Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 31, 2015

NANI KAMA MAMA-52


‘Ngoja nikaongee na huyo mama aniambie mwenyewe kuhusu huyo mtoto ambaye anadai kuwa mimi nimemchukulia…, maana sasa atanichanganya, mimi sijawahi kumchukua mtoto wake, na sijui kwa vipi…kwanini aendelee kusema kuwa mimi ndiye nimechukua mtoto wake…’akasema nesi kwa hasira

‘Kumbe ni wewe..!! maana , nilimsikia huyo mama akiongea na yule dakitari,  akisema kuna nesi mmoja alimchukua mtoto wake,…sasa sikujua kuwa ni wewe, kwani ilikuwaje?’ akauliza huyo mama.

‘Sio kweli mimi sijamchukua mtoto wake, huyo mama kachanganyikiwa tu….nimchhukue mtoto wa kazi gani…unajua huyu mama nisipokuwa makini atanitangaza dunia nzima kuwa mimi ni mwizi wa watoto, …sasa ngoja, nikapambane naye mimi siogopi cha uchawi au kuchanganyikiwa kwake…’ nesi akasema na kugeuka kurudi wodini.

‘Lakini uwe makini, huyo mama mimi naona sio wa kawaida, anaongea na watu waioneonekana….na nesi mimi nilikuwa nakuga….’yule mama akawa anaongea lakini nesi alishaanza kuondoka na mama huyo akakatiza maneno yake alipoona dakatri amemkaribia, ambaye walishaagana.

Dakitari yule alikuwa akipungia mkono toka mbali na huyo mama akajua huenda dakitari huyo anataka kuongea na yeye..kumbe dakitari huyo alimtaka huyo nesi..na japokuwa nesi aliioona ile ishara, lakini hakuijali, kwa muda huo hakutaka kuongea na huyo dakitari kwani alishajua ni kitu gani atakuja kuulizwa.

Nesi moja kwa moja akaingia wodini, tayari kwenda kupambana na huyo mama…

Tuendelee na kisa chetu


*********

Na wakati anakaribia kitanda cha huyo mama mara simu yake ikalia, kwanza akawa anaipuuza lakini alipoona inaita sana, akaitizama maana alikuwa nayo mkononi, akaona ni namba ya ndugu zake wa huko kijijini, akawa kasha fika kitandani, akaona ngoja aisikilize kwanza kwani kwa mara ya mwisho dada yake alimuambia kuwa anaumwa na mtoto analia-lia..na ndipo akayakumbuka mongezi yake na dada yake yaliyomsukuma kuja kuongea na huyo mama, .akakumbuka walivyoongea;

‘Dada kwani unaumwa nini, kwani ulipima malaria, typhoid…?’ akamuuliza nesi

‘Nilipima malaria tu wakasema sina..nikajua ni uchomvu tu kutokana na kazi nyingi, lakini naona hali sio nzuri, mwili unachoka, sijisiki vyema kabisa..’akasema dada mtu.

‘Ukiona vipi njoo huku , huku kuna vipimo bora zaidi, ..na …mimi nashauri uje huku…siwezi kusema lolote mpaka upimwe vyema’akasema nesi

‘Tutaangalia hilo, nitaongea na shemeji yako…, na kingine ni huyu mtoto, unajua alishatulia kabisa, afya njema, lakini ghafla kaanza kulia lia tena kama kipindi kile…, na hata kuchemka homa..’akasema.

‘Oh..jamani kanaumwa tena.., na yeye mkampeleka hospitalini wanasemaje?’ akauliza

‘Hana tatizo, wanadai huenda ni meno…au ni makuzi, anaununua mwili..’akasema dada mtu

‘Hahaha anaununua mwili wake…, ok, nimekuelewa, ina maana kila badiliko kwenye makuzi yake linampa shida..ni kawaida, hata hivyo mimi nashauri mje naye kabisa, tuone tutafanya  nini..’akasema

‘Shemeji yako anakusalimia, kawa mpole kweli..yaani hutaamini, ..na anaonekana mwingi wa mawazo’akasema.

‘Sasa kwanini imekuwa hivyo, mhh, sijui nitatafuta muda nije niongee naye, nijue ni kitu gani kinamsumbua, unahisi ana tatizo gani?’ akauliza

‘Kwakweli mimi nahisi ni kutokana na huyo mama wa mitaani, yeye si alijifanya mjanja haogopi, akalazimisha kumuona huyo mama sura yake basi nahis tatizo limeanzia hapo,  maaana wote waliotaka kufanya hivyo, wameishia kubaya, imebidi wahangaiek sana…na yeye hataki kuhangaika..’akasema.

‘Sio kweli hizo ni imani tu, maana huyu mama anaitibiwa hapa, na kuna watu wameshamuona lakini hawajapatwa na matatizo yoyote…acheni hizo imani dada…mnataka kujiingiza kwenye imani za kishirikina sasa…’akasema.

‘Mdogo wangu, imani nyingine huja kutokana na hali halisi , tumeona yaliyotokea, sio kwa kuhadithiwa,..tumeona kwa macho yetu wenyewe, hata wale askari imekuaje, si umesikia mpama wamerudishwa kwao….. sasa unataka tufanyeje, ..unajua akili inakubali sana mifano halisi,..hata imani za dini zinakuja kuachwa pale unapoona mifano hali ..mtu unasema aaha ngoja nijaribu huko…’akasema.

‘Sikiliza dada, mimi mwenyewe nataka nihakikishe namuona huyo mama sura yake…nilishataka kufanya hivyo, akanizuia lakini sasa ama kwa hiari yake au nitatumia mbinu za kitaalamu nimuone anafananaje…ili hayo mnayosema yanatokea yanitokee na mimi..’akasema nesi


‘Kwanini unataka kujiletea balaa, mdogo wangu achana naye, au bado anadai kuwa wewe ndiye umechukulia mtoto wake?’ akaulizwa.

‘Bado aandai hivyo..hata sasa kapona, hadi ile ya moja kwa moja , sasa anasema yupo nesi mmoja, alinichukulia mtoto wangu..na kawaambia hadi wakubwa zangu..’akasema.

‘Lakini unahisi anamtaka huyu mtoto wetu?’ akauliza dada mtu.

‘Hapana huyu mtoto wako mama yake ni marehemu,..na naomba msije kuliongea hilo mbele za watu, …kiukweli mama wa huyo mtoto alikuja kufariki na kuzikwa…,huyu mama wa mitaani ana lake jambo..’akasema nesi.

‘Hebu nikuulize mdogo wangu, huyo mama wa huyu mtoto..’akasema na kabla hajamalizia nesi akamkataizia kwa kusema;

‘Mama wa huyo mtoto ni wewe, acha kauli yako hiyo…nisikie na nielewe, inaweza kutokea unaongea na simu kama hivyo, akakusikia mtu..chunga sana kauli yako…’akasema nesi

‘Ndio najua, ninachotaka kufahamu ni kuwa je uliwahi kuiona sura ya huyo mama, ambaye mnasema alipotea na kuonekana amefariki?’ akaulizwa.

‘Dada kipindi hicho sikuwa makini sana ya kuangalia sura yake…walisema aliharibiwa uso kabisa..na kwa huruma sijui nini, hakuna aliyekuwa na hamsa ya kumtizama huyo mama,..aliyebahatika ni dakitari kijana ambaye alimpiga hata picha…’akasema

‘Mimi ninachojua huyo mama alijifungua kwa shida japo ni kwa upasuaji,…ilikuwa ni shida, mama huyo kateseka kweli….hata ile dawa ya maumivu ilikwisha mapema sana,..na kwa muda ule akili za amdakitari zilikuwa kwenye kumuokoa mtoto tu..’akatulia

‘Ndilo lilikuwa lengo la madakitari maana mama alichoka sana, damu ilipungua,wakajua huyo mama sio wa kuishi tena, hawakusema moja kwa moja lakini kwa dalili, ilionekana hivyo basi huyo mama nikuambie nini dada ,… uchungu  wa uzazi, uchungu wa majeraha..na ilikuwa afe tu kwa siku zile ….kwa juhudi za dakitari mmoja kijana, akafanikiwa kumuokoa huyo mtoto mchanga..’akasema

‘Mhh… ni dakitari kijana ndiye alimuokoa?’akaguna dada mtu na kuuliza.

‘Ndio ukilinganisha na mdakitari wenzake yeye alionekana mdogo, wakawa wanamuita hivyo…’akasema

‘Basi..mtoto akachukuliwa kwenye sehemu maalumu, maana unajua alizaliwa kwa upasuaji, kwahiyo mtoto akawekwa kwenye taratibu maalumu za kuhakikisha anakuwa salama, huyo mama akawa kapoteza fahamu, na ikawa watu tunasubiria muda wa huyo mama kukata roho tu maana hali yake ilikuwa ni mbaya, ….’akasema

‘Jamani…yaani madakitari make tu, hata hamuhangaiki kuona kama huyo mama atapona, yaani mnasubiria akate roho…’akasema dada mtu.

‘Huyu mama alipona..akaonyesha dalili za uhai, lakini hakufunguka moja kwa moja, akapoteza fahamu tena..na mimi ndio nikapewa kazi ya kuhakikisha kuwa akizindukana niwe karibu yake kutoa huduma au kuwaita madakitari, ..hapo ndipo balaa likatokea..’akasema

‘Oh ndio lile balaa ukampigia simu shemeji yako huku unalia…?’ akauliza

‘Si ndio hivyo,..maana yule mama alikuja kuzinduakana wakati mimi nimetoka, ..akatoroka, na badaye akakutwa akiwa amekufa… na hapo ikaambiwa ni uzembe na kifo chake ni mimi nimekisababisha,..nikawekwa chini ya ulinzi, na aliyeweza kunitetea ni huyo dakitari kijana akisema kwa vile kuna mtoto basi mimi adhabu yangu iwe kumchukua huyo mtoto na kumlea..ndio nikawaletea nyie, ilikuwa ni njia ya wewe kupata mtoto…’akasema.

‘Masikini mama wa watu…amekufa ili mimi nipate mtoto oh , mungu amlaze mahali pema peponi..’akasema dada mtu.

‘Sasa huyu mama wa mitaani, ananichanganya, anakuja na sera za kudai mtoto,..nahisi huenda alikuwa na mtoto huko kwao, kwa vile kachanganyikiwa wakamnyang’anya mtoto, ndio maana anadai kuwa mimi nimemchukua mtoto wake..’akasema nesi

‘Lakini mimi najiuliza kwanini wewe, kwanini asimnyoshee kidole  mtu mwingine, na kitu kingine ambacho naona ni cha ajabu, huyo mama alipokuwa hapa sikuwahi kumsikia akisema huyu mtoto hapa nyumbani ni mtoto wake, zaidi ya huyo mtoto kumpenda yeye kama mama yake vile..yaani ukiwaona utafikiri mama na mtoto wake mpaka nikawa nawaonea wivu..moyo ulikuwa unaiuma kweli..’akasema dada mtu.

‘Unaonaeeh, ina maana kuna chuki zake dhidi yangu, kama angesema huyo mtoto hapo nyumbani ni wake, tungesema ni kuhusu huyo mtoto…unajua dada hata sielewi, ndio maana nataka nipambane naye nione mwisho wake ni upi..’akasema nesi

‘Kwa vipi sasa?’ akauliza.

‘Kwanza nataka nimuone huyo mama alivyo, kisura, hasa usoni...halafu nisikie kauli yake thabiti, aseme huyo mtoto wake niliyemchukua ni yupi na wapi…athibitishe,..asinitie doa, maana hapa kazini mimi sasa ni nesi mkuu…’akasema

‘Mimi nakushauri achana na hilo wewe tulia tu, si atapona, akili itarejea vyema, atakuja kugundua mwenyewe ukweli, na kama atendelea kudai hivyo, basi ataelezea ilivyo kuwa labda, atasema alikuwa na mtoto akapotea, au ikawaje,  na yote yatakuja kujulikana kuliko kujitwika mzigo kabla haujatua kichwani…’akasema dada mtu.

‘Dada ingekuwa rahisi hivyo si ningelifurahia, lakini wakubwa zangu wamenikalia kooni, nina bahati mbaya na hawa watu, wao wamemuamini sana huyo mama kuwa eti ni kweli, kuwa mimi nimemchukua mtoto wa huyo mama, wanadai, mgonjwa kama huyo akizindukana, na kuanza kukumbuka, ni sahihi,..eti kile anachoongea kinakuwa ni cha ukweli, kwahiyo wanataka mimi nielezee tukio hili ..la huyo mtoto wetu lilikuwaje..’akasema.

‘Sasa linahusikanaje na huyo mama..kwani wanafahamu kuhusu huyu mtoto wetu?’ akauliza.

‘Hawafahamu, hiyo ni siri yangu na wale waliokuwepo kipindi kile, wote waliondolewa hapa na hata sijui wapo wapi kwa hivi sasa…sasa hawa wakubwa wanasema wanataka kujua tukio hilo lilikuwaje…’akasema

‘Nakuuliza walijuaje ?’ akaulizwa

‘Unajua dada hata sijui kwanini ilitokea nikaropoka…na hilo lilikuwa ni siri kubwa, hata wakubwa waliokuwepo muda huo walinionya nisije kusema kwa yoyote yule…, kwani walikiuka sheria…na kifo cha huyo mama ilitakiwa mimi niwajibike, wakalifunika hilo tukio kiaina…mimi nikajitoa mhanga..sasa hayo yalishapita…’akasema.

‘Mhh mdogo wangu, sasa utafanyaje…kwanini usimuambie huyo mkubwa wako ukweli, ili aone atakusaidia vipi?’ akauliza
‘Dada unajua siri…nilishaambiwa hata iweje, nisije kusema lolote kuhusu hilo tukio, na sasa najuta kwanini niligusia kuwa kulikuwa na tukio kama hilo ..sijui nilipitiwaje…hilo ndio limeniponza..lakini usijali dada nitapambana nao, ilimradi najua kuwa sijachukua mtoto wa huyo mama, …’akasema.

‘Mhh, mdogo wangu sasa naanza kuogopa…maana kuna ndoto za kutisha zinanijia…hata kabla hujaniambia hilo nilishaliona kwenye hiyo ndoto…’akasema dada mtu.

‘Na wewe umeanza tena… , ule mtindo wa ndoto zako umeanza tena..mimi naogopa hata kuzisikia , maana ukiota ndoto zako ni lazima litokee jambo, ndoto zako zinakuja kuwa ni kweli mmh, sasa safari hii umeota nini tena..?’ akauliza

‘Mhh, hata naogopa kuongea, ..’akasema

‘Kama unaogopa basi usiniambie kabisa, maana mhh, ….lakini uliota nini, hebu niambia isije kuwa umeota kuwa nimekufa…au nimefukuzwa kazi…’akasema nesi.

‘Hapana..ni kuhusu huyo mama wa mitaani..maana tunaishia kumuita hivyo badala ya mama wa mkono wa baraka…unajau nilivyoota, kama ulivyonihadithia, wakubwa wanakusakama, wakataka kukushitakia….sasa huyo mama akaja juu, ikaja hadi huku, , eti kaja ananinyang’anya huyu mtoto akidai kuwa ni mtoto wake,..’akasema akionyesha sauti ya uchungu.

‘Unajua ni ndoto, lakini hata nilipoamuka nikajikuata nalia…maana sasa ikafikia hatua ya maamuzi, mtoto akawekwa kati akaambiwa achagua mama yake ni nani, …nililia mapaka nazindukana nalia mume wangu akashangaa sana sijamuhadithia bado, nimekuhadithia wewe tu maana hatufichani siria…..lakini mdogo wangu,  sikubali hata kama ni hivyo..’akasema dada mtu

‘Ikawaje maana sasa unaanza kunitisha…’akasema nesi.

‘Mtoto akamuendea huyo mama, akadai kuwa ndiye mama yake halali..na anaongea utafikiri mtu mzima..ajabu kabisa, lakini ni ndoto tu..’akasema dada mtu.

‘Wasiwasi wangu ni kuwa ndoto zako mara nyingi ulizowahi kunihadithia zimekuja kuwa ni kweli..ooh, hiyo sasa sijui itakuwa kinyume chake, lakini hata iweje, kwa vile mama wa huyo mtoto alishakufa, mimi sina wasiwasi..nilichokuwa nahangaika nacho ni kupata ushahidi wa yule mama, picha zake,kumbukumbu za vipimo vya damu..vingesaidia kuthibitisha kuwa huyu mama wa sasa sio kweli… ni kibaka tu…’akasema nesi.

‘Basi vitafute kwa kila hali…maana naanza kuogopa, na hi hali ninayoisikia najisia ovyo ovyo tu…’akasema dada mtu.

‘Yaani we acha tu, tegemeo la mwisho ni kutoka kwa huyo dakitari kijana , kama atakuwa na huo ushahidi basi tutashinda hiyo kesi , maana nionavyo, huyo mama ataishia kushitaki, ..maana mimi sitakubali, ni bora twende mahakamani..’akasema nesi

‘Na siri hapo itafichuka…unaona ilivyo mtego, na wewe utafungwa, utapoteza kazi na sis itakuwaje sijui,….’akasema dada mtu.

‘Ndio hapo, nachanganyikiwa..’akasema nesi

‘Sasa..?’ akauliza dada mtu.

‘Ni lazima nipata wasaa wa kuongea na huyo mama, kuna mama mwingine yupo hapo karibu yake anafanana sana na yule mama marehemu, nilitaka kujua kama ni ndugu yake, kama ni ndugu yake tutakuwa na ushahidi mnzuri tu, nitaongea naye nione…’akasema

‘Basi kaongee naye atatusaidia sana… na jingine huyu mtoto ana macho ya ajabu kweli…’akasema dada mtu.

‘Macho ya ajabu yapoje,..ya matatizo..?’ akauliza

‘Hapana ni mzuri tu…..basi baadaye..’akasema na kukata simu

 Ndio maana nesi akaongea na huyo mama akitarajia kupata ushahidi, na aliona kama huyo mama anamficha huenda ni kweli huyo mama ana ndugu kama huyo hata kama sio wa tumbo moja,..kwanini wafanane, akapanga kuja kuongea naye tena, hakujua kuwa mwenzake keshaondoka…na kichwani akawa akiwazia neno la mwisho la dada yake kuwa

‘Na jingine huyu mtoto ana macho ya ajabu kweli…’


NB: Haya sehemu hii iishie hapa, mtaona kama tunarudia rudia yaliyopita….lakini ndivyo kisa hiki kilivyo, ni kama tamithilia ya maisha, kuna kukumbuka, kuna kuulizana, kuna kurejea….naomba mjenge tabia ya mabadiliko, sio kila kitu ni lazima kiwe kama tulivyozoea, emu-three analeta yaliyotofauti kidogo..kihivyo


WAZO LA LEO: Upendo wa dhati ni ule wa kujaliana, kuhurumiana na kusameheana. Kukoseana kunatokea, kusigishana kwa hili na lile, ndio kiubinadmu maana tabia zinatofautiana,  ndugu kwa ndugu, mke na mume, wazazi kwa watoto, majirani, tunakoseana kwa hili na lile, ikitokea hivyo basi tukae tuongee tuone tatizo lipo wapi, turekebishane, tusameheane, tupendane na tuzizuliane ubaya, au kuona kuwa huyu hapati hiki au kile kwa masilahi yetu binafsi huo ni uchoyo na roho mbaya na ni dhambi kuwekeana mafundo, visasi na chuki zisizoisha moyoni, wanaofanya hivyo hawataweza kuuona ufalame wa mbinguni, pepo kwao itakuwa ni hadithi. 
Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

https://meserti.com/products/type/prod/query/benjamin-adams-london-astor-womens-ivory-silk/?tag=na035-35 -
benjamin adams london - astor (women's) - ivory silk

I was excited to discover this web site. I want to to thank you for ones time for this wonderful read!!

I definitely appreciated every part of it and i also have you
saved to fav to see new information on your website.