Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 20, 2014

DUNIA YANGU-66



 Mahakama ilijaa isivyo kawaida, kinyume cha matarajio , kwani kesi hiyo ilitakiwa ifanyike kimia kimia, lakini watu walijaa utafikiri kulikuwa na tangazo kuwa leo kuna kesi kubwa itafanyika.

Kutokana na unyeti wa hii kesi  na wahusika wake, hakukutakiwa kuwe na watu wengi, kiusalama, na mapokezi yake kwa jamii, hasa kisiasa, lakini hilo halikuwezekana, taarifa zilisambaa kwa haraka na watu wakaambizana, na kile aliyesikia akawa anamwambia mwenzake ikawa ni kama lamgambo la kimia kimia kuwa, asiye na mwana aeleke jiwe.

Polisi kuona hivyo, ikabidi wafanye kazi ya ziada, kuzuia watu kuingia eneo la mahakamani, walioruhisiwa ni wale wanaohusika na kesi hiyo na watu wachache ambao  wahusika wao wapo kwenye hiyo kesi, hali kabla ya mahakama kuanza ikawa ni mvurugani kai ya polisi na watu waliofika kufatilia kesi hiyo, hata waandishi wa habari walikataliwa kuingia.

Kwa vile kila mmoja alitaka kuingia, ikabidi amri itolewe, kuwa watu wote wasiohusika waondoke eneo karibu na mahakama haraka iwezekanavyo , la sivyo, kikoso cha fanya  fujo uone kitakuja na kuwatawanya, watu wakakaidi, na waliojitahidi, wakasogea nji kidogo ya mhakama, na kukaa kusubiria , hata hivyo, baadaye hali ilikuwa shwari, watu wakakubali kukaa nje ya eneo la mahakama kusubiria, waone ni nini kitatokea.

Baadaye gari lililowabeba washitakiwa wa mwanzo likaingia, hakuna aliyelijali hilo gari sana, labda wana ndgu wa hao washukiwa, ndio waliojitahidi kutafuta njia angalau ya kuwasalimia, na baadaye gari lililosadikiwa kuwa ndilo la mshitakiwa mkuu, likaingia hapo kila mtu akasimama, na kujongea barabarani, lakini polisi wakahakikisha hakuna mtu anayekaribia eneo hilo, na gari hilo likaingia eneo la mahakama likiwa na ulinzi mkali, likitanguliwa na gari la askari wenye silaha za kisasa, na nyuma yake halikadhalika.

Mtu anayesadikiwa ndiye mshitakiwa mkuu, akateremka, akiwa kafungwa pingu mikononi na miguuni, ilibidi ashikiliwe huku na huku ili aweze kutembea, siji ni kutokana na hiyo minyororo au huenda ni kutokana na kipigo, na kutembea kwake kulikuwa kwa shida, ilikuwa mwendo wa taratibu hadi kufika mlango wa kingia mahakamani.

Jamaa huyo alikuwa kafunikwa usoni, sijui ni kwa kupenda yeye mwenyewe au ni kutokana na walivyoona wenyewe wahusika, kwahiyo hakuna aliyeona sura yake, na hili likazua gumzo, kila mmoja akisema lake, ilimradi una mdomo, kauli ni tashi wako,.. hata waandishi wa habari waliotaka kupata picha yake halisi walibakia kupiga picha za mtu asiyeonekana sura yake, na swali likabakia likiulizwa na watu wengi.

‘Je huyu mshitakiwa mkuu ni nani...’

‘Wamefanya hivi kwa vile wanaona aibu,....’mmoja akasema.

‘Wanaona aibu ya nini…?’ mwingine akauliza.

‘Wewe huoni, au hujasikia, kuwa huyo muhusika ni mmoja wa watu wakubwa wa idara ya usalama, sasa wanaona aibu kwa vile mshitakiwa ni kiongozi wao, kiongozi wa juu wa idara ya usalama , si aibu hiyo, hebu fikiria mtu anayetakiwa kulinda usalama leo hii inashitakiwa kwa dhamana aliyotakiwa kuilinda ....’akasema huyo mtu.

‘Mhh, hata mimi sijiu, ndio maana nimefika , kwani wanasema huyo mtu ni mtu wa miujiza, haonekani ovyo, wengine wanasema sio binadam huenda ni mzuka,..yaaani hata sielewi, kwani wewe unamfahamu mtu huyo ?’ akauliza.

‘Ni mfahamu wapi,…mengine ni ya kuzusha tu, huyo mwanzoni alikuwa ni  hao askari kanzu, akapanda vyeo hadi kufikia hapo alipo, sasa hivi alikuwa ni kiongozi  mmojawapo, kutokana na unyeti wa kazi zao, ndio maana kafichwa kama mwali..’akasema mwingine.

‘Ndio maana hawataki watu kuingia mahakamani, ...’akasema mwingine.

‘Lakini sasa ni mhalifu, unyeti, umuhim wake, haupo tena, kavunja kiapo cha kazi yake…..’akasema mwingine.

‘Ngoja usikie, maana hapa hakna kuona tena….’akasema mwingine.

Watu wakawa na hamasa ya kutaka kujua vyema,ni nini kitakachoendelea, lakini hakuna aliyepata nafsi hiyo  hata ya kusogea, au kusikia kinachoongelewa ndani ya mahakama, na kesi ikawa inaendelea kimiya kimiya ndani ya mahakama kukiwa na ulinzi mkali.

********

Ndani ya mahakama, hakimu alifika na kesi ikatajwa kama ada, na muendesha mashitaka akaelezea mlolongo mzima wa kesi hiyo, na sasa akawa anahitimisha muhutasari wake kwa kusema;

‘Leo kama tulivyoahidi muheshimiwa hakimu, tumemleta shahidi mkuu, ambaye sasa ameshikiliwa kama mshitakiwa mkuu, kutokana na ushahidi ulipatikana...’akasema muendesha mashitaka.

‘Kwahiyo huyo mtu kwa sasa ni mshitakiwa au ni shahidi..?’ akaulizwa.

‘Ni mashitakiwa mkuu muheshimiwa hakimu..’akasema muendesha mashitaka.

Basi mshitakiwa huyo akatakiwa kukubali au kukataa kosa, na hapo ndipo mlolongo wa pingamizi  na kauli za kushangaza zikatokea, kiasi kwamba hata hakimu alibakia kushindwa kuamua kwa muda huo, kwanza mshitakiwa akasema yeye hahitaji wakili, atajisimamia mwenyewe , na ikaja swali la kukubali au kukaata kosa, mshitakiwa  akasema;

‘Kwanza kabla ya yote, mshitakiwa aliyetajwa hapo na mahakama yako tukufu sio mimi....’akasema.

‘Una maana gani kusema hivyo?’ akaulizwa.

‘Mimi sitambulikani kama mlivyotaja hapo, mimi sio mkuu wa kitengo chenu cha usalama, nahisi kuna makosa yamefanyika, mimi ni mtu tofauti kabisa, nahisi mumefanya makosa, na henda  mliyemkamata sio huyo ambaye mlimuhitajia kwa kifupi ...mimi sio huyo mshitakiwa mkuu mliyemtaja hapo, kwahiyo naiomba mahakama yako tukuf iniachilie....’akasema.

‘Acha ujanja ujanja, unataka kusema wewe ni nani?’ akaulizwa.

‘Kuhusu mimi ni nani hili sio la msingi kwa sasa, la msingi je mimi ndiye mshitakiwa mkuu kama mlivyomtaja hapo, mimi ninachotaka kuhakikisha mbele ya mahakama hii ni kuwa mimi sio huyo aliyetajwa hapo kama mshitakiwa, ushahidi ninao..’akasema.

‘Unataka kuhakikishia mahakama hii kwa vipi, una ushahidi gani wakati wewe ni mkuu wa kitengo cha usalama, na umeshikwa kwa taratibu zote,…..? ‘ akaulizwa.

‘Siku hizi kuna utaalamu wa kumgundua mtu kuwa ndiye au siye, kuna vipimo vya DNA, naiomba mahakama yako tukufu ipime damu yangu ili uwe ni ushahidi kuwa mimi sio huyo mtu waliyemshitakia, kwa kifupi mimi sio mkuu wa kitengo hicho cha usalama, kufanana kwa sra isiwe ndio kigezo, mtu, ambaye wanadai ndiye mshitakiwa mkuu, hayupo hapa kamtafuteni, lakini sio mimi, mimi  ni mtu tofauti kabisa, nataka sheria inilinde...’akasema.

Hakimu akawa anamuangalia huyo mtu, halafu muendesha mashitaka, hakaingialia kwa muda huo, akawa anamsikiliza muendesha mashitaka.

‘Hebu tukuulize swali, wewe siye uliyekuwa mkuu wa kitengo cha usalama?’ akaulizwa.

‘Sio mimi nimeshawaambia….’akasema.

‘Hujawahi kufanya hiyo kazi?’ akaulizwa.

‘Nimeshawaambia sio mimi, msipoteze muda, pimeni hicho kipimo, na mfanye haraka kumtafta huyo mtu wenu…’akasema.

‘Hujaeleweka, kwasababu wewe ndiye uliyekamatwa, ukiwa ndani ya chumba, ambacho kinasadikiwa kuwa ni makao makuu ya kiongozi wa kundi haramu, pili wewe ni kiongozi, mkuu wa kitengo cha usalama, inajulikana hivyo, leo hii unakuja na hoja kuwa wewe sio kiongozi wa usalama..usitake kupoteza muda….’ Akaambiwa.

‘Ili kuhakikisha hilo, nataka mchukue damu yangu ipimwe, mtu hawezi kkwepa ukweli wake, kuwa ndio yeye au sio yeye kwa kupitia kipimo cha DNA ….’akasema.

‘Mimi nawahakikishia kuwa sio mimi mliyemkamata, kuna kosa mumefanya, pimeni haraka mtagundua kuwa kweli mumefanya makosa, huyo mkuu wenu wa usalama sio mimi,hayupo hapa ...tusipoteze muda, wataalamu wa damu, na vipimo vya namna hiyo waje wachukue damu yangu wapime…’akasema.

‘Na nawahakikishia, na kama kweli watathibitisha kuwa mimi ndiye kiongozi wao , mkuu wa kitengo hicho, basi nip tayari kujibu mashitaka hayo..lakini kama sio mimi, basi wanishitaki kama mtu baki sio huyo mtu waliyemtaja hapo....’akasema.

Hakimu, ikabidi amuite muendesha mashitaka wakateta, na kweli ikabidi damu ya huyo mtu ichukuliwe kwa haraka na vipimo vikafanyika na kweli ikabainika kuwa sio yeye, DNA, ilionyesha tofauti na DNA, ya mkuu wa kitengo cha usalama, japokuwa kundi la damu, lilikuwa ni sawa, Group O.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, naomba sheria ifuatwe, kesi dhidi yangu ifutwe, na watu wa usalama waafanye kazi yao kmtafuta mshitakiwa ….’akasema  huyo jamaaa.

‘Lakini tukulize, wewe siye uliyekuwa hospitalini  ukitibiwa, wewe siye uliyekamatwa ukiwa kwenye makao makuu ya kundi hilo haramu?’ akaulizwa.

‘Yawezekana nilibadilishwa na huyo mnayemtafuta , lakini maswali kama hayo hayana msingi kwa sasa, swali la msingi, ni je huyo mliyemshitakia ni mimi au sio…tumegundua kuwa sio mimi, hao mengine hayana hoja, muheshimiwa hakimu, naomba sheria ifuatwe,…’akasema mshitakiwa.

Muendesha mashitaka akageuka nyuma kuangalia , alikuwa akimtafuta Inspecta Moto ambaye kwa muda huo bado alikuwa hajafika, akasema;

‘Ndgu muheshimiwa hakimu, nahisi kuna makosa amefanyika , lakini ttukumbuke kuwa kundi hili lina mbinu nyingi, na hii inayotokea hapa ni oja ya  mbinu zao, mwenzangu anafuatilia ushahidi muhimu, kuna taizo limetokea, tunaiomba mahakama yako muda ..’akasema muendesha mashitaka.

‘Unahitajia muda kiasi gani, masaa au siku, …?’ akauliza hakimu
***********
Wakati hayo yakiendelea mahakamani, Inspecta Moto alikuwa akihangaika kumtafuta fundi wa komputa, ambaye alimkabidhi kile kifaa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kinafnguka, kwani nyumba aliyokuwa akikaa hayupo, na hakuna anayefahamu wapi kaelekea, na muda umeshakwisha, alitakiwa kuwa mahakamani.
Akajaribu kupiga simu ya huyo mtu ikawa haipatikani, akawasiliana na mtaalamu wa mitandao kama anaweza kusaidia lolote , lakini mtaalamu huyo akasema sio rahisi maana huyo mtu hajavaliswa, au kuwa na kitu ambacho kinaweza kumgundua wapi alipo, na simu yake haifanyi kazi, imezimwa.

Hapo Inspecta Moto, akachanganyikiwa, na kila mara alikuwa akipokea ujumbe kutoka mahakamani kwa muendesha mashitaka wa kutaka kujua yupo wapi, na ushahidi aliosema anao, upo wapi, unahitajika mahakamani, lakini alishindwa amjibu vipi huyo muendesha mashitaka.

Mara akakumbuka jambo, akamkumbuka nesi….

‘Yes, Nesi, atakuwa kafanya haya yote, ni lazima alifika akakutana na huyu mtu akamshawishi kama alivyoelekezwa na huyu mshitakiwa, inawezakana alimpa pesa na kukichukua hicho kifaa, ni lazima atakuwa nacho huyo nesi, na sizani kama ameweza kumfikishia mshitakiwa,…. ni lazima nimpate huyu nesi kwa haraka iwezekanavyo, ….’akasema na haraka akaingia kwenye pikipiki lake, huku akipiga simu ya nesi, ambayo ilikuwa inaita tu, haipokelewi.

Alifika nyumbani kwa huyo nesi, akitarajia kumkuta hapo, kwani jana yake Inspecta Moto alimpigia simu wakaongea, akitaka kujua  kama alipitia kwa huyo fundi kama alivyoelekezwa;

‘Ndio nilipita tu, nikafika nikakuta ana wateja, nikasubiri, nikaona napoteza muda, basi sikuona haja ya kusubiria nikaondoka zangu…..’akasema

‘Atakuwa wapi huyu fundi maana simu yake haipatikani…’akasema Moto.

‘Akuwa ana wateja wengi, yupo, wewe ukipata mda kesho , hata leo nenda utamuona huenda akikuona wewe kwasababu anakufahamu ataachana na wateja atakusikiliza…’akasema nesi.

‘Basi kama yupo kesho asubuhi nitampiia, una uhakika hujakichukua hicho kifaa?’ akauliza Moto.

‘Nichukua cha nini,…sina haja nacho…’akasema nesi, na Moo akamuamini, akijua kesho yake atapiia kwa huyo fundi, kwani askari waliyemuma alisema alifika nyumbani kwa huyo fundi, hakumkuta, akasubiri karibu siku nzima, lakini huyo fundi hakuonekana. Na alipoongea na nesi, akapata ahueni kuwa fundi huyo yupo, huenda alitoka tu, kipindi askari huyo alipofika hapo, akaweka hali ya kuamini.

Leo anafika kwa huyo fundi, fundi haonekani, ndio akajua huenda nesi kacheza mchezo, ni lazima nesi atakuwa na hicho kifaa na huenda anatafuta mwana wa kukifikisha hicho kifaa kwa mshitakiwa.

Inspecta alijua kuwa atamkuta huyo nesi, kwani nesi alisema siku hiyo ni ya mapumziko kwake, hatakwenda kazini, atakuwepo nyumbani , hata mahakamani hatafika. Inspecta akafika nyumbani kwa huyo nesi, na akiangalia muda, umekwenda kweli, alipofika akaambiwa nesi huyo katoka muda mchache uliopita,kaelekea mahakamani…Inspecta Moto hakupoteza muda, akaendesha pikipiki yake hadi mahakamani.

Alipofika akajaribu kumpigia nesi, lakini simu ilikuwa inaita tu haipokelewi, ina maana kaiweka isitoe sauti, kama yupo mahakamani, yeye moja kwa moja, akaingia mahakamani, na hapo akukutana na yale mabishano na akasogea kumnong’oneza kitu muendesha mashitaka, na muendesha mashitaka  hakukubaliana na hoja hiyo,  akasema;

‘Huyu mtu sio yeye keshatoa ushahidi wa DNA, sio yeye kabisa, inawezekana mkuu wako katoweka, kuna sehem kajificha, fanyeni mpango atafutwe haraka, tusipoteze muda…’akamwambia Moto.

‘Ndio yeye bwana, hawa wanataka kutuchezea, hebu akaguliwe begani kama hana jeraha la risasi, ….kama ana jeraha la risasi, ina maana yeye pia anahusika na mlipuko wa yale mabomu, ..’akasema.

‘Lakini badi haitasaidia, maana ushahidi wa kuwa sio yeye keshautoa…labda nipoteze muda, ili baadaye kesi ihahisrishwe, tujipange pya,..ushahidi umekuja nao…?’ akauliza.

‘Ushahidi umepotea fundi haonekani…’akasema Moto.

‘Sasa hapa hakuna kesi,….’akasema Muendesha mashitaka akiwa kakata tamaa,akamgeukia  hakimu aliyekuwa akiteta na watu wa baraza, akasema;

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, huyu mshitakiwa anahusika kwa yote tuliyomshitakiwa, kuna tatizo la huo utambulishi, hatujui kwa sasa ni kwanini DNA, imetokezea hivyo, ila huyumtu hata siku ile ya mlipuko wa mabom alikuwepo, na alionekana na Inspect Moto, wakati bomu linalipuliw akwenye ile nyumba.

Inspecta Moto alimfyatulia risasi na kumjeruhi begani, kama anabisha, tuone kama hana jeraha begani..’akaambiwa

‘Bado tunarudi kule kule..je mimi mnanishitaki kama nani, …..?’ akauliza huyo mshitakiwa.

anayemsengenya mwenzake, ni sawa na kumla nyama huyo unayemsengenya, tuacha tabia hiyo sio nzuri. ‘Hebu kwanza tuthibitish hilo..’akasema muendesha mashitaka
‘Muheshimiwa hakimu, hawa watu wanafahamu sheria, lakini hawataki kuzitumia, ninaweza nikawa na jeraha hilo, lakini sio lazima kuwa lilitokea hapo..kuna uthibitisho gani kuwa jereha hilo nililipata siku hiyo, na sio mahali kwingine…’akasema mshitakiwa.

Inspecta Moto akawa anatembeza macho kukagua mle ndani kama ataweza kumuona nesi, alikagua bila mafanikio, na wakati ameshakata tamaa, mara kwa pembeni ukutani karibu na mlango,akamuona….

Nesi akiwa kasimama, akionyesha uso wa wasiwasi, akiangalia mahakama inavyoendelea, na alionekana kama anataka kutoka nje, na Moto akaanza kutoka kumfuata, huku nyuma muendesha mashitaka akimuita, lakini hakumsikiliza….

Hakimu akawa anamuangalia huyo mtu kwa mshangao, maana yeye amafahamu, na siku zote anamfahamu kuwa ni kiongozi wa kitengo maalmu cha usalama, lakini lao anapinga, na hata uthibitisho wa DNA, umethibitisha hivyo, kuwa sio yeye,  sasa huyo mkuu anayetakiwa yupo wapi….’akawa anajiuliza.

NB: Samahani kwa kutokuweza kumalizia kisa hiki kwa leo , nilitaka nisubirishe hadi nikimalizie, lakini nimeona ili siku isiishe bure niweke sehemu hi muhimu ya mahakamani….swali je huyo mkuu kapotelea wapi, na huyu mtu ni nani?

WAZO LA LEO: Dunia sasa imeharibiwa na watu wenye nia mbaya , watu ambao wanatumia kila nafasi, kuwazalilisha wenzao, ama kwa mitandao, au kwa majungu, fitina  na kuesenganya ikiwa ndicho kigezo kikubwa. Kusengenya imekuwa hulka ya watu kila wanapukutana, utasikia muone yule, asikuambie kitu yupo hivi, kafanya hivi, ni mbaya, nk ..na kauli hizo zinaweza zisiwe za kweli, lakini nia ni kuchafuliana, kuharibiana, kwasababu ya wivu, choyo na husuda. Kusengenya ni dhambi, mtu 

1 comment :

Anonymous said...

Kazi nzuri mkuu, endeleza kisa usikatishe. ukikatisha utaharibu, kama watu wamechoka kivyao