Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, March 19, 2015

NANI KAMA MAMA-46‘Unajua …kuna yule sister, …’akasema rafiki wa dakitari kijana wakiongea.

‘Ssiter yupi..?’ akauliza

‘Yule nesi mkuu, …siku moja aliniambia kuwa wewe unajifanya huna habari na akina dada hapa kazini…kwanza akatania na kusema huenda..hahaha..’akacheka kwanza.

‘Huenda nini..?’ akauliza akiwa kakunja uso

‘Haupo kamili..una madhaifu ..eti ya kiume..’akasema mwenzake

‘Hayo ni mawazo yenu..na kama ninayo hayo madhaifu, basi yangu mwenyewe,..ila mimi mwenyewe  najua ni nini ninachokifanya,..’akasema akiwa kakunja uso.

‘Sio mimi mkuu, ni yule sister…lakini akasema anawajulia watu kama nyie, huwa mnajifanya hivyo kumbe mna yenu ya siri…na ni kwa vile hujaondolewa tongo tongo usoni…hahaha…nakutania tu mkuu, usikasirike…’akasema

‘Unafikiri mimi nayajali hayo,…najua ni nini ninchokifanya hilo ndilo la muhimu..’akasema

‘Mhh..sasa ujue yule dada anakufuatilia…siku ukifanya kosa na pengine likahusishwa na yule dada mnayefanya kazi naye ujue unalo..nasikia mara kwa mra unamtetea huyo nesi hasa akifanya kosa…’akasema

‘Eti nini!….lakini ni kawaida tu, maana yule dada nipo naye kwenye kazi nyingi, sitafurahi mtu akimsingizia uwongo…, unajua kuna makosa ya kibinadamu, eeh..sasa kwanini nisimtetee kama kakosea kibinadamu tu, sio makusudio yake….?’

‘Ndio hivyo…yeye anataka kuonyesha kuwa wewe una mahusiano na huyo dada..na wakati mwingine hamanyi kazi…, kwahiyo, kuwa makini..na kaahidi kuwa ipo siku atakunasa, aufichue unafiki wako..’akasema

‘Unafiki wangu…! Ok, ninachoweza kukuambia ni hivi, hawezi…mimi siogopi…kwanza mimi hapa nipo kwa muda tu…unajua, anapotea muda wake bure …’akasema

‘Lakini uhakiki wa utendaji wako,ambao  ndio utakufanya ufanikiwe huko mbele ukiharibiwa je huoni kuwa hutafanikiwa kwenye ndoto zako, lakini pia utamuachia taabu huyo nesi…, kwahiyo jichunge sana....uwe makini na huyo nesi..’mwenzake akamwambia.

‘Usijali, mimi sina mpango na nesi yoyote hapa kazini hilo nakuhakikishia…’akasema

Leo anajikuta yupo na nesi..na walivyokuwa wamesimama mtu yoyote atasema ni wapenzi…hakutaka kabisa ije kuonekane hivyo….na wakati anaangalia huku na kule mara akamuona, yule dada ..nesi mkuu akiwaangalia kwa mbali, na mkononi ana simu, simu inayoweza kuchukua picha kwa mbali..

Je huyo dada alikuwepo kwa muda gani,na je ana malengo gani,…

Tuendelee na kisa chetu

***********
Basi ile hali ya nesi kumkumbatia bila kutarajia ikamfanya akumbuke ahadi yake,..kwanza ilibidi ashikwe na mshangao…hakutarajia hilo kabisa , kwani alikuwa akimuona huyo nesi kama msichana mwenye aibu, na hawezi kufanya hicho alichokifanya hapo, japokuwa alihisi kuwa nesi huyo kafanya hivyo kwa nia tu ya kushukuru kwa kile alichofanyiwa....kiukweli hakulitajia hilo. Lakini akakumbuka kule kwenye jengo la pili kwa juu yupo nesi mkuu, na kama atakuwa kakiona hicho kitendo,..ni balaa,…

Dakitari kijana , kwanza kwa kujiamini, akamuangalia yule msichana usoni , wakawa wanaangaliana, halafu akakunja uso kama kutahayari, alipoona dalili za usoni kwa huyo msichana…akashangaa na kujiuliza ina maana kumbe kweli msichana huyo kadhamiria hicho alichokifanya..na huenda sio kafanya hivyo…kwa nia ya kumshukuru tu,  akasema hapana..ni kawaida tu ,…

Yeye kuonyesha msimamo wake, hakuinua kabisa  mikono yake kuitikia hilo tendo, akatulia vile vile kama alivyo kuwa awali, akazungusha macho hadi kule alipokuwa kasimama yuel nesi, ..hakumuona pale alipokuwa mwanzoni…

Alitarajia huyo nesi ataondoa mikono yake kwa haraka, na alipoona huyo nesi haondoi mikono yake kwa haraka, akapandisha mikono yake na kuiondoa ile mikono ya huyo nesi,..huku anageuka huku na kule sasa akiwa kaingiwa na wasiwasi, alichelea watu, alichelea yule nesi mnoko asije akamuharibia `sivii’ na msimamo wake.

Aakukumbuka kuwa yeye ndiye alimdhamini huyo dada na kumpigia chapuo kwa huyo dada hana kosa..sasaa kionekana anafanya hivo na huyo dada itaonekana dhahiri kuwa alifanya hivyo kwa vile yeye ni mpenzi wake.

‘Lakini huyu nesi mkuu kwanini ananiuatlia hivyo, ..ana lengo gani, pili mimi simuamini..’akawa anajiuliza kichwani, akakumbuka katika uchunguzi wa kupotea huyo mama, nesi mkuu alisema huyo nesi anayeshutumiwa kwa uzembe alionekana akiwa kasimama chumba walichokuwa wakifania upasuaji,..kama ni hivyo huyo nesi alikuwa wapi..je hakuona huyo mama akitoka kwenye hilo jengo…

‘Huyu mama nahisi ana kitu..’akasema moyoni

‘Ipo siku nitamnasa nay eye, ni kwa vile tu naondoka, sitakaa sana haap hospitalini, huyu dada, anaweza akawa pia anahusika na kupotea kwa huyo mama,…mmh, lakini sina uhakika…’akasema kimoyo moyo.

Wakati anawaza hayo, alimshika yule msichana mikono yake na kuiondoa mwilini mwake huku akijifanya kuwa ana haraka ya kuwahi jambo fulani. Na alipofanya hivyo mikono ya yule dada ikawa kama inaendelea kuwepo, sasa akataka kumsukuma na wakati anataka kufanya hivyo, alijikuta akiangaliana tena uso kwa uso na huyu nesi uso-kwa-uso, na hapo akajihisi kutahayari zaidi, na hisia za ujana zikataka kumtawala….akajikuta anahema..na ilikuwa kidogo tu,… kama wasingelisikia mtu anakohoa nyuma yao….bila kuangalia ni nani, akasema;

‘Unasikia sister, unatakiwa utafakari vyema hicho unachotaka kukifanya…’akasema

‘Mhh kwanini docta…kwani kuna ubaya gani, hebu nikuulize docta ..mimi nipoje…?’akasema nesi, na yeye hakutaka kumpa nafasi akasema;

‘Unajua sister…wewe kwa hivi sasa una majukumu mazito mbele yako..huu sio muda wa kufanya mambo mengine yatakayo kufanya usijisikie mnyonge…na kushindwa kutuliza kichwa kwa jukumu hilo kubwa ulilo nalo..sijui unanielewa…’akasema na nesi akiwa kama kaishiwa nguvu, akainama, na unyonge fulani ukamuingia, kwani alichotarajia hapo hakikutokea, akahisi huenda huyo dakitari kijana hampendi, kama alivyohisi yeye moyoni.

‘Mhh, haya bhana,…samahani kwa hili…bosi, ..najua  hujapendezewa, na usione kuwa mimi nimuhuni, hapana…imetokea tu…naomba tafadhali usije kunifikiria vibaya…nilitaka tu kukushukuru kihivyo…’akasema nesi,

‘Kwani umefanya nini sister..ni kawaida tu….muhimu ni kuchunga macho ya watu, macho ya watu yana tafsiri nyingi, hasa yakiona tendo lenye kuvuta hisia..hata kama sio kweli, akili za wapiga domo, akili washambenga, zitatafsiri kwa nia mbaya, ..unajua hilo. ..’akasema

‘Nikuambie kitu sister…, shati jeupe ni rahisi sana kuonekana uchafu wake, kuliko shati jeusi au lenye rangi inayofanana na uchafu..na ndivyo ilivyo kwa watenda wema, kwao wao wakifanya kosa dogo tu…itakuwa ni gumzo,propaganda, uzushi utasambazwa..kwanini, kwa vile wenye wema wana mitihani mingi sana…kwahiyo kuwa makini..’akasema dakitari.

‘Kwani…kuna nini kinachoendelea baada ya hiyo kesi..?’ akauliza nesia akionyesha wasiwasi

‘Bado wanafanya uchunguzi kuhakiki, kama kweli kuna kosa, japokuwa wamelinyamazisha kinamna..lakini kwa ufupi bado uchunguzi unafanyika, maana huyo mama hajulikani wapi kaenda, na kama litatokea baya ujue hospitali itabeba lawama..kwahiyo bado hali ni tete, na ni kuwa nesi mkuu, kapewa kazi ya kufualia nyendo zako….’akasema.

‘Nesi mkuu,..nesi mkuu…. huyo dada simpendi..…lakini ipo siku ..nina imani hiyo sehemu yake ipo siku nitakuja kuishika mimi , hizo ndio ndoto zangu…’akasema

‘Kila laheri…’akasema docta

‘Ahsante….’akasema na kujaribu kutabasamu.

‘Sasa sikiliza sister, pamoja na mengine ukumbuke kuwa huyo mtoto  ni mtoto mchanga…anahitajia huduma za ziada, sio kazi ndogo hiyo…na inahitajika uwe na maamuzi ya haraka, kuanzia sasa..’akasema dakitari.

‘Ndio hivyo,…kiukweli nilishakata tamaa kabisa, na nilitarajia kuwa utanisaidia kwa hilo, tukamlea huyo mtoto kwa pamoja..’akasema

‘Kumlea kwa pamoja mimi na wewe…!?’ akauliza docta kwa mshangao

‘Mhh…niliwazia hivyo tu..samahani kwa hilo..na uliposema haiwezekani, nikajua sasa ninalo..’akasema

‘Hapana sitaweza hilo..ila..kiushauri tupo pamoja…’akasema

‘Lakini hata hivyo nimefurahi sana…hasa ulipolitoa hilo wazo, la kama kuna nduguna ..wazo ambalo nilikuwa nimelisahau kabisa,..ukaniwezesha kukumbuka kuwa dada yangu alikuwa akihitajia mtoto, hata wa kulea… ,’akatulia akitabasamu.

‘Sawa haya ngoja mimi nikuache, maana tumesimama hapa kwa muda, na ..nilimuona yule nesi mkuu akituchunguza..’akasema

‘Wapi…., mungu wangu weeeh..’akasema nesi akiangalia huku na kule, lakini dakitari kijana hakujali, akasema;

‘Usijali, hujafanya kosa lolote, niamini….wewe hukusikia mtu akikohoa…alikuwa yeye, kaona kule mbali haitoshi kasogea karibu atakuwa maeneo ya hapa karibua natusikiliza..lakini usijali…’akasema huku akiwa kajiegemeza ukutani

‘Mhh, nashukuru bosi, nikiwa nawe najihisi salama..’akasema

‘Sawa usijali,ila… kuna kitu nataka kukuambia, samahani sana kama nitakuwa nimekuuzi..’akasema dkitar kijana na nesi kusikia hivyo moyo ukalipuka paah, akajua sasa huenda, dakitari anataka kusema lile la moyoni, ambalo linaweza kufungua ukurasa anaoutaka yeye, akatabasamu na kuinama chini kwa aibu.

‘Sister, kama nilivyokuambia, sio wote wanaokuchekea ukazani wana nia njema na wewe…kicheko, tabsamu linaweza kuwa la wema au ubaya, furaha au huzuni, au sio..yote yawezekana kwa binadamu, sasa…mimi , ningekushauri saaana, ili kuwa salama,…tukiwa hapa kazini, jaribu sana usiwe na mimi karibu karibu kama hivi…’akasema

‘Mhhhh..’akaguna nesi.

‘Unajua bado unafanyiwa uchunguzi…kama nilivyokuambia, na nesi mkuu kapewa jukumu la kuchunguza nyendo zako…sasa utawala ukiona upo na mimi kihali ya …kama hii, utanihisi vibaya kuwa mimi nimekusaidia kwa kuwa wewe ni rafiki yangu…’akasema

‘Mhh..ni kweli..hata hivyo, …wewe ni rafiki yangu kikazi..au sio…na sio mbaya sijui kama nimekosea..’akasema nesi.

‘Sister..sitaki kukuumiza, ..wewe unajua kabisa mimi na wewe hatuna mahusiano yoyote…, zaidi ya kuwa wewe umetokea kuwa ni mwenza katika kazi zetu.., na nataka iendelee kuwa hivyo na sio vinginevyo… naomba uelewe hivyo, samahani sana..’akasema huyo docta..

‘Mhh..samaahni docta..nimeshindwa tu kuvumilia…lakini..sijafanya vibaya, eti…kama nimekosea naomba unisamehe…nilishindwa kuvumilia, na ningekushuruje…hata hivyo,…sijui..nisamhe tu docto’akasema nesi akiwa kainama na sasa akitaka kuondoka.

‘Sikiliza sisiter, wala usijisikie vibaya…hujafanya vibaya…kuna kitu kingine nataka tu kukuambia…’akasema docta huyo sasa wakiwa wapo mbali mbali, na nesi akawa hasikii vyema, akageuka na wakaangaliana, na machozi yalishaanza kumtoka yule dada

Docta akanyosha mkono wake, na kumfuta yule dada yale machozi, wakawa wamesimama, japokuwa sio kwa karibu sana.. docta akatulia akilini akiwa anajiskia vibaya,a kihisi huenda kaongea jambo lililo muumiza huyo dada, hakupenda kabisa kumuumiza mtu ..hasa akina dada, akina mama, kwake yeye, anawaona kama watu wanaohitajia upendo wa hali ya juu, akawa najiuliza afanye nini kumliwaza huyo dada.

Bila kuogopa sasa akamsogelea huyo dada, akanyosha mikono na kumshika sister kwenye mabega kwa mikono yake miwili…, ni kwa mbali, hakuwa kama wamekumbatiana, wakawa wanaangaliana usoni, akasema;

‘Kwanza naona usisononeke…sio kwamba nimesema hivyo kwa vile labda,…sikupendi..hapana..nikuambie ukweli, wewe ni msichana wa peke yake hapa kazini, na mwanaume atakaye kupata wewe , atakuwa na bahati kubwa,..’akasema na kutabasamu.

‘Ahsante..’akasema nesi.

‘Mimi siwezi kukudanganya, bado nina safari ndefu ya masomo…sijataka kutulia na kujiingiza kwenye mahusiano na yoyote yule..muda ukifika hali itasema lakini kwa hivi sasa..hapana,…sitaki nije kumuumiza yoyote yule…’akasema

‘Hamna shida nimekuelewa…’akasema sister huku akiumia kimoyomoyo.

‘Sasa sikiliza…unajua ..kuna kitu nilikiwaza kabla, nataka nikuambie ...’akaanza kusema doctor,  na nesi moyoni nesi akawa anaombea dakitari huyo atamke neno tu la kumliwaza hasa la kimapenzi..ambalo litaonyesha kuwa huyo docta anampenda...japo..hata kwa baadaye.

‘Mhh…kitu gani… wewe sema tu, nakusikiliza wewe bosi wangu…’akasema nesi akimuangalia doctor sasa kwa macho yenye kuonesha huruma .

‘Ni kuhusu huyo mtoto na mama yake…’akasema.

‘Huyu mtoto...! sawa, lakini mama yake mhh, maana hayupo, kuanzia sasa mama yake ndio mimi,  au sio?’ akasema nesi kwa sauti ya unyonge na kukata tamaa.

‘Mhh…mimi nazungumiza mama yake wa asili, mama mzazi…unajua, nikuambie ukweli wa kutoka moyoni,… kama kuna kitu kinanigusa moyoni ni hali kama hiyo…’akasema akiangalia mbele, alikuwa hamtizami huyo nesi…

‘Mhhh..hali ipi…?’akaguna na kusema hivyo huyo nesi.

‘Hali hiyo ambayo inafikia hatua….mama ana ujauzito, na labda ujauzito wenyewe ni wa taabu na mashaka…na mungu bariki, anapata huyo mtoto kwa shida…, huku hana uwezo hata wa kumlea,..ukirudi nyuma kwenye maisha yake huenda…alikuwa akiishi kwa shida, majanga…na yote hayo,  huenda ni kutokana na ndoa.., ‘akatulia.

‘Tunasoma tunaenda shule, tunajifunza mengi tu…, ili iweje..ili tupate mkate tu wa kila siku ..hapana…tunahitajika kufanya jambo..maana kuna mambo yanahitajika kubadilishwa..dini zimesaidia sana…, lakini cha ajabu hivi sasa dini zinapigwa vita..sasa hizi, mila , desturi za ajabu ajabu zitaondokaje, maana kuna desturi za zamani, na kuna nyingine zinajitokeza mbaya zaidi, ni nani wa kuzikemea, maana zinaletwa na watu wenye uwezo, ni nani…’akawa kama anaulizwa.

‘Nikuambie ukweli nimefanya tafiti nyingi…akina mama wananyanyasika sana…hasa ndani ya ndoa….sijui kwanini, kwanini watu hawataki kuelewa ni nini maana ya ndoa…ndoa sasa hivi ni sanaa tu, inakuwa kama watu wanaigiza tu…’akasema dakitari kijana, na nesi akatabasamu….

‘Mhh, wewe unaelewaje maana ya ndoa maana hujaoa na umesema hutaki kuliwazia hilo…kwasasa maana muda wake bado?’akasema nesi kama anauliza na mdomo ukaonyesha tabasamu la mbali.

‘Mimi ni mtoto wa mkulima..nimesoma kwa shida sana usione hivi, isingelikuwa ni juhudi za wafadhili na kipaji changu cha darasani…sijui ingekuwaje…’akatulia

‘Wengi wakiniona hivi wanahisi natoka kwenye familia yenye uwezo..hapana…mimi nikuambie ukweli…, nimeishi kwenye familia zetu za kimasikini…, nimeona taabu za akina mama, kutoka kwa waume zao…mume muda wote ni hasira, kakunja uso utafikiri kaona nini…ajabu kabisa’akatabasamu kidogo lakini uso ukionyesha uchungu.

‘Mume na mke, wanaishi kama maadui…hata kitu kidogo tu, mume anamjibu mkewe kwa hasira…mke anajaraibu kujishusha, kunyenyekea, oooh, ndio utafikiri kapasha moto kwa mume…haya ni maisha gani…sivyo hivyo ndoa ilivyo.., hawa watu wameoana, ili `kuwe na raha…kwa hali hiyo raha ipo wapi…ni taabu kweli kweli.’ ‘akasema maneno hay kwa mapozi.

‘Umeonaeeh..’akasema nesi

‘Unajua mimi nijuavyo hata kwenye dini,..maana usionione hivi mimi nasoma kila kitabu, nasoma vitabu vyote vya dini zote…ili nijue yaliyomo…hasa kwenye fani yetu hii ni muhimu kuyaahamu hayo…nijuavo mimi , dini inasema,  ndoa ni raha..au sio..’akawa kama anauliza

‘Kwahiyo mke na mume hata wakiongea waonyeshe ile tabasamu…kuonyesha wapo kwenye raa, upendo wa dhati…maana ukifanya kinyume chake wewe huijui ndoa, unaikosea ndoa, na ni dhambi, kweli si kweli?’ akawa kama anauliza na hakusuiri jibu akasema
‘Unajua….mkiwa ndani hata nje mke na mume mnatakiwa muonyeshe upendo halisi,maana mumeshapewa ruhusa, nyi mpo uwanjani wengine ni watazamaji tu, sasa kwanini muihini ndoa…kiukweli, hapo ndipo pa kumaliza lile tabasamu la mwisho…unaniona….eeh..chuki haitakiwi kabisa, anayefanya hivyo hajui maana ya ndoa…’ akasema kiamwangalia nesi kwa kujiiba pale alipomuona nesi akitabasamu.

‘Unajua… mimi muda wote napenda kutabsamu, najaribu kujifunza nitakavyo tabasamu kwa mke wangu…lile tabasamu la mke wangu bado lipo sandukuni….hahaha..... yah, ndio hivyo…akasema

‘Ni kweli… hilo usemalo ni sahihi kabisa, ndoa, inatakiwa kuwe ni sehemu ya amani, na hata kaam umechoka ukirudi mkikutana na mke wako yale machomvu yote yaishe,..je yanaanika hayo, …na kiujumla wanawake wanajitahidi..lakini waume wanakuwa wagumu kuelewa, wanaona kuwa ukali, kukunja uso…kukaripia ndio njia ya kuwa kiongozi wa familia….kiujumla wanawake tunapata taabu sana..’akasema nesi.

‘Yah..ndio hivyo…nikutokuelewa..kwa mfano tu… hebu angalia huyu mama, …sijui kwanini kafanyiwa hivyo,..ukiangalia alivyo…yaani kaharibiwa uso....yaonekana kabisa kuna jambo baya lilimtokea…na aliyemfanyia hivyo aliataka kabisa kuharibu sura yake, …sasa baya zaidi, siji watu hao wana roho gani, hawakujali kabisa kuwa huyo mama ana kiumbe tumboni,  yaani namuonea huruma sana huyo mama, I wish, ningelipenda…nije niongee na huyo mama nijue chanzo cha hayo yote ninini…haiwezekani….’akasema wka uchungu.

‘Mhh..jamani..unanihamasisha,…docta, lakini acha tu..endelea kuongea..’akasema nesi.

‘Unajua pale nilipoambiwa tunamfanyia huyo mama upasuaji,  na tunatakiwa kuchagua, mama au mtoto, nilihisi machozi..yaani pale kabla sijaanza kazi, nikamuomba mungu kuwa mikono aliyonipa na kipaji alichonipa kisije kuishia kwenye kutenda ya kuua, …sio kwamba tunaua,… maana inafikia mahali unaambiwa hivyo, jitahidi umuokoe mtoto, mama achana naye au jitahidi umuokoe mama, mtoto achana naye, hapo kwangu naona kama ni kuua,… sikupenda na sitopenda ije itokee hivyo kwangu..ndio maana nikawa anjifunza zaidi mishipa ya ndani yenye kusaidia…ni uchunguzi mgumu na unahitajia imani zaidi..’akasema dakitari.

‘Kweli wewe ni dakitari mwenye moyo wa huruma, na ….sijui kwanini watu kaam nyie ni wmungu …lakini wewe hujaoa na unasema hutarajii kuchache sana hapa duniani…lakini mimi najiuliza wewe hujaoa, lakini unavyoongea utafikiri mtu mzima anayejua au aliyewahi kuishi kwenye ndoa…, umejifunzia wapi mambo hayo ya ndoa…na sijui mkeo atakuwaje…’akasema nesi.


‘Ni kweli, sijaoa..lakini kutokana na kazi yetu, unajikuta unasoma mambo mengi tu maana kazi yetu kiujumla ni utashi..ni moy, ni kutuma zaidi wanasema ni wito…kwahiyo ili uifanye kwa moyo mmoja, unahitajika, kunajifunza mengi…’akageuka kushoto na kulia , halafu akasema;

‘Unatakiwa kujiunza mengi na hata kupitiliza..mimi napenda kuwa dakitari bingwa wa akina mama, uzazi na matatizo yao tu, upasuaji, na saikolojia nzima ya ndoa..kwa hivi sasa nimejikita kuwa, Gynecologia..’akatulia kidogo.

Lakini sijajitosheleza..nataka nijiunze kwa undani zaidi..ili niweze kujitosheleza, yaani mambo yote ya` Obstetrics and Gynecology’…hayo..ndio fani yangu..lakini sitaishia hapo, nataka kuangalia na matatizo ya ndoa, yaani saikolojia nzima ya mke na mume, mpaka wanazaa, matatizo yao…ni ndoto lakini inawezekana..’akatulia.

‘Lakini mimi naona umeshahitimu tayari, tena kwa vitendo..’akasema nesi.

‘Bado sana..bado nina safari ndefu…nataka nitakapokaa kuwa dakitari nifenya miujiza..nataka akinamama muwe na raha…unajua…nilipokuona unatoa amchozi nilikumbuka mbalia sana, namkumbuka mama…oh, nani kama mama jamani….ndio maana sitaki kuona machozi….hasa yanayotoka kwa akinamama, nataka nione tabasamu na furaha usoni mwao…hiyo ndio ndoto yangu…’akasema na alionekana kuonyesha dhamira ya kweli usoni.

‘Mhh, jamani ukisema hivyo ndio unazidi kuniumiza..’akasema

‘Kwanini..?’ akauliza docta akimuangalai nesi kwa mshangao

‘Natamani niwe na mume wa namna yako, ..ndio maana sijaolewa mpaka sasa, wengi wanaonitaka kunioa hawana sifa nizitakazo mimi..naogopa sana ndoa na matatizo yake..nimeona machungu mengi wanayopitia akina mama,hasa kupitia kwenye ndoa zao…akikosa kuzaa lawama kwa mama, akizaa, lawama kwa mama, unazaa sana,au unazaa wanawake watupu..mtoto akiharibika tabia lawama kwa mama…nikifikiria hayo mmh, yaani naogopa.. sijui kama nitaolewa tena..’akasema

‘Usiseme hivyo..kuwa hujui kama utaolewa… muda ndio utakaosema,..nikuambie kitu muda wa kuolewa au kuoa ukifika, ..hakuna majadala, utajikuta umeolewa,au kuoa, na huenda ukaoa au kuolewa na hata mtu usiyemtarajia kabisa…kabisa, na hapo unaweza kufanya makosa ya uchaguzi…lakini yote ni heri muhimu ni wanandoa kufahamu nini maana ya ndoa, wengi hawafahamu hilo…’akasema docta

‘Sasa kwanini inakuwa hivyo docta…?’ akauliza nesi.

‘Ndivyo ilivyo..wenzetu wanaita `destiny’…kiujumla ni mungu mwenyewe kapanga iwe hivyo…na wengi wanakuwa na ndoto zao..hizoooh..mmm,lakini mwisho wa siku , muda ukifika, ..inatokea tofauti..japokuwa ni muhimu kujipanga na kuwa na malengo,na malengo ni dhamira ya kutoka moyoni na matendo…’akapiga piga miguu chini, halafu akasema.

‘Kiukweli, huwezi kusema nataka mume mwema, au mke mwema, wakati wewe mwenyewe haupo hivyo, sasa utamlaumu nani eeh, lakini pia kabla ya ndoa ni muhimu kwanza kuweka msingi wa maisha…maana ndoa bila kujiwekeza, ukajua mtaishije,..nayo ni mtihani…ndio hapo ukasikia mimi nikisema hilo la ndoa bado sijawa tayari…’akawa kama anatabasamu.

‘Lakini pia ni kujibidisha kwa kujifunza ndoa ni kitu gani, ni nini ndoa…hili ni tatizo…watu hawajui, yaani hilo nimejifunza, na ni kweli,..hebu nikuulize, hivi uliona watu wakienda shule kabla ya kuoa, kuwa wanasomea kuhusu ndoa…hakuna..watu wanachukulia uzoefu kutoka…kwa baba na mama..na hapo ndio nikagundua jambo muhimu sana..’akasema an kutulia.

‘Sister..nadharaia nzima ya ndoa…ina mapungufu mengi…lakini ngoja nimalize `project yangu’…kwa hivi sasa ninachoweza kusema ni kuwa...mungu anatufahamu kuliko tunavyojidanganya wenyewe…’akatulia kama anawaza jambo halafu akasema;

‘Wengi tunafahamu hivyo kuwa msingi wa maisha hujengeka kwenye elimu,…sasa najiuliza ni nani alikwenda shule kufahamu nini maana ya ndoa kabla hajafunga ndoa…nikachunguza nikaona hakuna…muda ukifika aah, mtarajiwa, aaah, keshaoa, ..mara ngumi, mara …kuachana…kosa lipo wapi hapo…na kuna kitu kinakosewa hapa…, kwa sisi, hasa waafrika, na sio waafrika walio wengi…tunakuja kujifunza kuwa kumbe msingi wa maisha ya mwandamu, ..elimu ya msingi..ya maisha ya mwanadamu, inatokana na maisha ya baba na mama,…’akatulia.

‘Hapa watu wengi hawajui hilo.. elimu inakuja baadaye ukishapevuka, na elimu hiyo ya kitabu, darasani, …unakuja tu kukupanua fikira zako na kukuwezesha ujue fani gani utakuwa nayo kama mimi nimechagua kuwa docta..unaona eeh..’akamuangalia nesi.

‘lakini msingi mama,…ni kutokana na jinsi baba na mama wanavyoishi, wakiwa na upendo..wanatarajia familia yenye upendo na furaha…na kinyume chake ni ndio hivyo, wakiwa na mihasira, kukemeana, mume ni kama simba..yaani taabu …basi watoto wanakuwa hivyo hivyo…’hilo ndilo asilia.

‘Sasa sehemu ukilichunguza hilo ukaona aaha, kumbe…baba na mama ndio msingi wa maisha…basi hapo hapo utagundua umuhimu wa kuchangua mwenza,..na ile nadharia ya mke mwema na mume mwema ndipo inakuja hapo..lakini hapa napo kuna walakini wake…’akatulia tena.

‘Unajua , wengi hawalichunguzi hili kwa makini..na kwa vile umepevuka, umeshajitoa kwa baba na mama, hebu basi chunguza mapungu yao na wewe uyaboreshe kwako, yale ya asili..ukali, eeh, udume, ok, haat ujike chuja na ujipange kivingine, na itawezekan basi kwa hata kulisomea hil..jifunze , chunguza…, ni nani mume mwema, na ni nani mke mwema…hapa kuna tatizo, na ndio chanzo cha majanga duniani…’akahema.

‘Unaona vita…watu wanauwana…watu wanachukiana, ni nani aliweza kuchunguza zaidi chanzo cha haya yote…, akagundua ni nini asili ya hayo yote, hebu niambia wewe ukiulizwa chanzo hasa cha uhasama, chuki hadi vita.. ni nini..’akamwangalia nesi.

‘Kiukweli…watu hawalisemi hilo, chanzo na huku nyuma ,…jinsi gani wawili waliishi, wakajenga kizazi chema, chenye maadili..jinsi gani ndoa ilichukuliwa kwa uzito wake, ndoa ikawa ni raha, upendo, na matokea ni kuzaa watoto wenye upendo , furaha, na kizazi kinakua hivyo..lakini duuuh..watu wakaifanya ndoa ni ndoana…sasa ndio hayo mnazaa watoto vichwa maji,..unafikiri itakuwaje, chuki , visasi….mihasira watu kuana wanaona kaamni raha tu…hawalisemi hilo…matokea yake wanaanza kuanzihs mambo ya ajabu, …eti wanavunja uasilia wa mwanadamu, watu wenye jinsia moja kuoana…hili litakuja kuigharikisha dunia…mtaona ..yatazuka magonjwa…mimi naogopa…dunia inapokwenda ni kubaya, maana tumeshataka kuiharibu asilia…ya baba na mama..’akatulia na kuangalia saa.

‘Ulisema unataka kuniambia nini, maana naona unaangalia saa, na kiukweli docta, natamani kuwa nawe kwa karibu sana, nikirudi kutoka kijijini naomba tukutane…naomba sana,please..tafadhali....’akasema nesi na dakitari akaabasamu hakusema neno na nesi akaendelea kusema

‘Mhh.. sasa hivi, mmh, huenda ukaitwa,na mimi, nataka kwenda kumuangalia huyo mtoto na kuona taratibu za kumchukua, hata leo, au kesho..naona tukizidi kuongea hapa…unazidi kuniumiza moyo wangu, lakini natamani nikae na wewe tuongee zaidi..kama hutojali lakini..’akasema nesi

‘Ehee..nilitaka tu nikuweke sawa…lakini ninachotaka kusema ni hiki….’akasema na nesi akatulia kumsikiliza

 ‘Sasa ni hivi, kuna kitu wanasema watu wenye hekima…, kitu bila kumbukumbu hupotea hewani, au sio….mimi haya yote nayafanya katika kutimiza lengo langu na nahitaji kuweka kumbukumbu kila hatua ya kazi zangu, nimeanza zamani….’akasema

‘Sasa kwa hili tukio la huyu mama, ..mmh, ..kutokana na hiyo hali, nikijua kuwa huenda mama akafariki,…nikawa najiuliza kama atafariki na mtoto anaishi bila mama, itakuwaje…najua huenda, ipo siku mmojawapo, atahitajia kumbukumbu za mwenzake ama mtoto ama mama, ..nikaona nifungue kabrasha moja, kwa ajili ya kumbukumbu za huyo mama na mtoto wake....’akasema

‘Lakini docta, hayo si yapo tu..lipo kabrasa lake la kumbukumbu  yapo mafaili kwa ajili ya wagonjwa..’akasema nesi

‘Mhh, sio kama hizo kumbukumbu za kiutawala…hapana..nilichofanya nikuchukua vipimo vyote vya huyo mtoto na mama yake, na maelezo yake…nilitaka nijue zaidi historia yake..na kila kitu, hata picha yake..unajua, na kila kitu…, ili vije kumsaidia huyo mtoto au mama yake huko baaadaye..’akasema dakitari.

‘Mhh, hata sijui umuhimu wake …naona dakitari wewe upo `too ambitions…’akasema nesi,

‘Mimi najua..hayo, nasoma vitabu vya hadithi, naangalia movie, sisomi au kuangalia tu..naangalia na kati kat ya mistari..maisha katika uhalisia wake… nimesoma na kusikia,…watoto waliokulia hivyo, wanavyohangaika kutafuta wapi walipotokea, mara nyingi hakuna jinsi ya kuweka hizi kumbukumbu za vizalia..na historia angalia kwa uchache…., hili ni kosa, kwa vile watu wnafanya yale wanayoona yanawashibisha tu, hawafikirii kizazi kijacho…’akasema

‘Najua itafika muda utachoka tu…kwa nchi….wapo walikuwa hivyo, na sasa wamejikalia tu…nina wasiwasi huo’akasema nesi.

‘Najua sana hilo, lakini kabla sijachoka niwe nimefanya jambo....’akasema na kuangalia saa yake.

‘Sasa ni hivi…huyo mtoto huenda baadaye akataka kujua wazazi wake ni nani,..na ni kitu gani kilitokea…unaona ilivyo,..mimi najaribu kujiweka sehemu ya huyo mtoto na kujiuliza maswali kama hayo..na majibu yake nimeshawaweka tayari… sasa ni vyema kumbukumbu kama hizo ziwepo mahali maalumu..’akasema

‘Sawa kweli..kama usemavyo..huenda akaja mmojawapo akaja kuzitafuta lakini kwa hali ya nchi yetu ilivyo mmh, hata sijui…maana mtoto atakulia wapi, maisha yenyewe yalivyo..au mzazi..mmh, wakitoka hapa wametoka, sijaona mtu akija kuulizia kihivyo..labda tu akija hapa kakwama kuhusu angazo la uzazi kwa ajili ya cheti cha kuzaliwa, lakini kudadisi, ilikuwaje…sijawahi kuona....’akasema nesi.

‘Ndio hivyo, ndio maisha yetu yalivyo..lakini lazima mmoja afanye jambo ili kueleta mabadiliko..lazima mmoja ajaribu kitu…Sasa mimi nimeanya hivyo, kwanza kwa huyu mama, nimechukua kumbukumbu zote zake na kuzihifadhi katika faili hilo hilo la mtoto…ni kitu tu kimenijia..na nimeona kwa vile hata mimi nafanya kitu kama `project’…basin a iwe hivyo’akatulia kwanza

‘Project ya nini..?’ akauliza nesi.

‘Ndio kama nilivyokuambia, nataka kusomea na maisha halisia, napenda kuita saikolojia ya ndoa, ambayo inakwenda hadi kwenye uzazi,..na kila kitu chake..unaonaeeh…’akasema na kuangalia saa tena.

‘Sasa nimeona pia nifungue mtandao maalumu kwa mambo hayo..,  ukiingia kwenye komputa yangu utaona nimeweka kumbukumbu nyingi tu, na huyu mama ipo pia….na nataka kulifuatilia hilo kwa karibu sana..hata nikiondoka hapa najua wewe utanisaidia kunipa taarifa zake..maana nimeshafungua `file endelevu’ maalumu kwa huyo mama na mtoto wake…’akasema

‘Mhh, na muda huo unao docta..naona utajichosha tu…maana mimi nikitoka kazini mambo ya kazini nataka niyasahau kabisa…sasa nianze kukaa kwenye komputa kuandika ..mmh, nakupa hongera…’akasema nesi

‘Nimekuambia tu wewe, kama itatokea, basi jaribu kukumbuka hivyo kuwa kumbukumbu hizo unaweza kuzipata zilipo…, maana mimi nipo kwa muda tu hapa…nimehifadhi hizo kumbukumbu  kwenye kabati namba 5, hili ni maalumu kwa kumbukumbu nyeti za kwetu kama madakitari, sitarajii kuwa hap zitaharibiwa....’akasema dakitari kijana, akiwa sasa anageuka kama kutaka kuondoka, lakini bado akawa kasimama hapo hapo.

Yule nesi mawazo yake kwa muda ule hayakuwepo hapo kabisa, alikuwa akimuwaza sana huyo dakitari kijana, alikuwa akijaribu kuhisi jinsi alivyojisikia pale alivyomkumbatia, na jinsi alivyo na ndoto zake ambazo, aliomba aje kuishi naye ili wasaidiane, ziweze kutimia…, akawa anaombea kupata mume wa namna hiyo….oh

‘Oh, jamani kama ingelikuwa hivyo kila siku ..niwe naye karibu tu..tuongee hivi na ikiwezekana, tuwe mke na mume mmmh, labda anaogopa umri, lakini, kiumri  mbona hatujapitana,..yeye kanidi kama mwaka au mika miwili…sina uhakika…..na ..sema kwa mwanaume ni lazima yeye aonekane kijana zaidi….mmmh’akawa anajiongelesha kichwani kimawzo.

‘Mhh, jamani, kwanini hanikubalii niwe mpendwa wake, nifanyeje ili anielewe..?’ akawa anazidi kujiuliza..akiwa kasahau kabisa kuwa bado yupo matatizoni…

‘Umesema wazazi wako wanaweza kukusaidia..?’ akauliza huyo dakitari sasa akigonga gonga kiatu sakafuni, kama anataka kuondoka, na nesi akawa kimia, kwa vile bado alikuwa akiwaza mengine , na dakitari huyo akasema;

‘Lakini naomba unielewe kitu sister..usijipe mawazo sana…muhimu kama ulivyosema,, kama unawaamini hawo ndugu wako kama ulivyosema, basi wasiliana nao kwanza kwa simu..usije kumbeba mtoto hadi huko…ukakuta mengine..’akasema

‘Kiukweli mimi nisingelipenda kiumbe hicho kije kupata taabu…na pia mimi ningeshauri hivi, ok, hata kama simu hazipatikani basi…wewe nenda moja kwa moja kwa hao wazazi wako kaongee nao na kama wanahitaji kuandikisha kama wazazi wa huyo mtoto, basi itakuwa ni vyema zaidi…

‘Mhh..ni kweli  …yaani ungelijua jinsi gani dada yangu anavyotafuta mtoto..hata wa kumlea, yaani kama hivi aambiwe huyu sasa ni wako..sijui atafurahije…japokuwa kiukweli anataka mtoto wake wa kuzaa..lakini bahati haijapafika kwao…sasa akipata huyu mtoto ..mmmh, sijui..’akasema nesi.

‘Na kama ni hivyo mimi naona hata kabla hujaondoka, basi wasiliana na utawala watakusaidia kwa hilo kisheria..…, lakini mhh..sijajua sheria za hapa hospitalii vyema,..kwahiyo…mmmh hilo la kummilikisha huyo mtoto moja kwa moja, naona lisiende kwa haraka sana. Huwezi jua, mama akapatikana, huwezi jua..’akasema

‘Ina maana wewe watarajia kuondoka lini..?’ akauliza

‘Sijui…bado nasubiria kitu..’akasema.

‘Oh..poa…lakini ombi langu lipo pale pale, nahitaji kuongea na wewe zaidi…ni ushauri tu…najua utanisaidia sana…’akasema nesi

‘Hamna shida…kama utaondoka leo mimi naona ni bora zaidi..ili ukutane na hao ndugu zako..’ akasema dakitari kijana huku sasa akianza kutembea kuondoka, akawa kama kakumbuka kitu

‘Kwani wewe ulikuwa unataka kuongea na mimi kuhusu nini, ni kuhusu huyo mtoto au…au kuna jingine zaidi?’ akauliza dakitari...lakini kwa ule umbali nesi hakusikia vyema, na docta akaona asipoteze muda, akafanya haraka kuondoka, na wakati huo huo nesi akawa anaongea akijua dakitari badi yupo akasema;

‘Mh, mimi nakusikiliza wewe tu…na kuhusu hilo la mtoto mimi nimekuelewa..docta, lakini..hata kama tunaweza kukuna kabla sijaondoka sio mbaya, tukaongea zaidi, kama marafiki..’akasema nesi, na wakati anaongea akawa kainama chini akichora chora na mguu, hakujua dakitari hayupo..lakini alijua yupo kwani alihisi kuwepo kwa mtu. ..

‘Na kwani wewe watarajia kuondoka lini huko masomoni sijui wapi…mimi kwenda kijijini, sijui nindoke kesho…eeh, kwani, wewe huwezi kufika kwangu..tuongee au  wasemaje kwa hilo…?’ alikuwa akongea akiwa kainamisha kichwa akichezesha mguu chini,..

Alipohisi ukimiya…hasikii sauti ya docta,… akainua kichwa, na  kuangalia pale alipokuwa kasimama dakitari, hakumona yeye na aliyekuwa kasimama hapo si mwingine..ni mkuu , bosi wake, nesi mkuu…na uso wa kejeli ukiwa unemeta meta…..

 WAZO LA LEO: Katika hali ya kimaisha wanadamu wote hatulingani, kuna wengine wamejaliwa kuwa na kipato na cha ziada, na wengine wanakuwa hawana kabisa, pia kuna matatizo yanatokea wengine hujikuta hawana jinsi ila kuomba, au kukopa nk kwa hali ilivyo …


Kwa tamaa,  kuna wengine wanatumia fursa hiyo kupata ziada kwa hao wenye shida,  wanatoza kitu kinachoitwa `riba’..anamkopesha mwenzake akijua kabisa kakopa hiyo pesa kwa shida, ana matatizo makubwa, …anamwambia ukirudisha unipe na ziada, `riba’…huyu kwa vile ana shida inabidi akubali tu,…Huyu mtu hakopi kwa raha, kwa biashara,anakopa kwa matatizo wewe unazidi kumlundikia matatizo, ..jamani huu sio uungwana..huu sio ubinadamu, riba ni dhuluma…tukumbuke tutakuja kuhukumiwa kwa hilo !

Ni mimi: emu-three

No comments :