Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, November 25, 2014

DUNIA YANGU-68


‘Sawa muheshimiwa hakimu, tupo tayari kwa hilo, tunaomba mtaalamu wa mitandao aje hapa atuwekee chombo kitakachowezesha sote kuona kila kitu kwa uwazi zaidi….’akasema na mshitakiwa akawa kashika mdomo,  huku akitoa kauli za kulalamika kuwa sheria haifuatwi,  lakini hakimu hakumsikiliza na mara ushahidi ukatolewa kwenye bahasha
...ukweli wote ukabainika, na ndoto za bwana Diamu, zikafikia ukingoni , na hapo hapo mtu huyu akadondoka na kupoteza fahamu.

Je kwenye huo ushahidi kulikuwa na nini, tuhitimishe kisa chetu kwa kumsikilza Inspecta Moto akitoa maelezo kwa waandishi wa habari….

**********

Inspecta Moto, akiwa ameongozana na muendesha mashitaka, walipotoka nje ya mahakama na hapo hapo wakajikuta wakikabiliwa na waandishi wa habari, waandishi wakitaka kujua kilichotokea ndani ya mahakamani, na muendesha mashitaka akamwambia Inspecta Moto awaelezee, kwani yeye kwa muda huo alikuwa na haraka ya kurudi kukutana na hakimu ili kumalizia hiyo kesi na taratibu nyingine za kisheria.

Baadaye gari la waginjwa lilifika na mtu aliyebebwa kwenye chombo cha wagonjwa akatolewa, akiwa katika uangalizi wa madakitari na walinzi….hapo kila mtu akawa anasogelea, waandishi wakjitahidi kupata picha …ikawa ni heka heka, hadi gari la wagonjwa lilipoondoka.

Baadaye Inspecta Moto,  akakaa na waandishi wa habari, ili wajue kilichotokea na kupata ufafanuzi, kwa hicho kichotokea huko mahakamani na ukweli wenyewe kwani yeye ndiye anayefahamu ukweli wote tokea mwanzo, akaanza kwa kusema;

‘Tumeona ni vyema tuwaambia ukweli, ili kusije kupotoswa…tunawafahamu waandishi mlivyo, na kitakachoongewa hapa ndio ukweli ulivyo, mkiandikka kinyume chake, mjue mnakosea, na mtahitajika kutoa ushahidi wa hicho mtakachokiandika, mjue mpaka sasa hukumu bado….’akaanza kusema.

‘Tunakuelewa mkuu, …..tunachohitaji ni ukweli tu…’wakasema

‘Nisingeliependelea maswali mengi,..mimi nitaelezea kwa ufasaha…nay ale nitakayoacha mjue ni mambo ya kisheria zaidi…’akasema

‘Muhimu ni kuhusu kilichoonekana kwenye huo ushahidi ulitolewa mahakamani….umekubalika, na yote yaliyoonekana ni kweli tupu…’akasema.

‘Kiukweli hata wakati chombo hicho cha komputa kinatolewa kama ushahidi, bado nilikuwa na mashaka, bado nilikuwa na wasiwasi kuwa huenda kile nilichokuwa nimekiwazai inawezekana isiwe hivyo,lakini mimi na wenzangu tulishaweka imani kuwa huo utakuwa ndio mwisho wa yote, mjue kundi hili ni wajanja sana, lakini mungu akasaidia, ikawa ni kweli na yote yakabainika.….’akatulia.

‘Kila kitu kiliwekwa wazi, chombo kilitusaidia sana kuweka mambo yote bayana, yakiwemo mikakati ya kundi hilo, na watu walioshirikishwa, na jinsi gani wahusika walivyojengwa,...wengine kwa kulazimishwa kwa `skendo’ na wengine kwa tamaa zao tu za kupata utajiri wa haraka…’akatulia

‘Humo walonekana wakubwa, matajiri, waheshimiwa ambao mkiwaona majukwaani mnajua hawa ndio watu, lakini moyoni mwao ni wachafu wananuka, wanayoyafanya, ni aibu, ni ulafi, ni tamaa, ufisadi uliokithiri ...lakini siwezi kuwataja hapa…hayo ni mambo ya kimahakama…..’akasema.

‘Tupe angalau sifa zo ni akina nani hao kwanini usiwataje…?’waandishi wakawa wanataka kuwajua, lakini Inspecta Moto akawaambia kisheria haruhusiwi kuwataja kwani watu hao wana kesi yao itakayofuata kwa kushirikiana na huyu muhusika mkuu..

‘Pia kati yao kuna waliokaidi, hawakupenda kabisa kuwa ndani ya kundi hilo hasa pale walipofahamu mikakati na mbinu za hilo kundi….’akasema

‘Lakini kwa vile walishaingia, na wameshakujua siri ya kundi, sio rahisi tena kukubaliwa kutoka…ndio maana kukawa na uzalilishaji, uteswaji, wengine hadi kuuwawa....kama mnamkumbuka muheshimiwa yule, aliyefariki, huyo ni mmojawapo wa watu wa mwanzoni waliuwawa na kundi hili, lakini ilionekana ni shinikizo la damu…’akasema Moto.

‘Ndani ya hili kundi, kuna wataalamu wa dawa, madawa yalitumika kufanya maasi,  sumu za ina yake zimetengenzwa, na mtu anapewa hiyo sumu anakufa inaokena ni kifo cha kawaida tu, kuna wengine walifikia hatua ya kujiua wenyewe, kutokana na matezo kutokana…, na majuto ya hayo waliyoyafanya, dhambi ainawasuta, kama mke wangu, mke wangu aliaamua kujiua, alishindwa kuvumilia....’akasema Inspecta kwa uchungu.

Hayo yapo kwenye hicho chombo, na kila kitu kitu kilihifadhiwa, ….mtaalamu wa mitandao, aliweza kuweka kitu ambacho kiliweza kunasa mengi,  …japokuwa mengona hakuweka yeye, lakini ule utaalamu wa kuwezesha kumbukumbu kuhifadhiwa sehemu moja…na walipokuja kugudnua kuwa kuna kitu kama hicho, ndio wakakitoa hicho chombo, na aliyekaa nacho ni mama…..hata hivyo mama alitaka kumbukumbu …..kwahiyo kikawa kwenye mamlaka yake.

Sasa kwenye hicho chombo, kuna sehemu nyeti ambazo hata mtaalamu wa mitandao, hakuwa kuziona…ni mama mtoto wake na watu wachache walioaminiwa, na wote sasa hivi ni marahemu kuacha huyu muhusika mkuu.

‘Sehemu muhimu  ni ile sehemu iliyobainisha ukweli kuhusu huyu mtu anayeitwa  Diamu. Diamu kwa tafsiri zao ni damu, au mtoto wa shetani,  huyu ndiye chanzo cha hili kundi, huyu ndiye aliyeingiwa na ndoto ya kuunda kundi, ambalo yeye aliona kaunda ‘dunia yake’. Huyu mtu ni hatari na mtu wa ajabu sana, sehemu hiyo ilionyesha yeye na mahusiano yake na mkuu wa kituo, ambaye ni mkuu wangu wa kazi.

‘Kikweli, hakuna aliyeamini hayo yaliyokuwepo, …tungeliongea kabla ya huo ushahidi tusingeliaminika,…lakini ukweli ndivyo ulivyokuwa, na ukabainika hadharani, iliyobakia ni mahakama kuamua, na kutoa hukumu...’akasema Moto na waandishi wakaona kama kamaliza na wakaanza kuuliza maswali kwa fujo ili kujua zaidi.

‘Kwani Dia-mu si alikuwa amekufa mapema tu, na mkuu wako ndio akawa mrithi wake?’ akauliza mwandishi wa habari aliyekuwa karibu na Iinspecta Moto

‘Ndio..Diamu-alikufa maema tu,…na aliyekuwa akiongoza hilo kundi ni mkuu wangu…..’akasema Moto.

‘Kiukweli, kwenu nyie ilitakiwa ionekane hivyo…’akatulia na waandishi wakaguna.

‘Unajua dunia hii inaongozwa na prpoganda,  na ndivyo matukio mengi yanavyofichwa na nyie waandishi wa habari mkatumika kama vyombo vya propaganda,…kalamu yenu hiyo itakuja kuwapeleka motoni,….’akatulia

‘Ndivyo ilivyotakiwa iwe hivyo….Diamu alikufa mapema, na akazikwa…. lakini  je ndivyo ilivyotokea,….kwenye hicho chombo ukweli ulikuja kubainika kwani, kila kitu kilikuja kubainika kama nitakavyoelezea, naomba mvute subira kwani mengine ni mpaka nipate kibali cha mahakama...’akasema Moto.

‘Tunahitajia ukweli…kwasababu kila kitu kipo wazi iliyobakia ni hukumu, na maelezo yako hayawezi kubadilisha kitu….’akasema mwandishi mmoja, na wakati huo Moto alikuwa akiwasiliana na muendesha mashitaka wake, na badaye akasema;

‘Kundi  hili lilipoundwa, na kukamilika, muhusika mkuu, yaani Diamu, akaona anahitajia kuwa mtu mkubwa…alitaka awe sehemu, awe ….yaani, zaidi ya raisi…ndoto za huyu mwendawazimu zilikuwa hivyo, lakini akaona aanzie sehmu nyei, ili kuhakikisha ndoo za dunia yake zinakamilika…..’akatulia kidogo.

‘Lakini angeliwezaje hayo,…mtu kma yeye kwenda kushikilia wadhifa mkubwa, au sehemu nyeti, sehemu, ambazo anaweza kufanya mambo yake bila kipangamizi,…na mwisho wa siku yeye awe kiongozi wa kweli, ashike nyadhifa mojawapo serikalini , awe hata zaidi ya raisi..ni ndoto za ajabu za huyu mtu…’akatulia

‘Sio rahisi kihivyo,….  lakini kwa ujanja wake alifanikiwa kupenya na kuingia sehemu nyeti, ni hatari kubwa sana ..ujue huyu mtu kasoma, lakini hakusomea nafasi aliyoitaka yeye…ana akaili za ziada, lakini zilitumikaje..ni tatizo…..akaanza kuwekeza kwenye ndoto yake.

‘Yeye kwa mawazo yake aliona ni muhimu awe kwenye kitengo nyeti, nafasi nyeti  ambayo kiongozi wake hachaguliwi ovyo…lakini akataka aipate hiyo sehemu, kwani akiwepo hapa, utawala, usalama utakuwa mikononi mwake….hebu fikiri mtu wa namna hii, mtu hatari kama huyu, ….lakini alichokifanya hutaamini…...

Diamu na mkuu wa kituo cha kati wakati huo, walikuwa marafiki sana, na urafiki wao ni kutoka  utotoni, kwani walikulia sehemu moja. Kwahiyo Diamu, anamfahamu huyu mtu na wamezoeana sana, na hata mwenzake alipojiunga na jeshi, yeye alishauriwa naye afanye hivyo, ila yeye alikataa….muda huo alikuwa na ndoto zak zingine tofauti na hizi za sasa.

Mkuu huyu yeye akasomea mambo hayo, na ukuu wake aliupata kwa juhudi kubwa za utendaji ,  hakuupata hivii hivi, unajua tena maswala ya jeshi. Mkuu huyu kwa uadilifu wake akaingizwa kwenye kitengo nyeti, mnakifahamu sina haja ya kukitaja….’akatulia.

Diamu, alipojiwa na ndoto zake,…baada ya kuupata utajiri kutoka kwa baba yake,  akawa anataka kumtumia mkuu huyu ili kupata yale anayoyahitajia, si rafiki yake bwana, wamekua pamoja, kwahiyo akazidisha urafiki huo zaidi,  na kwa vile alikuwa tajiri, haikuwa vigumu, kufanya mambo fulani fulani kwa mgongo wa huyu mkuu, ambaye alijitahidi kumlinda, japokuwa hakupenda. Diamu,akawa anaweza hata kufika kazini kwa rafiki huyo na kukaa wakaongea, na hapo akawa keshamjulia rafiki yake huyu nje ndani, mitaani na kazini.

‘Rafiki yake alipopandishwa cheo na kuwa mkuu wa kitengo hicho maalumu, ambacho ni nyeti ambacho ndio alichokuwa akikitafuta bwana Diamu, baada ya kuingiwa a ndoto yake hiyo ya ajabu. Bwana huyu akajiwa na husuda, tamaa, … akawa kaingiwa na ile hamasa yake ya kufika kule anapotaka, kuwa sehemu hiyo aliyoishikilia rafiki yake alitakiwa aipate yeye. Hebu fikiria mtu hajaisomea hiyo kazi, na sio fani yake, lakini kwa tamaa tu, anahitajia awe hapo.

‘Kwanza mawazo yake ya awali ilikuwa amtumie huyo rafiki yake na kumshirikisha huyo rafiki yake ili afanikiwe kupata kila anachokihitajia, lakini akaona bado inakuwa ni vigumu , maana mwenzake keshajengwa, yupo ndani ya sheria, maadili ya kazi yanamsuta….ikawa ni vigumu…ikawa hapati kila anachokitaka, na hata wakati mwingine anaogopa kumwambia huyo rafiki yake,...akaona aendelee na mpango mwingine…’plan B’, mpango wake wa siri, na mpango wake huo aliyekuwa akiufahamu ni mama yake tu…..

Mama yake alikuwa msiri wake mkuu, na mama yake ndiye aliyemfikisha hapo alipo, mama yake ndiye aliyemjenga huyo mtoto kuwa shetani….. bila mama yake huenda hata huo utajiri aliokuwa nao huyu mtu asingeupata, utajiri huo umepatikana kwa kumwaga damu, ukifuatilia historia yake ya nyuma utayagundua hayo yote. Historia ya maisha yake ya nyuma ni ndefu na siwezi kuwatajia leo hii, ni ya kutisha ….’akasema Moto

‘Yeye na mama yake wakapanga mpango huo wakiwa na uhakika kuwa inawezekana, kwani  mipango mingine ilishafanikiwa pesa nyingi ilishatumika kufanikisha mambo mengine , kama kuwajenga wataalamu, ambao ndio waliounda dunia yangu, kutokana na utaalamu wa mikono na akili zao….

‘Mtu huyu alishawekeza pesa nyingi sana kuwatengeneza watalaamu hao, kuwasomesha na huko walipopelekewa walisoma zaidi ya utaalamu waliotakiwa kuusomea, nia ni kufanikisha ndoto za huyu jamaa, na mmoja wa wataalmu hao alikuwepo dakitari  mtaalamu wa ngozi, ….huyu ni docta bingwa kweli,…hakujulikana sana kama Chize, lakini alikuwa docta bingwa kiukweli. Yeye alikubaliana na bwana huyo moja kwa moja toka awali.

‘Huyu alihitajika kwa maswala ambayo hayakuwekwa wazi mapema.

Mkuu wa kituo akawa anaingizwa kwenye kundi kidogo kidogo,kinamna…skondo zake zikawa zinahifadhiwa,..mwenyewe siku moja alipoonyeshwa, karibu afe kwa mshituko wa moyo, lakini akapozwa na rafiki yake huyo…akajengwa sasa kiushawishi….lakini sio kwa nia mbaya, akaambiwa ni kwa nia ya uwekezaji, japokuwa kwa wadhifa wake, hakutakiwa kushiriki sana kwenye mambo hayo, lakini rafiki yake akamtoa hofu kuwa  atamsimamia kwa hali na mali.

Mkuu huyu kama binadamu wengine, naye alihitajia maisha mazuri….akafikia mahali akaona hakuna tatizo, kama wengine wanafanya, wanaishi vyema, kwanini yeye…, akawa anashirikiana na mtu huyu, akawa anajiunga kwenye vikao vya uwekezaji, mkuu huyu akanogewa, ni nani asiyependa utajiri, mali na maisha bora, na ukionja asali utaweza kuonja mara kweli…..’akatulia Moto

‘Mkuu akaonogewa, na akawa anashiriki sasa  kwenye baadhi ya mipango,akawa miongoni mwa wanachama wa siri, yeye akijua  ni yupo na rafiki yake mwenzake, hata kama itatokea bahati mbaya akatimuliwa lakini sasa ana vitega uchumu, hana shida..ogopa uongozi wa serikali ukachanganya na uwekezaji binafsi, biashara na tamaa za utajiri mkuubwa….utashindwa kuwajibika, hapa kuna hekima sana, lakini hilo kwa sasa watu wanalidharau….’akasema Moto.

‘Siku moja mkuu huyu, akaitwa kuwa kuna kikao maalumu,…kipindi hiki mkuu huyu alianza kuumwa, umwa…ule mshituko alioupata wakati anaonyeshwa `skendo ‘ zake ulimuathiri sana kiafya, akaanza kuingiliwa na tatizo la shinikizo la damu,…unajua tena, ukichangana haya mambo, kazi za watu na huku una mambo yako ya siri, dhuluma inakuandama, moyo hautulii, …akawa kiafya sio mnzuri sana.

‘Mkuu kuna mpango maalumu, nataka tujadili mimi na wewe maana wewe ndiye msaidizi wangu, kama sipo duniani wewe ndiye utashiilia huu usukani…’akaambiwa na rafiki yake, na yeye kwa muda huo alikuwa  likizo ya kiafya, mapumziko mafupi….yeye akasema hakuna shida maana yupo lizoo fupi….yeye akijua ni moja ya mikutano yao ya siri, akaenda, kumbe wenzake walikuwa na ajenda nyingine ya siri.

Mkuu huyu alipofika, wakaanza kula a kunywa, wakiongea hili na lile , mikakai mingi ya uwezekaji…kumbe kule kunywa na kula kuna mambo yamewekwa kwenye vinywaji, akapoteza fahamu….alipozindukana akwa sio yeye tena…..’akatulia

*******

Walichofanya ni kwanza ni kumpoteza fahamu mkuu huyo, wakati hana fahamu, aliitwa yule docta bingwa wa maswala ya ngozi ambaye alikuwa keshaambiwa nini cha kufanya, akafika na kilichofanyika, ni kuchunwa kwa ngozi ya sura ya mkuu huyo ya usoni ikahamishwa…’hapo akatulia maana watu walikuwa wakishangaa kwa mshangao mkubwa.

‘Ndio, ndivyo ilivyofanyika,  ngozi ya uso wa mkuu ikahamishwa kwenda kwa bwana Diamu na ya bwana Diamu kwenda kwa mkuu huyo…..’akatulia na waandishi wakahema, kila mmoja akitaka hiyo hoja imuingie kwa makini, ili aweze kupamba kwenye vyombo  vyao vya habari…

Tukio hilo, jinsi livyofanyika tumeliona wazi wazi, sio kitu cha kutunga, na sio mchezo wa kuigiza…tukio zima lilionyeshwa wazi wazi kwenye kile chombo, jinsi dakitari huyo alivyofanya kuanzia mwanzo hadi mwisho, na akaonekana mkuu mpya, yaani Diamu,  akiwa hana tofauti na mkuu yule wa zamani, na Diamu mpya akiwa hana tofauti na yule wa zamani.

Lakini mungu kaumba vitu vyake na tabia zake, hulka nk…ujue hiki kimefanyika bila hiari ya mkuu , kashikwa kaleweshwa, na upasuaji umefanyika,tatizo ni  huyu Diamu mpya,....je atakubaliana na hiyo hali,..alipozindukana  ilikuwaje,….’akasema Moto, na waandishi wa habari kila mmoja akiw ana shauku, akisubiri kusikia zaidi…

NB: Hata mimi nina shauku kusikia,lakini kidole kinauma kwa kuchapa, tuonane kwenye sehemu ya pili ya hitimisho la kisa hiki

WAZO LA LEO: Uongozi  wa hekima, uongozi wenye kujali na kujua kuwa cheo ni dhamana, ni ule unaoweka msilahi  ya watu mbele.  Kiongozi huyu hafikirii kwanza tumbo lake, akijua kuwa kile atakachokila na kushiba yeye, ni jasho la anaowangoza, kwahiyo atajitaidi kwanza kuona kuwa katimiza wajibu wake, watu wake wameshakula, wamepata haki zao, na hapo ndipo atakunja magoti na kuanza kula. Kiongozi huyu ndiye kiongozi wa watu, na huyu ndiye tunatakiwa tumtafute. Uchaguzi unakaribia tuweni makini kwa hilo.
Ni mimi: emu-three

No comments :