Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, February 4, 2015

NANI KAMA MAMA-28


‘Sasa unakwenda wapi?’ aliulizwa mke wa familia, aliosimama kutaka kuondoka, bila kuwaangalia wenzake, akasema;

‘Nataka niwaachie nafasi, mkae nyie wawili muongee, mkubaliane, ili mjue jinsi gani ya kunihadaa…’akasema

‘Maana hapa mnajikanyaga, kila mtu anaongea lake, mimi ninachotaka ni ukweli, kama mlikaa mkpanga ili mlifanye hili kwa siri, ili tupate mtoto kwa njia hiyo, mimi hapa hatutaelewana …..’akasema huku akianza kuondoka, na mdogo wake akawa kama haelewi kinachoendelea, akamuangalai dada yake kama haamini kinachotokea, akasema;

‘Dada…mbona hivi,….kupanga nini na nani, ….dada mbona sijaongea ukweli kuhusu huyu mtoto, subirini niwaambie….’akasema mdogo mtu akitaka kuingilia kati, lakini dada yake alishaanza kuondoka kuelekea nje.

Shemeji mtu alipomuona shemeji yake akijaribu kusimama na mtoto, akamuonyeshea ishara ya mkono, kuwa atulia, akasema;

‘Hebu muache aende, naona ana mawenge yake kichwani, muache , wala usihangaike shemeji, wewe tulia, …’akasema shemeji yake lakini mdogo mtu akawa anamuweka mtoto kwenye sofa, ili aweze kusimama.

‘Huyu namfahamu shemeji huwa akikasirika anakuwa hivyo, muache akatulize hasira zake na ibilisi akimtoka tutaweza kuongea na kusikilizana vyema,…’akasema mume mtu, lakini mdogo mtu hakukubalia, akawa sasa kasimama akimuendea dada yake akasema;

‘Dada mtoto huyu ni moja ya chanzo cha yaliyotokea huko mjini…lakini pia ndiye muokozi wangu, kwani kama sio yeye ningelishafukuzwa kazi mapema…’akasema huku dada mua meshafiak mlangoni.

‘Dada nisikilize vyema kabla hujatoka ….kutokana na mtoto huyu, ndio maana nimekuja hapa, nimemlata huyu mtoto ili muweze kunisaidia, nahitaji sana msaada wenu, ili niweze kukabiliana na hilo lililotokea huko kazini,…. ‘
Akasema


‘Sasa dada kama hutaki kutulia nikawafahamisha kilichotokea huko kazini, basi,…ngojeni niondoke, najua nikifiak huko nikaambia….watakimbilia kunifukuza kazi, na hata kufungwa…’akasema na dada yake aliposikia kuwa kuna kufungwa, mddogo waka atakwenda kuungwa akasimama…

Tuendelee na kisa chetu

***************

'Dada, hii hatua niliyochukua ilikuwa haina hiari, …na kama ningekuwa na hiari basi nisingelikubali kulibeba hili jukumu, maana najua ni nzito kwa upande wangu, japokuwa kiubinadamu kila mtu mwenyenafasia anatakiwa kufanya hivyo, …’akaanza kuongea mdogo mtu.

‘Na kama ningelikuwa na mfanyakazi wandani na nafasi, nimejiandaa vyema, na  nikawa najimudu vyema, nisingelisumbuka kuja huku, lakini limetokea ghafla, sikutegemea, ndio maana nikafanya hivi....’akatulia kidogo.

‘Na kwa upendo wangu kwenu, nikachukua hatua hii ya kuja huku, niliamua kufanya hili pia nikijua kuwa haya ni majaliwa ya mungu, kwani ndugu zangu, walezi wangu, nimeishi nanyi, kiasi kikubwa mumeniwezesha nyie hadi kufika hapa nilipo,...nimeishi nanyi hapa,, nimewaona jinsi gani mkihangaika, kutaka muwe na mtoto kwa siku nyingi...'akatulia kidogo.

'Na, na, ..nakumbuka mlifikia hatua ya kusema, mnataka hata mtoto wa kulea…’akasema akimuangalai dada yake halafu shemeji yake kwa zamu.

‘Kwa hili pia mimi nimeona kama mungu kasikia kilio chenu, maana tumempata mtoto huyu hapa, …ndio maana nilipobebeshwa jukumu hili, kwanza nilipata shida sana, nililia sana,  nikijua sitaweza, lakini mungu akanionyesha njia, nikawakumbuka,... sikukata, tamaa, nikaona nije, nimlete huyu mtoto kwenu, sijui kama nimekosea…’akasogea pale alipomlaza mtoto huku akisema;

'Lakini kama mumebadili nia yenu, ya mungu mengi, huenda kuna lolote limetokea huku nyuma,  …hamtaki mtoto tena, basi niachieni mwenyewe,...japokuwa , nakiri kuwa mkiniachia sitaweza, niakuwa sina kazi...nitamleaje,..., litafanya hata kazi kamaitakuwepo tena, nishindwe,…'akatulia.

'Kiukweli, nitashindwa kushughulia mambo mawili kwa wakati mmoja, niliwaza niwapelekee wazazi , lakini nitawatesa,...ndio maana nikaja hapa, sasa ndugu zangu, sijui, kwanini,  …'akainama kama anataka kumchukua mtoto.

'Mimi najua huruma ya huko kazini, imewajia kutokana na huyu mtoto, kwani wakinifukuza kazi, ..huku nina huyu mtoto, atalelewaje, ….hamlioni hilo ndugu zanguni...naomba mliona kama letu sote....’ akakatisha maneno baada ya kusikia sauti nje.

‘Na-na-taka mtoto wangu…’ na sauti hiyo ikakatishwa na kilio cha mtoto, ambaye alikuwa kalala, lakini ile sauti kutoka nje, ilikuwa kama imemshitua huyo mtoto, na hapo hapo huyo mtoto akaanza kulia, dada mtu akageuka kumuangalia yule mtoto anavyolia, akataka kwenda kumchukua,lakini akasita. Na wakati huo mdogo mtu alikuwa kasimama pale pale, akishinuka vile alivyoaka kumchukau mtoto, na yeye alishiuka aliposikia hizo kelele huko nje.

Mtoto aliendelea kulia , wakati huko nje nako, wimbo unaendelea;
‘Na-na-na maka mtoto wangu…’

‘Mtoto analia huyo mpe maziwa yake….’akasema dada mtu huku akilini akiwa bado hajaelewa, akili yake bado ina mawimbi,..hasira na wivu... anahisi kuna mchezo kachezewa, lakini kilio cha mtoto, kikamjaza huruma, na huko nje, kelele zikawa zinaendelea;

‘Na-na-nataka mtoto wangu…’ kukawa kama kuna ghasia sasa huko nje.

Dada mtu aliposikia kilia cha yule mtoto kikizidi, akili yake ikampeleka mbali, akawa anakumbuka jinsi gani mama yake alivyokuwa akihangaika pale mdogo wake huyo alipokuwa akilia, hasa akiwa mgonjwa, mama alidiriki kumbeba na kitenge,au kanga, hata kama anapika,..au anachota maji,..leo hii leo, mtoto analia, mama …yake ambaye anahisi ni mdogo wake hataki kumbeba..huruma ikamuingia.

Mdogo mtu akawa kasimama bado akimuangalia dada yake, akionyesha kukata tamaa, hakuwa anajali sana kile kilio cha mtoto, kwani vilio kama hivyo anavisiia sana huko huko hospitalini, alijali kuhakikisha, anapata mlezi wa huyo mtoto.

Dada mtu akaona hawezi kuvumilia, mtoto anavyolia, anahitaji huruma ya wazazi, akasogea kwa hatua za haraka hadi pale alipolala mtoto, akamuinua yule mtoto na kumuangalia usoni, …..hapo! alipoiona ile sura,akili ikabadiliak tena,, hasira, wivu....ile sura, haina tofauti na mume wake,….hasira , chuki na wivu…hata hivyo, huruma ikamjaa, akaanza kumbeleza yule mtoto, huku akisema;

‘Jamani mtoto anahitaji nyonyo, kwanini humnyonyeshi, kwanini unatumia chupa, una matatizo gani, mpaka ushindwe kumnyonyesha mtoto, kwani wewe sio ndio mama yake…’akasema dada mtu akimkagua mdogo wake kwa macho, juu chini, ,..alivyovaa asingeliweza kugundua lolote, na mdogo wake akitabasamu akijua dada mtu anasema utani yeye akasema.

 `Dada kwa jinsi ilivyo, toka sasa hivi wewe ndio mama yake,..unaona hata mtoto kanyamaza, anajua kafika sehemu sahihi, kuanzia sasa,..na ilivo huko nilipotoka ni kuwa, wewe ulijifungua huko mjini, katika hospitali hiyo ninayofanyia kazi,…’akasema mdogo mtu akionyesha uso uliodhamiria.

Ndugu zake hao, wakamtolea macho, kila mmoja akizama kwenye hisia zake

**********

‘Eti nini…?’ aliyeng’aka kwa sauti ni shemeji mtu, huku mkewe akibakia ameduwaa, huku akimuangalia mdogo wake kwa macho yenye hasira, na kusema;

‘Una maana gani kusema hivyo, umefikia hatua ya kufanya hivyo, kunidharau kiasi hicho, kuwa mimi sitaweza kuzaa tena, au…mlilipanga hili na shemeji yako, au…ndio iliyotokea huko…hapana sema ukweli…..’akawa anaongea huku katoa macho ya hasira.

‘Ndugu zanguni, hili limetokea kwa miujiza ya mungu, najua fika mnahitaji mtoto, au sio..sasa huyu ni mtoto wenu…mchukueni mumulee…mungu kasikia kilio chenu kupitia mimi, ndio maana akanionyesha njia ya kufanya hivi ….’akasema.

‘Shemeji,..unataka kusema huyu sio mtoto wako…au umefanya nini huko shemeji, ulichukua mtoto wa mtu ili utupatie sisi..ndio maana kukatokea matatizo...., au ulimzaa ukamtelekeza, ndio maana kazini wakaamua kukuchukulia hatua..…hebu tueleze vyema, ?’ akauliza shemeji mtu.

‘Ni kweli, mtoto huyu amatokana na tatizo lilitokea huko mjini, hilo ni kweli sikatai…lakini jingine ni kuwa, mtoto huyu kazaliwa...alipozaliwa, mmmh, akawa hana baba hana mama, baba na mama yake ni nyie , kama munahitaji taratibu za kisheria, wenzangu wamesema wataziandaa, kuanzia sasa huyu ni mtoto wenu, mnataka niwaambieje …’akasema.

‘Na-na-nataka mtoto wangu,……nataka mtoto wangu…’kelele sasa zikasikika mlangoni.

‘Anataka mtoto wake??..ni nani huyo anaimba hivyo, eti anataka moo wake, huyo mtoto upo wapi, humu ndani..mbona anaimbia haapa...ndio huyo mama mliyesema haeleweki alipotoka, jamani mnatakiwa muwe makini, hasa, kwa hiki kiumba cha wau....….’akasema huyo mdada akisikiliza kwa makini maneno hayo.

Baba mtu akataka kwenda nje kuwafokea hao wanaoleta fujo huko nje, lakini akasimama pale aliposikia mke wake akisema;

‘Bado hamjanidanganya...siwaelewi kabisa,...acheni dhambi..unajua mtakuja kulaaniwa na mungu, unasikia kumfanyia hivi mtoto mchanga kama huyu..ambaye hajui hiki wala kile ni dhambi kubwa sana…’akasema dada mtu.

‘Ni kweli dada, ndio maana hata mimi ikaniingia huruma, nikaona nimlete huku, vinginevyo, unafikiri mimi ningelifanya nini, sijajiandaa kuwa na mtoto….’akasema.

'Wewe wakatii unafanya hayo madhambi hukujua atatokea hivi, mtu umesoma, halafu unasema hujajiandaa,...hebu muangalia mtoto anavyohangaika kutafuta kifua cha mama yake, akishike, ahisi yupo karibu na mama yake, leo hii mnaamua kufanya hivyo,..mdogo wangu, hata kama ni dhambi.. ya kuzaa…, imeshafanyika, …hili mnalotaka kufanya kwa sasa utalaaniwa ushindwe kuzaa baadaye,…’akasema dada mtu.

‘Dada una maana gani kusema hivyo, mbona sikuelewi…?’ akauliza mdogo mtu akiwa hajamuelewa dada yake ana maana gani akabakia ameduwaa, huku akimuangalia dada yake.

‘Kwanini unamkataa huyu mtoto, mpaka ufikie kutafuta mtu wa kulea…sawa mimi nakubali kubeba jukumu hilo, lakini sio kwa mtindo huo…au umefanya hivyo, eti…kwasababu baba yake ni mume wa dada yako, unaogopa aibu,..ukumbuke hilo utalikwepa hapa duniani, lakini dhambi yake hutaikwepa huko mbele, maana hujaitubu, ukasema ukweli…’akasema dada mtu.

‘Dada..hebu…!’ mdogo mtu akawa anasita akijaribu kuyaweka mawazo na hisa zake sawa sawa, akasema;

‘Dada, mbona unanichanganya, dhambi gani hiyo nimeifanya mim,..mimi sijamkataa huyu mtoto…’akatulia akitikisa kichwa.

'Hujamkataa...kweli, ...hujasema ukweli ulivyo...unajaribu kutuhadaaa..au kunihadaa mimi...'akasema dada mtu.

‘Kwani dada una maana gani,…dada kama ni dhambi,..sio mimi, …sikutegema hili kabisa, sikujua litatokea,…, ndio maana nimemchukua huyu mtoto na kuja naye huku, …'akasema na dada mtu akakunja uso, huku akionyesha uso wa kutokumuelewa ndugu yake huyo.

'Sasa dada, wewe ulitaka mimi nifanye nini…’akageuka kumuangalia shemeji yake, ambaye alikuwa katulia huku kashika shavu, akionekana kuzama kwenye mawazo mazito, na mdogo mtu alipoona shemeji yake hasemi neno akagauka kumuangalia dada yake na kusema;

'Kwani ulilazimishwa..si mlipanga..au...kwanini hutaki kusema ukweli, ?' akauliza dada mtu

‘Dada…, ndio maana nimekuja naye huku, tulipange vyema,...sasa dhambi hiyo ya nini…nataka nyie mnisaidia hili, ili nikirudi huko niwaambie kuwa mtoto yupo salama, na wazazi wake ni nyie, wasiwe na shaka na hilo,…nitawandikishia cheti cha kuzaliwa mtoto kwa majina yenu, ningeliamua moja kwa moja kuandikisha, lakini nimeona nije nipate rizaa yenu kwanza..’akasema.

‘Haya sasa niambie ukweli…maana umesema hujamkataa, lakini bado unataka kuuandikisha sisi kama wazazi wake, mimi sioni kuwa ni  shida,..kwani baba yake yupo hapa, japo anaye anajaribu kujifanya haelewi,…, kamuandikishe tu, sio shida...., ila mama yake aendelee kuwa ni wewe, unadike jina lako wewe,...usimkane kiumbe wa watu…mimi nitakuwa maam mlezi, kama ni hivyo....lakini nataka ukweli kwanza...’akasema.

‘Dada, mimi sijamkana kiumbe wa watu, bado atakuwa mtoto wangu, kwa vile pia nyie mumemkubali kuwa ni mtoto wenu.., ila baba na mama yake ni shemeji na wewe..mimi sijakataa majukumu, tutasaidiana kwa hili…kinachohitajika kwa sasa ni mlezi wa karibu, na nimeona kuliko kuwa mchoyo, niwaletee nyie, maana mumekuwa mkitafuta mtoto kwa siku nyingi…’akasema.

‘Sawa baba yake yupo atamlea usiwe na shida,..hilo usitie shaka ..tatizo ni wewe hutaki kusema ukweli,....sijui kwanini moyo haukusuti,… wewe unayezaa, halafu unamkana mtoto wako, una tofauti gani na hao wanatupa watoto wao….., hapo ndio hatuelewana, ..’akasema na mdogo wake, akakunja uso kwa kutahayari, akatikisa kichwa halafu akasema;

‘Dada mimi sijakuelewa, mimi-mi-kumzaa huyu mtoto!…hapana, ….labda hujanielewa vyema,…’akasema huku akionyesha kwa mikono.

‘Au …hatujaelewana,…huyu mtoto, hana baba wala mama,…nimeamua kuchukua jukumu hilo kwa niaba yenu, hapo sijui tuemelewana, dada mimi naona bado unajichanganya, dada kiukweli huyu mtoto hana mzazi, nielewe hivyo, mtoto hana baba, wala mama,….hana baba wala mama, narudia tena,..mtoto huyu kuanzia leo, wazazi wake ni nyie...’akasema.

‘Eti nini, kuna mtoto anazaliwa asiwe na baba au mama, hebu ondoeni huo uchuro wenu, ina maana wewe umeshakufa,…sitaki kusikia hilo, hebu wewe baba mtu chukua jukumu hilo, sema ukweli, yaishe…mlivyokutana na mdogo wangu mkalipanaga..hebu muangalieni huyu mtoto..hata umuulize nani, atasema huyu mtoto anafanana na mume wangu….sasa labda uniambie mengine….’akasema mke mtu akikwepa kumuangalia mke wake.

Mume mtu akacheka kidogo, halafu akamgeukia shemeji yake, na kusema;

‘Unajua shemeji hujamuelewa ndugu yako,…yote hayo unazunguka, na unazidi kumchanganya dada yako…sikiliza mimi nimshakuelewa sana, na jambo ulilolifanya ni zuri sana, kwani umeonyesha ubinadamu, cha muhimu, labda ungetuelezea, ilikuwaje kwa mama yake, amekufa…au ilikuwaje…’akasema mume wa familia.

‘Sawa mimi ngoja nitoke nje, na huyu mtoto nyie endeleeni kuongea mliweke sawa mkubaliane….’akasema dada mu akitaka kuondoka na mtoto.

‘Hondoki mtu hapa,..unasikia, wewe kama mke wangu, utabakia hapa, usikie hicho ninachotaka kukiongea, naona unajivika mambo yasiyokuwepo, kaa pale kwenye kiti,  usikie hayo ninayotaka kuaongea,…’akasema.

Mke wake, kwanza akasita,a kamuangalia mdogo wake, akatikisa kichwa, na machozi yakaanza kumtoka, mdogo mtu akawa anakunja uso wa kutahayari, akawa haelewi..akawa anawaza hili na lile.

‘Hivi dada yangu ana maana gani, ina maana anahisi kuwa mtoto huyu ni kwangu, nimemzaa mimi, aah, haiwezekani, mmh, haiwezekani, dada yangu mwenyewe asiniamini, imekuwaje, ..hapana dada yangu hawezi kufikia hapo..lakini kwanini anasema mtoto anafanana na mume wake….hapana dada yangu hawezi kunishuku hivyo, hapana…’akawa anajiuliza maswali mengi kichwani..na kujikuta akishika hata kidevu….

Na dada mtu bado alikuwa kasimama..mara akaanza kuzivuta hatua.. moja  mbili, akitaka kuelekea nje…Mumewe akamuangalia, kwa hasira akasema;

‘Wewe mwanamke…’akajikuta ametumia lugha ambayo hajaiwahi kuitumia kwa mke wake, maana siku zote ni `mke wangu, mke wangu..

‘Umenisikia ….ukitoka nje, basi …litakalotokea usije kunialamu…’ilikuwa sauti ya mume iliyoonyesha dhamira ya kweli…


NB: Haya haya, yasikie kwa wenzako tu,…ndoa ina mitihanai yake,..hebu jiulize, mtoto anafanana kabisa na mume wako…na aliyemshika ni mdogo wako,..kaja naye hivihivi,…halafu analeta hadithi kama hiyo, wewe utafanyaje,..utakubali maelezo kama hayo, jiweke kwenye sehemu yake ndipo utaona ukweli wa huyo mama.



WAZO LA LEO: Kila jambo linapotokea, liwe na heri au la shari, ujue kuna sababu, kwa akili ya kibinadamu, tunapenda kukimbilia yale yanayonufaisha au kutosheleza nafasi zetu. Sio rahisi kukubali lile lenye kukizana na matamanio au hisia zetu, hasa tukiona kuwa tutashindwa. Ukweli ni ukweli, hata tukiukana utabakia kuwa ni ukweli. Mungu ndiye mpangaji na anajua kila jambo.

Ni mimi: emu-three

No comments :