Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, January 27, 2015

NANI KAMA MAMA -24


‘Mke wangu  ni kweli nilipokea simu kutoka kwa mdogo wako...’ mke wake kusikia hivyo akatega sikio.

‘Akakuambiaje...kuna nini kimetokea, msiba ...na msiba ni-ni wa nani....?’ akaanza kuuliza maswali mfululizo.

‘Msiba...unasema msiba,...mke wangu vipi, mbona hivyo.....mdogo wako kanipigia simu, na ndio nilikuwa najipanaga kukuambia…, lakini naona mwenzangu una fikira nyingine  kabisa...hilo la simu nitakuambia usijali, ….’akatulia

‘Uta-niambia..kwanini….’mke akaanza kulalamika.

‘Mimi, nina mazungumzo mengine mazuri, muhimu sana, nataka tuyaongee kwanza….’akasema mume mtu, na kumfanya mkewe azidi kuchanganyikiwa.

‘Mume wangu vipi, mbona sikuelewi…., mimi nahisi nyie mna jambo mnanificha hutaki kuniambia…wewe umepokea simu kutoka kwa mdogo wangu, na inaonyesha ana matatizo, na ni kweli maana aliponigia japo ilikatika, lakini nilimsikia akilia, hapo inaashiria nini,...halafu wewe unasema halina umuhimu..hata sikuelewi...’
Akasema

‘Mke wangu yote yana umuhimu,...ila nilitaka tuongee hili linalokusumbua kila siku, ili tulitafutie ufumbuzi....’akasema

‘Lii hilo muhimu kuliko hilo linalomtoa mtu machozi,…Ina maana hilo la mdogo wangu sio la muhimu wakati kwa masikio yangu nimesikia akilia...mume wangu kuna kitu gani unanificha..kuna taarifa gani, iliyomfanya mdogo wangu afikie hadi kulia, na wewe unaiona sio muhimu …hivi unajua najisikiaje hapa nilipo, .., au unataka kupoteza muda tu, kwa vile unaogopa nitazimia,..hapana  mimi sasa ni mtu mzima, akili imepevuka, wewe niambie , tena haraka, mdogo wangu alipokupigia simu kakuambia nini…au kuna nini…niambie haraka..’akasema sasa akionyesha kukerwa.

‘Mke wangu ni kweli...., shameji kanipigia simu, kwanza alisema alikupigia wewe simu, lakini simu yako ikakatika kabla hajakuambia…’akaanza kumuelezea.

‘Ehe akasemaje, kuna kitu gani kimetokea, kuna msiba...na kama ni msiba ni wanani..usinificha tena mume wangu, utaniua kwa kusubiria...’akasema

Mume wake akamuangalia akionyesha wasiwasi, akawa anajiuliza ni kwanini mkewe kafikia kusema mambo hayo ya msiba, akaona asipoteze muda, amuambia tu kuhusu aliyoambiwa na shemeji yake na hilo lake lisuburie...

Kisa kinaendelea...

**********

Mume akaona hana ujanja, kile alichokuja nacho hakitasikilizwa, akaona amuhadithie mke wake kuhusu simu aliyoipokea kutoka kwa mdogo wa mke  wake, na wakati anataka kumsimulia mke wake, mara kukasikika kelele huko nje, kelele za watoto wakiimba, wimbo ule ule, na mume akashindwa kuvumilia, akasema kwa sauti;

 ‘Nyie watoto huko nje, sitaki kelele hapo nje kwangu, kwanza ondokeni hapo nje mkaimbie sehemu nyingine...’akasema kukatulia kidogo, lakini kabla hajapanua mdomo kuanza kumuelezea mke wake, mara kelele zikaanza tena, na sasa ilikuwa kama kuzomea unajua watoto tena.

Mume mtu hakustahimili, akasimama kwa hasira huku akiwa kakunja uso,na mkewe akamwambia;

‘Hao ni watoto tu, waache wataondoka, usiwafukuze, mimi inanipa raha kuwasikia, najishi na mimi mtoto wangu yupo hapo nje,…muhimi niambie mdogo wangu kakuambia nini...’akasema lakini mume akawa keshasimama na kuelekea mlangoni, akafungua mlango akiwa na hasira.

‘Hivi nyie watoto hakuna kwenu, mimi nimefika nyumbani nipate kupumzika na kuongea mambo yangu na mke wangu.....nyie mnatoka huko makwenu kuja kutusumbua,....’akawa anaongea huku kashikilia mlango nusu umefunguka akiwa katoa kichwa nje.

Kimiya kikatawala, na watoto wengine wakikimbilia barabarani, na wengine walibakia wakikaidi hilo agizo, na hapo mume huyu akaona atoke nje kupambana nao

Akafungua mlango, na kuanza kusema kwa hasira

Nyie watoto hebu muwe na adabu kidogo..kama mnataka kupiga makeleeni yenu m
Nendeni barabarani, sio hapa kwangu...’ akasema huku keshatoka nje kabisa, akiwa anawaangalia wale watoto waliosimama karibu na barabara lakini macho yao yalikuwa pale pale, na hamasa ya mume huyu ikamjia kuona ni kitu gani wanakigangalia.

Taratibu akageuza kichwa, akaona mtu mwanamke kajilaza pembeni ya nyumba yake,…yule mama alikuwa kajifunika usoni, na alionekana kama anachungulia kwa kupitia sehemu ndogo aliyoiacha ya machoni

Yule mwanaume, akawa sasa ana hamu ya kufahamu huyo mwanamke ni nani, akageuka sasa kumuangalia yule mwanamke, na yule mwanamke aliyelala pale kuona hivyo, akawa anajizoa zoa kutaka kusimama, na mara sehemu kubwa ya uso ikabakia wazi….mwanamume akashituka, na kubakia kukodoa macho ….ajabu kabisa…..!

‘Ni nani huyu mbona sijawahi kumuona…’akajikuta akisema, mara akashitulia na kelele za watoto ambao walishasogea tena karibu na nyumba yake, sasa wakimuangalia yule mama.

Huyu mwanaume akageuka kutaka kupambana nao, baada ya kuju akuwa watoto hawa wanamsumbua huyo mama mgeni, akawaambia;

‘Sitaki nimuone mtoto wa mu hapa, naona hatuelewani,….’akachukua fimbo, na hilo likasaidia kuwafanya watoto wale wakimbie, na wakati anafanya hivyo mara akasikia sauto nyuma;

‘Nata-nata, nataka, mtoto wangu’....

Akageuka, na kugundua kuwa sauti hiyo ilitokea kwa yule mama, akamwangalia na sauti hiyo ilijibiwa na watoto waliokuwa karibu;

‘Nata-nata, nataka, mtoto wangu’....

‘Unataka mtoto wako…yupo wapi huyo mtoto wako….?’ Akauliza na kumsogelea huyo mama, yule mama alipoona huyo mwanaume anamsogelea, akasogea nyuma kama anaogopa, na yeye kwanza akasimama kwa mshangao, akasema;
‘Wewe ni nani …..sijawahi kukuona eneo hili?’ akauliza

‘Nata-nata, nataka, mtoto wangu’....akasema huyo mama, na mara watoto wakadakia

‘Nata-nata, nataka, mtoto wangu’....

Mwanaume huyu akabakia na mshangao, akijiuliza kuna nini kinachoendelea kati a huyu mama na hawa watoto, na kwanini huyu mama anasema hayo maneno; `anataka mtoto wake..’

Akamsogelea huyo mama, ili amchunguze vyema, yule mama alipoona mtu  huyo anamsogelea, akageuka na kwa haraka, akakimbilia barabarani. Yule naye hamasa zikawa zimemuingia alitaka kumfahamu huyo mama ni nani, naye katoka na kuanza kumuatilia yule mama, na yule akawa anatembea  na kugeuka geuka nyuma kumuangalia huyo mwanaume.

Yule mama alipoona huyo mwanaume anamfuatilia akaanza kukimbia kidogo kidogo, na huyu mwanaume akaongeza mwendo, na hiyo ikamfanya huyo mama kukimbia kabisa, na hapo watoto wakatokea na kuanza kuimba …

‘Nata-nata, nataka, mtoto wangu’....

Yule mama aliposikia wale watoto wakianza wao kuimba akasimama, na huyu mwanaume akamkaribia, huyu mwanamke akasubiri hadi huyo mwaume alipomkaribia, huyu mwanaume akamsogelea nia ni kutaka kuion sura ya huyo mwanamke, yule mwanamke akasema;

‘Nataka mtoto wangu…..’akasema

‘Mtoto gani…?’ akauliza huyo mwanaume

 ‘Nimesema; nata-taka mtoto wangu…’yule mama akasema kwa ukali na kumfanya huyo mwanamke ashituke, mara watoto wakaja na kuanza kumzonga yule mama na yule mwanaume akaanza kuwafukuza, na watoto wengine vichwa maji wakafanya kama mchzo, katika ile hali ya kufukuzana na watoto akawa kaachana na yule mwanamke, sasa alipoona watoto wamekwenda mbali, akageuka ili aweze kuongea na yule mama.

Yule mama hayupo, kapotea…akageuka huku na kule, hakuona dalili ya huyo mama, akabakia mdomo wazi, ….
‘Haiwezekani, huyu mama alikuwepo hapa, katoweka vipi..?’ akawa anajiuliza sasa akageuka kutaka kuwauliza hao watoto huyo mama kaenda wapi, lakini hata watoto nao wakawa hawapo karibu, huyu mwanaume alipoona hivyo akageuka kurudi nyumbani kwake

Alipofika nyumbani kwake, akamkuta mkewe akiwa bado kainama vile vile akasema;

‘Ni ajabu kweli....sijawahi kuona mwanamke kama huyo...ni mwanamke wa ajabu sizani kama ni binadamu….’akasema na mkewe akawa kama kashituka kutoka kwenye dimbwi la mawazo akauliza;

‘Vipi mume wangu wamesemaje huko hospitalini.....hebu niambie haraka, sitaki kusikia jambo jingine zaidi ya hilo,....’akasema

‘Mke wangu, leo sijui kuna nini, ehee, unasema kuhusu hiyo simu, usiwe na shaka, nitakuambia ilivokuwa, ni mdogo wako alinipigia, ,... kweli kuna tatizo....’akasema

‘Oh, nilijua tu, nilijua nia yako ni kupoteza muda, sasa niambie ukweli ni nani kafa....?’ akauliza

‘Nani kafa!?’ mumewe akabakia kushangaa huku akimuangalia mkewe, na hapo akaingia na mashak  kuwa huenda mkewe kapokea taaarifa ya msiba.

‘Unasema nani kafa,..?’ akauliza mumewe.

‘Kwani mdogo wangu kakuambia nini?’ akauliza mkewe alipona mumewe anabakia kushangaa.

‘Lakini mke wangu , nani kazungumiza mambo ya kifo hapa, kuna mtu akakuambia kuna msiba, …?’ sasa ikawa ni zamu ya mwanaume kuikiria kuwa mkewe kaletewa taarakasema na mkewe akapumua akijua huenda kweli hakuna msiba.
Ifa ya msiba ndio maana alikuwa katika hali isiyo ya kawaida.

‘Sasa kama sio msiba kwanini mdogo wangu alikuwa akilia....?’ akauliza mkewe

‘Aaah, na wewe bwana mbona unaniweka roho juu,…..’akasema mumewe

‘Wewe ndio unafanya hivyo, haya niambia ukweli,….’akasema mkewe

‘Mdogo wako kanipigia simu, kuna matatizo ya kikazi siunajua tena nyie wanawake, ..kitu kidogo kulia, japokuwa kwakweli kuna tatizo kubwa lilitokea huko kazini kwao mpaka wakafikia hapo, sasa yeye anasema atafukuzwa kazi kwa sababu ya hilo kosa....’akasema

‘Kwani kuna tatizo gani lilitokea....?’ akauliza mke sasa akiwa na amani kidogo, japokuwa na hilo nalo la kufukuzwa mdogo wake kazi sio jambo dogo maana walishaona huyo atakuwa na ajira na ndiye anakuwa muokozi wa family yao huko kwa wazazi wake.

‘Inavyoonekana ni kuwa mdogo wako alikabidhiwa mgonjwa kumuhudumia, na mgonjwa huyo alikuwa kafanyiwa upasuaji,….alitakiwa siondoke karibu na huyo mgonjwa maana akizindukana kunaweza kutokea tatizo, na akitoa ile mipita aliyoweka anaweza kupoteza uhai….’akasema

‘Kwahiyo huyo mgonjwa akazindukana,…au?’ akauliza mke kwa hamasa.

‘Hapo ndio kwenye utata, maana hata simu yangu si unajua haikuwa na chaji, kabla hajanimalizia, simu kachaaa…ikazimika, nikaanza kuhangaika kutafuta marafiki zangu, unajua ni ajabu kabisa siku ya kufa nyani miti yote huteleza, kila niliemfikia ana tatizo hiilo hilo…..’akasema

‘Siungeenda kibanda cha kuchajia simu, wale wana majenereta…’akasema

‘Nilifanya hivyo…lakini simu ikawa haiwaki tena..ugonjwa wake ule wa zamani wa kukataa kuwaka ukaanza…yaani mke wangu nimehangaika wewe leo..ila cha muhimu ni kuwa tatizo alilo nalo mdogo wako ni hilo la kutokuwajibika, na…alisema yeye alitoka kwenda kuchukua dawa za kumpa mgonjwa….sasa sijui ikawaje….’akatulia.

‘Ina maana alipotoka huku nyuma mgonjwa alizindukana, akatoa ile mipira huenda akapoteza uhai au….?’ Akauliza mkewe

‘Hapo sina uhakika…maana si ndio simu ikazimika,..sasa sijui ni hivyo mgonjwa kapoteza uhai, na mdogo wako ana kesi ya kujibu au sijui kumetokea nini….’akasema mume mtu.

‘Kwahiyo na wewe ukshinda kupata mtu wa kusaidia kumpigia shemeji yako simu….haiwezekani….’akasema

‘Nilipata mtu, rafiki yangu mmoja alikuwa na simu yenye chaji tukawa tumeongezana naye nikamuomba simu nikampigia mdogo wako akawa hapatikani, nimejaribu mara karibu kumi, hapatikani kabisa, simu kazima,…sasa sijui….na cha ajabu baadaye simu yangu ikawaka, lakini tatizo mdogo wako kazima simu hapatikani ....simu hii hapa jaribu mwenyewe...’akasema na mkewe akachukua simu na kuanza kuipiga namba ya mdogo wake, lakini ikawa haipatikani.

‘Huenda polisi walikuja kumchukua na huko kituoni hawaruhusu simu…mimi natafuta usafiri nakwenda huko huko mjini, tutajua huko hko kinachoendelea, unafikiri, hivi kwa hali hii tutaweza kulala hapa, mume wangu twende huko huko...….’akasema dada mtu.

‘Kwenda wapi sa hizi mke wangu huo uasfiri wa kwenda mjini muda kama huu utaupatia wapi....?’ akauliza mume mtu.

‘Wewe unaliona hili dogo, matatizo kama hayo yakitokea kwa mtu, ....ukafikishwa polisi, ukawekwa ndani,  kama huna ndugu yako au mtu unayejuana naye huko kituoni, utaozea jela, …watu waliotakiwa kumsaidia ni waajiri wake, na hao hao ndio wamemshitakia, unafikiri nani atamsaidia mdogo wangu…hapana hili sio jambo la kusubiria…’akasema.

‘Lakini hajasema kuwa kashitakiwa,...huenda bado waajiri wake hawajaamua lolote, haya tunawaza sisi tu hapa,...kwa waajiriwa,  hilo ni jambo la kawaida mahala pa kazi, likitokea tatizo zito, ni lazima ahojiwe aliye na dhamana, na hata kuwajibika, na hicho alichofanya mdogo wako, kinachukuliwa kama ni uzembe, kwanini aliondoka akamuacha mgonjwa peke yake…’akasema

‘Na wewe unongea utafikiri umeitunga wewe hiyo sheria, ina maana sheria haina ubinadamu, yeye alitoka kuchukua dawa, huku nyuma mgonjwa akazindukana, akachomoa mipira, kwani s ile mipira ya kupitishia dawa, na gesi eehe…sasa hiyo ikichomolewa mtu anakufa….?’ Akauliza

‘Hayo ni yetu mke wangu, haya tunaongea sisi..hatujaambiwa hivyo, cha muhimu ni kuvuta subira kwanza, .... maana hata tukikurupuka hapa mbio mbio, hadi mjini ukifika huko utafanya nini, niambie mke wangu kwa muda kama huu utafanya nini, ,…kwanza tutawasiliana naye, tujue kumetokea nini, na nini kinachoendelea….’akasema

‘Mimi sikuelewi, wewe mwenyewe umesema umepigia simu hapokei, simu imezimwa, mimi nimejaribu hapa haipatikani, toka lini ukampigia simu shemeji yako usimpate, muda wote simu yake ipo hewani, wewe huoni kuwa kuna tatizo…..’akasema huku akijaribu kupiga tena, lakini simu ikasema unayempigia hapatikani.....

‘Mke wangu wewe tulia kwanza, …mpaka kesho tutajua la kufanya, na nikuulize kitu, huyo mwanamke aliyekuwa hapo nje unamfahamu vyema…?’ akauliza na mkewe akamuangalia mumewe kwa macho yaliojaa mshangao, na mumewe akajua kalitibua, akatulia kukawa na ukimia kidogo. Na mkewe baadaye akawa ndiye wa kwanza kuongea;

'Mfuate huyo mwanamke wako huko nje,….maana umeona hili tunaloongea hapa halina maana, hatujamazlia kupata ufumbuzi wa hili tatizo, wewe mawazo yako kwa huyo mwanamke, ni mwanamke gani huyo anayekuzuzua, au umeshaanza kuingiwa na tamaa ya kuoa mke mwingine, kama unamtaka mke mwingine wewe fuata taratibu, si mimi sizai bwana, tafuta anayezaa atakupatia mtoto,…..’akasema na kushusha sauti kwa unyonge

‘Mke wangu sio hivyo, jamani mbona umefika huko, na..na nilitaka tuliongelee hili, lakini hili la mdogo wake limezuia, lakini mke wangu si hivyo, naona wewe umeshakasirika….’akasema

‘Sio hivyo maana yake ni nini, ina maana wewe umezarau hili la mdogo wangu…basi mimi, kama wewe huwezi, kama wewe una mipango yako na huyo mwanamke...eeeh, mimi naomba ruhusa kesho asubuhi nawahi usafiri ..ni lazima nikajue kinachoendelea huko mjini, au unasemaje mume wangu ….?’akasema.

'Mke wangu....'akaanza kuongea lakini akakatishwa na mlio wa simu yake ambayo alikuwa nayo mke wake, 

Wote wakaiangalia ile simu...…

Je simu ilikuwa ya nini, na kuna maajabu gani kutoka kwa huyu mama wa mitaani.

WAZO LA LEO: Kuna wakati mwingine tunatakiwa tuwe makini katika kauli zetu, hasa unapoongea na mwenzako ambaye katahruki au yupo kwenye matatizo au anaumwa: mfano yeye ni mgonjwa, au kapatwa na tatizo;  mtu anafikia kusema; ‘kuna mtu alikuwa anaumwa hivyo hivyo juzi tumemzika,..ugonjwa huo huo alikuwa nao marehemu ndugu yangu…. au ugonjwa huo haponi, ukikupata wewe ni kufa tu…hizi sio kauli njema kwa mgonjwa…. Tuwe na hekima na kauli zetu, kwani ulimi unaweza ukaleta neema au balaa.
Ni mimi: emu-three

No comments :