Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, March 4, 2015

NANI KAMA MAMA-40


Baba mwenye nyumba alipogundua kuwa kaota ndoto inayomkumbusha maisha yake ya nyuma, na alipozindukana akajikuta karibu yake yupo yule mama aliyekuwa kwake ambaye wengi walijua kuwa kaungua na moto, lakini kwa bahati nzuri hakuungua na moto, lakini…

‘Watu wakiwa wanajua kuwa huyo mama keshafariki, lakini bado waliogopa kumsogelea au kumfunua, na waliojaribu kufanya hivyo, wakajikuta wakipatwa na mambo ya jabu hata kupoteza fahamu, mmojawapo alikuwa askari, …

 Mwishowe mwili wa mama huyo ukafikishwa hospitalini, pamoja na baba mwenye nyumba ambaye alipoteza fahamu pia.

Sintofahamu hii ya huyu mama, ikawagusa wengi, na hata alipofikishwa hospitalini, kukawa na ucheleweshaji wa kumpokea huyo mama, kwania anyehusika na kupokea maii alikuwa hayupo, katoka, na dakitari wa zamu alikuwa akihudumia mgonjwa wa dharura.

‘Kama mna uhakika amefariki, hamna shida, ..nyie muwekeni hapo..na huyo mwingine naona hana tatizo kubwa…kazindukana, na ….mengine docta atamuangalia..’akasema mpokeaji, ambaye ni dakitari pia lakini alikuwa hana mamlaka, na alikuwa kamaliza zamu yake anajiandaa kuondoka.

‘Alipoteza fahamu tu,lakini hana matatizo….’akasema askari aliyekuja na hao watu ambaye alikuwa kiongozi wa msafara,  akawa anamtikisa tikisa baba mwenye nyumba. Na baba mwenye nyumba akawa anajinyosha nyosha.

‘We muache tu…kama ana tatizo jingine docta atakuja kumuangalia..’akasema docta huku akichukua vifaa vyake,lakini akasema;

‘Oh ..unajua mashine yangu hii ina matatizo, ngoja tumsubirie docta atakuja sasa hivi, naona huyu mtu wenu hana matatizo….’akasema baada ya kumshika mkono nakuangalia mapigo ya moyo, akafunua kope za macho…

‘Sasa kuhusu huo mwili wa huyo mama, msubirini docta kwani ndiye mwenye dhamana, atampokea na mtaandikishiana,na kwa vile mpo watu wa usalama mumethibitisha hilo, sioni kama kuna tatizo…..mimi natoka maana muda wangu wa kazi umekwisha..’akasema docta huyo na kuondoka.

‘Sasa unasemaje baba mwenye nyumba upo tayari kuitambua hiyo maiti na kufanya yale tuliyoahidiana maana kwangu ni muhimu sana…ili nimalize uchunguzi wangu?’ akasema huyo askari, na baba mwenye nyumba akainua uso na kumuangalia aaskari huyo, akatabsamu na kusema;

‘Nipo tayari kuitambua ….kuufunua huo mwili…lakini kwa masharti..’akasema

 Na yule askari akatabasamu na kusimama, alionyesha kufurahia kauli hiyo akasema;

‘Safi kabisa sema lolote..tupo tayari.., ilimradi umtambe na umpige picha, tunahitajia sura ya huyo mama, ni masharti gani hayo…..?’akauliza.

‘Sharti langu ni hili..nataka nikitambua, nikimfunua huyo mama,…huyo…eeh, hiyo maiti..nataka niwe peke yangu, sitaki mtu mwingine humu ndani..ili kukidhi stahiki zake, kwani kama hakutaka watu wamuone kwanini sasa tuvunje miiko yake…, pili siwezi kumpiga picha….’akasema

‘Lakini tunahitajai hiyo picha ni muhimu kwetu…’akasema huyo askari.

‘Kwani picha yake itasaidia nini,..sawa kwanza niachieni nimtambue,  ..sitampiga picha kwasasa mpaka nijirizishe kama kweli ndio yeye..’akasema

‘Ujirizishe….?! Ok, lakini sisi tunachohitajia ni picha yake….ni muhimu sana…kabla madakitari hawajamchukua, maana bado sijamtambua sura yake, na ikiid tunahitajika kumtangaza kama ana ndugu zake waje kumtambua..unaona ilivyo muhimu ….’akasema afande

‘Mhh, ina maana dakitari hajamchunguza..?’ akauliza na kala hajajibiwa akasema;

‘Kwanini wanasubiria nini,…au  na wao wana,muogopa..? akauliza na kabla hajajibiwa akaongezea tena kwa kusema;

‘Masharti yangu ndio hayo,…lakini ni muhimu madakitari wangemuona kwanza, …hata hivyo kama ni yeye..ooh sijui,…ni bora tu ….iwe hivyo…sitaki na simtaki…ila kama ni muhimu  mpaka mimi nihakikishe, basi naomba mtoke nje, ..’akasema na yule askari akamuangalia kwa uso wa kujiuliza akasema;

‘Kama kweli ndio yeye!?…una maana gani, sisi tuna uhakika ndio yeye, tuna uhakika..naona kuzimia kwako kumekuchanganya sana…wewe fanya ufanyalo lakini sisi tunataka picha yake kabla madakitari hawajamchukua kumkagua…naona docta aliyeingia sasa kajiukuta na kazi nyingi..alifika mwanzoni tukamzuia kwanza,…maana kuna hilo zoezi hatujalikamilisha, …’akasema

‘Mkamzuia ,kwanini..maana yeye ndiye angelithibistisha kuwa huyo mama kafariki au …’akasema

‘Kafariki, afariki mara ngapi…we acha kuota, au kupoteza fahamu huko kumekupoteza akili..sasa sikiliza, fanya haraka…we mkague , mpiga picha…kamera hii hapa si unajua kuitumia…’akaambiwa.

‘Nafahamu…’akasema akipokea ile kamare, na wale askari na watu wengine waliokuwepo wakatoka nje.

Baba mwenye nyumba akiwa kabakia peke yake akasimama na kujinyosha, akasimama akiwa hajaangalia pale alipolazwa huyo mama, baadaye akageuka…

Akageuka kuangalia pale alipolazwa huyo mama…akatulia kwa muda akiangalia, akijitahidi kutokuogopa,  alikaa vile kwa muda, hadi aliposkia mlango ukifungwa nyuma yake, ..akajua sasa yupo peke yake….

Tuendelee na kisa chetu…

                             ************

Baba mwenye nyumba kichwani alikuwa katawaliwa na ile ndoto, akawa anajiuliza kwanini hiyo ndoto imsumbue,…

‘Tausi…sizani kama nikikutana naye nitamsamehe, alichonifania sio ubinadamu..japokuwa…anaonekanahana kosa, ..hasa kutokana na ndoto alivyoota ma kwani wazazi wao walikuwa hawana nguvu ya kufanya lolote, lakini kilichomuuma ni kuwa kwanini Tausi asiweze kutoroka kama walivyoahidi, ina maana aliona mali ni bora kuliko yeye masikini.

Badala ya kufanya kile alichotakiwa kufanya, akajikuta anawaza jingina akawa kasimama pale pale…, hasira zikamshika akawa akshikilia kitanda alichokuwa kalazwa, mkono ukitetemeka kwa hasira…mara akasikia sauti…

Akabakia vile vile akitega sikio, ..hiyo ni sauti kama ya mguno, kama mtu anathema..imetoka wapi, maana humo ndani wapo yeye na hiyo maiti…taratibu akageuza shingo kutizama pale alipolazwa huyo mama.

Akabakia kaduwaa…hakuamini macho yake, akajikuta akitamani kukimbia, lakini mwili hakuweza, akataka kupiga yowe lakini mdomo haukufungua,…akabakia katoa macho huku haamini anachokiona,..ilipita dakika mbili, baadaye kukawa kimiya.

‘Ina maana huyu mtu hajafa…’akasema sasa akawa anaogopa hata kumsogelea huyo mama, akilini akawa anajiwa mawazo mengi, ya vibwengo..ya ..shetani yaani ya vitu vya kutisha, na baadaye akukumbua ile sauti inayomjia mara kwa mara ikimuonya, ikasema;

‘Unaona..nilikuambia, sije kujaribu kuanya wanayotaka hao watu…huyo mama sio wa kawaida….ni mzimu huo…ukicheza utakunyonya damu, na utabakia mkavu…toka humu ndani haraka..’sauti ikamwambia.

‘Hapana siwezi kutoka humu mpaka nihakikishe huyu mama ni nani…’akasema na kujipa moyo, akatembea kwa haraka hadi pale alipo huyo mama, akamkuta katulia, na taratibu akainua mkono wake unaotetemeka na kuushika mkono wa huyo mama…joto, joto la uhai, akalihisi, akauachia haraka, na kugeuka nnyuma nia ni kama docta aje kuhakikisha.

‘Yupo hai, yupo hai….’akawa anema akirudia rudia maneno yake, lakini kuna kitu kikawa kinamvuta , akawa na hamasa ya kutaka kuhakiki kile kinachomsumbua akili yake, akageuka na kumtizama huyo mama.

‘Wewe ni nani?’ akauliza, akisahau kuwa swali kama hilo alishawahi kuliuliza mara nnyingi na hakuwahi kupata jibu la kumsaidia…kukawa kimia, akatulia, na kwa haraka akainu amkono na kushika ile nguo iliyomfunika huyo mama kichwani akaivuta kwa hasira..ikavuka, na kichwa kikabakia wazi..

Unajua mshituko, unajua kushangaa..jamaa alibakia mdomo wazi, ..akajikuta hawezzi kusema kitu, akawa anacheza mdomo,…na mwisho wake akasema;

‘Mamamama..kwanini…wamekukata hivyo…ooh,..ina maana ni wewe,,haiwezekani..haiwezekani,….oh,…’akajikuta akisema na huku akiwa aktoa macho, na sauti ikasema;

‘Umerizika,..nifunike kichwa changu..’ilikuwa sauti..japokuwa inakwaruza, lakini ni sauti ile ile, sauti ambayo aliipenda kuiskia, sauti iliyokuwa ikimliwaza hata akia na shidd zake akisikia sauti hiyo huliwazika..lakini…

Kwa haraka bila kubisha akachukua ile nguo na kumfunika huyo mama, halafu akasema;

‘Siamini …umeonaeeh,…, hiyo ndio adhabu ya msaliti….wameiharibu sura ako na mapanga..uziri wote sasa haupo, ….imebakia macho…hahaha…unakumbuak eeh,…’akasema.

‘Nataka mtoto wangu…’sauti ile ile ya yule mama ikasema, na akainua uso kumuangalia huyo mama, sasa alikuwa keshajifunika.

‘Unataka mtoto wako, unataak mtoto, unajianya umechenganyikiwa, au sio..au mume wako alikufania nini, mbona niliskia umeshafariki..au ndio umefufuke, au wewe ni mzimu wake tu..hahaha, …haya huyo mtoto uneyemtaka yupo wapi?’ akauliza

‘Namtaka mtoto wangu….’akasema

‘Tausi ndio wewe,…kweli dunia ina mambo, siamini,….hii kweli ni miujiza ya mungu….Tausi ndio wewe…siamini..’akasema

‘Tausi!….mimi so Tausi…na…namtaka mtoto wangu haraka..’sauti ikasema sasa ikitokea kwenye nguo iliyofunika mdomo wake,na kabla baba mwenye nyumaba hajasema zaidi,  mlango ukafunguliwa,akageuka kutizama ni nani aliyefungua mlango, akamuona dakitari.

‘Vipi …mbona..’docta akawa kasimama na yeye kuonyesha kushangaa, na mwenye nyumba, hakusema kitu akaanza mdogo mdogo, …..taratibu akatembea kutoka nje, huku akilini akiwa na yake….akiwa kachanganikiwa, akiwa haamini,….hakusema neno hadi akafika nje.

‘Tayari umeshampiga picha?’ akaulizwa na askari

‘Picha!? picha ya nini, ..sizani kama picha ina umuhimu huo..’akasema akitembea kuelekea pale aliposimama huyo askari.

‘Kwanini..umeshindwa, ..sasa umefanya nini, docta atampiga masindano yao, na hatutaweza kupata picha tunayoihitajia..’akasema huyo askari.

‘Ili iweje?’ akauliza huku akiwa kainua mkono juu kumkabidhi huyo askari kamera yake.

‘Tukamtangaze kwenye nyombo vya habari, ili wenyew e wakisikia…wafika, unajua vyombo vya habari vinasaida sana… wanaweza kupatikana ndugu zake, na hata wakisikia wataelekezwa kuwa maiti yao ipo hapa..’akasema huyo askari.

‘Hakuna maiti humo ndani….’akasema akiinua mkono kumkabidhi huyo askari kamera yake, na huyo askari akawa katulia akionyesha kushangaa, akasema;

‘Una maana gani kusema hivyo, kaenda wapi huyo maiti?’ akauliza huyu askari akiwa na wasiwasi.

‘Docta atawaambia mimi nawahi usafiri narudi nyumbani kwangu na sitaki ..mnasikia sitaki tena huyo mama kukanyaga nyumbani kwangu..sitaki..mumesikia, sitaki sitaki..nimuone nyumbani kwangu…’akasema huku anatembea kuelekea barabarani….

 Na kule kwenye mlango alipokuwa huyo mama, docta aakjitokeza,  akiongea na simu,…na mara kukaja kigari cha kubebea wagonjwa…kikaingizwa ndani haikupita muda, kile kigari kikatolewa huku kimebeba mtu, na mtu huyo sio mwingine ni yule mama.
‘Haiwezekani….’akasema huyo askari

‘Mpelekeni chumba cha uchunguzi nakuja..’akasema docta akielekea upande mwingine na askari akawa sasa anawafuatia nyuma wale watu waliombeba huyo mama, akitaka kupata maelezo.

‘Ina maana huyo mama hajafa?’ akauliza wale wahudumu wakageuka kumuangalia na wakasema;

‘Kwani alikuwa amekufa?’ wakauliza hao manesi, kwani wao walikuwa hawajui lolote.

‘Oh ni miujiza, sisi tulileta maiti…sasa tunaona ajabu..’akasema huyo askari

‘Labda maiti ipo…. imebakia huko ndani lakini hakuna maiti kule ndani, kwanini hamkumpima kabla ya kusema amekua..huyu mtu yupo hai, ila ana hali mbaya…anahitajia matibabu na uchunguzi wa hali ya juu..’akasema mmoja wa nesi

‘Mhh, sijawahi kukutana na tukio kama hili..na anhitaji kulifuatilia kwa karibu,…nataka nionane na huyo docta..’akasema

‘Kuna mgonjwa mwingine kaletwa yupo kwenye hali mbaya..sasa sijui atajigawaje..leo ipo kazi..’akalalamika nesi mmojawapo.

‘Hivi nesi mkuu anainga saa ngapi?’ akauliza,

‘Yule anakuja…’mwenzake akasema.

 Askari akageuka kumuangalia huyo nesi mkuu ambaye alionekana akija kwa mwendo wa haraka kuonyesha kuwa kachelewa…, akahisi kama anamkumbua akasubiria hadi huyo nesi akawakariba, na huyo nesi akawasalimia, huku akimuangalai huyo askari kwa amshaka, na kuulizia;

‘Docta yupo wapi?’ akauliza

‘Ana mgonjwa wa dharura..’akaambiwa

‘Mhh, jamani hospitali hii…yaani hakuna kulala, kila dakika mgonjwa anayeletwa hapa ni mahututi,..ni wa dharura…na wengie wana majeraha..na huyu vipi..?’ akauliza na kugeuka kuangalia, pale kwenye kigari cha wagonjwa, na kumuona huyo mama, kwanza akashituka, halafu akageuka kumuangalia askari..akaona wenzake wamebakia kimiya, nay eye akabakia kaduwaa…lakini akajiweka sawa, na kusema;

‘Katokea wapi huyu..naona mkono umeungua?’ akauliza

‘Katokea kijijini..’akaambiwa

‘Kijini ..kijiji cha wapi…. ?’ akauliza

‘Unamfahamu huyu mama?’ yule askari ambaye kwa muda mwingi alikuwa kimia alipofika huyo nesi akijiuliza ni wapi aliwahi kumuona huyu nesi, akauliza, baada ya kuhisi huenda alimuona hapo hapo hospitalini.

‘Sina uhakika kama ndio yeye…’akasema huyo nesi akimsogelea huyo mama...kumkagua akamuinamia na kusema;

‘Nataka mtoto wangu….’akasema na mara yule mama aliyekuwa kama kalala akashituka na yeye akasema;

‘Nataka mtoto wangu…’wote wakabakia wameduwaa, hasa askari, ambaye alikuwa akiangalia hilo tukio kwa aina yake, akasema;

‘Nesi unafahamu huyo mama?’ akauliza na mara docta akafika, na doct akaongea kidogo na huyo askari  walipomaliza kuongea huyo askari akawa anaondoka,..na alipowapita hao manesi akamgeukia huyo nesi mkuu na kusema;

‘Nesi nikija kesho nataka kuongea na wewe..’akasema na nesi akabakia kaduwaa tu, hakusema neno, na yule askari akaondoka zake.

************


Kwa hali aliyokuwa nayo huyo mama ailibidi apelekwe chumba maalumu cha uchunguzi, kwani hali yake ilikuwa mbaya, kwa majeraha ya moto na majeraha ya mapanga. Kwa muda huo alikuwa keshazindukana vyema, ila alikuwa akigugumia kwa maumivu na damu ilikuwa inamvuja kidogo kidogo.

‘Huyu mama anahali mbaya sana, kwani wamemkatakata na mapanga usoni,  miguuni, lakini hawakugusa sehemu za mwili, ..tumboni  hawakugusa kabisa…ndilo limesaidia…halafu kaungua sehemu kubwa ya mwili…mkononi na miguuni ….uzuri ni kuwa damu haikupungua sana, kwahiyo haina haja ya kumuongezea damu, ila anahitaji matibabu ya haraka..vdonda vimekaa muda bila kutibiwa…’ akasema dakitari.

‘Halafu huyu mama hasemi na wala hakumbuki kitu gani kimemtokea, ina maana ana matatizo mengine, ambayo yanahitaji utaalamu zaidi, ama ya akili au ana tatizo la kusahau…’ akasema dakitari, baada ya uachunguzi wa awali..

‘Hata jina halijulikani..’akasema nesi

‘Mhh, wewe andika mama mgonjwa wa moto…’akasema docta na wote wakacheka.

‘Na majeraha ya mapanga,..nafasi haitoshi..’akasema huyo nesi.

‘Lakini huyu mama kama sikosei nilishamuona huko kijijini kwetu, kuna kipndi nilikwenda huko, kabla sijakwenda kozi…nilimuona huyu mama akipita pita mitaaani na kuimba kuwa anamtaka mtoto wake, sijui ndio yeye, maana hata sura siijui, na hata sasa hataki kufunuliwa funuliwa, anamuamini docta wake tu…’akasema nesi.

‘Oh, nyie niachieni mama yangu kanitunuku, msione wivu ..lakini, mbona hajafika na ndugu yake yoyote?’ akauliza docta

‘Ina maana hana ndugu, kama ni huyo mama, …, nijuavyo mimi, alikuwa akipita pita mitaani akiimba imba tu,..na hulala popote..hata kule kijijini hawaju katokea wapi…’akasema

‘Aliletwa hapa na askari na jamaa mmoja ambaye tulijua ni ndugu yake, lakini kumbe sio ndugu yake, na huyo jamaa kaondoka hata bila kuaga,….huyo jamaa alikuja hapa akiwa naye kapoteza fahamu..’akasema docta

‘Kwasababu hii hii ya moto?’ akauliza nesi

‘Sina uhakika..labda tusubiri akija askari, maana huyu mama bado yupo mikononi mwa askari, wanasema hawajamaliza uchunguzi naye..’akasema

‘Oh,…jamani, sijui ni akina nani walimfanyia hivi huyu mama, wamekata kata na mapanga, hadi kuiharibu sura yake....halafu wakamuunguza na moto…naona pale hakutaka watu wamuengalie, mimi nikajiiba na kumuangalia, ....’akasema nesi.

‘Ndio hivyo dunia imeharibika kabisa..’akasema docta.

‘Kwanza umenikumbusha ngoja niwapigia ndugu zangu huko kijijini nijue kinachoendelea, …nina hamu ya kujua mtoto anaendeleaje…na siku yaani tangu niende kozi ..tunawasiliana kwa shida, kule mawasiliano mabovu..aaaah, nikaona kwanini njipe shida, nikaachana na simu..mpaka narudi sijui kinachoendelea huko kijijini kwetu..yaani nina hamu sana na ndugu zangu...’akasema nesi

‘Kwani wewe una mtoto..?’ akamuuliza docta

‘Hahaha..ninaye mtoto ndio…’akasema

‘Mbona hufanani kuwa na mtoto..’akasema

‘Mmmh, hapana ni mtoto wa dada yangu….nampenda sana huyo mtoto ana historia ya aina yake…’akasema

‘Ipoje hiyo historia?’ akauliza huyo docta.

‘Siwezi kukuambia, wewe jua hivyo tu….ngoja niongee na ndugu zangu, akasema huku simu ikiita bila kupokelewa.

‘Hawa watu vipi toka juzi simu inaiita hawapokei..sijui kuna nini,….oh, wananipa mashaka kweli…’akasema akijaribu tena na tena lakini simu ikawa haipokelewi.


NB: Sasa tupo mjini,…


WAZO LA LEO: Utu sasa haivi haupo, watu wanachojali zaidi ni masilahi,…watu wapo tayari kuua, kwasababu ya mali, ndugu kwa ndugu wanakosana kwasababu ya mali , marafiki wanakosana kwasababu ya mali,…hata mke na mume wanakosana kwasababu ya mali.Mali imekuwa ni mtihani, ..jamanii hebu turejeshe utu wetu, ..tupendane, tusaidiane..kwani utu una thamani kubwa zaidi ya hiyo mali tunayoithamini.
Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

I Ьlߋg often and I serioսsly thɑnk you for yоur information. The
article has truly peakeɗ my interest. I am going to book marƙ your website аnd keep checking fоr new
details about once per week. I opted in for your Feed as
well.

my page: halloween costumes for girls

Anonymous said...

Hi there i am kavin, its my first occasion to commenting anyplace, when i
read this post i thought i could also make comment due
to this good paragraph.

Take a look at my web-site - Used Stationary bikes