Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 18, 2014

DUNIA YANGU-65


Inspecta akawa sasa akitembea kuelekea kwenye hilo eneo, ilikuwa ni sehemu iliyojengwa kwa juu kwa aina yake ip kama inaelea hewani, chini imeshikiliwa na nguzo, na mzunguko wa kitu kama nusu dunia, ni ubunifu wa hali ya juu, ni kama vilr dunia ipo kwenye muhimili wake, cha ajabu ukiwa chini huwezi kuiona sehemu hiyo.

Inspecta akiwa na vijana wake wakasogelea hadi sehemu yenye ngazi za kuingilia sehemu hiyo, hadi kwenye mlango, lakini mlango ulikuwa umefungwa, na hapo Inspecta akawasiliana na watu kama yule mtu wa mitandao keshaweza kufanya lolote.

‘Ndio kapewa dawa na yule mzee, inaonekana zimefanya kazi, dawa za huyu mzee kiboko, haliyake  inakwenda vyema, sasa hivi yupo kwenye komputa akijaribu kuweka mambo sawa, ….’akambiwa

‘Ni muhimu sana, maana tumefika kwenye mlango, umefungwa, na hatutaki kutumia nguvu kuvunja huu mlango,nina uhakika mlango huu unafunguliwa kwa mtandao, na hatuna uhakika kama huyu mtu anatuona au tulivyozima mawasiliano ya mitandao yake atakuwa hawezi kutuona, …’akasema Moto,

‘Sasa tufanyeje mkuu..’ wakauliza.

‘Mtu wa kutusaidia kwa hivi sasa ni huyo mtaalamu wa mitandao,...sisi huku tunajaribu kufanya utafiti, tukimsubiria yeye, nina uhakika yeye ataweza kuufungua huo mlango, ila kama kuna simu yoyote itakayojaribikiwa kupigwa kwa huyu mtu, au yeye kupiga sehemu yoyote mufahamishe..’akasema Moto.

Kulipita muda kidogo, kila mmoja akijaribu kuangalia jinsi gani ya kuingia humo kwenye hicho chumba cha aina yake, lakini ilikwa ngumu, mlango ni sehemu moja tu, ni kila kitu kimetengenezwa kwa chuma,…na huwezi kuona ndani, hata walipojaribu kutumia darubuni za hali ya juu, hawekuweza kuona kitu.

‘Huu nu ubunif wa hali yajuu, maana inaonekana hata risasi hazipiti humu…’akasema Moto

‘Mimi naona tujaribu kuvunja, kwa risasi, pale kwenye lango, tunaweza kufanya hivyo mlango ukafunguka….’akasema askari mmojawapo.

‘Hapana, hiyo inaweza ikaharibu kila kitu, ngoja tuvute subira,….’akasema na mara simu ya inspecta ikaingiza ujumbe;

‘Jamaa anasema tayari ameshaingia kwenye anga za dunia yangu, ila amesema kwa kufanya hivyo ina maana jamaa naye atakuwa sasa anaweza kuona kinachoendelea, je aendelee…’akaulizwa.

‘Tunachohitaji kwa hivi sasa ni yeye kuwezesha mlango kufunguka, pili kumzuia huyo jamaa hata kama ataona kinachoendelea asiweze kufanya lolote je hilo linawezekana?’ akauliza.

‘Anasema, ameshamzuia huyo jamaa kufanya lolote, kwani yeye ndiye mwenye uwezo wa kuingia kila mahali, na kuweza kumruhusu mtu kufanya lolote kwenye mtandao wa kundi, kwahiyo alipoingia tu, akazuia watu wote kuweza kufanya chochote ..yeye tu ndio anaweza kufanya apendavyo….’akasema.

‘Je jamaa huko anaweza kuona kwa kiasi gani kinachoendelea?’ akaulizwa.

‘Ataona ile sehemu ya jengo, watu wanavyoingia na kutoka, lakini haweza kuzungusha kuona zaidi ya  hapo, na hawezzi kuwasiliana na yoyote yule….’akaambiwa.

‘Kuna kitu gani kingine alichokigundua ambacho kinaweza kuhatarisha maisha…?’ akaulizwa

‘Kuna kiashiia cha bomu, ambalo limewekewa muda, anasema bomu hilo walikuwa wameliweka kimajaribio huwa ikikaribua muda fulani, wanarudidha nyuma, lilikuwa la majaribio tu, lakini inavyoonekana jamaa yetu huo hapo anataka kulitumia, alishaliamrisha lije kufyatuka,…ndio anajaribu kutafuta njia ya kuongeza muda, au ikibidi kulizima kabisa, hiyo ndio inamsumbua kwa hivi sasa….’akaema.

‘Oh, sasa hiyo ni hatari , ina maana jamaa kazimiria kufanya unyama wa namna hiyo, hilo bomu likilipuka, litauwa watu wangapi, na uharibifii kiasi gani….ajitahidd awezavyo, na  tunashindwa kuwaarifu watu, ila ikibidi aseme haraka tuone jinsi gani tutawaokoa watu…..’akasema

‘Amesema usifanye hivyo, anajua jinsi gani ya kulizuia, ni swala la muda tu…na kwa vile vile ameshamzuia huyo mwendawazimu kufanya lolote, hakuna hatari itakayotokea, amesema tumpe muda….’akaambiwa.

‘Je huyo mtu ana silaha gani nyingine hapo alipo?’ akauliza Moto.

‘Hapo alipokaa, ni mtambo wenye silaha za kila namna…lakini mtaalamu hapa anasema ameshazizuia kufanya kazi, lakii hatuwezi kujua yeye mwenyewe anaweza akawa na silaha nyingine ambazo hazihitaji mtandao,…amejaribu kumkagua hajaziona…..’akasema.

‘Huyu mtu kwa hivi sasa mwenyewe yupo wapi?’ akaulizwa.

‘Yupo kwenye kiti chake cha enzi ambacho anazunguka nacho chumba kizima, ni kama ndege, inakwenda huku na kule, hiyo ndege ndiyo yenye hizo silaha….hutaamini ni sehemu ndogo kwa nje, lakini ukiingia ndani utaona ukubwa wake, chombo hicho kinaelea hewani, na akitka kutoka nacho nje, kinatoka kama ndege ya kawaida ndogo, na kimelengwa kwenda kutua baharini, na kikitua baharini kinageuka kuwa nyambizi,..kinazama na kutembea majini , chini kwa chini…’akaambiwa.

‘Je anaweza kufanya hivyo,akitaka?’ akauliza moto.

‘Hawezi kwa vile kinatumia mtandao, na jamaa keshakizuia, kwa hivi sasa kimesimamishwa kati kati ya chumba, hakiweza kwenda kokote,…..’akaambiwa.

‘Safi kabisa….’akasema Moto, na kutulia kidogo, haafu akauliza.

‘Hilo bomu linasema limebakiza dakika ngapi kulipuka, na madhara yake ni kiasi gani?’ akauliza.

‘Kama litalipuka madhara yake ni makubwa sana, litaathiri jengo zima,…likilipuka tu,  hicho chombo kama ndege kitatoka na kuruka haraka sana, kwahiyo yeye atasalamika kabisa na hatawezekana kuonekana  tena, kwani nyambizi hiyo ina kazi ya hali ya juu, jamaa anasema ameshakaribia kulidhibiti hilo bomu, tusiwe na wasiwasi…’akaambiwa.

‘Mlango hajaweza kufungua?’ akauliza moto, akiwa na hamasa ya kuingia ndani

‘Anasema ukifungua mlango tu, bomu lingeliweza kuongeza mwendo wa kilipuka, ndio maana hakufanya hivyo kwanza, alichokimbilia kufanya ni kutafuta njia ya kudhibiti hilo bomu,na kuangalia kama kuna silaha nyingine yoyote anayoweza kuitumia huyo jamaa, akimaliza hilo ndio awafungulie mlango..’akaambiwa.

‘Na huyo jamaa mnamuona moja kwa moja hapo mlipo, anafanya nini kwa hivi sasa anaonekanaje?’ akaulizwa.

‘Jamaa anaonekana kama roboti, yupo ndani ya hicho kiti chake cha enzi ambao kajivika vifaa kama roboti, huwezi kumuona sura yake…sasa hivi anajaribu kujinasua atoke, lakini haiwezekani tena, keshakata tamaa, na kila mara anajaribu kuwasiliana na mtaalamu hapa, lakini haiwezekani kwa vile keshamzuia….’akasema .

‘Ok, kazi nzuri, ngoja tumsubirie huyo jamaa amalize kazi yake, ili tuweze kuingia,….’akasema Moto.

‘Jamaa anasema anataka amumalize humo ndani ya chombo chake kwani alimtesa sana, na yeye ana kisasi naye, tumejaribu kumshauri, na kakubaliana na sisi….’akasema

‘Mwambie asije akafanya hivyo, huyo mtu anatakiwa afikishwe mahakamani na haki itendeke, akimuua, tutakuwa hatujafanya la maana, maana kuna mengi a kufahamu , huyu mtu ni nani, ni kweli ni yule mkuu wetu wa kazi,…’akasema Moto.

‘Ndiye huyo huyo…..unahis ni nani mwingine, alikuwa akituchezea akili tu, sijui ilikuwaje akabadilika hivyo, nahisi alipokutana na huyo mumiliki wa hiyo miradi ..akashawishika, na huenda, walikubaliana kuwa yeye awe mrithi wake, au wana udugu fulani….’akasema mwenzake.

‘Hiyo yawezekana, lakini mimi nina hisi anyingine, …na hilo tutalipaat zaidi kwenye hichi kifaa chake anachokitafuta,….’akasema Moto.

‘Kifaa gani hicho?’ akauliza mwenzake.

‘Kuna kifaa cha komputa, inavyoonekana humo kuna siri kbwa sana, ambayo hakutaka ijulikane..’akasema Moto.

‘Oh, najua nilishasahau kuwasiliana na huyo askari niliyemtuma, kwani kilikuw ani kifaa gani, ?’ akauliza mwenzake.

‘Hakikisha huyo askari anakipata mapema, iwezekanavyo kabls ahuyo nesi hajamfikia huyo jamaa, nilijua ameshakichukua ndio maana nikamwambia huyo nesi, afanye kama alivyoaizwa, sasa unaongea kitu gani, msije mkaharibu utaratibu…’akasema moto akijaribu kumpigia huyo jamaa aliyempa hicho kifaa akifanyie kazi, lakini simu yake ikawa haipatikani.

‘Kwani huyo nesi ni nani wake?’ akauliza mwenzake

‘Kwa hivi sasa ndiye mtu aliyebakia wa kumsaidia, walikuwa na mahusiano, urafiki wa siri, lakini kama umjuavyo jamaa huyu wetu hana rafiki wa kudumu, ukawa hana faida kwake, anakumaliza, umeshampigia huyo askari simu….?’akasema Moto na kuuliza

‘Ndio anasema sasa hivi yupo hapo kwenye eneo la nyumba ya huyo jamaa, na jamaa anaongea na mteja ndani

‘Muulize ni mteja gani?’ akauliza.

‘Oh simu yake haipatikani tena….’akasema mwenzangu

‘Ghoosh,….hebu nipe namba yake..’akasema Moto

‘Una uhakika huyo nesi hajafika sa hizi kwa huyo jamaa’ akauliza mwenzake.

‘Alisema anakwenda nymbani kwake kwanza, ….’akasema Moto akijaribu kuwasiliana na huyo askari, na alipompata akamuliza

‘Upo wapi?’ akamuliza

‘Nipo kwa huyu mtaalamu wa komputa…’akasema

‘Umeshaongea naye?’ akaulizwa

‘Bado ….namgongea hafungui mlango, naona kama anaongea na mtu ndani….’akasema

‘Ni mtu gani huyo anayeongea naye?’ akaulizwa

‘NI mwanadada….’akasema

‘Hakikisha huyo mwanadada hakipati hicho kifaa, ….lishaongea na huyo fundi kabla  kwenye simu?’ akamuliza

‘Ndio nilimambia kama ulivyoniagiza

‘Akasemaje?’ akaulizwa

‘Tutaongea ukija….alisema hivyo tu,….’akaambiwa

‘Nampigia hapatikani,….gonga kwa nguvu, ikibidi ungua mwambie polisi.ni muhimu sana….’akasema Moto, na mara simu yake nyingine ikawa inaita akaangalia kaona hakuna namba, akaipokea, na sauti ikasema;

‘Moto, welcome to my world, nakusubiri kwa hamu…..’sauti ya kujirudia ikasikika masikioni kwake, na mara ule mlango wa kile chumba ukafunguka

*********
Wakati hayo yakiendelea, nesi alifanya kama alivyoagizwa na mtu wake, akapitia kwa mhasibu, akpewa pesa nyingi tu zikiwa ndani ya briefcase, hakujua ni kiasi gani, na haraka akaelekea sehemu aliyoagizwa, kichwani alikuwa anashindwa kumkatalia mtu wake, lakini hapo hapo, akili nyingine ilishamuingia, akawaza kufanya jambo lenye manufaa mbeleni.

‘Huyu mtu sasa hivi watamkamata, wakimkamata ina maana na mimi nitakuwa mshukiwa, kwanini nisikipate hicho kifaa, nikakitumia kama silaha, nikatajirika na mimi zaidi, nikapata angalai moja ya kumi ya huu utajiri wa huyu jamaa, hata akinipa hisa kidogo nikawa sina shida ya maisha, ,…..’akasema

‘Mhh, nikikipata hicho kifaa, nitamwambia huyo mtu wangu, anipe pesa nyingi, nyumba keshanijengea, lakini nahitaji pesa zaidi nikamilishe nyumba ya huko kijijini, nifungue duka kubwa la vifaa vya jumla, nifungue na duka la madawa, niachane na hii kazi ya kuajiriwa….nitakitumia kwa malengo ya kujinufaisha, ..’akawa anawaza

‘Hapo hapo akakmbuka maswala ya polisi, akasema kimoyo moyo, ‘Hawa polisi wakikihitajia,mmmh…..sijiu, kwanza polisi watanipa, nini, hawana pesa….nitawaambia nimeshakiharibu,au nitatoa nakala ya kuwadanganyia….’akasema na muda huo alishafika kwenye nyumba aliyoelekezwa, akalisogeza gari lake sehemu salama, akatoka na ile briefcase.

‘Hakuna vibaka kweli huku….’akasema lakini kwa hali ilivyo pale hakuna mtu anayeweza kumvamia, kuna watu wengi na mishughuliko, akaondoa wasiwasi.

Akagonga mlango, na mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja akiwa kifua wazi, ni kama alikuwa akipika au alikuwa kwenye kazi ya kumtoa jasho akawa kasimama kati kati ya mlango, akasema;

‘Oh, kuna joto kweli……..’akasema

‘Wewe ndiye mtaalamu wa komputa?’ akauliza nesi akimkagua mtu mwenyewe, kwani alikuwa haelekei kabisa.

‘Haswa…na wewe ni nani na unataka nini kwangu, una tatizo la komputa yako, au unahitaji picha za urembo, nikikupiga picha wewe, nikaweka kwenye mtandao utakuwa tajiri, wewe ni mrembo sana, umbo lako linavutia, ulivyo hapo wewe ni pesa…unalijua hilo, karibu tufanye dili ya pesa, halafu utanikatia kidogo…unasemaje, ?’ akaulizwa

‘Hapana…sijafika hapa kwa hayo, sina shida ya pesa, pesa ninazo za kutosha,..ila kuna tajiri mmoja, ana pesa za kumwaga, hana shida ya pesa, pesa kwake ni kitu kidogo sasa kanituma kwako,…’akasema mdada, na yule jamaa kusikia neno pesa, tajiri… akaonekana kujilamba mdomo.

‘Pesa,..pesa mmmh,, tajiriieeh, ana pesa, mmh, hayo ndio maneno nayataka, lakini pesa anazo kiasi gani, maana pesa thamani yake ni wingi au sio, kwanza anataka nini kwangu?’ akauliza huyo jamaa akianza kujenga matumizi hewani, akikumbuka kuwa muda mchache uliopita alikuwa akigombana na mwenyenyumba aliyekuja kudai pesa yake ya pango, hajalipa mwezi wa pili sasa.

‘Ni kitu kidogo tu, ni kifaa ambacho  unacho wewe,….sasa ni wakati wako wa kuinuka, uwe na uwezo wa kuanzisha kampuni yako mwenyewe, uwe na nyumba yako mwenyewe, huyo jamaa ni tajiri sana, atakupa pesa nyingi tu, kwanza ukimpa hicho kifaa, kifaa chenyewe hakina thamani hiyo, lakini ni cha kwake, kilipotea, amesikia unacho wewe….’akasema Nesi

‘Mhh, kifaa, kifaa gani hicho, na huyo mtu ni nani..hapana nahisi umepotea, mimi sijawahi kuokota kifaa…kifaa gani hicho?’ akauliza huyo jamaa akijaribu kuwaza ni kifaa gani hicho cha kuhitajiwa kwa pesa nyingi.

‘Kumbuka kuwa huyo ni mtu ni tajiri sana…na matajiri huona mbali sana, unafikiri kakonaje kuwa una hicho kifaa, ..’akasema nesi, wakiwa wameshaingia ndani, kulikuwa ni chumba chenye kitanda, feni ndogo, vifaa vingi vya komputa vilikuwa mezani, …joto lilikuwa kali kweli, na nesi alitamani atoke humo ndani haraka, akasema;

‘Unaona hizi pesa hapa, zote ni zako, lakini anachohitajia ni hicho kifaaa…’akasema nesi na kufungua briefcase iliyojazwa manoti,..na jamaa alipoona yale manoti, akajilamba, na macho yakamtoka pima kwa tamaa, hakuamini

‘Zote ni zangu, mimi sina kifaa chenye thamani kubwa kiasi hicho, sema ni kifaa gani, mimi nitakupa, kwa pesa kama hiyo, ninaweza kukupa vitu vyote nilivyo navyo humu, havifikii thamani ya hiyo pesa, ni kifaa gani hicho?’ akauliza akiwa anazikagua zile pesa na kwa mahesabu ya haraka, zinaweza kufikia hata zaidi ya milioni hamsini….zinaonekana zimepangwa kwa milioni milioni…

‘Kifaa alichokupa jamaa mmoja anayeitwa Moto….’akaambiwa

‘Oooh, nini….oh, Moto,..sasa huo mtihani’ akasema na kukaa kwenye kiti akionyesha kuwaza na akilini akawa akiwaza…..`lakini tangu huyu Moto afike hapa,hajarudi tena, yeye kazi yake kupiga simu, kuulizia nimfikia wapi, yeye anafikiri mimi nitaishije, ....'

Na hapo hapo akakumbuka kuna mtu aliyesema ni askari, aliyedai kuwa katumwa na Moto, kasema atakuja kukichkua hicho kifaa, akamuahidi kuwa kama kazi imeisha atakuja na chochote, chochote inaweza ikawa elifu kumi au hata thelethini,sasa hiyo itamsaidia nini, yeye atabakia na umasikini wake, na wakati kuna mtu kaja na mamilioni, kwanini aikate hii bahati…...' akawa anawaza

Yule jamaa akageuka kuiangalia bahasha, ambayo alishakiweka hicho kifaa ndani ya hiyo bahasha ili akija huyo askari amkabidhi,..yeye alipohakikisha kimefunguka, akawa hana kazi nacho,  hakutaka hata kuangalia ndani kuna nini, akakichuka na kuweka kwenye bahasha, na muda huo ndio alikuja mwenye nyumba wakaanza kuzozana, ikamfanya asahau kila kitu.

‘Kumbe kifaa chenyewe ni mali…ningelijua nikatoa hata nakala moja au nika-save kwenye kumbukumbu zangu….’akawa anajilaumu kichwani

‘Nitakupa hicho kifaa..lakini….’akasema na kusimama na huyo nesi akadakia, kwa kusema;

‘Nionyeshe hicho kifaa kwanza nihakikishe kuwa ni chenyewe, na pesa hizi ni zako….’akasema nesi akilifunga lile briefcase na kulishika mkononi, na mara mlango ukagongwa kwa nguvu, na nesi akasema;

‘Ni nani huyo….?’ Akauliza kwa mashaka

‘Hao ni wateja….usiwe na wasiwasi nao nimeshawazoea acha wagonge wakichoka wataondoka….’akasema akisogelea ile bahasha yenye kile kifaa, tayari kumkabidhi huyo mdada, na moyoni, akipanga kuwa huyo mdada akitoka tu, na yeye anatoka kwa mlango huo huo, acha huyo anayegonga agonge mpaka kesho, yeye akitoka tu anatafuta bajaji, anaondoka eneo hilo na kutafuta sehemu nyingine ya kuishi, kuanza maisha mapya akiwa tajiri.

‘Huo mlango wa nyuma mbona haufunguki, hebu nifungulie nitoke huko, kipo wapi hicho kifaa…nataka niondoke…?’ akauliza nesi,na wakati huo mlango ukawa unagongwa kwa nguvu, na yule jamaa akawa ameshatoka kile kifaa kumthibitishia huyo nesi.

'Ndio hiki, hii ni external hard drive, ina nguvu sana na huhifadhi vitu vingi sana,ilikuwa wamei-lock, nikafungua kwahiyo sasa unaweza kufungua bila shida, ...mimi sijiu kuna nini ndani yake.....'akasema

Nesi hakuwa na uhakika nacho, maana hajawahi kukiona kabla kama ndio hicho au huyu jamaa katumia mbinu, lakini akaamini kuwa ndio chenyewe, akasema;

‘Kiweke humo humo kwenye bahasha,..nipe niondoke,..kama utaleta ujanja nakuapia haitapita sikuu ya leo utakuwa marehem....’akasema na jamaa akasogezewa hilo briefcase kwa sasa ni mali yake, akiwa haamini, macho yake yakiwa yanaiangala ile briefcase na tamaa ya matumizi ikawa imeshamteka moyoni.

‘Usiwe na wasiwasi kabisa, hiki ndicho alichonipa Moto,....kama huyo tajiri ndicho anachohitajia ndio chenyewe, labda kiwe ni kiti kingine...'akasema

'Sawa mimi nimekuamini...'akasema nesi akikipokea, na kukiweka vyema mkononi

'Sasa wewe tokea mlango huo, na hakikisha hauonekani, mimi mwenyewe nitatokea hapo hapo, sihitaji wateja tena….’akasema na mlango sasa ukawa unagongwa karibu ya kuvunjika, na sauti ikasema

‘Mimi ni polisi fungua mlango haraka…..’ na yule nesi akawa ameshafungua mlango, na kuanza kutoka nje, na jamaa naye akawa anavaa flana yake, tayari kutoka na kutokomoe mitaani.


WAZO LA LEO: Shida zinaweza kumfanya mtu akawa mtumwa,akauza hata utu wake, hata kuzalilika, yote hayo ni mitihani ya kimaisha. Ndugu ukikabiliwa na shida, matatizo sikate tamaa, na usikubali kuuza utu wako, ukarubuniwa kwenye mambo yasiyofaa, kama ya uhalifu, au tabia chafu, kumbuka utajiri, pesa, vyote ni vya kupita tu, lakini utu wako, na heshima yako ina thamani zaidi ya hivyo vitu.


mimi: emu-three

No comments :