Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 17, 2015

NANI KAMA MAMA-45


Mhh,unajua docta nimekumbuka jambo,  uliposema kama kuna tukio mama alijifungua akafariki…kuna tukio liliwahi kutokea hapa hospitalini ni muda sasa umepita…, lakini halihusiani na huyu mama…nina uhakika kabisa sio huyu mama,….maana huyo mama tulikuja kusikia kaokotwa akiwa amefariki, akazikwa, na mmoja wa nesi wa hapa alihudhuria mazishi yake…’akasema nesi ,


Je  huyu mama ni nani na kwanini mama huyu aje kudai kuwa kuna mtoto wake alijifungulia hapo, na wakati muhuska mwenyewe, yaani  mama aliyemzaa mtoto hapo akapotea kimujiza, anatambulikana kuwa ni marehemu?, …..

‘Kulikuwa na tukio la mama na mtoto si ndio, .., mama akajifungua kukatokea kitu huyo mama akapotea,….halafu unasema akaokotwa, akiwa amekufa…..sasa sisi tunahitajia kulifahamu hilo tukio, hata kama sio lenyewe, lakini huenda likaleta picha…

‘Docta…’nesi akajitetea

‘Tunataka kusikia kuhusu hilo tukio, chukua muda fikiria kumbuka halafu utuambia kuhuus hilo tukio...unasikia nesi’akasisitiza docta bingwa wa mambo hayo

Tuendelee na kisa chetu

**********

Nesi akabakia kaduwaa akikumbuka kuwa tukio hilo lilikuwa ni siri, ni siri kati yake na wakubwa wake waliokuwepo siku hiyo maana linahusiana na kesi ya mauji ya uzembe,..kesi ambayo ilitakiw akufikishwa mbele ya sheria, lakini ikazimwa kinamna na yeye akiwa mshukiwa mkubwa,..lakini aliyejitahidi kumtetea kwa juhudi zote ni docta aliyekuwa kijana kuliko wote siku hiyo…nakumbuka docta huyo alimtetea na kupendekeza kumchukua mtoto amlee yeye.

Siku ile baada ya kutoka kuchukua maji ya kumuongezea mgonjwa na dawa nyingine, alirudi chumba alicholazwa huyo mgonjwa,…na kukuta huyo mgonjwa hayupo kitandani, na mipira imebakia ikiwa imening’inia kuonyesha kuwa mgonjwa huyo ama kazichomoa mwenyewe au kuna mtu kaja kumuondoa ..

Alipoona hivyo akashikwa na butwaa hadi kudondodsha sinia lililokuwa na maji na daa nyingine…akawa anajiuliza;

Huyu mama kaenda wapi?

Wazo kubwa kwake kwanza ilikuwa huenda  madakitari walikuja kwa haraka wakamkuta huyo mama kwenye hali mbaya wakaamua kumchukua kwenda chumba cha wagonjwa mahututi….akawazia hivyo, lakini kwa jinis ilie mipira ya kuongezea maji ilivyo, haiwezekani madocta wakafanya hivo, ipo shangala baghala bila mpangilio..sio kawaida ya kiutendaji.

Au labda huyo mama alishakata roho wakamchukua kwenda chumba cha maiti? Lakini tendo hilo limefanyika hivyo saa ngapi,..kwani aonavyo yeye hakukawia huko alipokuwa amekwenda,… na kwanini lifanyike haraka kiasi hicho hata bila ya huyo nesi kujua.

Haya yalikuwa maswali ya nesi siku ile.

Alipozinduka kwenye huo mshituka, akahisi huenda mgonjwa kazindukana akatoka kwenda kjisaidia,..basi wazo hilo lilipomjia akilini,  haraka haraka akakimbilia kukagua maeneo mbali mbali, chooni na oisi ndogo iliyokuwepo hapo,..

‘Huenda kadondoka bafuni au chooni, akitaka kwenda kujisaidia au kachanganyikiwa akawa anajiendea ovyo…’akawa anajiongelesha mwenyewe. Na alipohakikisha kuwa sehemu zote hayupo, ndio kwa haraka akatoka mbio kuelekea kule walipo madakitari wakiwa kwenye chumba cha mapumziko….

*********
 Madocta wao walipona huyo nesi haeleweki wakakimbilio hapo wodini…


Madaktari walipofika pale wodini na kukuta kuwa huyo mgonjwa hayupo, walishikwa na mshituko, iweje mtu alikuwa katika ile hali,  kazimia..hajiwezi, aweze kuinuka mwenyewe, na kujichomoa ile mipira na kutoweka, kwa haraka kiasi hicho…au imetokea kitu gani…

Wote sasa wakageuka kwa hasira, na muda hu nesi aliachwa nyuma, na docta mkuu alieuwepo siku hiyo kwenye tukio hilo, akawa wa kwanza kugeuka kutaka kurejea kuel alipomuacha nesi kupata ajibu ya maswali aliyokuwa nayo kichwani lakini kabla hawajarudi huko, nesi akawa keshafika, na kila mmoja akamdaka kwa maswali yasiyokuwa na mpangilio…

‘Huyu mgonjwa yupo wapi, nes umefanya nini..nesi imekuwaje,..nesi.nesi….’

Nesi alibakia kachanganyikiwa hakujua amjibu yupi na majibu gani atakayatoa ambayo yatawaridhisha hawa watu waliotahayari, kwani mgonjwa keshatoweka , na haikujulikana moja kwa moja kuwa mgonjwa ameenda wapi,na ni kitu gani  kimemsibu.

‘Mimi sijui nilitka kwenda kuchukua maji ya kumuongezea, niliporudi nimekuta hivyo..kama mnavyoona..’akasema nesi, na hapo kukawa hakuna maswali zaidi ikabakia vitendo tu.

Ikabidi msako wa harakaharaka ufanyike kila kona, na kila eneo hapo hospitalini, lakini hakupatikana cha mgonjwa au dalili zake, na haikujulikana wapi alipoelekea kama alitoka nje au la, …hata walinzi wakadai kuwa wao hakuwakuuona mgonjwa wa namna hiyo akitoka.

Wakati msako unaendelea, kikao cha dharura kikaitishwa na maswali mengi yakaulizwa na yote aliulizwa nesi, kama ilikuwaje, kwanini uliondoka kwa hali kama ile, je ulichukua muda gani, na uliporudi ulikuta nini…, naye alielezea ilivyokuwa, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza wale madakitari.

Wote waliishia kumlaumu kuwa alifanya uzembe.

Yeye aliendelea kujitetea kuwa alitoka kidogo kwenda kuchukua dawa na dripi za maji kwasababu iliyokuwepo ilikuwa inaanza kuisha, na wapo mashahidi waliomuona..na aliporudi akakuta mlango upo wazi, na alipoingia ndani akakuta mgonjwa hayupo kitandani, na ilionyesha wazi kuwa aliinuka na kuchomoa ile mipira yote mwilini mwake na kuondoka humo ndani.

‘Una uhakika kuwa alichomoa yeye mwenyewe, au alichomolewa…? akaulizwa

`Je ulijaribu kutafuta vyumba vingine kwa muda huo kama hakukuwa na mtu mwingine wa kumsaidia…?' walimuuliza maswali mengi kwa mafululizo

`Nani angekuja amchomoe hiyo mipira na …sidhani kama kuna mtu alifanya hivyo zaidi yake mwenyewe…’akasema docta mwingine.

‘Kwa hali kama ile inawezekana kweli..anaweza kuwa alizinduka,a akiwa kachanganyikiwa..lakini yule mama alikuwa mzaifu sana…’akasema docta mwingine.

‘Nesi akasema alipofika nakuona hivyo, alikagua sehemu zote lakini hakuona hata dalili ya huyo mama..na ndio nikakimbiak kuja kuwafahamisha.., kwani nilifikiria labda mumekuja kumchukua …' alisema huku akitetemeka.

Msako ukwa unaendelea hadi kufika meneo jirani..eneo lote la hospitalini, chumba hadi chumba, vyooni, na kila mahala na mkuu wa ulinzi alikuwa keshapitia kila mahala meneo yote kuzunguka hospitalini..vijna wakasambazwa kila kona, lakini hawakukuta au kupata dalili ya mgonjwa kama huyo, ikawa kama kayeyuka hewani!. Mwishowe ikabakia madocta kujiuliza watasema nini kwa jamaa za mgonjwa pindi wakija kumuulizia mgonjwa wao…

Basi baadaye, baada ya kuhakikisha kuwa huyo mgonjwa hayupo eneo la hospitalini, kikao cha nidhamu kiliitishwa, na hili lilifanyika baada ya kuwahusisha mlinzi mkuu;

‘Sasa huyu mgonjwa inavyoonekana kapotea..na ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kutokea,..tunaogopa kukimbilia haraka kutoa taarifa kituo cha polisi,…unasemaje mkuu wa ulinzi?’ akauliza mkuu.

‘Ni muhimu kama kuwafahamisha polisi maana hatujui ni kitu gani kimetokea, lakini ni badaya kujirizisha wenyewe kuwa kweli tumeshindwa kumpata maana hata tukitoa taarifa mara nyingi unaambiwa kusubiri masaa 24..sasa sisi hayo tuyafanie kazi kwanza..’akasema mkuu

‘Haya endelee ni kazi yenu ila sisi ndio tutakaowaarifu ni nini cha kufanya, ili tuone tatizo lipo wapi..’wakaambiwa walinzi na masako uliendelea kwa siku hiyo na hata kesho yake.

 Baadaye utawala ukaonana polisi waarifiwe, na kituo cha karibu kikapewa taarifa, na wao wakasema watafuatilia… na anayehusika na uzembe akaamiwa afike kituoni, na katika hali ya utendaji wakaoiomba polisi kuwa mtu wao asishikiliwe kwanza, kwani bado wao kama utawala wanafanya uchunguzi, kukawa na maelewano ya chini kwa chini….basi polisi wakasema uchunguzi utafanyika..hakuna kilichoendelea kwa siku hiyo, na hakuna kilichopatikana.

Kikao cha nidhamu kikautana, na kama ilivyotarajiwa na wengi kuwa kikao hicho kikuatana kinakuwa hakina huruma..moja kwa moja ,ikaamuliwa kuwa huyo nesi asimamishwe kazi kwa muda wakati uchunguzi unaendelea kufanyika, na kama ikigundulika kuwa ni sababu ya uzembe wake itabidi afukuzwe kazi!

Nesi akaitwa kujiteta zaidi,…siku hiyo nesi hakuweza kuvumilia,aliishia kulia na hakuwa na la kujitetea, angelijiteteaje, …alibaki kuwaza mengi, kuwa sasa kazi ndio kaikosa, na ataishije,na hiyo ndio ilikuwa ni ndoto yake…aliomba asamehewe….na wakati anaomba msamaha, akasikia sauti ambayo aliiona kama `muokozi’ wake wa siku ile’

‘Jamani mimi naona tutakuwa hatujamtendea haki huyu nesi,…’ akainuka dakitari kijana kumtetea yule nesi, lakini kabla hajaelezea lolote. Yule dakitari bingwa akamkatiza

‘Sikiliza kijana, huyu nesi alijua kabisa kuwa huyo mgonjwa yupo katika hali mahututi, ndio maana tukamuacha na huyo mgonjwa, na anajua kabisa alitoka kwenda, huko kuchukua dawa, lakini akajisahau na kuanza kupiga soga, ..tumeulizia wenzake, na hata mkuu wa manesi kasema alimkuta akiwa anachngulia mdirishani.

‘Huu ni uzembe..alifika pale tunapofanyia kazi akawa anachungulia kuona kama tumemaliza kazi, ili atoroke, au alikuwa na sababu gani nyingine ya kuja kutuchungulia tukiwa tunaanya kazi..hili halivumiliki….halisameheki…nawajua sana hawa manesi wa hapa, wanapenda sana kuongea kuliko kuchapa kazi, nami, napendekeza kuwa itolewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine…’. akasema dakitari bingwa wa kitengo hicho !

‘Hili hata mimi nakuunga mkono, nimeona tabia isiyorizisha kwa watendaji wetu hasa manesi, wagonjwa wamekuwa wakilalamika…wana lugh chafu…wanawabeza wagonjwa…huduma mbovu,..sasa hili litatuweka uchi kama likiika kwa watu…kabla hatujaharibu kazi zetu mimi naona adhabu kali itolewe….’ akasema kwa hasira yule dakitari mwingine!

‘Kwani wewe kijana ulikuwa unataka kusema nini , naona ulikuwa na hoja, hebu tumsikilze kwanza huyu kijana..’ akasema mkuu wa hiyo hosptali.

‘Kutokana na maelezo ya huyo nesi inaonyesha kuwa , hata angekuwa nani kosa hilo lingetokea…! Ndio alitakiwa kutumia simu kumfahamisha mwenzake alete hizo dawa, lakini kama ujuavyo, unaweza ukapiga simu mpaka ukachoka, mwenzako asikujibu, yeye aliona mgonjwa bado yupo kwenye ‘koma’, akaona akimbie mara moja kuichukua hiyo dawa na atamkuta hajaamuka, inavyoonyesha huyo mgonjwa alizinduka ghafla na kuondoka.

‘Yah, lakini je alijaribu kupiga simu..maana usilaumu tu kuwa ukipiga simu hakifanyiki kitu..yeye hakujaribu kufanya hivyo, kweli si kweli..?’ akauliza docta bingwa.

‘Ndio kosa limefanyika, lakini kwa kumhurumia, mimi napendekeza kuwa yeye abebe jukumu la kumlea huyo mtoto, tukumbuke kuwa kuna mtoto mchanga kaachwa, je mtoto huyo atalelewa na nani, ..sijui kuna taratibu gani, mimi najiuliza kichanga hicho hakina mama wala baba au ndugu yoyote, nani atachukua jukumu hilo…’ akasema dakitari kijana.

Kauli ya dakitari huyo kijana ikafanya jopoo zima la nidhamu kukaa kimia kwa muda, kwani maneno yake yana hekima, ikabidi  madakitari  waangaliane, walipogundua kuwa kweli mtoto anahitaji mtu wa karibu wa kumuhudumia, wakawa kimya kidogo kuwaza kila mmoja akijua kuwa kumbe kuna jukumu jingine, kama hakuna mu mmojawapo atabeba hilo jukumu…!.

‘Sawa kabisa,…mimi  naona Kijana kanena vyema,..jamani,  hilo hatukulifikiria, na mwisho wa siku tungelihangaika wapi pa kumpeleka huyo mtoto. Na nafikiri hili halina mjadala, litakuwa jukumu lako wewe nesi kutafuta jinsi gani ya kumhudumia huyo mtoto, na kama kuna mambo ya kisheria yatahitajika baadaye, kama huyo mama au jamaa zake hawataonekana basi, hospitali itatoa msaada huo.

‘Na sio kwamba sheri itakaa kimia bado tunaliuatilia hili jambo kwa ukaribu wake,…kwa hivi sasa tunalifanya hili kwa kumsaidia nesi..kwahiyo iwe siri….hili tunakubaliana hapa hapa..huku tukisema uchunguzi bado unafanyika….’akasema mkuu huyo

Eti mnaonaje…nesi atamchukua huyo mtoto na yeye atajua la kufanya, kama atahitajia msaada wa kisheria…hilo tutaliangalia…u kuna lolote zaidi uhusu hilo jukumu..?’ akasema mkuu wa hospitalini na alipoona hakuna hoja ya zaidi, akamgeukia yule nesi na kumuuliza kama analakusema, au bado anaona kaonewa kwa adhabu hiyo, kwani vinginevyo angeishia kufukuzwa kazi….

Yule nesi akasema hana la kusema zaidi na atajaribu kutafuta njia za kumlea huyo mtoto mpaka mama yake atakapoonekana…

Nesi japokuwa alikubaliana na hilo lakini kichwani akawa anajiuliza kweli ataweza jukumu hilo, jisni gani ataweza kujigawa, kazi na kulea huyo mtoto, ni kitu ambacho hakukitarajia na hakikuwa katika mpangilio wa maisha yake ya karibuni, lakini akawa hana jinsi, vinginevyo kazi ataikosa, na hata kufungwa…!

Baada ya hicho kikao, yule nesi alimtafuta dakitari kijana ili apate angalau kumshukuru kwa kumukoa kwenye janga la kufukuzwa kazi, lakini ikawa vigumu, kwani kazi zilikuwa nyingi wagonjwa mahututi walikuwa ni wengi,…na wakitoka hapo wamechoka..lakini baadaye akapata nafasi ya kukutana naye;

 Ilikuwa wakati yeya anatoka kuelekea huko alipo mtoto kuangalia taratibu za kumchukua huyo mtoto na dakitari kijana alikuwa katokea huko wanapohifadhiwa watoto, akiwa na simu ambayo ina vii vingi ikiwemo kamera ya hali ya juu, video..na inaonekana alikuwa akiitumia.

Kila mmoja alikuwa na haraka, wakajikuta wanagongana..na walioanaliana kila mmoja akamtaja mwenzake kwa cheo chake;

‘Docta…

‘Nesi..

Nesi akiwa anaokota barua aliyopewa na utawala, akasimama haraka kutaka kuongea na huyo dakitari kabla hajaondoka kwenye upeo wake, akasema;

‘Samahani docta naona siku ya leo itapita bila kupata muda wa kuushukuru…japo kuwa kwa kaui tu..kauli tu ya kushukuru..’akasema nesi,a na docta ambaye alishaanza kuondoka…akasema;

‘Oh..nesi.., usijali..ni kawaida tu…na usiwe na wasiwasi kwa hilo.., hiyo ndio mitihani ya kikazi,a na tunapokutana sehemu za kazi kama hivi na kuna namna ya kusaidiana ni wajibu wa kila mmoja wetu kufana hivyo, sisi kutokana na kazi ni ndugu, hakuna cha ubosi au nani..anayejiona ni toauti, kwasababu ya cheo huo ni ubainfasi wake tu..…’akasema docta.

‘Ni kweli lakini ueona ilivyokuwa,…madiktari wote walishakubaliana kuwa nifukuzwe kazi kasoro wewe tu…yaani wamesahu mazuri yangu yote…na hili sikukusuadia kabisa…na sikujua kabisa litatokea,…lakini nakushuru sana wewe maana ..hata sijui niseme nini, umenitetea..sikutarajia kabisa…’akaziaid kusema.

‘Hawakufanya hivyo kwa nia mbaya kuwa wanakuchukia hapana…ila sheria inawabana..na mhh, usijali…mimi nilifanya nikijua ni sahihi kuanya hivyo, hata wewe, ungelifanya hivyo…ni swala la kusema unavyoona ..au sio…’akasema docta na nesi akawa anajaribu kusikiliza kwa makini anachoongea docta huyo, lakini kwa jinsi kulivyokuwa na kelele , uoande ule wa ili wanapokuwa wagonjwa wa nje, hakuweza kusikia vyema…akawa kama anabahatisha tu kuwa mwenzake kasema nini.

‘Je wewe una mipango gani, kwani inatakiwa uhakikishe kuwa mtoto anapata huduma zote, je utakuwa na nafasi hiyo?’ dakitari kijana akasema sasa akijaribu kutaka kusema jambo muhimu kwa huyo nesi, na alitaka asikia anachosema kwani aliona kuna umuhimu wa kuongea naye. Sasa akaonekana kutulia, japokuwa mwanzoni alionekana kuwa na haraka.

‘Mipango ya nini…?’ akauliza nesi, hakusikia maneno ya mwanzoni, vyema

‘Ya kulea huyo mtoto..?’ akasema docta.

‘Mhh, mimi kwakweli nimekubali tu maana hebu nambia pale ningelisema nini tena…kwa hivi sasa hata sijui nitafanyaje..maana hata jinsi ya kuishi na mtoto..mmh, sijajipanga kwa kweli najiuliza na kukosa jibu, ..’akasema nesi  huku akionekana kuwa mbali kimawazo, na dakitari akalijua hilo kuwa huyo nesi anahitajia ushauri.

‘Kama unahitajia ushauri mawazo…useme mimi nipo, wapo madakitari wengine ni muhimu upate ushauri wa kuja kukusaidia,..japokuw amamuzi yameshatolewa..’akasema dakitari kijana.

‘Yaani kwa hivi sasa hata sijui niombe ushauri gani…mwenyewe kichwani hata siamini..maana matukioo ametokea kwa haraka hili linakuja ..mara jingine…unaonaeeh…nimejiuliza sana nifanye nini , nimeshindwa, na ….’ Akakatisha maneno alipoona dakitari kijana anamsogelea karibu yake kusikia alichokisema maana hapo walipokuwa akiongelea kulikuwa na kelele nyingi za wagonjwa.

Nesi akainua uso kumuangalia huyo dakitari,  kwani alikuwa karibu yake sana na hakutarajia itakuwa hivyo, kuwa naye wakiwa wawili, na sehemu ya upweke japokuwa sio sana, maana watu wanaopita mwisho wajengo kwenye milango mikuwa ya kutokea wanawaona.

Nesi alipoona dakitari huyo kijana kamsogelea,  na sasa wanaangaliana…akabakia kaduwaa, dakitari alifanya hivyo akitarajia na nesi naye atasogea mbele zaidi ili kuzikwea zile kelele, lakini nesi akawa kasimama pale pale, sasa wakawa wanaangaliana  uso kwa uso, ilikuwa ni kwenye korido na sehemu hiyo ni nyembamba kidogo, mtu akiwaona atajua hao ni wapenzi.…

Nesi hakutarajia hilo…na hakusogea, akawa kasimama pale pale tu…na ile kuwa karibu  na huyo dakitari, ambaye muda mwingi alikuwa akimuwaza, ilimfanya yeye  ajisahau..na akili akiyasahau yaliyopo mbele yake… .

Nesi ghafla , bila kutajia akajihisi mwili mzima ukisisimuka. Nesi kwa akili yake ya haraka alijua kuwa mwenzake kamsogelea hivyo kwa nia ya kumliwaza kwa kumkumbatia, kwahiyo aakwa anasubiria kushikwa kinamna..., kumbe Dakitari kijana, alimsogelea ili asikie nini anachoongea, kwani sauti ilikuwa haisikiki vizuri, kutokana na upepo.

Akili ilivyo, tamaa na hamasa hutekwa mara moja na majambo kama hayo,..hasa kwa matendo yale ya kufurahisha nafsi,..nesi akakumbuka jinsi gani alivyokuwa akiisubiria hiyo nafasi na kuiombea itokee japokuwa, angalau kama hivyo…japokuwa imekuja muda ambao sio muafaka..lakini akaona sasa muda ndio huo akiukosa tena …basi, atajijutia..sasa akataka japokuwa sio sahihi, kumuonyesha huyo dakitari kuwa kweli anamapenda...

Akainua uso wake kumtizama dakitari kijana usoni,….., akajikuta dakitari kijana akiwa kamgeuzia sikio..akaona ajabu….,’Au kageuka tu kutizama kwingine baada ya kuniona niminama, siuangalii…’…akawa anajiulia nesi

‘Umesema nini maana nilikuwa sikusikii vyema,..unajua kuna kelele..unaweza kusogea huko, huko…ki-do-go…’dakitari kijana akaongea na kuonyeshea kwa kiganja cha mkono ili nesi asogee, lakini nesi hakusikia hilo, ..alishazama kwenye dunia nyingine, akawa kasimama pale pale macho yake hayabanduki kumungalia huyo dakitari usoni, akajikuta akisema;….

‘Ohhh, …hata sijui niseme nini…nikushukuruje dakitari wangu, bosi wangu mhhh… mimi nakusikiliza wewe tu,  maana hapa akili sio yangu..leo kurwa natauta muda tuongee, nikushukuru…yaani we acha tu….nilikuwa siku nyingi natafuta….’akasema nesi, lakini docta akamkatiza.

‘Sister, sikiliza nilikuwa nakuuliza hivi kwani wewe huna ndugu, ambao wana nyumba,…yeney nafasi…si unajua…au  ndugu wanahitaji mtoto..si unaelewa,…., kwani dunia hii ilivyo…., wakati wengine wanatupa watoto, kuna watu wengine wanawatafuta watoto hao hao..’akasema docta na nesi akawa kimia.

‘Siumesikia hilo mara nyingi, hata kwa redio au kwenye runinga au sio…hata wewe mwenyewe kulithibitisha hilo, au sio, kuna watu hawalali, wanatamani kupata mtoto hata wa kule, …kwa udi na uvumba..au nimekosea sister hawo…?’ Docta kijana alimwambia, na aliposema hayo maneno nesi akakumbuka kitu…..

Nesi uso ukapanuka kwa furaha..ni kama vile mtu kapewa kitu cha thamani au zawadi ulani asiyoitarajia, jinsi gani uso unevyomemeteka kwa kuonyesha ile furaha, ndivyo ilivyokuwa kwa huyu nesi, …akatoa tabasamu la nguvu, huku akimuangalia dakitari kwa uso uliojaa bashasha…kwanza akatulia…, halafu akasema;

‘Umesema nyumba yenye nafasi…kwangu twaweza kuongea..kwangu unapafahamu eeh…hata leo…kwani wewe ulisema unaishi bado na wazazi wako kwasasa…?’ akauliza huku akionekana kuwa na furaha hata dakitari akashangaa.

‘Kiukweli docta leo…ooh, pamoja na balaa hilo..lakini sijui nisemeje..yaani niseme tu  furaha isiyomithilika. ..kwanza umenisaidia,..maana nilishakata tamaa, unajua niliwapigia ndugu zangu simu, nikashindwa hata la kuwaambia nikawa nalia tu,..nilijua nakwenda kufungwa…na ukatokea wewe muokozi wangu…yaani..hata nisemeje,,,maana umenisaidia sana na bado..umeniambia jambo..oh, docta niruhusu..oh’akatulia akionekana kujawa na furaha.

‘Kwani vipi sister mbona umebadilika ghafla….?’ Akauliza dakitari kijana.

‘Unajau docta umeifungua akili yangu….maana sijui nisemeje…unajua mungu ni mkubwa, bado tu… unaendelea kunipa ushauri ambao sikuwa nimeukumbuka…, kwakweli niameamini kuwa wewe ni sehemu yangu kwenye nafsi yangu, moyoni mwangu, nisamehe tu kama nitaongea vibaya, lakini kwanza hebu nifafanulie, kwanza umeniulizia kuwa kuna sehemu yenye nafasi…ukasema nyumba yenye nafasi, ni ili tuongee au….?’ akauliza nesi

‘Hapana..sikumaanisha hivyo… unajua nesi, nikaumbie ukweli,  mimi hapa hospitalini, nipo kwa muda tu, na nina lengo moja kufanikisha ndoto zangu za kuwa dakitarii bingwa..ni kiukweli mimi…bado naishi na wazazi..sijajipanga kuwa na kwangu,…na- na bado naendelea kusoma, sijajua mipangilio itakuwaje huko baadaye…’akasema dakitari.

‘Lakini unaweza kuanza mipango yako sasa haiwezi kuzuia kusoma au ? na vitu kama seehmu ya kukaa, hata chumba, au vyumba ni muhimu uwe navyo au? Na wewe unahitajika hata kupewa nyumba, si ndio…halau mengina kama mke,..ynakuja au..na mke inaanzia kwenye urafiki, au unaye tayari..?’ akauliza nesi.

‘Unajua sisiter..nimekuelewa, lakini kiukweli,… kila kitu na muda wake..mimi hayo muda wake bado, siwezi kujidanganya…lakini ndio kam binadamu ni lazima uwe na matarajio ya baadaye, yaweza ikawa ndoto, kama hutayafanyia kazi,…mimi ni mwanasayansi, sitakiw sana kuishi kwenye ndoto…si unajua, naangalia uhalisia,..’akasema

‘Najua…’akasema nesi.

‘Ndio…, nikianza kazi, na kutulia hayo ya sehemu ya kukaa, mke..yatakuja yenyewe,....kwa hivi sasa hilo halijaniumiza kichwa ila mimi..sister,  nilikuwa nakuulizia wewe...maana sasa una mtoto, hana baba, lakini  mama yake ni wewe, na kwa ajili hiyo unahitajia sehemu yenye nafasi…au sio’akasema

‘Yah…nimekulewa, lakini kwa hali hii, najuauananihurumia sana, na naogopa hata kukuombamsaada zaidi, …nikisema hata wewe unaweza kuwa baba yake, sijui kama nitakwua nimekosea..au sio?’akasema nesi na dakitari akatabasamu na kusema

‘Ni kweli …kiujumla huyo mtoto kila mwenye moyo wa huruma atakuwa ni baba yake…wapo watoto kama hao, wengi, ..unawakuta mitaani, jamii haiwajali,  mimi ni baba wa hao watoto na kila mwenye hekima, mwenye moyow a huruma ataliona hilo,..hebu jiulize wao walipenda iwe hivyo, au tujiulize ina maana mungu hana huruma kwao, awaache hivyo…hapana hilo ni mtihani kwetu, …ndio maana mimi kama baba nimeanza kwa kujitolea kimawazo, au sio..’akasema dakitari.

‘Ndio ..dakitari, mawazo yangu ..natamani iwe hivyo, mimi na wewe tunaweza tukamtunza huyu mtoto kwa pamoja, yaani akajiona kama ana wazazi aisgundue kabisa....mimi na wewe kwani haiwezekani…?’akasema nesi, na dakitari akatabasamu zaidi na kusema.

‘Acha,utani sister, mimi bado ..sinimekuambia bado nasoma…sasa sister, naona tusipoteze muda,…hili ninalotaka kukuambia ni muhimu sana…nilitaka kuulizia, kama unao ndugu ambao wanaweza kukusaidia, au ndugu ambao wanahitajia mtoto, itakuwa bora zaidi kwako,..unaonaje hilo wazo..?’ akasema dakitari ambaye alionekana kutokutulia kwa kuwa karibu karibu hivyo na huyo nesi, wakiangalaina uso kwa uso.

‘Oh…ndio maana nikakuambia nina furaha sana moyoni, furaha isiyoelezeka,..wewe umenikumbusha jambo, jambo muhimu sana, sijui kwanini sikulikumbuka kabla…, …kweli wewe ni wa pekee …ahsante sana dakitari, unajua wazo kama hilo lilikuwa limenitoka kabisa..naona wewe mmmh, hata sijui niseme nini ..tungeishi pamoja ingelikuwa ni bora zaidi, maana mawazo yako yanakwenda sambamba na ya kwangu unaonaje…usinifikirie vibaya, ila naona hivyo tu samahani kama nimekosea..’akasema nesi

‘Kwanini…ni kweli nimejiuliza sana furaha hiyo kubwa imetoka wapi ghafla, maana tokea kwenye kikao nilikiona umenyong’onyea..?’ Akauliza dakitari kijana, sasa akiwa anajaribu kusogea nyuma.

‘Mhh..unajua nahisi tukio hili limetokea kwangu ili …dada yangu apate mtoto..’ akatabasamu na kuinua  uso kumuangalia dakitari kijana,..na dakitari kijana akakwepesha macho na kuangalai kwingine.

‘Dada yako…apate mtoto..anahitajia mtoto au?’ akauliza dakitari kijana kwa mshangao

Nesi alijikuta tu, keshainua mikono, huku akiwa kamsogelea dakiatri kijana, na sijui ilikuwaje akajikuta kamkumbatia..na kwa haraka akambusu shavuni…. Na tendo hili lilimuacha dikitari kijana akiwa kashikwa na butwaa.

‘Ahsante sana..yaani ungelijua… sijui hata nikushukuruje……’akasema nesi, na akataka kuachia mikono yake, kwani alijiona huenda kafanya jambo lisilofaa, lakini alitamani liwe hivyo, na mikono ikawa mizito kuondoka mwilini kwa dakitari huyo.

Dakitari kijana kwa muda ule hakulitarajia hilo tendo kabisa, na kiukweli, japokuwa kama kijana alikuwa na damu inachemka…lakini hakupendelea kabisa hali hiyo imtawale kipindi cha kazi, na mazingira yenyewe ambayo aliona yamejaaa mitego mitego…alishajijengea msimamo wake, na hakutaka kuuvunja, akajaribu kujizuia, na kuzuia hisia zozote kwa hasa kwa hao manesi hapo hospitalini.

Ndio kama kijana kuna siku na siku analiwazia sana hilo, na hata akikutana na wenzake kuna muda wanaliongelea, hasa ikizingatiwa kuwa hospitali hiyo imejaliwa kuwa na manesi wazuri na warembo…basi wakikutana na wenzake kuna muda wanabadilishana mawazo, na maswala kama hayo hayakosekani ..

Ni katika kuongea pia na wengine, kunahali ya kutaniana…na kwa vile alikuwa kijana ukilinganisha na wenzake..na pia alijaliwa sura ya kuvutia, wenzake wakawa wanamuulizia kuwa je yeye kamchagua nani kati ya warembo waliokuwepo hapo..yeye kiukweli kama ingelikuwa ni lazima kufanya hivyo, kuchagua rafiki,  huyo nesi angelikuwa ni chaguo lake..,. Yalikuwa ni mawazo tu kichwani.

Hata siku moja wakati anaongea na wenzake, alisema;

‘Najua kabisa, ukijiingiza kwenye maswala ya mahusiano, ..hasa kwenye sehemu za kazi utajikuta ukikwazika hapa na pale, na matokea yake hutaweza kutimiza malengo yako..na utendaji wako unaweza kuwa na mapungufu …. Mimi sitaki mahusiano na nesi yoyote hapa au sehemu yoyote nitakayokuja kufanyia kazi…’akasema na wenzake wakawa wanamtania kuwa anawaficha ukweli, ni lazima anaye rafiki hapo hospitalini.

‘Hii ni kawaida kwenye kazi zetu, maana sisi hapa tunajuana,…ilivyo kwa vile muda wote tupo pamoja..hatuwezi kudanganyana.. kazi hizi zinachosha bwana…, na sia mbaay ukipata muda kuwa na mwenzako mkabadilishan mawazo au sio..kazi na dawa..au sio….’akaamba na jamaa ake waliyekuwa karibu naye sana, yeye akacheka tu

‘Ndo hivyo…najua unaye ndio maana unacheka…, wakati mwingine unaweza kukutana na staff mwenzako maana mumezoeana naye, mkaliwazana..sio lazima muwe wapenzi wa kabisa kabisa..ni kupotezeana mawazo tu..’akawa anashawishiwa na wenzake.

‘Mmm..mimi naona muda huo sina kwa hivi sasa..,hasa kwa wafanyazi wenzangu wa kike, …..nawaheshimu kama dada zangu tu…si zaidi, ‘akasema

‘Mhh..wewe wasema tu…najua wewe una aibu sana,..lakini ipo siku nitakufuma na yule nesi, nitakupiga picha niibandike ukutani…’akasema mwenzake.

‘Hahaha…haitatokea..wewe hunijui eeh,… ujue mimi nina msimamo..usinione hivi…yaani unikute kipindi cha kazi nipo na msichana, tunakumbatiana,..aah, hapana, mimi kwangu naona ni makosa ya kazi…na sitaki kabisa nifanya hayo makosa, nina mengi ya kufanya nikiwa kazini sio hilo….’akasema

‘Nakuambia utakuja kuon siku yake unajifanya msiri sana..yule yule mnayekuwa naye kazini wakati wote, huyo huyo anaweza kukubadili mawazo …ipo siku nitakunasa naye..’akaambiwa.

‘Niamini, hilo halitaweza kutokea..’akasema

‘Unajua …kuna yule sister,  nesi mkuu, aliniambia kuwa wewe unajifanya huna habari na akina dada, lakini una madhaifu yako,..kwa vile tu hujapata wa kukuchangamsha..na kaahidi kuwa ipo siku atakunasa, aufichue unafiki wako..kwani kashakuona kuwa wewe na yule nesi mpo marafiki, mnaangaliana kwa kujificha… na kasema siku akigundua tu…si unamfahamu huyo dada alivyo.’akasema

‘Yule dada ..hata simuelewi…kuna siku kaniganda..unajua nilitamani nimtie kibao…yaani dada mtu mzima,...yule si kaolewa na watoto hata wajukuu anao ….hutaamini,..nilimchenjia… mdada mzima ovyo…, ana..weeeh, nilikasirika mpaka akajua kweli nimekasirika…, halafu eti… badala ya kuona kuwa katenda kosa,anacheka, …kwa dharau kweli…’akasema huyo dakitari kijana.

‘Yule ndivyo alivyo bhana…, ukimjulia wala huwi na shida naye, ni mtu mnzuri sana, wewe akianza matani yake wewe jifanye kama unampenda vile…basi anaona rahaaa…. Wewe waakti mwingine fanya atakavyo…ilimradi usiende mbali…maana anakutega ukijifanya umenasa, atakuumbua, sio kweli anavyofanya ukahisi kadhamiria,..’akasema

‘Sasa kwanini anafanya vile?’ akauliza

‘Ni mtu wa kihivyo, utani, mwingi…nakuonya usije ukahadaika ukafikiri ni muhuni… uwe makini sana naye, kuna watu wameumbuliwa…basi ukimjulia …aaha, utafurahia kuwa naye kazini lakini ukijifanya unamdharau atakuchezea..atakufanyia vituko na ole wako uje kufanya kosa…hatakusamehe…’akasema

‘Mimi nilitata kumshitaki..’akasema dakitari kijana, na mwenzake akacheka hadi kutoa machozi

‘Hahaha..kumshika, kwa kosa gani…hahaha, hivi wewe upoje..wewe mwanaume kweli..hahahaha..nikuambie kitu ungefanya hivyo ungeumbuka…., hivi unamfahamu yule dada alivyo, madakitari wenyewe wanamuheshimu…watu wasiomjua wanaweza kumuhisi vibaya, lakini ..fika nyumbani kwake, huwezi amini..yeye anafana hivyo kama kuwafanya watu wajione wapo pamoja..ni ..sijui niseme nini..katabia kake tu…’akasema

‘Kwangu mimi nimemzarau…kiukweli sikutarajia kuwa atanifanyia hivyo…lakini nimemsamehe..kama ni utani tu, basi,….’akasema

‘Unajua nikuambie kitu, yule dada anajua kuongea anajua kugeuzia mambo..ungejidanganya ukaenda kushitaki,a ngetoaboa siri zako zote..auanjua mengi kuhusu wafanyakazi,…nakuambia siku hiyo ungeaibika..’akasema mwenzake.

‘Mimi niliona ajabu anavyowashika -shika hata wasichana  ‘akasema

‘Ndivyo alivyo..ni utani tu, na wasiomfahamu wanamfikiria vibaya, hana lolote yule..ni seehmu ya kuwafanya wasichana wafurahi tu na wachape kazi, …pamoja na utani hataki uzembe……’akasema mwenzake.

‘Mhh, hata mimi huko alipokwenda nilishambadilikia …mimi nikiwa kazini ni kazini tu…’akasema

‘Mhh…ngoja ipo siku atakunasa na huyo nesi, ..humjui yule dada, atakutundika uchi….unajua kutundikwa uchi, anakutangaza kusipofaa…nikuambie kitu mchukulie kama mtani wako tu…utafurahia maisha yake..’akasema.

‘Unajau mmi sijui nipoje…naona kuwa nikiwa  na urafiki wa namna hiyo kazini nitashindwa kuwajibika..na kama nikitaka kutafuta rafiki nitafanya hivyo kwa wakati muafaka, na sio hapa kazini, au sehemu nitakayofanyia kazi…….sitaki nije kushindwa kazi kwa sababu ya mapenzi…’ alisema hivyo akiaongea na rafiki yake, ambaye alitaka kujua kwanini yeye hana rafiki wa kike.

Leo anajikuta yupo na nesi..na walivyokuwa wamesimama mtu yoyote atasema ni wapenzi…hakutaka kabisa aonekane na wakati anaangalia huku na kule mara akamuona

Alikuwa yule mkuu wa nesi, alikuwa kwenye chumba cha juu akiwaangalia na mwani yake akijifanya anasoma makabrasha yake…, na kashika kitu kama simu…, ndio maana alijisogeza karibu na huyo nesi ilikuwa mbali na upeo wa kuonekana,…na ilikuwa ni pamoja na kutaka kusikia anchoongea huyo nesi,na kwa muda ule nesi yeye hakujua lengo la mwenzake


Nesi hakulifahamu hilo….

WAZO LA LEO: Kiongozi bora ni yule aliye mfano bora kwa watendaji wake, kitabia kikazi na hekima, na asiwe mkali wa kutisha na kuwafanya watendaji wake kama watumwa na kumuogopa yeye kama mnyapara...yeye kama kiongozi bora anatakiwa awe karibu na watendaji wake..na watendaji wake wajihisi ni sehemu ya familia hapo kazini.... 
Na kwenye masilahi, kiongozi bora, ni yule anayejali watu wake `kwanza', kabla hajajali 'tumbo' lake, na ajue kwa anabeba dhima, sio kwa hao watendaji wake tu na hata afikirie na familia za hao watendaji wake, kwani utendaji huanzia toka nyumbani, kwani akili ikitulia toka nyumbani, ndivyo utendaji utakavyokuwa mzuri ofisini na sehemu za kazi.


Ni mimi: emu-three

No comments :