Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 20, 2015

NANI KAMA MAMA-35

  

 ‘Msiniue, mimi sio mwanga, mimi sio mchawi… jamani…nimewakosea nini walimwengu…kwanini mnataka kuniua…..mimi namtaka mtotow angu tu……nataka mtoto wangu..msiniue msiniue….’ akaanza kupiga ukelele mara mbili, halafu akatulia kimia..

Haikupita muda, yule mama akatikisika mguuni, na akawa kama unajivuta, na miguu ikatikisika  mara moja mbili na ya tatu akawa kimia..ni kama vile mtu anakata roho..

‘Oh, amekufa…’alisema baba mwenye nyumba akiwa kaduwaa..

Baba mwenye nyumba kuona vile akapanua macho kama haamini akashika kichwa , halafu akachuchuma na kumshika mwili wa huyo mama akise kwa masikitiko,

‘Hapana, usife…nataka kuwa na uhakika..nataka kukujua, ..nataka kujue kuwa kweli ni wewe, nataka kukujua wewe ni nani, na kama ni wewe..ooh, ..’akawa anasema na kuinama huku akihangaika, akitafuta sehemu ya kushika, akitafuta, la kufanya, mikono ikawa inacheza cheza hewani, na akashituka anashikwa begani, alishituka na kusimama …akitaka kukimbia.

********


‘Mkuu huo moto sio wa bahati mbaya…

‘Nilishahisi hivyo..’akasema

‘Watu wa uchunguzi fanyeni kazi yenu, ila kwanza nataka kuiona sura ya huyu marehemu…’akasema akisogea pale alipolzwa huyo mwanamama.

‘Na kwanini wamefunga hivi, wasije wakawa wamemkata kichwa…hebu mfungue tuone kichwa na sura yake…’akasema huyo askari kiongozi wao.

‘Hajafungwa na mtu huyo…ndivyo alivyokuwa toka awali..ndio maana nawaambia kachanganyikiwa huyo..mnapoteza muda wenu bure…’akasema mjumbe aliyekuwa akichungulia kwa mbali.

‘Hebu mfunue kabisa eneo la kichwani, kuna shida kufunua hapo,…ooh, ‘akasema huyo askari kiongozi alipoona mwwenzake akiangaika kuifungua ile nguo.

‘Na kwanini kajifunga hivyo, ok,..’akasema na aliposkia mjumbe anasema kuwa wanapoteza muda bure, yeye kwanza akawa kama hmjalia lakini baadaye akasema;

‘Mjumbe sisi kufanya hivi hatupoezi muda hapa…hii ni kazi yetu, tunatakiwa kufanya uchunguzi kujua ukweli, hatuangalii huyo mtu yupoje, hata kama kachanganyikiwa lakini yeye kama binadamu ana haki ya kuishi….’akasema huyo askari na yeye akisaidia kufungua ile nguo iliyofungwa shingoni.

‘Sijasema kuwa hana haki hiyo, ila naona mwisho wa siku mtagundua kuwa hakuna lolote baya lilifanywa, ni …..kwa vile kachanganyikiwa,..nyie hamuoni mtu akajifungaje hivyo kama anajinyonga….’akasema mjumbe.

‘Na kuna jingine, watu walipoona huyo mama anajiunika hivyo, wakais kuna tatizo,kwahiyo wakatafuta njia ya kumfunua, kilichowapata watakuambia….ina maana haitakiw huyo mama kufunuliwa..mtakuja kuniambia….’akasema mjumbe.
Askari huyo kiongozi akamuangalia mjumbe, huku mwenzake akiendelea kufungua sehemu ya mwisho ya hiyo nguo iliyozungushiwa shingoni, ..huyu mkuu akatabasamu alivyoskia mjumbe akiema hivyo, akasema;

‘Yaonekana na wewe mjumbe unaamini sana mambo ya kishirikina…sisi askari hatuogopi hayo, ulishawahi askari amelogwa…hatulogeki sisi…..’akasema na kumgeukia mwenzake aliyekuwa sasa anavuta sehemu nyingine ya nguo.

Yule polisi akawa anamfungua uso yule mama, na akawa sasa anataka kuvuta ile sehemu ya juu, iliyomfunika yule mama kichwani,.. ili uso wa huyo mama uonekane…mara kwa nje, kulitokea upepo mkali…watu wakawa wanakohoa, hata huyo muu alizidiwa kwa kukohoa…

Baadaye ule upepo ukaisha, na kulipotulia, yule mkuu akasema;

‘Haya endelea kumfungua…’akasema huyo mkuu akijifuta futa mavumbi.

`Koho koho…koho…’ ilikuwa kikohozi..kikohozi kilichomfanya polisi kuachia ile nguo na kurudi hatua moja nyuma,…akagongana na mkuu wake, aliyekuwa kasimama nyuma yake, wakajikuta wanataka kudondokeana,….wote wakabakia midomo wazi….

Tuendelee na kisa chetu

***************
Mkuu wa askari hao, akiwa ameshikana na askari mwenzake kujuzuia wasianguke, huku wakiwa wametizamana, na kila mmoja akawa anachezesha mdomo kutaka kusema neno, lakini hakuna aliyetamka hata kauli moja, kwa sekunde kadhaa…. Baadae yule mkuu akasema;

‘Ni wewe umekohoa?’ akauliza

‘Sio mimi mkuu…sssi-sijui..sina uhakika..mi-mi –oh, mkuu siamini…au ni wew eumekohoa mkuu, kunitisha..’akasema askari mwenzake.

‘Hapana, …ni wewe umekohoa..haiwezekani…nimekusikia kabisa..haiwezekni, kwanini unafanya hivyo…’akasema sasa akitizama kwa wasiwasi , hakutaka kutizama pale alipolazwa huyo mama, alitazama upande kwa askari mwenzake , upande kwa mjumbe, mjumbe kwa muda huo yeye alikuwa kwa mbali akiwa anaonyesa uso wa kushangaa, akauliza;

‘Kwani kuna nini tena huko mbona kama mnashikana?’akauliza

‘Mjumbe mna uhakika …?’ akauliza huyo askari

‘Uhakika wa nini tena kila kitu nimeshawaambia?’ akauliza mjumbe

‘Ulisemaje kuwa huyu mama yupoje, kwanini tusimfunue tukaona sura yake?’ akauliza huyo mkuu

‘Kwa ushauri wangu, huyu mama akiwa hai alikuwa hapendi kabisa kufunuliwa uso wake, sasa nyie mnachukua jukumu la kumfunua,…sawa nyie ni askari labda mna nguvu za ziada,…endeleeni..msije mkasema sikuwaambia..maumeona huo upepo, upepo kama huo wazee wetu wangelikutafsiria..sio bure…’akasema mjumbe.

‘Lakini mjumbe, kwani tukimfunua kuna nini , maana ni muhimu tumjue sura yake ikibid tumuweke kwenye magazeti ili mwenye huyu ndugu ajitokeze, hapo kuna ubaya gani, ..lakini pia huyu aanokena kakatwa na mapanga…je ni wapi na wapi, labda huko usoni kuna majeraha pia…, ni muhumi tukamilishe uchunguzi wetu…’akasema huyo askari wakiwa sasa wamesimama wakimuangalia huyo mama.

‘Nyie watu, mkumbuke kuna waliojaribu kumfunua sasa hivi hawajiwezi…mimi nawapa kama angalizo, sio kwamba naingilia kazi yenu..hapaan hapaan msije mkasema mjumbe alisema hivi…mmmh, sitaki,!’ akasema akigeuza uso upande wa pili..

‘Niuhasuri wako, ..hauna ubaya, lakini ni lazima tufanye kazi yetu..;akasema askari huyo.

‘Ndio..anyeni..mbona mnasita…, ingelikuwa mimi, aaah, huyo tungelishazika zamani ..maana hatujui ya mbeleni, huenda kweli ni mwanga, huenda kweli….ka-katokea kuzimu na ukimfanyia asilolitaka, anakugeukia, atakujia usiku kama jinni, au kibwengo, atakutisha,..…’akasema na kuwafanya wale askari wawili kuangaliana.

‘Mimi siwatishi…lakini hayo nimeshayasikia, kwa umri wangu huu, nimeyasiki na mengine kuyaona..si ndio hayo..watu wapo kitndani hawajiwezi..sasa..sijui,..nyi askari mnaojifanya hamlogeiki, haya  endeleeni mbona mumeacha..kwasababu ya vumbi, naona vikohozi vimewazidi...au ndio huko kuogopa?’akasema mjumbe

‘Tunaendelea mjumbe sisi hayo hayatutishi…’akasema huyo mkuu akimuangalia mwenzeke akasema;

‘Endelee kumfunua, ila acha tabia ya kunitishia…tuache kabisa, nitakufanga.ohooo, kama ni wewe umekohoa halau unaniishia mimi,..ok, endelea kumfunua…’akasema huyo mkuu akimuangalai mwenzake, ambaye sasa lionekana kuwa na wasiwasi, akawa anasita kuendelea kumfunua huyo mama.

Akasogea na kwa mkno sasa ulioonyesha kutetemeka, akawa anaanza kuvuta ile nguo ya juu ili uso ubakiwa wazi..akavuta..nguo hatoki, akavuta….hiyo ikaanza kutoka….

******

Baba mwenye nyumba ambaye alikuwa kwa nje, akataka kuingia kuona ni kitu gani kinachoendelea, lakini kulikuwa na watu wamesimama mlangoni, na hawakutaka kuachia nafasi ili aweze kupita, kila mmoja alikuwa akihangaiak kupata upenyo wa kuangalia ni kitu gani kinachoendelea huko ndani, baada ya upepo huo mkali kupita.

‘Huo upepo unaashiria nini mzee mwenzangu..?’ wazee wawili wakawa wanaongea.
‘Ingelikuwa enzi za mababu zetu, huo upepo ni ishara ya kitu…onyo..au kumetokea jambo lisilo la halali…’akasema mwenzake.

‘Mhh, hata mimi nakumbuka kitu kama hicho ndio maana nikataka kuwa na uhakika..sasa kwa hili huoni kuwa inawezekana…kuna onyo hapa, kuna ishara hapa tnapewa, lakini nani atakusikiliza..’akasema huyo mzee.

‘Aaah, mzee mwenzangu hayo yalikuwa ya enzi hizo,..maana hata ujana wetu tulishaanza kupuuzia puuzia ya wazee wetu..kila karne inakuja na mambo yake..’akasema

‘Na kweli na karne hizi mmh, tunashuhudia mengi…sijui…’akasema mwenzake.

‘Mzee mwenzangu, kwa sasa tuache waendelee na sera zao, ukiongea hapo utaambiwa wewe umepitwa na wakati umesikia wale vijana walivyokuwa wakisema muda ule..’akasema mwenzake.

‘Waliesemaje?’ akauliza

‘Wenyewe wameshaanza kutuita sisi wazeee ni wanga,…sisi wazee ni wachawi,… eti kwasababu ya macho yetu..macho yataacha kubadilika rangi na hali yenyewe ilivyo, hakuna chakula bora, tunishi kwa shida,..ndani hakuna taa, mnatumia kibatali..moshi metanda…ufukuto, macho yataacha kubadlika rangi kweli, hili hawalioni na usomi wao..ooh, jamani natamani nijiondokee, nikapumzike huko tusipopajua…’akasema mzee mwenzake.

‘Usije ukatamani kurudi, na ujue ukienda huko hakuna kurudi..unasikia mzee mwenzangu,.. ukienda huko hakuna kurudi, uliwahi kuona, au kusiki kuna mtu kaenda huko akarudi,kamweeh, ukifa ndio bye bye..sasa acha kauli zako hizo za kutamani uamauti ..uamuti hautamaniwi, siku ikifika imefika, mtoa roho hafanyi makosa…nikuambia kiu mzee mwenzangu, ilimradi unapumua, hata kama unapata taau lakini una nafasi ya kupumua, mshukuru mungu wako, ..’akasema

‘Kwkweli tunaongea tu..hapa nilipo tumbo linasokota kwa njaa, …mmh mzee mwenzangu, kufa hatufi ila cha moto tutakiona…’akasema mzee mwenzake.

‘Sasa kuhusu huo upepo…’akaanza kuongea mzee mwingine aliyekuwa kimia wakati wote…

Lakini kabala hajaongea akakatishwa pale alipoona mwenye nyumba akikatisha kuelekea mlango wa kuingia huko walipo hao maaskari wakifanya uchunguzi kwenye mwili wa huyo mama. Na mzee kama ada alitaka kumpa huyo mwenye nyumba mkono wa pole..

Na ndio kipindi kile upoepp umetulia, na watu wengi sasa wanahangaika kutaka kujua kinachoendelea huko ndani na mwenye nyumba naye kama wengine akawa anahangaika kupata nafasi ya kuangalia huko ndani , akawa kasimama mlangoni huku akiangalia kile kinachoendelea pale alipowekwa huyo mama, japokuwa kichwani alikuwa na mawazo mengi.

Mawazo yake yalizidi kuchanganywa hasa aliposiki hayo mazungumzo ya hao wazee wawili, kuwa upepo kama huo ni ishara ya onyo, au kuna jambo limefanyika lisilo la kawaida, sio jambo sahihi….akasema kimoyo moyo,

‘Huenda wamejaribu kumfunua..kuangalia uso wake…watabakia kushangaa kama nilivyoshangaa mimi na huenda yakawakuta yaliyowakuta haoo wengine waliojaribu kufanya hivyo..mmh hata simwambii mtu nilichokiona kwa huyo mama..’akabenua mdomo akiabsamu.

‘Hahaha, sio kwamba naogopa kufa,..kuwa nikisema nitakufa, …mmmh hapana..ila ile sura haielezeki, sijui ndio hayo mapanga, sijui..lakini hata hivyo, kuna jambo kwenye sura ya huyo mama, sio sura yake ya kawaida, mmm na yake macho..’akasema

‘Yale macho mmh yananikumbusha mbali, hata hivyo,sio yeye...hapana, sio yeye..’akawa anarudia rudi hayo maneno, huku akitikisa kichwa kukataa.

Na kwa namna nyingine huyo mwenye nyumba  alijawa na huzuni sio tu kamkosa mtu ambaye anahisi ana jambo, ana mswali mengi yanyohitaji majibu kutokwa kwake,.na pia ana hasira, ana chuki…ana kisasi…, lakini ni mtu ambaye alishaweza kuibadili hali ya maisha yao.

Maisha yake yalianza kubadilika pindi huyo mama alipohamia hapo kwake, kipato kikaongezeka, mahitaji ya ndani hayakuwa ni tatizo tena kwake, akaanza kukarabati nyumba yake, akaweza kukitengeneza vyema hicho chumba cha uwani na alishaanza kufyatua matofali kwa ajili ya kuongezea chumba kingine..

Huko kwa mkewe biashara ikapanuka, na wakawa na wasaidizi zaidi ya mmoja wa kusaidia kwenye biashara yao huko sokoni…oh, yote hiyo ni kutokana na baraka za huyo mama..sasa ndio huyo keshakufa…sasa..oh jamani…akajikuta machozi yakitaka kumtoka

‘Mhh, kama ni kufanana,..lakini hapana...sio yeye, haiwezekani,..sio yeye...kama ni yeye kwanini afe….kwanini afe , kwanini hakusubiria kunipa majibu ya maswali yangu…’akawa anongea mwenyewe, hakujua kuwa kaongea kwa sauti na yule aliyekuwa karibu yake akasema;

‘Mhh, huyo mama, kweli kila mtu alikuwa na maswali mengi ya kumuuliza…sasa wamemuua..mimi sijui wanadamu wengine wana mawazo gani…, sijui waliomuua sasa wamepata nini kwake, eti ni mwanga, eti ni mchawi, mtu mwenyewe kachanganyikiwa atamloga nani..’akasema huyo aliyekuwa jirani yake

‘We acha tu…aheri wasingelimuua…unajua kafa mikononi mwangu…, namuona hivi hivi..yaani inasikitisha sana, sijui kwanini walifanya hivyo,..hata hivyo, …wakati mwingine nawaza mbali..nawaza ingelikuwa mimi niifanye hiyo kazi..’akasema

‘Uifanye hiyo kazi, kazi gani…?’ akauliza mwenzake huku akimsogelea huyo mwenye nyumba kusikia kauli yake..lakini mwenye nyumba akawa anajisogeza mbali na huyo mtu akitafuta upenyo wa kupita, hakuna aliyemjali kuwa ni mwenye nyumba,..

‘Hivi kwanini hawaendelei  na akzi yao, ..nasiki awalikuwa wanataka kumfunua, nyie mnaoweza kuangalia huko ndani hebu tupeni taarifa…maana nilisikia sasa wanataka kuiona sura yake, mara kukatokea upepo mkali… si walitaka kuiona sura yake, hata mimi nina hamu ya kuiona, mbona wamesitisha hilo zoezi?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Hata naelewa…hawa askari wapo ‘slow’  sana.. si sijui ndio mambo ya kisasa maana kila hatua wanataka kuchukua picha..nahisi ni kwa ajili ya ushaidi mahakamani, siku hizi njia hizi za utandwazi zimerahisha mambo…, na kwa vile wameona kuwa huyo mama ana majeraha, basi wameshachkulia kuwa hiyo ni kesi ya mauji, kwahiyo wanataka kuwa waangalifu kila hatua..’akasema mwingine.

‘Mhh, nimesikia mjumbe akiwaonya kuwa huyo mama hatakiwi kufunuliwa hata kama hayupo duniani, ..mimi naona ni sawa, watu wakumuangalia ni watu wake wa karibu..sasa hao polisi wanataka nini kwa huyo mama?’ akauliza mtu mwingine.

‘Wansema huenda kuna majeraha usoni, huenda  wa wamemchinja na kukiunga kichwa vile ili kusionekane..lakini pia wanataka kuitambua sura yake, wapige pichana ikibid wamtoe kwenye vyomba vya habari kama kuna mtu wake aliyepotolewa na ndugu basi watamuona…’akasema mwingine.

‘Lakini kwa hali halisi, kama angelikuwa hai,angelikubali kufanyiwa hivyo…habu tuweni wakweli,kama mtu mwenyewe hakupenda sura yake ionekane akiwa hai kwanini sasa kafa wanang’ang’ania kutaka kumuona, wakimuona ndio watamrejesha duniani, na hata hao ndugu zao,..muda wote huo mbona hawakuhai kujitokeza,..hana ndugu huyu mama..mama nahisi ..sio mama wa kawaida…nyie mnalionaje hilo?’ akauliza mwenzake, na mara kukazuka vurumai,..watu waliokuwepo pale mlangoni wakageuka, kutaka kutoka nje..

‘Kuna nini tena huko ndani, mliambiwa hamuhusiki sasa manakimbia nini..?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Hata hatujui..mimi nimeshitukai tu namuona askari mmoja yupo chini, na mwenzake anataka kukimbia…’akasema na mwingine akadakia.

‘Ohh, kweli yule mama hatakiwi kufungulia, hata akiwa mfu …hutaamini yule askari aliyekuwa akimfunua kala mwereka,..kadondoka chini na mwenzake akageuka kukimbia..’akasema mtu mmoja aliyekuwa mlangoni akichungulia, na baada ya kusema hivyo, kila mtu akakimbilia pale mlangoni kutizama ndani, na wale waliokuwepo ndani ambao walikaidi amri ya askari kuwa wasiingie ndani lakini baadaye wakaingia, wakawa sasa wanataka kutoka nje, ikawa sasa ni mgongano pale mlangoni.

‘Tupisheni tupite…hili sasa ni balaa..’wakawa wanasema

‘Kwani kumetokea nini?’ wakauliza waliokuwepo nje, na baba mwenye nyumba ambaye pale aliposimama hakuweza kuone vyema, akawa anahangaika kuchungulia lakini hakuona kinachotokea zaidi ya askari mmoja kuwa yupo sakafuni, na mwenzake akiwa kasimama huku akiwa anaangalia pale alipolazwa huyo mama.

Mjumbe alikuwa ameshafika mlangoni, akiwa anataka kutoka nje, na watu wakambana kwa maswali

‘Mjumbe tuambie kumetoeka nini huko ndani mbona watu wanakimbia kutoka nje..?’ akaulizwa

‘Hapana niacheni,..mimi niliwaambia hawakutaka kuniskia, nasikia hata hata hao washukiwa…waliotenda hicho kitendo, hali zao ni mbaya…wanaweweseka ovyo…’akasema mjumbe

‘Ina maana unawafahamu hao wtu mjumbe..?’ akaulizwa

‘Hapana nimesikia watu wakisema..oh, jamani niacheni maana nina haja….nataka kwenda haja…nipisheni jamani, waliyoyataka wameyapata…nipisheni nitawakojolea..’akasema mjumbe huku akiharakisha kutoka nje, na alipopata upenyo, mbio akatokomea upande wa pili ambapo haonekani.

NB Kuna nini kimetokea, watu wanakimbia, askari wanadondoka, kulikoni


WAZO LA LEO: Tuweni na tabia ya kusamehe mauzi tunayotendewa, kwani kama binadamu walivyo na wingi wao, mauzi hayakosekani, kuna watu hawajui kauli nzuri, kuna watu wana tabia zisizo njema kwa majirani zao..lakini wapo miongoni mwetu, tutafanya nini, inabidi kuvumiliana, ..Hata hivyo kiuungwana tujifunze kukatazana kutenda maovu, ili kujenga jamii yenye amani. ..na zaidi tuelekezane kutenda yaliyo mema, ili tujenge upendo ulio sahihi. Huko ndio kufunzu kuliko na ukweli.

Ni mimi: emu-three

No comments :