Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, February 19, 2015

NANI KAMA MAMA-34


Wakati anahangaika akajikwaa..!

Mhh, hisia zilimuambia hu uliojikwaa nao ni mguu wa mtu, akainama kutizama, ni kweli ulikuwa mguu wa mtu, lakini kutokana na majivu ulikuwa hauonekani vyema,  alipohakikisha kuwa ni mguu wa mtu, akaona ili kumtoa vyema hapo alipo inabidi kuinua kitanda. …, akainua kile kitanda, na kukiangushia upande mwingine kukabkia wazi,..sasa akaweza kuuvuta ule mguu, na mtu akaonekana..ni yeye,…

Alikuwa ni yeye, ….lakini je yupo hai….?

Alitaka kuhakiki kuwa yupo hai akautumia ujuzi wa kuzaliwa, kwanza akashika mkono karibu na kiganja, akawa anasikilizia mapigo ya moyo,…hakuweza kupata mapigo ya moyo vyema..hakukata tamaa.

Akapiga mogiti na kuinamisha kichwa chake na kuweka masikio sehemu karibu na kifuani mwa yule mama, maana bado alikuwa kalala upande upande..,..bado akawa hana uhakika..

Sasa akataka kushika sehemu ya shingoni!

Sehemu ya shingoni hadi kichwani kumefunikwa,..na hali ile aliiona kuwa kama huyo mama bado yupo hai, itamfanya akose hewa, hilo aliliona lakini hakuataka kuharaisha, kumuondoa hizo nguo za juu, yeye alitaka kupata upengo wa vidole viwi tu ili aweze kuvieweka kwenye sehemu ambayo ataweza kuhisi mapigo ya moyo.

 Lakini kutokana na jinsi alivyovyaa, haikuwa rahisi, mama huyu alikuwa anahakikisha sehemu hizo haionekani, kichwa hadi mabegani, na katikati ya sgingi alikuwa amejifunga barabara…

‘Huyu mama amejifunga utafikiri alitaka kujinyonga..’akasema baba mwenye nyumba huku akihangaika kutafuta upenyo wa kuingiza vidole vyake. Lakini zile nguo zilivyo, hakuweza  kutumbukiza vidole vyake,  ikabidi ajaribu kusogeza zile nguo, akawa sasa kama anavuta kwa juu, na alipona hapati nafasi, akaona ni bora kuondoa zile za sehemu yote ya juu, hadi kichwani, lakini akasita moyo ulimwambia kuwa anafanya makosa.

‘Atanisamehe tu..’akasema akianza kuifanya ile kazi ya kumvua hiz nguo sehemu ya juu…’alaihis mikono yake ikimtetemeka, kama vile anahisi baridi, akasita kufanya hivyo, na akilini akawa anakumbuka onyo la watu kuwa kuna waliojaribu kumvua nguo zake za kichwani wakapatwa na madhara.

Akawa anasogeza zile nguo hadi akapata upenyo wa kutumbukiza vidole a kushika sehemu ya shingoni aliyokuwa akiitafuta…
Hapo akahisi mapigo ya moyo, lakini hakuwa na uhakika sana…Kwa hilo ili kuapta uhakika sasa akajiwa na hamasa nyingine alitaka kumfunua kabisa sehemu ya juu, abakie wazi ili amuonevyema huyo mama, sio tu kwa vile alitaka huyo mama apate hewa, lakini aione sura ya huyo mama ipoje…hamasa ikamjia…

‘Aaah, sioni ubaya, kwanza ni kwa ajili apate hewa…sioni ubaya…’akasema na kuanza kazi ya kutoa hizo nguo za juu, na...taratibu ikafungua ile iliyofungwa shingoni ambayo ilikuwa kizuizi cha kuivua hiyo nguo ya juu, alipomaliza hapo, sasa ikawa rahis kuvuta ile ya juu…taratibu akawa anaivua ile nguo,..., na kila hatua akawa anashangaa, ilikuwa sura ya ajabu!....

Moyo ukawa unamuenda mbio, wasiwasi, na mwili mzima ulikuwa ukimtetemeka, hadi uso wote unabakia wazi, ilikuwa kama mtu aayevuta kitu kigumu kwa kutumia nguvu sana,…hatimaye uso ukabakia wazi…

‘Khaaaaa….’akashika mdomo, na sijui kwanini, alihis kizunguzungu na tahamaki kadondoka na kukaa kitako, ..haaamini…

Akiwa pale chini, akapangusa macho yake, huku mwili ukimtetemeka, alishangaa ..anakumbuka kuna siku huyo mama alipokuwa pale nje kwakwe aliwahi kumuona kidogo tu sehemu ya uso..na kitu alichokiona kwanza yalikuwa macho…

‘Yale macho…’akakumbuka

Akili ikampeleka mblia sana,…macho….macho….hapana sio yeye…akawa anakataa akilini, akawa anapingana na kumbukumbu, akiwa bado amekaa kitako, na alihisi kitu, akajiinua kidogo kutizama, akaona asimame

Hata kule kusimama ilikuwa shida, alishisi mwili hauna nguvu..akawa anasema; ‘Ni yale yale waliyosema, huyu mama hatakiwi kutizimwa usoni..sasa kakiuka miiko.

Akajitutumua na kusimama,…taratibu akamsogelea yule mama, na kumuangalia tena, sasa badala ya kukuta uso ukiwa wazi, akaukuta umefunikwa!

‘Khaaaa, nani kamfunika tena, miujiza, kama …hajazindukana na kujifunika mwenyewe, basi nitaamini maneno ya watu kuwa mama huyu ni mama wa miujiza,..haiwezekani,…akamsogelea,..uso ulikuwa umefunikwa japokuwa haukuwa umefungwa kama mwanzoni.

‘Basi huyu mama kweli ni wa miujiza, kama nguo imejirudiaha yenyewe, na kumfunika, ina maana hatakiwi kutizimwa..oh, nisamehe, sikuwa na nia mbaya…’akasema na kuinama kumtizima, na akataka kuhakikisha kuwa kweli ile nguo imejifunika yenyewe, au mwenyewe yupo hai, kajifunika, akasogeza mkono na tarataibu akataka kumfunua tena, lakini ilikuwa ni kwa haraka sana, jinni smkono wa huyo mama ulivyoinuliwa na kushika ile sehamu ya nguo,  hakuamini…

Yule mama akawa kashikilia ile sehemu kuzuia nguo hiyo ya juu isitolewe, na kabla baba mwenye nyumba huyu hajafanya lolote sauti ya huyo mama ikasikika, akipiga ukelele

‘Msiniue, mimi sio mwanga, mimi sio mchawi… jamani…nimewakosea nini walimwengu…kwanini mnataka kuniua…..mimi namtaka mtotow angu tu……nataka mtoto wangu..msiniue msiniue….’ akaanza kupiga ukelele mara mbili, halafu akatulia kimia..

Hikupita muda, yule mama akatikisika mguuni, na akawa kama unajivuta mara mbili nay a tatu akawa kimia..ni kama vile mtu anakata roho..

‘Oh, amekufa…’alisema baba mwenye nyumba akiwa kaduwaa..


Tuendelee na kisa chetu…

***********

‘Hapana, usife…nataka kuwa na uhakika..nataka kukujua, ..nataka kujue kuwa ni kweli, ..’akawa anasema na kuinama huku akihangaika, akitafuta sehemu ya kushika, akitafuta, la kufanya, mikono ikawa inacheza cheza hewani, na akashituka anashikwa begani, alishituka na kusimama …akitaka kukimbia.

Akageuka,..kutizama nyuma huku mwili ukiwa unatetemeka ,..hakuona mtu, na anauhakika kuna mtu alimshika begani, akageuka kumtizama huyo mama, alimuona yupo kimia, kuashiria hana uhai tena, alitaka kuthibitisha hilo, lakini akawa anajiuliza ni nani kamshika bega,..

Akasogea hadi ukutani, akawa anachungulia kule walipo wenzake, wenzake walikuwa kwa nje, wakisubiria, na alipohakikisha hakuna mtu karibu, akageuka huku na kule..

‘Humu ndani kumeingiwa na mashetani…haiwezekani,..ina maana huyu mama..ni kweli..hapana..hapana..kwanza ..hapana..sio yeye….’akawa anawewezekan na mara ukuta wa nyumba ukadondoka, karibu sana na yule mama, jamaa aliruka juu kama kukwepa, na katika ile hali ya kuruka, akajikwaa, na kudondoka chini, akamdondokea huyo mama, akawa kama kama kamlalia..
Alsimama kwa haraka,..kama vile mtu alilalai kitu cha kutisha, kama mtu aliyelalia nyoka bila kujijua na alipogundua akawa anaruka kwa uwoga..

‘Khaaa. ….’akasema  na akainama kumtizama yule mama, sasa sehemu ya uso ilikuwa wazi, …macho yamefumba..lakini hata hivyo, nyuzi..na sehemu ile ya eneo la macho..akawa anaiona vyema…uso haukuwa wa kawaida…akajikuta sasa mwili unatetemeka, …akashika kichwa, akaona haitoshi akashika kiuno akaona haitoshi, akasogea hadi pale alipolala huyo mama.

‘Hata kama umekufa…sitakusamehe…’akajikuta anasema, akageuka,…akaangalia huku na kule, akaona chuma, akakishika kile chuma, akasogea pale alipo huyo mama

‘Niliahidi..na natimiza nnadhiri yangu…wewe hsutahili kuishi..unajua, unakumbuka, ..siamini,….’akawa sasa kainua kile chuma kutimiza nadhiri yake…

‘Mzee umemuona huyo mama….’sauti ilisikika nyuma yake, ilimfanya ashituke, na ule mshituka ukamfanya akirushe kile chuma mbali….akageuka, na alipoona huyu aliyemuita bado hajaingia ndani, akamsogelea huyo mama, kwa haraka akamfunika, na kumfunga vyema kama alivyokuwa mwanzo, hauku akisema;

‘Ipo siku..sitaki kuchukua hukumu hii ukiwa hujitambuei, hata kama umekufa…ipo siku….’akasema

*********

Baba mwenye nyumba alishikwa na butwaa, alikuwa kama kazibwa mdomo kusema, na mwili wote ulikuwa ukitetemeka, na hakujua kwanini atetemeke, hata tabia ya kuogopa kihivyo, hadi kutetemeka, akatikisa kichwa kama kuondoa hiyo hali, lakini moyoni alikuwa na jambo limemgusa, lakini lisingelimfanya kutetemeka,

Akajikutaakisema; ‘Oh, kweli, ama kweli, dunia ni duara…’ akahisi hayupo peke yake, akageuka na sasa alikutana na nyuso za wenzake wakiwa na wao wameshikiwa na uso wa butwa, kila mmoja akiwa anachungulia pale chini;

‘Huyu mama yupo hai..hajaungua.., ina maana hakuungua na moto, kweli huyo ni shetani, sio biandamu , aosife na huo moto wote, hapana, huyo sio binadamu…’ alikuwa kijana mmojawapo aliyeanza kuongea.

‘Lakini sizani kama yupo hai…’akasema mwenye nyumba na kugeuka kuhakikisha kama kweli huyo mama kamfunika vyema na moyoni akawa anasema;

‘Hata kama…hata kama nilitamani kukumalizia..lakini najua umeshakua, sikupenda ufe hivyo, … ila hustahili kuadhirika ..natii utashi wako, watu wasione ulivyo ..sijui kwanini walikufanyia huo unyama,..hiyo sio haki, yale yatakuwa ni mapanga..oh, hata hivyo sitaki kujihusisha na wewe, watajua wenyewe, …’akasema akigeuka kutaka kuondoka.

Watu wakawa wanajazana kuja kumuangalia huyo mama, na baba mwenye nyumba akawa anatembea kuondoka eneo hilo,sasa hakutaka hata kugeuka nyuma au kuongea na yeyote…na aliyefika hapo kwa muda huo kuangalia kinachoendelea alikuwa mjumbe.

‘Yupoje, anabebeka,amungueje…?’ akawa anauliza huku akitembea kuelekea kwenya tukio

‘Mjumbe huwezi amini, hajaungua…tulizani tutakuta kakamaa, lakini hajaungua ..kaungus kidogo tu..’mmoja akasema

‘Haiwezekani..moto wote huo…mmh, maajabu’akasema mjumbe na kufika kwenye tukio na kukuta watu wameinama wakimchungulia kila mtu akiongea lake, na alipohakikisha kuwa kweli hajaungua, akauliza

‘Lakini amekufa?’ akauliza

‘Ndio..baba mwenye nyumbaaksema hivyo…’akasema

‘Basi mbebeni… , mtoeni hapo….’akasema mjumbe akigeuka kuondoka hilo eneo, lakini mmoja wa waliokuwepo akasema;

‘Mjumbe unasema abebwe..umemuana jinsi alivyo…?’ akauliza

‘Kwani yupoje..kama kafa hata aweje haitasaidia kitu, mtu akifa ni kuzikwa tu, wewe unataak kusema nini..?’ akauliza.

‘Hapana mjumbe, kama kafa, haturuhusiwi kumtoa hapo alipo, kazi hiyo tutaifanya baada ya polis kufika kwenye tukio, na wakisema tumtoe wenyewe tutafanya hivy, la sivyo, hiyo ni kazi ya polisi wenyewe….’akasema jamaa mmoja.

‘Polisi watasaidia nini bwana,..mambo mengine ni kuwapa kazi polsi, kila jambo polis, hata lile ambal sisi kama kijiji tunaweza kulifanya, tusubiri mpaka polisi waje, mtu kafa kwa moto, tusubiri mpaka polisi wafike, kwanini, akianza kunuka hapa..’akasema mjumbe.

‘Hata kama kafa hawezi kunuka kwa siku moja….’akasema mtu mwingine.

‘Sasa kwanini tusubiri mpaka polisi waje.. nni kasema tusubiri polisi wakati tunajua kafa kwa moto…?’ akauliza mtu mwingine.

‘Huu moto sio wa kawaida, huu moto unaonekana ni hujuma..kwahiyo tuwaachie polisi wafanye uchunguzi.., na pia huyu mtu hatujui katokea wapi, tunazika, wenywe wakijikeza, tutawaambiaje…’akasema mzee mwingine.

‘Nani kasema huu moto ni hujuma, nyumba ngapi zinaungua kwa moto hapa kijijini, hatujawahi kuona polisi wakija, kwanini hii imekuwa ni tofauti, au kwa vile huyo mama ni mama wa ajabu..hebu acheni upuuzi, tufanye haraka tukamzike watu wasahau, wafanye shughuli nyingine, katangulia na sisi tutafuata…’kijana mmoja akasema.

‘Lakini mumemchunguza vyema huyo mama…mbona anaonekana kuwa na majeraha ya mapanga..’akasema mtu mmoja, na alipotamka hivyo mjumbe akaruka juu  kama kushituka, akasema;

‘Majereha ya mapanga,…hapana ..hawakutakiwa kufanya hivyo…’akasema mjumbe

‘Akina nani hao, inaonekana mjumbe unafahamu zaidi yetu..’akasema yue jamaa wa kwanza , akawa anamuangalia mjumbe kwa macho ya kutokumuamini. Wanasema jamaa huyo ni mpinzani mkubwa wa mjumbe na alitaka nafsi hiyo iwe yake, na alipoongea hivyo wengie waliona ni upinzani wao.

‘Nasema hivi, hata kama ni unyama hawakutakiwa kufanya hivyo, wamkate kate na mapanga, wamuchome moto, huo ni unyama uliokithiri…tatizo lako kila jambo unataka kunipinga, kama ndio huo ujumbe unatafuta kwa njia hiyo utashindwa..kwani sigeombei tena safari ijayo utachukua wewe hii nafasi…’akasema mjumbe.

‘Aaah mjumbe tatizo lenu nyie viongozi wa siasa, mkiambiwa ukweli, mwaona sijui tunataka kuwanyang’anya madaraka..sio hivyo mzee,…ni kukumbusha tu, na kama huamini hebu njoo uone mwenyewe kwa macho yako,..’akasema akimshika mjumbe mkono na kumvuta pale alipolala huyo mama.
Mjumbe akaonekana hataki kwenda, akasema;
‘Sikiliza..yote ni sawa, hakuna haja ya mimi kumuona,..ina kiukweli hao watu waliomfanyia hivi huyu mama sio binadamu wa kawaida…lakini nijuavyo mimi mpaka polisi wafike hapa, na hili joto, unafikiri hii maiti itakuwaje…’akasema

‘Haya mzee sisi tumekushauri hivyo….mengine utajua wewe mwenyewe..’yule jamaa akasema…maana siku hizi watu wambedilika wamekuwa wanyama, sijui wanafaidkika nini hapo, huyo mama kahujumiwa, …., naona walitaka kumkata kata huyu mama vipande...’akawa anaonngea huyo mtu akiwa hariziki na uamuzi wa mjumbe.

Mjumbe akasogea pale alipo huyo mama na kumuangalia kwa makini pale alipolala, akasema; ‘Mimi naona uamuziwa ngu ndio huo vijan wangu mtoeni hapa, kuna joto, ataharibika …mimi mwenyewe nitaongea na polisi, kama watauliza...’akasema na bijana wakafnay hivyo.

*************

Baba mwenye nyumba wakati huo alishafika eneo la nyumba yake anapoishi na familia yake, akageuka nyuma kuona kinachoendelea, na kwa muda huo watu walikuwa wamebeba mwili wa yule mama ukiletwa sehemu ya uwazi, akajikuta machozi yanamlengalenga..

Pamoja na yote..hakustahili kufa..kwanini amekufa..kwanini….’akawa anasema kimoyo moyo. Na mara hasia zikatanda moyoni, sijui kwa nini alihisi hasira...kwa muda huo huyo mama alikuwa keshafikishwa eneo alipokuwa kasimama yeye, waksiubiri yeye atasema nini, na alikuwa kaunikwa mwili mzima..Baba akamsogelea akawa kachuchumaa akiwa kama anamuombea au anawaza jambo.

‘Kama ni yeye hastahili kuishi...’akajkuta akisema

‘Ni heri afe, sitaki hata kumuona tena...’akasema na kusimama kutaka kuondoka.

‘Mzee, tuambie tufanye nini..kwanini unasema hutaki hata kumuona?’ akaulizwa na jamaa mmoja.

‘Huyu nilimuhiadhi mimi..lakini mimi sio jamaa yake..’akasema

‘Kiubinadamu kwa vile kafia kwako, msiba unatakiwa kuwa hapa kwako, hadi hapo jamaa zake watakapofika…’akasema mzee mmoja na wengi wakakubali kauli hiyo.

 Huruma, mapenzi, ubinadamu ukamjaa moyoni,…akikumbuka yaliyopita,  akajikuta anaanza kulia, akajaribu kujizuia lakini haikuwezekana, ikawa watu sasa wanamsihi,  na kumshika asijekuanguka,…lakini ghafla, akakumbuka kitu,na hapo hapo hasira zikamtanda, akageuka na kusimama,  hasira zikazidi kipimo, akakunja uso, kama vile anaona kitu,..akajitoa kwa wale watu waliokuwa wamemshika, akatembea hadi pale alipolazwa huyo mama, akasema;

‘Haya inueni, tumpeleke ndani..’akasema

Watu wakasaidiana, hapo tena kwa vile kila mtu anajua kabeba maiti, heshima na adabu ikatawala, na huyo mama akaingizwa ndani na kutafutiwa sehemu ya kuweka,, kitanda cha kamba kikatafutwa, na kuweka swa, na huyo mama akalazwa juu yake, ikabaki sasa kuulizana cha kufanya….!


***********
Wakati wapo ndani , nje kulikuwa na mazungumzo, mjumbe alikuwa akiongea na watu, wengi walitaka kujua kilichotokea, hasa wale waliowahi kufanyiwa wema na huyo mama.

‘Mjume sisi tunataka kujua ukweli…’watu wakaanza

‘Ukweli gani mnaohitajia nyie…huyo mama kafa kutokana na moto, …moto namjua ulivyo, na walioshuhudia ukiwaka, waliamini kabisa tutakuta majivu..au mwili ulioharibika kabisa..lakini kwa bahati..huyo mama haukuungua sana…lakini huenda kutokana moshi, kukosa hewa, ndio akapoteza uhai….ndio hivyo..’akasema mjumbe

‘Kama kafa kwa moto, sisi tunahoji kwanini ana majeraha ya mapanga, ..?’ watu wengine wakauliza..?’ wengine wakauliza.

‘Mimi hayo ya mpanga siyajui…’akasema mjumbe

‘Ina maana hukumchunguza?’ akaulizwa

‘Hiyo so kazi yangu…’akasema kwa mkato

‘Mjumbe hapo kuna hujuma, mjumbe kaijulishe polisi, ije ifanye uchunguzi.’wengine wakasema.

‘Hamna haja,...mimi naona apelekwe chumba cha maiti hospitalini, kwanza mtu mwenyewe hajuliani wapi alipotoka, huko watasubiria akipatikana mtu wao, basi wao watajua la kufanya…’akasema msaidizi wa mjumbe.

‘Mhh, hilo ni wazo zuri..lakini hospitali hawawezi kumpokea mtu kama huyo..ana majeraha…’akasema mtu mwingine.

‘Kuondoa yote hayo, tumzikeni, …’akasema mwingine na mjumba akatikisa kicchwa kukubaliana na hilo.

‘Mjumbe wewe ndiye kiongozi wetu, na wewe ndiye unayetakiwa kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake, huoni kama tukifanya hivyo, kukimbilia kumzika, unakiuka majukumu yako, kesho na kesho kutwa utakuja kubeba lawama kubwa..tuwaite polisi, waje, wao watajua cha kufanya na wewe utakuwa salama…’akasema jamaa mmoja.

‘Mbona mumeng’ang’ania polisi..hivi mnawajua polisi, wakifika hapa, tutaacha kazi zetu zote tutakuwa tukiwasikiliza wao…na huenda watu wakabebwa hapa kupelekwa rumande,..na kuingia rumande ni rahisi, lakini kutoka sio rahisi…si mnajua mambo ya huko…’akasema mjumbe

‘Lakini ni bora iwe hivyo,kwa ajili ya kukwepa lawama…hatujui huyu mama katokea wapi….’akasema mtu mwingine.

‘Sawa mimi ni kingozi wenu, na mara nyingi nakuwa mstari wa mbele kusikia matakwa yenu…kama mumeona hilo bora, ngoja niwatume vijana wangu, waifanye hiyo kazi, wao wanajua jinsi gani ya kuongea na hao watu, yatakwisha tu…unafikiri..’akasema na kutikisa kichwa kama kujiamini.

‘Haya yatakwisha…, ingelikuwa kunamauaji , mtu kauliwa,hapo ingekuwa habari nyingine, lakini huyu kafa na moto, hilo la kukatwa na mapanga,mimi sijui, mtu mwenyewe haeleweki, labda alitishia mvuta bangi mmoja wakapiagana, akakatwa mapanga, sasa hayo sio kazi yangu…’akasema mjumbe.

‘Unaona hapo mjumbe, umejileta mwenyewe,..umesemaje hapo, hapo sio kazi yako, sasa tuambie hiyo ni kazi ya nani?’ wakamuuliza

‘Ni kazi ya polisi…nisikilizenu veyma, kama kuna uhakika, au kama kuna malalamiko..au kama kuna ushahidi, kuwa huyo mtu kauwawa, basi haina budu kuwaita polisi…lakini kwa kesi hii, mnabuni tu, kupoteza muda, mliwahi kumchunguza kabla yupoje mtu mwenyewe haeleweki, labda kajikata mwenyewe…’akasema mjumbe

‘Mjumbe sisi tumemuona huyu mama, ana majeraha, tena majeraha makubwa, inaonyesha kabisa, kakatwa na mapanga, zile alama ni za mapanga, hata kama ni tahira vipi hawezi kujikata hivyo, usitufanye sisi hatuna macho au akili ya kufikiria….na hao hao waliomkata inawezekana ndio hao hao..waliochoma hiyo nyumba moto kupoteza ushahidi,…’akasema mtu mmoja

‘Sio nyumba..ni chumba, usikuze mambo….’akasema mjumbe

‘Kwahiyo sisi tumemuona, na walioona ni wengi, tumashahidi wa hilo…japokuwa hatukuona usoni kupoje, lakini inaonyesha wazi hao watu walitaka kumuua kabisa…na ili kuhakikisha kafa bila ushahidi wakaamua kuchoma nyumba au chumba hicho moto…watu wameona watalifikisha mbali…’akasema mwingine na wengi waliokuwepo wakasema.

‘Tumeonaaah…tuatasemaaaah…’ikawa kelele sasa kila mtu anaongea lake.

‘Sawa kwani kuna ugomvi hapaaah! Nyie si mnawatak polisi wafike…eeh, ngoja tuwatume vijana, wataongea nao, ..na mkitaka watafika, watachunguza, na ukweli mnaotaka utabainika au sio..mimi ni mjumbe wenu bwana, sifanyi kazi hi kwa kubabaisha, wapinzani wanaikodolea macho, wanahisi nafaidi..sina malipo yoyote hapa..ni kujitolea tu…’akasema

‘Kwanini uwatume vijana, piga simu jitambulishe kuwa wewe ni mjumbe , shina namba kadhaa, wenyewe watafika, kwanini mpaka utume watu waende huko, tunapoteza muda, ushahidi unapotea..hata hivyo kumuondoa pale tukio lilipotokea tayari tumeshaharibu ushahidi..’akasema huyo jamaa.

‘Msinifundishe kazi..siu hii hapa.. na namba zao ninazo, mnafikiri mimi sijui kazi, ..sasa hivi wanafika, hebu subiri..07....eeeh, ndio hii, hebu angalia hapa kumeandikwa kituo cha polisi..eeh, ndio hiyo…wacha nipige…’akasema msaidizi wake aliposema ndio namba yanyewe .

Mjumbe akapiga simu polisi, na kujitambulisha, na polisi wakauliza chanzo cha moto, na kama kuna majeruhi, akaambiwa kilichotokea, na polisi wakasema kuwa wamefanya makosa kumuondoa huyo muhanga wa huo moto kabla hawajafika, hata hivyo, wanakuja, na watu wasifike hilo eneo mpaka wao wafike.

Baada ya saa moja hivi,  polisi wakafika  na landrove, na kuanza kazi yao..na mojawapo akataka kujua huyo mhanga wa moto yupo wapi, akaambiwa kahifadhiwa ndani.

‘Kama kafa, kwanini mkamuondoa eneo hilo la tukio?’ akauliza

‘Joto la pale lingesabisha kuoza haraka…na pia moto haueleweki,..tukaona tumuhifadhi ndani’akasema mjumbe

‘Sasa huku ndani mlipoiweka hiyo maiti, si kuna joto pia, itasaidia nini kama hijapigwa sindano za kuzuia kuoza, basi mngemkimbiza hospitalini kwenye sehemu safi ya kuhifadhia maiti…hapo mumevuruga ushahidi..lakini tutaona la kufanya…’akasema huyo askari.

‘Ndio tulikuwa tunasubiria nyie mfike kwanza…kama mkiruhusu haina haja ya kupeleka huko muchwari, tutamzika tu…kwanza hana ndugu hapa…’akasema mjumbe na huyo askari akawa anasogelea mlango wa kuingia alipowekwa huyo mama, kabla hajafungua mlango , mara askari aliyekuwa nje, akaja na kusema;

‘Mkuu tumegundua kitu, kama inawezekaan uje kwanza, ..’akasema

‘Mumegundua nini,….maana nataka nimalizane na huku ndani kwanza, nyie chukueni yale yaliyo muhimu ninakuja, kwani ni kitu gani muhimu mumegundua,..?’ akuliza akiwa kashikilia kitasa cha mlango wa kuingilia chumba alipohifadhiwa huyo mama.

‘Mkuu huo moto sio wa bahati mbaya…’akasema huyo askari wake na mjumbe akaonekana akikunja uso kwa hasira, aliwewesa maneno kama;

‘Hayo ndio nilikuwa sitaki….aaah, hawa wapinzani bwana…’aliyasema kwa chini chini akimnong’oneza msaidizi wake aliyekuwa karibu yake, mara ningi hataki huyo msaidizi wake awe mbali na yeye..akidai macho yanamsumbua, na huyo msaidizi wake atakuwa akimsaidia kusoma, au kuandika kwa haraka.

Yule askari akageuka kumuangalia mjumbe na kusema;

‘Yah, nilishahisi hivyo, unajua wanasema kuku mgeni hakosi kamba mguuni, …sasa mjumbe, maana wewe umesema umebeba jukumu lote hili…, ndio wewe umeamua huo mwili utolewe pale, kwasababu ulizosema….nataka maelezo yako kwa kina….’akasema akiwa kaachia kile kitasa akimkabidli mjumbe.

‘Lakini mimi sijui lolote kuhusu chanzo cha huo moto, mimi najua ni moto wa kawaida tu, na sio mara ya kwanza kutokea moto kama huo…si unajua nyumba nyingi za  huku kwetu zimeezekwa kwa majani, hilo sio geni kwako na umekuwa ukifika huku mara kwa mara..tunashukuru kwa hilo..’akawa anajitetea mjumbe.

‘Lakini hiyo nyumba, ..eeh kilikuwa ni chumba, au sio?,.. hakikuwa kimezeekwa kwa majani…tumeona mabati yaliyoteketea,…au sio?’akauliza huyo polisi mchunguzi akimuangalia mjumbe halafu mkuu wake wa kazi.

‘Ndio..iliezekwa kwa mabati, wengi sasa wanajitahidi kufanya hivyo,… lakini mimi nilikuwa nazungumzia ajali za moto zilizopita, na nimejitahidi kutoa taarifa kila kukitokea ajali, kwani ni moja ya majukumu yangu..kiukweli kuna matukio mengi ya moto hapa kijijini kwetu , na hiyo inasababishwa…eeh,… na ya kuwa nyuma nyingi hapa kijijini zimeezekwa kwa majani..’akasema mjumbe akionyesha kwa mikono kivitendo.

Mkuu akainua kichwa kuangalia juu ya dari, na kutabasamu, akasema;

‘Ni kweli tumepoeka taarifa nyingi kutoka kwenu, na zote mlisema ni moto wa kawaida, lakini kuna dalili nyingine zinzonyesha kuwa kuna jambo…huu moto na mazingira yake huoni kuwa kuna dalili za hujuma..wewe kama mjumbe tuambie ukweli kabla hatujaendelea na uchunguzi wetu, ..?’ akamuuliza mjumbe, na mjumbe akageuza kichwa huku na kule, akatabasamu kuonyesha kuwa hana wasiwasi.

‘Sina uhakika na hilo….sijafanya uchunguzi , mimi nilichoona ni jinsi gani ya kuhakikisha huo mwili unakuwa mahali salama,…maana mimi ni mjumbe wa watu… maana pale kuna joto, na moto unaweza kuendelea kuwaka,..huwezi jua kuna upepo mkali kipindi hiki, mwili ungeungua tena na sio ubinadamu hata kama kafa…..mengine mtajua wenyewe ndio maana nikaona niwapigie nyie simu ili mje mfanye kazi yenu…’akasema mjumbe.

‘Sawa mjumbe, ngoja tufanye kazi yetu..askari wa kuchunguza, endelea na kazi yako, nitakuja huko ..ngoja tufanye utaratibu wa huku kwanza ili hii maiti iwahishwe muchwari,..wale wa kikosi cha upande wa kuchukua picha anzeni kazi, …maana  hii sasa ni kesi ya mauaji…’ akasema huyo askari kiongozi wao akifungua mlango na kuingia sehemu hiyo alipowekwa huyo mama.

Mjumbe aliposikia kuwa hii sasa ni kesi ya mauaji, akamuangalai msaidizi wake na kusema;

‘Ndio niliyoyakataa haya hata wewe uliunga mkono kuwa tuwaite hawa polisi..sasa ni usumbufu, unasikia ni kesi ya mauji, sasa wewe ni msomi, nataka upambane nao, mimi nahisi kama haja…’akasema akigeuka kama kutaka kuondoka.

 ‘Mjumbe , wakati vijana wangu wanafanya kazi yao ya kuchukua picha…, hebu niambieni kulitokeaje…’yule askari kiongozi akasema na mjumbe ambaye alishageuka kuondoka akasimama na kucheka kujibaragua.

‘Nitawahoji wahusika wengine  mmoja mmoja, lakini wewe kama mtendaji unaweza kunirahisishia kazi, hebu niambie kulivyotokea..?’ akauliza huyo askari, sasa akiwa kamkazia macho mjumbe.

Mjumbe akaelezea ilivyokuwa, kama alivyoambiwa na mwenye nyumba na majirani, na akamalizia kusema;

‘Zaidi san asana muulize mwenye nyumba…’akamalizia hivyo akigeuka kumuangalia msaidizi wake ambaye alitikisa kichwa kukubaliana naye

‘Nitaongea na mwenye nyumba baadaye, kwanza nataka kumuona huyo maiti alivyo…hata hivyo mjumbe hayo maelezo yako yana walakini…’akasema

‘Walakini..!?...’akasema kama kushituka akamuangalia msaidizi wake, halafu akasema;

‘Mimi nimekuelezea jinsi nilivyosikia..sasa kama kuna walakini kwenye maelezo yangu, utajua mwenyewe jinsi gani ya kuyaweka sawa…unielewe vyema, nimeambiwa…sasa swala la kuambiwa sio sawa na swala la kuona…mnielewe hapo,..na nikwa msisistizo nimewashauri, kama mtendaji wa kijiji, muongee na mmoja wa wakazi wangu ambaye ni mwenye nyumba..kuna walakini gani hapo…’akasema na yule askari akatabasamu, na kusema;

‘Ndio nataka niyaweke sawa kama ifuatavyo, wewe umesema walikuambia kwanza walisikia kelele, kama kilio…baadaye wakahisi moshi,…ndio wakatoka nje na kuona moto..huoni hiyo pekee yake inaonyesha kuwa kuna kitu kilitokea kabla ya moto, kelele, kilio, kilikuwa cha nini….?’ Akaulizwa mjumbe.

‘Kwani moto ukitokea mtu atakaa kimia, si lazima atapiga kelele…mimi nahisi alipoona kuna moto akapiga kelele ya kuomba msaada…kwanza unamfahamu mtu mwenyewe,  ni kama kachanganyikiwa, huenda alikuwa akichezea kibiriti,… akaungua mkono, akapiga ukelele, akarusha njiti , na njiti ikashika nguo, au kitu chochote cha kuanzisha moto....’akasema mjumbe akicheka kimzaha.

‘Unasema huyo eeh, mama, ok, ….mhanga wa moto ana matatizo ya akili, ay una maana gani kusema kachanganyikiwa..?’ akaulizwa

‘Hivi ukimuona alivyo mwenyewe utaaini maneno yangu ….kazi yake siku nzima na kupita barabarani akiimba na watoto wadogo, huyo atakuwa na akili kweli…japokuwa wengine wanasema ni mwanga,..unajua tena watu wa huku kijijini, wanamini sana mambo ya uchawi…sasa sijui kama kweli ni mchawi au hana akili nzuri, lakini kwa jinsi alivyo haeleweki eleweki…’akasema mjumbe akionyeshea kwa ishara kichwani kuwa huyo mama kachanganyikiwa.

‘Kwahiyo unahisi kutokana na kuchanganyikiwa huko anaweza akawa kasaabisha huo moto, au vinginevyo, kutokana na shutuma za kuwa huyo mama ni mchawi watu wanaweza wakachoma moto kumuangamiza?’ akaulizwa

‘Hilo sina uhakika nalo..nyie mtachunguza wenyewe, lakini nilichoona mimi ni kuwa huyo mama atakuwa na mapungufu kichwani..sasa huenda, akawa ndio chanzo cha moto, huenda..hayo ya watu wengine, si zani…sijui..kiukweli sina uhakika..’akasema mjumbe sasa akiwa katulia kama anawaza jambo.

‘Umesema huyo mama hamjui alipotokea sawa, na nilipowahoji wengine huko nje, mara wanasema alitokea mbinguni…hahaha, nyie watu kuna nini hapa kijijini, nahisi kuna kitu mnaficha hapa..’ yule askari akasema akiangalia watu baadh walioingia kuangalai kinachoendelea.

‘Eti mjumbe…’akasema na mjumbe akainu akichwa kumuangalia huyo askari huku kakunja uso kuonyesha yupo kazini.

‘Wewe kama mtendaji…’akasema huyo askari

‘Naamu, ndio kazi yangu…’akasema mjumbe.

‘Sasa kama ndio kazi yako, atakujaje mtu kwenye eneo lako bila kujua wapi alipotokea..na mnasema kafika hapa kijijini  muda sasa, hukufanya uchunguzi kujua ukweli, kama hana akili sawasawa, au katokea wapi..hiyo ni kazi yako mjumbe au sio..?’ akaulizwa.

‘Wanakuja wageni wengi…na jinsi ilivyo siwezi kujua kwa haraka huyu katokea wapi, alikuja lini,..hivi mimi nalipwa…niacha kazi zangu nianze kuzungukia majumba ya watu....’akasema mjumbe akigeuka kuwaanglai watu walioingia .

‘Lakini kwa huyu mama nilifanya tafiti za macho, na wenzangu wataniunga mkono,   nikamuona humu kwenye kichwa kuna mapungufu…hata hivyo sikuweza kujua katokea wapi..hilo siwezi kukudanganya, hakuna anayejua, wangeniambia watu wangu tunashirikina nao vyema, wangeniambia…, na kwa vile nilimuona kama kachanganikiwa basi nilichohakikisha ni kuona hafanyi uharibifu au kuumiza watu..hakuwa na tabia hiyo, angeleta vurugu aaah, sisi tuna mgambo wa kijiji, angedhibitiwa na kupelekwa kuna husika …’akasema mjumbe.

‘Sawa nitaongea na wewe baadaye ngoja niuone huo  mwili kwanza….’akasema akiwaashiria vijana wake, wampe vitendea kazi ..

‘Haya kama mnataka kujipa kazi ya kumchunguza zaidi hilo ni jukumu lenu, lakini huo ndio ukweli..’akasema mjumbe na yule polisi akamtupia jicho mjumbe kama kutaka kumuuliza kitu lakini akagairi, akageuka kuangalia mbele, akisubiri mjumbe atangulie.

Mjumbe aliyekuwa mbele akasimama, kumpisha huyo askari apite mbele, mjumbe alionekana kusita kusogelea pale alipolazwa huyo mama, na polisi akageuka kumuangalia mwenzake aliyekuwa naye ambaye alishavalia kinga za mkononi, akamuashir kumuashiria amfunue huyo mama, na yule polisi mwingine akafanya hivyo, na kuna mwingine akawa anapiga picha…na ile shuka ya juu ilipotolewa, polisi huyo kiongozi akauliza

‘Mbona amefungwa usoni kihivi, kaachia sehemu ya macho tu…kwanini…?’ akauliza

‘Ndivyo alivyokuwa hivyo tangu aje…tangia aonekane kwenye eneo letu hili, hakuna anayemfahamu sura yake..ndio maana nakuambia akili zake sio sawa…’akasema mjumbe

Askari yule wa awali, akavuta nguo uapnde wa chini, kutoka miguuni…akasita alipoona damu na majeraha, na yule askari kiongozi, akasogea kuangalia zile damu na majeraha…picha zikapigwa

‘Na mbona ana majeraha, ..haya sio majeraha ya mapanga, hebu funuo vyema,…ooh, this is a marder case….’akasema akitikisa kichwa, halafu akasema

‘Hebu funua na huko mkononi…hata huku mkononi pia…yaonekana aliumizwa na mapanga..japokuwa sehemu nyingine..damu zimeganda..na ni majeraha makubwa, na hajaungua sana, sababu ya kifo haiwezi kuungua, …’akasema akizidi kuchunguza

‘Mjumbe, huyu mama kakatwa katwa na mapanga, mjumbe hebu  sogea huku,..wewe kwanza tutakushika kwa mujibu wa sheria…unaona huyu mama, kakatwa katwa na mapanga,…haya ni mauji, wewe umesema kafa kw akuungua moto,…’akasema sasa akijiweka sawa, na mjumbe akajifanya kama ndio kwanza anayaona hayo majeraha.

‘Mhh..kweli, hayo ni mpanga…lakini kufa kwa moto sio lazima uungue, kuna kukosa hewa…na eeh, mi-mi-mi, sikujua kakatwa na mapanga…hiyo sasa ni kzi yenu anyeni uchunguzi tugundue ni nani kafanya hivyo, au sio..ndio maana nikawaita..sikutaka kupekenyue-pekenyua , ningevuruga ushahidi, unaona hapo…’akasema mjumbe.

‘Ina maana hukuona haya majeraha kabla hamjambeba kumuingiz ahuku ndani?’ akaulizwa

‘Mimi sikuwa na haja ya kufanya hivyo,…sikuwamchunguza,… nilijua nyie mtakuja mtamchunguza na mtaona chanzo cha kifo chake..zaidi mtu kama mimi ningeema kafa kwasababu ya moto..’akasema mjumbe.

‘Umefanya makosa kukimbilia kusema aletwe huku, na kwa  kauli yako umesema aharakishwe kuzikwa, mtu mnaona kakatwa na mapanga mnakimbili kumzika huoni kama kun jambo hapo linatakiwa kufichwa...’akasema akizidi kumchunguza huyo mama, na picha zikazidi kuchukuliwa.

‘Mimi nimekuambia sijamchunguza vyema huyo marehemu…, hiyo ni kazi yenu, mimi nilichofanya ni kuhakikisha maiti hiyo ipo salama, na ndio nikawaita,..na muelewe kabisa mimi sio mtaalamu wa kuchunguza maiti, sijui mnanielewa….’akajitetea mjumbe.

‘Sasa sitaki watu wengi humu ndani achieni kikosi chetu cha polisi kifanye kazi yake..ila mjumbe usiwe mbali,..nataka maelezo yako, na wewe ndiye uliyetoa amri ya maiti hii kuletwa huku, sawa si sawa…sasa kwanza, ngoja..’akasema huyo askari akiandika maelezo yake kwenye kijitabu kidogo.

‘Watu wa uchunguzi fanyeni kazi yenu, ila kwanza nataka kuiona sura ya huyu mtu…kwanini wamefunga hivi, wasije wakawa wamemkata kichwa…hebu mfungue tuone kichwa na sura yake…’akasema huyo askari kiongozi wao.

‘Hajafungwa na mtu huyo…ndivyo alivyokuwa toka awali..ndio maana nawaambia kachanganyikiwa huyo..mnapoteza muda wenu bure…’akasema mjumbe

‘Hebu mfunue kabisa eneo la kichwani, kuna shida kufunua hapo,…ooh, kwanini kajifunga hivyo, ok, mjumbe hatupoezi muda hapa, ni kazi yetu kufanya uchunguzi kujua ukweli, hatuangalii huyo mtu yupoje, hata kama kachanganyikiwa lakini ana haki ya kuishi….’akasema huyo askari na yeye akisaidia kufungua ile nguo iliyofungwa shingoni.

Yule polisi akawa anamfungua uso yule mama, na akawa sasa anataka kuvuta ile sehemu ya juu, iliyomfunika yule mama kichwani,.. ili uso wa huyo mama uonekane…mara kwa nje, kulitokea upepo mkali..dirisha lililokuwa nusu wazi likafungua lote, na upepo wa nje, ukarusha vumbi la nje, na kwa vile kulikuwa na mavumbi ya mabaki ya kuungua kwa nyumba, vumbi lilikuwa kali sana, na kuwafanya watu pale kuhangaika kuziba uso, na wengine kuanza kukohoa

Hata yule askari aliyekuwa akimfunua huyo mama akajikuta anaacha ile kazi na kuanza kujifuta vumbi usoni, na machoni, na askari mkuu wa msafara naye akawa anahangaika kivyake.

‘Huo upepo umetoka wapi…mmmh, hebu funga hilo dirisha,…’akasema

‘Unapita tu huo..tutakuwa hatuoni vyema tukifunga dirisha..’akasema huyo aliyekuwa akimfunua huyo mama

‘Haya endelea…’akasema mkuu wao.

`Koho koho…koho…’ ilikuwa kikohozi..kikohozi kilichomfanya polisi kuachia ile nguo na kurudi hatua moja nyuma,…akagongana na mkuu wake, aliyekuwa kasimama nyuma yake, wakajikuta wanataka kudondokeana,….wote wakabakia midomo wazi….

NB: Ni nini kimetokea

WAZO LA LEO: Katika jamii kuna hali tofauti za kiimani, na itikadi mbali mbali, nakila mtu ana imani yake moyoni, na huenda kutofautiana huko kwa imani kukawa ni adha au kukwazika kwa huyu au yule kutegemeana na imani hizo. Kihekima, ni muhimu kila mtu akajali imani za wenzake hata kama anaona hizo imani kwake hazifai au hazina maana, na hata kama kuna tokea majadilioano ya kujua imani za huyu au yule basi hayo majadiliano yaendeshwe ki hekima. Kuwe na kuvumiliana, na kusiwe na kukejeliana kwa kashifa zilizovuka mpaka.

Viongozi mna jukukumu kubwa..kiongozi anaweza akawa na imani yake , lakini katika utendaji hatakiwi kuonyesha hisia za imani yake, kwani anaweza asijue kabisa imani za wenzake zipoje, na kwanini wanafanya hivyo,..muhimu ni kujua tu kuwa anaongoza watu wenye imani tofauti na wenye imani hizo wana haki  ya kutekeleza imani zao, kwa mujibu wa maandiko yao.


 Sasa hivi wajanja wamegundua kuwa kwenye imani za dini ni rahisi kutumbukiza ajenda zao, wakiwa na malengo na njama zao… hili halikuanza leo..ubeberu na ukoloni ulifanya hivyo hivyo wakitafuta maliasili... Yaliyokuwepo yatatatokea, hata kama ni kwa mbinu nyingine, tuweni makini,..tuzilinde maliasili zetu kwa vizazi vyetu vijavyo, na muhimu ni kujua sote ni ndugu, taifa ni letu sote, hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine na amani na haki, ndiyo itakayotufanya tuishi kwa furaha na kuweza kueleta maendeleo.
Ni mimi: emu-three

No comments :