Nesi akiwa kapewa nafasi ya mwisho,
vinginevyo utawala unamchukulia hatua za kinidhamu, na haitaishia hapo, hatua
itakayofuata ni yeye kufikishw mhakamani kwa kosa la kumchukua mtoto wa mama wa
mitaani…
‘Mama keshasema akitoka hapa anakwenda
mahakamani, japokuwa alisema mwanzoni yeye hahitaji kwenda mahakamani anaweza
kuomba kwa mungu jambobaya likampata kila aliyeshiriki, lakini kaona kuwa
walimchukua mtoto wake hawakuwa na nia nje..’aliambiwa
‘Unaona kwa vile anajua hana haki..ni
mwongo huyo mama, anatumia viini macho kuwahadaa watu,mimi bado sijamuamini na
pia sina lolote kuhusiana na hizo shutuma..’akasema
‘Kama wewe umejiaminia hivyo, acha sisi
tuone la kufanya..ila tunakumpa nafasi ya mwisho ya kulifikiria hili usije
kutuona wabaya..’akambiwa
Basi nei alipotoka hapo akiwa hajui hata
afanye nini, akaona akajaribu kumigia simu tena dakitari kijana kama anaweza
kupatikana, na akimaliza hilo inabidi akaongee na ndugu zake ili wajua ni nini
kinachoendelea hakupenda kabiasa kuwahusisha na kinachoendelea mpaka awe na
uhakika, lakini kwa hali ilivyo, anajua kuwa ndugu zake hao wanaweza kuingiliwa
na polisi, ..
‘Hapana, kwanini…kwanini hawa ambosi zangu
hawanielewi….’akawa anaongea peke yake.
‘Ni wakati nesi anatoka,…akiwa akili
imevurugika mara macho yake yakaona jambo…
Kwenye wodi ya wazazi, alimuona mama akiingia , akahisi huyo mama hastahiki
kuingia huko..na alikuwa na uhakika sio mfanyaakzi wa hapo, na kulishapigwa
marufuku mtu ambaye sio mfanyaakzi wa hapo kuingia eneo hilo tena kwa kupitia
mlangowa dharura…kuna mpango bango limewekwa hapo mlangoni,…akaona aende
kuongea na nesi aliyekuwepo hapo kwa muda huo,.
Kitu kilichomtia mashaka nesi huyu mkuu ni
uvaaji wa yule mama , mama huyo alijifunika kama yule mama wa mitaani,
nesi akaamua kumfuatilia huyo mama kwa
nyuma, na kwa kumbukumbu zake yule mama wa mitaani likuwa wodini kwake kalala,
sasa huyu mama ni mama gani. Alikimbia hadi kwenye wodi hiyo ya wazazi, na
kukuta mhusika pale naye katoka, akaaanza kuhisi wasiwasi.
‘Na huyu nesi naye kaenda wapi kwanini
kaacha mlango huu wa dharura wazi..’akaanza kusema ukali, lakini kabala
hajafanya lolote mara akasikia sauti nyuma yake.
‘Vipi mbona upo mbiombio…ni maswala ya
huyo mama nini…’ akagutuka na kugeuka nyuma, na nesi aliyekuwa zamu kwenye wodi
hiyo ya wazazi alikuwa kabeba sinia la dawa na vifaa vingine.
‘Mbona umeacha mlango wazi..?’ akauliza
‘Mlango wazi, hapana mimi nilihakikisha
nimefunga huo mlango kabla ya kutoka, labda kaja mtu mwingine akaufungua,
..’akasema huku akionyesha ufunguo wake.
‘Nahisi kuna mama kaingia humu kwa kupitia
mlango huu.., ambaye hastahili kuingia humu, na…’ aliposema hilo akasikia sauti
ikiita kutokea ndani
‘Wewe nesi upo wapi, nataka mtoto wangu…’
ilikuwa ni sauti ya mama wa mitaani, nesi mkuu akashituka, akageuka nyuma kama
vile anaweza kuona kule kwenye wodi maalumu, maana ana uhakika huyo mama
alikuwa kalala, na kama katoka basi atakuwa aktumia mlango wa dharura kutoka
kwenye wodi hiyo, na mlango wa dharura aliufunga yeye..
‘Mhh haiwezekani….’akasema
Tuendelee na kisa chetu
***
Yule mwenzake kusikia sauti huko ndani kwa haraka akikimbilia huko
wodini huku akikumbuka matukio yaliyowahi kutokea kwa mama mmoja kupita
mahospitalini na kuiba watoto, akitumia visngizio mbali mbali…alimuacha nesi
mkuu akiwa kashikwa na mshangao.
Nesi huyo wa zamu kwenye hiyo wodi, alipofika akamkuta mama
aliyejifunika uso akikagua vitanda vya wazazi na kila aliyempita alikuwa akimuulizia
kuwa anajua lolote kuhusiana na mtoto ambaye hana mama…na akina mama waliolazwa
hapo ambao wengi ni wajawazito wakawa wanashangaa tu.
Yule nesi naye alipomuona huyo mama akabaki kaduwaa, akishindwa kuelewa
maana huyo mama alitakiwa kuwa wodi ya wagonjwa maalumu na alijua yupo
huko,..sasa hapa kaja kufuata nini,…akashindwa hata afanyaje,…
‘Mhhh ni huyu mama mbona leo limenikuta….hata sijui nifenye…’
alijikuta akisema kwani alishasikia visa
vya huyo mama, na vingi vya ajabu ajabu, akaogopa kumsogelea akijua dhahama
lake,… lakini kwa vile yupo kazini akaamua kuchukua hatua akamsogelea yule mama
na kutaka kumuuliza, na alipomkaribia tu yule mama kwa haraka akageuza kichwa
kumuelekea huyo nesi na kwa sauti ya ukali, akasema;
‘Sio wewe ninayekutafuta…namataka yule mwezenu , yule mnayemuita
nesi mkuu…’sauti nzito ikamtoka huyo mama wa mitaani, ikamfanya nesi huyo wa
zamani kurudi nyuma na kusimama.
‘Samahani mama, humu
hakuruhusiwi kuingia mtu baki, unaona hao akina mama wote humu wanasubiri
kujifungua,wewe unakuja huku kufuata nini… na huyo nesi ana ofis yake mfuate
huko ofisini kwake…’akasema
Yule mama akamgeukia huyo nesi, na wakawa wamesimama karibu karibu
wakiwa wameangaliana nesi akahisi mkojo kumtoka…alikuja kusema kuwa aliona
kwenye matundu ya macho ya huyo mama, kwenye kile kitu alichovaa, macho ya
ajabu..lakini akajitahidi akajipa moyo, akasimama vile vile.
Cha ajabu huyo mama, kwa
haraka akapiga magoti na kuanza kuongea;
‘Sio wewe ninayekutafuta,namtaka yule nesi mwingine, anajua wapi
mtoto wangu alipo, au na wewe sijui kama unajua lolote kuhusiana na mtoto
aliyekosa mzazi wake…ulishawahikusiki kitu kama hicho hapa hospitalini kwenu….?’akasema
huyo mama, nesi huyo akiwa kaduwaa tu,
hakusema kituna baadaye huyo mama akarudia yale maneno na kusema zaidi.
‘……mimi ndiye mzazi wa mtoto huyo….tafadhali kama umesikia niambie
haraka…’akasema
‘Mtoto aliyekosa wazazi , mbona hakuna mtoto kama huyo..’akasema
nesi.
‘Unajua ni muda,..nafahamu mtoto wangu kwa sasa atakuwa mkubwa…huenda
keshaanza kutembea, jamani….’akasema kwa sauti ya huruma.
‘Nesi…tafadhali….’akasema akiinua uso kumuangalia nesi..
‘Mtoto wangu yupo wapi..’akasema sasa akiwa kainua uso kumuangali
nesi.
‘Sikiliza mama sisi hapa tupo kazini, nakuomba utoke humu
ndani..’akasema nesi
‘Tafadhali nesi naomba msaada wako, nipo chini ya miguu yako, kama
unajua lolote kuhusu mtoto aliyeachwa na mama yake,….naomba unionyeshe wapi
alipo…nesi hebu fikiria wewe umejifungua mtoto halafu unapatwa na
..kuchanganyikiwa unaondoka…..’akatulia.
‘Haoa hatuhifadhi watoto, akina mama wakishajinfungua wanakwenda
wodini hapa hakuna mtoto ..’akasema nesi
‘Nesi tafadhali….mimi sikupenda kabisa kumuacha mwanangu, naomba
tafadhali unisaidie, wewe kama mzazi , wewe kama mke, wewe kama nesi, naomba
tafadhali ..’ akiwa bado kapiga magoti na kumshika huyo nesi miguu, na yule
nesi akawa anashangaa tu, hakujua kabisa nini kinachoendelea, hakujua amfanyeje
yule mama…
‘Wewe mama…’mara mlango ukafunguliwa
**********
Wakati haya yakiendelea huku kwa dada yake nesi, kulikuwa na
fuaraha kubwa sana, baada ya sherehe fupi ya kujipongeza, waliamua kufunga
safari kuja huku mjini, kumutembelea ndugu yao, na walipofika walisubiri
mapokezi, huku ndugu yao akitafutwa, kwani simu yake ilikuwa haipatikani na
wapi alipokwenda ikawa ni kitendawili.
‘Nyie subirini , huyo yupo kwenue mihangaiko, yeye hapa ni nesi
mkuu, kwahiyo kila sehemu anapitia kuona mambo yapo kama yanavyotakiwa
kuwa…nilijua atakuwa huko kwenye wodi maalumu, lakini huko tumeambiwa
katoka….’akasema mtu wa mapokezi.
‘Tatizo tumekuja bila kumuarifu…’akasem dada mtu.
‘Msijali, mtaonana naye tu…’akasema huyo mtu wa mapokezi.
Nesi aliyekuwa akitafutwa kumbe alikuwa kashikwa na kichwa cha
ghafla, akasikia kitu kama kizunguzungu akadondoka na kupoteza fahamu,
aliyekuja kumuona ni mlinzi,akatoa taarifa na huyo nesi akabebwa hadi chumba
cha dakitari, na alipofikishwa huko akazindukana.
‘Vipi nesi ..kazi zimekuwa nyingi nini, …?’ akaulizwa
‘Kwani yule mama yupo wapi?’ akauliza
‘Mama yupi, ..?’ akaulizwa
‘Mimi nina uhakika nilimuacha wodini, akiwa kalala..sasa huku
kafuata nini…waiteni walinzi wamrudishe wodini kwake..’akasema
‘Nesi tulia kwanza, kwa hali kama hii utachanganyikiwa, unajua
umeokotwa nje ukiwa umedondoka, umepoteza fahamu…’akaambiwa
‘Hapana,..sija……oh, lakini hilo ninalokuambia ni muhimu yule mama
wa mitaani kaingi wodi ya wazazi anaweza kuleta madhara, waiteni walinzi
wamarudishe wodini kwake….’akawa anasema na yule dakitari akawa kama anamshngaa
nesi, akaona kama huyu nes kachanganyikiwa nini,….alichoweza kusema ni..
‘Kwani nesi unajisikiaje kwa sasa..?’ akaulizwa
‘Umenielewa lakini docta, ..ngoja niende mwenyewe.’nesi akasema
akitaka kuondoka
‘Nesi tulia kwanza, upo kwenye kuchunguza hali yako,huwezi
kuondoka kwanza, hebu nisikilize..’akasema docta
‘Sikilizadocta hili ninalokuambia ni muhimu sana, mimi hapa
sijambo,,,unanielewa, yule mama wa mitaani katoroka wodini kwake, na kwenda
wosi ya wazazi, wakati namfuatilia ndio nikadondoka….’akasema nesi.
‘Lakini yule mama yupo wodini kwake, mimi nimetokea huko
..nilipoitwa kuwa wewe umeokotwa nje ukiwa umedondoka..’akasema huyo docta.
‘Mhh,…una uhakika, umemuacha huyo mama wodini kwake..?’ akaulizwa
‘Mimi nimetokea huko sasa hivi huyo mama kama ndiye unayemsema
nimemuona kwa macho yangu yupo kalala…’akasema
‘Haihawezekani…basi kuna jambo, kuna …hapana, hili sasa sitaweza
kulivumilia tena,..huyo mama sio wa kawaida, kumbe anaweza kujigeuza hivyo
…..hapana mimi nemshindwa…’nesi akawa anaongea mwenyewe kama kapagawa.
‘Wewe una uhakika ulimuona huyo mama…?’ akauliza docta akipiga
simu kwenye hiyo wodi maalumu.
‘Eti huyo mama ….eeh, yupo kitandani kwake, mna uhakika…?’
akauliza na kukapita muda, baadaye akarudisha simu mahali pake akasema
‘Yupo kalala….’akasema docta.
‘Mhh hiyo mpya, kama mnbisha hebu muulizeni nesi wa waodi ya akina
mama, atawambia hayo yote..’akasema
‘Lakini cha muhimu ni kuwa huyo mama yupo kalala wodini kwake,
kwanini tuhangaike kuulizia hayo, kwani kuna tatizo..’akasema huyo dakitari.
‘Docta mimi sasa nimechoka, unajua kuchoka…mimi nilikuwa na nia njema, lakini sasa ..hapana
huyu mama ataniua, hata mansema huyo mama huko kwenye wodi ya wazazi sio yeye,
basi kuna tatizo…. sitaweza kuvumilia tena…’akawa anaongea huku akishuke kwenye
kile kitanda alichokuwa kalala na dakitari akawa anamuangalia tu.
‘Docta mimi nipo safi naweza kuondoka..?’ akauliza nesi akiwa
kasimama na akamuona huyo dakitari akimuangalia tu, na nesi alipoona hivyo
akaanza kuondoka, na huyo dakitari akasema;
‘Unaweza kwenda lakini ningekushauri uende nyumbani ukapumzike…’akasema
‘Haaah, unafikiri, mimi nipo safi mbona docta, sina tatizo…’akasema
‘Kama huna tatizo kwanini ukapoteza fahamu?’ akamuuliza
‘Hata sijui, kuna kitu kilinijia tu…nikahisi kizunguzungu, na
sikumbuko kilichotokea, na nilipozindukana najikuta nipo hapa…lakini sina
matatizo akinyosha nyosha nguo yake, na
kutoka pale kwa dakitari..na alipofika nje ndio akakutana na mtu wa kupeleka
ujumbe na kusambaza barua.
‘Nesi kuna wageni wako wamefika muda tu..’akaambiwa
‘Wageni wangu kutoka wapi?’ akauliza
‘Kutoka kijijini…’akaambiwa
‘Mhh kuna nini tena..mhh afadhali wamefika, sasa nitaongea nao kila
kitu..’akasema na kuelekea sehemu ya wageni.
Yule nesi alipita wodi ile ya wazazi, wakati anaelekea sehemu ya
wageni, akaona apitie hapo wodini kuhakikisha alipofika akamkuta nesi mwingine.
‘Nesi uliyemkuta keshaondoka..?’ akauliza
‘Kaondoka, na..siunajua anaanza likizo, ..’akasema
‘Oh kweli..hakukuambia lolote kuwa kuna mama kaingia humu, wodini..?’
akauliza
‘Hapana…na sikuwa na muda wa kuongea naye maana alikuwa akiwahi
usafiri anasafiri leo kwenda kwako mkoani kwake…kwahiyo sasa hivi atakuwa kwenye
basi la kwenda kwao..’akaambiwa
‘Mhh….’akasema an kulipitia daftari la kumbukumbu ambalo kama kuna
tukio muhusika anatakiwa kuandika, akaona hakuna kilichoandikwa, akataka kwenda
wodi maalumu alipolazwa huyo mama lakini akakumbuka kuwa hana simu yake hakukumbuka
wapi walipoiacha…baadaye akakumbuka kuwa kaicha ofisini kwake.
Akapitia ofisini kwake kwanza,ili kuichukua simu yake akakuta
imezima.., na ilipowaka akakuta kuna simu zilikuwa zikimtafuta na mojawapo ni
simu ya dada yake, akaipiga hiyo simu ya dada yake..
‘Vipi sisi tunataka kuondoka tumekuja muda mrefu, wanasema
hauonekani wapi ulipo, upo nje ya hospitalini nini..na mbona umezima simu yako…?’
akauliza dada yake.
‘Hapana…, nipo humu humu hospitalini, subirini nakuja….’akasema na
kukata simu. Alikimbilia haraka mapokezi na kuwakuta dada yake na shemeji yake.
‘Vipi jamani, mbona mwaja bila taarifa kuna jema huko..’ akauliza
akimuangalia shemeji yake ambaye siku nyingi hawajaonana hata kupigiana simu,
kila akimpigia simu anajikuta anaongea na dada yake.
‘Kuna jema sana, ..yaani ni furaha kwa kwenda mbele…na ndio maana
tumekuja , kwani tumekusubiri tukaona huji labda kuna matatizo huku kazini…’akasema
dada mtu akijitikisa tikisa kuonyesha furaha.
‘Haukuna matatizo, ni mambo ya kawaida tu…ila kiukweli nilitaka
kuja huko..’akasema nesi akisita sita kuongea alicho nacho moyoni
‘Kuja , ungekuja tu, …nyumbani kwako huko…’akasema dada mtu,
shemeji mtu ambaye mara nyingi wakikutana anakuwa muongeaji lakini kwa leo
hakuonekana hivyo na nesi akamtupia jicho na akashindwa kuvumilia akauliza;
‘Shemji vipi, upo sawa kweli...nakuona kama haupo hapa, umekuja
kwa mkeo halafu unamfikiria mwingine unanitisha bwana…’akasema akimuangalia
shemeji yake na shemeji yake akatabsamu na kusema;
‘Mhh, mambo mengi, kichwa kina mambo mengi…najikuta kuchoka, hata
sijijui..sijui ndio uzee, hata sijielewi…watu wengi wananiambia nimebadilika
ghafla, lakini mimi najiona kawaida tu…ni kuchoka tu..’akasema.
‘Kiukweli bila kuficha umebadilika shemji yangu, nahisi una
tatizo, ni bora uongee, useme kuna tatizo gani ili tuweze kukusaidia, … au
mumeshaliongea ndio maana mna furaha…..’akasema nesi.
‘Sina tatizo, kama ningekuwa nalo ningelisema…usijali shemeji ….’akasema
shemeji mtu.
‘Sasa jamani mimi huku kuna tatizo nilikuwa nataka kuja huko tuongea
nanyi faragha, naona hata hapa hapafai kuliongelea hilo tatizo...mimi naona
twendeni kule kwenye ofisi za madakitari. Kule kuna ofisi yangu huko tunaweza
kuongea bila wasiwasi....’akasema akiwaangalia mmoja mmoja
‘Mhh ni kuhusu nini..?’ akauliza shemeji mtu akisita
‘Nitaambiwa tu tukifika huko,. Kwanza mtoto anaendeleaje?’
akauliza nesi kuwaondoa mashaka.
‘Mtoto hajambo kabisa..kuna muda alikuwa analia lia sana,..lakini
ikaja ikapotea, sasa hivi anaendelea vyema, tulitaka kuja naye, lakini baba
yake akasema huku hakustahiki kuleta watoto labda awe anaumwa..’akasema
‘Ni kweli, hamna shida….kiukweli nina hamu ya kumuona mtoto….najua
sasa kawazoea sana hana mashaka yoyote,..’akasema akionyesha uso wa huzuni.
‘Kwanini asituzoee na sisi ndio wazazi wake..mtoto wetu hana shaka
kabisa, yaani ukimuona…keshakuwa mkubwa, hutoamini…yaani tunavyompenda, mmh,
sijui nikuambie nini, mtoto yule hivi sasa hamtako yoyote zaidi ya wazazi wake…,
hataki kuachana na mimi na baba yake akirudi mbio mbio kumpokea, yaani
tunampenda mtoto wetu siwezi kukuelezea..’akasema dada yake, na nesi
akamuangalia dada yake na alipoona chozi linataka kumtoka akageuka kuangalia
nje.
Akatoa leso ya kwa haraka akajifanya ana mafua akapikicha macho na
kujiweka sawa, halafu akasema
‘Mhh, nakumbuka siku moja tuliongea ukasema mtoto ana macho mazuri
, kwani macho yake yapoje, unajua mimi sikuwahi kumchunguza vyema kwenye macho
yake kwani yapoje….?’ akauliza
‘Wewe utamchunguzaje mtoto sio wako, sisi wenye mtoto ndio tunaweza
kumchunguza, …mmh, macho yake mmh, unajua siku ile nakupigia simu nilikuwa
namuangalia, macho yake ni mazuri sana, na macho kama hayo mara nyingi wanakuwa
nayo wazungu..’akasema
‘Hahaha..dada naye, yaani mumempenda mtoto mpaka mnafikiri hivyo,
sasa kama yanafanana na mzungu, nyie nani anafanana na mzungu,..kwani hayo
macho yanafanana na macho ya nani, baba au mama..?’ akauliza nesi na dada mtu
akamtupia jicho mume wake, akasema;
‘Mhh, kiukweli macho…mmh, hakuna anayefanana naye kati yetu wawili,..lakini
kwa sura ,…kwa mbali anafanana na baba yake….’akasema na shemeji mtu akawa
kaangalia pembeni akatikisa kichwa kaam kukubaliana na mkewe.
Wakati huo walikuwa wameshafika ofisini kwa huyo nesi, nesi akawa
anafungua mlango na wakati anafungua mlango, mkuu wa hospitalia akaonekana kwa
mbali akija kuelekea hapo , lakini alipoona kuna wageni akageuka kurudi.
‘Yule ndio bosi wangu,mkuu wa hii hospitali, naona alikuwa na
jambo, lakini nitaonana naye baadaye..’akasema huyo nesi
‘Kama ni maswala ya kikazi endelea tu, sisi tulikuja kukuona tu,na
ilimradi upo salama, sisi tunaondoka..’akasema shemeji mtu.
‘Hapana mumefunga safari kote kuja kuniona, ingieni ndani tuongee,
na kama nitaona nina nafasi tutakwenda nyumbani kwangu..’akasema mdogo mtu.
‘Nyumbani kwako hatuwezi kwenda kwa leo….’akasema shemeji mtu.
‘Tatizo lako mume wangu una wivu unafikiri labda kuna mwenzako
huko , hakuna yoyote zaidi yako..’akasema akimtania shemeji yake.
‘Mhh,..nitajuaje nawe hutaki kuja nyumbani, huenda yupo..na kama
yupo nikimuona nitaishia jela, ndio maana naogopa kwenda huko….haya tuambie ,
maana ulisema kuna tatizo, …’akasema shemeji mtu.
‘Kwanza kaeni kwenye viti maana hili jambo tunatakiwa tuliongee na
mnielewe, …lakini kwanza kabla hatujaliongelea hilo,..hebu niambieni furaha
yenu, maana furaha ni muhimu kuliko tatizo, na tatizo hilo ni la kawaida
tu…’akasema nesi
‘Aaah, wewe tuambie kwanza, umesema kuna tatizo…, kwani jambo letu
ni jema tu, lakini wewe lako umesema ni tatizo, kwahiyo umeshatutia mashaka,
hebu tuambie kwanza kuhusu hilo tatizo lako, …’ akasema shemeji mtu.
‘Kweli hili ninalotaka kuwaambia, ni jambo zito, na nilipanga
nilisubirishe kwanza ili nipate uhakika, lakini baadaye naona mambo yanazidi
kuwa magumu. Yaani hamtaamini leo hii
nilidondoka na kupoteza fahamu….hata sijui kilichonitokea, nimejikuta
nipo chumba cha dakitari wananiambia nilidondoka nje….mmh, sijui….’akasema
akitikisa kichwa
‘Oh, imekuwa hivyo, kwani kuna nini….usije ukawa una
mimba…’akasema dada mtu akimkagua mdogo wake kwa macho…na akaona kaongea jambo
ambalo huenda hakutakiwa kuliongea mbele ya mume wake, ingefaa waongee kwanza
na mdogo wake ndipo kama ni lazima amuambie mume wake. Akatabasamu kuonyesha ni
utani tu.
Shemji mtu akawa makini sasa, akawa anamuangalia shemeji kwa jicho
la haraka haalfu akatizama pembeni, sasa naye akionyesha wasiwasi.
‘Hahaha..mimba itoke wapi…mimi dada naitunza ahadi yangu mpaka
ndoa,…hilo niamini..ni-ni mambo ya kikazi tu, na kama mlivyomuona bosi wangu, alikuwa anakuja
kutaka kuongea na mimi kuhusu hilo tatizo na nisingeliweza kuongea naye kabla
sijakutana na nyie..kwahiyo namshukuru mungu mumefika wakati muafaka…’akasema
‘Mhh ni kuhusu nini maana unaanza kututisha hebu ongea moja kwa
moja linahusu nini hilo tatizo….?’ Wakamuuliza sasa wakiwa wote wamenuangalia
nesi, ambaye ni mdogo mtu na shemeji mtu.
‘Ni kuhusu huyo mtoto wenu…’akasema kwa suati ya chini,
halafu kwa haraka akasimama na kugeukia
dirishani machozi yakaanza kumtoka.
‘Mtoto wetu ana nini….?’ Akauliza dada mtu, na shemji mtu kwa
pamoja utafikiri walipanga kuuliza hivyo kwa pamoja….
NB: Mmmm jamani muda umekwisha salio linakata..
WAZO LA LEO: Ubinadamu na utu wema ni; ujirani, upendo
, kuhurumiana na kuaidiana, katika kutimiza haya, ni muhimu sana kutembeleana
na kujuliana hali, hii ni desturi yetu waafrika sanasana, lakini inaonyesha
jinsi gani tulivyo na mashirikiano mema.
Mkitembeleana mkajuana hali, bila kujali hali za vipato, bila kujali
tofauti za kiitikadi, kimila au vyovyote vile…tunajenga upendo, na amani.
Kuna watu wao wanajiona ni
tofauti na wengine, majirani zao…, hawataki kujuliana hali, na kama ni kufanya
hivyo wanajaribu kuchagua wale wanaoendana na wao kihali, ..tukumbuke kuwaa
sote ni wamoja, mali, ukubwa, ni vya kupita tu… sote ni watoto wa Adamu na
Hawa, tukianza kujibagua, tujue tunajenga matabaka, na matabaka ni chanzo cha
chuki, husuda, na uhasma, na ikitokea
siku hali ikibadilika basi huruma
itakuwa ni adimu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment