Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, November 19, 2014

DUNIA YANGU -HITIMISHO-MAONI





Wakati tunaingia mwisho wa kisa hiki, ina maana tunatakiwa tuwe na maandalizi na kisa kitakachofuata, na utaratibu tulio nao kwa hivi sasa, kutokana na ushauri wa watu wengi ni kuvirejea vile visa ambavyo tuliviandika bila ukamlifu wake, vipo visa vipya vinahitajika kuwekwa hewani, lakini tunahisi tukiendelea tu na visa vipya tutakuwa na viporwa vingi nyuma.

Labda nipate mawazo yenu wapendwa wa blog hii, na kwa wale waliokuwa nami kwa muda, wanaweza kukumbuka visa vingi nilivyotunga nyuma, na amabvyo tunahisi ni vyema kuvirejea ili vikamilike vyema, lakini tuanze na kipi, ndio maana nahitaji ushauri wenu; kuna visa, kama;

 ’’Nani kama mama'' kinahusu mama na watoto wake, na mateso aliyoyapata hadi kuharibika sura ya uso wake’’…

Kuna kisa cha ‘`Kikulacho ki-nguoni mwako’’ ambacho kinahusu mwanamke anayeota kwa vitendo(Somnambulism story), yaani yeye akiota anafanya kwa vitendo, anaweza kutoka nje akafana kazi, lakini yupo kwenye ndoto, na jinsi baadaye alivyoamua kuvunja ndoa yake na kujiunga na kundi la wasamaria wema, ili kusije kuazaliwa watoto watakaorithi tabia yake hiyo.

Kuna kisa kingine cha `dawa ya moto ni moto’ hiki nacho ni kisa kilichogubikwa na mauji, usaliti wa ndoa, na malezi ya shida, ambapo tutamuona baba watoto wake, binti anazaliwa kwingine, anakuja kugundua kuwa baba yake ni jambazi, na yeye akiwa mstari wa mbele kuhakikisha baba huyo anahukmiwa, hakujua, anakuja kufahamu mwishoni wakati baba yake huyo amekwisha kuhukumiwa miaka 70 jela…kuna visa vingi vipo ndani ya diary yangu tuliviandika kwa kifupi kifupi kama utangulizi tu….na vyote vinahitajika kukamlishwa mungu akipenda, tatizo ni muda….

Tumuombe mungu atupe uhai, afya na nafasi ili blog hii iweze kusheheni visa vingi zaidi vyenye maadili mema, mafunzo mema kwa vizazi vyetu....

********

Ili kukamilisha hitimisho la kisa chetu tunachoendelea nacho cha dunia yangu, kisa ambacho kinaonyesha jinsi gani vijana wetu, ambao wana akili za ziada, lakini kwa vile jamii, hasa huku kwetu, hazina jinsi gani ya kuwawezesha hawa watu, wakawa na sehemu ya kuendeleza vipaji vyao kwa maendelea, wao kutokana na jinsi jamii ilivyo kuwa kila mtu na lake, kila mtu anafukzia tmbo lake, wanaamua kujiingiza kwenye makundi,..
 Nia ni kupata tajiri, sifa na utawala...

 Tumemuona bwana Diamu, na ndoto yake ya kuwa na dunia yake, ndoto ya kujijenga kwa kutmia watu wenye vipaji, maana kila mtu ana kipaji chake lakini kuna wengine wana vipaji zaidi na zaidi, watu kama hawa wangeliweza kufanya maajab, ndio maana wenzetu wana maabra mbali mbali za uchunguzi, wanakwenda angani, na wamefanikiwa kwa kuwatumia watu kama hawa wenye vipaji vya ziada, sasahuku kwetu watu kama hao wanakosa uwekezaji ndio hao wanaanzisha makundi haramu.


Tunarejea kukipiia kisa kizima kwa haraka kabla ya hitimisho, ili tuone kama kuna kitu tumebakiza,au hakijaeleweka vyema, na kama una lolote kuhusiana na kisa hiki tujuze mapema, kabla ya kuweka mwisho wa kisa ambao takuwa ni hitimisho la kisa chenyewe.



Ni mimi: emu-three

No comments :