Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 12, 2014

DUNIA YANGU-61


Inspecta Moto, alipotoka mahakamani moja kwa moja alielekea huko hospitali alipokuwa kalazwa mkuu wake wa kazi,..akilini akitaka kujua jinsi gani huyo mtu aliweza kutoroka hapo hospitalini, na wapi mtu huyo amekimbilia, na alijua sehemu ambayo itampa fununu, ni hapo hapo hospitalini, na atakayeweza kumsadia ni huyo nesi aliyekuwepo siku hiyo, na huyo docta msaidizi lakini kwanza lengo lake ni kuonana na huyo nesi.

Muhimu alihakikisha hao mashahidi hasa huyo aliyekuwa akitumiwa kwa mitandao na mawasiliano, wapo kwenye sehemu ambayo hawawezi kuwasiliana na mtu yoyote nje, na kama wakifanya hivyo, mawasiliano yao yadhibitiwe, alishajua kabisa, kundi hilo hutegemea sana mawasiliano na mitandao , na hiyo kwa kiiasi kikubwa sasa wameshaidhibiti....

Akawasiliana na watu wake waliopo huko hospitalini akaambiwa huyo nesi yupo toka asubuhi na ikifika saa kumi ataondoka kwahiyo asichelewe akawaambia wasije kumwambia huyo nesi kuwa yeye anafika hapo kuonana naye naye, anataka amshitukizie tu...

Kwa haraka akafika eneo la hospitali hiyo, alipofika mlangoni, akakutana na mwanadada akitaka kufungua mlango kingie, Inspecta akamuuliza kama anafanya kazi hapo, na huyo  mwanadada akasema yeye ni nesi  wa hapo ndio anaingia ili wale wa asubuhi waweze kuondoka;

‘Ninataka kuonana na nesi mmoja alikuwepo toka asubuhi..’akasema Inspecta

‘Umekuja kwa mataibabu au una miadi na huyo nesi….?’ Akauliza

‘Nina miadi naye..?’ akasema Inspecta na huyo dada akatabasamu na kusema

‘Bado atakuwepo, nahisi atakuwa keshabadili nguo za kazi, ukiingia ndani utamuona….’akasema huyo mwanadada akiendelea kutabasamu

‘Kwanini unatabasamu sana?’ akamuuliza

‘Hapana nimefurahi sana,…najua mwenzangu anakwenda kupumzika  kwa raha, maana hizi kazi zetu zinachosha, inatakiwa ukitoka, angalau ujipongeze, uondoe usongo wa siku nzima…..’akasema

‘Nimekuelewa, vipi kuna mgonjwa nasikia alitoroka…?’ akauliza

‘Huyo huyo utamuuliza, maana yeye alikuwepo siku hiyo, na hayo ni maswala ya kiofsi zaidi..karibu ingia, ndani….’akasema yeye akionyesha anamsubiri mtu aliyekuwa akija muelekeo huo na aianspecta hakupoteza muda akafungua mlango kuingia

********

Inspecta akafungua mlango, na macho yake yakatua sehemu wanapokaa manesi watoa huduma mbali mbali, na kwa bahati nzuri, akamuona nesi mmoja mmoja, akionekana yupo tayari kuondoka, kwani alikuwa kashikilia mkoba, na simu akiangalia mlangoni,....

‘Huyu naye anachelewa kuingia hajui muda umekwisha, wengine tuna videti vyetu….’akasema na mara macho yake yakakutana na ya Inspecta

Inspecta alipomtupia jicho huyo nesi,, akugunda kuwa ndio huyo aliyeambiwa kuwa ndiye aliyekuwa akimuhudumia huyo mgonjwa aliyetoroka...

'Huyu ni lazima atakuwa anajua wapo huyo mtu yupo, nitambana mpaka aniambie ukweli....' Inspecta akasema kimoyo moyo

Wakati anaingia pale mlangoni, alimuona huyo nesi akiwa ameshashika mkoba wake, na sasa uso wake ukawa kama unamkagua Inspecta kwa bashasha, Inspecta akaona hiyo ndio nafasi adimu, hatakiwi kuipoteza, akatembea kuelekea pale alipokuwa huyo mwanadada.

‘Huyo mwanadada, alikuwa kavalaia vizuri, akionyesha kuwa akitoka hapo kuna sehemu anaelekea, sio mvao wa kulekea nyumbani, ni mvwao wa kipekee, na kutokana na ile kauli aliyoisikia kutoka kwa huyo mdada kuwa ana `kideti’ akajua huyo dada kuna sehemu atakuwa anakwenda, na moyoni akasema;

‘Huenda huko unapotarajia kwenda usiiende, yote inategemea ushirikiano wako….’

********
Yule nesi alipomuona Inspecta anaingia kwanza akaachia ule mkoba ukatulia mezani, akamtupia jicho huyo mtu aliyeingia sasa hivi, akajaribu kukumbuka kama alishawahi kumuona kabla, lakini sura ikawa haimjii akilini, lakini huenda ni mteja kaja kutibiwa, na inaweza ikawa Bahati ya saa kuondokea, akatabasamu tabasamu la kukaribisha...

Akahesabu moja mbili, na tatu akaachia ule mkoba pale mezani , na kuanza kutoka pale mezani kumpkea huyo mgeni, japokuwa aliju amuda wake wa kazi umekwisha, taratibu kwa madawa, akajivuta kumpokea huyo mgeni, akamsogelea mteja, kumpokea, kwa tabasamu, yeye kama nesi, licha ya kazi yake hiyo, lakini pia anajua jinsi gani ya kumvuta mteja, kwani mteja kwenye hospitali hiyo ni mfalme anatakiwa kupokelewa kwa bashasha....

Lakini pia moyoni, kwa muonekano wa huyo mgeni,  alihisi inaweza ikawa Bahati ya kukutana na mtu atakayeweza kumsahaulisha mihamaniko ya siku nzima, ....kwani mgeni huyo alikuwa mtanashati, mrembo, na ana maumbile ya kimazoezi, na pia hayo mavazi yanaashiria mmmh anazo....

Mhh, ama kweli kazi na dawa…

*********

Yule nesi akamsogelea yule mtu, na akajikuta akitoa mkono wa kushoto kusalimiana, na yule mtu akatoa mkono wa kushoto pia, hiyo ni ishara muhimu kwake kwa wateja maalumu ambao wakiingia humo anatakiwa kuwatambua, wateja hao hupata huduma kipkee,  lakini bado hakuwa na uhakika na huyo mtu, kwani hakumbuki kumuona kabla, akasema;

‘Oh,….dunia yangu ya leo imeshatoka, sijui yako vipi…’akasema.

Hakupata jibu alilolitegemea, hapo hapo akajua kuwa huyo sio wale wateja maalumu, akasema;

‘Samahani kaka,  mimi ndio naondoka, muda wa kazi imekwisha…unahitaji kuonana na docta, au…?’ akauliza

‘Mhh, kwanza nataka kuongea na wewe, kujua taratibu zenu….’akasema

‘Oh karibu, naweza kuksaidia kwa muda, wakati tukimsubiria mwenzangu, naona kwa mbali anakuja….’akasema.

Inspecta naye akiwa na tabasamu mdomoni , akajua sasa anaweza kupata alichokitaka kutoka kwa mwanadada huyo, kwani kwa muda kama huo watendaji hawa huwa wameshachoka, ukiongea nao unaweza kupata jibu la kukatisha, tamaa, lakini alichokipokea ni tabasamu murua na yeye hakuwa na ajizi akalijubu kwa lile tabasamu lake la mitego,  na kweli nesi akasawajika.

‘Mhh, mimi nimekuja kuonana na wewe….’akasema huyo mtu mgeni na kumfanya nesi atabasamu kwa macho y udadisi

‘Mmmh, lakini mbona mimi sikujui….’akasema  huyo nesi akitabasamu kwa kuonyesha aibu ya kike.

‘Utanijua tu, ...mrembo, umependeza kweli mrembo, …utafikiri sio yule aliyekuwa na lile vazi la kuwajibika…naona tukitoka wote leo nitaumia kwa wivu…..’akasema Moto

‘Hahaha , kwanini, mmh, mbona ni kawaida, tu, mmmh, ehe nambie….’akasema wakiwa wameshafika kwenye sofa la wageni, na wote wakakaa, na nesi akakunja nne, na sehem fulani ya mapaja ikawa wazi, Inspecta hakujifanya hajamuona, ila akaona, asipoteze muda, akasema;

‘Mimi ni mara kama ya pili hivi kufika hapa lakini sijawahi kukuona,….’akaanza kusema

‘Unajua tupo wengi, na wakati mwingine, kama kuna akzi nyingi sana, tunakuwa na zamu fupi fupi, lakini kipindi kama hiki hakuna kazi sana, wengi wanapewa likizo fupi kujipumzisha, kazi zenyewe zinachosha…’akasema

‘Kwahiyo wewe sasa hivi umeshamaliza zamu yako unakwenda nyumbani?’ akamuuliza

‘Mhh, sio lazima niende nyumbani, ukiwa singe unakuwa huru, huna majukumu, kwahiyo naweza kupitia sehemu nikapoteza mawazo kidogo, kabla ya kwenda nyumbani..’akasema

‘Kuna mtu unatarajia kuonana naye?’ akamuuliza

‘Mhh, ….yawezekana hayo ni mambo binafsi,… haya nambie, maana nataka kukabidhiana na mwenzangu,leo kanichelewesha kweli, muda huu nimeshaondoka…’akasema

‘Kabidhiana naye basi, nataka tuongee kidogo….’akasema

‘Mimi nilijua umekuja kutibiwa….’akasema kwa mshangao

‘Mhh, kwa leo, nimekuona wewe, ..na naona nisipoteze Bahati hiyo huwezi kujua, bahati  kama hii haiji mara mbili , nenda mkakabidhiane mimi nakusubiri hapa….’akasema na hyo nesi akionyesha uso wa furaha, akakunjua ile nne kwa madhaha yake, halafu akasimama akavuta sketi  yake iliyokuwa imepanda juu kidogo, kuonyesha heshima, halafu akatembea kuelekea ofisi yao ya kazi, huo mwendo wa kutoka hapo, ulimfanya Inspecta atabasamu, na moyoni akasema;

‘Huo mwendo utausahau tu….japokuwa ni mdada mrembo, lakini simuamini kabisa, naisi kuna jambo kwa huyu mdada…ni hao hao….’akasema kimoyo moyo

Inspecta akachukua muda huo kukagua kwa macho huku na kule, alitaka kusimama kutembea huku na kule, lakini kabla hajafanya hivyo huyo nesi akarudi, na kuja kukaa pale kwenye sofa, akakunja nne yake kama kawaida inaonekana anapendelea kufanya hivyo, au…. Na kabla Inspecta hajamaliza kuwaza hivyo huyo mdada akasema

‘Haya nambie…..’akasema huyo mdada akimgeukia kumuangalia usoni Inspecta na tabasamu tele usoni, na hapo Inspecta Moto akaona asipoteze muda, kwani kaja kikazi na muda ni muhimu sana, akasema;

‘Mimi ni ofisa usalama nahitaji kukuhoji mambo fulani kuhusiana na mgonjwa aliyetoroka hapa hospitalini kwenu…’akasema Inspecta Moto na huyo mdada,akageuza uso taratibu na kuanglai mbele, uso uliokuwa umejaa tabasamu ukabadilika, na ukaja uso mwingine uliojaa hasira, na huyo mdada akakunjua ile nne na kuweka miguu yake sawa, akasema;

‘Lakini nimeshaongea na askari mwingine aliyenihoji, sasa nitaongea na askari wangapi, mjue na mimi nachoka kuongea, saa hizi nimetoka kazini, nimeshajichokea, ..unajua kuna muda  natamani nikimbie….kiukweli  umeshaharibika siku yangu….’akaanza kulalamika na maneno haya ya mwisho aliyaongea kwa sauti ndogo `umeshaniharibia siku yangu’

‘Samahani kwa hilo…na sizani kama siku yako itaharibika kama ukienda na mimi sambamba, sina nia mbaya na wewe, ni kiasi cha kuniambia ukweli tu unaoufahamu, kwani inabidi nifanye hivi kikazi zaidi, maana huyu mtu aliyepotea ni mtu muhimu sana kwetu, unafahamu cheo cha huyo mtu aliyepotea…?’akauliza Moto

‘Cheo chake kinanihusu nini mimi,  hakinisaidii chochote, na wala sijui kama ni askari, mimi kwenye kazi yangu nikiwa hapa hospitalini ni kuhudumia watu wote bila kujali yupoje…ana cheo gani, au ana rangi gani hayanihusu kinachohusu ni kuwa kaja kutibiwa….’akasema akionyesha kukerwa.

‘Basi huyo mgonjwa  ni mtu mkubwa sana, na kupotea kwake, kunatupa mashaka , haiwezekani itokee hivyo, ndio maana nimeona nije niongee na wewe moja kwa moja, samahani kwa kukupotezea muda wako wa mapumziko, lakini ni bora tuongee sasa hivi, kuliko mtu kuja nyumbani kwako wakati umeshaanza kupumzika…’akasema Inspecta

‘Lakini mimi siruhusi kuongea mambo ya humu, kwanini usiende kuonana na msaidizi wa mkuu, yupo ofisini kwake, na anaendelea vyema tu,….ofisi yake ile pale….’akasema akionyeshea kidole na kutaka kusimama inspecta akaweka mkono mapajani kwa huyo nesi kumzuia asisimame, na huyo nesi akaangalia ule mkono, akakunja uso….

‘Hapana mimi nataka kuongea na wewe, na ikibidi nitakwenda kwake, ama kwa mambo ya kiofisi usijali nimeshapata kibali kutoka kwa docta wenu mkuu, tulikuwa naye mahakamani….’akasema na kumfanya huyo nesi anywee, akatulia, halafu akasema;

‘Docta mkuu mlikuwa naye….kwani kapatikana….ooh, mimi najua hajapatikana, mbona mambo yameharibika, ..ooh, ok, ok….kwahiyo unasemaje?’ akawa anababaika

‘Basi tulia tuongee, ujue upo huru na salama, docta mkuu wenu yupo nyuma yenu, na usiwe na shaka kabisa, toa ushirikiano tuweze kulimaliza hili….’akasema Inspecta na nesi huyo akaonekana kuwaza jambo, na baadaye akasema;

‘Kwanini mnahangaika kumtafuta huyo mtu, mimi sioni kama ana tatizo kubwa sana, yeye ni mtu mzima hawezi kupotea,…’akasema na inspecta akamwangalia na kutabasamu, na huyo nesi akionyesha kuwa mashaka, alionekana sasa kuwaza jambo;

‘Ni muhimu apatikane…’akasema Moto

‘Haya niambie unataka nini kwangu, au maswali ni yale yale, maana kila kitu nimeshamuambia huyo askari mwenzenu kwanza nitajuaje kuwa wewe ni askari…’akasema na Inspecta akatoa kitamblisho chake, na huyo nesi akakitazama bila kukigusa, halafu akasema

‘Kumbe ndio wewe, Moto wa kuotea mbali….’akasema akimkagua Inspecta usoni.

‘Moto wa kuotea mbali una maana gani,…. umeniskia wapi nikitajwa, anyaway achana na hilo, …..nataka tuongee faragha, wapi patakuwa pazuri?’ akauliza Inspecta Moto

‘Hapa hapa panatosha….’akasema huyo nesi sasa akionyesha kuwa na wasiwasi.Na Inspecta Moto akaona amtoe mashaka akasema;

‘Najua wewe kama nesi unakutana na majaribu mengi tu, wagonjwa wa kila aina sizani kama moyo wako unaweza kutekwa na mashaka kwa vile unaongea na mtu wa usalama, umeshaongea nao sana, au sio,..na sioni kwanini uwe na mashaka, hujakosa hujafanya  lolote baya au sio….kwahiyo ni lazima ujiamini, …kwanza wewe ni mrembo, na urembo wako ni hazina au sio….’akasema Inspecta na huyo nesi akajibarugua na kutabasamu.

‘Wanaume bwana , nyie kila mkimuona mwanadada mnakimbilia huko, mzuri, mrembo, unapendeza,…aah, nimeshawazoea….haya niambie, maana natoka kuondoka, umeshaniharibia siku yangu….’akasema

‘Hahaha…usijali, hiyo ni hulka, ya kibinadamu,…usiwe na shaka siku yako ipo pale pale…..’akasema Moto, na alipoona huyo mdada amekaa sawa, akaanza kumuhoji kuhusiana na kutoweka kwa magonjwa huyo na nesi alielezea kama taarifa iliyopewa Inspecta kutoka kwa watendaji wake, na Inspecta akaendelea  kumhoji huyo nesi kwa undani zaidi;

‘Wewe ukiwa zamu mara nyingi ndiye unayemuhudumia huyo mgonjwa?’ akaulizwa

‘Hapana sio siku zote, inategemea umuhimu na hali ya huyo mgonjwa, na pia inategemea unaweza kufika ukapangiwa kazi nyingine, mwingine akamuhudumia huyo mgonjwa...’akasema huyo nesi kwa kutaka kujiamini

‘Huyu mgonjwa ulikuwa ukimfahamu kabla?’ akaulizwa

‘Naweza kusema ndio,kwasababu ni mteja wa mara kwa mara kwenye hii hospitali…kama mgonjwa, na  kwa vile mara nyingi  akiumwa anafika kutibiwa hapa…’akasema

‘Je anafika hapa kwa matibabu tu au kuna wakati mwingine anakuja kuongea, au kuonana na docta?’ akauliza na kumfanya nesi kukunja uso, kama anatafakari, akasema;

‘Mhh, mara nyingine anafika akiwa na maongezi na docta mkuu wa hospitali hii, sio kila mara akija hapa anakuja kutibiwa....’akasema

 ‘Umesema wakati mwingine anakuja kwa maongezi tu, hapa ni hospialini, unahisi anakuja kwa maongezi gani zaidi ya kutibiwa?’ akaulizwa

‘Siwezi kujua ni maongezi gani, nasema kwa maongezi, maana kama angelikuwa kafika kwa ajili ya matibabu, angelipitia zile taratibu za matibabu, lakini anafika kwa ajili hiyo, anakwenda moja kwa moja kuonana na mkuu, hapimwi wala hachukui dawa, anaongia wakaongea, na anaondoka zake...’akasema

‘Hebu nikumbushe kidogo, siku ile huyo mgonjwa alipotoroka, umesema mgonjwa alianza kujipiga piga, na kuhangaika, akionyesha kuhisi maumivu, je ilishawahi kutokea hivyo kabla?’ akaulizwa

‘Ndio tangu alipofika hapa, mgonjwa huyo amekuwa akituhangaisha sana, maana akianza kulalamika maumivu inabidi mpaka kupigwa hiyo sindano ya kumfanya alale…na akianza kujipiga piga mwenyewe utamuhurumia, unashindwa kuamini kuwa kweli ni yule mtu aliyekuwa akifika hapa kwa mbwembwe,..kabadilika kwakweli…., nahisi ana matatizo mengine , sio hayo maumivu tu....’akasema huyo nesi, na alionekana kushtuka, kama vila hakutakiwa kuongea hayo aliyoyaongea.

‘Kwanini unasema hivyo kuwa kabadilika, ….yaonyesha kama kumfahamu zaidi?’ akaulizwa

‘Mhhh, ni hisia zangu tu, lakini nahisi hivyo, kutokana na jinsi anavyofika hapa akionyesha ni mtu tajiri na gari lake, leo hii unamuona akijipiga piga, ni kama vile kapandwa na mashetani, ukimona utajua kwanini nasema hivyo, japokuwa docta kasema hiyo ni kawaida, maana yaonekana alijigonga kichwani alipopatwa na hiyo ajali....’akasema

‘Uliwahi kumhudumia ukaona majeraha yake ya mwilini?’ akaulizwa

**********

NB: Hapa hapa, tumbane huyu nesi anajua mengi…ngoja tuone, tupo pamoja

WAZO LA LEO: Heshima ni kitu cha bure tu, ukikifanya hugharamii sana sana unajiongezea hadhi  na utu wako. Heshima ni kwa mkubwa na mdogo, na heshima, ipo katika mtizamo tofauti, kimatendo, maadili, maongezi na katika utendaji wa kazi za kila siku. Heshima pia ni hekima na busara , inayokukurubisha na wenzako, uonekane vyema, katika matamshi yako, matendo yako na jinsi unavyojiweka, na usipokuwa na heshima, ukajiheshimu, utu na hadi yako hushuka, watu watakadharau, tujitahidi kuwa na heshima ili tuwe karibu na jamii.

No comments :