Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 26, 2014

DUNIA YANGU-69Ndio,.... ndivyo ilivyofanyika,  ngozi ya uso wa mkuu wangu ikahamishwa kwenda kwa bwana Diamu na ya bwana Diamu kwenda kwa mkuu huyo…..Diamu akawa mkuu na mkuu akawa Diamu…..!’

‘Lakini mungu kaumba vitu vyake na tabia zake, hulka nk…ujue hiki kimefanyika bila hiari ya mkuu , mkuu aliitwa, akijua anakwenda kwenye kikao, kafika kaleweshwa, na akiwa hajitambui hayo yakafanyika, anazindukana, anajikuta yupo katika hali nyingine.

Je baada ya upasuaji huu na Mkuu kujikuta yupo katik ahali nyingine, itauwaje, maana kwa Mkuu mpya hakuna tatizo, yeye alipenda hiyo hali, lakini tatizo ni  kwa huyu Diamu mpya,....je  Diamu mpya atakubaliana na hiyo hali,..

Tuendelee na kisa chetu…..

****************

Diamu mpya akazindukana, na akawa anahisi mabadiliko,mwili wa binadamu, huhisi …wao kwa hatua za awali, walichojitahidi kwanza ni kuhakikisha haoni sura yake,…akawa anauliza kuna nini kimetokea, kinachoendelea, akawa hapaji jibu lenye kurizisha....

'Wewe unaumwa, shinikizo lilikupata ukapoteza fahamu, ndio maana upo hivyo, tumekutibia docta huyo hapo....'akaambiwa siku ya kwanza, ya pili....lakini mbona sijielewi...akawa najiuliza.

Na kama unavyojua hapo alipokuwepo ni ofisi, na watu wakimuona wanafahamu huyo Diamu..huwa anatoka kutembea humo ndani, anakutana na wafanyakazi, wengine hawajui kinachoendelea,wanamuuliza mambo ya kikazi...anashindwa kuajibu, anajiuliza kwanini wanamuuliza mambo kam hayo...

 Siku moja akawa kwenye chumba chake, akasikia chumba cha pili kikifunguliwa, akaona atoke, akafungua mlango ka siri, akamuona mtu,...

'Oh, mbona yule mu anafanana na mimi, akashikwa na mshangao mkubwa maana yule mtu sura ni kama yeye…akashituka, …haikutakiwa kabisa aje kumuona huyo mtu mapema hivyo, alitakiwa kujengwa taratibu halafu watafute njia za kumweka sawa,lakini hali hiyo ikaja kugundulikana mapema.

Jamaa akahisi kuna tatizo, kwanza kuona jinsi gani anavyochungwa haruhusiwi kutoka akiulizwa anaambiwa alizidiwa na akawa kama kachanganyikiwa ndio maana wanahakikisha kuwa hali yake ipo salama kwanza, kabla hawajamruhusu kutoka hapo, na docta yupo kwa kwa jili hiyo.

‘Kama ni hivyo kwanini sijapelekwa hospitalini?’ akauliza

‘Hili sio tatizo la hospitalini kwa hivi sasa, na docta yupo hapa, anakuangalia usiwe na wasiwasi,…wewe tulia utapona tu….’akaambiwa.

Sasa siku hiyo akamuona mtu anayefanana naye, sura kama yake...kila mtu anajifahamu sura yake au sio.....akamuona mtu akiingia kwenye chumba cha jirani yake, sura kama yake,..akasubiri, akitaka kuhakikisha, na mara mtu huyo akatoka akiwa kavalia sare zake za kikazi, sare ambazo huzivaa kwa siku maalumu, akienda kukutana na wakubwa zake wa kazi.

'Haiwezekani....'akasema na hapo, akili ikamjia, akajua kuna kitu kachezewa, akimbilia kutafuta kiyoo, hadi akakipata kujiangalia…loooh, mshituka alioupata hakutegemea.

Ukumbuke huyu mtu alishaanza kuwa na tatizo la shinikio la damu, kwahiyo mshituko huo ukazidi kumauthiri, akapoteza fahamu, na Bahati nzuri, walikuwa wakimchunga kwa kumuangalia kwenye video , kwenye mtandao, docta alipoona hivyo akafika,a kamfanyia huduma ya kwanza.

‘Nataka kuonana na huyu mshenzi…’akasema

‘Mshenzi gani?’ akauliza docta

‘Huyu aliyenifanyia hivi…’akasema

‘Hapo sasa ikaanza kujengwa hoja kuwa jamaa  kachanganyikiwa, anadai mambo ambayo hayapo, mara yeye ni mkuu, mara kabadilishwa sura, …ikaenea kuwa Diamu kachanganyikiwa…

Ukumbuke maumbile ya hawa watu yanafanana sana, kwahiyo hakuna mtu angaliweza kutilia mashaka, na ukumbuke watu hawa walikuwa marafiki wakubwa, kwahiyo Diamu alishamsoma rafiki yake, tabia zake, na kama ulivyoona mara kwa mara alikuwa kimtembelea rafiki yake huyo ofisini kwake, na huko ofisini kwake aliweka mitego yake ambayo aliweza kuona kila kitu mwenzake anachokifanya.

Bwana Diamu, ni mtaalmu, anajua kuigiza, anajua kujibadili akafanya mambo kutegemeana na nyakati, kwahiyo kwa rafiki yake huyo haikuwa kazi ngumu kumuigiza na kuwa kama yeye, na kila kilichowahi kufanyika hapo ofisi alikuwa anakifahamu, ….Japokuwa sio yote aliyawezea, hasa yale ya kitaalamu zaidi , lakini kwa kiasi kikubwa alishajivika tabia ya mkuu huyo kabla tendo halijafanyika.

‘Na upasuaji ulifanyika vyema kabisa,  Diamu akawa ndiye mkuu, na mkuu akawa ndiye Diamu, hata hivyo siku zilivyozidi kwenda ikaonekana ni hatari , mkuu huyo ambaye sasa ni Diamu, akawa analeta fujo, ….akawa kila mara anapigwa msindano ya kumtuliza,

‘Sasa huyu mtu ni hatari, akitoka hapa anaweza kuharibu kila kitu, hatujui jinsi gani anaweza kulithibitisha hilo, kwani watu wameshajua kuwa amechanganyikiwa…..’wahusika wakaongea.

‘Huyu dawa yake ni moja tu….’akasema mama

‘Tumfanyeje?’ akauliza mtoto mtu

‘Si kachanganyikiwa huyu, kwa mtu kama huyu anaweza kufanya lolote,..doct aongeze madawa ya kuchanganyikiwa,….na ni lazima atajimaliz amwenyewe..’akasema mama.
Madawa ya namna hiyo yakuharibu akili yalikuwepo. Docta bingwa mwingine mtalamu wa madawa akaagizwa dawa za namna hiyo, na huyo docta alikuwa hajui kinachoendelea, ya akaitikia wito na kuwakabidhi hizo dawa.

Jamaa, yaani mkuu, ambaye sasa ni bwana Diamu,  akapigwa sindani ya hizo dawa,ambazo lengo lake ni kumuharibu akili, sasa akawa kachanganyikIwa, akawa anajipiga piga ovyo, na siku hiyo mlango ukaachwa makusdi jamaa akatoka akiwa kachanganyikiwa kabisa….

Ungelimuona muda hu ungelimuonea huruma, kwani  alikuwa akijikwangua, anajipiga piga kichwani, kuashiria kuna kitu kinamkera kichwani, maumivu au hayo madawa yanaleta shida kichwani, akakimbilia baharini, kwani hayo yote yalikuwa yakifanyika kule eneo la makaburini kwenye ofisi ya chini ya ardhi..

Taarifa ikatolewa kuwa Diamu kachanganikiwa kapotea, hata taarifa ikafika polisi, watu wakaanza kumtafuta, na mara ikaja taarifa kuwa maiti yake imeonekana ufukweni mwa bahari, na taarifa akafikishwa kwa familia, na familia ambayo ni mama , sasa mama ni wa kufikia, mama akafika kukagua maiti akakubali kuwa ni mwanae,...!

Msiba ukatangazwa japokuwa hakutanganzwa sana, ilikuwa kimiya kimiya....

Mazishi yakafanyika kisiri...na watu wa kijijini wa kimila wakaitwa, na wao walijua kuwa kweli wamemzika mrithi wa kiti maalumu cha kimila..japokuwa kuna wazee walihisi kuna jambo, lakini wakanyamazishwa kwa vitisho na pesa, na ukumbuke kuwa mama huy alikuwa akiogopewa, kwa imani za kishirikina.

Mama, akaonekana akiombeleza kifo cha mwanae, japokuwa ni kwa geresha,  ..lakni akilini mwenyewe anafahamu ni kitu gani kilichofanyika. Kosa walilolifanya ni kuweka kumbukumbu hizi zote kwenye  chombo hicho, ….chombo hicho kilicholetwa mahakamani kama ushahidi, ndicho kilichowezesha hayo kufahamika,…na mama ndiye aliyekuwa mlinzi wa hiki chombo..mama huyu alitaka iwe hivyo, alisema anahitaji kumbukumbu za kila kitu za kumuhusu mwanae, maana hajui huko mbeleni itakuwaje.

Sasa mkuu mpya kaingia kazini, baada ya kutoka mapumziko ya muda  kiutaratibu wa kiofisi, ndivyo ilivyojulikana hivyo kazini kwake, na kazi zake zikawa zinafanywa na msaidizi wake, utakumbuka kuwa msaidizi wake alikuwa akifanya karibu kila kazi baadaye,..kitu ambacho hakikuwepo kabla, enzi za mkuu mwenyewe alikuwa mchapakazi sana, lakini alipokuja huyu mkuu wa bandia, kazi nyingi zikawa zinafanywa na huyu msaidizi, hata watu walikuja kujiuliza inakuwaje, mkuu hafanyi kazi kama ilivyokuwa kabla, lakini baadaye walikuja kumzoea, wakijua ni kwa vile alishaanza kuumwa umwa.

Mkuu huyu mpya ni mjanja, ana akaili ya ziada, akili ya kuweza kumsoma mtu na kufanya kama alivyokuwa huyo mkuu wa awali, lakini ujue yeye aliingia hapo kwa lengo gani, kwahiyo chini kwa chini akawa anajenga himaya yake ndani ya kitengo hicho, hadi akawa kakidhibiti, , lakini  kuna kazi za kiutendaji zenye utaalamu wa hali ya juu, hizi asingeliweza kuzifanya bila msaidizi wake. Akamjenga msaidizi wake kiujanja, akamuwezesha, na msaidizi huyo akawa sasa kama bendera kufuata upepo.

Kuna watu wengine ambao aliamua kuwaingiza moja kwa moja kama akina Maneno, na watendaji wengine, kuna wengine wakawa wanatumiwa kama chambo, kama Mrembo Jembe, ambaye alikujaiwa na akatumika kama chambo, akitokea  nyumba ya mama urembo,....

Baadaye siri hii ikaonekana inaweza kuvuja, ikaanza kutafutwa njia ya kuhakikisha kuwa wale wote wanaofahamu wanazibwa mdomo, ndio ikaonekana watu kupotea, kuonekana wamekufa au kujiua. Wakawa sasa wamebakia wale wataalamu wa kazi mbalimbali, kama Docta, mtaalamu wa mitandao, mama Urembo, na wengineo....hawa nao walitakuwa kuondolewa mmoja mmoja, kutegemeana na unyeti wa kazi yenyewe.

‘Docta wa upasuaji, alikuwa anafahamu siri kubwa sana, huyo alionekana kama ataendelea kuwepo ipo siku atavujisha siri, ukumbuke docta huyo sio docta Chize,docta Chize alikuwa na utaalamu wake mwingine wa madawa na upasuaji wa mambo mengine tofauti na docta huyu, hata docta Chize hakujua kilichofanyika siku hiyo ya kubadilisha sura, yeye aliombwa madawa ya namna fulani na fulani, lakini hakujua kabisa dawa hizo zilikuja kufanya nini.

Baadaye huyu docta wa ngozi akauliwa , na ndio siku ile kesho yake yakatokea mabomu, nia ya yale mabomu ni kuharibu kumbukumbu zote za nyuma....kwani eneo hilo chini ya ardhi ndipo kulikuwa na mitambo na mambo mengi yaliyokuwa yakifanyika humo, na mambo hayo yakatakiwa kuharibiwa kinamna, kwani kuna habari kuwa siri za hapo zimeshavuja.

Ikapangwa pamoja na kuharibu mitambo hiyo na eneo hilo, pia waharibu, na kuwamaliza kabisa wataalamu wote, na hapo ndipo mtu huyu atajiona yupo huru kufanya mambo yake. Lakini ya mungu mengi, hayo hayakufanikiwa,kwani wataalamu hao walikuja kuokolewa kimiujiza.

‘Je waliokolewaje kimiujiza akauliza mmoja wa waandishi wa habari

**********

Aliyekuja kuwaokoa ni kiongozi wa usalama mstaafu , baba mkwe wangu, ambaye alishalichunguza kwa undani kundi hilo kwa siri, baada ya binti yake kufariki, na alihisi kufa kwake kuna sababu, katika kuitafuta hiyo sababu ndio akaligundua hilo kundi. 

Tunamshukuru sana mzee wetu huyu, hii inaonyesha kuwa wazee wetu hao ni hazina kubwa, ambayo tunahitajika kuitumia vyema, na cha kuwalipa hawa watu ni kuwaenzi kwa kuwatunza, tuwape matunzo mema.

Siku ile ya tukio mzee huyo kwa kutumia uzoefu wake, alifika huko, alishafahamu kitakachotokea, hakushirikiana na mtu, maana hali ilivyokuwa usiingeliweza kumuamini yoyote, ...wataalamu hao walipoingia, wakiwa wanasubiri kwenye chumba maalumu cha kikao, wakajikuta wanapambana na gesi, gesi maalumu ya kupoteza fahamu, na wote wakazimia,...alifanya hivyo Diamu, akijua watakuja kufa na bomu na itakuwa mwisho wao.

Mzee wetu huyu akawa ameshafika eneo hilo, alichofanya ni kuwatoa hao wahusika kutoka mle ndani, uzuri kulikuwa na kigari cha kukokota kwa mkono ndicho kilichomsaidia kuwahamisha hao watu peke yake. Na mle ndani kulikuwa na maiti za watu wengine waliokwisha uliwa na hilo kundi, ambao walisubiria kuja kutupwa, waonekane wamejiua, lakini kwa pale ilitakiwa wote waonekane wamefia humo kwenye huo mlipuko.

Muda huo, Diamu au mkuu wa kituo alikuwa anawajibika kama kiongozi, na alisubiria muda muafaka, ambao sisi tutaingia, kwani alishatoa amri hiyo kuwa kikosi chetu kingie na kukagua humo ndani kuona kama kuna watu au vifaa vyovyote.

‘Yeye alikuwa na mipango yake, kuhakikisha kuwa kweli hicho kifaa hakipo, ndicho kilichofanya aingie tena humo ndani,...

‘Huyu kiongozi mstaafu akafanya kazi ya ziada, hakutaka hali hiyo igundulikane mapema, kwani ingeliharibu kila kitu, alichofanya ni kuwavalisha  wale marehemu nguo za hao watu waliotakiwa kuuwawa, akina Chize, mama urembo, mtaalamu wa mitandao na wataalamu wengine, alifanya kazi hiyo kwa haraka sana, akawatoa hao watu ambao walishaleweshwa na madawa, akawaficha nyumba ya jirani. Nikitendo cha ujasiri, na aliweza kufanikiwa.

Alipokuja Diamu, ambaye ndiye mkuu wa kituo mpya, akajua ni wale watu wake, waliotakiwa kuuwawa, wakati huo akili yake ilikuwa kukitafuta hicho kifaa, akawa anahangaika huku na kule, kwahiyo hakupata muda wa kuchunguza tena hilo bomu, alipoona nachelewa akaona atoke,..

Wakati huo sisi na kikosi changu tulishaingia ndani,…ukumbuke kiongozi huyu mstaafu alikuwa ni mtaalamu wa mabomu pia, yeye alishaliona hilo bomu likiwa limetegeshwa, alichokifanya ni kuligeuza  muelekeo kitaalmu…lilipuke kuelekea muelekeo wa baharini

‘Na pia hilo bomu, aliyelitengeneza, hakuliweka kama ilivyotakiwa alitengeneza kivingine kinyume na maagizo ya bosi wake, kwani hata yeye hakutaka mauaji zaidi yaendelee, na alijua akifanya kama alivyotaka huyo bwana mkubwa, watu wengi wangaliweza kufa siku hiyo, na wakati alipoambiwa alitengeneze hakujua kuwa na na yeye ni mmoja wa watu waliotakiwa kufa na hilo bomu.

‘Yeye akili ikamtuma kulitengeneza  kwa namna itakayopunguza uharibufu na mauaji zaidi, ni kama umeme, unaweza kuunganisha waya , na umeme ukawa ni wa kurusha, au wa kunasa,..sasa bomu hilo akalitengeneza likawa kama umeme wa kurusha,akalitengeneza anavyojua yeye, kwahiyo lile bomu likawa halina nguvu, likawa kama upepo wenye nguvu, ndio maana kile kilichotakiwa kufanyika kikawa kinyume chake, lililipuka,lakini halikuweza kuleta hayo madhara.

Kipindi bomu linalipuka kuna muda bwana Diamu alifika hapo kama mvuvi...anapofika eneo hilo hujabadilisha akavaa kama mvuvi, akitoka hapo hupitia mlango mwingine akaingia nyumba ya jirani ambapo alikuwa na chumba, hubadilisha nguo akawa mtu mwingine tofauti, kavalia kofia pana na koti la kawaida, hutoka hapo akaingia hoteli za karibu akavalia vizuri, ....kikazi au mfanyabiashara...

Kilichomfanya kuingia mle siku ile, aligundua kuwa mama yake kumbe alificha hicho kifaa cha komputa chenye kumbukumbu humo ndani, ndio maana akaingia humo ndani  kukitafuta, lakini hakujua kuwa muda wa kulipuka hilo bomu ulipunguzwa, akajikuta ananaswa mwenyewe humo ndani, na lilipolipuka akawa humo ndani, lakini akawahi kuruka dirishani....

Wakati anaruka dirishani mimi nikamuona,  sikujua kuwa ni yeye, lakini nilijua ni mmoja wa hao watu wa hilo kundi, na haraka nikaitumia silaha yangu, nikiwa hewani, maana tulisharushwa na bomu, ….kama askari  unakuwa mwepesi,  nikafyatua risasi iliyomjeruhi huyo mtu…eneo la begani.

Lengo langu halikuwa kumuua, kumbe hiyo risasi ilimuathiri sana, na sehemu yake ya matibabu ni hospitali ya bwana Chize, na docta huyo ni mmoja wa watu aliotaka wafe , na alijua kwa muda huo ameshakufa na hilo bomu, hata hivyo, kulikuwa na docta mwingine, huyo alijua jinsi gani ya kumuweka sawa. Kwahiyo alipofika hapo hospitalini, akaagiza docta huy afike, na akamuarifu amfanyie matibabu ya haraka.

Docta huyu ni mtaalmu wa upasuaji, ni docta bingwa pia, japokuw akiwango chake sio sawa na cha docta Chize, kwahiyo huyu docta ndiye aliyeweza huyu mtu maana kwa muda huo alikuwa katika hli mbaya, kuungua na moto wa lile bomu, na risasi iliyomjeruhi na damu ningi ilishapotea.

Kiongozi huyu alipotoka hapo akiwa kajeruhiwa, akakutana na watu wake wa karibu, akawapa mikakati, kuwa inahitajika ajali ya haraka maana hataki kujulikana kuwa kaumia kwenye mapambano…yeye aliwaambia kaumia kwenye mapambano ya kupambana na kundi haramu, watu wake wana akili za haraka, wakajua nini bosi wao anataka, ....

‘Ajali ikatengenezwa kuwa yeye wakati anakuja kushirikiana na wenzake kwenye hayo mapambano na kundi haramu, kwenye eneo hilo lilipotokea mabomu, ndipo akakutana na hiyo ajali, kwa haraka gari lake  likapelekwa mahali likatengenezewa ajali, na mkuu huyo, ikaonekana alikuwepo, na akachukuliwa hadi kwenye hiyo hospitali na zoezi hilo likafanikiwa, mkuu akawa anatibiwa kimiya kimiya ikijulikana kuwa kaumia kwenye ajali, na risasi ikatolewa kwa siri na docta msaidizi.

Wakati anafanyiwa upasuaji, ikabidi docta aulize, ili ajue nini cha kuandika kwenye taarifa yake, akauliza swali ilikuwaje, ulipigwa wapi hiyo risasi.Aliyeuliza swali hilo alikuwa docta msaidizi wa docta Chize, swali hilo hakulipenda huyu mtu, lakini alitaka kutumia busara, ili mambo yasije kuharibika.

Ujue docta Msaidizi hakuwa miongoni mwa kundi, ni wale wanachama wanaotumiwa tu bila kujijua ila wanafaidika kinamna, kwa kupewa mishahara mikubwa, kuwezeshwa, na hali zao za kiuchumi ziliboreshwa, kwahiyo hawana shida,wanachoambiwa na wakubwa zao wanafuata tu....Yeye aliambiwa na huyo mgonjwa kuwa;

‘Ajali hii imetokana na maadui zangu, wakati naendesha gari walitaka kuniua, kuna mtu nilimuona akitaka kunipiga risasi, nikakwepesha gari, lakini alishafyatua hiyo risasii ndio risasi hii ikanilenga hapa begani, lakini, sitaki hili lijulikane, ikijuliakana nitawapa nafasi maadui zangu kujigamba, kwahiyo nataka iwe siri…unasikia…’akasema mkuu huyo.

Alifanya hivyo, kwa vile hakutaka watu kama akina Moto kuja kumgundua,alijua mtu, hasa Inspecta Moto, angeliweza kuunganisha mambo na kuja kumgundua kuwa ndio yeye aliyekuwepo siku ile, kutokana na hilo jeraha la risasi. Kwahiyo swala la kujeruhiwa na risasi haikujulikana kabisa. Ikawa ni siri kati ya mkuu huyu na huyo docta.

Baada ya tukio hilo, mkuu akawa anaombea apone haraka, akajua akipona, mambo sasa ni huru, hakuna atakayemfahamu kabisa….lakini wasiwasi wake ilikuwa hicho chombo chenye hizo kumbukumbu zake, hakuwa na uhakika kama kweli kilikuwepo kwenye lile jengo, na je kama kilikuwepo kitakuwa kimeharibiwa na huo mlipuko wa bomu, lakini kwa kumbukumbu zake, chombo hicho ni imara sana ..hakiungui au kuharibika kirahisi….hilo likawa linampa shida, ndio maana akawa anataka kutoka mara kwa mara kuchunguza akimtumia nesi, aliyemrubuni.

Siku  kabla ya huo mlipuko, wakati mama yake akiwa hai, bwana Diamu, aliwahi kumuuliza mama huyo kuhusu  hicho kifaa cha kumbukumbu kipo wapi, mbona hakionekani  sehemu yake, lakini alipomuuliza mama yake, kiajabu kabisa mama yake akasema hajui kilipo,…
Mtoto akajua kuwa mama yake kumbukumbu zake zimeshaanza kuleta shida, na kweli kipindi hicho mama huyu alikuwa ameshaanza kujiwa na hali kama ya kuchangabyikiwa akawa anaanza kuropoka ovyo, kuna muda anamkana mtoto wake huyo akija kumsalimia, anamwambia yeye sio mtoto wake, mtoto wake hana sura kama hiyo….

‘Wewe sio mtoto wangu, mtoto wangu ni huyu hapa, wewe sio mtoto wangu, ondoka hapa, sikutaki, namtaka mtoto wangu mwenye sura hii hapa….’anamwambia akimuonyesha picha yake ambayo alikuwa akilala nayo…hadi mtoto huyo akaja kuichkua na kuiharibu.

‘Kwa hali ile ikaonekana kuwa mama huyu anaweza kufichua siri, lakini huyu ni mama yake bila yeye hayo yote aliyo nayo asingeliyapata…ikawa nayo inampa shida, ikabidi mama huyo awe na ulinzi wa ziada, hakuna kutokatoka nje kuonana na watu....

NB: Haya naona sehemu ya pili ya hitimisho inazidi kuwa kubwa, ngoja tuishie hapa , tutakuka kumalizia kwenye sehemu ya tatu, Je chombo hiki aligundua kipo wapi, na alifanya nini…na ni yeye aliyemuua mama yake.

WAZO LA  LEO: Malezi ya watoto huanzia kwa wazazi,hiyo ni shule ya kwanza ya binadamu, shule ya sili aliyoiridhia mungu. Mtoto hapa humfahamu mama yake kwa vile muda wote yupo naye na akisikia njaa, anajua wapi pa kushika na kupata nyonyo yake. Lakini kutokana na nakama za kimaisha, wazazi huwaachia watoto wadogo, wafanyakazi wa ndani.


Tatizo linalojitokeza hapa ni uwezo na tabia ya hawa wafanyakazi wa ndani. Kwani tunahitaji kubana matumizi , tunahitaji wale ambao hawajajua gharama , tuwalipe mshahara kidogo. Wafanyakazi hawa wengine walishindikana na wazazi wao, wengine kutokana na malezi, hawajui nini maana ya upendo, hawajui  jinsi gani ya ulezi, na huduma kwa watoto.

 Ni kweli inabidi wazazi tuhangaike, lakini tukumbuke kosa dogo kwa hawa watoto wetu linaweza kumharibu huyu mtoto, achilia mbali  afya yake, lakini kuna swala la  tabia…mtoto huyu kwa vile aanshinda na mfanyakazi wa ndani, basi ujue hata tabia atakayoifahamu kwa haraka ni ile ya mlezi  wake huyo.Tuweni makini kwa hili. 
Ni mimi: emu-three

No comments :