Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, April 2, 2015

NANI KAMA MAMA-53

  

  'Hivi ni kwanini madocta wa nesi wamamkazania nesi awasimulie kisa cha tukio ambalo nesi hakutaka kukihadithia kwa vile kina siri kubwa kwake...na kuna siri gani katika macho, mbona macho, macho...'

Tuendee na kisa hiki tuweze kuligundua hilo

                                   ***************
Nesi alipofika kwa yule mama, alimkuta kalala, na invyoonekana hakuwa katika hali nzuri, akapewa dawa za maumivu na usingizi,..kwahiyo akashindwa tena kuongea naye, hata docta alipokuja alishauri kuwa huyo mama hatakiwi kusumbuliwa kwa hali aliyo nayo;

‘Huyu sasa kumbukumbu zinaanza kumrejea kwa kasi, kwahiyo anakuwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, muache apumzike, ….kwani ulikuwa na jambo naye..?’ akauliza docta

‘Hapana ni katika majukumu yangu ya kazi tu….’akasema nesi na docta akawa anamkagua kwa macho huyo nesi, na nesi alipoona docta anamuangalia sana akageuka kutaka kuondoka na docta akasema;

‘Umependeza sana leo,….hata hivyo nilitaka tuongee, lakini kwa bahati mbaya kuna dharura, kuna mgonjwa kaletwa huko anahitajia upasuaji wa haraka…., nikimaliza hiyo kazi mapema nataka tukae tuongee, mimi na wewe tu..’akasema

‘Kuhusu nini?’ akauliza nesi akionyesha wasiwasi na mshangao, akilini akawa akijiuliza mengi, akahisi ni yale yale ya bosi wa zamani nini….

‘Sana sana ni kuhusu huyo mgonjwa, huyo mama, kidogo nimepata muda wa kuongea naye kwa mapana..na muda huo alikuwa kidogo anaanza kukumbuka mambo..na inavyoonekana hayo aliyonielezea yana ukweli….sitaki kuhakiki sana, lakini mimi kama docta naweza kubaini kuwa kauli hiyo ni sahihi au imetokana na kuchanganyikiwa tu…’akatulia akimuangalia nesi na nesi akawa kakunja uso kuashiria kutokupendezewa na hicho anachoongea docta

‘Kitu ambacho kimenitia mashaka zaidi ni kuwa huyu mama bado anazidi kukumbushia dai lake,..’akasema na nesi akamkatishia kwa kuulizia

‘Dai gani…?’ akauliza nesi kwa hasira, na docta akiwa anaongea kwa sauti ya pole pole kama baba anayeongea na binti yake akasema;

‘Huyu mama tangu mwanzo amekuwa akidai kuwa mtoto wake alichukuliwa hapa hospitalini, …na anasema ni kipindi cha nyuma, alifika hapa hajitambui akafanyiwa upasuaji,..lakini mtoto wake alichukuliwa..’akasema

‘Na nani na ni muda gani maana ukumbuke kuwa muda fulani nilikwenda chuoni kusoma, sasa isje ikawa ndio huo muda..’akasema nesi

‘Yawezekana mimi sikatai…lakini kwanini aseme ni wewe uliyemchukua huyo mtoto..’akasema

‘Karudia kusema hivyo?’ akauliza nesi

‘Safari hii hakukutaja wewe moja kwa moja, safari hii kasema ni nesi aliyekuwa akimuhudumia,..alipewa kazi ya kuwa karibu naye, ….’akasema

‘Bado haiwezekani ukasema ni mimi, ni kwa vile mwanzoni alisema hivyo, ndio maana bado unashikilia kuwa ni mimi, ..docta nikuulize kwanini mimi nimchukue mtoto wake?’ akauliza nesi

‘Sijui..labda kwa vile alichanganyikiwa mkaona  hataweza kumlea huyo mtoto..siwezi kukisia kwanini, ndio maana nilitaka tuongee, nijue hilo tukio ulilosema wewe lilikuwaje,….’akasema

‘Docta..’nesi akataka kuingilia sasa akiwa kakasirika lakini dakitari yule akaanza kuondoka akisema

‘Tutaongea tu usijali,…nina mambo ambayo yanaonyesha kuwa huenda tukio hilo linamuhusu huyu mama, sasa sijui kwa vipi kama huyo mama alikufa kwanini kuwe na sababu, na dalili za huyu mama kufanana na huyo mama mnyesema alikufa..’akasema

‘Sababu na dalili zipi?’ akauliza nesi

‘Hebu kwanza nikuulize huyo mama marehemu alikuwaje,..macho yake…?’ akauliza na nesi aliposikia hivyo akashituka…akajikuta akiuliza

‘Macho yake..macho yake yana nini?’ akauliza

‘Na huyo mama alipokuja hapa alikuwaje usoni?’ akaulizwa

‘Mhh, hapo unanichanganya,..kwanza umesema macho, haalafu usoni alikuwaje,…mimi nilikuwa nesi tu..na huyu mama alifika hapa akiwa hajitambui, ina maana macho yalikuwa yamefumba, ningayaonaje..?’ akauliza

‘Na uso wake ulikuwaje?’ akaulizwa
‘Nakumbuka aliharibiwa na kitu kama ….kuchanwa chanwa na na kitu kama miba, au seng’eng’e..’akasema

‘Yap…you’r right..’akasema huyo docta halafu hakufafanua zaidi akasema;

‘Inabidi tuongee, …. ngoja ni muwahi huyo mgonjwa…inabidi tuongee la sivyo, ohoo…’akawa keshaondoka na nesi akabakia peke yake na mgonjwa.

Nesi alijikuta mwili hauna nguvu akaogopa hata kugeuka kumuangalia huyo mama, alihis akilini kama vile huyo mama ni mzuka,..au kibwengo,…au mfu aliyefufuka, taratibu akageuza kicha kumuangalia huyo mama.

‘Haiwezekani sio yeye….hapana, docta ana lake jambo….’akasema na wakati huo huo akageuka kile kitanda kingine, akawa anashangaa kuona yule mgonjwa mwingine harudi kitandani kwake, kwani alikuwa na maongezi naye…akaona akaulize kwa nesi aliyekuwepo hapo toka asubuhi…akaenda kwenye ofisi yao ndogo wanapokaa wakisubiria kuwahudumia wagonjwa.

‘Nesi hivi yule mgonjwa wa kile kitanda kahamishwa maana..?’ akauliza

‘Yule mgonjwa kesharuhusiwa mbona…, hukuona kwenye hiyo ripoti yangu,…?’ akauliza huyo nesi

‘Yaani hata sijaipitia hiyo ripoti yako, kwani nimefika hapa nikiwa na hamasa ya kuongea na huyu mgonjwa, nilikutana naye hapo nje, nikajua ataingia ndani ili nipate kuongea anye….oh kumbe kesharuhusiwa. Sasa na huyu mama hapa mbona ananichanganya...’akasema
‘Kwa vipi nesi..?’ akauliza
‘We acha tu, …na huyu aliyeruhusiwa unajua wapi anaishi?’ akauliza

‘Yule mama anakaa kijiji cha mbali sana, ….na cha ajabu hakuna ndugu yake aliyefika kumfuata angalau wakamsaidia,..hana haat pesa ya nauli…kosa kalifanya mume wake, na ndugu wa mume wanasema kuwa yeye ndiye kumuunguza ndugu yao, kwahiyo na wao wameenda mahakamani kudai kuwa huyu mwanamke ni mkosaji…..’akasema

‘Duuh, ndio imekuwa hayo..kumbe kuna mambo mazito nyuma ya pazia kwa huyo mama,…..sasa kama ni hivyo,… badala ya kulisawazisha hilo jambo, inawezekana kukazuka mgongano wa familia hizo mbili, wasiohusika wanaweza wakasababisha ndoa hiyo kuvunjika..’akasema nesi.

‘Na ndivyo inavyoelekea huko, kitu nilichokiona hapa, mke kajitahidi sana kuwa karibu na mume wake..yeye alishamsamehe mume wake kuwa aliyafanya hayo kwa sababu ya ulevi…, maana hata hapa japokuwa wote ni wagonjwa lakini mke alikuwa akienda kumsalimia mumewe kumujulia hali,..tatizo sasa ni ndugu, maana hata mume alionekana kuongea na mkewe..’akasema.

‘Mhh maswala ya ndoa hayo…nayaogopa kweli kweli, wapendane wengine wapambe ndio wawe washabiki,…ushabiki mbaya…na kiukweli kwa hali hiyo, hao wanandoa wasipokuwa makini wataachana…kisa kujali matakwa ya wanafamilia’akasema nesi

‘Ni bora tu waachane ,..kwangu mimi, ningeona bora iwe hivyo, maana kama wamefikia kuunguzana na maji ya moto, si baadaye watachomana visu au kutiliana sumu….mhh, lakini mke anaonekana kupenda sana….’akasema mwenzake.

‘Hebu nikuulize huyo mama uliwahi kumdadisi vyema wapi anapotoka, kijini gani cha mbali..je  ana ndugu yake wanaofanana…?’ akauliza nesi

‘Nimekuwa nikiongea naye sana, nikitaka kujua ilikuwaje, siunajua mimi ni mdadisi sana…ndio maana unaniita visinipite....mhh, ni kweli aliniambia kuwa kuna ndugu yake kwa baba mwingine, wanafanana sana nay eye hata walifikia kuonekana kama mapacha… lakini ndugu yake huyo ni marehemu kwa sasa...’akasema.

‘Eti nini ni marehemu eheee, ilikuwaje, alikufa kufaje?’ akauliza nesi akionyesha hamasa hadi mwenzake akabaki kuduwaa na kushangaa, na baadaye akasema;

‘Yaani we acha akikuhadithia maisha yao utamsikitikia, maana anasema ni kama balaa kwake na familia yake hasa upande wa mama, …anasema ndugu yake huyo kwanza waliivana sana kwa vile wanafana, jpokuwa hawakuzaliwa tumbo moja, baadaye ikatokea wakampenda mume mmoja, basi ikawa ni vurugu,…wivu uhasama, na urafiki na udugu ukavunjika, kisa ni kugombea mume,  baadaye ndugu yake huyo akaolewa yeye na huyo mume,…’akatulia

‘Ehe, lete mambo sister visinipite..’akasema nesi

‘Huyu yeye akakubali yaishe,..mara yule ndugu yake aliyeolewa huko akaanza kuumwa, kama kuchanganyikiwa, ..wakasema huyu kamloga mwenzake kwa vile kamkosa mume, wakati huo huyu alishaolewa na huyo mume mwingine ….huyo cha pombe, …unaonaeeh..’akasema.

‘Acha lugha yako hiyo akikusikia je..’akasema nesi

‘Sasa hali ile ya kuchanganyikiwa ikawa haiponi, …akaanza hata kutembea ovyo barabarani, kukimbia na hata kupotea, na ndio mara ya mwisho wakamuokota akiwa amekufa…’akasema

‘Ina maana kufa kwake ilitokea kuwa kapotea,…sio kwamba alitokea hospitalini?’ akaulizwa.

‘Ilivyo ni kuwa wengine wanadai, alipelekwa hospitalini, …na kipindi hicho alikuwa mja mnzito…., akajifungulia huko alipopotelea…na watu hawana uhakika na mtoto wake, wengine wanasema huenda mtoto alikufa…sasa hapo ndio hata sielewi, maana huyo mama alikuwa akiongea na kuchanganya mada akilia maana inasikitisha kweli....’akasema.

‘Mungu wangu, atakuwa ndio huyo..sijui nimpataje..unasema kijijini gani?’ akauliza sasa akiandaa kuondoka.

‘Mhh, alisema kijiji cha mbali kweli..hata jina silikumbuki vyema…, kwani vipi?’ akaulizwa

‘Atakuwa ndio yeye…ni ndugu yake, sasa nimepata ufumbuzi, lakini mpaka nimuone huyo mama….sasa sasa..nitampataje…oh’akasema nesi 

‘Sikuelewi..’akasema mwenzake na nesi akageuka kuondoka, akitaka ikibidi aombe ruhusa asafiri hadi hicho kijiji cha huyo mama, na wakati anatoka akasikia simu yake ikiita;

Akaangalia akaona ni simu ya kutoka nje

‘Halloh, …dakitari ehe..’akaita

‘Ile komputa yangu inaweza kutengenezeka nimefurhi kweli ipo kwa fundi,…ila nilitaka kujua taarifa za yule mama, mbona nimesikia kuwa alikufa.. ni kweli?’ akauliza

‘Ndio kwani ulikuwa hujui?’ akauliza nesi kwa mshangao

‘Nilikuwa sijui, mimi nilijua tu kapotea….nimepiga simu yenu ya mezani na nilipokuwa naomba kama wamebahatika kupata hizo kumbukumbu zangu ndio, nikaongea na yule rafiki yako, ndio akaniambia kuwa huyo mama alikufa..oh hata siamini,, ilikuwaje?’ akauliza

‘Alikutwaa amekufa… na sasa nimempta ndugu yake kabisa, wanafanana sana..’akasema

‘Hata macho..?’ akauliza

‘Macho…mmh, sijui, ..oh macho, ….sina uhakika sanai..’akasema nesi kwani Alishahisi vibaya baadaya ya kusikia kuwa dakitari huyo aliongea na rafiki yake.

‘Mhh jamani mama huyo…..niliyapenda sana macho yake….’akasema dakitari na kutuli alionyesha kuhuzunika, na baadaye akasema;

‘Hebu nambie unamkumbukaje huyo mama, alikuwaje, anafananaje..na hayo macho yalikuwaje?’ akauliza nesi

‘Zaidi eeh, alikuwa na macho mazuri sana ya aina yake….nyusi ndefu, nyeusi..macho makubwa…na kingine usoni, aliharibika sana, alichanwa chanwa na kitu kama miba au waya kali… usoni ulikuwa hautamaniki, …nilikuwa na picha yake kwenye hizo kumbukumbu, na kama komputa yangu itapona nitaweza kumuona vyema....’akasema

‘Oh, macho ya aina yake yapoje hayo…., ndio siku ile ulitaka kuniambia hivyo..ulisema kitu kama hicho nikajua unaniongelea mimi?’ akauliza nesi

‘Mimi, mmmh, labda ,…nilikuwa nakusifia wewe, kuwa hata wewe macho yako ni mazuri kama ya huyo mama…macho makubwa, nyusi eeh…’akasema huyo docta na nesi akatabasamu.

‘Kama ya huyo mama!!..?’ akauliza na simu ikakatika….

Nesi akajaribu kuipiga ile simu mara kadhaa, lakini ikawa haipatikani, akasikitika kuwa amekosa kitu cha muhimu sana, akasema kimoyomoyo,  nitakuja kumpigia tena, nione kama komputa yake imepona...najua huko kuna kumbukumbu za kuweza kusaidia….

`Najua hata yeye anahangaika kunitafuta huko,.. ngoja nisubiri kidogo’ akasema huku akitembea kuelekea wodi nyingine!

‘Macho yako ni mazuri kama ya huyo mama’…alikuwa ana maanisha nini, kwani machi yangu ni mazuri, ina maana macho yangu yapoje, …au alikuwa ana maana gani, akayakariri haya maeneo mara mbili na huku akitafakari haya maneno mapya kutoka kwa huyo dakitari kijana ambayo sasa yanafana na yale ya dakitari bosi wake.

Cha ajabu alichofanya, ni kwenda chooni, na kujiangalia kwenye kiyoo kikubwa kilichopo kwenye choo chao cha staff..Akiwa anajiangalia macho yake kwenye kiyoo, huku akitabasamu, alijaribu kumkumbuka docta kijana, siku ile ya mwisho,..lakini mbona hakuwahi kumsifia kitu kama hicho…macho macho..

Mara akakumbuka kitu..kuwa dada yake alisema mtoto ana macho mazuri…mmh, kuna nini kwenye macho macho,…..’akawa anarudia hilo neno macho macho..macho..mapaka akahisi kichwa kinamuuma.

Siku hiyo ikapita hivyo….

**************
 Kesho yake akawahi wodini akiwa na nia ya kuongea na huyo mama wa mitaani akiwa na uhakika atakuwa keshatulia na huenda kumbukumbu zitakuwa safi..

Alipofika alimkuta akiwa kakaa kitandani, lakini alionekana kuwa na mawazo sana, akamuuliza hali yake, akamuonyeshea kwa vitendo kuwa kichwa kinamuuma

Nesi akakagua kumbukumbu zake, akaona keshapewa dawa, na kwahiyo hakuwa na la kufanya, akamuangalia huyo mama, na huyo mama alionekana kumuangalia nesi, japokuwa kajifunika vile vile ..lakini nesi alihisi huyo mama anamuangalia yeye bila kupepesa macho, nesi akahisi mwili ukimsismuka

‘Mhh, sasa hata namugopa huyu mama..’akasema kimoyo moyo, hata hivyo alijikaza asionekane hisia zake akasema.

‘Kama kichwa kinauma lala, kitapoa,..’akasema nesi na kuanza kuondoka, kabla hajafika mbali, akasikia kitu kama kinadondoka, alipogeuka akaona yule mama yupo sakafuni akajinyonga nyonga..

‘Oh sasa hili balaa..’akasema akiogopa hata kumsogelea, akaguka kule kwenye chumba cha manesi na kumuita mwenzake.

‘Nesi mpigie simu docta , huyu mama kazidiwa..’akasema na kusogea pale alipolala huyo mama.

 Akainama kutaka kumshika, lakini alihis mikono ikigoma kufanya hivyo,..hakujua kwanini kaingiwa nauwoga wa ghafla wakati yeye hana tabia hiyo, akajipa moyo, na kujitahidi tu, akamshika yule mama pale sakafuni asizidi kujinyonga nyonga huku akiuliza huyo mama anajisikiaje..yule mama akawa anaweweseka na kuwa kama anataabika…na kitu alichosikia ni kauli ile ile, kuwa anataka mtoto wake, ..

Na mara dakitari akafika na huyo mama akabebwa na kuwekwa kitandani.

Dakitari akaagiza huyo mama awekewe dripu yenye dawa, na haikuchukua muda yule mama akawa kalala..katulia..

Nesi katika ile hali ya purukushani alibahatika kujiiba na kuvuta ile nguo ya usoni, katikati ya macho, haikuweza kuvuka na aliogopa asije kuonekana anataka kumuangalia huyo mama..kwenye matundu ya macho…alichoona ni kuwa yule mama kweli ana nyusi ndefu…nyeusi…mmh huyu mama anaonekana kuwa na macho mazuri, angeyaweka wazi tuyaone..’akawa anawaza nesi,  na mara akakumbuka kauli ya dakitari kijana

Macho yako ni mazuri kama ya huyo mama….

Na alipokumbuka hivyo yeye kwanza akawa anjiuliza kama kweli yeye macho yake ni mazuri kihivyo, ni kweli kuwa hata yeye ana nyuzi ndefu na macho makubwa,….lakini sio ndefu kama za huyo mama,…

‘Macho…’akajikuta anarudia hayo maneno, na alitaka kama docta ataondoka atamfunua huyo mama aone macho yake yapoje…lakini atakuwa kayafumba hayo macho, nitawezaje kuyaona..macho ya aina yake..yapoje hayo

Mara akahisi sauti ikitokea kwa huyo mama, nesi akageuka kumuangalia, kwa kipindi hicho docta alikuwa kasimama kitanda kingine akimuhudmia maam aliyeletwa hapo karibuni,  nesi akahisi huyo mama anaota, au anahisi maumivu mahala fulani , lakini kwa muda ule hakujua ni wapi, na wakati anamsogelea akiwa na nia ya kumshika aone kuwa ana joto au kumkagua vyema..na ikiwezekana achukue nafasi hiyo kumuondoa kile kitamba usoni.

Mara akasikia sauti nyuma yake ilikuwa ya huyo dakitari.

‘Vipi kuna tatizo?’ akauliza yule dakitari wake

‘Huyu mama naona anagugumia kama anaota,…’ akasem yule nesi

 Yule dakiatri akamsogelea yule mama na kuweka mkono shingoni mwa yule mama, aliuondoa mkono wake haraka na kumtizama yule mama halafu akamtizama nesi

‘Ana joto kali sana….’ Akasema dakitari sasa akiweka kipimo cha joto kwapani kwa huyo mama. Baadaye alikitoa na kusema;

‘Joto ni lile lile..’akasema akiangalia kadi ya huyo mama, halafu akachukua kipimo cha shinikizo la damu, akampima na baadaye akachukua katarasi na kuandika maelekezo.

‘Huyu sasa mtambadilishia dawa, baadaye kama nusu saa hivi mpe hii dawa, nitakuja kumuona baadaye ngoja nikahudimie wagonjwa wengine..’akasema docta

‘Na nakumbuka hatujaongea..’akasema docta akigeuka kumtizama huyo nesi

‘Ndio hatujaongea, na mimi bado sijakamilisha uchunguzi wangu..’akasema nesi

‘Uchunguzi wako…!?’ akauliza docta kwa kuonyesha mshangao

‘Si niliwaambi a kuwa kuna mambo nataka kujirizisha nayo kwanza…ikiwemo kuwasiliana na wale madakitari waliokuwepo kipindi hicho..’akasema

‘Nimeshawasiliana nao..’akasema huyo docta

‘Oh, umewaambia nini..?’ akauliza nesi akionyesha kushtuka

‘Kuhusu huyu mgonjwa...huyo mama’akasema docta

‘Waka-ka-semaje….?’ Nesi akawa hatulii akionyesha wasiwasi mwingi

‘Unajua nahisi kuna jambo lilitokea,…na sijui kwanini, maana hata wao hawakutaka kuniambia ilikuwaje…., na wamesema hawajui lolote au kukumbuka chochote kuhusu mama ..kwani eti kulikuwa na wagonjwa wengiwa namna hiyo…basi yaonyesha kabisa kuna jambo kubwa lilitokea na mkapanga kulificha…’akasema

‘Sasa kama wao wameshidwa kutoa ushirikiano kwanini unanishinikiza mimi?’ akauliza

‘Kwasababu wamesema kama wewe ulisema kulikuwan na tukio basi wewe utakuwa unakumbuka vyema…. kama kuna kitu nimekisema basi tukubane wewe, na uwajibike mwenyewe…maana wao hawakumbuki vyema ni mama gani huyo..’akasema

‘Mungu wangu ndio wanasema hivyo?’ akauliza.

‘Ndio maana nataka tushirikiane, mimi pamoja na kuletwa hapa nikuambie ukweli, ni pamoja na kuhakikisha uchafu wote wa nyuma unazolewa, na kama kuna masalia,..na kama kuna watu walizembea, na kusababisha mabilioni ya pesa za hapa kupotea basi inabidi wafikishwe mbele ya sheria…sasa kama wewe hutashirikiana na mimi basi itabidi uwe kwenye hilo kundi,..nakupa tu kama dondoo..’akasema huyo docta

‘Ina maana wewe umeletwa hapa kuchunguza?’ akaulizwa

‘Nimeletwa hapa kama kiongozi, ..na kuhakikisha kuwa hii hospitali inarejea katika hali yake iliyokuwepo kabla…, unajua hapa tulikuwa tunapata wahisani wengi, wahisani wakakata misaada yao baada ya kugundua kuwa kuna ubadhirifu kuna rushwa…kuna uzembe na ufisadi…na hata wagonjwa wakafikia kulalamika..sasa na hilo la kupotea watoto lipo kwenye kumbukumbu..’akasema

‘Kupotea watoto , mbona haijawahi kutokea?’ akauliza nesi kwa mshangao

‘Ipo kwenye kumbukumbu za madai ya watu, na ushahid ni kama huo kutoka kwa huyu mama, kama atathibitisha hilo ..nesi utakuwa hatarini, ni bora ukaniambia ukweli nikajua jinsi gani ya kukutetea, kama itawezekana kufanya hivyo..’akasema.

 Nesi akabakia kimia hakujua hata aseme nini..akakumbuka kauli ya bibi yake, kuwa kama huna uhakika na la kuongea ni bora ukae kimia..lakini baadaye, akasema;

‘Ngoja nitaongea na mwenzangu nijua atanishauri vipi..’akasema

‘Na mwenzako!?, mwenzako nani?’ akauliza docta kwa mshangao
‘Si ndio hao madakitari…’akasema kwa hasira.

‘Ok..lakini nimeshaongea nao, labda….kupeana mikakati zaidi..ila nesi, usije ukasema sikukutahadharisha..’akasema dakitari na kuondoka.

‘lakini mimi nina kosa gani?’ akauliza nesi kwa sauti ya kusikitika.

‘La kuficha ukweli… na pind hivi unaweza kujikuta unaitwa au kukutana na askari usalama’akasema docta

‘Askari usalama kwa nini..?’ nesi akasema kwa wasiwasi akikumbuka kuwa kuna muda alimsikia huyo docta akiongea na mtu, na akawa anataja neno afande,…na kusema ‘atakuwa anafahamu kitu huyu nesi, uje uonane naye..umbane atajkuambia ukweli..’

‘Ina maana umeshanishitakia?’ akauliza nesi

‘Siwezi kufanya hivyo…watakaofnya hivyo ni hao waliokosewa kama huyo mama..’akasema na nesi akageuka kuangalia pale alipokuwa kalala huyo mama, na kumuona kasimama, akageuka kumuangalia docta na kusema

‘Docta….’akiashiria docta kuangalia kule alipokuwa huyo mama huku akionyesha uso wa wasiwasi na kama kutaka kukimbia.

NB: Haya kwa leo ndio hayo


WAZO LA LEO: Japokuwa umasikini ni mtihani, na ukiwa huna kitu unazalilika, unaonekana huna maana, lakini isiwe ndio tija ya wewe kufanya yasiyofaa, ukageuka kuwa omba omba, au ukaiba..au ukajizalilisha. Umasikini kwa mungu unathamani kubwa sana, kwani yeye anafahamu kwanini akakufanya hivyo, huenda ungelikuwa tajiri ungetakabari na kuwa mtu mbaya sana…Muhimu, rizika na kile ulichojaliwa nacho, huku ukifanya bidii kupata pato lako la halali, kwani riziki ya halali ipo tu kama utajituma na kusimamia kwenye kutenda yaliyo haki na ukweli…

mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Good way оf explaining, and nice piece օf writing to obtain information about my presentation topic, which i am going
to delіѵer in academy.

Hɑve a look at my page temp2