Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, February 6, 2015

NANI KAMA MAMA-29


 Mume mtu alikuwa ametulia kimia akiwa kainama, akionyesha yupo kwenye lindi la mawazo, na aliposikia mke wake akisema kuwa mtoto huyo anafanana na yeye, akainua kichwa na kumuangalia yule mtoto akiwa mkononi mwa mke wake.

Yeye alishafahamu mke wake ana maana gani, lakini kwa vile mdogo wake alikuwa akimuamini sana dada yake, hakuwa na mawazo kama hayo kuwa dada yake anaweza kumshuku kitu kama hicho.

Mume mtu akaona hicho kinachoendelea kinaweza kuleta uatata zaidi, akaona sasa aingilie kati, kwanza akamuangalia shemeji yake na kucheka kidogo, akasema;

‘Unajua shemeji hujamuelewa ndugu yako,…yeye ana hisia nyingine kabisa, na unavyozid kuelezea hayo anakuona kama unazunguka yeye keshajenga dhana yake,…simlaumu sana, lakini…hatuwezi kwenda hivyo, kama tumeishi miaka yote hii tunaaminiana, kwanini hili liwe ni tatizo, ….kufanana ..kwanza hiki kiumbe ado kidogo, h huwezi kuhitimisha ..ukasema mimi..hapana…’akaongea huku akitikisa kichwa.

‘Sasa shemeji…sikiliza mimi nimshakuelewa sana, na jambo ulilolifanya ni zuri sana, japokuwa, linaleta sintofahamu kwenye kichwa cha dada yako,…ila ulichofanya ni ubinadamu, cha muhimu, labda ungetuelezea, ilikuwaje kwa mama yake,…ina maana mama yake amekufa…au ilikuwaje…?’akauliza mume wa familia akimuangalia shemeji yake na mke mtu akaona kama kadharauliwa.

‘Haya naona mnataak kuongea wawili,…Sawa mimi naona  nitoke nje, niwaachie ukumbi, …natoka na huyu mtoto ili asiwasumbue,  nyie endeleeni kuongea mliweke hili jambo sawa mkubaliane, msilete hadaaa, ukweli upo dhahiri, hata nani asingelihadaika,  sawa ongeeni mimi natoka nje….’akasema dada mtu akitaka kuondoka na mtoto. Mume mtu akageuka na kumuangalia mke wake, akasema;

‘Hatoki mtu nje, haondoki mtu hapa, hili ni letu sote, ….’akasema.

‘Ni letu sote lakini kwanza mkubaliane..mimi sikatai, umenoa ni mke wako, nitafuata yote unayotaka wewe, lakini kama wewe na mzazi mwenzako hamjaolewana, mii nitafanya nini, kazi yangu ni kutii tu…si keshakupatia mtoto….’akasema na kumfanya mdogo wake akunje uso kwa masikitiko, hakusema neno akawa anasubiria wanandoa hao waongee.

‘Nimesema hivi, hatoki mtu nje,  natuma umesnisikia, wewe kama mke wangu, utabakia hapa, usikie hicho ninachotaka kukiongea, naona sasa unataka kujivika mambo yasiyokuwepo, ibilisi kauteka ubongo wako , hutaki kuelewa, hata mdogo wako naye…kwakweli umekosea sana,..lakini tuatalimaliza tu…’akasema mume mtu.

‘Hata mimi nashangaa, hata mdogo wangu, unafikia kunifanyia hivyo…..hapana, mimi sikai humu ndani….sitaweza kuvumilia, nita…..’akaanza kulia

‘Nimesema  kaa pale kwenye kiti,  usikie hayo ninayotaka kuaongea,…wewe si unataak ukweli, sasa kaa pale tuyaongee, ukweli wote utaufahamu kama kweli tulikaa mimi na mdogo wako tukapanga haya, kwa mtandao, sawa….’akasema mume wake.

Mke wake, kwanza akasita,akaguka na kumuangalia mdogo wake, akatikisa kichwa, kwa masikitiko, akili ilikuwa imeshafungwa, ….imania ile , upendo ule, …udugu ule, ukawa haupo tena, …na machozi yakaendeela kumtoka, mdogo mtu akawa anakunja uso wa kutahayari, akawa haelewi..haaimini, hivi ina maana dada yake anawaza mengine,….akawa anawaza hili na lile.

‘Hivi dada yangu ana maana gani, ina maana anahisi kuwa mtoto huyu ni wa kwangu, nimemzaa mimi,… aah, haiwezekani, mmh, haiwezekani, dada yangu mwenyewe asiniamini, imekuwaje, ..hapana dada yangu hawezi kufikia hapo..lakini kwanini anasema mtoto anafanana na mume wake….hapana dada yangu hawezi kunishuku hivyo, hapana…mimi niwe na mahusiano  na shemeji ..ndivyo anavyowaza hivyo…..mmh’akawa anajiuliza maswali mengi kichwani..na kujikuta akishika hata kidevu….

Na dada mtu bado alikuwa kasimama..mara akaanza kuzivuta hatua.. moja  mbili, akitaka kuelekea nje…mdogo mtu akasogea akitaka kumzuia, lakini mume mtu akamuashiria kwa mkono kuwa atulie …dada mtu akawa sasa anaeleeka nje, na mume mtu akasema kwa ukali;

‘Wewe mwanamke…’akajikuta ametumia lugha ambayo hajaiwahi kuitumia kwa mke wake kabla, maana siku zote lugha ni `mke wangu, mke wangu’ na mke wake aliposikia hiyo kauli akageuka kumuangalia mume wake kwa uso uliojaa hasira, hakusema neno, hakujali akaanza kutembea sasa anakaribia mlangoni, mume wake akasema tena.

‘Umenisikia ….ukitoka nje, basi …litakalotokea usije kunialamu…’ilikuwa sauti ya mume iliyoonyesha dhamira ya kweli…mke hapo akasimama, akiwa kamshikilia mto akapiga magoti.

Wote wakashangaa,

Tuendelee na kisa chetu.

******

Mke wa familia akapiga magoti, …mdogo mtu na mume mtu wakawa wanamuangalia kwa mshangao, akainua kichwa kumuangalia mume wake kabla hajafunua mdomo kutka kukiongea hicho alichotaka kukiongea, mdogo mtu akasema;

‘Dada nakuomba kwa jina la mwenyezimungu, niamini..mimi ni mdogo wako, nakuomba uniamini, hakuna lolote baya nililolitenda, huyu mtoto sio wa kwangu kwa kumzaa, dada mtoto huyu sijamzaa mimi,..sijawahi kupata mimba…huo ndio ukweli dada…’akasema mdogo mtu, na dada mtu aliyekuwa bado kapiga magoti huku machozi yakimtoka, akainua uso na kumuangalia mdogo wake.

‘Una..una…uhakika na unachokisema?’ akauliza huku akiwa haamini.

‘Dada…dada ina maana kwa muda wote huo ulikuwa hujanielewa, au unamawazo gani, kuwa huyu mtoto nimemzaa mimi, ..dada hapana sijamzaa mimi, sijavunja kiapo nilichokuahidi siku ile.. huyu mtoto sijamzaa mimi dada ila nimechukua jukumu la kuwa mama yake, jukumu ambalo nawakabidhi nyie,…dada niamini mimi, sijawahi kupata mimba…hilo nakuapia na mungu ni shahidi yangu, huyu mtoto amezaliwa huko hospitalini, na ……’kabla hajatamka neno nje kelele ikasikika.

‘Na-na-namtaak mtoto wangu….namtaka mtoto wangu…. ‘ kauli ikamfana mtoto aanze kulia, na dada mtu akasimama huku akiangalia nje, na baadaye akamuangalia yule mtoto, akawa katoka macho kama ya kuogopa, na mara mtoto akatulia kulia.

‘Mhh, jamani kuna nini hapa…hivi hamlioni hili….hapana..huyo mama sio wa kawaida..kuna kitu….’akasema

‘Dada kuna kiu gani umekiona?’ akaulizwa na mdogo mtu..

‘Hapana..kuna kitu…kuna hali nimeihisi …hapana kuna kitu hapa, kwanini iwe hivi, huyo akiimba mtoto huyu anaanza kulia…?’ akauliza na kumuangalia mdogo mtu.

‘Kulia si kawaida, ..imetokea kwa anataka kulia na wakati huo ho huyo anaimba, dada usijivike kilemba kabla hujakipanga…’akasema mdogo mtu.

Dada akiwa sasa kasimama, akamuangalia yule mtoto, akamshikilia kifuani kama vile anamkumbatia, alikaa vile kwa muda, akiwa kafumba macho, halafu akiwa kamshika kwa mbele kama anataka kumkabidhi mtu,  akatembea hatua hadi pale aliposimama mume wake, akamuangalia mume wake machoni na kusema;

‘Mume wangu, hebu muangalie vyema huyu mtoto, nataka kauli yako ya ukweli, uniambie yaliyo na ukweli..mdogo wangu anasema hajamzaa yeye huyu mtoto, mimi nimemuamini, sioni haja ya kutokumuamini, lakini bado kuna swali kichwani mwangu, na mwenye jibu sahihi ni wewe, unaweza ukaficha ukweli, kuwa wewe hujahusika na uja uzito wa mtoto huyu, lakini mimi ninachotaka kukuulize tena..ni swali moja..’ akatulia kidogo.

‘mke wangu ina maana huniamni…?’ akauliza mume mtu.

‘Swala la kukuamini ni jingine, naweza kukuamini, lakini sina uwezo wa kuisoma nafsi yako, nafsi ya mtu ni kichaak chenye giza nene..nitajuaje siri iliyopo kwenye nafsi yako….’akasema mke mtu.

‘Haya niulize unachotaka kuniuliza…’akasema mume mtu.

‘Muangalia huyu mtoto kwa makini,…umeiona sura yake..?’ akauliza mke mtu.

‘Ndio nimeiona….’akasema mume mtu akimuangalai yule mtoto.

‘Huyu mtoto anafanana na nani?’ akauliza mke mtu

‘Mbona hilo swali tumeshalijibu awali,…’akasema mume mtu.

‘Aaah, nataka unijibu, sasa hivi, kwa kauli yako mwenyewe..’akasema mke mtu.

‘Mtoto huyu ni kweli anafanana na mimi,..siwezi kukataa, ni kweli nimuonavyo anaonekana kufanana na mimi, lakini…’akasema na kuataka kutoa maelezo

‘Rudia tena..’akasema mke wake

‘Nirudi tena, kwanini..ok, sawa, ndio anafanana na mimi,ila nataka kutoa ufafanuzi, wa kuanana….’akataka kuendelea kuongea, lakini mke wake akiwa kamshikilia ule mtoto akasema;

‘Pokea mtoto wako, anahitajia baraka zako….’akasema na mume mtu akamuangalia mkewe kwa macho yenye mashaka, halafu akageuka kumuangalai shemeji yake, na shemeji yake akaonyesha ishara kuwa akuali kumpokea, mume mtu akampokea. Na mkewe akarudi nyuma hatua moja na kusema;

‘Mimi sitaki kusikia utetezi wako….kwa hivi sasa, naomba nipate muda wa kulifikiri hili, nahitajia kutuliza akili yangu, na nimuombe mungu anisamehe kwa hili, maana hatujui ukweli sahihi..mungu peke yake ndiye anayefahamu ukweli …hata kama tutauficha, na namuoma mungu anisamehe, kwa hilo…nilishamshuku vibaya mdogo wangu…nisameheni…ndio maana nilipiga magoti..’akasema na kumgeukia mdogo wake, na mdogo wake akawa anatabasamu tu.

‘Dada usijali…hiyo hutokea hata mimi ningelifikiria hivyo, ila nataka uniamini dada, siwezi kamwe, kufanya huo uchafu…ina maana hakuna wanaume wengine mpaka nikusaliti, hapana siwezi kufanya hivyo.

‘Kiukweli,dada huko ulikokuwa umefikia, ulipotoka, nakuomba urudishe imani yako kwangu na kwa mume wako,..kumbeni nyie mlinichukua nikiwa bado sijakuwa msichana mkawa wazazi wangu wa kunilea, mkanisomesha, ….’akatulia.

‘Dada hivi kuna mtu anaweza kufanya hayo kwa mzazi wake,..maana nyie ni kama wazazi wangu wa kunilea, mwenye akili timamu hawezi kulifanya hilo…..dada mimi nachukua nafasi hii kukuomba msamahani kwa kutokuliweka hili wazi mapema, nahisi kama mimi ndiye nimesababisha yote haya.…’akasema mdogo mtu.

‘Sawa,….nimekuelewa mdogo wangu, akamsogelea mdogo wake na kukumabtiana kila mmoja akitokwa na machozi, sijui ni ya furaha au …waliendelea kukaa vile hadi mume mtu alipokohoa, na kusema;

‘Oh,…kweli mungu mkubwa,..kweli huyu mtoto anafanaan na mimi, imetokeaje..hata sielewi, mungu peke yake anayajua haya..’akasema na wote wakageuka kumuangalia, na wakamuona akiwa anamtizama yule mtoto, na bila kujalia zaidi wakaendelea kuongea.

‘Shemeji usimuache wazi hivo, mfunike kabisa…’akasema shemeji mtu alipomuona shemeji yake anamtizima yule mtoto kwa mshangao, huku yupo wazi. Na wawili hawa wakawa wanaongea huku macho yao mara kwa mara yakigeuzwa kumuangalia mume mtu kwa jainsi anavyoonyesha furaha kwa yule mtoto.

‘Dada tatizo lililotokea huko hospitalini, limenifanya nipate mtoto huyo bila kupenda, lakini nikawaza sana, mmi bado sijakuwa na uwezo wa kulea mtoto, nikaona kwanini nisiwaletee nyie, nyie ndio mim, ndio maana nikachukua hatua hiyo..

‘Dada mtoto huyo aliachwa, hana mama wala hana baba, nani atamlea, kama sio mimi na nyie, mzazi wa watoto kama huyo ni mimi na wewe, na yoyote yule mwenye kumuogopa mungu. Mtoto huyo hakupenda iwe hivyo, ….alitakiwa naye aanze kunyonya titi la mama yake, lakini ya mungu mengi…’akatulia.

‘Nilitaka nisikimbilie kuwaelezea hili kiundani,maana bado mambo hayajawa sawa, nitawachanganya …ila nilataka hili liwaguse kwanza,.. nimepanga niwaelezee hatua kwa hatua kila nikija, na mwisho wake tusije kuingia kwenye matatizo, maana huyo mtoto sasa hivi hajui lolote, atakuwa mkubwa ataambiwa hili na lile, kama sio nyie ni majirani…lakini chonde, chonde, huyu mtoto ni wenu, akue akijua hivyo, ndivyo inavyotakiwa kwa mtoto kama huyo…’akasema na mara mtoto akaanza kulia.

Wawili hawa wakageuka kuangalia kule alipokuwa amepakatwa na mume mtu, na mume mtu alikuwa akiwa kama anacheza naye ila alipoanza kulia akageuza kichwa kuwaangalia mkewe na shemeji yake, huku akianza kumbembeleza, na mdogo mtu akasema;

‘Dada, ngoja nimtengenezee mtoto maziwa yake…halafu sogea huku dada nikuonyeshe jinsi gani ya kuyatengeneza, huu ni muda wa kumpa maziwa..’ akasema na kuchukua kopo la maziwa, akachota na kijiko, huku akisema;

‘Dada….., inatakiwa umpe maziwa haya niliyoleta, vipimo vyake vipo kwenye hii chupa..unaona hapa wameandika nini…hapa, na kijiko hiki ni kipimo kimekamilika, ukichota saizi hii kikaja, basi unamimina kwenye maji ya uvugu vugu…yaliyochemka kabla….unaona eeh, hakikisha maji ni salama, …’akawa anamuonyeshea dada yake.

‘Mhh, mdogo wangu unaniona mtoto eeh, kutokuzaa sio kwamba sijui kulea,..hayo nimeshajifnza kwa vitendo, na kwa kusoma…muda mwingi nilikuwa nasoma jinsi gani ya kulea, mimba, ukizaa uweje, ..jinsi ya kulea mtoto, kunyonesha..hayo yote nilishajiandaa nayo, najua….huna haja ya kunionyesha…’akasema dada yake sasa akiwana na uso ulio na uhai kidogo.

‘Dada, mimi ni wajibu wangu kukuambia, ….unaona haya maziwa, ni maalumu kwa watoto wachanga kama hawa, humpi mengi sana, ila kadri siku zinavyokwenda ndivyo utakavyomuongezea kipimo chake, tatizo akina mama wengi, wakiona mtoto analia tu, wanakimbilia kumpa mtoto maziwa, hawaangalii kuna tatizo gani kwa mtoto.

‘ Mtoto anaweza kulia kwa tatizo jingine, wewe ukakimbili kumpa maziwa, ni kweli anaweza kunyamaza,lakini hujaweza kulitatua tatiz lililo mfanya alie,…tatizo lililomliza linaweza kuendelea kuwepo na hata kujificha, mtoto anaumia, mwishowe anaanza kuumwa,,…’akasema.

‘Sasa dada, chukua mtoto kwa shemeji uanza kumnyonyesha, kama ulivyosema umeshasomea hayo, basi, mimi sina shaka tena, kuanzia leo huyu ni mtoto wenu….’akasema na mara kwa nje wakasikia sauti ile ile..

‘Na-na-nataka mtoto wangu…nataka mtoto wangu…’ wakasikia kelele nje ikiendelea kwa nguvu lakini safari hii mtoto hakulia, alikuwa macho tu akinyoneshwa maziwa na mama yake wa kufikia. Mdogo mtu, akawa anaangalia huko sauti inapotokea, akasema;

‘Hivi huyo mama…mnamuelewa lakini, kwanini aimbe hayo maneno, ana akili sawa awa kweli..mumejaribu kumchunguza vyema alivyo mimi nahisi kama …’akatulia na dada mtu akasema.

‘Kama vile alikuwa na mtoto, na kwa hali yake ilivyo wakamchukua huyo mtoto ndio maana anaimba hivyo, si ndivyo unavyofikiria hivyo..utasema nimeanza kutunga hadithi…’ akamkatiza dada mtu na mdogo mtu akasema.

‘Hivyo hivyo ndivyo nilivyokuwa nikiwazia….’akasema.

‘We acha tu…huyo mama sasa hivi ni gumzo hapa kijijini,…, na kutokana na huo uvumi ulio-enea hapa mitaani, watu wanaitikia kila wakisikia sauti yake, kama ingeliwezekana kunasa sauti za kutoka majumbani ungelisikia wakimuitikia….’akasema dada mtu.

‘Wanamuitikia anavyoimba..?’ akauliza mdogo mtu.

‘Ndio..kutokana na huo uvumi,  ukiitikia unapata baraka …..wanasema ni mama wa neema kutoka mbinguni,..maana hajulikani wai katokea, wanasema mama huyo, kaja kuleta baraka…’akasema dada mtu.

‘Unaisikia sauti yake ilivyo ndogo, inakuwa kama sauti yanye mpenyo fulani moyoni, ndogooo….sasa ukimuitikia anavyoimba na wewe unaingiwa na baraka, na sisi hapa tulitakiwa tumuitike anavoimba ili uzipate hizo baraka,…’akasema na wkatulia, na mara wakasikia akiimba huyo mama, na kama vile waliamrishwa wote wakaitikia hata mume wa familia.

‘Na-na-taka mtoto wangu, nataka mtoto wangu..’ wakaishia kucheka.

‘Sasa mbona mnacheka tena, hivi imani inafanyiwa mnzaha..’akasema mume mtu aliyekuwa kimia kwa muda, ,,japo naye aliitikia huo wimbo. Mume mtu baada ya kupokewa mtoto ili anyweshwe maziwa, yeye alibakia kimia kwa muda mwingi,  alionekana katingwa na mawazo sana, na alijitahidi kutokuonyesha hiyo hali , lakini haikuweza kujificha.

‘Haya shemeji nahisi tumetulizana, kiu yetu ni kusiki hayo yaliyotokea huko kazini kwako na jinsi gani ulivyompta huyu mtoto….’akasema shemji mtu.

‘Ndugu zanguni, kwa hivi sasa, mimi naona mlijue hilo kwanza, maana hata mimi ukiniuliza undani wa tukio lenyewe…sina uelewi wa kiundani zaidi, nitaelewa vyema nikirudi huko…, huyo mama alivyoletwa pale kujifungua, hadi ikafiki hapa, bado sijaweza kuyaweka akilini vyema,..sisi kama manesi tulikuwa wahudumiaji tu…ngojeni nikirud huko, nitajua vyema…. mpaka sasa naona kama miujiza ya mungu tu…’akasema

‘Ina maana hata huyo mama wa huyu mtoto humfahamu vyema….alivyoletwa hukumuona vyema?’ akaulizwa.

‘Mhh, nilimuona, lakini ….sura siwezi kuikumbuka vyema, …kwani alili.ana majeraha, alikuwa kafungwa fungwa,…nitakuja kuwasimulia vyema siku ikifika, lakini sio leo, leo ninalotaka kuliweka sawa ni hili,..huyu ni mtoto wenu..iwe ndio kauli yenu, wakiuliza sana, kaeni kimia, maana haya mambo bado yapo mikononi mwa wakuu wa hospitalini…’akasema
‘Sasa hapo bado ulipewa pewaje huyu mtoto…?’ akauliza shemeji mtu.

‘Mtoto hana mama, mtoto , hana baba, hakuna ndugu yoyote, yupo hapo hospitalini, na kuna muda inatokea na watoto hao hupelekwa vituo vya hisani, lakini wa huyu ikatokwa kuwa tofauti….’akasema

‘Ina maana wewe ulipewa huyu mtoto kama adhabu….nakumbuka kwenye simu ulisema uliondoka kwenye wodi, ukiwa umepewa jukumu la kumlindana kumuhudimia mgonjwa, ukaondoka kufuata dawa, au sio, uliporudi ikawaje sijui….’akasema shemeji mtu.

‘Ndio..ni hivyo, sasa ikawaje, nitaawambia nikija tena, kwani huko kuna kesi, kuna mkitani , kuna uchunguzi,….lakini hili swala linatakiwa liishe kimia kimia, ikiwezekana issijulikane kabisa kama kulikuwa na tukio kama hilo..’akasema.

‘Mhh, sasa..ikatokea mtu kuja kudai, huyu ni mtoto wake,…au anafanana na jamaa zao..?’ akauliza shemji mtu.

‘Tutakuja kuliongelea hilo..nimechoka kweli ..mimi naomba nikapumzika, kesho asubuhi naondoka,…ngoja nikaongee na huyo dereva,kwani aliatakiwa kunisubiria nirudi naye, lakini kwa hali niliyo nayo ni bora nilale, nitaondoka kesho, yeye aondoke tu, kesho nitatauta usafiri mwingine,….’akasema na kutoka nje, hakuchelewa akarudi, na shemeji yake akamuongelesha.

‘Sasa shemeji ni kweli umetuleetea neema, lakini shemeji, imakuwaje mpaka unione kuwa mimi sitaweza kuzaa tena, na kama nisipozaa na dada yako ningelizaa na wewe, wewe si mke wangu pia…’ mume mtu akaongea kiutani’

‘Hahaha, shemeji, umeanza tena, unataka kumtonyesha dada vidonda vyake…’akasema na kugeuka kumuangalia dada yake, lakini dada yake kumbe alishaamua kulala, na alionekana kapitiwa na usingizi, akiwa kalala kwenye sofa, na pembeni yake yupo huyo mtoto mchanga.

‘Mhh, shemeji …sijui nikupe nini…tulikuwa tunatamani sana kuwa na mtoto, ..lakini kwa mazingira ya haapa kijijini, ..unakuwa uancehelea, unaogopa watu kuja kutusema, ..siunajua tena maisha ya kijijini,…watasema tumeona hatutazaa,..hili na lile,..lakini mmmh, mtoto huyu kwa sasa atakuwa ni faraja sana kwetu, hadi hapo tutakapojaliwa kuwa na watoto wetu wenyewe,..mimi nina imani tutapata watoto tu…’akasema shemji mtu.

‘Ni kweli…na kwa vile mlishapima mkaonekana hamna tatizo, ipo siku mimba itatunga tu shemeji, hili msikate tamaa, naona dada kalala, ngoja…nami nikapumzike ndani…’akasema lakini akaona amuamushe dada yake aliyekuwa kama anaongea kwenye ndo

‘Dada vipi mbona unaota mchana.. mimi nataka kujipumzisha kidogo ndani…’akasema mdogo mtu na dada yake akainuka pale alipokuwa kajilaza, na kusema;

‘Ingia chumbani kwako, kupo vile vile….sijui uende na huyu mtoto , maaana naona kalala, tatizo ni hao wanaosumbua huko nje, najua wakianza kuimba hapa watamfanya mtoto aanze kulia,…’akasema.

‘Sawa ngoja nimchukue…na inabidi tumbadilishe hii chupi ya mkojo…’akasema nana akawa anatoa chupi nyingine ya mkojo.

‘Mhh, na haya machupi ya mdukani mimi siyapendi sana….’akasema dada mtu.

‘Haya ni salama, wala usiwe na shaka nayo..yanasaidia, maana yanaynya mkojo, ila usiache kwa muda mrefu..’akasema mdogo mtu.

‘Mhh, hii ndoto nayo inanitia mawazo,…unajua hapa nilipolala, kidogo nilianza kuota ndoto ya ajabu…’akasema

‘Mh, haya tupe hadithi, umeota ndoto gani tena?’ akauliza mume mtu.

‘Huyo mama anayeimba, kanijia, akiwa na sura ya ajabu…kwanza aliponitokea alikuwa kajifunika uso wake,…akanijia na kudai nimpe mtoto wake, nikamwambia mimi sina mtoto wake,..akasema, unaye mtoto wangu,..nipe mtoto wangu kwasababu na wewe una mtoto wako.

‘Eeeh, nikaona hayo makubwa, ila kwanza nikamwambia ajifunue ili nimuone sura yake, maana kuna wanawake wezi wa watoto…akasema sura yake haitakiw a kuonekana, mimi nikamsihi kuwa kama asiponionyesha sura yake simpi mtoto wake, basi akaamua kunionesha, alipojifunua uso wake ukawa unamemeta meta…nikamuuliza wewe ni nani na unataka nini,….’

‘Akasema mimi ni mama wa karama, nimekuja kumtafuta mtoto wangu, aliyechukuliwa…nikamuuliza kachukuliwa na nani, akasema na mimi, eti mimi ndiye nimechukua mtoto wake, nikamuliza yupo wapi, akasema huyo hapo ….nikawa nainama kumtizama…huku namuuliza na mtoto wangu unayesema ninaye yupo wapi, akasema, wa kwako yupo hapo tumbaoni kwako..

Sasa nikawa nainama kuangalai mawili, mtoto wake anayemtaka, na pia kutizama tumbo langu ambali anasema lina mtoto, mara nikashituka unaniita…’akasema

‘Mawazo, mawazo dada, hayo ni mawazo yako ya kuwa na mtoto….usiwe nayo tena, mtoto huyo unaye huyo ni mtoto wako…’akaambiwa na mdogo wake huku akimchukua mtoto kuondoka naye.

Sasa wakabaki mke na mume,…, kimiya kikatanda, kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani, mume akiwa anawaza tukio zima, na alionekana kuzama kwene dimbwi la mawazo, na mkewe akawa kila mara anamtupia jicho la kujiiba. Mke alikuwa na yake kichwani, yaliyohitaji majibu, alitaka kujua ukweli…lakini kimia kikatanda, utafikiri hawajuani.

Mara mume akafungua mdomo, na kuanza kuongea…

NB. Haya mazito yasikie tu….


WAZO LA LEO: Ndoa nyingi huingia kwenye migogoro kutokana na mambo madogo madogo ambayo yalitakiwa kuwekwa wazi na kujadiliwa kabla, ..wanandoa wanakutana, na kila mmoj alikuwa na yake huko nyuma. Kuna mambo ambayo yana umuhimu kuyaweka wazi, ili kila mmoja aelewe, lakini wengi wetu tunafichana. 

Mara kunatokea tatizo kutokana na yaliyopita, ndoa zinaanza kuingiwa na mitihani,uaminifu unaanza kupungua…maelewano yanakuwa hayapo tena chanzo ni kutokuwa wawazi. Ni muhimu mkiwa kitu kimoja mkaelezena ukweli wa mambo yenu, yaliyopita ni ndwele, myaongee kama ni kuyabeba mshirikiane, kama hayafai myasahau… msiwe na tabia ya kufichana mambo, mnafichana nini, wakati nyie ni kitu kimoja…
Ni mimi: emu-three

No comments :