Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, February 24, 2015

NANI KAMA MAMA-36


‘Kuna nini tena huko ndani, mliambiwa hamuhusiki sasa mnakimbia nini..?’ akauliza baba mwenye nyumba naye akijaribu kutafuta upenyo wa kuona ni nini kinachotkea huko ndani, walipo polisi na huyo mama wanayemchunguza

Mara mmoja wapo aliyekuwa pale mlangoni, ndani akatokeza na kumwambia baba mwenyenyumba;

‘Huko ndani naona hakukaliki, ...mimi naona nijiondokee zangu..’akasema

‘Kwani wewe umeona nini?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Hata sikuona vyema, maana nilipopata upenyo wakuangalia...nikamuona askari mmoja yupo chini, na mwenzake anataka kukimbia…’akasema na mwingine akadakia.
‘Asari anakimbia....! hapana, sio kweli, labda hukuona vyema, mimi nasikia askari hawaogopi uchawi..’akasema mtu mwingine.

‘Kwani ilikuwaje?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Ohh, kweli yule mama hatakiwi kufungulia, hata akiwa mfu …hutaamini yule askari aliyekuwa akimfunua kala mwereka,..kadondoka chini na mwenzake ....mimi nimeona kwa macho yangu mwenyewe...’akatokea mwingine akiongea huku akionyesha hamasa.

‘Yule askari aliyekuwa akitoa amri, kuona mwenzake kala mwereka...akageuka kukimbia..’akasema huyo aliyetokea ndani.

Baada ya huyo mtu kusema hivyo, kila mtu akakimbilia pale mlangoni kutizama ndani, na wale waliokuwepo ndani ambao walikaidi amri ya askari kuwa wasiingie ndani lakini baadaye wakaingia kwa uchu wa kujua kinachoendelea, wakawa sasa wanataka kutoka nje, wakionyesha wasiwasi, na kwa hali hiyo ikawa sasa ni mgongano pale mlangoni, wanaotaa kutoka, na wanatotaka kuingia kuona kilichotokea.

‘Tupisheni tupite…hili sasa ni balaa..’wakawa wanasema waliokuwepo huko ndani

‘Kwani kumetokea nini?’ wakauliza waliokuwepo nje, na baba mwenye nyumba ambaye pale aliposimama hakuweza kuone vyema, akawa anahangaika kuchungulia lakini hakuona kinachotokea zaidi ya askari mmoja kuwa yupo sakafuni, na mwenzake akiwa kasimama huku akiwa anaangalia pale alipolazwa huyo mama.

Haikupita muda akatokea mjumbe mlangoni, mjumbe alikuwa ndani na sasa anataka kutoka nje, na wale waliokuwepo nje walipomuona mjumbe wakaona ndiyo nafasi yao ya kujua kilichotokea huko ndani, wakambana kwa maswali;

‘Ehee mjumbe wewe umetokea ndani, kwanza tuambie kwanini unatoka mbio mbo kama unakimbia...?’ akauliza mtu mmoja

‘Mjumbe tuambie kumetoeka nini huko ndani mbona watu wanakimbia kutoka nje..?’ akauliza mtu mwingine

‘Ohooo, sina muda wa kujibu maswali yenu, kwanza niacheni nipite,..mimi niliwaambia hawakutaka kunisikia...yule mama sio wa kawaida, wakaona mimi ni naamini ushirikina...sasa unaona....wenyewe wamathibitisha..’akasema

‘Eheee..ona eeeh, sasa mjumbe tupe picha kamili....imetokea nini....maana haya mambo uyaone mwenyewe..’akasema mtu wmingine.

‘Hawakutaka kuamini yamekuwa kama yale yale .....ya hao walioambiwa hakutaak kusikia,..., nasikia hata hao washukiwawa humo moto japokuwa jawajakamatwa… hali zao ni mbaya…wanaweweseka ovyo…’akasema mjumbe na aligeuka upande wa pili akamuona baba mwenye nyumba akashituka na kugeuka upande mwingine akitafuta sehemu ya kupita, huku jamaa mmpja akiendelea kumhoji mjumbe

‘Ina maana unawafahamu hao watu mjumbe..hao washukiwa wa moto, kumbe kweli kuna watu walifanya hujuma, mjumbe unawafahamu ni akina nani?’ akaulizwa

‘Hapana nimesikia watu wakisema tu..oh, jamani niacheni maana nina haja….nataka kwenda haja…nipisheni jamani, waliyoyataka wameyapata…nipisheni nitawakojolea..’akasema mjumbe huku akiharakisha kutoka nje, na alipopata upenyo, mbio akatokomea upande wa pili ambapo haonekani.

Tuendeele na kisa chetu


‘Ina maana ni kweli kuwa kuna hujuma zilifanyika, na mjumbe anafahamu hili,…wamechoma nyumba yangu kwa …aaah, …hapana ?’ alikuwa baba mwenye nyumba ambaye aliweza kumsikia mjumbe pale aliposema;

‘’….nasikia hata hao washukiwawa huo moto japokuwa hawajakamatwa… baadhi yao hali zao ni mbaya sana…wanaweweseka ovyo…’’

Na jinsi alivyoshituka alipomuona baba mwenye nyumba inaonyesha dhahiri alitaka kuongea mengi, ila alikatisha tu alipomuona baba mwenye nyumba,..

Baba mweny nyumba akageuka kuangalia upande ule alipoelekea huyo mjumbe hakumuona, …alishatokomea upande wa pili wa nyumba, ambapo hakuna choo, sasa sijui alikuwa anakwenda haja ipi, yaonyesha kabisa mjumbe alikuwa na nia ya kuondoka hapo.

Baba mwenye nyumba akaamua kumfuata , akijia huenda atamkuta hapo nje, au au kama kaamua kuondoka atamkuta akiwa hajafika mbali, ..akatafuta upenyo na kutoka nje, akaangalia huku na kule hakuona dalili za mjumbe, akajaribu kuwauliza watu walikuwa wanakuja hapo kama walimuona mjumbe, na watu hao wakasema hawajamuona.

‘Atakuwa kaenda wapi..?’ akajiuliza na alipohakikisha kuwa kweli mjumbe keshakimbia, hayupo sehemu ya kuonekana akaamua kurudi ndani tu.

Akilini mwake, hata yeye alishahisi huenda moto huo si wa ajali, lakini hakutaka kuweka tetesi za uvumi kichwani mwake, akajipa moyo kuwa akikutana na mjumbe atamdadisi ili ajue vyema, akakumbuka jinsi mke wake alivyoongea walipokutana baada ya kutoka kule kwenye jengo lililoungua….
‘Mume wangu una hatari kweli, sasa ni nini kilikupeleka huko, na hali moto bado ulikuwa haujazimika vyema..angalia ulivyounguza hiyo shati…na mbona una damu..?’ mkewe akamuuliza na alipogundua hilo, akakimilia ndani na kubadili shati, akatoka na kukutanana mkewe.

‘Mke wangu sasa tutafanyaje,…maana sasa huu ni msiba na upo haa[a nyumbani, inabidi utoe akiba yao, kuwahudumia watu…’akasema mume mtu.

‘Kwani wanasemaje,..ulihahakikisha wewe mwenyewe kuwa amekufa..?’ akauliza mkewe.

‘Ina maana hmjaamini kuwa kafariki…nimemshuhudia mwenyewe akikata roho..muhimu kwa sasa ni kuona tutajipangaje…tukijua huu msiba ni wa hapa, labda watokee ndugu zake…’akasema mume mtu.

‘Haya sisi tunawasikiliza nyie.. ujue pamoja na yote huenda huyu mtu ana ndugu zake, hatuwezi kutangaza msiba huo kama wetu, wakati ndugu zake wapo..inabidi kuangazwe kama kuna mtu anamfahamu, au ana tetesi zozote wapo anapotokea..’akasema mke wake.

‘Tumekaa naye hapa, hakuwahi kusema ana ndugu, hajui ..na sina uhakika kama anaficha…mimi nahisi hataki au hakuwa anaelewana na ndugu zake…sina uhakika..’akasema mume wake.

‘Yote hayo hayatasaidia kitu…mimi naona tujipange tu, kuwa msiba ni wetu…’akasema mama mwenye nyumba.

‘Basi ngoja niongee na mjumbe nitarudi baadaye, tatizo mjumbe yupo na askari, wanamuhoji,..’akasema

‘Lakini mumewangu kuna kitu nataka kukuambia…’akasema na kumshika mume wake, wakasogea mbali kabsa na watu, akasema;

‘Mume wangu unasikia watu wanavyosema..eti moto huu umewashwa na watu wakikusudia kumuua huyo mama, wanadai huyo mama ni mchawi, kwahiyo watu wakaamua wamchome moto…’akasema mke wake.

‘Maneno hayo umeyasikia kutoka kwanani, usiwasikilize watu, najua yatasemwa mengi ..sisi kwa hivi sasa tuchukulie ni ajali tu…maana tukitaka kudadisi sana, tutazidi kuumia, na hasara tumeshapata hata aikijulikana kuwa kuna watu wamefanya hivyo, unafiri tutajengewa, hiyo imekula kwetu....’akasema mume wake.

‘Mimi nakuambia nilivyosikia kwa watu,..hata mimi sikutaka kuamini mambo yao, lakini kuna wanawake watatu wanasema waliona kwa macho yao wakiwa wametokea mjini …’akasema

‘Wanawake gani hao, na wameonaje?’ akauliza mume mtu akiwa na hamasa, mke mtu akageuka huku na kule kuhakikisha hakuna mtu anayewaona au kuwasikiliza wanachoongea, alipoona kuna uhakika wa kutokusikiwa akasema;

‘Mume wangu…hao akina mama ni wenyeji wa hapa,..ni mabinti wanaofanya akzi mjini, mimi naona wewe huna haja ya kuwajua,maana wanawake wenyewe hawajatulia, ukikutana nao, nikujuavyo..mmh,...’akasema

‘Mke wangu ina maana huniamini, hilo limetokea wapi tena,..yaani bado tu..aah, kama mambo yenyewe ni hayo haina haja ya kuniambia, wewe rudi kwa akina mama muendelee na mipangilio….’akasema mume mtu.

‘S.ilaio kwambasikuamini….ila sizipendi tabia zao , nilishawahi kuongea nao…sasa wao wakati wanatokea mjini, wakati wanapita, wakaona kundi la vijana,…kama watano hivi au zaidi, ilikuwa ni usikuwa giza..hakuna mbalamwezi,…walimuona mmojawapo akiwa na galoni , hizi za mafuta ya taa..’akasema.

‘Hao wanawake usiku wote huo walikuwa wanatokea wapi?’ akauliza mume mtu.

‘Hao wanawake wanafanya kazi mjini, inavyoonekana walikuwa wamekuja likizo, wao walisema, gari lao liliharibika walipofika maeneo ya huku kwetu ni mbali …, walisubiria sana gari hilo litengenezwe, lakini halikutengemaa, ikabidi waanza kutafuta njia za kufika huku, kwa mgu ni mbali sana,…wakahangaika mpaka kukatokea gari moja ndipo wakaweza kuletwa hadi hapo njia panda, na wakawa wanatembea kwenda majumbani mwao..

‘Sasa walipofika eneo karibu na nyumbani kwetu, kwanza wakahisi harufu ya petrol, wakawa wanaulizana, harufu hiyo imetokea wapi…mara wakawaona watu wakitembea kuzunguka eneo la nyumba yetu..wakasikia mmoja akisema;.

‘Lazima yupo humo ndani…hakuan sehemu nyingine ya kutokea..’mmojawao akasema, na ara wakaonekana hao mabinti, na hakukuwa na njia nyingine ya kujificha

‘Wanadai kuwa wale vijana walipowaona hao mabinti wakaanza kuwakimbiza hao wasichana,hao wasichana wakatimua mbio, kila mmoja kivyake…walikimbizwa hadi wakafika mbali na baadaye hao vijana wakarudi, inaonekana hawakutaka kuendelea kuwafukuza hao wasicahana. Baadaye wale wasichana wakakutana na kwenda kulala sehemu moja kwa mmoja wao.

Wale vijana wakarudi wakijua wana kazi ya kufanya..’akasema

‘Kwahiyo hawakuthibitisha kwa kuona huo moto ukiwashwa na hao vijana …?’ akauliza mume mtu.


‘Hilo hawakuthibitisha, ila waliona hao vijana wakiwa na galoni,..na harufu ilisikika wazi kuwa ni ya petrol , kwahiyo hiyo harufu ilikuwa na maana gani, ina maana walishamwaga hiyo petrol..’akasema.

‘Walimwaga wapi, nani aliwaona wakimwaga..polisi watakuhoji sana ukitoe taarifa za tetesi…je waliona dalili kuwa petrol hiyo ilimwagwa wapi?’ akauliza mume mtu.

‘Ina maana hunielewi,..hao wasichana hawakuona maana wao walipofika hapo, na kuonekana tu, walikimbizwa..na walisikia hiyo harufu wakati wanapita wakawa wanaulizana kuhusu hiyo harufu ndipo wakawaona hao vijana mmoja akiwa na galoni..sasa wangejuaje hiyo petrol ilimwagwa wapi..’akasema mama mwenye nyumba

‘Kwahiyo kwa kifupi ni kuwa hawakuona wapi wapomwaga hiyo petrol, na hawakuona moto ukiwashwa...ila walihisi harufu tu…na kuwaona hao vijana…hawa ushahidi kuwa ndio wao waliwasha huo moto…’akasema.

‘Ndio hivyo….’akasema mke mtu

‘Huo ushahidi hautoshi mahakamani....maana hao vijana wakikamatwa watadai kuwa kweli walikuwa na galoni ya petrol, na huenda hiyo petrol ilimwagika kwa bahati mbaya wakati wanakwenda kwenye shughulizi zao..je hao wasichana hawawezi kuongea na polisi?’ akaulizwa.

‘Hao wasichana hawapo, ..’akasema mke mtu

‘Hawapo! si umesema walitokea mjini, wamekuja likizo au kuwatembelea ndugu zao au sio..sasa iweje waondoke haraka kihivyo? Akauliza baba mwenye nyumba

‘Ndivyo ilivyokuwa,…kuwa wamekuja likizo, au mapumziko ya siku kadhaa,… lakini wanadai walipata taarifa usiku huo huko, taarifa za vitisho kuwa wakionekana hapa kijijini watauwawa, kwahiyo asubuhi na mapema, wakaondoka kwa haraka na hawajulikani kama wamerudi mjini au wameelekea wapi, wanawake wenyewe hawajatulia…’akasema.

‘Sasa wewe nani kakupa hizo taarifa..ni isiwe na wao wanahusika ndio maana wamekimbia?’ akaulizwa.

‘Unajua masikio hayana pazia, wakati nipo kwenye mihangaiko ya kuangalia watu wakae vipi, nikawafuma akina hao akina mama wawili wakiongea..mama mmoja ni mama wa kati ya hao mabinti…’akasema

‘Ehee ukamuuliza?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Mama huyo hakukubali kuniambia ukweli….’akasema

‘Sasa yote hayo uliyapataje…?’ akaulizwa

‘Niliwasikia wakiongea na shiga yake , hawakujua kuwa mimi nipo nyuma yao ….’akasema

‘Kwahiyo wewe uliwasikia wakiongea nini haswa kitakachosaidia…?’ akaulizwa

‘Kama hivyo nilivyokuambia kuwa hao wasichana walitokea mjini, wakafika eneo hilo, wakasikia harufu, wakakimizwa…..huyo mama mmoja ndio alikuwa akimsimulia mwenzake, na waliponiona wakanyamaza,na yule aliyekuwa akimuhadithia mwenzake akawa anaondoka, nikaona nimfuate kumuulizia, nikamfuatilia hadi nje, …, nikamuuliza, akakataa kata kata kuniambia ukweli, akasema yeye hajui lolote…’akasema.

‘Haya mambo sitaki kuyakuza sana maana kama ni hasara tumeshapata , muhimu ni kutoa ushirikiano na polisi ikibidi…nasema ikibidi, …lakini tusiongee lolote kuhusu fununu au kusikia, hayo wao wenyewe watajua jinsi gani ya kufanya, ukijianya unajua sana, siji umesikia, utaingia matatani...’akasema mume mtu.

‘Mume wangu, mimi nawaogopa sana polisi maana wakianza kukuhoji unaweza kujikuta umetegewa, ukaongea hata yale uliyokuw a hukukusudia kuwaambia,… na hao vijana wamesikiwa wakisema atakayewataja watahakikisha wanamuua…wapo tayari kufa, kwani kufa kwao ni kitu cha kawaida tu…’akasema.

‘Sikiliza mke wangu, hata mimi siwezi kusema lolote kwa hivi sasa, maana hapa nilipo kichwa changu hakipo sawa…nahitajia muda wa kuliwazia hilo, najua polisi watatuita kutuhoji, ninachokuomba ni kutokuongea hayo ya kusikia, waachie polisi wenyewe wagundue hilo…najua watafikia huko na watagundua ukweli…’akasema.

‘Hata mimi nilikuwa na wazo hilo hilo...na jingine nimeonana na mke wa mjumbe na yeye akawa ananimbia yake…’akasema.

‘Mhh, mjumbe, mkewe…ehe,…na yeye kasemaje, yeye uliongea naye, ..hukumsikia.. niambie maana huyu mjumbe mimi simuamini sana, anaongea kupitiliza..’akasema mume mtu.

‘Mkewe anasema , mume wake wakati anatoka usiku kufuatilia…’akasema

‘Kufuatilia nini usiku?’ akadaikia muem wake.

‘Si baada ya kusikia ukelele wa huo moto, …sasa wakati mume wake anaamuka kutoka nje, akasema huenda hao wapinzani wake wameamua kumfanyizia…’akasema.

‘Kwa vipi?’ akaulizwa

‘Anadai wamekuwa wakitafuta upenyo wa kuonyesha kuwa kijiji hiki hakina amani, hakina mjumbe anayefaa, na yakuwa mjumbe hajui wajibu wake, anawakaribisha watu wasiofaa akiwemo huyo mama …’akasema mkewe.

‘Mhh, najua yatasemwa mengi, …na hasa kama limegusishwa na kisiasa, basi sisi tusubiri ..tutasikia mengi…lakini bado sijaelewa, unasema mke wa mjumbe  alimsikia mume wake akisema… anawakaribisha watu wasiofaa akiwemo huyo mama sasa,..walijuaje kuwa moto huo umetokea kwa huyo mama…?’akasema mume mtu na kuuliza.

‘Aaah, mimi sijui…hebu na wewe nikuulize ulipofika huko alipokuwepo huyo mama, ulimkutaje..watu wanadai hawezi kufa maana ni mama kutoka mbinguni…na hata huo moto hauwezi kumuunguza…ati ni kweli hajaungua kabisa?’ akaulizwa

‘Hajaungua sana na moto, ni majeraha machache, sana sana..miguuni na mikononi lakini sio saana…kwenye mwili hajaungua maana angelikuwa kaungua nguo alizovaa zingekuwa zimengua, nimekuta na nguo zake kama kawaida…’akasema na kuongezea;

‘Kiukweli kama ni kufa, labda kafa kwa kukosa hewa, ..na pia jinsi alivyojifunga,..moshi hakuweza kumuathiri sana, labda huko kukosa hewa…sasa sijui ..sina uhakika ,..ila ana mjeraha ya mapanga,..sasa hapo ndio nahisi kuwa huenda kafa kwa kupoteza damu nyingi…’akasema

‘Uliona damu hapo alipokuwepo?’ akaulizwa.

‘Ndio hapo nashindwa kuelewa, hakukuwa na damu pale ardhini,  ..sikuona damu zaidi ya matone kidogo tu…, niliangalia kote sikuona sehemu kuna damu nyingi ardhini, maana hayo majeraha ni makubwa,.damu itakuwa imetoka kwa wingi...’akasema.

‘Ina maana gani sasa mume wangu..?’ akauliza.

‘Nahisi atakuwa katendewa hivyo, kakatwa na mapanga nje ya chumba, na huenda alikimbilia hapo ndani, na..kuingia mvunguni kujificha…wakawa wanamfuatilia, walipofika hapo nyumbani hawakumkuta, na kwa vile wana uhakika kuwa aliingia hapo ndani,ndio wakaona wachome nyumba moto…’akasema mume mtu.

‘Duuh,  unaona eeh,…kwa vile ni mama kutoka mbinguni, hana damu…na nikuambie kitu mume wangu..huyo mama yawezekana hajafa..mwenyewe utaona…hapo anatafuta upenyo, watu wakizubaa tu..huyoo, anapaa anaondoka zake…’akasema mkewe

‘Mke wangu hebu acha hizo imani haba….mtu yupo kalala pale mfu…unasema hajafa, ina maana sisi ni wajinga..’akasema mume wake.

‘Haya, sasa mwili wake si unatakiwa upelekwe hospitali, maana kama ni majeraha namna hiyo akiendelea kukaa hapo, mwili utaoza haraka, …?’ akauliza mke mtu.

‘Ndio polisi wanamchunguza huko ndani…ngoja niingie nisikie kinachoendelea nitakuja kukuambia la kufanya, jipangeni tu , …’akasema mume mtu na kuondoka upande huo walipokuwepo akina mama.

*************

Kwa upande mwingine kulikuwepo na kikosi kingine ambacho kilipewa kazi ya kuchunguza sehemu ya moto na pia kati yao kulipokuwepo na askari wawili waliokuwa wakikusanya maelzo ya watu.

Kikosi kile cha kuangalai moto ulivyowaka, kama ni wa kawaida au ni hujuma, kiliweza kwenda mbali zaidi, na kugundua baadhi ya vitu vinavyoweza kusadikiwa kuwa ni vifaa vilivyotumika kuwashia huo moto, lakini havikiwa na nguvu sana, kilipatikana kibiriti, na njiti zake na kitambaa kilichoungua nusu, chenye harufu ya petrol

‘Bado hatujapata kitu cha uhakika..lakini harufu iliyoenea huku, hasa hapa kwenye majani aonekana ni ya petrol…’akasema mwenzake.

‘Na huu moto ulianzia pale….’.akasogea hadi hapo anapohis moto ulianzia,..

‘Huu moto waonekana ulianzia hapa…ukazunguka,…mmh, unaona…kuna galani hapa mkuu, hebu njoo uione…’akasema mwingine na mwenzake akasogea hadi hapo ilipo hiyo galoni

‘Mkuu..unaona huu moto umeanzishwa na watu kwa makusudi..unaona hata hii galani haijateketea kabisa..haijaungua sana..’akasema na akiwa kavalia kinga akasogea kutaka kuichukua.

‘Subiri…ngoja nikamuite mkuu, aje aone mwenyewe..nilijua tu..huu moto umeanzishwa na watu..’akasema na kuelekea huko kwa mkuu wake, na baadaye akarudi.

‘Nimekuja na huyu mpiga picha, ngoja achukue matukio,..na mkuu kasema tuendelee, sasa cha muhimu kabla hatujaingia ndani kabisa, kwenye mabaki mabaki naona tuzunguke kote kwa nyuma…’akasema

Kabla ya hapo, kundi hili lilikuwa na watu zaidi, ila waliamua kugawana majukumu, wawili wakabakia kutafuta chanzo cha moto,na kukusanya ushahidi, na wengine wakaenda kuwahoji watu walioshuhudia huo moto…na kundi la kuangalia chanzo cha moto likiwa linaendelea kwa upande mwingine kulikuwa na kundi la kuwahoji watu…

*************

‘Nataka kuongea na baba mwenye nyumba yupo wapi?’ akauliza askari wa kundi la kuwahoji watu, na wakati huo baba mwenye nyumba ndio alikuwa katoka kumfuatilia mjumbe, aliporudi tu akakutana na huyo askari kanzu.

‘Mimi ni askari na kazi yangu ni kutafuta ukweli kuhusiana na huo moto..kwanza nikupe pole kwa maafa hayo..najua ni hasara na ikizngatia kuwa huku kijijini hatuna huduma za bima, kwahiyo ni hasara isiyo na marejesho, au sio…’akasema

‘Tumeshapoa…’akasema baba mwenye nyumba.

‘Muhimu ni kujua ukweli..hata kama kuna hasara lakini je haara hii ni ajali a kawaida au ni ya watu wameamua kufanya hujuma..’akasema askari mwingine

‘Na ukweli huo hatuwezi kuupata kama hatutpata ushiriakino kutoka kwenu..na ni vyema mkatuelezea kila kitu, ili tuweze kuchanganua wenyewe, maana kuna kusikia, kuna kuona, na kuna kudhani..yote sisi tunahitaji..’akasema na mwenzake akaongezea kwa kusema.

‘Ila mara nyingi ukifika mahakamani wao sana sana wanahitajia ulivyoona wewe…unaona, lakini  sisi tunataka yote, kama uliona, itakuwa ni bora zaidi..lakini hukuona umesikia,..tunahitaji hilo pia, litatusaidia kufuatulia, au unavyodhani, unavyofikiria wewe hata hilo tunalihatajia ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu…’akasema askari mpelelezi.

Baba mwenye nyumba akawa katulia akiwaza ni nini akiseme na ni nini asikiseme maana ya kusikia ni mengi na hayo ya kusikia yanaweza kumtia mtu hatiani , ….alpwaza hivyo moyini akasema ‘hapa natakiwa kuwa makini.

Akilini akawa anamuwaza huyo mama,…ambaye sasa anajulikana ni marehemu pamoja na mengi, pamoja na kumbukumu zake, lakini moyoni aliona hakustahili kufa kifo cha namna hiyo…walivyomkata kata na mapanga, ni unyama….hata hivyo hakupenda kujiingiza zaidi, akaona akijiingiza zaidi anaweza kujitia matatani.

NB: Haya kwa leo inatosha


WAZO LA LEO: Usiwe mwepesi kukubali taarifa za kusikia, kwani nyingine zinaweza kuwa uchonganishi tu, na unaposikia taarifa kama hizo kama zina umuhimi kwako zifanyie uchunguzi kwanza kabla ya kuziamini au kuzitangaza kwa watu wengine.
Ni mimi: emu-three

No comments :