Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 10, 2014

DUNIA YANGU-60


‘Ndugu muheshimiwa hakimu kwa vile mashahdi wengine bado hali zao hazijawa njema kuongea, tuliwaleta hapa tu kama ushahidi kuona jinsi gani walivyotendewa, na tulitarajia kuwa docta akiwapa dawa wangeliweza kuwa na hali nzuri, lakini imeonekana tofauti na docta kasema itachkua muda hali zao kutengamaa.

Hata hivo tulitarajia kuwepo kwa shahidi mwingine, shahidi huyu ilibidi tuombe kibali kwanza, kwani  yeye ni mtu mnzito, na kutokana na kazi zake na majukumu yake hatungeliweza kumfunganisha na mashahidi wengine, au yeye kuongea hadharani moja kwa moja, hata hivyo,  tulitakiwa kuthibitisha pia kwa wakubwa zaidi, kuwa kweli na yeye anaweza kuhusika kwa namna moja au nyingine katika hili kundi…’akasema muendesha mashitaka

‘Tulipeleka maombi yetu makao makuu, na ushahidi uliotakiwa, na makao makuu wakataka muda wa kupitia na kuchunguza,  na kufuatilia taratabu za kiusalama, maana huyo mtu ni mtendaji wao mkuu, na makao makuu, wakasema tuwape muda, huku tukiendelea na kesi yetu , kwahiyo wakati kesi inaendelea, bado tulikuwa tukisubiria , kibali kutoka makao makuu, ....’akatulia hakimu akawa anatafakari jambo, akageuka kuwaangalia wenzake halafu akageuka kumuangalia muendesha mashitaka, na kuuliza

‘Hakuna mtu mnzito kwenye sheria, kama mnaona huyo mtu anawajibika kisheria kutoa ushahidi, basi mngalifuata uataratibu wa mashahidi akaitwa mbele ya mahakama, kama mna taratibu zenu za kiusalama, sisi kama mahakama tungaliangalia jinsi gani ya kumlinda,..maana kuna mashahidi wengine kutokana na utendaji wao wa kikazi hawatakiwa kujulikana, hilo lipo wazi, yote hayo sisi kama mahakama tungeliweza kuliangalia hilo…lakini hamuwezi kuja na hoja sasa hivi…’akasema hakimu.

‘Muheshimiwa hakimu, mambo mengo amekuja kugundulikana, katika dakika za mwisho wakati kesi imeshafikishwa kwako, na siku a kesi imeshafika….’akajitetea muendesha mashitaka.
‘Sasa hebu mtuambie yeye huyo mtu hawezi kusimamishwa hapa kutokana na utendaji wake wa kikazi au kwa ukubwa wake wa kicheo?’ akaulizwa na hakimu

‘Kwa yote mawili muheshimiwa hakimu.....’akasema muendesha mashitaka

‘Basi wakili muendesha mashitaka na Inspecta Moto, tuanane dakika kumi, na baadaye nataka tukutana na mawakili wa pande zote mbili, tukimaliza kuteta na hawa waendesha mashitaka,tutaangalia kama kesi inaweza kuendelea leo au tuahirishe, ...’akasema hakimu na kukawa na dakika za mapumziko.

Wakiwa na hakimu, muendesha mashitaka, aliweza kuelezea yote kuhusu shahidi huyo, na mwishoni akasema;

‘Hata hivyo muheshimiwa hakimu, kumekuja taarifa kuwa shahidi huyo ametoroka, shahidi huyo huyo alikuwa haospitali akitibiwa, kutokana na ajali, katika chumba cha wagonywa mahututi, akawa anaendelea vyema, na angeliweza kuja kutoa ushahidi, na tulifanya taratibu za kumweka katika hali ya madawa, ili asizindukane mapema, na ili asijue kinachoendelea...’akasema

‘Kwanini mkamuweka katika taratibu za madawa…na kwanini asije kinachoendelea wakati yeye ni shahidi tu…?’ akaulizwa.

‘Tuna uhakika kuwa asingelikubali kuja kutoa ushahidi, na haya yaliyotokea ya kutoroka, ndicho tulichokuwa tunakiogopea, na kwa kufanya hivyo atakuwa akitafuta mbinu za kuharibu ushahidi, lakini kila kitu tumeshakipata dhidi yake, hata hivyo  ni muhimu ashikwe haraka iwezekanavyo.....’akasema

‘Kwahiyo yeye zaidi sio shahidii mnamuhisi kuwa anahusika katika kundi hilo haramu…..?’ akaulizwa.

‘Ndio muheshimiwa hakimu, anahusika na tuna ushahidi wa kutosha, lakini kama walivyokuwa docta na wenzake , akawa hawezi kujitoa, au kuelezea, uwepo kwake kwenye kundi ukizingatia yeye ni mtu mkubwa katika vitengo vya usalama, ...’akasema.

‘Mna uhakika na hilo, maana hilo ni kosa kubwa, na huyu ni mtu mkubwa sana, na kunahitajika tahadhari za hali ya juu, je makao makuu anasemaje....’akaulizwa.

‘Kama hao mashahidi wote wangeliweza kuongea, tungelithibitisha hilo kutokana na maelezo yao, kama alivyokwisha anza kueleza docta, kuwa yeye aliwahi kupeleka taarifa zake polisi kuhusiana na hilo kundi, na taarifa hizo zilipokelewa kituoni, na aliyekuwa kiongozi wa kituo hicho wakati huo na huyo mtu, kabla huyo mtu hajapandishwa cheo,....’akatulia.

‘Sawa lakini hilo haliwezi kuwa ni sababu ya moja kwa moja ya kumuweka hatiani  mtu huyo…mimi siwapingi, mimi hakimu natakiwa kuwasikiliza pande zote , lakni ninachochelea hapa, ni kuwa huyo ni mtu mkubwa, na kama itatokea vinginevyo hamuoni kuwa, mtaiweka idara yenu kwenye sintofahamu..na nyie wenyewe mtakuwa mumevunja uamunifu wen katika kazi….’akasema hakimu

‘Ndio maana tunataka hili lifanyike kimahakama zaidi za uraiani, ili kusafisha idara yetu, na tumeona kama tutalisimamia huko kwetu, kuna hali ya kutokuaminiana kwa sasa, ni nani anahusika na ni nani hahusiki, ….....’akasema Moto

‘Mnahisi kuna watu wengi wanahusika katika idara yenu?’ akaulizwa.

‘Ndio muheshimiwa hakimu, lakini wote wameshajulikana, na wengi wao wamekiri wenyewe kuwemo, kuwa walikuwa wakifanya hayo kwa shinikizo...’akasema Moto.

‘Sasa niambieni huyo mtu katoroka vipi, kwani baadaye anaweza kujitokeza na kudai kuwa hajatoroka, au sio, akaja na hoja nzito…?’ akauliza.

‘Alipokuwa hospitalini akiwa amedungwa madawa, ambayo alikuwa akipewa, kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo, …na tunahisi alikuwa akifanya mchezo ili ionekane hivyo, ….na alipoona hali sasa inakwenda vibaya alipozindukana, akawa anatapatapa, kuashiria kuwa ana maumivu, nesi aliyekuwa akimuhudimia akakimbia kwenda kumuita docta,...’akasema.

‘Docta gani aliitwa, si umesema kalazwa hospitali ya huyu docta Chize, na docta Chize alikuwa mahakamani kwa muda huo?’ akaulizwa.

‘Alikuwepo docta masaidizi wa docta Chize…..’akaambiwa hakimu.

‘Nesi anasema alipomwambia docta huyo, akachukua vifaa akijua anahitajika kwenda kumdunga yule mtu sindani anayodungwa, ambayo akidungwa , analala…nesi yeye akabakia nyuma hakuingia kwenye kile chumba,

‘Nesi anasema alikaa kama  dakika kumi,..akahisi ukimiya, kwani alitarajia docta huyo angemuita kwa kazi hii au ile,…alipoona hivyo, akaamua kuingia kwenye hicho chumba, alipokuwa huyo mgonjwa, cha ajabu aliyemkuta kalala pale kitandani ni docta huyo msaidizi badala ya mgonjwa, docta akiwa katika hali mbaya,..akiwa kadungwa yeye hizo dawa..za kupoteza nguvu,mgonjwa hayupo…alisema huyo nesi…’

‘Nesi huyo akatoa taarifa kwa walinzi waliokuwepo, kukaanza msako, na walinzi wanadai kuwa hakuna mtu aliyetoka, kwahiyo ni lazima atakuwepo hapo hospitalini, lakini walitafuta sehemu zote hakupatikana,....uchunguzi ukapanuka zaidi hadi nyumbani kwake na sehemu zote anazoweza kuwepo, lakini hadi sasa hajapatikana....’akasema Moto.

‘Unahisi kaenda wapi,...?’ akaulizwa

‘Hii inaonyesha bado kuna watu wanaofanya kazi nao, ambao walimsaidia kutoroka, lakini sisi tuna imani hajaenda mbali tutampata tu...’akasema moto

‘Kwahiyo nyinyi mnataka nini, kesi iahirishwe, au mna mashahidi wengine?’ wakaulizwa

‘Kwa hali ilivyo tunaomba kesi iahisrishwe, na mashidi hao muhimu, docta na wenzake wote wapewe ulinzi wa kutosha, maana hili kundi ni hatari sana, kitakachosaidia ni kuwa docta ambaye anahusika katika utoaji wa  madawa hatari ya kuwadhuru watu, tunaye,….lakini hatuwezi kuwa na uhakika wa moja kwa moja, kuwa hakuna madawa mengine yanayoweza kutumika, …hata silaha za moto zinaweza kutimika, japokuwa sio tartibu waanzotumia ..kundi hili limekuwa likitumia silaha za aina yao akiwemo madawa

‘Kwa hali hiyo basi, inabidi  hospitali ya docta chize iwe kwenye ulinzi mkali,na huyo docta msaidizi naye ashikiliwe, na huduma zake hiyo hospitli tunaomba kibali chako zisimamishwe, japokuwa kuna wagonjwa wapo mle, lakini tutaona jinsi gani ya kuweza kuwapatia huduma kutoka kwa madocta wengine....’akasema muendesha mashitaka.

‘Basi ngoja niongee na mawakili wote…ili tuliweke hili swa,…..’akasema hakimu, halafu kabla hajatoa agizo hawa watu wawili watoke, akasema;

‘Ila wewe inspecta Moto kawajibike, hakikisheni huyo mtu anapatikana haraka iwezekanavyo, natumai utawasiliana na makao makuu, na mtajua jinsi gani ya kufanya, tunahitajia huyo mtu afikishwe mahakamani, najua kuna taratibu zenu za kiusalama za mtu kama huyo kushitakiwa uraiani, hilo nataka niongee na muendesha mashitaka….’akasema.

Inspecta Moto akaanza kuondoka, na wakati anatoka, akapokea simu ujumbe wa simu…

‘DUNIA YANGU IPO PALE PALE…JIANDAE KUPATA KIPIGO…..’

WAZO LA LEO: Unapokuwa kiongozi, unahitajika pamoja na taaluma yako ya uongozi, unatakiwa pia uujaze moyo na akili yako hekima, kuwa na busara ya jinsi gani ya kuongea na watu wa aina tofauti tofauti jinsi gani kuishi na hao unaowaongoza. Kuna wakati mwingine inabidi uweke sheria pembeni, utumie busara na hekima, ili watu wakuelewe, maana sio wote wenye uelewa mpana, Jitahidi sana kutokutumia ubabe kama silaha yako ya kuwafanya walio chini yako wakuelewe au kukufuata. Usiwe na lugha mbaya, dharau, uwongo ,vitisho, au kuwa kigeugeu wa kuwagawa watu wako kimadaraja au makundi yenye mlengo wa kuwafanya wengine wajihisi wanyonge. 


Ni mimi: emu-three

No comments :