Mara akasikia simu yake ikiita, iliita kwa
mara ya kwanza, nay eye hakuwa na haraka ya kuipokea akijua huenda ni watu
wanapiga tu hawana la umuhimu, ikatulia, haikuchukua muda ikaanza kuita tena,
hapo akajua mpigaji ana jambo muhimu, akaipokea simu yake na akagundua kuwa ni
mdogo wake anayefanyia kazi hospitali ya rufaa mjini.
Wakasalamiana kama ada, lakini mdogo mtu
akaanza kulia na kulia huko kuliashiria tatizo, dada mtu kihekima hakutaka
kulichukuli jambo hilo kihofu zaidi, lakini moyoni alijua kuwa kuna tatizo
kubwa, dada mtu akauliza ;
‘Vipi habari za huko..?’ akaulizi
akijaribu kujipa moyo , alihisi sauti ya mdogo wake, japo anajitahidi lakini
yupo katika wakati mgumu, kuna jambo baya limetokea huko anakofanyia kazi, au
kuna taaarifa ya msiba. Lakini hakutakiwa kuipokea kwa pupa, ndio maana
akamuuliza kama vile ni jambo la kawaida. Mdogo mtu naye akajikaza na kusema;
‘Dada habari za huku sio nzuri ….kuna
matatizo…..’akasema na kilichofuata hapo ni kilio, mdogo mtu ikimashinda akawa
analia badala ya kuongea.
‘Unasema kuna matatizo, tatizo gani ,
kwani imekuwaje, sema basi mbona unaanza
kulia kwanza, mimi unanitisha, kuna msiba au kumetokea nini…’ akauliza dada mtu
na kusubiria jibu kwa mdogo wake, lakini simu ikakatika. Kukawa hakuna mawasiliano, dada mtu akaitoa
simu sikioni na kuikagua simu yake kwa macho
Alipoangalia akakuta simu yake imezima,
kumbe haina chaji, akakumbuka kuwa
alisahau kuichaji usiku, kwasababu umeme ulikatika, Akakimbilia kuichaji,
lakini akakuta umeme haujarudi…tatizo la umeme….
Alihangaika huku na huku mpaka akaamua
kwenda kwa jirani kuomba simu, lakini hata jirani naye hakuwepo, akarudi
nyumbani kutauta fikira nyingine huku akiomba mume wake arudi haraka,….
Wakati ameshakata tamaa, mara mlango
ukagongwa, na mgongaji naye alimtia wasiwasi, kwani sio kawaida yake kugonga
hivyo, akajua ehee, ni yale yale ya mdogo wake kupiga simu analia huenda
taarifa ndio zinaanza kuja, akilini akawa anajiuliza ni nani kafa….
Hebu tuendee na kisa chetu…
*************
Mama huyu akauendea mlango huku mkono ukitetemeka mwili umeisha
nguvu, akajitahidi hivyo hivyo na kushika kitasa kuufungua mlango. Mlango
ulipofunguka akamuona mumewe kasimama huku kashika mizigo miwili huku na huku,
yeye akaenda kumpokea, na mumewe akampa mziogo mmoja mwingine akbakai nao.
‘Vipi mbona nagonga mlango mara mbili lakini hakuna majibu, au
ndio unazifanyia kazi hizo baraka za huyo mtu wako, na huenda zimeanza kufanya
kazi?’ akauliza lakini hakusikia kauli ya mkewe.
Tofauti na ilivyokuwa siku nyingine mkewe akimpkea kuna bashabasha
fulani, tabasamu,..lakini leo kuna utoauti, au mkewe keshagundua…huenda kuna
watu wameshampaka majungu..akawa anawaza.
Mawazo hayo ya kuwa mkewe kapewa majungu yamejitokeza leo kwa vila
tu ana jambo la kutaka kumuambia, jambo ambalo anachelea kabisa kuliongelea,
lakini kwa vile imekuwa ni kero akaona kuna umhimu wa kuliongelea, lakini je
ataanzaje.
Akamtupia jicho mkewe la haraka, ile fuaraha ya mchana haikuwepo
usoni kwa mkewe…na mkewe alipompokea mzigo hakusema neno, na hata hapo
alipomuulizia, kwanini hakufungua mlango mapema mkewe hakusema neno,
alichofanya mkewe ni kumpkea mzigo na kuingia ndo ndani na yeye akamuatia nyuma.
‘Hapa leo pagumu, sizani kama nitaweza kuliongelea hili…’mume mtu
akawa anawaza na huku mkewe akawa anawaza jambo jingine kabsa jambo la kupkea
taarifa mbaya.
Mume wake aliingia ndani akiwa na mzigo mwingine, akajipweteka
kwenye sofa, alionyesha kuchoka, akageuka huku na kule, na mkewe akarudi na
kuchukua huo mzigo mwingine akaiuniza sehemu wanapoweka mizigo kama hiyo kabla
hajaiunguliwa.
Mkewe aakaelekea sehemu wanapoweka maji ya kunywa, akayajaza
kwenye jagi kubwa, halafu akarudi nayo pale alipokaa mumewe, akamimina yale maji kwenye chombo maalumu cha
mumewe, maana mumewe ana chombo chake kikubwa ambacho anataka awekewe, maji ya
kutosha, na mume wake akayapokea na kuyabugia kama ana kiu ya siku mbili.
‘Ohuuu, mke wangu, mmh nimechoka kweli, mwili na akili pia…, yaani
hayo maji yamepita kama sijanywa, lakini ngoja nipumzike kwanza kabla sijanywa
mengine…’akasema huku akijinyosha, akahisi kuna kitu mkewe kakisahau, na hilo
likampa mawazo kuwa mkewe hayupo sawa,..
‘Hapa hapaongeliki hili swala…’akasema kimoo moyo, kumbe mkewe
naye akagundua kuwa kuna jambo hajalianya kwa mumewe, na akili yake ikamjenga
kuwa ni kwa vile kuna taaarifa mbaya inakuja.
Mke wake alipoligundua hilo akaja na kukaa karibu ya mume wake,
akamsogelea mume wake na taratibu akawa anamvua mumewe koti,kwani mume wake
anapenda sana kuvaa koti, tai utafikiri ni mkurugenzi fulani.. zamani alikuwa
akifanya kazi ofisini na tabia ile ya ofisini akawa nayo hata akiwa huku
kijijini.
‘Mke wangu japokuwa sina kazi nimepunguzwa kazi sio,….wamenionea
tu, lakini usijali, yote maisha,… , lakini mimi napenda kuvaa vyema, hata
nikiwa sina kazi, ila napenda kuvaa hivi hata hizi kazi za vibarua
zisizostahiki hadhi ya kuvaa koti na tai, mimi sitajivunga, utanashati ni hadhi
, ukiwa nayo, unathaminiwa….’siku hiyo akamwambia mkewe.
Na kweli kila akienda huko kwenye vibarua vyake, ni lazima avae
kitanashati, suti safi, au shati na tai…na mkewe anajua hivyo, kwahiyo huwa
anamnyoshea nguo zake sai kabisa, na akirudi haraka anamvua koti , tai na shati,
halafu anamkanda kanda mabegani na mgongoni, mumewe anapenda sana kufanyiwa
hivyo.
‘Mke wangu ukinifanyia hivyo, nafurahi sana, nahisi mapenzi ya
hali ya juu, ….’akamwambia
‘Mhh, mume wangu, hata hivi tu….’akasema
‘Yaani ni zaidi na unavyofikiria, wewe hutaki kufanyiwa hivyo
sijui kwanini, …wewe wapenda nikufanyie nini?’ akamuuliza
‘Unitahimini tu kama mke wako….unijali, ni kuniheshimu…..’akasema
mkewe, basi mume wake akawa anajitahidi sana kuchunga heshima ya mkewe, na
akirudi aghalabu, hakosi kuwa na zawadi hii na ile kwa mkewe.
Basi mkewe alipokumbuka
kuwa kasahau jambo muhimu, akamsogelea mumewe na kumvua koti lake…..alipomaliza
kumvua mavazi ya juu, akawa anamkanda kanda mabegani, kwa mikono yake, kwa hali
ile mke akawa anawaza huku akisubiria hiyo taarifa, moyoni akawa anavuta pumzi, akijua kurudi
haraka kwa mume wake ni lazima kaja na hiyo taarifa.
‘Mdogo wangu alitaka kunipa taarifa mbaya..na nahis ni msiba tu,
aisngeliweza kulia vile kwenye simu…’akawa anajismea moyoni.
‘Najua mume wangu hawezi kuniambia mapema, ni kawaida, ngoja
nivute subira, atulie ataniambia,…namshukuru sana mungu kwa nkunipa mume mwema
anayenijali, na mimi nitajitahidi kuwa mke wake mwema, kwani kwa hali kama hii,
wangelikuwa wanaume wengine wangelishakimbilia kuoa mke mwingine …’akawa
anawaza.
‘Mke wangu….’mumewe akasema na mkewe akashituka akajua ehee, taarifa
hiyo inakuja. Moyo ukaanza kumuenda mbio, akili ikawa anajaribu kuhisi ni jambo
gani, msiba …na kama ni msiba ni wa nani….au ….
‘Labeka mume wangu….’mkewe akasema sasa akijisogeza karibu na mume
wake,…bila kujijua akawa anamimina maji mengine kwenye kile chombo alichompa
maji mumewe mara ya kwanza kutoka kwenye jagi la maji, na huku akuvuta pumzi, ili kama akisikia
taarifa mbaya sana asidondoke mbali na mume wake.
Mumewe alimwangalia mkewe bila kusema neno, huku naye akiwaza yale
yale kuwa mola kamjalia kupata mke mwema, na yeye kama mume , atajitahidi kadri
ya uwezo wake kuhakikisha wanaishi kwa amani hata kama wana mtihani huo wa
kutokupta mtoto. Na ikibid hilo la kuoa mke mwingine kama mkewe hapendi basi
hatafanya hivyo, sasa je ataanzaje kuliongelea hilo…
Akawa anakumbuka jinsi alivyoitwa na familia yao kuhusu hilo jambo
la kutokupata mtoto, walimdadisi kujua yeye ana mtizamo gani, au wao
wamefuatilia kwa vipimo wakagundua kuna tatizo lolote, na yeye aliwaambia yeye
hana mtizamo mwingine zaidi ya kuvuta subira.
‘Subira mpaka mzeeke, vipi wewe bwana au hujioni kuwa umri
umekwenda?’ akaulizwa.
‘Au kuna tatizo kama kuna tatizo ongea tuone jinsi gani ya
kukusaidia…’akasema shangazi yake
‘Mimi siwaelezi, kwa hli kama hii nyinyi mnataka nifanye nini?’
akawauliza
‘Kama una uhakika kuwa huna tatizo…basi kuna njia moja tu ambayo
hata wewe unaiahamu..’akasema mjomba
‘Njia ipi mjomba?’ akauliza
‘Uoe mke mwingine…’akasema shangazi.
‘Yaani hata wewe shngazi unasema hivyo, nilijua wewe utamtetea
mwenzako,hebu niambie kama mimi nikiamua kufanya hivyo, na wakati huo huo
tumegundua kuwa sote hatuna matiatizo, na mwenzako naye akaolewe kwingine au
maana naye anahitaji mtoto….’akasema.
‘Hivi wewe unataka tukuambie nini…mwenye maamuzi hapo ni mwanaume,
kuhusu mke, hilo ni jambo jingine, na huenda ukio make mwingine inaweza kuwa ni
baraka..’akasema baba yake.
‘Mimi nawauliza mwenzangu naye hana tatizo hilo tumehakikisha, Je
na yeye naye afanye nini, …maana naye pia anataka mtoto, na yeye akamtafute kwa
nani, jamani tuangalia kote kote,msiniangalia mimi tu, hili ni mtihani kwenye
ndoa , mimi na mwenzangu tunarizika, tumemuachia mungu, na kuoa mke wa pili
kunahitaji maandalizi,..uadilifu na…je mwenzangu atalikubali, isije ikawa ni
vita …’akasema.
‘Wewe jifanya huelewi, lakini hili tunalokushauri ni muhimu kwako,…umri
unakwenda , utazaa huku unaitwa na mtoto wako babu, shauri lako…’akaambiwa
Kwakweli kikao hicho hakikumrizisha wakatawanyika bila kuafikiana,
na hauwahi kumsimulia mkewe kuhusu kikao hicho, ilikuwa siri yake.
Hata hivyo pamoja na changamoto hilo, moyoni alijisifia kuwa kweli
kamapata mke mwema, na anampenda sana, hakutaka kabisa kumuuzi, kwani licha
yeye kuwa chaguo lake, lakini hata wazazi na familia yao wanampenda sana mke
wake huyu, ila sasa tatizo ni hilo, la kutokupa mtoto. Tatizo hilo hata yeye sasa
limeanza kumkera, maana kila akikutana na ndugu ni hilo hilo, na hata mkewe
sasa keshaanza kuliongelea.
Sasa kama hata mkewe analiongea, na wakati mwingine wanabishana
kuhus hilo mpaka wanaishia kununiana, …. basi umuhimu wake umekuwa mkubwa,
kwake imekuwa ni kero, sasa yeye
afanyeje…basi kwake ikawa ni adhabu ya mawazo.
‘Hivi kumbe swala la kupata mtoto ni swala nyeti sana kiasi hiki…’
akasema siku hiyo alipokuwa akongea na raiki yake.
‘Oooh, ndio maana nilitaka kuongea na wewe kuhus hilo jambo, mimi
kama raiki yako ni lazima nikushauri jambo muhimu, …’akawa kachokoza
‘Jambo gani na wewe usiwe kama wazee wangu maana wanachonishauri
ni ubinafasi mupu, wananiangalia mimi tu, hawamjali mkewe wangu….’akasema.
‘Mimi nakushauri kwa nia njema , tafuta mke mwingine uone…’akasema
rafiki yake na akilini akasema ‘ni yale yale…’
Rafiki yake huyo alimshawishi aoe mke wa pili ili ajaribu bahati
huenda akapata mtoto. Lakini yeye alipinga kabisa swala hili, akamwambi kuwa
yeye na mkewe wanapendana sana na huenda akioa mke wa pili, itakuwa chanzo cha wao
kukosana.
‘Sasa wewe umeoa ili iweje, mkae tu mpaka uzeeni, na nani
ataiendeleza familia yako, ukifa, na mali yako atairithi nani..wewe hulioni
hilo..’ akamuuliza rafiki yake
‘Mimi nina mali gani ya kuritiwa hicho kibanda cha matope…aah,
kama mungu atapenda iwe hivyo, siwezi kukalifisha nafsi..unakumbuka mtume
Ibrahim, alikaa miaka mingapi bila mtoto…nyie watoto mnaona ndio kila kitu’
akasema
‘Sasa wewe unajilinganisha na mitume, wao walipewa umri mrefu,
sisi kama umejitahidi sana utafikia miaka themanini, tisini, ..hapo umeshakuwa
kizee, huna uweze tena wa kuzaa, sisi unatakiwa uzae mapema, ukichelewa sana
isizidi miaka thelethini na saba..’akaambiwa,
‘Rafiki yangu hilo wazo la
kuoa mke mwingine, hapana, mimi mapenzi kwa mke wangu niliye naye ndio muhimu
sana, ilimradi tunapendana na mke wangu, sioni sababu ya kukosana naye
kwasababu ya watoto…kama tutapata tutapata tu…’ akasema akionyesha kukerwa na
hilo jambo, kwani haya mazunguzmo yamekuwa kero, kila akikutana na jamaa yake
yoyote ndio gumzo.
Akaona akaliongelee vyena na mke wake, kama atakubali basi atafanya
hivyo, lakini iwe kwa ridhaa ya mke wake, akaona apitie sokoni anunue vitu
vizuri, amnunulie mkewe zawadi nzuri, ili wakiongea mke wake ajue kuwa
anampenda, na hataki kufanya hivyo kwa tamaa …
Aliponunua vitu hivyo akaharakisha kurudi nyumbani, akagonga
mlango kwa mbwembwe ili mkewe aje kumpokea, lakini hali aliyoiona kwa mkewe alipofungua
mlango na kuja kumpokea, ilikuwa sio ile hali ya siku zote, ile hali ilimtia
mashaka, na hata lile wazo la kuongea naye kuhusu hoja ya kuoa mke wa pili
ikamtoka, kwanza alijiuliza atamuanzaje mkewe, maana mwanzo wa jambo ni kianzio
chema.
‘Vipi mume wangu umeniita , kama una jambo, lakini umebakia kimia
unaniweka roho juu..’akasema. mkewe huku akimuangalia machoni, yeye kwa kuliona
lile jambo alilotaka kumuambia ni kama la aibu, akakwepesha macho yake
kuangalia na mkewe na mkewe kuona hivyo akajua lazima mume wake ana jambo
kubwa, na hilo lawezekana ni msiba.
‘Aaah we acha tu mke wangu , kazi hii ninayofanya sasa inachosha,
nimechoka sana leo, nikaona leo nirudi mapema, maana uliniambia leo alikuja
huyo mama, mleta baraka , sasa huenda barakahizo ni za kweli, tuzifanyie kazi…’akasema
mume wake akijaribu kuvuta hisia za mkewe aili akianza kuliongelea hilo jamb
lisiwe ni jambo gumu .
‘Mume wangu naye, ina maana umetoka kazini mapema kwa hilo au kuna
jingine, nahisi kuna jambo jjingine hutaki kuniambia kwa haraka, kwanini
huaniambii hilo jambo, …’akasema na mume wake akashangaa, ina maana mkewe
keshahisi kuwa yeye ana jambo anataka kumuambia akakohoa kama kusafisha koo, na
kusema;
‘Mke wangu ina maana unahisi kuwa nina jambo nataka kukuambia,
kwanini umesema hivyo, usiwe na wasiwasi mke wangu, mimi nakupenda sana, ndio
maana nataka tuongee…’akasema na mkewe akaona ehee, hiyo ndiyo kauli ya waume
wakitaka kutoa taaria mbaya kwa mkewe, sasa ngoja asubirie kusikia hiyo taarifa
mbaya, alikumbuka jinsi baba yake alivyokuwa akifanya akitaka kumuambia mama
taarifa ya huzuni, alikuwa akifanya hivyo hivyo
‘Haya niambie mume wangu maana hapa nilipo sina amani, kuna nini
kimetokea…’akasema na mumewe akawa katulia hakusema kitu, alikuwa akitafakari
jinsi y akuanza, na mkewe alipona hivyo akasema;
‘Mume wangu, niambie kuna taarifa gani, mimi siwezi kusbiria tena….’akasema
sasa akishika kichwa
‘Taarifa, taarifa gani mke wangu, mimi nilikuwa nataka tu tuongee,
mambo yetu , hasa nilipofika mchana ukasema wewe upo tayari kufuatili jambo
lolote linalohusu kupata mtoto,…sasa mke wangu, hivi hakuna njia nyingine
tunaweza kupata watoto….’akasema na mkewe akabakia kaduwaa, na muemwe kuona
vile akahis keshaanza kumuuzi mke wake akaona huenda kaanza vibaya, akasema;
‘Mke wangu lakini hili umelitaka wewe, na kila mara nikija ni wewe
unaniuliza kuhusu hili, ndio maana nimerudi mapema, ..wewe unasema kuhusu
taarifa, taarifa kutoka kwa nani, ..au umepokea simu kutoka kwa mdogo wako au…?’akasema
Mkewe akaanza kuhisi mwili unamtetemeka, pale aliposikia taarifa
kutoka kwa mdogo wake, moyoni akajua sasa mume wake anataka kumuambia hilo
jambo.
‘Ndio …niambie kuna nini kimetokea…ndio nimepokea simu kutoka
kwake, lakini…haya niambia kuna nini kimetokea?’ akauliza mkewe sasa akionyesha
hamasa
‘Mke wangu…..ndio nimepokea simu kutoka kwa mdogo wako , na
kiukweli …’akatulia maana kweli alisahau kuhusu hiyo simu kutoka kwa shemeji
yake, yeye alililiona hilo kama swala la kuongea baadaye tu, na kilichomfanya hata asahau ni kutoka na
mazunguzmo yake na rafiki yake, kimachanganya akaona leo akifika cha muhimu ni
hilo tatizo la siku nyingi, na hilo la shemeji yake akaliweka sehemu ya pili ya
mazungumzo yake na mkewe.
Alipokumbuka hivyo akatahayari, hakutaka kusema alisahau, akaona akisema alisahau ataonekana hana
mapenzi na ndugu za mkewe, akatulia kidogo. Kwa kutulia vile hakujau ndio
kunampa mkewe wasiwasi na mashaka mwenzake akijua kuwa kuna jambo kubwa
anafichwa, labda akiambiwa litamshitua
‘Kuna nini kimetokea, naona unanizungusha tu kwanini usiniambie
ukweli, au yule mgonjwa ameshafariki….au
kuna msiba mwingine, niambie mume wangu usiogope nipo tayari kupokea taarifa
hiyo…’akasema sasa akikaa vyema.
`Mke wangu,….yule mgonjwa, mgonjwa yupi huyo,….?’ Mume we akauliza
akijaribu kutafakari na kabla mkewe hajasema neno akaendelea kusema;
‘Mke wangu ni kweli
nilipokea simu kutoka kwa mdogo wako, na ndio nilikuwa najipanaga kukuambia…,
lakini naona mwenzangu una fikira nyingine
kabisa, tulia mke wangu, nina mazungumzo mengine mazuri, muhimu sana, nataka
tuyaongee kwanza….’akasema. Na mkewe akamtolea macho na kusema;
‘Mume wangu una nini leo….ina maana hilo la mdogo wangu, na
taarifa hiyo sio muhimu …hivi unajua najisikiaje hapa nilipo, .., au unataka
kupoteza muda tu, kwa vile unaogopa nitazimia,..hapana mimi sasa ni mtu mzima, akili imepevuka, wewe
niambie , tena haraka, mdogo wangu alipokupigia simu kasemaje…au kuna nini…niambie
haraka..’akasema sasa akionyesha kukerwa.
‘Mke wangu ni kweli, shameji kanipigia simu, kwanza alisema
alikupigia wewe simu, lakini simu yako ikakatika kabla hajakuambia…’akaanza
kumuelezea.
NB: Naona niishie hapa kwa leo,
WAZO LA LEO: Kuna vitu vidogo tukiviboresha kwenye
ndoa zetu vinaleta tija , furaha na baraka, kwani ndoa ni raha na furaha,lakini
vitu hivyo tunavidharau. Kwasababu mumeshaoana basi vitu hivyo havina umuhimu ,
kwa pande zote mke na mume. Vitu kama kupeana zawadi za kushitukiza, kupokeana
mizigo, kusalimiana na bashasha, na mume au mke akitoka kazini kukaa na
kunyoshana viungo(massage), ni tendo litaonekana dogo lakini moyoni linavuta
hisia kuwa mwenzangu ananijali, ananipenda. Tujitahidi kuboresha matendo mazuri
katika ndoa zetu .
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment