Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 24, 2015

NANI KAMA MAMA-48‘Kuna taarifa za kutatanisha kuhusu huyo mama, lakini mimi siwezi kukuambia nitaarifa gani….’ Aliambiwa na nesi mkuu

Sasa leo karudi toka kijijini mara kakutana na shoga yake na kupewa taarifa kuwa kuna jambo, lakini kama alivyo nesi, naye shoga yake hakutaka kumuambia ukweli

‘Hivi umesikia kilichotokea..?’ akaulizwa shoga yake na nesi akamuangalia shoga yake wa zamani kutaka kusikia zaidi, akauliza;

‘Kuhusu nini?’ akauliza

‘Ina maana hujui,…?!’ akaulizwa shoga wake kwa mshangao, na hata alivyojaribu kuadadisi zaidi hakupata jibu kuwa kuna kitu gani kimetokea….`              

Hata hivyo nesi hakutilia maanani kwani alijua huyo ni mmoja wa wapinzani wake…na kicghwani alishajaa mawimbi, kuhusu kuondoka kwa dakitari kijana bila kumpa taarifa….huyoo, moja kwa moja…,akaelekea ofisi anapofanyia kazi, na kukutana na mmoja wa wafanyakazi wenzake, na hapo akaambiwa…

‘Ulikuwa unahitajiwa kwa mkuu wa hospitali…’

‘Una maana kwa Dakitari mkuu wa hospitali, kuna nini tena huko..?’ akauliza

‘Mhh, najua..hapa hospitalini siku hizi kuna mambo ya siri-siri, na kila mmoja anaogopa maana huyo nesi mkuu na sikio la utawala, ukijifanya uan mdomo mrefu…mmmh, ngoja hata nisiongee mengi..’akasema

‘Lakini najiuliza mbona ndio nimefika tu, halafu naitwa, na inaonekana kuna jambo limetokea lakini wenzangu hamtaki kuniambia..’akasema
‘Mimi sijui, ila tu uwe makini na huyo dakitari mkuu….anapenda dodgo dogo…aijui mke wake hamtoshelezi..’akasema

‘Mhh….unanitisha…’akasema na kabla hajatulia vyema, mara, akaja mfanyakazi ambaye kazi yake ni kutumwa huku na kule(tarishi wa ofisini) akamwambia;
         
‘Nesi unaitwa ofisini kwa dakitari mkuu, haraka…’….

Hiyo kauli ilimfanya nesi ashutuke, kwani ni amri, na mtoaji  hiyo kauli sio mtu wa kutoa amri kihivyo, ila kawaida yeye ni mjumbe tu, kwahiyo kaitamka,kama ilivyo, na  inaonyesha ina msisitizo.

Tuendelee na kisa chetu.
**************

‘Kwani kuna nini?’nesi akamuulize yule mjumbe

‘Mhh, sister wangu… hata sijui,..kazi yangu ni kufikisha ujumbe, … nimeitwa na mkuu, kufika ofisini kwake akanipa huo ujumbe….ila kwa kukutonya, …sio umbea, nakuambia wewe kwa vile ni sister wangu,  naona pale ofisini kwake kuna mgeni au….wageni.. .’akasema

‘Kuna mgeni, au wageni gani?’ akauliza nesi

‘Niliyemuona kwa uwazi, ni huyo mmoja,…yule pale..niiii, naona ni ofisa usalama japokuwa hajavaa mavazi yake rasmi,..nasikia siku hizi ndiye mkuu wa kituo, kazi ipo, … hata kama hajavaa yale manguo yao, mimi namatambua…’akasema

‘Ofisa usalama! Mkuu wa kituo! Mhh ni yule jamaa watu wanasema ana roho mbaya..mmmh, sasa kuna kitu gani tena jamani…’akasema nesi

‘Bora nenda sister wangu mungu yupo pamoja na wewe, kwa hivi sasa nakushauri, usijitwike mzigo kabla haujatua kichwani..’ akasema huyo mjumbe, na kuondoka zake.

Nesi akapitia maliwatoni,(washroom), akajiweka sawa, na kwaharaka akatoka na kuanza kutembea kuelekea ofisi ya dakitari mkuu, na wafanyakazi wa hapo wanajua ukienda hiyo ofisi kuna mawili, kupewa barua ya majukuu mapya, au kufukuzwa kazi…

*************
  Nesi akiendelea kukumbuka tukio hilo ambalo hakupenda lijirudie tena kichwani kwa jinsi lilivyo, akageuka kuwaangalia, mabosi wake ambao walikuwa wakiendelea na kazi nyingine wakisubiria yeye atoe melezo waliyoyataka, na akaona asiwapotezee muda wao, akasema;

‘Bosi zangu, mimi naomba mnipe muda niweze kulifikiria hili tukio vyema, maana kipindi hicho sikuwepo peke yangu, walikuwepo wakubwa zangu wa kazi na kipindi hicho mimi nilikuwa nesi wa kawaida tu…., na kama ni hilo tukio la huyo mama, ambaye nina imani sio huyu, basi ni jukumu ambalo lipo juu ya uwezo wangu….’akasema nesi

‘Lakini ukisema hivyo, ina maanisha nini, kuwa ni jambo ambalo wewe ulipewa maagizo tu na hukuwa na hiari nalo..na unaogopa nini kutuambia, maana sisi ni wakubwa wako hapa na tuypo tayari kubeba hilo jukumu, kwani livyokuwa, ilikuwa sio kikazi, yaani lilitokea kibinafsi zaidi, au kuna nini?’ akaulizwa

‘Tafadhali wakubwa zangu, kwa hilo naombeni sana mniwie radhi, sitaweza kusema lolote mpaka nijirizishe kutoka kwao…’akasema nesi na wale madakitari wakaangaliana na halafu wote wakamgeukia nesi na dakitari bingwa akauliza;

‘Unahitajia siku ngapi..maana hapa tunapambana na muda, sio kwamba nakushurutisha kusema ...hapana lakini ni muhimu kwetu…mgonjwa anahitajia huduma, na moja ya huduma ni kujaribu kuangalia yale anayoyahitajia, kama yana uzito basi ni muhimu tumtimizie….pili ana toa shutuma kwako…’akasema dakitari huyo.

‘Lakini shutuma zake sio za kweli….’akajitetea nesi

‘Na tatu, kutokana na kazi yangu, kama jambo lina utata, tunahitajia kufanya uchunguzi, kwa lengo la kumsaidia mgonjwa ili aweze kukumbuka vyema ..na hili linaonekana lina utata…’akasema

‘Mimi naona ni kuchanganyikiwa tu akiwa sawa, hilo tatizo litaisha..’akasema nesi.


‘Nesi unayeongea naye ni dakitari bingwa wa maswala hayo,…mimi najua kabisa kuna kitu kilitokea kwa huyu mama,…na ukumbuke kuwa mgonjwa bado anadai kuwa wewe ndiye uliyemchkua mtoto wake,..sasa tuchukulie kaona hayo madai ni kweli akiamua kwenda kushitaki polisi sisi tutajiteteaje…’akasema huyo dakitari.

‘Sasa mnataka mimi nifanye nini, maana nimejaribu kuwafahamisha halai halisi…mimi ninachowamboa, kwa nia njema tufanye tufanyalo… ili tuvute muda, mimi nitajitahidi kuwasiliana na wakubwa waliokuwepo, kipindi hicho, wote hata sijui wapo wapi hivi sasa…’akatulia na wale madakitari wakaangaliana tena.

‘Lakini nitaulizia watu wanaowafahamu… na ili na mimi nipate …kujirizisha mwenyewe, kiukweli huyu mama ana lake jambo sio bure, …kama ni hilo tukio huyo mama sio huyu, huyu ni mwingine kabisa,…hyule mama alikufa, sasa huyu katoka wapi’akazidi kusisistiza na dakitari bingwa ajkatabasamu na kugeuka kuangalia dirishani, huku akisema.

‘Wewe unasema huyo mama alikufa akazikwa na unadai kuwa kuna mfanyakazi, alikuwepo, ambaye alihudhuria hayo mazishi, huyo mfanyakazi bado yupo hapa?’ akaulizwa

‘Hapana, hayupo,…’akasema

‘Na hatuna jinsi ya kumpata…?’ akaulizwa

‘Hata sijui yupo wapi  siku hizi…nitajaribu kutafuta kama kuna mtu anafahamu wapi alipo, lakini ni mtu aliyekuwa akiaminika, ..’akasema

‘Kwa vipi?’ akaulizwa na huyo dakitari mwingine

‘Alikuwa ndiye nesi mkuu kipindi hicho…’akasema

‘Mhhh, naona manesi wakuu, mna kazi kubwa hapa, kuficha siri eeh….sasa tusipoteze muda wewe jitahidi leo …eeeh, au…eeh...kesho..mmmh, utaweza kutupatia hiyo taarifa lini hivi…?’ akaulizwa

‘Kesho nitawaambia kama naweza kuelezea ilivyokuwa nikikumbuka kila kitu…., kama nitashindwa, basi nitawaunganisha na hao wakubwa waliokuwepo muongee nao wenyewe, maana nisibebe jukumu ambalo sina uwezo nao…’akasema

‘Kwanini usituunganishie tukaongea nao hao waliokuwepo kwenye hilo tukio moja kwa moja…kwani kipindi hicho dakitari mkuu alikuwa nani..?’ akauliza dakitari bingwa

‘Bosi,..tafadhali..naona unataka kucheza mchezo wa askari kanzu..nieleweni jamani, hilo hata nyie mngelikuwepo, mngajikuta hivyo hivyo….., sio jambo la kujitakia, lakini ilibidi ifanyike hivyo, sasa msinibebeshe lawama…na bado nashindwa kujua kwanini mnalivalia njuga wakati nimeshawaelewesha kuwa huyo mama alishafariki….’akasema akiona kama kukerwa, lakini kwa vile hao ni mabosi wake, akawa haongei sauti ya hasira.

‘Ok tumekuelewa nesi…., haya nenda kafuatilie…na, kesho nahitajia taarifa ya kwamba imewezekana au la…basi kama haiwezekani..huna budu…. itabidi utusimulie kisa chote ili sisi tujue ni nini cha kufanya…vinginevyo, tutamwambia huyo mama ashitaki kwa utawala, au aende polisi…..’akasema na nesi akatoka hapo ofisini akiwa hata hajui aanzie wapi na hapo akakumbuka tahadhari ya aliyekuwa mkuu wa hospitali hiyo kipindi hicho;

 ‘Hata itokee vipi, usije kusema lolote, au kunitaja mimi au mkuu wa kituo…hili liwe kama halikuwahi kutokea,…. maana hii inawezeza kuchukuliwa kama kesi ya kuua bila kukusudia, au sio mkuu, na imetokana na uzembe wako…’

 Na hapo kumbukumbu za siku ile zikaanza kurejea kichwani,..na kuanza kukumbuka pale alipoambiwa na mjumbe aliyetumwa kuwa anahitajika kwa dakitari mkuu kwa haraka, ….

************

Nesi kwa haraka akaelekea huko kwa dakitari mkuu, …ambaye ndiye kiongozi mku wa hiyo hospitali, na alipofika kwa adabu akagonga mlango, …alipogonga mara tatu bila kusikia sauti ya karibu, yeye akafungua mlango….., akaingia ndani na hata kabla hajasalimiana na hao waliokuwepo,  akaambiwa;

‘Nesi karibu na funga huo mlango….’ilikuwa sauti ya dakitari mkuu, na alipogeuza macho pembeni akamuona jamaa mmoja kashikili gazeti, likiwa limemziba kabisa uso wake, ila aliposikia hiyo karibu, akashuka lile gazeti na kumtumpia macho huyo nesi, halafu akendelea kusoma lile gazeti sasa akiwa kalishusha na kuweka sehemu ya uso wake wazi...huku akishika shika kikombe cha chai

Nesi kwa haraka akamtambua ni nina huyo jamaa…, akamkumbuka, alikuwa afisa usalama wa kituo cha hapo kwao, na baadaye wakasikia kuwa kawa mkuu wa hicho kituo, Huyu ofisa, wengi wanamuogopa…anajulikana kwa roho mbaya, mara nyingi kesi ikienda kwake ujue wewe umefungwa.

‘Huyu ni  mkuu wa kituo..wengi hawajalifahamu hilo, bado wakimuona wanamtambua kama ofisa usalama, sasa hivi ndiye mkuu wa kituo, baada ya yule wa mwanzo kustaafu…’akasema na nesi akasogea na kunyosha mkono kumsalimia na yule ofisa akasimama na kuupokea huko mkono,

‘Haya kaa hapo kwenye kiti maana hili tunalotaka kuliongelea hapa ni muhimu sana..ofisa …ooh, mkuu, samahani, mkuu wa kituo…kaja na taarifa…taarifa hiyo ni nzito sana..’akaanza kuongea dakitari mkuu.

‘Kiujumla tukio lile, nikisema hivyo natumai umenielewa, tukio lililokupeleka kijijini, ..la huyo mama aliyepotea lilipotokea tulijaribu kufuata taratibu zote…..’akasema dakitari mkuu akigeuka kumuangalia huyo mkuu wa kituo, halafu tena anageuka kumuangalia nesi.

‘Ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kituoni,na uzuri aliyefikishiwa taarifa hizo ni huyu rafiki yangu, ..ni rafiki yangu, tumesoma naye huko shule ya msingi mwenzangu akajiunga na usalama, na mimi kwenye utabibu..lakini hapa hatuzungumzii urafiki tena..’akasema akimkazia nesi macho.

‘Sasa ni hivi…, baada ya lile tukio, askari wa usalama wakafanya uchunguzi, lakini huyo mama hakupatikana, ikawekwa kama tahadhari kuwa atakayemuona au kuona dalili za wapi huyo mama kaelekea taarifa zifike kwa walengwa…yaani polisi…lakini huyo mama hakupatikana kwa siku …mbili eeh..kitu kama hicho…’akasema

‘Wakati hayo yanaendelea sisi kama utawala, tukapata wazo,…hasa kuhusu huyo mtoto mchanga…atakwenda wapi , ni nani wa kumlea..tukaongea tukaona wazo hilo tulilolifanya linafaa…mimi nikamfahamisha ofisa usalama..ambaye alifikisha ujumbe kwa mkuu wake …, akasema kwa hali ilivyo, huyo mtoto ni wetu, tufanye kile tunachoona kinafaa…, maana mtoto yule angechukuliwa na nani…unaona ilivyo…’akasema dakitari mkuu akimwangalia huyo mkuu, halafu nesi.

‘Sasa taarifa zimefika, huyo mama kaokotwa njiani, bondeni, kafariki…’akasema

‘Ohh, mungu wangu, mama wa watu jamani….mungu nisamehe jamani...sikufanya makusudi…najuata kwanini niliondoka kufuata hizo dawa…..isingelitokea hayo…’nesi akaanza kulia.

‘Mhhh, hatutaki kilio hapa..unasikia, imeshatokea, na ni uzembe wako…, lakini tutafanyaje, na tumeongea na mwenzangu hapa tukaona, kifo kimeshatokea, na..hata tufanyeje,..haitasaidia kitu..sasa tufanyeje..sisi tukaoana tuendelee kubeba hili jukumu…kinamna tuonavyo ni sahihi…’akatulia

‘Maana ilivyo ilitakiwa wewe ukalale rumande, huku uchunguzi unafanyika, lakini tukaona mtoto mrembo kama wewe..hapana, na pia tumekwisha kupa jukumu la kulea huyo mtoto..hatujui hilo kuwa umempa dada yako..maana tukisema hivyo ina maana kumbe wewe unaweza kwenda jela kwa uzembe wako…tunajua wewe huyo mtoto unaye, na ukienda jela mtoto atalelewa na nani’akasema

‘Lakini tujiulize kwa hali kama hiyo, je isingliweza kutokea kwa yoyote yule kama angelikuwa kwenye nafasi yako…ni makosa ndio, ni uzembe ndio…lakini..inatokea,…kiujumla mimi kama unavyonifahamu sitaki uzembe...lakini kwa nia ya kumsaidia mtoto,…tuendelee kulinyamazia hili kuwa mtoto hayupo…’akasema huku akigeuka kumuangalia huyo ofisa ambaye alikuwa kaangalia nje kwa kupitia dirishani.

‘Imebidi tufanye tufanyalo…ni hatari kiutendaji, usione tunaamua kubeba hili jukumu tu, na kwa namna nyingine pia ni gharama..watu wanaojua wote wanatakiwa kunyamazishwa..sasa ni ..anyway …ni hatari…’akatulia halafu akasema

‘Sasa usikie nesi, sisi kwa kukujali wewe, tukaona tubebe hilo jukumu…utasema kwanini…sikiliza huyo mtoto anahitajia huduma, na familia anayotoka huyo mama ni masikini,masikini kweli..….ina maana kama tutaamua kumpeleka huyo mtoto huko na kusema mtoto wenu huyu…sijui kama ataishi, wanaweza hata kumuua…’akasema

‘Unajua..nesi mambo mengine inabidi yafanyike kihivyo…ndio maana nimekuita hapa usikie vyema..sasa…hili tumelifanya kama siri, ndio maana nikakuita wewe, na sikutaka mtu mwingine, kiujumla huyo mtoto hakuzaliwa hai…unasikia,  huyo mtoto hakufanya nini..?’ akaulizwa

‘Lakini..’nesi akaanza kujitetea.

‘Kama hutaki, basi ongozana na huyo mtu wa usalama mkaandikishane, ukiri wewe mwenyewe kuwa wewe ndiye uliyefanya huo uzembe…basi wao watajua ni nini la kufanya, mimi sipo tena….’akatulia

‘Na..sio vizuri wewe kuwekwa jela…unajua kituo chao kilivyo,kuna wanaume wenye laana…sijui ukitoka hapo utakuwaje..nimelifikiria hilo,… samahani mkuu kusema hivyo, …sijakusudia kuharibu jina la kituo chako,….ila nataka huyu nesi aelewe kwanini sisi tukaona tumsaidie…’akasema akimuangalia huyo mkuu, na huyo mkuu akawa kama hayupo anafungua fungua gazeti.

‘Kwanza ujue…,  nimefanya hili kwa vile nakujali…mimi kiukweli nakupenda, sitaki upate shida…naongea mbele ya rafiki yangu hapa maana tunajuana..usione kwanini naongea hivyo..usiwe na shaka naye…’akasema huyo dakitari akimgeukia mwenzake, na mwenzake alikuwa kama vile hasikilizi.

Neno nakupenda lilimshitua sana huyo nesi, kwani ni kweli dakiatri huyo amekuwa akimtongoza,..mwanzaoni alijua ni utani wa kikakazi…lakini baadaye akajua kuwa mwenzake kazamiria…nesi akajitahidi kuweka msimamo wake, akijua kuwa huyo dakitari ana mke na familia yake,…

Huyu mkuu alipoona nesi haelekei, akawa hamfuati fuati tena, ila alimpa onyo kuwa ajitahidi asifanye kosa,kwani kosa dogo itabidi alilipe kwa namna yake…. sasa kauli hiyo ya `nakupenda’  inaweza ikawa na maana hiyo, ..lakini akatulia asikie ni nini kitakachofutia.

‘Sasa nesi kwanza ni wewe kuonyesha upo tayari, hatua ya pili, ambayo sio shida sana, ni kubadili kila kitu…ionekane huyo mtoto hakuzaliwa hai, ..na dada yako ndiye mama halali wa huyo mtoto, basi…je upo tayari?’ akaulizwa

‘Nipo tayar i kwa vipi?’ akauliza nesi akiwa kama haelewi, lakini akilini alikuwa kalenga mambo mawili, kwanza je akikubali kuna nini cha kulipa, pili, yupo tayari kwa kufanya nini…huenda kuna m zigo ambaoa ataubeba usiobebeka, kwahiyo akaona awe na tahadhari.

‘Kubeba hilo jukumu na kuhakikisha siri hii inakaa moyoni mwako, maana ikijulikana umeniharibia kazi na mwenzangu hapa, sisi tumefanya haya kwa ajili yako na dada yako,… vinginevyo unahitajika ukafungwe, na mtoto aende kwenye maisha yasiyo na matarijio…unaona huruma yetu inavyotuponza….sasa tuambie je hilo tulilofanya sio jambo jema..?’akasema kama anauliza.

‘Ni jambo jema,..ila nina shaka ..nitajiona nimekosa sitaishi kwa raha…hata hivyo nashukuruni sana…mimi kwa hilo la kuweka siri, nitajithidi maana najua mtoto keshafika sehemu sahihi, ..lakini kama kuna jingine..hapana sipo tayari...’akasema

‘Hahaha, kama kuna jambo jingine….anyway, Usijali, mengine, tupo pamoja,..muhimu ni hilo,…. hakikisha hata iweje, usije kuliongelea hili, ni kama vile halikuwepo, na wala usije kunitaja kwa namana yoyote ile kuwa mimi nilikushauri..tukafanya hili na lile…, au kumtaja mwenzangu, ..unasikia…kama haupo tayari basi..tuanze michakato mingine..’akasema na kumgeukia huyo ofisa usalama.

Ofisa usalama au mkuu wa kitu alipoona anaangaliwa akagundua kuwa kaulizwa swali akaweka gazeti  mezani, akamtizama kwanza nesi, halafu akageuka kumtizama dakitari mkuu, akasema;

‘Mimi sioni kama kuna tatizo hapa, maana kilichotokea ..ndio ni uzembe, lakini ni jambo ambalo lingeliweza kutokea hata kwa yoyote,…kitu kikubwa ni kuwa tunahitajia huyo mtoto aishi sehemu apate yote yanayostahiki….maana hali ya ile familia ni mbaya, mimi naifahamu sana ile familia....pale ni ulevi, kupigana..hakuna amani, inaonekana hata huyo mama alikimbia hayo maisha, na mwisho wake uka ndio hivyo…’akasema.

‘Ni kweli kafariki, na..tulikuwa na kumbukumbu za kutoroka kwake hospitalini, na kakutwa kafariki, akiwa na sare za hapa…kwahiyo ni wajibu wetu kuja kuulizia tena hapa, ..na kama wanandugu watashinikiza kutafuta ukweli, basi tutaona la kufanya kitu ambacho naona hakipo…’akasema

‘Huyo mama unamfahamu vyema kwa sura…tabia?’ akauliza nesi.

‘Unajua ni siku nyingi mimi niliondoka huko., sikumbuki vyema…hata sura siikumbuki vyema…lakini ile familia yenyewe naifahamu, kuna muda nilitembelea huko nikakutana kesi ya ndugu wa hiyo familia wamekatana mapanga, kisa ni wivu tu…sasa hata ukiangalia yale maisha yao ni ya hatari.

‘Na…na mmojawapo wa huyo aliyepigana ndiye mume wa huyo mke, …kakimbia hayupo hapo kijijini muda hajulikana wapi alipo…sasa huyo mtoto utakwenda kumpa nani…wakati wanafamilia wenyewe wana visasi…’akasema

‘Kwahiyo ndugu zake wanajua kuwa mke wa ndugu yao alikuwa mja mzito na alitarajia kujifunguao?’ akauliza nesi na huyo mkuu wa kituo akamgeukia dakitari mkuu, inaonekana hakutaka kulijibu hilo swali yeye na dakitari mkuu akasema;

‘Hutaamini hakuna aliyewahi kuuliza hilo, ..aliyeongea kwa niaba yetu, ni nesi aliyehudhuria hayo mazishi maana yeye anaishi huko…., na yeye tulishamwambia asiongee lolote kuhusu mtoto, na alifanya hivyo, kwahiyo huyo naye ujue kabeba siri yako,siri yetu..yeye sina shaka naye...umuheshimu sana huyo mdada, na umtii…’akasema.

‘Yah,,..ni bosi wangu namtii na kumuheshimu, na sivinginevyo..’akasema nesi na yule mkuu wa kituo akamtupia jicho la mara moja halafu akaendelea kusoma gazeti, nesi alikumbuka kuwa kuna siku nesi mkuu alimwambia mkuu huyo anamtaka, na kwahiyo yeye anataka kuweka njia ya wao kukutana mara kwa mara kwa siri, na nesi akakataa.

‘Na mtu mwingine aliyejifanya anakupenda sana..akajitolea kukutetea ni yule dakitari kijana,mmh,  napenda dhamira yake na juhudi zake kikazi…lakini kimaisha bado kijana, hajaiva, madakitari bingwa waamsifia sana..lakini ndio hivyo hajatulia..…unaona alivyo, katoa ushauri, halafu yeye huyo kaenda zake ulaya hivi ulikuwa unajua kuwa anakwenda kusoma Ulaya, je alikuaga?’ akauliza dakitari mkuu.

‘Wala sikuwa nafahamu hilo…na hakuniaga, maana alisema hana uhakika kama atakwenda lini kusoma, ..na hakugusia kusoma nje ya nchi..’akasema nesi akionyesha masikitiko. Na kwa muda ule alikuwa kakasirika, na alione kweli alichofanya dakitari kijana sio sahihi, kwanini hakumgusia, lakini hakufikia kumchukia.

‘Unaona ndio vijana walivyo kudanganyana…sasa huyo achana naye,  na hakuna hata haja ya kuwasiliana naye, kama kuna lolote nione mimi…na kama tutahitajia mambo ya usalama nitaongea na mwenzangu hapa, huyu ni mtu wangu hana matatizo labda ukiuke sheria, …’akasema na yule mtu wa usalama akatikisa kichwa na kusema;

‘Mimi naona tumemaliza..muhimu docta…. , ule mzigo…’akasema akimkazia macho mwenzake na  dakitari mkuu wa hospitali akatabasamu, na kusema;

‘Usijali…hilo ni mimi na wewe….wewe weka sehemu safi, mzigo utafika, ….haya mambo yapo kwa mwenyewe…’akasema na kumgeukia nesi, akisema;

‘Nesi nilichokuitia ndio hicho kama una swali..uliza, au unaweza kuja baadaye tukaongea vyema, au sio,  kwaheri, ….tutaonana kazini,..nakuahidi hutapata shida, ilimradi mimi nipo..na ili usiwe na mashaka sana kuna nafasi za kusoma…mimi nitakutupa huko ukasome,..au unasemaje?’ akamuuliza nesi

Kama kuna kitu ambacho alikuwa akikihitajia hapo kazini, basi kimojawapo kikubwa ni kwenda kusoma,na aliposikia hivyo, akajikuta akitabasamu na kwa furaha akasema;

‘Nashukuru sana mkuu, kama itakwua hivy nitafurahi sana, ..’akasema.

‘Najua..ukienda kusoma, utakuwa akili yako kwenye masomo…na huko hutakutana na watu wa kukuulizia kuhusu mtoto, nani…siunajua, na..ukirudi ..basi wewe utashika nafasi nzuri tu nakuahidi hilo….unaona ninavyokujali, ni wewe tu sasa…’akasema na kusimama maana yule mkuu wa kituo naye alishasimama kuondoka, nesi hakutaka hata kusubiria maana alishaona dalili za huyo dakitari wao mkuu za kumsogelea, yeye kwa haraka akasimama na kwa haraka akatoka mbio mbio..

‘Mhhh..’alisikia mguno wa huyo mkuu, na mwenzake akasema

‘Huyo ni wako…’

Nesi alitoka pale kichwa kikikuwa kina mawingu, ina maana pamoja na hayo kuna mambo mengine yamefanyika, kwa ajili ya kufanikisha hilo…je yeye atabebeshwa mzigo gani…maana hajambiwa atoee pesa…na kauli hiyo ya `huyo ni wako ina maana ganiWAZO  LA LEO: Cheo ni dhamana kamwe usipende kukitumia cheo chako kwa masilahi  binafsi ..ukumbuke kuwa cheo hicho mwingine anaweza kuja kukishika na akafanya zaidi yako, kwahiyo hicho sio cheo chako, bali ni dhima, ni jukumu, na ni dhamana.
Ni mimi: emu-three

No comments :