Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, December 15, 2014

NANI KAMA MAMA-6


‘Kama huamini hayo ninayoakuambia,  ninaweza kuwathibitishia na kumweka hadharani mchawi wenu…nitakuelezea sifa zake ili mmfahamu mbaya wenu…’ hiyo ilikuwa suati ya ajabu ikitoka mdomono mwa mke wangu….

 ‘Mbaya huo muda wa kukabidhi mikoba yake umefika, ndio maana alikuja na mkoba mweusi, ambao hautakiwi kushikwa na mtu mwingine zaidi ya mrithi wake na mrithi wake, na kikawaida mrithi wake anakuwa kipenzi chake, na kipenzi chake ndio hicho kinachoumwa mara kwa mara, na kuumwa kwake  ni sababu ya uchawi unangizwa mwilini mwake ili mwisho wa siku mtoto anakuwa mwanga….’

‘Katika hatu za kuukabidhi huo uchawi, inabidi kuwa karibu na mtu wake, na kila mara anatumia mkono wake wenye nguvu ya uchawi, kwa kushika kichwa cha mrithi wake, hiyo ndiyo njia ya kumwingizia madawa yake na kujifanya anamsomea kumbe anamwekea mazindiko yake, na yote hayo yanafanywa ili mtoto arithi uchawi na mikoba hiyo. …je sio kweli?

‘Natumai kwa sifa hizi mtakuwa mumemjua mbaya wenu, sasa kazi kwenu…’

Mara mke wangu akadondoka chini na kutulia kimiya , akihema mhemo wa mtu aliye usingizini.

Tuendelee na kisa chetu…

           *************

 Akili mwanadamu ilivyo huwa inaamini kirahisi pale inapoona mifano halisi, hata kama mifano hiyo ni viini macho tu,  sijui ni kwanini, kwani zile dalili alizozitaja huyo mke wangu kwa kupitia hiyo sauti sijui ndio shetani aliyemuingia mke wangu zilikuwa sawa sawa kabisa.

‘Au ni kwa vile mke wangu alimuona mama akifanya ndio maana ikawa rahisi kusema hivyo’ nikasema moyoni, lakini ukumbuke aliyekuwa akiongea si mke wangu nikiwa na maana sauti ilikuwa tofauti kabisa na ya mke wangu, je ina maana mke wangu kafanga kuigiza hiyo sauti,

Akili ikaanza kutafakari upande wa pili, nikianzia kukumbuka kuwa matatizo haya yalianza pale tu mama alipokuja kuishi na sisi, kabla ya hapo kulikuwa hakuna matatizo, mtoto alikuwa haumwi, mke alikuwa hana hayo mashetani, na kazini mambo yalikuwa sio mabaya, nilionekana mchapaakzi hodairi japokuwa malipo hayakuwa mazuri saana ...

‘Mkoba mweusi…’

Ni kweli mama alikuja na mkoba fulani mweusi, hakutaka  upokelewe, na hadi sasa sijui ulipo. Ina maana kweli humo ndio kuna vitu alivyotaka mjukuu wake arithi, sizani, nitamuuliza vyema kuhusu huo mkoba na wapi alipouweka,…hapo nikageuka kumuangalia mama kutaka kumuuliza lakini nilihis kama nikimuuliza hivyo ataona nimeamini hayo mambo.

Pia ni kweli kuwa mama ana tabia ya kumshika mtoto kichwa kama vile anamuomba , na mimi sikuona ubaya wa hilo, na ni kweli pia mama ni kipenzi cha mjukuu wake, kwani hapo kuna ubaya gani, lakini kwanini hayo yasemwe na hilo sijui ni shetani au ni kitu gani...nikaanza kuhisi kitu kikinipa mtihani kichwani.

Nikahema kwa muda halafu nikamwangalia mke wangu kuhakikisha kuwa ile hali aliyokuwa nayo imekwisha, alikuwa katulia pale alipokuwa , haonyeshi dalili ya kutingishwa tena, akili yangu ikazama kwenye mawazo….

Nikawa nawaza ni kwanini hayo yaongelewe kumuhusu mama, na sio mtu mwingine je ni kwa ajili ya chuki, kama ni chuki ni chuki za nini kwa mama, kwani mama ana kitu gani cha kufanya watu wamchukie, au ni kwasababu hatakiwi humu ndani , kwanini hatakiwi wakati mimi ni mwanae, na mke wangu mwenyewe ndiye alitoa pendekezo hilo kuwa mama aje kuishi na sisi, kw avile huko kijijini anapata shida…!

‘Labda kuna mtu ana chuki na familia hii akapanga hayo yatokee, sasa kama ni kupanga walipanga saa ngapi,, na jinsi gani waliweza kumfanya mke wangu aweze kuigiza sauti kama hiyo ya kiume, ya kiume kweli...nilipofikia hapo nikataka nimuulize mama maswali angalai akili yangu itulie huenda akanisaidia, taratibu nikagauke kumuangalia mama ambaye  kwa muda huo alikuwa kainama chini, alikuwa kakiangalia chakula huku kijiko kikiwa nusu kwenye sahani na nusu kwenye meza.

Nilitaka niwe mimi na mama tu waakti namuuliza, sikutaka mtu mwingine, kwahiyo nikaona nitafute njia ya kumtoa hapo huyo shemeji yangu, nikageuka kumuangalia shemeji, ambaye alikuwa akimtengeneza mtoto vizuri asiumwe na mmbu.

Kabla sijasema lolote, mara mke wangu akainuka pale alipokuwa amekaa akasimama, akatutizama akionyesha kushangaa, akakunja uso kama kujiuliza kumetokea nini, akajikagua, akageuka kuangalia mlangoni, moyoni nikasema anatafuta njia ya kukimbia, nikajiandaa kumdaka

Akageuka akamuangalia mama, alimuangalia mama kwa muda, halafu akageuza kichwa huku na kule, kama anatafuta kitu,  halafu  taratibu akatembea kuelekea chumbani, tukaona hakuna haja ya kumsumbua tena. Tulibaki mimi na mama na shemeji yangu na mtoto, mtoto kwa muda huo alikuwa amepitiwa na usingizi.

Nikataka kuhakikisha kuwa hana homa, na kweli alikuwa hana homa, alikuwa na hali ya kawaida ila mwili ulikuwa umelegea, hana nguvu, utafikiri kanyweshwa madawa ya kulevya, alikuwa hapendi kula kabisa

Mama ndiye aliyeanza kuongea baada ya kimya kirefu, na kauli yake ndiyo iliyonifanya nisinyae na yale mawimbi ambayo yalishatanda kichwani na kuniweka njia panda yaliyeyuka ghafula. Mama alisema hivi;

‘Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi, na mzazi ninayemzungumzia hapa ni mama, sizani kama kuna mzazi anaweza kuyasahau machungu ya uzazi wake, hasa ukiwa washida,…kwa mwanamke aliyezaa anaweza kunielewa haya ninayoyaongea.


‘Na uchungu wa uzazi unatofautiana, wengine wanaponea tundu la sindani, kama ulivyokuwa uchungu wangu, wakati nahangaika kukuzaa wewe mwanangu....uchungu huo humfanya kila mara mzazi ashituke pale mtoto wake anapopatwa na matatzo hata kama yupo mbali vipi....’akahema na kutulia

‘Mwanangu nimekuzaa kwa shida sana, wakati mwingine nafikia kuwaza kuwa hakuna mwanamke aliyepitia machungu hayo niliyopitia mimi. Kumbuka wakati nakuzaa wewe ilikuwa ni maamuzi kuwa uzaliwe wewe mimi nife au wewe ufe mimi nizaliwe,…nilivumilia machungu, nilijitahidi, na kwa uwezo wa mungu, mimi nauita ni muujiza tulipona sote. Na baaada yaw ewe kutoka duniani nilipoteza fahamu.

Mwaanngu nilipozindukana, nilijikuta nipo chumba cha upasuaji, ilibidi wanifanyie upasuaji wa haraka, na kilichoamuliwa ni kutolewa kizazi, ili niweze kuishi, wanajua wenyewe madakitari kuwa ilikuwa ni sababu gani..kwangu mimi , muhimu ni kuwa wewe umezaliwa upo hai, hata nikifa tena, basi...

Mwanangu, nilipokuzaa wewe, na mungu akahakikisha sitapata mtoto mwingine tena, labda ni kwa manufaa yangu au labda ni kwa ajili ya mitihani mingine ya ulimwengu huu. Je kama ningewazaa watoto wawili au watatu na umasikini niliokuwa nao ningeliwalea vipi, labda …sijui labda, baba yako angeliweza kumudu, hata hivyo, siwezi kujua mungu kwanini alipanga hivyo.....’akatulia kidogo

‘Huenda ilitakiwa iwe hivyo ili niendelee kupata mitihani ya dunia, kwani kutokuzaa tena ikawa ni tatizo kwangu, ndicho kilichofanya niachane na baba yako kwasababu nilikuwa na uwezi wa kumpatia mtoto wmingine...mwanamke gani asiyezaa.. binadamu hana shukurani.’akatulia kidogo

‘Hahaha, mwanangu, leo hii eti naambiwa, mimi nimekuwa mchawi, ninataka kumuua mwanangu,…niiue damu yangu,  kwanini sikumuua wakati namzaa, kwanini sikumuua wakati nahangaika naye nikiwa sina mbele wala nyuma, nije kumuua sasa hivi akiwa ndiye msaada wangu....hilo lifikirie kwa makini mwanngu,….eti pia nataka kumuua mjukuu wangu, haah, hivi kwel inaingia akilini…’akatulia mama

‘Mjukuu wangu nimemuona kama mtoto wangu wa pili, maana kizazi kilishatoka kwa ajili yako mwanangu, na mungu akaona anipe mjukuu  au wajukuu badili yake, sasa mimi niwaue,….ooh, jamani, kweli hili limeniuma sana, sana, lakini nitafanyaje....’akatulia kidogo

‘Lakini huyo ni mke wako una haki ya kumsikiliza mwanangu, mimi ni mama tu, huenda wakati wangu ulishapita, baada ya kubeba mimba miezi nane, sijui, nikakuzaa kwa shida, nikakulea kwa shida, nani atayajua hayo, labda yaliyopita si ndwele tugange yajayo, sisi tumeshapitwa na wakati, sasa ni zamu ya mke wako, ....mapenzi sasa ni kwa mke, ...msikilize mke wako...’akasema mama

‘Nakumbuka kuna siku za mwanzoni, nilikuwa mara kwa ma ra nakupigia simu kila nikikwama, mke wako akanipigia simu na kuniambia, nisizani kuwa nyie huku mjini mnafaidi,...mnahangaika kutafuta, kwa shida, nipunguze kukupigia simu kukuambia shida zangu,  ...’akatulia

‘Baada ya kuupata ujumbe huo, ndio maana nikawa sihangaiki kuwapigia simu tena, watu wenyewe , wale waliowhi kuja kwangu au kupita hapo ninapoishi ndio waliokuja kuwasumbua,  sikupenda kabisa mwanangu iwe hivyo, nitafanya kazi kwanani kwa hali hii, shambani ukilima hakuna mavuno, na jembe lenyewe ni jembe basi…ni maisha ya shida niliyoishi, ninabakia kuomba omba…

‘Kwahiyo mwanangu, sikupenda kuja kuwasumbua, msikilize mke wako,..kwani hata wewe kuja kunichukua sikufurahia, najua nitawakwaza, lakini sio kiasi cha kuniita mimi mchawi, ni chuki gani hiyo inayofikia hatu ya kumvunja mzazi nguvu kiasi hicho, hivi mnaelewa, ni jinis gani mtu anavyojisikia akiitwa mchawi, kitu ambacho hakijua, ….’akasema na mimi nikaingiwa na mshangao, ina maana mke wangu aliwahi kumpigia mama simu na kumwambia hivyo.

‘Unajua mwanangu kuna muda natamani mungu aichukue roho yangu tu nijifie nikaenda kupumzika tu, ili niaachane  na haya mateso ya dunia, maana kila hatua ya maisha yangu imekuwa ni mateso, sikumbuki kuiona raha yah ii dunia, labda kipindi naishi na mama, naishi na wazazi wangu, baada ya hapo, dunia ikanitenga….sasa nina mtoto nilitamani na mimi nipumzike, nile jasho langu, kumbe ndio bado kabisa mambo yanaongezeka  …’ akasema mama.

Mama aliinama chini kama anaomba, halafu akainuka kuelekea alipolala mtoto wetu, na akainua mkono wake kama kawaida yake akauweka juu ya kichwani cha mtoto, sijui alikuwa akisema maneno gani, na kwa muda ule mke wangu alikuwa anatokeza mlangoni,,,,,

Mimi kwa vile nilishamfahamu mama kuwa kila akitaka kulala huwa anamfanyia mjukuu wake vile kama kumuombea dua ya usiku mwema, sikuwa na shaka, kumbe kwa muda huo mke wangu alikuwa akitoka, kutokea chumbani alipokuwa,  na wakati anafika mlangoni akakiona kile kitendo cha mama kumshika mjuu wake kichwani.

Shemaji yangu aliyekuwa kambeba mtoto alikuwa akimuangalia mama kwa chuki akitaka kumzuia, ….tahamaki, mke wangu akakurupuka kutoka pale mlangoni na kumrukia mama, akamsukuma mama kwa nguvu zote,  msukumo ambao ulimfanya mama adondoke chini na kwa bahati mbaya kichwa chake kikagonga kwenye meza na mama akapoteza fahamu.

Niliduwa ghafla, nilimtizama mke wangu nilihisi labda alikuwa kapandisha, kwani akipinadisha  mashetani yake huwa hivyo, na huwezi kumlaumu, lakini  nikagundua kuwa yupo katika hali yake ya kawaida, ila kilichoonekana pale ni chuki ya wazi machoni, na alionyesha kuwa angeendelea kumuumiza mama kama angeinuka,

Kiukweli sikuweza kuvumilia, hapo hapo nikainuka kwenye kiti. Na kumwangalia mama akiwa katulia kimya, na akilini nikajua mama keshakufa, mwili ulinitetemekea kwa hasira, moyoni nikajua mke wangu keshamuua mama yangu, …nilimwendea mke wangu kwa hasira na kumshika mabegani..

Hasira zilinipanda, sijui ni kwasababu ya yaliyotokea au ni kwasababu ya kusukumwa kwa mama..na sijui kama mama yupo hai au vipi, …,ila nakumbuka nilimzoazoa mke wangu na kumtupia pembeni ….kwanza sikutaka kuchukua hatua ya kipigo, kwni ningelifanya hivyo ningeliua, subira ikanisaidia,…mimi nikageuka kumuangalia mama pale alipolala, sijui nilipata nguvu wapi za kumbeba mama, maana mama ni mnzitp…nilimuinua mama na kumweka kwenye sofa;

Nilimtikisa mama, kimiya,…ina maana mama kweli amekufa, nikaanza kulia

‘Mama, mama, mama.. usife mama, bado nakuhitaji sana mwanao…’

Nililia kwa muda mrefu, huku namtingisha mama aamuke, nikiyaruidia hayo maneno kuwa;

 `Mama nakuomba usife bado nakuhitaji sana mwanao…’

Unajua kulia, nililia, hadi machozi yakamlowesha mama, na kama miujiza mama alifumbua macho nakuniangalia sana,na baadaye naye akaanza kulia, nilimkumbatia kichwa chake kama mtu amkumbatia mtoto kifuani.

Mama baadaye aliinuka kwa shida huku akishika kichwa kuonyesha kuwa kina maumivu, nilitafuta kidonge cha kutuliza maumivu nikampa akanywa. Halafu nikachukua maji ya bairidi na kuanza kumkanda..baadaye akatulia .

Nilikaa kwenye sofa, nikaweka kichwa cha mama mapajani, mama akatulia na nilihiai akiwa kapitiwa na usingizi, na mimi nikashikwa na kauzingizi.

Nilipofumbua macho, mama alikuwa keshaamuka, kaka kwenye sofa pembeni yangu, na aliponiona nimefumbua macho, akasema;

‘Mwanangu nitafutie nauli niondoke…sitaki niwakosanishe wewe na mke wako, lakni kabla sijaondoka, nataka nikuhadithia maisha yangu yaliyopita, ambayo hujawahi kuyasikia,….

‘Mama nilishakuambia huwezi kuondoka hapa nyumbani, ..huwezi kuniacha..’nikasema

‘Hapa ilivyo mke wako keshatoa tamko, ama mimi ama yeye…je unahisi hapo utafanya nini, …huwezi kumuacha mke kwasababu yangu mimi, hilo silikubali, mke wako ni muhimu sana,….’akasema mama.

‘Mama, haya nitayamaliza kwa amani, wewe utaona tu, ninachoomba ni wewe moyo wako utulia, utusamehe…najua haya yoye ni kwa ajili mama una kinyongo na sisi….’nikamwambia mama.

‘Ningekuwa na kinyongo na nyie nisingalikubali kuja kuishi na nyie hapa ….moyo wangu ulishasamehe kila kitu, na nilishawasahemeeh hata hao walionifanyia niwe hivi…’akasema

‘Mama, mimi ni mwanao, na ukitaka kuondoka utaenda kuishije huko kijijini, huoni utazidi kunifanya mimi nizidi kuteseka, mama haya na mke wangu yatakwisha tu, najua ni mitihani tu, hali aliyo nayo ndiyo inamsumbua…’nikasema

‘Mwaanngu naomba utulie usikie kisa cha maisha yangu, ujue wapi ulipotokea, na hao wanaosema mimi ni mchawi, …wajue kuwa mimi nilikuzaa vipi na isingelikuwa mimi kukubali niteseke ili tu wewe uje uzaliwe, wasingelikuwa nawe hii leo,…’akasema mama

Mimi nikaona kusikia hicho kisa ni kitu kingine, lakini kuondoka kwa mama sitakubalina nako kamwe….



WAZO LA LEO . Ibilisi wa mtu ni mtu…watu wanaweza kuwa chanzo cha mfarakano katika jamii, wakajenga fitina, wakitumia njia mbali mbali ikiwemo ua ushirikina, Shiriki ni mbaya na adui mkubwa wa binadamu. Tujiepushe kabisa na ushirikina, kwani tukifanya hivyo tutakuwa tunashindana na mungu, na kuwa wakala wa shetani na shetani ni aadu wa mwenyezimungu.

Ni mimi: emu-three

No comments :