Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, February 25, 2015

NANI KAMA MAMA-37''Nataka kuongea na baba mwenye nyumba…..’akasema na kugeuka kushoto na kulia kuwaangalia watu waliokuwepo, na alipoona kupo kimia akaongeza kwa kusema;

‘Yupo wapi?’ akauliza askari wa kundi la kuwahoji watu, na wakati huo baba mwenye nyumba ndio alikuwa katoka kumfuatilia mjumbe, aliporudi tu akakutana na huyo askari kanzu.

‘Askari anataka kuongea nawe..’akanong’onezwa na mmoja wa watu waliokuwepo hapo.Mwenyenyumba akamsogelea yule askari na askari mwingine akawa anawaambia watu walikuwepo hapo watoke wakakakae nje, ili wapate nafasi ya kuongea na watu wanaohitajika.

‘Mimi ni askari, na ule mwenzangu,  na kazi yetu ni kutafuta ukweli kuhusiana na huo moto..kwanza nikupe pole kwa maafa hayo..najua ni hasara na ikizingatia kuwa huku kijijini hatuna huduma za bima, kwahiyo ni hasara isiyo na marejesho, au sio…?’akasema huyo askari akimuangalia mwenzake aliyefika kutoka kuwaondoa watu. Na askari mwenzake akatiskisa kichwa kukubali , japokuwa hakuwa na uhakika mwenzake kaongea nini

‘Tumeshapoa…afande..’akasema baba mwenye nyumba.

‘Kwanza tunataka ukweli…je ilikuwaje siku hiyo..kwa hivi sasa usijali hasara ukaongea kwa jaziba ukihisi hasara na kutaka kulipiza kisasi, maana …utalipiza kisasi kwa nani…’akasema

‘Muhimu ni kujua ukweli..hata kama kuna hasara lakini je hasara hii ni ya ajali kweli au ni ya watu wameamua kufanya hujuma..’akasema askari mwingine akiwa sasa nay eye katulia akiwa kashikilai kidaftari kidogo kuandika kinachoongewa.

‘Na ukweli huo hatuwezi kuupata kama hatutapata ushiriakino kutoka kwenu..na ni vyema ukatuelezea kila kitu, ili tuweze kuchanganua wenyewe, maana kuna kusikia, kuna kuona, na kuna kudhani..yote sisi tunahitaji..’akasema na mwenzake.

‘Ila mara nyingi ukifika mahakamani wao sana sana wanahitajia ulivyoona wewe…unaona…’akawa anaongea akiwa anaangaliana na mwenzake kama wanajadili jambo kabla hawajakabiliana na muulizwaji.

‘Lakini  sisi tunataka yote…si unaona hapo…, kama uliona, itakuwa ni bora zaidi..lakini kama hukuona umesikia yule aansema, huyu anaongea hivi,..tunahitaji hilo pia,eeeh,’akasema na kugeuka kumuangalai muhojiwa.

‘Hata hilo litatusaidia katika kufuatulia, au pia jinsi wewe unavyodhania..maana una maadui, kuna watu hawakupendi..kitu kama hicho…sasa hivyo unavyofikiria wewe hata lenyewe tunalihatajia ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu…’akasema askari mpelelezi.

Baba mwenye nyumba akawa katulia akiwaaangalia wanavyoongea kwa kupkezana, japokuwa alikuwa akiwaangalia na kusikia wanachoogea, lakini akili yake kwa isai kikubwa haikuwepo hapo…na akili ilivurugika pale alipoambiwa na mtu aliyekutana naye mlangoni, akimtahadharisha kwa kusema;

‘Uwe makini sana na hao askari, ni wajanja kupita kiasi, utafikiri wanaigiza lakini… ..mmh,…. sasa jifanye unajua kuongea sana, ..hao hao ukifika maeneo yao, utafikiri sio yeye..uso umebadilika, anakuonyesha kumbukumbu zake ulivyosema….sikutishi ila uwe makini..’akasema.

Kwahiyo mwenye nyumba lipofika mbele ya askari hao akawa anajaribu kuwazia, lipi la kuongea,..japokuwa watu hao wamesema aongee kila kitu….alichoona, ni kweli aliona moto, ….ni kweli alimuona huyo mama, tena akikata roho mbele yake, ni kweli huyo mama kakatwa na mapanga,..ni kweli…..’akatulia.

Ya kusikia ndio usiseme…kuwa kweli moto huo sio ajali, kuna vijana wameonekana, na kuna….oooh, kasikia mengi sana, lakini je ana uhakika nayo..hapana hapo napo natakiwa kuwa makini

Mara akili ikaanza kumuwaza huyu mama,…ambaye sasa anajulikana ni marehemu pamoja na mengi, yeye kama binadamu, hakustahili kuwawa kihivyo,yeye kwanza mwanamke….mama…hapana huo ni unyama, na yeye kama binadamu mwenye utu, anatakiwa kumtetea, hata kama kafa, lakini….mmh, nikijifanya kuongea sana nitawezeza kuishia jela au kusmbuliwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

‘Mhh, hapa naogopa, kujiingiza kwenye mambo yasiyonihusu, ..nina mke , nina mtoto, nina maisha yangu…sasa nifanyeje….’akajikuta akiongea taratibu, bila kutoa sauti

‘Sasa kwa kuanza, hebu tuambia ilivyotokea….?’ Akasikia swali likiulizwa
‘Mhh…..kabla yakuuliza hili tuanzie mbali zaidi, huyu mama…eeh huyu marehemu, wewe unamualewaje, ni nani kwako..?’ swali likaulizwa na huyo askari mwingine?

‘Sasa nijibu swali gani,…?’ akauliza

*************
‘Huyu mama ni nani kwako?’ akaulizwa

‘Huyu mama alifika hapa kwangu tu, sina udugu naye…kama raia mwema nikajitolea kumuhifadhi…’akasema.

‘Ina maana alifika kwako akakuomba hifadhi?’ akaulizwa.

‘Hapana,…sio kwamba alifika kwangu na kuniomba hifadhi..haikutokea kihivyo.., mama huyo alikuwa na kawaida ya kuja kwangu usiku na kulala upenuni mwa nyumba yangu…’ akasema

‘Kila mara alikuwa akija kulala upenuni mwa nyumba yako tu…?’ akaulizwa

‘Hapana sio kila mara, ila ni mara nyingi sana,…alikuwa akija kwangu…na usiku kunakuwa na baridi sana, ukitoka nje muda huo unamuona jinsi alivyojikunyata,..mmh kama binadamu, nikaona hapana ngoja alale banda la uwani…’akasema.

‘Wewe ndiye ulisema hivyo, au ni mke wako, au…ilikuwaje?’ akaulizwa

‘Mke wangu ndiye alitoa pendekezo hilo, na mke wangu alilipata pendekezo hilo…’akatulia kidogo, na askari hakutaka kuliuliziai zaidi akauliza swali jingine

‘Kwani huyu mama katokea wapi?’ akaulizwa

‘Sijui…’akajibu kwa mkato na askari wakawa wametuli wakijua atatoa ufafanuzi lakini haikuwa hivyo na mmojawapo akauliza;

‘Mimi naona ajabu mtu humjui kaja kwako, unamkaribisha, huoni hiyo ni hatari,wewe una kawaida ya kukaribisha watu kihivyo, au ilitokea bahati tu kwa huyo mama…?’ akaulizwa.

‘Kijijini ni sehemu yenye ubinadamu, sisi pamoja na hali zetu ngumu, lakini pale unapoona mtu anahitajia kusaidiwa unafanya hivyo,..na kwa huyo mama , sisi tuliona tunawajibika kufanya hivyo…’akasema.

‘Sisi swali letu ni hili, ni kwanini uliamua kumkaribisha mtu ambaye huna udugu naye, humjui alipotokea, na hali kwa hivi sasa sio ya kueleweka, wema unaweza ukawa ni hatari kwako, hebu tuambie ukweli, ulifanya hivyo kwa ubianadamu tu, au kuna sababu nyingine….?’ Akaulizwa na swali hili akaliona kama mtego, akajibu;

‘Kikweli afande, hatua ya kuamua aje kulala kwenye banda la uwani, haikuja kirahidi hivyo…kuna mambo yalitokea, najua umeshayasikia kwa watu wengi…kwanza huyu mama ana mambo ya ajabu, anaonekana kama hana akili sawa..’akasema.

‘Anaonekana kama hana akili sawasawa....au ndivyo alivyo…kuwa ana matatizo ya akili?’ akaulizwa
‘Kwa mimi ambaye nimewahi kuishi naye kwa karibu, siwezi kusema ana mtindio wa akili kihivyo wanavyosema watu..ndio ukimuangalia juu juu, ni kweli hana tabia za kawaida…lakini siwezi kumuita hivyo..hapana..’akasema

‘Kumuita hivyo kwa vipi, hebu faanua hapo vyema..?’ akaulizwa.

‘Mimi, nahisi kuna jambo…huenda…nasema huenda, maana sina uhakika…maana ukimuuliza mambo ya nyuma,… hakumbuki…, au huenda hataki kusema…sasa nahisi huenda ana matatizo ambayo yamefanya awe kama kachanganyikiwa,..lakini …mmh..nasema huenda..mnielewe hivyo…’akatulia alipogundua kuwa kaongea yale ambayo alitakiwa awe na tahadhari nayo…hisia zake nay a kuambiwa.

‘Unajua tunaona unaongea na kujipinga mwenyewe, unasema huyo mama alivyo, anaonekana kama kachanganyikiwa, kuchanganyikiwa maana yake ni nini..na unaposema hana mtindio wa akili, una maanisha nini,..?’ akalizwa

‘Mtu unaweza kuwa na mawazo sana ukafikia kuchanganyikiwa japokuwa huna mtindio wa akili…unapagawa tu, na ukienda kupimwa ..hutaonekana kama mgonjwa wa mtindio wa akili, kweli si kweli..?’ akawa kama anauliza na hakusubiria jibu akaendelea kuongea;

‘Na ndivyo ilivyo kwa huyu mama…mimi nahisi kuna tatizo lililomfanya awe hivyo, sizani kama ana mtindio wa akili, nahisi, naomba hapo mnielewe vyema, nahisi ana matatizo aliyokumbana nayo hadi akafikia kuwa hivyo…’akasema.

‘Hebu hili tumuachie mtaalamu wa mambo hayo, anaweza kulifuatilia hilo wakati ukifika kama ikibidi…’mwenzake akasema .

‘Sawa….tutafanya hivyo, sasa umesema hadi kumkaribisha kwako, ilichukua muda kutoa maamuzi hayo, huenda mlikuwa mnajadiliana na mkeo, huenda…mliogopa kuwa huyo mama ‘huenda’…ana matatizo ya akili, au..hebu tuambie ilikuwaje mpaka mkafikia maamuzi hayo….achilia mbali hilo la hali ya hewa, ubaridi..’akaulizwa.

‘Huyu mama ni mpenzi sana wa watoto…tangu afike hapa, utaona muda wote yupo na watoto, anatembea mitaani akiimba na watoto….akiona mtoto analia, atamuhurumia sana, na kumuendea mwenye mtoto kuomba ambembeleze…sasa hapo ndipo watu wakaanza kumuona ni mtu wa aajabu…’akasema

‘Mtu wa ajabu kwa kupenda watoto…!?’ akauliza askari kwa mshangao.

‘Mtu wa ajabu kwa vile kama kamuona mtoto analia, akamchukua yeye mtoto huyo hutulia, huacha kabisa kulia, hutaamini lakini ndio hivyo…’akasema.

‘Ni kwamba anajua vyema, kubembeleza sana watoto kwa vile anawapenda..au inakuwaje?’ akaulizwa

‘Hapana,..sio hivyo…yeye kwanza anamchukua mtoto ……eeh, hambembelezi sana,…’akaonyesha kama kambeba mtoto na kuigiza wanavyombembeleza mtoto.

‘Yeye anachofanya ni kumshika huyo mtoto kichwani na kusema;  ‘mtoto mnzuri nyamaza eeeh…’’yaani hivyo tu, mtoto anatulia na kunyamaza, na hata kucheka…ni ajabu kabisa….’akasema

‘Mhh, hilo unalionaje mwenzangu…’wakaulizana wakiangaliana huku wakionyesha kutabasamu kama vile ni kitu kisichoaminika.

‘Mhh, labda uone kwa macho yako,….yaani yeye anaweka mkono wake kichwani kwa mtoto aliyekuwa akilia sana…na kwa hali hiyo wewe kama mzazi, mlezi ...hujui kwanini mtoto analia si ndio…labda mtoto kanyamaza..nasema, `huenda mtoto huyo alikuwa na  sehemu inamuuma, au alikuwa akihitajia nyonyo ya mama yake..sasa anakuja huyu mama,  yeye bila kujali hayo anamshika mtoto kichwani, mtoto ananyamaza, na kuanza kucheka…ndio hivyo….?’ Akaulizwa

‘Afande hata mimi nilipoambiwa hivyo nilikataa..sikukubali haraka kihivyo…, hadi niliposhuhudia kwa macho yangu mwenyewe..’akasema

‘Ulishudiaje…hebu tuelezee..’akasema huyo askari.

‘Kuna siku mtoto alikuwa akilia mimi mwenyewe nilikuwepo hiyo siku,…nikaona nimchukue mwenyewe, nijaribu kumbembeleza, nikahakikisha mtoto hana kitu cha kumpa joto, kila kiuongo kipo safi… nikambembeleza weeeh, nikachemsha nikampa mama yake, akafanya hivyo, na kujaribu kumnyonyesha, lakini wapi…akachmesha..’akasema

‘Haat nyono ya mma yake alikataa..?’ akaulizwa, hapo mwenye nyumba akajibu kama alivyoulizwa, hakusem zaidi kuhusu nyonyo anayotumia mtoto kwa njia ya kuficha jambo akasema

‘Hata nyonyo aliyompa mama yake pia alikataa., ..tulihangaika wee, na mara tukamuona mfanyakazi wa ndani akakimbia nje..haikuchukua muda yule mfanakazi akarudi akiwa na huyo mama, yule mama akamchukua huyo mtoto, akamshika kichwa, na kusema maneno kama hayo, ..haya mtoto nyamaza eeh, nyamazaeee..’mtoto akanyamaza..’akasema

‘Labda alishachoka kulia..labda sehemu iliyokuwa ikimuuma ilishatulia…labda…hilo mimi siwezi kulithibitisha kuwa kweli inaonekana huyo mama ana kipaji hicho..hebu niambie wewe licha ya kuliona hilo kuna nani na nani alifanyiwa hivyo mpaka ukakubali kuwa mama huyo ana kipaji..ana..nini tuseme…uwezo wa kumtuliza mtoto anyamaze…?’ akaulizwa

‘Mimi nina mtoto mdogo..mtoto wangu alikuwa na tabia ya kulia lia kipindi fulani…huyu mama akaliondoa hilo tatizo,…watu , majirani, waliokuwa na watoto wao wanaolia lia, au wana matatizo kama dege dege…kushitika shutuka na kupiga kelele,..’akatulia kama anawaza.

‘Na..na vitu kama hivyo…wengine  hata watu wazima wana matatizo ya kichwa kuuma tu ukija kwake akakushika kichwa, akasema haya kicha pona, kama sio kichwa cha maradhi pona…kichwa kinatulia….lakini kwa watu wa kubwa sio sana,…yeye hasa ni kwa watoto kulia..kuna kule kulia kusipo kwa kawaida,..mtoto analia hadi kukakamaa, si kuna mataizo kama hayo…’akawa kama anauliza na kuendelea kusema;

‘Basi, mama huyu anauwezo wa kuyaondoa hayo matatizo hayo kwa watoto..hasa kwa watoto kwa mkono wake tu…’akasema

‘Mhh..hilo nalo linahitaji utaalamu wake eti mwenzangu, unalionaje hilo, mimi nahisi lina hitajia utaalamu…kulithibitisha…sasa kutokana na hilo ndio ukaamua aje akae kwako, kwa kulipa fadhila au?’ akaulizwa

‘Kama nilivyosema, mama huyo kwa kiasi kikubwa alipenda kuja kukaa eneo la nyumba yangu..hasa wakati wa usiku…, na usiku akawa analala upenuni mwa nyumba yangu…mhh, kibinadamu,….hapana hatukuweza kuvumilia, hatungeliweza kumfukuza…’akasema na kukaza macho kuangalai mbele, huku skiendelea kuongea;

‘Na mtoto wetu akawa anampenda sana huyo mama,….akiwemo huyo mama, mtoto wetu anakuwa na raha muda wote, utafikiri yeye ndiye mama yake aliyemzaa,..ikafikia muda…, tukaona kwanini tusiwe na ubinadamu…basi siku moja mimi na mwenzangu tukaamua huyo mama awe analala chumba cha uwani…’akasema.
‘Wengine pia wana watoto au sio, na hufanya hivyo kwa wengine kama anavyofanya kwako, au sio..lakini nyie ubinadamu ukawazidi..nahisi kuna jambo zaidi..huenda kuna kitu mlitegemea kutoka kwake, ….hebu tuambie ukweli…’akasema askari.
‘Kitu gani kutoka kwa mama kama huyo..hakuna ..ni ubinadamu tu….’akasema

‘Nyie mna mfanyakazi wa ndani?’ akaulizwa

‘Yupo, tunaye, alikuwepo hata kabla ya huyo mama hajafika kukaa na sisi..’akasema

‘Kwahiyo huyo mfanyakazi yupo anamlea mtoto na kazi nyingine za ndani, na akaja huyo mama, na wote wakawa wanaishi pamoja,..na huyo mfanyakazi akiwa na mtoto akianza kulia hata yeye ambaye tunaweza kusema mtoto kamzoea zaidi kwa vile anashinda naye mtoto…mtoto akianza kulia hanyaamzi hadi huyo mama awepo?’ akaulizwa

‘Kuna kipindi mtoto analia kupitiliza..nazungumiza kipindi hicho, kuna kule kulia kwa kawaida,..huko ..aah,…sasa mtoto akianza kulia kwa hali hiyo..ile hali ya kulia kusipo kwa kawaida..hataki mfanyakazi mama wala baba…, ni mpaka huyo mama afike..ndio ananyamaza..’akasema.

‘Hebu niambie tatizo hilo la kulia watoto mnalichukuliaje,..lilikuwepo kabla au baadaya huyo mama kufika ndio likazidi, kwa mtizamo wako, umelionaje hilo?’ akaulizwa

‘Watoto wanalia ..ni kawaida lakini kuna kilio kingine sio cha kawaida..ilikuwepo…mimi nakumbuka hata wazazi wangu walishaniambia hivyo..inatokea, hukuna sababu, …ni hali ya makuzi…’akasema na kutulia.

‘Hebu nikuulize hivi, sitaki ujibu kama alivosema mama yako au nani..nauliza katika ujuvi wako, hapa kijijini, …hii hali ilikuwepo, watoto kulia, au hata ilikuwepo, lakini unavo wewe imezidi zaidi baada ya kuonekana kwa huyu mama?’ akaulizwa

‘Nataka unielwe na mimi hivyo,..maana tusikuze mambo, huku kijijini watu wanapenda kukuza, utasikia ooh, bundi kalia usiku msiba, oooh, nyoka wa vichwa viwili..ni hisia kwa vile ilitokea ikatokea..mimi japokuwa naishi huku lakini sipendi sana hizo hisia…na imani hizo, nashkuru hata mke wangu anaelekea huko..’akasema

‘Sawa..lakini ulivyoona,..sema ukweli wako,…’akaambiwa.

‘Kiukweli..kuna hali ya kuzidi…siji ni kwanini, lakini siwezi nikasema limetokana na huyo mama,..hapana, ..labda ni hali ya hewa..na sio kwamba halikuwepo kabla..hapana…kwa watu wenye watoto wanalifahamu sana, kuna kipindi mtoto analia tu….unajua mtoto hawezi kuongea, kuongea kwake ni kulia..sasa siwezi kusema hilo tatizo halikuwepo,…lilikuwepo, na limekuja kipindi huyu mama yupo, sasa yeye anabebeshwa lawama…’akatulia.

‘Kwahiyo hiyo dhana ya watu kuwa watoto wameanza kulia sana alipofika huyo mama wewe kwako sio kweli?’ akaulizwa

‘Mhh..mimi hapo sijui..mimi kama baba muda mwingi nakuwa kazini..sasa kama kuna kuongezeka kwa kulia kwa watoto baada ya huyu mama kuja,mimi sijui…labda kwa hao wenye watoto siku ningi, ..ila mimi siwezi kukubali huo usemi..’akatulia kama anawaza jambo.

‘Wewe unamtetea huyo mama, kwa vile ni marehemu au kwa vile umeishi naye na umafahamu au kuna nini mpaka usiwe na msimamo sawa na wenzako?’ akaulizwa

‘Hahaha..afande, mimi nimtetee huyo mama kwa lipi….mtu simjui…nasema ukweli tu….lakini…wenzangu huenda wana mtizamo wao, siwezi kuwapinga, ila mimi nasimamia kama mimi..’akasema

‘Na huoni ajabu, watoto wengi kuletwa kwa huyo mama, kama ingelikuwa ni kawaida wasingelisumbuka ..wewe walionaje hilo?’

‘Mimi, nahisi kwa vile imetokea hivyo kuwa huyo mama akifanya hivyo mtoto hutulia, basi hata mtoto akilia kidogo tu, kikawaida..kihivyo…basi wazazi wanachukulia …kihivyo.. kitu ambacho kilikuwepo…ni imani  tu..mimi naona ilikuwepo, sema watu walikuwa hawalichukulii maanani..’akasema.

‘Kwahiyo kutokana na hali ya ..hewa, kutokana na kipaji cha huyo mama, kutokana na upendo wake kwa watoto, nyie mkaona mchukue nafasi hiyo,..mumuwahi huyo mama mapema ili aje kukaa kwenu,..kuna fadida ndani yake vizawadi eeh.. si ndio hivyo..au kuna sababu nyingine, maana huyo mama ni mgeni hamjui wapi alipotokea, pia wengine wanahisi kuwa ana matatizo ya akili…?’ akaulizwa

‘Kama nilivyosema, maamuzi hayo ya kumchukua, sio maamuzi ya siku moja..ilichukua muda, …nikuambie ukweli afande, hebu fikiria na ubaridi ulivyo huyo mama kajikunyata, anahangaika kujifunika na kiganja cha mkono, anatetemeka baridi unatoka unamuona alivyolala kwa shida..hapana… utu ulijaa…’akasema na kuweka mkono kifuani

‘Utu…’afande mmoja naye akaweka mkono kiuani kumfuatishia.

‘Ndio utu…hata kama ingelikuwa ni wewe, …utu utakuingia tu, hata kama una kutu ndani ya moyo, kutu italainika na kubakia utu, huruma ya kibandamu itakutawala…pamoja na mengineyo, lakini kwangu mimi hilo lilinigusa sana, hata mke wangu alipotoa pendekezo hilo, mimi nilimkubalia tu…’akasema.

‘Uliwahi kuongea na huyo mama kwa karibu?’ akaulizwa

‘Mara chache sana..’akasema

‘Hizo mara chache mliongea nini?’ akaulizwa

‘Niliwahi kumuuliza yeye ni nani, katokea ,….jina lake ni nani..’akasema

‘Ulipata majibu yake..?’ kaulizwa

‘Majibu yake…hahahha..’hapo akacheka, na wale maaskari wakaangaliana na kuuuliza;

‘Mbona wakacheka…kuna cha kuchekesha hapo..?’ akaulizwa

‘Labda kwa hayo majibu ndio unaweza kusema huyo mama huenda …lakini mimi siwezi kusema ana mtindio wa akili..sijui wa ubongo,…majibu yake yanakuwa hayana uhalisia..’akasema

‘Alikujibuje..ndio swali letu…sizani hilo jibi linachekesha au…’akaambiwa

‘Jina laki nani…anajibu `mama mtoto….’ Nimekuuliza jina lako nani, atasema; ‘Nani kama mama…ukiuliza tena jina lako nani….’namtaka mtoto wangu…jina lako nani…anatoa majibu yasiyoendana na  swali…yaani majibu ni mengi tu…’akasema

‘Haya ulipomuuliza katokea wapi alisema nini?’ akaulizwa

‘Katokea mbinguni…’akasema na askari wakaangaliana

‘Anaseme hivyo, kuwa katokea mbinguni au watu ndivyo wanavyosema…au wewe wasema hivyo?’ akaulizwa

‘Mimi nilimuuliza swali umetokea wapi, akajibu nimetokea mbinguni, wasikia sana…nikamuuliza mbinguni wapi, akaangalia juu kuniashiria hivyo…’akasema

‘Unasema ulimuuliza swali, yeye ni nani, na baadaye ukamuuliza jina lake ni nani…?’ kwanini ukauliza maswali yenye mtizamo mmoja, ..ulitarajia majibu gani na kwanini ukauliza maswali kama hayo….sijui umenielewa hapo,..hebu fikiria unamuuliza mtu wewe ni nani, na baadaye unamuuliza jina lako ni nani…?’ akaulizwa

‘Ni kweli nilimuuliza hivyo nikiwa na maana yangu, nilimuuliza yeye ni nani..maana hafahamiki,..haeleweki, ni mwanadamu au ni mtu gani, maana ….hahaha’akacheka kidogo na askari wakaangaliana tena na mmoja akatabasamu na mwingine akacheka kabisa…

‘Maana nini…?’ mwenzake akauliza akiwa anatabasamu, ..kiukweli hawa askari wanavyoongea hapo, waliondoa kabisa ile hali ya uaskari, ya kukunja uso, ukakamavu, kulazimisha jambo, waliongea kama raia, …hii imewawezesha kupata taarifa kwa watu bila kuogopwa, lakini wanaowafahamu, ukifika ofisini kwao, hutaamini, kuwa ni hao hao waliokuwa wakiongea kwa tabasamu mitaani.

‘Watu walishavumisha kuwa huyo mama sio wa kawaida…ni mama kutoka mbinguni, ..na mimi nilijiwa hivyo hivyo baadaye..kabla nilisikia hivyo…, au sio…’akasema akma anauliza

‘Wengine wenye imani zao,….tunatofautiana walidiriki kwenda mbali n akumuita eti ni malaika..ajabu kabisa na wale wenye nia mbaya wakamuita shetani…wengine wakamuita…’akashika kichwa kama kutafakari jina, halafu hakumalizia akasema

‘Ndio maana nacheka, kwani hata mimi nilishindwa nimuoneje huyo mama…ni mtu kawaida, au kachanganyikiwa,…., je ni binadamu, na je ni hivyo wanavyotafsiri watu..basi mimi nikajikuta namuuliza hilo swalo, wewe ni nani…nikajiona na mimi kama nimetekwa ndio maana najicheka…’akasema

‘Yeye alikujibuje, ulipouliza swali kama hilo….?’ akaulizwa

‘Mama mtoto…’akasema

‘Mama mtoto!…hilo jibu,…walionaje,  ni kama vile wewe ulizaa naye, kwahiyo anakutanabahisha kuwa yeye ni mama wa mtoto wako, au….’akasema na mwenye nyumba akawa kama kakereheka, akageuka upande wa pili, halafu akasema;

‘Hilo ndilo jibu alilonipa…na mimi simjui, mimi nina mke na mtoto, angekuwa mke wangu amesema hivyo ningekubaliana na kauli yako..lakini huyu ni mtu nisiyemjua, katokea wapi sijui,….anasema hivyo..nilichukulia hivyo kuwa hajui analoliongea..na jibi sio hilo tu..ukimuuliza swali hilo hilo atajibu vinngine..’akasema

‘Hakuwahi kusema mimi ni mpenzi wako, mimi ni mke wako, mimi..vitu kama hivyo..?’ akauliza askari akiwa haonyeshi tabasamu mdomoni.

‘Hapana sikuwahi kusikia jibu kama hilo..’baba mwenye nyumba akasema baada ya kumuangalia huyo askari kwa muda bila kumjibu.

‘Kwa majibu hayo…wewe huoni kuwa mama huyo hayupo sawa,…hukubali kuwa ana matatizo ya akili..au..?’ akaulizwa

‘Sijsema hivyo….’akasema

‘Kama hana matatizo ya akili…ina maana yote aliyokuwa akiyajibu yana usahihi, anajua ni nini anachokisema, yana mantiki….au….na unakiri kuwa yupo sawa, kama ana akili sawa, kwanini atoe hilo jibu kuwa ni `mama mtoto’….?’ Akaulizwa nay eye akakaa kimia, na huyoa skari akasema;

‘Sio kwamba tunakutuhumu, sisi tunajaribu kutafsiri haya maneno yake huenda yana ujumbe tusioujua na tukujua tunaweza kugundua jambo…..’akasema

‘Afande…mimi smjui huyu mama..na kusema hivyo, unaweza kutafsiri upendavyo maana inaweza ikawa ni mama wa mtoto fulani..akini sio maana ya kumaanisha kuwa ni mama wa mtoto wangu..kuwa labda mimi nimezaa naye la khasha….’akajitetea hivyo.

‘Swali muhimu…uliwahi kuiona sura yake…maana nasikia muda wote kajifunika usoni?’ akaulizwa

‘Mwenyewe umesema ..na kujipa jibu mwenyewe..mama huyo muda wote kajifunika kichwani, ningemuonaje..’akajibu akionyesha kuwa kidogo alishakirihika na swali lililopita, na watu hao walishagundua hilo na kwao ni muhimu sana.

‘Mtu mumeishi naye nyumba moja..hata siku moja usipate muda wa kuiona sura ake haijatokea akajifunua, au ikatokea ukaingia kwake ukamkuta hajajifunika..au mke wako hakuwahi kumuona…?’ akaulizwa.

‘Nikuambie ukweli, akina mama kama hao wanakuwa makini sana…inaweza ikatokea bahati mbaya kama unavyosema, lakini akigundua atajifunika haraka sana..na kama hukuwa makini huwezi kugundua ..kukumbuka alivyokuwa, na kwa vile najua kuwa muda wote anajifunika, siwezi kuwa makini na hilo…’akasema.

‘Tunataka hiyo bahati mbaya, ilitokea…swali je uliwahi kumuona sura yake iwe bahati mbaya, au …vinginevyo, kukusudia kutaka kumuona, …unaweza kama mdadisi kutaka kuona anafananaje, huyu ni nani maana ni mtu kaja kwako, kama mchungi wa familia, kama mlinzi wa familia, unatakiwa kuwa makini na watu wasiojulikana, je wewe hukufanya hilo, kwa nia njema tu ya uchunguzi…, ya kiusalama..?’ akaulizwa.

‘Mhh..,kama ilitokea, ilikuwa bahati mbaya,..lakini ….’akasita na kumbukumbu za tukio hilo zikamjia akilini…

‘Sawa…ilikua bahati mbaya….hatuna nia ya kumzalilisha, maana ana sababu yake kujifunika hivyo na wewe unalinda utashi wake, au sio….yeye yupoje, anafananaje…ni binadamu kama wengine au….maana watu wamesema mengi, wengine huyo ni shetani , wengine..yaani kila mtu kasema lake, ..je wewe ulipomuona ulimuonaje….?’ Akauliza askari na jamaa akajikuta kaduwaaa..akili ikawa sasa haipo hapo,na kuna kitu kikawa kinamkanya, sauti ikawa inasema akilini

‘Usiseme..ole wako useme..unakumbuka eeh,.., waliosema ukisema unakufa…hebu kumbuka wenzako, hivi hawajitambui, usiseme utakufa…..utakufa..utakufa..’neno utakufa likawa linajirudia rudia akilini….

NB: Haya mambo ndio hayo


WAZO LA LEO: Siri ya mtu uitunze, moja ya dalili za mnafiki ni mtu kupewa siri akaahidi kuitunza, na badala yake akaitoa, pi a ni mtu akongea huongopa…. Kuna marafiki wanakutana na mmoja anamuelezea mwenzake siri yake anamuambia usije kusema kwa yoyote yule,,,,na huyo rafiki anakutana na mpenzi wake, au yupo yeye na mke wake ambaye waliahidiana kutokifichana siri , na huyo mkewe akauliza jambo lile lile aliloambiwa na rafiki yake asimwambie yoyote,au mkewe akataka kujua walikuwa wakiongea nini na rafiki yake…swali hapo, wewe kama wewe utafanyaje?
Ni mimi: emu-three

No comments :