Kukasikika kilio!....kilio cha nani, kilio
kimetokea wapi....?
Kila mtu akawa anajiuliza hicho kilio ni cha
nani na kimetokea wapi, hata kwenye nyumba ambapo kunasadikiwa ndipo hicho kilio
kimetokea, na wakati kilio hicho kinatokea, wakazi wake walikuwa ndani ya
usingizi mnzito,...
Japokuwa walishituka, lakini hawakuwa na
uhakika kuwa kilio hicho kimetokea hapo kwao, au kimetokea kwenye nyumba nyingine ya jirani.
Wakazi
wa nyumba hiyo ambao ndio wamiliki wa nyumba hiyo, walipozindukana kutokana
kwenye usingizi, na kuanza kuulizana...
‘Umesikia..?’ mmoja akauliza
‘Nahisi kuna kilio..tena kama kilio cha
hatari vile,.....’akasema mwingine
‘Hata mimi nimesikia...lakini nilihisi
kama naota, kiukweli hata sijui kimetokea wapi?’ akauliza mwenzake
‘Hata sina uhakika, leo nilikuwa na
usingizi mnzito kweli haijawahi kuto;kea hivi...’akasema mwenzake.
‘Oh, mtoto, ..hebu muangalia mtoto, ...’akasema
mwenzake
‘Mtoto kalala..jana, mama wa baraka alimpa
baraka zake, basi mtoto kalala utafikiri hataki kuamuka...sio yeye aliyelia,
kilio kimetokea huko nje...’akasema
‘Mimi, sioni kama kuna tatizo....kama ingeuwa
ni tatizo, kilio kingesikika tena...’akasema baba mwenye nyumba. Basi wakaona
waendelee kulala lakini kabla hawajaanza kuuita usingizi ulipotea, mara mama
mwenye nyumba akasema;
‘Nahisi kama hewa ni nzito....’akasema
‘Hewa nzito..na harufu isiyo ya kawaida,
kama ya moto...’akasema mwenzake.
‘Mimi nasikia kama harufu ya moshi…husikii,
...?’akasema mama mwenye nyumba akiuliza.
‘Sijui nani kachoma mataka taka usiku
huu…’akasema baba mwenye nyumba.
‘Hiyo sio haraufu ya mataka taka….nahisi
kuna moto..mume wangu, kuna moto nje..amka haraka...’akasema mke mtu, na mume mtu
aliposikia moto, akakurupuka na kukaa kitandani, akajaribu kuchunguza kwa hisia
za pua na yeye akahisi hivyo.
Wote wakaamuka na kuanza kutoka nje, hapo
hakuna aliyejali kavaa nini, mbio, hadi nje, kuona kuna nini, walipotoka nje tu,
kutaka kuelekea sehemu ya uwani ambapo kuna chumba hicho, wakarudishwa na moto,!
‘Moto…’mfanyakazi wa ndani aliekuwa wa
kwanza, akarudi mbio, alikuwa keshatangulia nje akikimbilia kumuamusha mama wa
mkono wa baraka, kumbe huko anapokwenda ndipo moto ulipotokea.
‘Nyie tokeni nje haraka, mchukue mtoto,
kaeni mbali kabisa na mtoto..na mke wangu ita majirani…..’ilikuwa amri ya baba
mwenye nyumba, mtoto alishaanza kulia yeye hakujali tena kulia kwa mtoto
akaelekea sehemu huko kwenye chumba cha uwani kupambana na moto.
Alipofika na kuona jinsi moto ulivyo
akajua ni hasara na huenda mama aliyekuwa akiishi humo kama hakuwahi kutoka
basi atakuwa kateketea na huo moto, akageuka huku na kule kutafuta njia ya
kufanya, na akaliona pipa la maji, lilikuwa limejaa maji, na lilikuwa juu ya
chetezo kilichotengenezwa kwa mbao,..
Akalisogelea, na kuanza kulisukuma, huku
akiweka mawe kwa chini ili liiname kuelekea kwenye huo moto, akajitutumua kw
nguvu zote, na kweli likadondoka na maji ya ruka kupamana na huo moto,..sehemu
ya chini ikazimwa na hayo maji..juu mto ulikuwa ukiruka na kuwaka kwa kazi..paa
la nyumba lilikuwa limeshadondoka.
‘Mama wa baraka, yupo wapi...?’ akauliza
mfanyakazi, na hakuna aliyempa jibu, kila mtu alikuwa akiharakisha kutoka nje.
Na mama wa nyumba akaanza kupiga ukelele wa kuomba msaada,na majirani amboa
walishahisi hiyo hali walishaa kujitokeza, na kusikia kelee hizo wakaja kwa
iwngi utafikiri walikuwa sehemu wakisubiria.
‘Kwa hivi sasa cha muhimu ni kuuzima huo
moto, sizani kama kuna uhai kwenye hilo eneo tena, yule mama alikuwa analala
humo?’ akauliza mjumbe, wakati huo watu wanaendelea kuuzima moto.
‘Ndio…’akasema baba mwenye nyumba.
‘Mhh, kama yupo huko ndani,...na huo moto
sijui kama atakuwa hai...’wakasema majirani waliokwisha kufika.
‘Moto..moto….saidia kuzima
moto..moto…’.ikawa sasa ni ujirani mwema kila mmoja anakimbilia ndoo na maji,
kila mbinu za kuuzima huo moto zikafanyika…..’
Tuendelee na kisa chetu..
***********
Moto huo ulikuwa ukiwaka sehemu ile aliyokuwa akiishi huyo mama ambaye
watu sasa walikuwa wakimuita mama wa mkono wa baraka na ulikuwa moto mkubwa
uliozunguka eneo lote la chumba, utashangaa jinsi ilivyo, maana haukuwa
unakwenda kwingine zaidi ya kuzunguka eneo hilo la chumba...watu wakahangaika
kuuzima kila mmoja kwa mbinu zake, kila aliyetoka kwake akawa kafika na ndoo ya
maji, michanga, matawi ya miti...ulikuwa moto mkali kweli..
‘Jamani kimetokea nini, na huyu mama anayelala hapa yupo wapi..’
ikawa watu wanaulizana huku wakiendelea kuzima moto.
‘Naona hilo jibu kwasasa ni gumu kulipata muhimu ni moto uzimike,
na huku hakuna cha gari la zima moto, ndio maisha yetu ya kijijini, kukitokea
moto mjue mumeangamia…..’akasema mwenzake akimwagia maji kwenye moto
‘Mimi nahisi ni madawa ya
huo mama yamelipuka…’ wabaya wa huyu mama wakaanza visa.
‘Kwani huyu mama alikuwa na madawa, mimi sikuwahi kumuona akitumia
madawa, alikuwa anaombea tu, n asana sana alikuwa akitumia maji ....huo ni
moto, na inaonekana moto huu umezunguka sehemu yote ya chumba, huu sio moto wa
kutoka ndani...ni moto wa kupangwa huu...’watu wengine wakasema.
‘Hayo ni ya kwako bwana kama ni wa kupangwa basi ni wewe
umauwasha, umaejuaje kuwa ni moto wa kupangwa...’akasema mwingine ambaye
hakuonekana akihangaika sana.
Baadaye moto ukafanikiwa kuzimwa, lakini kwa asilimia kubwa sehemu
kubwa ya chumba hicho iliteketea kabisa, na kama ni kujenga hichoo chumba inabidi
kujenga upya, na hakukuonekana kusalimika kwa vitu, vitu vyote vlivyokuwepo
humo ndani viliungua vyote na huo moto.
‘Mhh, hapa hakuna uhai wa mtu...’akasema mmojawapo.
‘Lakini yeye si mama wa kutoka mbinguni, huenda amepaa, na kuucha
moto ukiwaka..’akasema mwingine kwa mzaha.
‘Mbele ya moto, hata uwe nani kama umo kati yake unageuka kuwa
mafuta ya kuuwasha zaidi….mmh, masikini mama wa watu, hata sura hatumfahamu…’wakawa
wengine wakiongea kwa mzaha, wakijidai kumsikitikia
‘Kama alikuwa mwanga hio ndio adhabu yake..’kijana mmoja alisema,
na watu wakamuangalia kwa mashaka, alipooa hivyo akajibaragua, na kusema;
‘Nilisikia watu wakisema hivyo kuwa mkono wake ni mkono wa mtoto
mchanga anautumua kuwangia watu…ndio maana nasema kama ni hivyo, naona zambi
zake zimemuandama..’akasema
‘Ni nani alithibitisha hilo kuwa mkono wake ni mkono wa mtoto
mchanga, huo ni ushirikina wa dhana, na kama kun awatu wamefanya hivyo
wakidhania hivyo, basi wao ndio wachawi,…maana wameua mtu asiye na hatia…’akasema
mzee mmoja.
‘Na wewe mzee ndio nyie,…’akasema kijana mwingine akageuka kumnong’onezea
mwenzake;
‘Ndio hao hao, unamuona macho yake,…bado zamu yake, hawa lazima
tuwamalize…’
Wakati kundi hilo
likiongea, kundi kubwa lililokuwa mbele likihangaika kuuzim huo moto, likawa
sasa linamalizia malizia, na mmoja wao akasema;
‘Hebu angalia pale kwenye mlango, naona kama mlango ulidondokea
kwa ndani, na pale moto haujazimika vyema...mwagia maji pale…’akasema mmojawapo.
‘Pale hapaingiliki kwa sasa..inabidi tusubiri mpaka kupoe
kwanza...maana lile paa lililodondokea pale ni la moto…ukishika bati lake ngozi inabakia
kwenye bati…’akasema.
Kwa wakati huo baba mwenye nyumba alikuwa keshasogea sehemu ya eneo
hilo, akihangaika huku na kule, kwani hasara ilishamchanganya kichwa hakujali
maonyo ya watu kuwa moo bado haujazimika ukiingia hpo unaweza ukaungua viabaya
sana,…yeye hakutaka kusubiria kupoe, yeye akasogea sehemu ile ya mlango,
uliokuwa bado unafuka moshi.
Alipoufikia huo mlango
akausukuma kwa mguu, ule mlango ukadondoka kwa ndani, …na paa lililokuwa
limedondokea pale likazidi kuporomoka chini, ukuta ulishadndoak sehemu ya hapo mlangoni..ulionekana hauna
nguvu..akazama ndani.
‘Wewe unataka kueleta balaa, utaungua huko, hapo moto bado upo
chini kwa chini..usijadanganye ndugu….’watu walisema, walikuwa hawajui kuwa
mwenye nyumba alipomwaga yale maji ya kwenye pipa, moto wa chini ulikuwa
umezimika, na hiyo ilimsaidia baba mwenye nyumba kukanyaga bila kuungua.
Baba mwenye nyumba akasogea hadi sehemu ambayo ana uhakika ndipo
kitanda kilikuwepo, alitaka kuhakikisha mwenyewe kama huyo mama kateketea na
huo moto au bado yupo salama. Akawa anainua sehemu ya mabati ya paa la nyumba,
na kuondoa mabaki mabaki ili kupata upenyo, akaweza sasa kuingia ndani. Joto la
moto na moto wenyewe bado ulikuwepo, hakujali..
Alishangaa sana, kwani yeye katika hali ya kawaida, anaogopa sana
moto lakini alishangaa kupata uajsiri huo, na kuweza kuuingilia, kuna kitu
kilikuwa kikimvuta kufanya hivyo..ulikuwa sio utashi wake,..na akili ilikuwa
kama inagongana, kuna hali inamkanya, na kuna hali inamvuta kufanya hivyo, na
kujikuta kama anatetemeka vile.
Alipoingia ndani, akatizama
eneo la kitanda, ...kwenye eneo la kitanada, kulikuwa na sehemu kubwa ya paa na
mabaki ya paa yalikuwa yamedondokea hapo, sehemu hiyo kwa juu waliweka wa mbati
ya akiba, na yale mabati yalikuwa yamedondokea kitandani, na kikawa kama
kimevunjika…akawa anayainua yale mabati mengine yalikuwa yameungua kabisa, utafikiri
karatasi, mengine yalibakia bakia, kuna ya chini kabisa yalikuwa mazima.
Akayainua yale mazima na kuanza kuyapenga sehemu nyingine nia ni
ili afikie kitanda..na hatimaye akafikia kitanda, hutaamini, akakuta kitanda na
godoro, havijaungua sana,..inonekana lile paa lilisaidia kuzuia moto usifike,
hapo kitandani...lakini hakumuona huyo mamapale kitandani!.
‘Khaaa. Huyu mama yupo wapi…!?’ akawa anajiuliza kwa mshangao
**********
‘Huyu mama atakuwa hayupo nini..?’ akawa anajiuliza na hapo
akajipa moyo kuwa huenda huyo mama aliwahi kukimbia kabla moto haujapamba moto
Akawa sasa anahangaika kuinua bati moja moja, yale yalikuwa
mazima, na akiyatupia mbele, na baadhi ya watu wakawa wanajisogeza kwa mbali,
na kusema;
‘Tupi huku mzee, tuyapange kwa nje, moto usije ukazuka tena na
kuyaunguza, angalau umebahatika kupata kidogo kilichobakia, watu wengine wakawa
wanafika kwa mashaka kuyapokea na kuyasogeza kwa mbali.
‘Angalia mzee hapo bado kuna moto…’akasikia watu wakimuambia, watu
wengi walishachoka na wengi walikuwa wakusubiria kupoe kabisa, na walishaona
kama kulikuwa na mtu humo watamkuta maiti tu.
‘Sasa mbona mnapumzika vijana, hakikisheni kama moto umezimika
wote, unaweza kulipuka tena ukaunguza nyumba iliyobakia,..nyie ndio vina
tunawategemea,..na kama kuna…mtu au maiti basi mhakikishe anatolewa, huo ndio ubin-adamu..’akasema
mjumbe.
‘Kama kuna mtu hapo ni maiti..na tunaona tuvute subira, maana
maiti ya mtu aliyeungua inatisha kidogo..’wakasema hao vijana.
‘Inawezekana bado yupo hai, ni muhimu kwenda kusaidia..’akasema
mzee mwingine.
‘Labda awe ni shetani maana mashetani yametengenezwa kwa moto,
kwahiyo hayaungui…’akasema kijana mwingine.
‘Nyie vijana mna laana, kama kweli mnafikiria hivyo, kweli maisha
yenu yatakuwa mabaya…’akasema
‘Nyie ndio mnafanya maisha yetu yawe mabaya, mlishatumia ujana
wenu, sasa mnataka kutufanya sisi tusufaidi ujane wetu…moto tumeshazima
inatosha, ngoja tupumzike kidogo….’akasema mmojawapo.
‘Kwa vipi..nani kawafanya hivyo, ina maana sisi kuwakanya msifanya
machafu, ndio mantuona wabaya, tuaache tu mvute mabangi yetu, tusiwakemee
mkibiwa madawa ya kulevya..hamuoni kama mnajiangamiza wenyewe, na kutusingizia
sisi wazee wenu…’akasema mzee mmoja ambaye mara kwa mara anatanaia na hao
vijana.
‘Mzee wewe tunakufahamu huna ubaya na sisi, lakini kuna wazee
wengine, vigagula..wanatuwangia usiku ili tusiwe na maendeleo, hao ndio
tumetangaza vita dhidi yao…’akasema kijana mwingine.
‘Huwezi kutangaza vita na mtu ambaye hajiwezi, kama mna minguvu
hiyo nendeni mkaitumie shambani, limeni, fanyani kazi za kuwaingizia kipato,…mkitumia
minguvu yenu kupambana na wazee waliojichokea, mnajitafutia laana,…’akasema
huyo mzee.
‘Laana haitupai..mwanga atamlani nani…atajilaani mwenyewe..’akasema
mwingine.
‘Nyie vijana kila siku nawaasa, acheni kukaa vijiweni na
kujidanganya, kuwa kuna wazee wachawi,..uchawi mnajitafutia wenyewe kwa hayo
madawa, mipombe…na bangi…mjichawia wenyewe na kukosa maendeleo, kama ngejituma
mashuleni, mkafaulu mitihani mngelikuwa mbali..angalieni wenzenu huko Ulaya,…wanajituma
ndio maana wana maendeleo…nmkibakia hivyo, kulalamika, mwisho wenu utakuwa
mbaya zaidi..’akasema huy mzee.
‘Hutuambi kitu mzee, hiyo ni onyo kwa vigagula,..mmoja mmoja
ataondoka, na hata wewe tukithibitisha kuwa una mikoba mzee hatutakuacha…,
..dawa yake ndio hiyo…habari ndio hiyo..’akasema mmoja akionyesha kashalewa na
madawa ya kulevya.
‘Mwenyewe hapo ulipo unasubiri kujifia..hayo madawa yatakumaliza
siku si zako..’akaamiwa na wenzake wakawa wanamcheka.
‘Mimi sifi, mtaniona hivi hivi….’akasema akiondoka huku akipepesuka.
Baba mwenye nyumba akawa sasa keshakifikia kitanda, na akawa anajaribu
kukinua, kwanza akaondoa godoro, lilikua limeungua upande akaweza sasa kukiona
kitanda, chini ya godoro kulikuwa na mkeka, mkeka ulikuwa bado mzima.
Wakati anahangaika akajikwaa, akainama chini kutizama, akaona mguu wa mtu, akainua kile kitanda, na
kukiangushia upande, akauvuta ule mguu., ni mtu..ni yeye,…
‘Oh, ni yeye…’akawa anasema kwa sauti japokuwa hakuwa na uhakika
kama huyo mtu ni mzima.
‘Ni mama wa mkono wa baraka…’akasema akihis watu huenda
wamemsikia, lakini sauti haikutoka, koo lilikuwa kavu, alikuwa kama anakoroma.
Akawa sasa anaondoa, mabaki yaliyokuwa yamemtanda yule mama, …kweli
alikuwa yule mama wa mkono wa baraka....na kwa juhudu sana akaweza kumtoa sehemu
ile na kumsogeza pembeni.
Yaonekana huyo mama, alikuwa kajitumbukiza chini ya kitanda..sijui
alikuwa anajificha au ilikuwaje, kwa wakai huo huyo mama likuwa kalala kitumbo
tumbo, akamgeuza na kuangalia juu, alikuwa katapaa damu, ...
‘Mbona katapaa damu….miguuni, mikononi...mwili mzima ulikuwa na
majeraha, kama ya kukatwa katwa na mapanga , akashangaa, alichojua yeye ni
moto, sasa iweje huyu mama awe kama kakatwa katwa na mapanga. Alimsogelea karibu
yule mama, na kumkuta akiwa katika hali mbaya sana, akamuinua na kuangalia kuwa
bado yupo hai.
Alishika eneo la mikononi hakuweza kupata mapigo ya moyo vyema,
akainamisha kichwa na kuweka sehemu ya kifuani,..bado akawa hana
uhakika..akataka kushika sehemu ya shingoni, lakini zile nguo zilivyo, hakuweza
kutumbukiza kidole, ikabidi ajaribu kusogeza zile nguo, akawa sasa
kama anavuta kwa juu, na alipona hapati nafasi, akaona ni bora kuondoa ile
sehemu yote ya juu, hadi kichwani
‘Oh, sijui nitakosea, lakini lazima nifanye hivi kuona kama yupo
hai..atanisamehe tu...’akasema na kuanza kuivuta ile nguo ya sehemu ya kichwani
, ilikuwa ni kazi, maana inaonekana mama huyo alikuwa kama kajifunga shongoni
ili nguo istoke...
Akapata upenyo, na akagundua kuwa mapigo ya moyo bado yapo. Na
hapo hamu ya kumfunua kabisa ile sehemu ya usoni ikamjia, akataka aone sura ya
huyo mama ipoje, na kwanini siku zote anakuwa kajifunika,...alijua anafanya
kosa, lakini hamasa ikamzidi.
‘Usifanye hivyo utapatwa na madahara kama yliyowapta waliojaribu
kufanya hivyo…’ilikuwa sauti ikimuonya kichwani, kwani alishasikia kuwa kuna
watu walijaribu kumfunua hiyo nguo ya kichwani ili wamuone sura yake, sasa hivi
wapo kitandani waganjwa wamekuwa kama wamechanganyikiwa.
Yeye kwanza alichelea kufanya hivyo, sio kwasabau ya kuogopa hayo
aliyosikia, bali kwa kuogopa kuwa anafanya kkitu ambacho mwenyewe hakupenda
kifanike, kama mwenyewe hakupenda uso wake uonekane kwanini afanya sasa, lakini
hata hivyo hamasa ya kumtambua huyo mama ikamjua, akaanza kuvua ile nguo ya
kichwani.
Akatumia nguvu na kuivuta ile nguo iliyokuwa imefunika
kichwani...taratibu ikawa inavuka baada ya lile fundo la shingoni kuachia,...,
na kila hatua akawa anashangaa, ilikuwa sura ya ajabu..…baadaye akakivua
kabisa, uso ukabakia wazi…alishikwa na butwaa, akajikuta anadondoak chini....
Akiwa pale chini, akapangusa macho yake, huku mwili ukimtetemeka, alishangaa
kwa nini ..lakini hata kabla wakati alipoamua kuuvaa huo maoto na kuingia hapo,
alihis mwili ukimtetemeka..mwanzoni alihis huenda anaumwa malaria,..sasa kule
kutetemeka kulizidi.
Akajitutumua na kusimama, akarudi kumwangalia tena yule mama,
lakini ile nguo ambayo alikuwa na uhakika kuwa aliitoa, akaikuta imerudi mahali
pake, uso umejifunika tena,....akaona ajabu ina maana huyo mama yupo hai
kajifunika mwenyewe tena, ..., huyu ni mtu au…mbona …hapana,… akajaribu kuivuta
tena ili kumfunua amuone vyema usoni…huku akisema;
‘Hapana..haiwezekani, ..sio yeye, hapana…hapana…’akawa anarudia
hayo maneno huku akijaribu kuvuta ile ngo
Na alipofanya hivyo, yule mama akainua mkono na kushika ile nguo
kuzuia...jamaa akarudi nyuma, akabakia kaduwaa...na akaona mtikisiko wa mwili
wa yule mama akawa anahangaika akijaribu kuinua mguu, lakini ilionekana mguu
una majeraha, akawa anagugumia maumivi huku akisema;
‘Msiniue, mimi sio mwanga, mimi sio mchawi… jamani…nimewakosea
nini walimwengu…kwanini mnataka kuniua…..niemkuaj kumtafuta mtoto wangu…nataka
mtoto wangu’ akaanza kupiga ukelele mara mbili, halafu akaulia kimia..akatikisa
mgu mara mbili, halafu akatulia….
NB: Kumbe yupo hai, je mwenye nyumba aliona nini kwa huyo mama….
WAZO LA LEO: Kulalamika tu hakutoshi,..muhimi ni
vitendo vya dhati. Kabla ya kulalamika, kwanza tujiulize tumefanya juhudi gani,
je tulijibidisha kwenye kazi, tukatimiza wajibu wetu sawasawa,..kama ndio basi
tuna wajibu wa kudai haki zetu, lakini
kama sisi wenyewe tunaongoza kwenye utegaji wa kazi, kutwa nzima tupo
vijiweni, wanafunzi hatusomi, tunashindana
kwa usharobaro,…kata k, mbano shepu sijui..nk …kuimba kwa kukariri bila
kusomea,..kuota doto za Alinacha,…utamlalamikia nani. Hebu jiulize kama kila mtu
atafanya hvyo unafikiri taifa litakuwaje..tusitafute mchawi, uchawi
tumeutengeneza sisi wenyewe.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Ni muda mrefu sijapita hapa. Ama kweli kazi zako nazihehimu sana endelea kutuelimisha ..Hakuna kama mama.
Post a Comment