sana…’akasema mdogo mtu na kuwafanya hao wanandoa wawili kuangaliana.

‘Tunamfahamu kwa vipi, ..?’ wakauliza

‘Hamtaamini nikiwaambia kuwa huyu mama mliishi naye kwenye nyumba moja, na huyo huyo ndiye kaja hapa kudai kuwa mtoto wake nimemchukua mimi..’akasema

‘Mama gani huyo..?’ akaulizwa

‘Yule mama wa mitaani,..’akasema mdogo mtu, na wote wakamtolea macho kila mmoja akionyesha uso uliojaa maulizo

***********

‘Mama wa mitaani, ni mama gani huyo….?’ Shemeji mtu akataka kuuliza lakini akakatisha, kuonyesha kakumbuka jambo, akageuka kumuangalia mkewe lakini mkewe akatangulia kusema;

‘Mimi sijaelewa ni mama gani huyo?’ akauliza dada mtu naye akigeuka kumuangalia mumewe, na akawa kakumbuka jambo, na kugeuka kumuangalia mdogo wake, na mdogo wake akaona asipoteze muda, akasema;

‘Ni yule mama mliyekuwa mkiishi naye, aliyekuwa akiitwa mama wa mitaani, akaja kuitwa mama wa mkono wa baraka, ambaye aliletwa hapa kutibiwa kutoka huko kwenu akiwa kaungua…ndiye huyo anayedai kuwa mimi nimemchukua mtoto wake…sasa mtoto huyo ni nani, kama sio huyo mtoto wenu….’ akasema nesi

Nesi akatega sikio akahisi kama kuna mtu alikuwa anakuja hapo ofisini kwake, lakini hajasikia mtu akigonga, akataka kusimama kwenda kufungua mlango na kuona ni nani kasimama hapo, lakini akasita.

Kwa muda huo dada mtu alikuwa katoa macho, akamwangalia mume wake , na mume wake naye alibakia mdomo wazi, na nesi akanyamaza kwa muda akitafakari nini cha kuwaambia zaidi hawa watu ili wamuelewe vyema,na huku akijiuliza ni nani kaja hapo mlangoni na hajagongwa au kuonyesha kuwa kaondoka.

Shemeji mtu ambaye alikuwa kakaa sasa akasimama, na kuanza kukuna kichwa mfufululizo, akainama akiwaza jambo, halafu akainua kichwa na kumuangalia mkewe, akatembea hatua moja mbele, halafu akasimama…

Mkewe ambaye alikuwa kasimama, sasa akarudi kwenye kiti alichokuwa kakaa mwanzoni, na kukaa, na hakusema neno kwa muda huo, akainamisha kichwa chini, aliona mwili umemuishia nguvu, akawa katulia vile vile akiwa kainamisha kichwa  chini, kama anawaza jambo…

Mume mtu akasogea hadi pale alipokaa mkewe, akasema;

‘Twende zetu….’hiyo sauti ikawafanya wote sasa wajitambue, mke mtu akainua kichwa kumuangalai mumewe, na mumewe, akawa kageuka kumuangalia nesi na nesi  aliyekuwa katulia, akiangalia ile hali, akijua sasa keshawapa nafasi ya kuliwaza hilo akataka kusema neno,.lakini sauti ya shemeji yake ikasikika ikisema….

‘Nimesema inuka tuondoke..’akasema mume mtu akiwa kabadilika sura, utafikiri kala pilipili.

Nesi akaona asipoteze muda, akasimama na kuelekea mlangoni akafungua mlango na kuangalia nje, hakuona mtu, akaangza huku na kule hakuona mtu, lakini alikuwa na uhakika kuwa kuna mtu alikuwa anakuja hapo,na baadaye kukawa kimia, alipotosheka kuwa hakuna mtu akaufunga huo mlnago na kurudi pale alipokua amekaa akwa anawaangalia ndugu zake hao.

‘Twende wapi mume wangu, ngoja tusikilize kinachoendelea maana mpaka sasa sijaelewa kitu…na tukiondoka hapa tutakuja kusema nini, tutajua ni kitu gani kimeendelea huku, je…tufanyeje, ngoja tuyamalize hapa hapa tujue moja….’akasema mkewe na kukatisha maneno kwani alihisi kuumia pale aliposhika mumewe kwenye bega.

‘Aaaah, unaniumiza..’akalalama mke mtu.

Mume mtu sasa akawa anatetemeka mwili mzima kwa hasira, na kila akitaka kusema neno anaishia kushikwa na kigugumizi, na mkono uliokuwa umeshika bega la mkewe ukawa unaliminya lile bega na kumfanya mkewe ahisi maumivu na ndio akasema;

‘Aaah unaniumiza…’ na kuutoa mkono wa mumewe kwa nguvu , na mkono ulivyokuwa umeganda kwenye bega ilikuwa kama sumaku imenasa kwenye chuma..

 Hali hii ilimshitua sana mke wake ambaye licha ya kushikwa na mshangao, lakini aliponuona mume wake akibadilika ghafla, mawazo yake na hisia zake zikamlenga mume wake, kwa wasi wasi kuwa ana tatizo jingine la kiafya, ambalo linahitaji msaada!

‘Vipi baba nanihii…baba ….’ Akauliza mkewe huku akisita kumtaja mwanae, kitu ambacho sio kawaida yao, kwani nyumbani, walikuwa wakiitana kwa jina la mtoto,  mama nanihii au baba nanihii ….

Nesi akaiona hiyo hali, akajua kuwa shemeji yake kapatwa na jambo na asipofanya kitu , shemeji yake huyo anaweza kupatwa na shinikizo la damu au hata kiharusi, akasimama kwenye kutoa msaada,…


************

Huku wodini  chumba maalumu , dakitari bingwa alikuwa akiongea na mgonjwa wake, baada ya heka heka za kumtuliza, na mama akakubali kutulia, na walikuwa wamekaa kitandani kwa huyo mama.


‘Sikiliza mama mpendwa, mimi ni dakitari wako kwa sasa, nataka nikusaidie , lakini sitaweza kukusaidia kama sitajua undani wa tatizo lako, kwahiyo naomba unielezee kuhusu huyo mtoto wako, ulimpataje..mume wako ni nani, hujaweza kukumbuka hilo…?’ Docta akauliza.

‘Docta hilo sio la kuniuliza mimi kwa sasa wa kuulizwa na huyo nesi wenu, muulizeni huyo mtoto kampeleka wapi…’akasema

‘Lakini una uhakika gani kuacha hiyo ndoto,kuna ushahidi gani mwingine kuwa huyo nesi alimchukua mtoto wako..akiwa hai..?’ akaulizwa na huyo mama aliposikia kauli hiyo akainua kichwa na kumuangalai docta akasema;

‘Acha uchuro..sitaki kusikia tena hiyo kauli, …eti akiwa hai..mnataka kusema nini…haya hata kama ni maiti, nipeni hiyo maiti yake basi, au nionyesheni hilo kaburi lake..’akasema kwa hasira.

‘Tatizo ni kuwa hilo tukio limetokea siku nyingi, na waliokuwepo kipindi hicho hawapo….’akasema

‘Hawapo , unauhakika na kauli yako hiyo, huyo nesi hakuwepo siku hiyo..?’ akauliza

‘Nasema madakitari,…’akasema
‘Hilo mnalijua nyinyi, nyinyi ndio madaktari mliopo sasa na mnachukua majukumu hayo..mimi nawaona sasa lenu moja, …..’ akasema huyo mama.

‘Ndio, sisi ni madaktari, na tunachukua hilo jukumu, lakini hatuwezi kufanya lolote mpaka tupate msaada kutoka kwako, tunahitajia ushahidi wa kutosha…’ akasema yule dakitari na kabla hajamaliza, yule mama akainuka, na yule dakitari akashituka akijua huyo mama anataka kukimbia

Mara yule mama akavuta nguo, sehemu ndogo inayoonyesha sehemu ya tumbo, na kuonyesha pale aliposhonwa, na haraka akajifunika…

‘Huu ni ushahidi mmojawapo,….unataka nini zaidi..’akasema

 Docta alipaona na alishaambiwa na dakitari mwenzake kuhusu hilo , lakini bado alihitajia maelezo zaidi kutoka kwa huyo mama, na akitoka hapo atakwenda kuongea na nesi ili kusikia kauli yake juu ya hilo.

‘Mama hiyo peke yake haiwezi kusaidia,maana utaulizwa ni ushahidi gani kuwa ulijifungulia kwenye hii hospitali,…unaona hapo, kwahiyo sisi bado tunahitajia kumbukumbu zako zaidi.’akasema docta.

‘Mkitaka usahhidi mwingine ni huyo nesi,..na kama ataendelea kukaidi, basi msija kunilaumu, uvumilivu una mwisho wake…mulizeni kilichomtokea asubuhi, …’akasema

‘Kwani kilitokea nini?’ akauliza docta

‘Kamuulize mwenyewe, na hao washirika zake, waulizeni huko njiani walipokuwa wakija walipatwa na majanga gani….’akasema

‘Washirika wake..?’ akauliza docta.

‘Mhh, tatizo hata …..mimi,….’akashika kichwa huyo mama kuonyesha kuwa kinauma, docta akaliona hilo, akagundua kuwa mama huyo kuna dawa aliakiwa kuzipata na yeye alimchelewesha akitaka kumhoji kwanza.

‘Chukua dawa hizi zimeze….’akasema huku akimpa huyo mama hizo dawa akachukulia maji na kumpa, yule mama akazipokea na kuzimeza, na haikupita muda,huyo mama akawa kashikwa na usingizi.

‘Washirika wake..ni akina nani hao..?’ docta akawa anajiuliza akitoka chumba kile kuelekea kwa mkuu wa hiyo hospitali, lakini kabla hajafika huko akaona aende kuonana na huyo nesi ajaribu kumshawishi kama anaweza kupata lolote kutokakwa huyo nesi.

Akiwa anatembea kulekea huko, akiwa anamuwaza huyo nesi , ni kwanini anasita kuelezea tukio ambalo alisema linafanana na huyo mama, je huenda huyo nesi anafahamu kuwa huyo mama ndiye huyo aliyekuwepo kipindi hicho….’akawa anajiuliza

‘Basi kama hataki kuelezea hilo tatizo ni lazima kuna jambo, ni lazima kuna kitu anajaribu kukiwepa…na je huyo mtoto anaye kweli, je huyo mtoto alifariki….hapo tunahitaji majibu sahihi kutoka kwa huyu nesi….ngoja nikaongee naye …’akasema huku sasa anakaribia mlango wa huyo nesi.

Alipofika mlangoni akasikia watu wakiongea, akajua nesi huyo anawageni, akageuka kutaak kuondoka lakini kauli aliyoisikia ikamfanya arudi na kuegemea mlango kusikia kinachoongewa huko ndani.

‘Mama wa mitaani, ni….?’ Ilikuwa sauti ya kiume

‘Mimi sijaelewa ni mama gani huyo?’ Sauti ya kike.

‘Ni yule mliyekuwa mkiishi naye, aliyekuwa akiitwa mama wa mitaani, akaja kuitwa mama wa mkono wa baraka, ambaye aliletwa hapa kutibiwa kutoka huko kwenu akiwa kaungua…’ Hiyo ni sauti ya nesi

Kumbe…..hao wageni ndio waliokuwa wakiishi na huyo mama, sasa nimeanza kuelewa,….ni lazima nionane na hao wageni niongee nao, watakuwa wanafahamu vyema kuhusu huyu mama.

Hakutaak kusbiria zaidi akaondoka pale mlangoni na kwenda kuongea na mlinzi kuwa hao wageni wa nesi wakitoka waambiwe wanahitajika kwa maongezi kwa dakitari mkuu wa hiyo hospitali, na yeye akaelekea huko kuongea na mkuu huyo kumuelezea alichosikia.

NB Tutaona yaliyoajiri


WAZO LA LEO: Mshukuru mola wako kwa kila jambo, kwani yote anayajua ni huenda heri ikapatikana katika shari.
Ni mimi: emu-three

No comments :