Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, March 30, 2015

NANI KAMA MAMA-51


 Nesi akiwa nyumbani kwake....ulikuwa ni muda wa mapumziko na wakati anataka kujipumzisha mara akasikia simu yake ikiita,kwa haraka akaichukua simu yale ilikuwa mezani, na kuangalia ni nani aliyemmpigia, akakuta ni ile namba ya nje, akaipokea kwa hamasa, akiwa amesimama, akasema

‘Halloh nani mwenzangu…’akauliza akiwa anajaribu kuwaza ni nani huyo

‘Mimi mliyekuwa mkimuita Docta Kijana…’sauti ikasema na nesi kusikia hivyo akapanua uso kwa furaha na ha akajikuta akisema;

‘Mhh, Docta Kijana,  hatimaye nimekupata....!’ nesi akajikuta akisema hivyo huku akitabasamu kama vile anamuona huyo anayepiga simu akajaribu kuvuta taswira ya dakitari huyo…

‘Unasema hatimaye umenipata, ...kwa vipi?’ sauti ikauliza na nesi akatikisa kichwa kama anakubali kitu, kuwa ndio mwenyewe, akasema;

‘Ni siku nyingi docta na nimekuwa anikikutafuta sana lakini sikuwa na namba yako..yaani ulichonifanyia, unaondoka bila kuniaga, nilikukosea nini ..’akasema nesi,  na kukawa kimia kidogo.

‘Samahani kwa hilo, yaliyotokea ilikuwa ni ghafla..na sikuwa na  nafasi ya kuagana, …yaani we acha tu, binadamu wana roho mabaya sana…hapa nilipo mawasiliano ni mabovu, kwahiyo ..hatutasikilizana vyema…’akasema

‘Sasa namba yangu uliipataje..kama uliweza kuondoka bila kuniaga na bado ulikuwa na namba yamngu muda wote huo kwanini usinipigie simu kuniambia ?’ akauliza nesi

‘Mimi nilipewa namba yako na….nesi yule rafiki yako..’akasema

‘Oh, kumbe mnawasiliana naye?’ akauliza nesi akiwa anakunja uso kwa kutokufuraha kauli hiyo

‘Hapana…imetokea kila nikipiga simu hapo hospitalini anayepokea ni huyo sister...na jana ndio kaweza kunipa namba yako..’akasema.

‘Sawa najua yule ni rafiki yako sana…’akasema nesi akiwa keshatahayari.

‘Hapana sio rafiki yangu….,kama alikuambia hivyo amekudanganya..siku ile ya mwisho alikuja kuniambia hivyo kuwa ananipenda..anataka tuwe wapenzi,..nilishangaa kidogo, alisema mengi..lakini sikuwa na muda wa kuongea naye, maana nilikuwa na mambo mengi kichwani, ..nilifurahi tu kwa vile ni yeye aligundua barua yangu ikiwa imefichwa..’akasema

‘Ilikuwa imefichwa na nani?’ akauliza nesi

‘Mmmh, ni hadithi ndefu, …ni huyo aliyekuwa mkuu wa hiyo hospitali…sijui kwanini alifanya hivyo, na bahati nzuri huyo nesi rafiki yako akaigundua hiyo barua na kuniletea,..ilionekana ilifika muda tu, na huyo mkuu akawa kaiweka kwenye droo za meza yake..nilipoipata nikamuuliza kwanini kafanya hivyo akadai yeye hajawahi kuiona..basi nikaona hakuna shida, …ndio huyo nesi akatumia nafasi hiyo kuniambia ammbo yake…’akasema

‘Oh pole sana kumbe ndio ilikuwa hivyo..huyu mtu kumbe mbaya sana ..ndio maana akanifanyia visa na kunitega….kumbe, ningelijua nisingelikubaliana naye..’akasema

‘Alikufanya nini?’ akauliza

‘We acha tu,….ila kanisaidia nikaenda kusoma…’akasema nesi

‘Hongera, najua sio bure..yule mtu hafanyi kitu bila gharama, kwa muda mfupi niliokaa hapaoo nilimgundua kuwa ni mtu mbaya…mbinafsi, anacheka mdomoni lakini moyoni ana roho mbaya….nilikuja kugundua kuwa anafanya biashara ya dawa, nilimfuma siku moja akishirikiana na yule nesi mkuu, akaniambia eti wanazipeleka bohari zina makosa…kumbe ndio biashara yao,….wanaiba dawa za hospitalini na kuziuza kwa wenye mahospitali au maduka ya dawa mitaani’akasema

‘Mhh, …kumbe ulikuwa unajua hilo, na kumbe walikuwa wakishirikiana na nesi mkuu..ohh, ndio maana kumbee…’akasema nesi akionyesha mshangao.

‘Yah, yule alikuwa mtu wake wa karibu sana, na ndiye aliyekuwa akimkuwadia….najua yote hayo, lakini niliona kwangu haina maana, …nikawa kimia,…niligundua kuwa hiyo hospitali ina viongozi wabovu, wenye tamaa binafsi, …ndio maana nilitaka usome uhame hapo,..’akasema

‘Mhh, mbona hukuniambia hayo mapema..’akasema nesi .

‘Sikutaka kukuingilia maisha yako, na kujiingiza kwenye umbea, sikuja hapo kwa kazi hiyo…na yule rafiki yako ndiye alikuwa akijaribu sana kuwa karibu na mimi, nilimkwepa sana…hadi siku ya mwisho aliponieletea hiyo barua…unajua nilimshukuru sana, maana bila yeye ingekuwaje, lakini sikuwa na muda naye..ni hivyo tu…’akasema

‘Mhh, mbona kaniambia kuwa mnaelewana sana..’akasema

‘Sio kweli….mimi nilishakuambia msimamo wangu..sasa sister sikiliza naona muda utakwisha kabla sijakuambia la msingi…, mimi nilikuwa nakupigia simu kukuulizia maswala ya yule mtoto… na kumbukumbu nyingine na ….’akasema.

‘Mtoto gani , mtoto wetu…?’ nesi akajikuta akisema
hivyo.

‘Mtoto wetu!?’ akauliza docta kwa mshangao.

‘Wewe umesemaje..?’ akauliza nesi

‘Kuna yule mtoto uliyemchukua wewe ukasema unampeleka kwa dada yako. Unakumbuka?’ akasema Docta Kijana,…

‘Mhh, ndio nakumbuka…..’akasema nesi huku akikaa vyema kwenye kiti, na kukunja nne.. moyoni akiwa na hamasa ya kutaka kujua mengi na kuongea mengi ikibidi.

‘Ni kweli ni siku nyingi, lakini hata mimi nilikuwa nahangaika kukutafuta….kwanza nilimpata nesi mwenzako, ..naona kila nikipiga yeye anakuwa hewani, yeye ndio mpokeaji simu siku hizi…?’ akauliza

‘Mhh..hapana anasaidia saidia tu kama yule muhusika hayupo,..’akasema nesi

‘Basi ….yeye mara ya kwanza nilimuomba niongee na wewe akasema upo masomoni, na ….wewe na huyo mkuu ni ..marafiki,..au….nikamwambia anipe namba yako akasema hana…na komputa yangu niliyokuja nayo huku ambayo niliweka namba zenu na kila kitu ilinigomea, imeharibika…nahisi wakati naondoka kwa haraka niliigonga mahali….’akatulia

Nesi, aliposikia hivyo kuwa hata huyo dakitari alikuwa akimtafuta moyo wake ukawa unamdunda isivyo kawaida…kumbe mwenzake aliwahi kuambia atoe namba yake lakini hakupenda kuitoa…akawa na fundo, akapanga akitoka hapo atakwenda kupambana na huyo aliyekuwa rafiki yake kwanini alimfanyia hivyo…alijikuta badala ya kusikiliza anachoulizwa akajiona anajawa na hasira, na alipoligundua kosa lake akasema kwa sauti ya kukwaruza hadi iakbidi akohoe kwanza….

‘Sijui hata nisemeji, nina hamu sana ya kuongea na wewe nina mambo mengi ya kukuambia, mimi nilijua umeshanisaahu,..kumbe ni huyu aliyekuwa rafiki yangu, ngoja, nitakutana naye…hebu nikuulize hujaoa mke wa kizungu huko, ...?’akajikuta amesema hivyo.

‘Sister acha utani wako , mimi nipo huku kwa ajili ya kusoma, ….bado muda wangu wa kuoa kabisaaa..bado sana….’akasema na mara kukawa na mawasiliano mabovu, na docta akawa anaita halloh, na nesi naye halloh, na baadaye, docta akasema;

‘Halloh, sister upo,..naona kuna mawasiliano mabovu, …ila cha muhimu nilikuwa  naulizia kuhusu yule mtoto…je hajambo?’ sauti ikauliza tena lakini nesi akawa hakusikia vyema, akajua anasalimiwa, ila alisikia kitu kama mtoto, akasema;.

‘Sijambo docta,….unasema nini, kuhusu mtoto, …yupi ooh..mtoto wetu…?..aah yule mtoto, tena hilo ndilo nataka kuongea na wewe…?’akasema nesi

‘Ana matatizo yoyote?’ akauliza docta

‘Hana matatizo, yupo kwa dada yangu… analelewa na watu wenye upendo, kwahiyo hilo lisikutie wasiwasi, ila nilitaka kukuulizia kuhusu yule mama, aliyetoroka hospitali, mama mzazi wa huyo mtoto, kumbukumbu zake zipo wapi…’ akauliza harakaharaka.

‘Kwanza nikuulie kwanini unarudia kusema mtoto wetu,..kwani tulikuwa na mtoto mimi na wewe,  mimi ninayemzungumzia ni yule mtoto ambaye alizaliwa na yule mama, halafu mama yake akatoweka.....hivi ilikuwaje badaye?’akaulizwa.

‘Yule mama …..mm hata sijui nikuambie nini…yametokea mengi sana…’akasema nesi na mara kukawa hakuna mawasiliano, na baadaye mawasiliano yalipokuwa shwari docta akasema

‘Oh, nimkuelewa…,japo mawasiliano sio mazuri....’akasema docta

‘Sasa docta mimi huku kuna tatizo …na tatizo hilo linahitajia zile kumbukumbu za yule mama na mtoto wake zipo wapi?’ akauliza

‘Kumbukumbu zile nilikuambia kuwa niliziweka kwenye kabati linalohifadhiwa nyaraka muhimu…lilikuwa kabati namba tano , yale makabati yalikuwa na namba…na huyo mama imekuwaje?.’akasema na kuuliza lakini swali la mwisho nesi hakulisikia vyema, nesi akasema;

‘Makabati yale yalihamishwa na nyaraka karibu zote zimepotea..na zilizopo zimeharibika kabisa… na umeulizaje tena..?’akasema nesi

‘Mhhh...hilo sasa ni tatizo , hata sina jinsi nyingine ya kuzipata, maana nilijua hiyo ndio sehemu salama....nahitajia kumbukumbu za yule mama ndilo muhimu …’akasema docta.

‘Lakini wewe siulisema…kwenye komputa yako kuna kumbukumbu..ooh, ndio umesema imeharibika, bahati mbaya, sijui itakuwaje…’akasema nesi, na alihisi kama hakuna mawasiliaono akawa anasema halloh, hallow na mara , docta akasema;

‘Halloh, nipo, nasema hivi…kama waliondoa kumbukumbu zilizokuwemo kwenye lile kabati.. basi kuna mahali wamezihifadhi, labda kwenye maboksi ya kumbukumbu za  zamani mwambie muhusika akajaribu kuzitafuta huko atazipata tu…’akasema

‘Hazipo….na hapo kwenye store ni nyumba ya panya,..kiujumla kumbukumbu hizo zimepotea kabisa....’akasema nesi.

‘Oh, nesi kuna siku niliwapigia hapo hospitalini, kuhusu kumbukumbu za zamani kipindi kidogo, kwasababu komputa niliyokuwa nimehifadhia hizo kumbukumbu iliharibika, na kulikuwa na kumbukumbu zangu nyingi,..na zinenisaidia kwenye masomo yangu,..wakasema watanitafutia…..lakini kila nikipiga inakuwa jibu ni hilo hilo…’akasema!

‘Huwezi kuzipta, hilo mimi nakuambia, naona kama ni njama za kuhakikisha kumbukumbu zote za zamani hazipatikani..’akasema

‘Njama, kwanini njama?’ akauliza docta

‘Kuna mambo mengi yametokea, hata wale viongozi wa zamani hawapo tena..ni kutokana na utawala wao mbovu, …na mengi hata sitaweza kukuambia kwa leo..’akasema nesi

‘Oh, basi itabidi niingie gharama tu ya kuitengenezesha komputa yangu ya zamani…maana kuna mambo yangu muhimi sitaki yapotee…na humo nitaweza kupata kumbukumbu zote za huyo mama…mimi nilijua tu, huo uatawala utakuja kuondoka, …kulikuwa na mambo machafu hapo, nilijaribu kutoa ushauri ndio nikawa adui….’akasema

‘Pole sana…docta sasa hebu niambie yule mama….anafananaje usoni…?’ akauliza nesi

‘Macho…’sauti ikakatika..na simu ikawa haipo hewani, akarabi kuita lakini wapi, akaweka salio akapiga ikawa haiptaikani kabisa.

`Macho yana nini….?’ Akauliza nesi akiwazia ni kitu gani docta alitaka kumuambia, na akaanzia na neno macho.

‘Macho….ana maana gani alitaka kuniambia nini kuhusu macho…?’nesi  akawa anajiuliza, akaona arudi wodini tena kumuangalia yule mama mwingine anayemshuku kuwa huenda …maana huyo mama wanaymezngumiz ani marehemu, na haikuwa n hata haja ya kumuuliza docta, akakumbuka kuwa hakuwahi kumuambia huyo docta kuwa huyo mama ni marehemu, alihis huenda alishaambiwa na hao aliowapigia mwanzoni.

Kwa vile siku hiyo aliipanga rasmi kwa kuongea na huyo mama mwingine ambaye aliungua na moto alitaka kujua kama alikuwa na mahusiano yoyote na yule mama aliyewahi kufika hapo akapotea, na kujulikana kuwa amefariki kwani kwa uoni wake wanafanana sana.

Basi akaingia wodini, na kwa muda huo huyo mama alitoka nje, yeye alikuwa hajifuniki kujificha maana hata yeye alikuwa na makovu ya kuungua usoni, na uzuri wa huyo mama, yeye aliweza kutembea tembea, basi alipoona hayupo, akaona atoke nje, atarudi baadaye kwani yule mama wa mitaani alikuwa amelala, hakutaka kumsumbua, akamtupia jicho la haraka na kuondoka humo wodini, na wakati anatoka akakutana na huyo mama mwingine akiwa anarudi huko alipokuwa, na mazungumo yakaanzia hapo.

 Nesi akajaribu kumuelezea kuhusu kitu anachotaka kumuulizia, kuwa hapo kipindi kidogo kulikuwa na mama alifika hapo kujifungua ,lakini mama huyo alitoroka na baadaye wakapata taarifa kuwa amekufa, sasa je hakuwa an ndugu wa namna hiyo

‘Hapana..mimi kwetu ndiye mkubwa na wengine wote ni watoto wa kiume, bahati mbaya nikaja kuolewa na mume mkorofi mlevi..ndugu zangu wa kiume walinikata sana nikawa mbishi, na matokea yake ndio haya..’akasema kwa uchungu.

‘Mhh, mnafanana sana na huyo mama nilijua ni wewe..’akasema nesi

‘Hapana siwezi kukudanganya sio mimi…nilisikia mkiongea na yule,..yule mama ana matatizo gani, maana usiku anapiga kelele..na jana na juzi akilala, anakuwa kama anaongea peke yake, masikini mdada naye kaungua kama mimi,….’akasema kwa uchungu

 ‘Kwani unamfahamu huyo mama…’ akauliza nesi

‘Namemfahamia hapahapa tu..huwa namuita dada…’akasema

‘Hivi niambie kwanza wewe ilikuwaje..mana sijawahi kupata muda wa kuongea na wewe vyema, huenda ukanisaidia jambo?’ akauliza nesi

‘Mimi niliunguzwa na maji ya moto na mume wake, mume wake akilewa anakuwa na hasira za haraka haraka, …ameshauriwa asinywe, lakini ndio hivyo..basi siku hiyo, aliporudi toka ulevini, akakuta chakula hakijaiva na maji ya kusongea ugali yapo jikoni yakiwa yanachemka..’akatulia akikunuja uso, kama kuhisi hiyo hali.

‘Basi mume wangu kutokana na ulevi wake, na hasira akayachukua yale maji kutoka jikoni akanimwagia…na yeye katika kunimwangaia yakamwagikia..maana aliungua mkono,…akahisi kuungua vidole, akaachia sufuria, maji yakamuunguza na yeye mwenyewe, halafu akapepesuka na kudondokea jikoni, akaungua vibaya sana hata kuliko mkewe ..’akasema huyo mama.

‘Kaadhibiwa kwa ubaya wake..’akasema nesi

‘Ni zaidi ya kuadhibiwa ukimuona utamuonea huruma..’akasema

‘nimeshamuona , sikujua ndio mume wako….ni yule mwanaume aliyeungua vibaya sana na ana pingu mkononi?’ akauliza nesi

‘Ndiye mume wangu ndio ana pingu mkononi kwani ana kesi ya kujibu…., sasa hivi nilitoka kumsalimia, lakini ndio hivyo yupo kwenye ulinzi, …siunajua tena mambo ya kisheria, …najua akiruhusiwa tutayamaliza kienyeji maana aliyafanya hayo kwa ulevi tu…mimi nimeshamsamehe’akasema huyo mama kwa sauti ya upole, anaonekana ni mama mpole sana.

‘Yaani upo tayari myamalize kienyeji, ..kwa jindi alivyokufanyia hivyo…? mtu kakumwangalia maji ya moto, huoni angekupofua kabisa…., hapana usikubalia, kwanini nyie akina mama mnaonewa halafu mnakuja kukubali kirahisi hamuoni mnafuga huo ugonjwa,..?’ akadadisi yule nesi.

‘Mhh…sasa mtu nimeshazaa naye…na hata nikirudi kwa ndugu zangu hawatanipokea tena..na nikifanya hivyo watoto wangu watakuja kuishi na mama mwingine huenda asiwepende…hapana ni heri yaishe kienjeji, najua atakuja kujirudi na kuacha huo ulevi, …na nitarudi kwanini,  maana nilishawageuka ndugu zangu tulipanga nisiolewe, mimi nikatoroka..,..sikuwasikiliza, ni bora tu niishi  na mume wangu maana nimeshamzoea, tatizo ni ulevi tu… na ipo siku litakwisha tu…’akasema

‘Haya hilo ni lako, kama upo taayri kufa kwa ajili ya huyo mlevi usija kujutia baadaye…Hebu niambia kuhusu jirani yako pale pembeni unamuonaje?’ akamuliza nesi, na yule mama akamuangalai nesi kama vile anataka kujua ni nani, lakini akakumbuka jirani yake humo ndani ni mmoja tu, akasema;

‘Oooh , yule mama, unajua mwanzoni alikuwa haongeia kabisa, lakini amekuwa rafiki yangu maana kila ninacholetewa ninampa nay eye….sasa kawa rafiki yangu kweli, na jana akanisimulia kuwa ana uhakika alikuwa na kichanga’akasema

‘Kichanga, una maana mtoto?’ akauliza

‘Ndio …lakini mazungumzo hayo hayakuoendelea , kwani wakati tunaongea dakitari alikuja, tukakatisha mazungumzo na sikuwahi kumuulizia tena…nakumbuka kitu kama hicho…’ akasema huyo mama

‘Alisema aliwahi kujifungua hapa, kwenye hii hospitali? ….au ilikuwa hospitalini nyingine…?’ akauliza nesi akiwa na shauku sana.

‘Mimi sijui, sikuweza kumdadisi zaidi..kama nilivyokuambia dakitari alifika, basi ikabidi tukatishe mazungumzo yetu…, kwani vipi mbona unamuulizia sana mambo yake…’ akasema huyo mama.

‘Mhh, unajua huyu mama ananichanganya, hata kama alipoteza kichanga, kwanini aninyoshee kidole mimi na hakuwahi kukuambia alipotezaje,..au ilikuwa mara ya kwanza kuongea naye mazungumzo kama hayo..?’ akauliza nesi

‘Si kama nilivyokuambia kipindi cha nyuma alikuwa haongeai kabisa..sasa kuanza kuongea ni juzi na jana, ..juzi ilikuwa kuulizana hali tu...jana ndio kasema hayo, na sikuwahi kumdadisi zaidi..’akasema..


‘Mhh, kuna kazi, nilijua nitayamaliza hayo,…. lakini kama bado anaendelea na msimamo wake huo nahisi kuna jambo,..’akasema nesi na yule mama akawa anageuka kutaka kuondoka, na nesi akamuuliza

‘Pamoja na hayo ana kitu gani kingine cha ajabu, na je uliwahi kumuona sura yake?’ akamuuliza

‘Sura yake hapana…anajichunga sana asionekane sura yake…ila anaota sana usiku anakuwa kama anaongea na mtu hivi

‘Anaota, unajuaje kuwa anaota….?’akasema

‘Maana unasikia sauti na mazungumzo..mara anambembeleza mtoto…wkati mwingine kama anajibishana na watu…., husiki sauti ya mtu mwingine unasikia yeye akijibu au kuongea na mtu, ukiangalia huoni huyo mtu mwingine..sasa hapo naona kama anaota..’akasema

‘Mhh, ndio zake hizo docta ansema ndio dalili za kurejea kumbukumbu zake…je hakuna wimbo wowote anaimba..? ’akauliza nesi

‘Kuimba wimbo!?’ akauliza huyo mama kwa mshangao

‘Huwa alikuwa kama anaimba wimbo hivi akisema anamtaka mtoto wake…’ akasema

‘Anaongea kitu kama hicho, na docta alipokuja jana wakakaa wakawa wanaongea vizuri tu, na alikuwa akimsimulia kuhusu huyo mtoto wake..na inaonekana wanaelewana vyema na huyo dakitari…kiujumla huyo mama kabadilika kabisa, anaongea kama kawaida….’akaambiwa

‘Kuhusu huyo mtoto, ina maana hata docta keshamini kuwa huyo mama ana mtoto na kachukuliwa hapa?’ akauliza

‘Kwa jinsi nilivyosikia …docta keshaamini kuwa kweli huyo mama ana mtoto, na docta akaahidi kuwa mtoto wake atapatika tu,..sasa sijui ni hapa au ni wapi…’akasema huyo mama, na nesi akahisi kuchanganyikiwa, akageuka kuangalia kule wodini, akasema

‘Ngoja nikaongee na huyo mama aniambie mwenyewe kuhusu huyo mtoto maana sasa atanichanganya, mimi sijawahi kumchukua mtoto wake…kwanini aendele kusema mimi ndiye nimechukua mtoto wake…sasa ataniambia kama kachanganyikiwa itaonekana wazi..sikubali…’akasema na kugeuka kurudi wodini.

Na kabla hajaingia ndani kabisa akamuona yule dakitari mkuu, akija na yule dakitari alionekana kunyiosha mkono kama ishara kuwa huyo nesi amsubirie na nesi ikawa kama hamsikii akawa keshaiingia wodini tayari kwenda kupambana na huyo mama…

Na wakati anakaribia kitanda cha huyo mama mara simu yake ikalia, akawa anaipuuza lakini alipoona inaita sana, akaitizama maana alikuwa nayo mkononi, akaona ni namba ya ndugu zake kijijini, akawa kasha fika kitandani, akaona ngoja aisikilize kwanza;

‘Halloh, …’akaita na aliyekuwa hewani ni dada yake, akasema;

‘Nina habari nzuri…lakini pia tunataka kuja kukutembelea  na mtoto, ..tumeona tuje mtoto amuone mlezi wake. Maana analia lia sana...’wakasema

‘H-h-hapana…’akasema na mara docta akawa ameshafika,…


WAZO LA LEO:Kutoa taarifa za uwongo ili kujipatia kitu, au kuonekana wewe ni zaidi au kwa ajili ya kujulikana na watu ili kupata kura, umaarufu… au jambo lolote huo ni wizi, na sio tabia njema, na tabia hiyo inaonyesha wewe humuogopi mungu, wewe sio mwaminifu..na haufai kuongoza jamii.Kuna watu wana tabia hizo na wanaona ni jambo rahisi tu kumzulia mwingine uwongo, au kuzua jambo, kuahidi uwongo,… ili tu kuonekane tunaweza…au sisi ni zaidi, ..au kitu fulani hakifai , kisipitishwe, hii ni tabia iliyojengeka sasa ya propaganga potofu, tukumbuke tabia hiyo ni unafiki na njia za mnafiki ni fupi tu..

Ni mimi: emu-three

No comments :