Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, January 20, 2015

NANI KAMA MAMA-20



Nesi ambaye aikuwa kavalia kile kitambaa cha kuzua hewa mdomoni, alifungua mlango chumba cha mapumziko cha madakitari, akawakuta ndio wanabadili nguo zao, na docta kijana alikuwa karibuna mlango akitaka kuondoka, lakini docta bingwa akauashiria kusubiri, 

Nesi akawa ameduwa, hakujua aanze vipi,  akawa anawakodolea macho hao madocta, macho yalionyesha wasiwasi. Mdocta wale walipomuona huyo nesi katika hali ile walijua kabisa kuna jambo kubwa limetokea kwa yule mama,….wakawa wanasubiria nesi aseme lolote,

Kilichowashanagza madocta na kuona huyo nesi kafika badala ya kuongea ambekia kuduwaa, kama vile kaona kitu cha kumshitua, nesi akashindwa la kuongea, huku mkononi, kashikilia maji na vifaa vya kumuongezea mgonjwa, hasemi neno…


‘Kwani vipi mbona upo hivyo, nesi…'akauliza docta bingwa

’Vipi hali ya mgonjwa?’ akauliza docta kijana, lakini nesi akawa kimiya kila akijaribu kuinua mdomo sauti haitoki,...Docta kijana yeye hakusubiria, akakaidi amri ya bsi wake akatoka mbio, alipotoka huku nyuma nesi akajaribu kuongea, 

Tuendelee na kisa chetu....

                           ************ 
‘Mgonjwa muda wote alikuwa katika hali ile ile, ila kuna muda alionyesha dalili, kidole kilicheza mara moja,…nikasubiria kuona kama kuna dalili nyingine, lakini haikutokea, na maji aliyokuwa kawekewa yakawa yanakaribia kuisha nikaona nitoke kwenda kuchukua maji mengine….’akaanza kuongea.

‘Kwani kuna tatizo gani….?’ Akauliza docta mkuu wao alipoona nesi anapoteza muda kwa habari ndefu,  na yeye sasa akiwa anataka kutoka mle ndani kuelekea huko alipo mgonjwa, na madocta wengine wakasimama kutaka kufanya hivyo.

Nesi akilini alikuwa akiwaza maana anavyokumbuka kabisa hakuchukua muda mrefu, alikumbuka kabisa alivyotoka mle  mgonjwa hakuwa na dalili yote ya kuzindukana, …hakumbuki ilikuwa saa ngapi alitoka mle ndani kwani alijua kuwa ni swala la kuchukua maji na kurudi, lakini kwa makadirio ya haraka hakuchukua zaidi ya robo saa, lakini robo saa kwa mgonjwa ni muda mrefu, aliogopa kusema hivyo.

Alikumbuka ilivyokuwa, kuwa alipofika chumba cha madawa bahati mbaya alimkuta mwenzake, ambaye ni rafiki yake mkubwa, akiwa na wagonjwa wengi waliohitaji huduma ya kupewa dawa, wakiwa na vyeti vyao kutoka kwa madakitari. Kwa hali ilivyo, aliona kama ataamua kuwasubiri hawo wagonjwa wahudumiwe kwanza, atachelewa.

Kwahiyo yeye kama nesi mwenye dhamana, aliweza kuingia  moja kwa moja hadi ndani wanapohifadhia madawa na kuchukua alichohitajia, lakini baada ya kuomba ruhusa kwa mwenzake, ili asije kuonekana kuwa anamwingilia mwenzake kazi yake.

‘Naomba chupa ya maji, ile ya mwanzo tuliyomuwekea  yule mgonjwa inakaribia kwisha, .....’aajieleza kwa mwenzake.
‘Mgonjwa yupi huyo maana huko theater, sasa hivi kuna wagonjwa wawili?’ akauliza huyo nesi anayegawa dawa.

‘Yule mama aliyeharibiwa uso.... mgonjwa mwenyewe haonyeshi hata dalili ya kuzindukana, sijui hawa madakitari watachukua hatua gani wakitoka huko kwa huyo mgonjwa mpya…’ akamwongelesha mwenzake ambaye alikuwa kabanwa sana na wagonjwa wanaohitaji dawa.

‘Kwahiyo unatakaje, huoni nipo bize na wagonjwa?’ akauliza

‘Unipe hivyo vifaa siunajua tena hiyo ni dharura, wagonjwa wanaelewa....’akasema

‘Wewe nawe kwani ni mgeni hapa pita chukua pale usisahau kuandika kwenye daftari, tafadhali…maana unajua utaratibu…mmmh, umesema nini, kuhusu huyo mgonjwa…..hizo meza kutwa mara tatu… aah, hapa sasa utanichanganya’ akawa anawahudumia wagonjwa huku akiongea na rafiki yake.

‘Kuwa makini usije ukaua wagonjwa kwa kuwapa dawa isiyostahiki, na hayao mawani yako yamekupendeza kweli, hivi umebadili fremu nini…..? ’akasema na kuuliza

‘Hahaha, hii kazi nina uzoefu nayo sifanyi makosa,hii miwani ni ningine mpendwa, inaona zaidi ya unavyofikiria wewe,…sasa hebu niambie, huyo mama hakuweza kusema lolote, kilimkuta nini, na je kweli kwa hali ile anaweza kupona, lakini mmmh hayo wanajua hawo wataalamu wetu….maana wanaweza wakawa wanaoteza muda tu kumbe mtu keshajifia tayari…. lakini yule mgonjwa anatisha, ule uso ulifanya nini?’ akauliza mwenzake huku anachukua dawa kabatini.

‘We acha tu, dunia hii ina vituko, hasa eneo hili, kwakweli limevunja rekodi, asilimia kubwa ya wagonjwa hapa ni wa vidonda, hasa vya kupigana na kukatana na mapanga au visu, watu wanachinjana kama ng’ombe…lakini nashangaa, kwanini maugomvi haya yawahusishe na akina mama...’akasema.

‘Huku hakuna cha akina mama au akina baba, wote utaikiri wamevuta, mtu akipandisha hasira hakuna kutishana, ni kupigana tu, silaha yoyote inatumika, mimi sioni ajabu, uwoga wangu isje ikanikuta na mimi siku moja...nawaogopa sana hawa watu….’akasema akiwaangalia wagonjwa ambao wengine walikuwa wakicheka tu kama kitu cha kawaida.

‘Nasema hivi, majereha kama hayo yangeliwafaa wanaume, kwani wao kupigana kwa kuumizana haitaleta maswali mengi, lakini hata akina mama na kesi nyingi hivi karibuni zimekuwa zikiwahusu akina mama, waliopigwa na waume zao, wameumizwa vibaya kweli, hata akina mama wajawazito, mbona huo sio ubinadamu…’akasema

‘Mhh, mimi ndio maana sitaki kabisa kuolewa huku,….hata nikipata bwana wa maeneo haya sijui kama nitakubali kuolewa na yeye….’akasema mwenzake.

‘Usiseme hivyo, hujapata wa kumpata ukampenda, ukahadaika kupendwa, kama wasemavyo waswahili, ukipenda, hata chongo utaita kengeza, hayo mawazo yako yote yatabadilika, hutasikiliza la mtu, mpaka uingie kwenye anga zao, siku mbili tatu unaanza kupiga ukunga uwi nakufa uwi ananiua…..Bila kupigwa huku, pendo halijanoga, na ukijifanya unajua kujibishana ndio yanakukuta kama hayo….’akasema

‘Thubutu, sura hii sio ya kuchanwa chanwa na visu, hivi umeiona sura ya huyo mama alivyo, ni kama mtu alichukua nyaya au miba mikali, yenye ncha kali akaanza kumchana chana uso, kwa nguvu, nyama za uso zikagawanika vipande, yaani hata akishonwa, uso sijui utakuwaje, utakuwa unatisha…unajua kutisha, sasa hivi walimshona shona kiaina… , siunajua tena, yaani uso hautazamiki….’akasema

‘Sasa si mpaka apone, mtu mwenyewe nahisi hatatamani kuishi, kama ni hivyo, sijui atajionea heri afe, lakini aliamua kuvumilia hadi mtoto wake atoke duniani, sijui akizindukana atasema nini, akimuona mtoto ambaye huenda ia ndio chanz cha hayo yote….’akasema mwenzake huku akiona kapoteza muda kwa haraka akaandika kwenye daftari la kuchukua vitu na akawa anelekea mlangoni kuondoka…lakini kama hajatoka, akawa kama kakumbuka jambo akasema;

‘Shoga, ngoja niondoke, maana wasije wakarudi wakanikuta sipo na mgonjwa. Siunamjua tena yule dakitari kijana, kamkomalia yule mgonjwa utafikiri ndugu yake. Anasema lazima atapona, hakubaliani kabisa na bosi wao….na bosi wake anamsikiliza, kaamua kusubiri,…’ akasema huku kashikilia mlango.

‘Lakini,..mmmh, hiyoo ndiyo azima yetu, kama madakitari,…kuwa mgonjwa atapona, kwa vyovyote iwavyo, vinginevyo, kua ni majaliwa tu, na sio tegemeo letu, au vipi,…?’ akawa kama anauliza.

‘Ndio hivyo, ….’akasema akicheza mlango, na kuna jambo alitaka kuliongea lakini akawa anasita, na mwenzake muda huo alikuwa kiongea.

‘Kama lngo letu, na adhima ya dakitari yoyote ni mgonjwa kupona. Umesema dkitari kijana, eehe, …mmh, sasa kuna wagonjwa, lakini kiukweli mimi nampenda sana yule dakitari kijana,….’akasema

‘Yah, sio wewe tu, ..’akasema
‘Lakini, vipi uliwahi kuongea naye kuhusu lile swala langu…’ akasema na kuacha kugawa dawa, kuonyesha kuwa hilo swala alilomuelezea mwenzake lilikuwa la muhimu sana!

‘Na wewe bwana mimi, nilikuambia subiri, halau huo muda wa kuongea naye nitaupata wapi, ….hivi wewe unafikiri ni jambo rahisi mimi kama mwanamke nitamuanzaje,…..hahaha….unanichekesha kweli, hivi utamtuma mtu mwenye kiu maji ya kunywa…hahaha….’akacheka huku akiwa kashikilia lile sinia alilowekea maji na dawa nyingine akionyesha anataka kuondoka.

‘Bwan acha kunizingua , ina maana hata wewe unamezea mate nilijua tu….lakini …’akasema huku akitoa dawa kwa mgonjwa, uzuri wakingea ndani kuna kiyoo, mazunguzmo yao sio rahisi kusikika nje kwa hao wagonjwa wanaohudumia, na muda huo nesi huyo akawa kazama kwenye mawazo akimikiria huyo docta kijana.

 Nesi huyu aliyekuwa akihudumia wagonjwa wa dawa, siku alipomuona huyo docta kijana, alivutika sana kwake, lakini kutokana na kazi zao hakuweza kuwa karibu naye, akimaliza zamu yake anakuta huyo docta keshaondoka, au siku nyingine yeye anatoka kabla ya huyo docta.

Akawa anajaribu sana kuwa karibu na huyo docta hata kujituma kazi kule anapofania kazi huyo docta ili tu amuone,  lakini ilikuwa vigumu kuongea naye, na ikitokea Bahati wakakutana naye, anajikuta akibabaika, asijue la kumwambia zaidi ya kumsalimia tu.

Dakitari kijana naye akahisi kuwa huyo nesi ana kitu dhidi yake, lakini hakutaka kumuuliza , kwani muda mwingi alikuwa na majukumu, hakuwa na muda wa kuongea naye, na adhima yake kubwa ni jambo lililomleta hapo, la kufanya utafiti wa kile alichojifunza..

Hata hivyo  kama kijana, dami inachemka, akawa pia na hamu ya kukutana na huyo nesi ambaye alionekana ni mcheshi lakini wakinana na yeye, ule uchesi hupungua, akajua ndio tabia za wasichana aibu ilikuwa ni jadi. Alipomuona akibabaika mara mbili wakati walipokutana akajua kuna jambo, na moyoni akasema , labada dada huyu kanitamani kimapenzi..aaah, …kaini sina muda huo kwasasa, japokuwa ni dada mrembo!

Hata hivyo docta huyu moyoni alishavutika zaidi na nesi aliyekuwa akifanya kazi naye…kama ni kuchagua  angelimchagua yeye zaidi kuliko huyo nesi wa upande wa madawa…lakini hata hivyo, kutokana na majukumu na dhamira yake, hakutaka kuliweka hilo mbele,  kazi yake ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kwa muda ule.

‘Kila jambo lina muda wake, kwasasa sitaki kujihusisha na mambo hayo mpaka lengo langu litimie..’ akajisema moyoni huyo dakitari kijana, na wakati mwingine alikuwa akijiuliza ni kwanini yeye hana hamasa sana na maswala ya mapenzi, kama walivyo kuwa wenzake ….aaah, nahis ni malengo, malengo yangu kwa sasa ni kazi,…akawa anajisemea moyoni..

*********

‘Wewe ukoje, utamuanzaje mwanaume hivihivi…nilishakuambia, mimi mwenyewe namezea mate, na kiukweli nampenda sana huyo docta, ….. pengine zaidi yako, sasa nikutafutie dawa  wewe kwanza wakati na mimi ni mgonjwa…hahaha…we zubaa tu, utashangaa chombo kinaeleea baharini. …’ Akasema huyo nesi, huku anatoka kwenye chumba cha madawa.

‘Shoga, shiga….we haya tu, tutakosana kwa hilo, yule ni wangu, nilishamuwahi,..ukijaribu kunisaliti, urafiki wetu utakwisha….’mwenzake akasema kwa sauti iliyoonyesha dhamira ya kweli.

Nesi mwenzake alikuwa keshaondoka mbio mbio akilekea chumba alicholazwa huyo mama mgonjwa na kichwani akawa na mipango kuwa kama itawezekana, leo hii atajitahidi aongee na huyo docta kijana kabla mwenzake hajamuwahi.

‘Hapo ni kuwahi tu….bahati ndio hii, leo hii nikipata mwanya tu nitajarabu kuibaragua kwake, nimuonyeshe hisia zangu….lakini mmh, ni kazi kweli …haelekei, haonyeshi kunipenda, hata nikimtupia jicho la …la…kuomuonyesha nampenda haniangalia moja kwa moja usoni.

Hapo akasimama akivuta picha ya huyo docta kijana, akawa anajisemesha mawazoni,’Hii tabu kweli, ningekuwa na uwezo wa kumuambia moja kwa moja, ningelimuambia,....lakini mmmh siwezi kwanza atanionaje mimi, …..hapana, lakini leo ngoja….’akaanza kutembea kwa haraka haraka sasa, alihisi kapoteza muda, lakini alijua mgonjwa huyo hataweza kuzindukana kwa jinsi alivyomuacha hakuwa na dalili kabisa….

 Alipofika karibu na chumba cha upasuaji ambapo wapo madaktari wanafanya kazi yao, akaona afike tu achungulie angalau , labda ataweza kumuona dakitari kijana, akajaribu kuchungulia kwenye dirisha dogo, nia ilikuwa amwangalie dakitari kijana sura yake japokuwa anafahamu fika kuwa wakiwa kwenye kazi hiyo sura zao huwa hazionekani wanakuwa wamavalia makofia usoni.

‘leo nikipata mwanya mimi na yeye nikizubaa hapa mwenzangu atanipiga bao, sikubali…..’akawa anaweza dhamira na akasogea kwenye mlango, kwenye ule mlango kuna sehemu ina kiyoo, unaweza kuona ndani , japokuwa sio kwa uzuri zaidi, akainama kuchungulia.

‘Mhh, huyu dakitari tangu afike hapa, kanibadilisha mawazo yangu kabisa, nilishakata tamaa ya wanaume……mmmh, handsome docta, I need you….’akawa anaongea peke yake, akajisahau kuwa kaongea kwa sauti.

‘Eti huyu mshamba anataka mimi nimukuwadie,…hana akili kweli, … ana wazimu kweli, nitamuanzaje ,..mimi mwenyewe namuwazia, jinsi gani nitaongea naye lakini nashindwa, …mmh, hapa sasa ni ushindani zaidi, na inaonyesha nikilaza damu mwenzangu atamuwahi huyu mtu….mmh, lakini mimi sipendi hii tabia ya kushindani mapenzi, kama ananipenda, ataniambia,…lakini mmm, hapa nikiliza damu nitamkosa ’ akawa anawaza .

‘Nitajitahidi , sitajali cha urafiki,  kama ni urafiki bora uishe tu, ….’akajisema moyoni

 Yeye mwenyewe alihis kuwa kuwa umri wake unakwenda mbio sasa hivi anahitajia mchumba, umri wake unahitaji mume, lakini hajatokea anayenifaa…sasa katokea huyo docta, akavutika naye.

‘Huyu...ananifaa, nahisi huyu dakitari kijana anafaa kuwa mume wangu…nitampata wapi kama huyu, na watu kama hawa wanaringa ni adimu kweli,  na bahati mbaya  kila nimuonaye kama yeye anakuwa na mchumba wake tayari, …mungu wangu nionyesha njia….’akawa anawaza na kuomba.

 Alimkumbuka jamaa aliyemuhadaa kuwa atamuoa, sasa miaka mitatu, anamsubiria, haonyeshi dalili ya kuoa, au hata kumchumbia kwa kumvalisha pete,…, na hata hivyo hana hadhi kama ya dakitari kijana….hata kama hana hadhi, angalau angelionyesha nia basi, wakikutana naye ni maongezi ya kwaida tu….’akajisemea.

Alishagundua kuwa huenda jamaa huyo anamuhadaa tu, kwahiyo lazima achangamkie mtu kama dakitari kijana. Alichungulia kwenye hichokidirisha, lakini ilikuwa sio rahisi kuona ndani vyema, na wakati anakodoa macho kuangalia ndani, akahisi kuna mtu nyuma yake akimkaribia, na kabla hajakaa sawa, mara mikono miwili ikashika kiunoni mwake kwa nyuma, alishituka karibu adondoshe ile sinia yenye  chupa ya maji aliyoshika.

‘Naaani..ni wewee…’akasema akishusha pumzi. Hapo hospitalini wasichana wenzake wana mtindo huo wa kushikana kihivyo, alijua labda ni mmoja wa wafanyakazi wenzake, akataka kushusha tusi, lakini mdomo ukawa mnzito, akageuka

‘Wewe unafanya nini hapa saizi, wewe siumepewa jukumu la kumwangalia yule mama mgonjwa, unachungulia nini tena huko…’ alikuwa `matroni’ ambaye ni mkali kama pilipili, hamkopeshi mtu kwenye kazi yake. Na akianza kuongea utafikiri ni mkanda wa video umewashwa.

‘Ndio matroni, nimetoka kuchukua chupa ya maji, ile ya mwanzo inakaribia kwisha…’ akasema huyo nesi huku akiwa na wasiwasi, . Cha ajabu yule `matroni, akawa anamchezea nywele zake kichwani, na mara akawa anashusha mkono mabegani, akawa anambinyabinya mabegani.

Yule nesi akawa anashangaa hicho anachokifanya huyo bosi wao, kwanza ile hali ya kumshika kiuno, halafu hili tendo analolifanya, na alitarajia ukali kwa kile alichokuwa akikiana, lakini kinachoendelea hapo ilikuwa tofauti,  akakumbuka maneno ya wenzake kuhusu tabia ya huyo bosi wao

Yule matroni akawa anaendelea kumshika shika, na huyo nesi alipokumbuka hayo aliyoysikia, akakunja uso, na kujigeuza, akitaka kuondoka, lakini matroni akasogea na kusimama mbele yake, nesi akashangaa, hakuweza kufanya lolote kujitetea, kuondoa mikono ya huo bosi wake,maana mikono yote miwili ilikuwa  imeshika sinia lenye yale maji na dawa, sasa akaona atumie mdomo kujitetea ;

‘Matroni mbona hivi…..’

‘Wewe huoni kosa lako….’akasema huyo bosi wake akitabasamu kiaina.

‘Lakini bosi….’akawa anajitetea, na matroni akaweka kidole mdomoni mwa huyo nesi na kusema

‘Shiiiiiiis’ na huyo nesi akakumbuka yale aliyoyasikia kutoka kwa rafiki yake kuhus huyo bosi,

`Hivi yule matroni unemuelewa vyema,  mama mtu mzima, lakini anatabia za ajabu ajabu kweli…’akakumbuka alichosema rafiki yake, akamuuliza;

‘Kwani yupoje?’ akamuuliza mwenzake

‘Ina maana wewe hayajawahi kutokea kwako?’ akamuuliza mwenzake

‘Sina uhakika hayo unayoyasema , kwani yupoje?’ akamuuliza

‘Huyo mama mtu mzima…ana tabia za ajabu-ajabu, akikukuta upo peke yako, ana tabia ya ku-kushika shika, na anawaanyia sana  wasichana, anawashika kinamna ambayo unahisi vibaya, sijui ana nini, wakati mwingine eti ana dai kuwa anafanya ukaguzii wa usafi…hivi kweli ukaguzu ndio umshike shike mtu kila sehemu….hapana yule mama ana lake jambo..’alisikia mwenzake akisema, na yeye akawa akimtetea kwa kusema;

`Lakini mimi sioni ubaya wake kufanya hivyo, labda anapenda kuwakagua kwa kuwashikashika ili kuhakikisha mumevaa vyema ni wajibu na kazi yake…atajuaje usafi wako, umevaa nini…na…mimi sijawahi kufanyiwa jambo la ajabu…’akawaambia

Leo na yeye yamemkuta…


‘Hahaha, mtoto wewe…ole wako nisikie kumetokea tatizo, badala ya kwenda kumuangalia mgonjwa, unachungulia wanaume wakiwa kazini..’matroni akasema.


‘Ha-hapana bosi, nilikuwa…..’akashindwa kumalizia huku huyo mama bado akiendelea kumshika shika na nesi akawa sasa anayasadikisha maneno ya rafiki yake, alivyokuwa akimuambia

Leo na mimi yamenikuta, kama kweli ukaguzi wenyewe ndio huu,  mmmh, inatia shaka kidogo, alivyonishika leo mbona anapapasa kiaina-aina..au kweli wanavyosema watu, ..dunia ina mambo….’ Akawa anajisemea kimoyo moyo

Huyu nesi hakuwahi kukutana na mambo hayo kwa huyo matroni leo akaona hizo dalili, nesi akajikuta akishikwa na mshangao, lakini mara matroni akamgeuzia kibao kikazi, na kauli yake ya kuwa anachungulia wanaume ilimpata kweli, akawa anajiuliza ina maana bosi wake huyu keshajua dhamira yake, hapo akajishusha na kutulia kidogo. Lakini moyoni akasema ngoja nisimpe nafasi hiyo..’ akajisogeza mbali na yule mama.

Matroni akamsogelea na kuwa kama anamzuia njia nesi akawa anamkwepa matroni amasogelea, ikawa kama kamchezo, nesi sasa akataka kukasirika, kwanza akatulia na matroni akawa anaendelea na tabia yake ya kumshika-shika, mara nywele , mara mabega, mara..ooh.….nesi akasema;

‘ Vipi matroni, mbona hivi, sikuelewi, ni tabia gani hii…..’akasema nesi na matroni akainamisha kichwa chini kama anawaza kwa hisia akasema.

‘Una nywele nzuri sana, na hata maumbile yako mazuri…mmh, hivi mchumba wako ni nani…maana we acha tu…’akasema huku akimuangalia sasa usoni moja kwa moja, nesi akajisogeza mbali na huyo matroni , na huyo matroni,akacheka, na kusema;

‘Hahahaha….mmh, ipo siku, haya wewe nenda kamwekee huyo mgonjwa hayo maji…lakini chunga sana, siku ukifanya makosa ukaja kwenye anga zangu, utanikumbuka…’ kasema huyo matroni huku akiwa kama anajilamba lamba mdomoni, nesi akawa anamuangalia huyo mama kwa mshangao

Nesi yule akakunja uso kwa hasira, na woga, hakuwahi , na hakutarajia kitendo kama hicho, akaamini waliyosema wenzake, kwa haraka akatembea kuondoka pale, kuelekea kwa mgonjwa wake. Huku nyuma yule akawa bado akamuangalia yule nesi anavyotembea.

 Nesi alipoika mlangoni akageuka kumuangalia huyo mama, akamuona bado huyo mama anamtizama, kwa haraka akashikilia lile sinia na kukunja mguu  akaweka sinia kwenye paja ili mkono mwingine uweze kufungua mlango.

Akawa anashindwa kufungua mlango, …alihisi mwili ukimtemtemeka, sijui kwa hasira au ni kitu gani kilimpata, ikabidi aweke sinia kwenye meza iliyopo hapo mlangoni, kwanza huku akilini akisema…`Huyu mama ni mwanga sio bure,…..Aaah, ngoja nikaiondoe ile chupa ya maji hata kama haijaisha kabisa, maana naweza kujisahau nikakuta imekwisha….na huyu mama keshanipania, mwanga mkubwa yule….na huyo dakitari bingwa naye oh, …..’akasema huku akisukuma mlango.

‘Yule dakitari bingwa namuogopa kama nini, anaweza kukumeza mzimamzima, hana utani kwenye kazi yake…na..na anaweza akasababisha ukafukuzwa kazi hivihivi, hivi nikifukuzwa kazi nitakuwa mgeni wa nani, kodi inanisubiria, kuna wanaume wameshaniwekea ahadi kuwa nikikwama nitakwenda kuwapigia magoti…oh,…oh..…..’akawa anawaza na malango ulipofunguka macho yake yalikuwa kitandani kwa mgonjwa.

 Alijikuta anashikwa na kigugumizi pale alipofungua mlango na mcho yake yakiwa yametua kitanda alichokuwa amelala yule mgonjwa. Mshangao uliomkuta ulimfanya macho yake yasiamini , akajikuta kaachia lile sinia lenye maji ya chupa ya kumuongezea mgonjwa na kudondoka chini, lakini kwa bahati nzuri ile chupa ya maji ikatua kwenye sehemu laini haikupasuka.

Alijikuta akitetemeka kwa woga, na kutamani akimbie, lakini angekimbilia wapi,…akatamani apige yowe, lakini ingesaidia nini…akashikwa na bumbuazi kwa dakika moja, huku akishindwa afanyeje…
Je ni nini kimetokea humo wodini

WAZO LA LEO: Kuna tabia ambazo ni kinyume cha maumbile ya mwanadamu, na tabia hizi zinazidi kukua, ni tabia za kuiga ambazo ni kasumba tu ya kuiga, kwani mwili wa mwanadamu ulivyo ukiuzoesha jambo, kama ilivyo kwa sigara, au pombe, basi hulowea huko huko na mtu kuwa mtumwa wa mambo hayo, na matendo hayo machafu yaliyo kinyume na maumbile ya mwanadamu, ndivyo asili yake ilivyo.

Tunasahau maandiko, jami zilivyoangamizwa kwa hilo, tunasahau madhara ya uchafu huo, vijana wanaharibika, jamii inaharibika, matendo machafu yanaongezeka, lakini cha ajabu kuna watu wanaotetea eti ni haki za binadamu. Hivi kweli hii ni haki ya binadam, kutenda yaliyokinyume na maumbile ya mwanadamu mimi naona ndio ukiukwaji wa haki za binadamu. Jamani tunakwenda wapi, haya yataiangamiza jamii kama ilivyotokea huko nyuma tusipoyakemea, na kuyapiga vita.


Ni mimi: emu-three

No comments :