‘Sasa sikiliza shemeji, usiwe na shaka, kwa vile wanataka kukaa kikao kulijadili hilo, wewe subiri kwanza, usijiweke roho juu, kwani huna hatia, kutokana na maelezo uliyotupa, hilo lingetokea kwa yoyote…sidhani kwamba wao watachukua hatua kama hiyo ya kukufukuza kazi…na polisi watategemea maamuzi ya kazini kwako, kazini kwako wakiona huna hatia sizani kama polisi watashinikiza kuwa una kosa….’ Akasema.
‘Ndugu zanguni, polisi ni polisi,…na kosa lenyewe sio dogo, kwahiyo hata kama kazini watasema sina kosa, ..je kuna ufumbuzi gani wa tukio lenyewe,…tunachoombea ni uchnguzi ulipatie ufumbuzi hilo tukio kwa haraka…na ikipita muda mrafu, sizani kama nitakuwa na kazi…..’akasema, na maneno hayo ya mwisho yalimshitua sana mke wake.
Mke mtu alifikiria mbali hali yao na wazazi wake ambao walishaona kuwa binti yao huyo atawasaidia kwa vile ana kazi, wao walishapata ahueni, kuwa mshahara anaopta huyo ndugu yake unawasaidia na wazazi wake, kwani wao kipato chao wanachopata ni kidogo, wasingeliweza kuwasaidia wazazi wake, sasa mdogo mtu ndio huyo kafukuzwa kazi, na huenda kutahitajika chochote ili kuizima hiyo keso, watapatia wapi pesa…
Mke wake akamshika mumewe bega, na mume mtu akageuka kumuangalia mkewe na alichoona machoni kwa mkewe ni machozi, hali hii hakuweza kuivumilia, na kabla hajajibu alichoulizwa kwenye simu, kwani mpigaji simu aliuliza swali;
‘Kwani siku hizi kuna shule ya watoto hapo karibu….’akaulizwa kwenye simu na shemeji mtu, akawa anaondoa mkono toka mlangoni, alipokuwa kashikilia, nia yake ilikuwa amfute machozi mkewe, lakini mkewe akawa keshageukia upande mwingine.
Mkewe alimuonea huruma mume wake, kwani anajua kipato chao, anajua jinsi gani mumewe anavyohangaika usiku na mchana kuhakikisha wanakula,…lakini kwa upande mwingina akwa anamkumbuka mama yake alivyoteseka kumlea, akakumbuka enzi mama yake bado mama, hjazeeka, akiwa kambeba mgongoni, hapo akaanza kulia huku akisema;
‘Nani kama mama,…sasa mama nani atawasaidia, baba naye ndiye haishi kuumwa…wakisikia binti yao kafukuzwa kazi wataumia sana,…ooh, hili sasa litamzidishia mumewe wangu mzigo mnzito asioweza kuubeba. Hapo bika kujua akamshika mume wake begani kama kumonea huruma, na alipoona mumewe kageuka, akajigeuza haraka upande mwingine ili sione machozi yaliyokwisha kujaa machoni.
‘Ni watoto tu sijui wametoka wapi na kuna…..’akasema huku anageuka kuangalia nje, pale alipoona mkewe kageukia upande mwingine na alipogauka tu kuangalia nje, akakutana na kauli kutoka kwa mwanamama aliyekuwa kajifunika usoni, akisema ;
‘Na-na-mtaka mtoto wangu…’
‘Mtoto gani….?’ Akauliza huyu mwanaume, na huko kwenye simu akasikia sauti ikisema;
‘Mtoto wa kiume…’shemeji mtu akasema.
‘Na-nataka mtoto wangu, watoto wakajibu kwa shangwe…na akawa kama kachanganyikiwa, maana huku shemeji yupo kwenye simu, huku huyo mwanamke wa ajabu anadai mtoto wake…sijui ni mtoto gani, akasema kumjibu shemeji yake;
‘Nilikuwa naongea na hawa watu huku, ….unasema..?’ akauliza na huku kelele zikizidi na kukawa hakuna maelewano mazuri, maana sauti zawatoto nje, zikawa zimezidi, na baba mwenye nyumba akaona ni kero akampa mkewe simu aendelee kuongea na ndugu yake, na mkewe alipoishika ile simu kwa Bahati mbaya akawa kashika kitufe cha kuzimia simu, bila kukusudia simu ikawa imezima kukawa hakuna mawasiliano hata alipoweka sikioni hakusikia kitu.
Akaiangalia huku akionyesha mshangao, akasema;
‘Mbona hakuna mawasiliano…’akasema na mumewe kwa muda huo alishatoka nje, mke mtu akajaribu kuipiga ile namba kwanza ikasema unayempigia anaongea, na alipopiga tena ikawa haipatikani.
Mume wake kwa hasira akawa katoka nje, kuwatimua hawo watoto na alipotoka nje, hakumuona yule mama, waliokuwepo hapo ni watoto wakipigana, na wenzao wakiwashanglia na kuwashibakia waendelee kupigana,…ikabidi kuingilia kati kuwaamulia hao watoto wanaopigana.
‘Hivi nyie watoto mnatoka wapi, na kwanini mnakuwa hamna adabu…angalia sasa mnapigana mumeumizana..mnataak niwachape…?’akasema akimuona mtoto mmojawapo aliyekuwa akipigana akitoka damu puani.
‘Ni huyu hapa mchokozi, ….’akasema yule aliyemuumiza mwenzake.
‘Ndio umuumize mwenzako kiasi hichoo..’akasema
‘Kanianza yeye mwenyewe ..’akasema kujitetea
‘Haya wewe njoo hapa niambieni kwanini mnapiagana..’akasema akimuita yule aliyeumizwa,.
Wale watoto wakaanza kujielezea, kuwa walikuwa wakimsogelea huyo mama kuitikia wimbo, na huyo mwenzake akawa anamvuta shati kwa nyuma alipomuuliza kwanini anafanya hivyo, akapigwa teke nay eye akajibisha, na ndipo wakaanza kupigana.
‘Kwanini mnataka kumuona huyo mama, hamuoni kuwa mnamsumbua huyo mama wa watu, na huyo mama yupo wapi , anatokea wapi…?’ akajikuta anauliza maswali mengi, akigeuka huku na kule kuangalia kama anaweza kumuona huyo mama, na ghafla wale watoto wakaondoka mbio, hata wale walikuwa wakipigana wote wakawafuatia wenzao huko walikokimbilia, na sauti ya huo wimbo wa aina yake ukawa unasikika kwa mbali;
‘Na-na-mtaka mtoto wangu…’
Huyu mwanaume akawa anawaza sana kuhusu huo wimbo au sijui ni kibwagizo kina maana gani;
‘Mbona wimbo na kauli ya huyo mama vinafanana,…eti anataka mtoto wake, mtoto gani huyo….?’ Akawa anajiuliza, huku akirudi ndani na alimkuta mke wake akiwa kashikilia simu, na machoni alionekana han raha;
‘Mke wangu vipi, ulikuwa unalai, sasa unalia nini tena..?’ akasema
‘Wewe hujiu tu mume wangu, kama wamemfukuza mdogo wangu kazi , wale wazee wangu watalelewa na nani. Mdogo wangu alipopata kazi, ilikuwa furaha kwetu, baada ya kujitolea kumsomesha, akawa ndiye tegemeo la wazee wangu, unaona jinsi gani wazee wangu walivyochoka, mazao hakuna, unafikiri hali yao itakuwaje, na mimi nakuonea huruma wewe mume wangu maana unabeba jukumu kubwa zaidi ya uwezo wako, je kipato tunachopata kitaweza kuwasaidia na wazee wangu….’akasema
‘Mke wangu yote ni kudra ya mungu,..na sioni kwanini ufikie hatua hiyo ya kulia na kukata tamaa, hawajasema kuwa shemeji kafukuzwa kazi, kwani bado wanachunguza, na kama alivyosema shemeji ndio hivyo nilivyoelewa mimi, atarudishwa kazi tu…’akasema
‘Kama ni wakurudishwa kazi, kwanini asema anakuja huku, kwanini kuna uchunguzi wa polisi, ina maana kuna ….kasababisha kifo au,..na kama ni hivyo mpaka uchunguzi ukamilike, ni miaka, nijuavyo mimi, kwahiyo hapo hana kazi, ndio maana anakuja huku kuishi nasi hapa tena,…si ndio maana yake…’akasema mkewe.
‘Kasema kuna jambo anataka kuja kujadiliana nasi, ambalo wamekubaliana huko, ….na ni muhimu, hatujui ni jambo gani, cha muhimu tuvute subira mpaka akifika, ..na sijui anakuja lini, akifika tutajua la kufanya, hayo mengine tumuachie mungu,.usianze kujitwika mzigo kabla haujatua kichwani...’akasema mume mtu.
‘Haya mume wangu nimekuelewa,….’akasema akimkabidhi mumewe simu yake, na mumewe akataka kupiga kuongea na shemeji yake tena ili apate ufafanuzi, lakini mkewe akasema;
‘Unataka kuwapigia tena?’ akauliza mkewe, akitaka kumuambia kuwa kajaribu kupiga lakini hapatikani tena huyo ndugu yake.
‘Ndio ili niweze kuelewa vyema, hawa watoto wameleta zogo hapo nje, wamefikia hadi kupigana, na kuumizana, sijui kuna nini hapa mtaani leo, ….’akasema
‘Nahisi ni huyo mama nilyekuambia mchana, nahisi ndiye huyo huyo watoto wanamfuatilia anapoimba huo wimbo wa ajabu..’akasema
‘Ndiye huyo alikuwa kalala hapo upenuni mwa nyumba yetu?’ akauliza mumewe akonyesha mshangao.
‘Unasema alilala hapo upenuni mwa nyumba yetu?’ akauliza mkewe akionyesha hamsa na mshangao, uso ukimeta meta kama kasikia jambo la furaha.
‘Ndio…sijui ndiye huyo unayemzungumzia au yupo mwingine, ila ….mmmh, sijui sijawahi kuona ….mmh, kwani unajua anatokea wapi..’akawa anaongea mume matu akionyesha kama kushangaa.
‘Atakuwa huyo huyo, hakuna anayejua katokea wapi, na kila mmoja anaongea lake, na kuna kauli kuwa ni mama wa kutoka mbinguni, kaja kuleta neema, na akifika kwako ujiandae kupokea neema…’akasema na mumewe akajizuia kucheka akatabasamu na kusema;
‘Akifika kwako kwa vipi, mtu mwenyewe anadai kuwa anataka mtoto wake… kama analeta neema mbona mwenyewe hana neema, ….achana na imani hizo’akasema
‘Huo ndio wimbo wake, kuwa anataka mtoto wake, na akisema hivyo na wewe unatakiwa kuitikia, usipoitikia utaikosa hiyo neema, ulitakiwa na wewe uitikie hivyo hivyo….’akasema
‘Niitikie vipi…?’ akauliza mumewe huku akionyesha uso wa kushangaa.
‘Anavyoimba yeye, hayo maneno,…na-nataka mtoto wangu, na wewe unaitikia hivyo hivyo. Na mume mtu akajikuta akiitikia, kama kuyafuatilia yale maneno
‘Na-na-na taka mtoto wangu….ndio unapata neema ukiitikia hivyo’akasema na kutabasamu, na mkewe naye akatabasamu kwa mara ya kwanza tangu itokee hiyo sintofahamu siku hiyo, na kabla hawajaendelea kuongea mara wakaisikia mngurumo wa gari ukikaribia hapo kwao, na wote wakatega sikio.
‘Nasikia kama mngurumo wa gari….’akasema mke mtu
‘Yah, …labda kuna mtu kakosea njia, sijui huku anafuata nini,…..’akasema akielekea dirishani kuangalia nje na mara gari likafika na kusimama nje ya nyumba yao, wakajikuta wanandoa hawa wakiangaliana
‘Mhh, tatizo..nenda wewe…sio polisi hao,’akasema mke mtu
‘Kwani unajua ni akina nani,polisi, kwanini, ooh, siwezi kujipeleka tu, subiri kwanza….’akasema mume mtu na mara mlango ukagongwa
NB: Ni nani hao....kuna nini ? tuwepo pamoja
WAZO LA LEO: Kila ukila na kulala kwa starehe, kumbuka kuna ambao hawajapata chakula, hawana cha kula, na hata usingizi hawaupati kwasababu ya njaa. Kila ukiendesha gari lako kwa furaha, huku ukiongea na simu yako kuwalekeza wafanyakazi wako wa nyumbani cha kufanya ukumbuke kuna ambao wanatembea mwendo mrefu kwa miguu, miguuni wamevaa ndala zilizochakaa, wapo kwenye jua kali, kutafuta angalau tonge moja la kupoteza nja, wanatembea mwendo mrefu kutafuta tiba, kutafuta maji, kutafuta….angalau na wao waweze kuishi maisha bora...kwao ni ndoto.
Kila ukihangaika kutafuta shule gani ya kimataifa ya kuwapeleka watoto wako, bila kujali gharama kubwa ukumbuke kuna watoto wanakalia mchanga, wanaogombea kitabu kimoja, hawana walimu,…wansoma huku wanapiga miayo ya njaa, ambao mwisho wa siku wanapambanishwa na watoto wako wanaosomea shule za kifahari, ili kupata mtoto aliyefanya vizuri kitaifa.
Ukumbuke kuwa, pesa ulizofisidi, pesa uliyokwepesha kulipa kodi,....hizo zinatokana na jasho la hao wanyonge…ambao leo hii wanateseka wao na watoto wao, Tujue na tukumbuke kuwa na wao wana haki sawa kama ulivyo wewe na watoto wako.
Ni mimi: emu-three
No comments :
Post a Comment