Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, March 9, 2015

NANI KAMA MAMA -42


‘Mhh, ina maana huyo mama ni mtu gani, na kwanini watu wachanganyikiwe wakimuangalia.au wakitaka kumuangalia sura yake…?

‘Lakini docta bingwa kaweza kumuhudumia na ili kufanya hivyo yeye ilibidi kuiona sura yake, mbona hajachanganykiwa..?’

Hayo yalikuwa maswali ya nesi akitembea kuelekea huko kwa docta aliyemuita ambaye ndiye anayeshughulika na huyo mama.

Tuendelee na kisa chetu

*************

‘Nesi mkuu tumekuita hapa, maana kuna kazi kubwa, sio kazi kubwa sana kama tutazingatia taaluma yetu…’akasema docta mkuu wakiwa kwenye jopo maalumu, ofisini kwa docta bingwa….

‘Huyu mama kaletwa hapa kwa matibabu, na kiujumla hatujui sana historia yake, kwani waliomleta hapa hawakuweza kutuelezea vyema, walisema watarudi tena lakini hawajawahi kufanya hivyo….kwanza mkumbuke walipomleta hapa, walimleta kama maiti na haya ya kuwa mama huyu bado yupo hai, wamechukulia kama huyu mama kafufuka..’akaanza kuelezea docta mkuu.

‘Mimi siku ile …nikiwa nakabidhiwa na mwenzangu…tulipata taarifa kuwa kuna maiti imeletwa na mgonjwa mmoja….kwahiyo kama ni maiti hatukuchukuliwa uharaka sana, tukawa tunatibia walwe wenye dharura…nilishawaambia hilo.

‘Na kama mlivyosikia….’akasema na kucheka kidogo kuonyesha kuwa ni kichekesho.

‘Nilipofika kumkagua huyo mama, badala ya maiti mimi  nikakuta yupo hai…na muda huo alikuwepo mtu mmoja ambaye nilijua ni ndugu yake, na nilipogeuka kumuangalia nikakuta huyo mtu keshaondoka,..sijui ni kwasababu ya kuogopa maana kama walileta maiti, ..na sasa mtu yupo hai, unajua tena,…’akasema docta.

‘Na kwa muda ule sikuwa na haja ya kufuatilia sana, nikijua ndugu zake wapo…na zaidi ningelipata taarifa yoyote kutoka kwa hao askari waliomleta, maana aliletwa na maaskari…’akaendelea kuongea docta.

‘Sasa huyu mama kama mnavyoona hataki kabisa kufunuliwa hiyo nguo aliyojifunika usoni mimi nimetii matakwa na utashi wake, na ni emfanya hivyo hivyo…mimi ili niweze kumtibia…nilimuomba samahani,… kuwa mimi ni docta bingwa, na nina haki ya kumuangalia usoni kwa dharura kwa ajili ya kumtibia, ni hekima ndogo tu kwa watu kama hao, wanaelewa….nilimuomba sana na kumuahidi kuwa sitatoa siri yake..kama kuna siri kutokana na yaliyopo usoni mwake, au kama ni kutokana na imani yake….’akasema docta.

‘Ilichukua muda kukubali….na nilipoanza kumfunua hakuleta pingamizi nikafanya yale yanayostahiki, na nikamwambia wazi kuwa nitajitahidi kutokusema yale ambayo hakutaka yaonekane kwa watu….kiufupi ni hivyo…na nyie mnatakiwa kuyafahamu hivyo…ila kiukweli huyo mama kajeruhiwa usoni…kakatwa katwa na mapanga, lakini yale majeraha hayakuingia ndani kugusa mfupa wa kichwa, ..ila yameharibu wajihi wa usoni…’akatulia

‘Sina uhakika sana kuwa mama huyu  ..labda ni imani yake kufanya hivyo….na sijui kwakweli kuwa hali hiyo alikuwa nayo toka zamani , au ameamua kujifunika hivyo kutokana na majeraha aliyo nayo…’akasema docta

‘Toka zamani alikuwa akijunika hivyo..’akasema nesi na kumfanya docta amgeukie  nesi huyo kwa hamasa, akasema;

‘Kwahiyo ni kweli wewe unamfahamu vyema huyu mama?’ akauliza docta.

‘Kidogo…kuna kipindi nilikwenda huko kijijini nikakutana naye akipita mabarabarani akiimba, ni hivyo tu kumfahamu kwangu na kipindi hicho ni muda, kabla hata hajavamiwa na watu na kujeruhiwa hivyo…kwahiyo mimi sizani kuwa anajifunika hivyo kwasababu ya kuharibiwa sura na mapanga…nahisi kuna sababu nyingine…’akasema nesi.

‘Oh sasa kama unamfahamu japo kidogo tutapata nafuu…na je huenda kama ulijaribu kumfuatilia..na kumjua zaidi…mimi ningelipenda kujua je huko kijijini alikuwa akiishi na nani , au alikuwa kitembea tembea tu?’ akaulizwa nesi.

‘Ina maana hamjaongea na polisi, akawaelezea ilivyo, nakumbuka ulisema kuwa utaongea na polisi wanaochunguza hilo tukio….maana mimi kumjua kwangu ndio huko kumuone akipita barabarani ….sijui zaidi docta’ akasema nesi akijaribu kuficha ukweli .Hakutaka kujihusisha zaidi na huyo mama kutokana na yanaoongewa na watu.

‘Hutaamini..yule askari aliyemleta huyo mama, nasikia naye anaumwa sana, kichwa, halafu…nasikia kama kama kachanganyikiwa…na zaidi yule mwenzake ambaye alikuwa ni dakitari wa kundi lao…kachanganyikiwa kabisa, …’akasema docta akitabasamu kidogo.

‘Mhh imekuwa hayo..mbona balaaa..’akasema nesi mwingije aliyeitwa kwenye hilo jopo.

‘Yaani ukihadithiwa ….hili tukio, sijalipaat vyema, lakini kidogo nilichokipata utaona ni kitu cha ajabu..lakini..ni …hali halisi ya eneo hilo..watu hawanielewi nikisema..haya mabangi, na ufinyu wa elimu…nah ii tabia ya kuuana uana, damu za watu zanamwagwa tu kiholela…unajua kitaalamu yana atahari zake…sasa huyo askari mwingine imebidi wamrudishe kijijini kwao wakashughulikie kienyeji…sijui....’akasema docta.

‘Mungu wangu kwanini…ni kwasababu ya huyu mama?’ akauliza nesi.

‘Sizani,….mimi sina uhakika sana kuwa ni kwasababu ya huyo mama,…huyu mama kwa vile imeangukia kwake, anachukuliw akama kigezo,…na unajua mwanadamu akishindwa hoja…akawa hana njia nyingine atatafuta upenyo tu..hata kama ni kwa kusingizia..ilimradi afanikiwe kile anachokitaka…sasa huyu mama wanamtumia tu…  kwani huyu mama ana nini cha kuwafanya wao wachanganyikiwe..?’ akauliza docta.

‘Si wanasema hataki watu wamuangalia usoni…’akasema nesi.

‘Unajau kuna kitu tukiangalie kwa makini,..ni kweli kuna imani na kuna utashi wa mtu…kila mwanadamua na utashi wake, mimi naweza kusema sitaki miguu yangu ionekane, nikawa najifunika hivyo…haitakiwi mtu kuja kuniingilia, …sasa ingia ndani kabisa kwenye imani za watu ambazo zinagusa hisia ya ndani…,’akasema docta.

‘Lakini kwa huyo mama…docta sizani kama anafanya hivyo kwa iamni..kachanganyikiwa tu..’akasema nesi.

‘Una uhakika…?’ akauliza docta na kabla hajajibiwa akasema;

‘Kiukweli kuna watu wana imani zao…hawataki kuangaliwa baadhi ya sehemu za miili yao, kwao ni aibu..ni fedheha, ni dhambi… na imani hizo zikakita ndani kabisa ya miyo yao… sio kwa unafiki, anafanya vile kwa dhamira moja…ukimlazimisha mtu kama huyo..lolote linaweza kukutokea....tunatakiwa tuheshimu utashi wao….’akasema docta.

‘Lakini docta twende mbele na kurudi nyuma, maana wewe mwenyewe kila siku unasema kwanza vipimo, mengine baadaye, lakini kauli yako hiyo inapinga msimamo wako..sasa huyu mama kaja hapa kutibiwa, ina maana tusimfunua tumkatibia,….hata hapa hospitalini?’ akauliza nesi.

‘Inategemea….. je kweli unataka kumtibia au kumuangalia…maana hata sisi na utaalamu weu bado tuna madhaifu ya kibiandamu, lengo linaweza lisiwe kumtibia…je ni kweli lengo letu lilikuwa hivyo….?’ akauliza docta.

‘Docta kwani sisi hapa tunafanya nini,…tumeajiriwa kufanya tiba..na ili tufanya kazi yetu vyema, wagonjwa wnastahiki kujiweka wazi, ikiwa ni pamoja na mauongo yao yale yanayostahiki kutibiwa… tunataka kutibia ndio maana tunamwambia ajifunue..’akasema nesi.

‘Je ni kweli…kuwa nia yako ni hiyo tu..?’ akauliza docta.

‘Docta hata sikuelewi….ina maana unaamini kuwa sisi nia yetu ni kumuangalia tu….sawa basi wewe unayeoona hilo utamtibia mwenyewe..’akasema nesi akionyesha kukerwa.

‘Mimi najaribu kuingia kwenye kichwa cha huyo mama, na kujaribu kuona kwanini hataki kuwaruhusu watu wengine, hata sisi ambao tunawajibu wa kuanya hivyo…sio kwamba nawaona kuwa hamfai au mna malengo mengine…najaribu kuona …msimamo wa huyo mama,….anyway….sasa hebu niambie wewe nesi mkuu wewe ulisikia nini kuhusu huyu mama?’ akaulizwa nesi mkuu.

‘Kusikia nini..docta mimi nimekuambia kuwa nilimuona tu njiani..’akasema nesi na kama kashtuka jambo akatulia.

‘Nasikia kuna watu walikuja kutaka kumuona na …ni ndugu zako au nimekosea?’ akauliza docta na nesi akakumbuka kuwa kumbe kuna ndugu zake walifika na huenda walishaongea na waliokutana nao na wakajitambulisha kama ni ndugu zake, na taarifa zimeshafika kwa huyo docta…, akaona hana ujanja akasema;

‘Mhh, ni kweli, kuna ile siku walikuja ndugu zangu, ndugu zangu walibahatiska kuishi na huyu mama , kama kumsaidia, mimi nilikuwa siyajui hayo kuwa huyo mama alikuaj akaishi na ndugu zangu hao…wanasema ni kweli huyu mama hapendi kufunuliwa usoni, kama alivyojifunika na kila aliyejaribu kufanya hivyo, bila ridhaa yake yanamkuta makubwa..kuchanganyikiwa na kitu kama hicho….’akasema nesi

‘Na hata wao hawajawahi kumuona sura yake..mhh yawezekana kweli, mtu muishi pamoja kwa muda..isitokee hata mara moja?’ akauliza docta mwingine.

‘Hawajawahi kumuona kabisa…hata wao wenyewe hawakuwahi  kumuona sura yake yaani ndivyo ilivyo....’akasema huyo nesi

‘Je hao waliowahi kumuona au kutaka kumuona ndio hao wanaochanganyikiwa..?’ akauliza huyo docta mwingine, na kabla hajajibiwa docta bingwa akasema.

‘Mbona mimi sijachanganyikiwa, na nimemuona…mimi naona tusiweke hoja hiyo au ulitaka kusema nini docta?’ akauliza docta bingwa

‘Mimi naona ni kwasababu kakubali wewe ufanye hivyo,na kwa vile wewe ni docta bingwa akaona hana jinsi, na kwa vile anahitajia matibabu…’akasema nesi

‘Mhh…umeona eeh, kwa vile kaona kuwa nia yangu ni njema kwake…’akasema docta bingwa.

‘Unajua mambo mengi hayaingilii akilini…sasa tufanyeje..maana kama ilivyo huyo mama hataki mtu mwingine kumuhudumia hadi zaidi yako wewe,..na wewe una  safari, sas auanondoka unafikiri atakubalia nani mwingine amuangalia,..amtibie hayo majeraha….’akasema docta mwingine.

‘Kiukweli kwa hivi sasa ilivyo huko usoni hakuhitaji matibabu ya zaidi…vile vidonda vimeshajifunga..ila …anahitaji utaratibu mnzuri tu…mimi naona tiini utashi wake, msije mkapatwa na mengine mkasingizia kuwa ni huyo mama..maana naona mioyo ya ya wengi hapa imeshaathirika kwa wasiwasi..’akasema huyo docta.

‘Kwani yupoje,..si mwanadamu kama sisi…?’ akuliza nesi mwingine aliyekuwepo hapo.

‘Mhh,..ni binadamu, aminini hivyo hana tofauti…msije mkazua ya kuzua, mimi ninachowaomba ni kuwa huyo mama, anahitajia utulivu…anahitajia ushauri…na taratibu atapona...huko baadaye, …kwa hali aliyo nayo,..japokuwa sikuweza kumshona..kwani majeraha yalishajifunga….kiujumla uso wake umeharibika…waliyomfanyia hivyo sio watu wema…wamehakikisha uso unakatwa katwa na mapanga….aah, lakini hana shida sana…’akasema docta.

‘Kwahiyo unataka kusema nini..?’ akauliza nesi mkuu akiwa na wasi wasi.

‘Unajua.niliposikia kuwa kuna ndugu zako walikuja kumuona huyu mgonjwa, nilitaka kujua kama unamfahamu zaidi..hata hivyo mimi napendekeza kuwa ufuatilie kujua huyu mama ni nani, na….ili tuweze kupata historia yake, maana tukianza matibabu yake ya akili…ndio sehemu yetu ya pili itafuata huko…, tunatakiwa kujua historia yake kwa ujumla,….inavyoonekana kaathirika kisaikolojia,..lakini sizani kama ana …mtindio wa ubongo ..hapana hilo…ok, tutaona huko baadaye.., …’akasema docta bingwa

‘Mhh, docta kwahiyo unataka mimi nifanye nini….maana nona huo ni mtihani kwangu…’akauliza nesi

‘Mtihani gani?’ akauliza docta msaidizi.

‘Kwanza..ukiangalia hayo yaliyowakuta wengine ni sababu hizo hizo za kutaka kumchimba huyo mama…kumfunua na kuona yupoje…’akasema

‘Mhh..nia yetu iwe njema, sio kumchimba,..au kumfunua kutokana na hizo tetesi… bali tufanye hivyo tukiwa nalengo jema la kumtibia…hilo liwe akilini kwenu, mkiwa hivyo, ..tutaweza kumsaidia huyu mama..huyu mama ana matatizo makubwa..angalia walivyomfanya, hivi wewe ufanyiwe hivyo, bado uzingiziwe mambo yasiyostahiki..kiukweli utaathirika kisaikolojia utaona kama hutakiw hapao duniani..hasa kwa akina mama, ambao wengi miyo yao, haina utahabiti wa kuhimili..….’akasema docta.

‘Unajua docta hata ndugu zangu waliokuwa wakiishi naye wameshaanza kuogopa…maana watu wamechoma hadi nyumba ya ndugu zangu kwa ajili ya huyu mama, watu hao waliofanya hivyo wanadai huyu mama ni mchawi…’akasema nesi.

‘Je na wewe unaamini hivyo..au na hao ndugu zako wanaamini hivy, waliwahi kuona dalili kama hizo za kiuchawi…?’ akauliza docta

‘Hapana docta..mimi siamini hao kuwa mama kama huyu anawezaje kuwa mchawi, hata ndugu zangu hawaamini hivyo…..isitoshe kumbe huyu mama alikuwa akiwasidia watu kuwa..tibia matatizo ya watoto wao…wema wake huo haukuangaliwa, waliona kama anafaiadi…nahisi hivyo wakaona wamuharibie…’akasema nesi

‘Kuwatibia kwa vipi?’ akauliza docta akimuangalia huyo nesi machoni, na huyo nesi akawa kama kainama …kuonyesha anaongea na bosi wake, akasema;

‘Wanasema huyu mama ana karama…mtoto akiwa analia…au anaweweseka…na vitu kama hivyo huyu mama akimuwekea mkono wake kwenye hicho kichwa cha mtoto, ananyamaza na yale matatizo yanakwisha..’akasema nesi

‘Hahahaha…mmmh,..unjajua  hata mimi nimewahi kusikia kuwa kuna watu wenye karama kama hizo, sikatai…lakini jinsi gani ya kuthibitisha hayo kitaalamu ni ngumu kidogo..sisi kama docta tunasimamia kwenye vipimo..sikatai kuwa hayo hayapo yapo..mimi na ani yangu hii nimekutana nayo nayafahamu,…lakini…..’akasema docta na kusita kumalizia.

‘Aaah, docta sio kwamba nimeyaona hayo kwa macho yangu au kuyaamini, ila mimi nasema wanavyodai watu wa huko kijijini waliwahi kumuona….sio mimi docta..’akasema nesi na docta akamuangalia kukatulia kidogo na docta akasema;

‘Sasa tufanyeje…?’ akauliza akigeuka kumuangalia msaidizi wake, halafu akasgeuka kumuangalai nesi akasema;

‘Mmmh, hebu nikuulize,..lini hao ndugu zako watakuja tena kumtembelea mgonjwa…, maana mimi sitakuwepo kesho, au kesho kutwa, ..ina maana hiyo kazi nakuachia wewe na..docta …eeeh….,wakija muwahoji , muongee nao, mjue histora ya huyo mama vyema… ‘akasema huyo docta akimgeukiwa docta mwenzake.

‘Sawa..’akasema docta mwenzake akitikisa kichwa kukubali.

‘Japokuwa kama mnavyoona tatizo la huyu mama ni kuwa hataki mtu mwingine hata docta mwenzangu hapa alikataliwa kumfunua uso wake…unaona ilivyo…sasa..anyway..kama kutakuwa na dharura mtajua la kufanya..’akasema huyo docta bingwa

‘Sawa docta, lakini..huo sasa ni mtihani…sijui kwa dcta yeye atajua la kufanya lkini mimi mmmmh, nahisi huo ni mtihani…’akasema nesi.

‘Yah..ni mtihani….lakini ndio kazi zetu zilivyo…wakati mwingine changamoto kama hizi hutokea, na inabidi kutafuta njia ya kupambana nazo…ila msimlazimishe kama hataki jambo fulani lifanyike…hilo nataka nilifanyie kazi mwenyewe nikirudi….nina imani kuna jambo kwa huyo mama..anahitajia uchunguzi wa tarataibu …nitaona nikirudi…..’akasema huyo docta na wakatawanyika, na nesi akataka kupitia kue alipo huyo mama kumuangalia tena, akiwa na mengi ya kujiuliza
**********

Matibabu ya yule mama yaliendelea,..kuna muda alikuwa akazidiwa hadi kupoteza fahamu inakuwa akzi ya kukimbizan huku na kule..lakini hali hiyo ikaanza kupungua..ikabakia ile hali a kushituka shituka na kutaka kukimbi,a na hiyo hali nayo ikaanza kupungua kidogo kidogo…

Mama huyu akaanza kuwa nah alia yenye mategemei  na akaanza kuinuka na siku hiyo alipoweza kuinuka, alikuwa kazungukwa na madakitari, wakikabidhiana, yeye aliinuka kama kawaida na alipotizama ile hali ya watu kumzunguka, alitulia kwa muda akawa kama anashngaa anaangalia huku na kule…na mara akakurupuka, na kuanza kukimbia, …

Siku hiyo ikawa mshike mshike tena, na madakitari kwa utaalamu wao wakamuweka sawa, nafikiri kukimbio huko kulitokana na hio tukio la kupigwa na kukatwa mapanga, kwahiyo bado alikuwa akihisi watu hao waliomzunguka wanataka kumfanyio hivyo tena! Lakini baadaye hiyo hali ilitulia.

 Siku ya pili yake akawa na nafuu, na akaweza kuinuka na kwenda kujisaidia mwenyewe, ila akiwa katika uangalizi wa karibukaribu. Na siku hiyo mdogo wa dada mtu akawa yupo zamu, na alipofika kwa huyu mama akaanza kumuulizia hali yake. Yule mama alikuwa akijibu kimkatomkato, hakuwa anaongea sana, na maswali mengine akiulizwa alikuwa akishangaa, hata jina alikuwa hajui kuwa yeye ni nani…

‘Naomba uondoe hiyo nguo uliojifunika usoni, kwani huko kwenye uso kuna majeraha, yanahitaji hewa na kusafishwa…’ akamuomba yule mama ajifunue.  Dakitari wake alikuwa akimsafisha kwa siri hakuna aliyetakiwa kuwa karibu naye na nesi alikuwa akijaribu kumshawishi ili abadilike….

Yule mama alipoambiwa hivyo kuwa aondoe ile nguo aliyjifunika nayo kichwani na usoni, akaangalia huku na kule, alisita kujifunua akabakia kimiaya hakusema kitu au kufanya lolote, na nesi akaona hakuna haja ya kumlazimisha akaangalia yale yanayofaa kuangaliwa halafu akataka kuondoka.

‘Mtoto wangu yupo wapi..?’ nesi akasikia sauti kutoka kwa huy mama, akageuka kumuangalia, halafu akasema

‘Mtoto gani unayemtaka, ..?’ akauliza

‘Nataka mtoto wangu..’akasema huyo mama

Yule nesi alimwangalia….akawa anawaza amuambia nini huyo mama, akilini alikuwa akiwaza meng, hasa aliposikia kuwa askari waliofika kufanya uchunguzi siku ho ya tukio wamekabailiwa an magonjwa yasiyofahamika, kisa watu wanasema walilazimisha kutaka kuuangalai huyo mama uso wake..shemeji ake naye kawa kama mtualiyechanganyikia, anaongea peke yake…

‘Kwanini unawatesa watu?’ akasema huyo nesi bila kufikiria kauli yake hiyo na huyo mama akawa kimia tu.

‘Watu wote waiojaribu kukutizama au kuataka kukutizama usoni wamechanganyikiwa, …ina maana gani, kuwa wewe hutakiwi kuangaliwa uso wako, au …’akasema na kukatiza kile alichotaka kukisema.

‘Mimi mwenyewe sijui uso wangu upoje…kwanini watu wengine watke kuuangalia…mimi sijui waulize waliotaka niwe hivyo…’huyo mama akasema
‘Akina nani…?’ akamuuliza

‘Sijui…’akasema
‘Kwani wewe umetokea wapi?’ akamuuliza

‘Sijui..labda mbinguni, kwanini wewe unajua umetokea wapi?’ akauliza huyo mama, na naesi akawa kimia

‘Ina maana hata mimi nikitaka kukuangalia kwa nguvu, nitachanganyikiwa?’ akamuuliza.

‘Hivi na mimi nikitaka kukufunua ukabakia uchi nikuangalia utakubali?’ akauliza huyo mama.

‘Lakini tunachotaka kukuangalia ni uso wako..sio sehemu nyingine ya mwili..’akasema.

‘Na mimi nataka kuakuangalia uchi wako sio sehemu nyingine ya mwili..’akasema huyo mama, na nesi kwanza akawa kama kashituka kwa ile kauli,..akatulia huku akiwazia ile kauli…halafu akageuka kuondoka na kabla hajainua hatua ya tatu, mara sauti ya yule mama ikasikika ikisema kwa hasira;

‘Umenisikia,nataka mtoto wangu…’ilikuwa sauti kali ya kuonyesha kukasirika, na nesi akahisi uwoga, hakutaka hata kugeuka kumuangalua yule mama, alihis kama yupo nyuma kwake anataka kumzuru…, akakimbia kuelekea ofisi ya  dakitari wake ,WAZO LA LEO: Tuheshimuni utashi na imani za watu wengine..kuna watu kutokana na imani zao, wana taratibu zao za maisha, iwe ni mavazi..kufanya ibada, au vyakula na jinsi gani ya kuishi …kutokana na imani zai wanafahamu zaidi kwanini wanafanya hivyo, …wewe kama unaona wanavyofanya hivyo sio sahihi,..au kutokana na imani zako inakizana na imani hizo…usiwe kikwazo kwako ukazuia…, muhimu ni kujenga uvumilivu, na kuheshimu imani hizo ili kuwe na mahusiano mema. Tabia ya kuzarau imani nyingine na kubeza, ndio chanzo cha mifarakano kwenye jamii, kama kuna mijadala ya kufahamu kwanini,…au kutangaza imani kwa kulinganisha basi ifanyeni kiuungwana na kwa hekima.

Ni mimi: emu-three

No comments :