Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, January 19, 2015

NANI KAMA MAMA-19  Kazi ya kumfanyia upasuaji  mgonjwa mpya iliwatinga madakitari , kiasi kwamba mpaka wanamaliza kumhudumia huyo mgonjwa mpya ikawa imeshafika jioni, na kwa vile walishaacha majukumu kwa nesi kuhusu mgonjwa wao wa zamani, hawakuwa na wasiwasi, walipomaliza kazi yao wakwa wanabadilisha nguo kwa taratibu tu.

Walipokuwa wanabadilisha nguo, mkuu wao, akawa anawauliza madaitari wake kuhusu kazi yao hiyo na walichojifunza, na hapo hapo akaulizia kuhusu mgonjwa wa zamani;

‘Sasa akili zetu zirudi kwa mgonjwa wa zamani ….naona kimia nesi hajafika, huenda hali bado ni ile ile....’akasema mkuu wao huyo.

‘Mimi nahisi hali ni ile ile, maana nesi tuliyemuachia kazi hajaja kusema lolote…mhh, nimechoka kweli, tangu asubuhi hatujapumzika bosi....’akasema mmoja wa madakitari akionyesha kuchoka na akzi waliyokwisha kuimaliza, na mkuu wao huyo akamgeukia docta kijana.

‘Vipi docta kijana, naona umefanya kazi nzuri sana , hii ndio inatakiwa, sasa nenda kwa mgonjwa watu wa zamani uone kama kuna lolote, na kama hakuna lolote, mimi sioni kwanini tuendelee kumuwekea mashine, iliyobakia kwasasa, na kitaalamu, inabidi mashine hiyo iondolewe, hatuwezi kuendelea kumuwekea mashine hiyo  .....’akasema docta bingwa

Docta Kijana akawa sasa keshayaonda mawazo yake ya kazi mpya waliyoifanya na moyoni alikuwa na furaha kwani kazi hiyo waliyoifanya kwa mgonjwa huyo mpya ilileta mafanikio makubwa.

‘Mkuu ngoja nikamuangalie lakini …’akasema huku akiangalia saa,  akili yake ikarejea kwa mgonjwa wa zamani, alitaka kujua hali yake ipoje, na kauli ya dakitari bingwa ilimkatisha tamaa, akawa anajiuliza kuna tatizo gani kwa huyo mama, mbona hakuweza kufanikiwa.

Kwa haraka akiwa na hamasa ya kwenda kumuona huyo mama, akaharakisha kuyavua yale magwanda ya upasuaji, na wenzake walikuwa hawana haraka, wengine walikuwa na simu zao wakiwasiliana na jamaa zao, mwingine alimua kujilaza tu maana walichoka....kazi ya upasuaji inahitaji kusimama kwa muda wote.

Docta kijana alikuwa tayari ameshavua nguo zake, na sasa anageuka kuelekea mlangoni kwenda kumuona mgonjwa wa zamani, amuwahi  kabla bosi wao hajafika kutoa amri ya kuondolewa mashine, moyoni bado alikuwa na matumaini kuwa huyo mama atazindukana tu ....

Mara mlango ukafunguliwa.....

**********

Nesi aliyekuwa akimuhudumia mgonjwa wa zamani,  alifika chumba cha upasuaji, akiwa na sinia lenye maji na dawa za kumuwekea mgonjwa wa zamani, ilionyesha wazi kuwa alitoka bohari ya dawa kuchukua hivyo vifaa, lakini ni kwanini apitie chumba cha upasuaji ambao alitakiwa kufika tu kama kuna dharura,….?

Madocta wote mle ndani wakajianda kusikia taarifa hata yule aliyeonyesha kuchoka, akasimama, akimuangalia yule, .....

**************

Nesi huyo ndiye aliyeachiwa huyo mgonjwa wa zamani, na alifika hapo akiwa kashikilia hilo sinia la dawa mkononi, akiwa katokea chumba cha upasuaji ambapo alipitia kuona kama anaweza kuwakuta madocta huko, na huenda.....atakuta lolote la kumpa matumaini, kuwa huenda alichelewa, madocta wakafika mgonjwa na wakawa na maamuzi mengine.

Alipofika chumba cha upasuaji akawakuta madocta wameshamaliza kazi yao hawapo, alimkuta nesi aliyeachiwa kazi ndogo ndogo za usafi, akauliza kwa sauti ya kutetemeka.

‘Mado-docta wapo wapi?’ akauliza kama vile hafahamu , kwani kawaida anafahamu kuwa wakimaliza kazi ya upasuaji wanakuwa wapi, nesi mwenzake hakutaka kumuangalia aliendelea na kazi yake ya usafi na kumweka mgonjwa mpya vyema, kuhakikisha maji yanaingia vyema kwenye mipra na dawa, na mashina ya kuonyesha mapigo ya moyo inafana kazi,.., akajibu.

‘Sehemu yao ya kawaida wakimaliza kazi kama hii, .....kwani unasemaje?’ nesi huyo akamuuliza na sasa akageuka kumuangalia mwenzake, lakini nesi mwenzake alishageuka kuelekea huko, ambapo anajua atawakuta hao madocta , alikuwa katika mwendo wa haraka kama kukimbia, mwenzake ikabidi amuangalai kwa uso wa kushangaa, moyoni akahisi kuna tatizo.

‘Au yule mama keshakata roho nini…?’ akawa anajisemea mwenyewe maana ndicho wlichokuwa wakisubiria. Moyoni akawa na huzuni akimkumbuka yule kichanga, akijaribu kuwaza jinsi gania atalelewa bila mama, na hakuna hata ndugu aliyewahi kuja kumtizama huyo mama, hata wale waliomleta hawajarudi tena.

Yule nesi alipofika chumba cha mapumziko ambapo alijua kuwa mdocta hao wapo, akasimama, kwanza akasita kugonga mlango, lakini ni jambo la haraka hakutakiwa kupoteza muda, …, alihisi mwili mzima ukimtetemeka, hakujua hata afanye nini, akawa anajiuliza afanye nini agonge kwanza, au ni akifika atasema nini, , huku akiwa ameshikilia sinia lile mkononi, akanyosha mkono kutaka kugonga, huku akitafakari cha kusema;

Kutokana na ile hali ya kuchanganyikiwa akajikuta ameshashikilia mlango, mlango ambao ulikuwa haujafungwa vyema, ukajifungua, na kujikuta anaangaliana na docta kijana ambale alikuwa karibu na mlango akitaka kufungua,  na wale madocta wengine wakageuka kuangalia mlangoni, wakamuona huyo nesi akiwa na sinia mkononi.


Nesi ambaye aikuwa kavalia kile kitambaa cha kuzua hewa mdomoni kufuata masharti, akawa anawakodolea macho hao madocta, macho yalionyesha wasiwasi. Mdocta wale walipomuona katika ile hali walijua kuna jambo kubwa limetokea kwa yule mama,….


Kilichowashanagza madocta na kuona huyo nesi kafika badala ya kuongea ambeakia wa muduwaa, kama vile kaona kitu cha kumshitua, akashindwa la kuongea, huku mkononi, kashikilia maji na vifaa vya kumuongezea mgonjwa maji, na ameingia, hasemi neno…


‘Kwani vipi mbona upo hivyo, nesi…’vipi hali ya mgonjwa?’ akauliza docta kijana lakini nesi bado alikuwa kaduwaa haongei....

 Madakitari wote wakawa kimya kusikiliza nini atasema huyo nesi, na docta kijana kijana alikuwa ameshashikilia mlango akitaka kutoka, lakini docta bingwa akamuashiria asubiri kwanza.

Docta kijana akatiai amri ya bosi wake, akasimama na alikuwa karibu kabisa na yule nesi,  huku akiona nesi huyo anachelewesha kusema kilichomleta na akilini mwake alishahisi kuna tatizo kwa mgonjwa...huyo mama!

 Nesi huyo, akilini alipofika hapo, alihisi huenda akifika hapo madocta watamuambia jambo, kuwa walifika kwa huyo mama yeye akiwa kaenda kuchukua maji na vifaa vya kumuongezea huyo mama maji …,

Lakini hali aliyoikuta mle ndani ilionyesha taswira tofauti ya kukatisha tamaa zaidi, akajikuta mwili unamnyong’onyea, karibu aidondoshe tena ile chupa ya maji iliyokuwepo mkononi mwake.

Yule docta kijana akawa keshahisi ile hali, , docta huyo akasogea pale aliposimama huyo nesi,….akasogeza mkono na kushikilia lile sinia, na huyo nesi akageuka kuangalia na huyo docta kijana, ilikuwa muda mchache lakini wenye maswali mengi yasiyo na majibu, na yule docta kijana hakutaka kupoteza muda tena.

'Shikakilia vyema sinia lako....'akasema docta kijana, akasubiri kama nesi atasema kitu, lakini akaona nesi anachelewa, yeye akamtupia bsi wao jicho, na bosi wao alikuwa akimuangalai nesi.

Docta kijana hakusubiri, akakaidi agizo la bosi wake,  kwa haraka akageuka na kukimbilia kwenye hicho chumba maalumu alichokuwa kalazwa huyo wagonjwa mama. Huku nyuma nesi akaanza kuelezea ilivyokuwa….

NB, Kidogo ni bora kuliko kuacha kabisa, tutaendeleza sehemu hii,  sehemu ija

WAZO LA LEO: Tunapokuwa kazini akili yetu iwe kwenye kazi, tusipende kuchanganya kazi na mambo yasiyoendana na kazi. Tuwe na hekima ya utendaji wetu hasa kwa wateja wetu. Kuna watendaji wengine wanakuwa kazini huku wana mambo yao mengine kinyume na kazi, wengine wanawasiliana na marafiki zao, bila kujali kuwa aliyekuja kwake ana shida, na huenda ni mgonjwa au anahitaji huduma muhimu, lakini mtendaji huyo anakuwa hamjali anaendelea kuongea na simu, hata bila kumtafadhalisha. Hii inaleta picha mbaya hata kama simu hiyo ni muhimu hebu jaribu kusema `taadhali au smahani naomba niongee na hii simu..’
Ni mimi: emu-three