Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, January 14, 2015

NANI KAMA MAMA-17


Mama mkunga alipofungua mlango, akijua ni mmoja wa majirani kaja kuta taarifa ya mtu wake, labda yupo tayari kujifungua au ana matatizo ya uzazi, kwahiyo akafungua mlango akiwa hana wasiwasi.

Mlango ulipofunguka, akajikuta anakutana na mtu wa ajabu, mtu ambaye uso umevimba na kuleta sura ya ajabu, na sehehemu nyingine nyama zinaonekana, kama mtu alikuwa akikwangua uso na kitu chenye ncha kali.

Ilikuwa ni sura ya kutisha, hata hutamani kuiangalia mara mbili, ..uso umevimba, hata macho hayaonekani vyema, ni kama dude lenye kichwa na matundu ya macho, kifuani kumelowana damu,...

Mama huyu mkunga alipoona hivyo akahisi huy ni shetani, na kwa vile alishasikia watu wakiongelea mashetani wala watu, akahisi hilo ni mojawapo limekuja kumuingilia,…..akataka kupiaga yowe…lakini aliposhusha macho kumuangalia huyo mtu wa ajabu,  akashangaa mtu huyo ni mja mnzito, au kama sio mja mnzito basi ni shetani limeshiba nyama za watu….

 Japokuwa mama huyu mkunga ana ujasiri, kazoea kucheza na damu za watu, lakini sura aliyoiona mbele yake ilimtisha sana akataka kufunga mlango kwa haraka, lakini mama alishaingiza mguu mmoja ndani na alikuwa sasa anayumba yumba akitaka kudondoka.

Yule mama mkunga akataka kupiga yowe la msaada ili kibidi mume wake aje, lakini kabla hajafanya hivyo, huyo mama akayumba na akawa sasa anataka kudondokea ndani kilichokuwa kimemzuia ni huo mlango……mama mkunga akawa bado kashikilia mlango, akili ikawa inashindwa kuamau afanye nini, na hapo akawa kachelewa.........

Mama yule akadonokea ndani , mama mkunga hakuweza hata kumshikilia bado akili ilikuwa inaogopa, ...

Tuendelee na kisa chetu

**********

Mama  mkungwa alimtizama huyu mama, pale sakafuni alipodondokea, kwa tahadhari, Aliogopa hata kumsogelea, lakini baadaye akapiga moyo konde, akamjongelea, alipomkaribia,akamgusa kwa mguu, akaona mama katulia, akainama na kuweka kidole shingoni, akaona mapigo ya moyo yanafanya kazi akajua bado mzima,

Kwa tahadhari akamchunguza, hadi akili yake iliporizika kuwa huyo ni mwanadamu, ila kwa hali aliyo nayo, anahitajia usafi wa haraka, alichofanya mama huyu,ni kutafuta maji ya haraka, akapitia jikoni na kwa bahati nzuri kulikuwa na jiko bado lina moto, walikuwa wameka sufuria kubwa kwa kwa ajili ya maji yao ya kunywa.

Akachota maji, yalikuwa bado na uvuguvugu,….akaongeza kuni jikoni, akachukua yale ya uvuguvugu, na kurudi kwa mgonjwa. Akajaribu kumgeuza vyema huyo mama,

‘Hapa nahitaji msaidizi, lakini kwa hali aliyo nayo, hatamaniki, ngoja ni msafishe, sijui hii mimba ina muda gani,...’akawa anajiuliza huku akipitisha mkono tumboni, na akasikia mguno wa maumivu,

‘Mhh, hii sio kazi ndogo, ……’akasema na kujaribu kumweka vyema alichokuwa akisikia kwa sasa ni mguno wa maumivu, mama alikuwa kigugumia kuashiria maumivu makali.

‘Hebu niambie wewe ni nani, na umepatwa na nini?’ akamuuliza, lakini hakupata jibu, mama akawa anatumia yale maji ya uvugu vugu kujaribu kumsafisha, akaona hayo hayafai yanahitajika maji mengi ya moto kidogo.

Maji yaliyokuwa jikoni yakawa yameshapata moto wa kutosha, akachukua kitambaa na kuanza kumfanyia usafi wa mwili mzima, nguo alizokuwa kavaa huyo mama,ni vitambaa, tambaa tu , vimeraruka. Huyu mama mkunga akaingia ndani na kutafuta moja ya nguo zake, akarudi nayo akamfunika huyo mama,

‘Sasa huu ni mtihani…hii mimba ni ya muda gani?’ akawa anajiuliza lakini hakupata jibu. Mama mkunga akaendelea na kazi ya kumsafisha huyo mama kadri alivyoweza

Alipomaliza kazi hiyo akajua kuwa huyo kweli ni mwanadamu, uso kidogo ukaanza kunywea, na kuonekana kama mtu, ‘ sasa kidogo anatizamika’ akasema na, sasa akataka kumchunguza vyema, ili aweze kukisia hali ya mimba je ipo na muda gani, kwa utaalamu wake ni rahisi kujua, dalili zote za kujifungua zikaonekana

‘Mhh, sasa huu ni mtihani, kwa hali uliyo nayo, tuombe mungu....’akajisemea mwenyewe

‘Kwanza huyu mtu umefanya nini, kuna madhila gani yamemkuta huyo mama hadi uso kuharibiwa kiasi hicho.....?’ akawa anajiuliza

‘Hilo sio muhimu sana kwa sasa, muhimu ni huo uja uzito, huyu mama  anahitaji msaada wa haraka…nifanyeje.’akasema huku akigeuka huku na kule, na akili ikikumbuka agizo la serkali kuwa ukunga wa mila marufuku, kwani kulitokea tatizo hapo nyuma akaishia jela.

‘Mhh, jele nyingine hiyoo inanukia, lakini nitafanyaje kwa hili…’akasema huku akiangalia  huku na kule kuona kama anaweza kupata kitu cha kusaidia, akili yake ilishajawa na utu. Akaona amuarifu mume wake, waone watafanya nini, haraka akamuita mume wake, na mume wake akatoka akiwa bado na usingizi, akauliza.

‘Vipi kuna nini?’ akauliza mume wake huku akipiga miayo na akakatiza huo muayo, pale alipotupa macho pembeni na kumuona huyo mama kalala sakafuni.

‘Mhh kuna mgonjwa!!....na-na-na huyo, mbona kalala sakafuni…?’ akauliza mumewe kw kigugumizi, usingizi wote ukamuishia

‘Usiulize zaidi kawaite wale akina mama wanaonisaidia hii kazi, hii kazi sio yangu peke yangu sitaiweza, huyu mama inaonekama keshafikia muda wake wa kujifungua na hali aliyo nayo sizani kama anaweza kufika kituo cha zahanati….’akasema

‘Eti nini, umesahau eeh,….hapana hili huwezi kulianya kwenye hii nyumba, ’akasema mume wake akionyesha wasiwasi.

‘Wewe unafikiri hapa tutafanya nini, fikiria kama ndio wewe, au mkeo yamemkuta haya, …ubinadamu unahitajika hapa…., ‘akasema

‘Mke wangu unakumbuska, uliwekwa ndani kwa mambo haya haya, huruma yako itakuponza,….huyu tumtoe nje kabisa…..’akasema huku akimsogelea.

‘Haya mtoe….’akasema mama mkunga akimuangalia mume wake ambaye alikuwa akionyesha wasiwasi hata wa kumsogelea.

‘Unaona hali aliyo nayo….hatuna ujanaj hapa, najua kabisa kwa hali aliyo nayo kujiungulia hapa ni hatari, lakini waite wenzangu tuone tutafanyaje..maana kwa hali kama hiyo hata mimi sijui tufanyeje…mimi naona bora tujitahidi afike angalau kituo cha zahanati kwa ushahidi...’akasema huyo mama

‘Wewe nakuona umesahau,… unataka kuleta kesi nyingine hapa nyumbani hujasahau onyo ulilopewa na serikali, hawakujali kuwa ulijitolea kuanya ubinadamu, wakakuweka ndani….halafu huyu ni mtu gani mbona uso umeharibika hivyo....?’ akauliza mume mtu

‘Kimbia kawaite wasaidizi..hii sio swala lako tena na muda hapa ni mali....’akasema mama mkunga, na mume wake akatoka nje kwa haraka kwenda kuwaita wanawake wasaidizi ambao wanaishi nyumba za jirani.

Walipofika, walimkuta mama huyo akiwa kashikilia kitambaa akiendelea kumsafisha huyo mama, akiwa na baadhi ya vifaa vyake vya kazi, na wenzake walipofika na kumkaribua huyo mgonjwa kila aliyemtupia jicho, akawa anashituka, na kurudi nyuma.

‘Mhh, huyu ni mwanadamu gani, mbona uso umekuwa hivyo…’wakauliza

‘Ni heri kwa sasa nilipomkanda na maji ya moto na dawa kidogo uvimbe umepungua, ungelimuona mwanzoni,….sijui kaanyiwa ukatili huo na nani…’akasema mama mkunga.

‘Sasa hii sio kesi ya polisi…’akasema mwingine

‘Kwa hali aliyo nayo mpaka tuwaite polisi, tutapoteza mtu,….’akasema mama mkunga

‘Sasa tufanyeje….tunakusikiliza wewe uliyetuita….’akasema mama mwingine

‘Mimi nimeshindwa hata kumweka mahali pazuri, …hebu sogeza huo mkeka, tumuweke hapo, …’akasema

‘Kile kitanda kipo wapi, maana alivyo , na anavyolalamika naona kama anakaribia kujifungua…’akasema

‘Ndio hivyo, wasiwasi wangu, kapoteza damu nyingi, nilijaribu kumnywesha yale maji ya kuongeza damu, ….lakini anakunywa kwa shida, unaona mdomo ulivyovimba,….’akasema huku wakimkagua kagua.

‘Una uhakika huyu ni binadamu…’mmoja aliyekuwa kimiya wakati wote akauliza kwa kunong’ona.

‘Hakikisha mwenyewe….’akasema mama mkungwa, wale akina mama na wao wakamsogelea tena, wakawa wanamshika huku na kule

Walipomkagua na kuona ni mtu kweli wakajaribu kumhoji, lakini mama alikuwa akijaribu kuinua mdomo kuongea, mdomo ulikuwa haufunguki, ulikuwa mzito kwasababu ya uvime,

‘Jamani huyu mtu anahitaji huduma ya haraka., leteni maji ya moto mengine yaliyochanganywa na chumvi, na yale majani ya kutuliza maumivu..’ mama mkunga akatoa amri kwa akina mama waliokuwepo humo. Mambo hayo yakafanyika harahaharaka na huduma ya kwanza ikafanyika kwa mama.

‘Jamani hapa tukifanya mchezo tutampoteza huyu mtu, mnakumbuka serikali ilivyotangaza juzi, ukunga wa jadi ni mwiko, na hali ya huyu mama haitamaniki, na naona kama mtoto amekaa vibaya tumboni, na inaonekana hayo majeraha aliyoyapata yatakuwa yamepoteza damu nyingi, hili sio swala letu kabisa, hili ni swala la hospitali, sasa tufanyeje…’ akasema yula mama mkunga.

‘Na hizi mvua barabara inaendeka kweli, tungeliazima hata baiskeli, awepo mwanaume wa kuendesha, sisi tufuatilie kwa nyuma....’akasema mmojawapo

Ukumbuke huko ni kijijini hakuna magari ya kukodi, magari yapo maeneo ya mbele kidogo, na kwa hali livyo hakuna ambaye angekubali gari lake like eneo hilo na hospitali ipo mbali sana, wakashauriana kuwa itafutwe baiskeli haraka iwezekanavyo.

Baiskeli ikapatikana ambayo ilikuwa na kitu nyuma kama mkokoteni, na safari ya kwenda hospitali ikaanza. Haikuchukua muda Mama akaanza kuvuja damu, na mama mkunga akamuangalai mwenzake kwa ishata kuonyesha hali ya hatari.

Wenzao wengine walikuwa wakija kwa nyuma, lakini walikuwa mbali kidogo, wao wawili walikaa kwenye huo mkokoteni kwa ajili ya msaada, kazi ilikuwa kwa kumuendeshaji.

‘Damu inavuja, hii ni ishara mbaya….na tukijaliwa kufika huko hospitali salama, kutahitajika damu, hatujui ndugu zake, mjiandae kujitolea damu….’akasema mama mkunga.

‘Mhh, mimi sina damu ya kutosha kutoa….’akasema mwenzake

‘Sijui wenzetu, lakini yote tutajulia huko mbele, tuombe tufike salama…’akasema mama mkunga.

Walipofika hospitali ambayo ni kituo kidogo tu, Ile hospitali wakaogopa kabisa kumpokea yule mgonjwa kutokana na hali aliyokuwa nayo. Walisema lazima kuwe na barua ya polisi, kwani inavyoonekana huyo mama kapigwa na hawajui kapigwaje, je watasema nini kama akipoteza maisha , hasa kwa jamaa zake.

‘Lakini mfanyieni huduma ya kwanza, mnaona hali aliyo nayo….’akasema mama mkunga lakini wale madakitari pale waliogopa hata kumshika, mmojawapo akajitolea na kutoa dawa za huduma ya kwanza, huku akisema;

‘Tafuteni usafiri, huyu mtu yupo kwenye hali mbaya…’akasema na wakati anaongea mara dakitari mkuu wa hiyo hospitalia katokea na gari lake, akamuona huyo mgonjwa.
‘Huyu mgonjwa sio wa kucheleweshwa, awahishwe hospitali kuu….’akasema huy dakitari mkuu.

‘Usafiri…’akasema mama mkungwa

‘Oh, …..’akaguna huyo dakitari, akaingia kwenye gari lake, na kusema;

‘Haya muingizeni tumfikishe huko hospitalini,

 Ikatoka hiyo Bahati,  na mama akaingizwa kwenye gari, ikawa safari ya kwenda hospitali ya wilaya.

Alipofikishwa hospitalini ya wilaya hali ya mama ilizidi kuwa mbaya kwani damu nyingi ilishapotea, majeraha ya miba yalimuharibu sana usoni na sehemu nyingine za mwili, na vile vipigo vilikuwa vimeathiri tumboni.

Madakitari wa Wilaya, nao wakaogopa, walihitajia barua ya polisi, lakini kwa hali aliyokuwa nayo mama, wakaona wamuhudumie kwanza,huku barua ya polisi ikitafutwa. Hospitali ile ya wilaya ikachemsha, vifaa walivyo navyo ni duni, na wataalamu wa operesheni kama ile hakuna,….kwani kwa hali aliyokuwa nayo mama, hatakuwa na uwezo wa kujiungua kwa njia ya kawaida, wakashauri apelekwe hospitali ya rufaa, …

‘Tutapawa wapi gari, maana aliyemleta mgonjwa alishaondoka kurudi kazini kwake...wakaangaliana, usafiri wa haraka upo wapi, je kuna jamaa wa huyu mama anaweza kusaidia, wakaulizwa waliomleta na wao wakasema;

‘Sisi hata hatumjui tumejitolea tu kama wasamaria wema…..’wakasema.

Huku na huku na ya mungu mengi likapatikana gari ambalo lilikuwa likielekea huko mjini, mwenye gari akawa tayari kutoa msaada, hadi hospitali ya rufaa na huko kwa bahati nzuri walimkuta mtaalamu wa akina mama ambaye alikuwepo hapo kwa muda, mtaalamu huyu alipomchunguza mama huyo akasema kuna mawili mama au mtoto mmoja atapoteza maisha

‘Hapa ni mtihani, mpelekeni chumba cha upasuaji haraka....’akasema dakitari huyo.....

Kazi kweli kweli…sasa ilikuwaje vile, ngojeni nijaribu kukumbuka, simtajua kisa hiki ni cha muda kidogo.

Tuendee kuwepo, tuishie sehemu hii,  mambo yanakuja msijali …


WAZO LA LEO: Utu wa mtu mtu haupimwi kwa hali ya mtu aliyo nayo, awe ni masikini au tajiri utu wake upo pale pale.  Kama unawajibika kusaidia, kuongoza, kuhudumia, usiangalie hali ya mtu, wewe angalia utu na wajibu wako kwake. 
Ni mimi: emu-three

No comments :