Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 31, 2014

DUNIA YANGU-56

Usijali,..hilo tumeshalishughulikia, hali ya mkuu wangu ipo kwa madocta sahihi,  inaendelea vyema, na yupo salama, usiwe na shaka naye, muhimu ni wewe kujitokeza…kwasababu ya hao watu uliowadunga madawa, unajua muda gani yanatakiwa yatolewe mwilini, ukichelewa, wakadhurika, ujue wewe ndiye muuaji wao…’akaambiwa

‘Najua, najua….ok, tutakutana mahakamani…’akasema na simu ikakatika. Moto akamgeukia Muendesha mashitaka na muendesha mashitaka akauliza;

‘Unamwamini huyo mtu…?’ akauliza.


‘Kwa hali ilivyo hivi sasa ni lazima tumuamini, unajua wazazi ni kitu kingine, huyu mtu anawajali sana wazazi wake,na ndio maana aliposikia kuwa hata wazazi wake wamekamatwa, akaamua kujitokeza, hata hivyo vijana bado wanamtafuta na atapatikana tu….’akasema Moto.

Tuendelee na kisa chetu......


*********


 Kesi ilianza kama muda ulivyopangwa na hadi wakati kesi inaanza Inspecta Moto alikuwa hajafika,  na muendesha mashitaka akawa anampigia Inspecta huyo simu, lakini simu  yake ilikuwa haipatikani, kiasi kwamba muendesha mashitaka akahisi kuwa huenda mwenzake huyo yupo hatarini, akawasiliana na mtu wa karibu wa Inspecta Moto kuwa afuatilie kuhakikisha kuwa Inspecta huyo yupo salama.

Kwa vile mpangilio wa kesi ulikuwa tayari umeshapangwa, na kutokana na hali ilivyokuwa, muendesha mashitaka alikuwa amewapanga mashahidi wengine wa kawaida kuanza kutoa maelezo yao kinyume na ilivyotakiwa awali kuwa siku hiyo wataongea wale mashahidi muhimu, alimuelezea hakimu kwanini anafanya hivyo, na ikakubalika,akaendelea kama kawaida akawaita mashahidi wa mwanzo ambao hujenga kesi yenyewe kabla ya wale mashahidi wakubwa ambao hali zao zilikuwa bado ni kitendawili.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kuna mashahidi ambao tulipanga wasimame leo hapa mahakamani, lakini hali za afya zao bado ni tete, na hii ni kutokana na hujuma za hili kundi, kama nilivyoeleza awali kundi hili lina vitengo vingi kwenye kil nyanya, na wana kitengo chao cha hatari zaidi, hiki ni kitengo cha  madawa, na utibabu, na kutengeneza mabomu, wana wataalamu wa hali ya juu, na miongoni mwao ni docta mashuhuri hapa nchini, ambaye wengi wetu tunamfahamu kwa uhodari wake wa tiba za magonjwa ya akili, magonjwa ya akina mama, na ni mtaalmu wa magonjwa mengi tu….’akatulia

‘Ni weli mtu huyu ni mtaalamu sana, lakini ndani yake ni kama chui aliyevaa ngozi ya kondoo, ni hatari kuliko tunavyomfahamu, huyu docta ametumiwa na kundi hili haramu kutengeneza madawa hatari, madawa ya kupumbaza akili za wanadamu, na kutokana na dawa hizo ndio maana mashahidi wetu hao muhimu wameshindwa kufika hapa mahakamani….’akasema, na kundi la watetezi wakapinga na kusema hizo ni hoja za kujitetea hazina msingi.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, ili kulithibitisha hilo,kama waanavotaka watetezi, tutawaleta hao wagonjwa ili mahakama ithibitishe…..’akatulia, kwani simu yake ilitoa mlio wa ujumbe, akaangalia  simu yake kwa haraka akiwa kama anasoma makabrasha yake, halafu, akatikisa kichwa kufurahia jambo

‘Ndugu muheshimiwa hakimu samahani sana, kwa kupokea ujumbe huu mbele yako, lakini nilfanya hivyo nikijua kuwa kuna jambo muhimu nalisubiria, na ningelipenda kukuarifu kuwa shahidi wetu tuliyekuwa tukimsubiria ameshafika, ambaye atathibitisha haya niliyokuambia, kabla hatujawafikisha hao waginjwa kama ushahidi ….’akasema na watu wakawa kimia

‘Shahidi wetu huyo ni docta Chize…..’aliposema hivyo watu wakaguna, wengine wakashangilia na upande wa utetezi ukawa umetulia ukijua ni yale yale, kwani huyo shahidi sio mara ya kwanza kusimamishwa, japokuwa kwa sasa hawajajua msimamo wake ni nini.
Docta Chize akaingia akiwa na nguo zake za kikazi , akiwa an mkoba wake ,utafikiri katokea hopitalini, akapita pale mbele na kuapa na kuanza kuhojiwa

‘Docta, karibu sana, hebu tuambie unatokea wapi sasa hivi, maana ulikuwa unatafutwa kwa muda mrefu sana, ..?’ akaulizwa, na docta akageuka kuangalia upande wa utetezi, akakunja uso, halafu akageuka upande mwingine, akawaona wazazi wake wamekaa mama yake akiwa kashika tama, …akainama chini kuashiria aibu.

‘Nilikuwa nimejificha…’akasema na watu wakacheka.

‘Kwanini ujifiche, na wewe ni docta, una kitengo chako cha ulinzi, wewe ni tajiri, miongoni mwa madocta matajiri…?’ akaulizwa

‘Utajiri wangu, ulinzi nilio nao, pesa nilizo nazo, haziwezi kushindana na hao waliokuwa wakitaka kuniua…’akasema

‘Ina maana hao watu wana nguvu zaidi ya serkali yako, maana serikali yako ilishakuhakikishia usalama wako, je huiamini serikali yako, walinzi wako,…?’akaambiwa

‘Wangapi wamepoteza maisha wakiwa mikononi mwa walinzi wenu, …tusidanganyane hapo, wenyewe mnafahamu hilo, kuwa watu mnaopambana nao wana nguvu kiasi gani,huwezi kujua ni yupo yumo na yupi hayumo kwenye hilo kundi,…kwahiyo mimi nikaona njia nzuri ni kutafuta namna nitakavyojiokoa mimi mwenyewe, kwa vile nawafahamu hao watu vyema..’akasema

‘Unaposema unawafahamu hao watu vyema, una maana gani , ni watu gani hao?’ akaulizwa, na wapinzani wakaweka pingamizi

‘Ndugu muhehimiwa hakimu, huyu docta anasema alitoweka akitaka kujiokoa na watu wanaotaka kumuua, nahii ni mahakama, inatakiwa ithibitishiwe hilo, na hapa ndipo kwenye sheria, na sheria ndio itakayomlinda , na mbele ya mahakama hii anatakiwa kuonyesha kwa jinsi gani anashindwa kuamini kuwa usalama wake usingeliweza kulindwa hata na kwa watu wa usalama waliopewa jukumu hilo…’akasema na hakimu akasema muendesha mashitaka  aendelee kumuhoji mtu wake

‘Umesema wewe unawafahamu hao watu vyema kwanini unasema hivyo?’ akaulizwa

‘Kwasababu nimefanya kazi nao, ….’akasema

‘Kwahiyo na wewe ni miongoni mwao?’ akaulizwa, na hapo akakaa kimia

‘Je wewe ulijiunga na hilo kundi lini?’ akaulizwa na pia akaendelea kukaa kimia kama vila anatafakari jambo.

‘Docta, wewe dakitari unayejiamini, una ujuzi wako wa hali ya juu, ina maana moja ya kazi yako ilikuwa kusomea kuwadhuru wanadamu wenzako?’ akaulizwa.

Na mara mlango ukafunguliwa, na watu wakawa wanasongamana kule mlangoni, kuashiria kuna watu wanatka kuingia,, na watu wote wakageuka kuangalia mlangoni, kukawa kunaingizwa vigari vya kukokotwa na watu, cha kwanza , cha pili, hadi vigari  vitano na kila kimoja kina mtu ndani yake na nyuma yao akaingia Inspecta Moto, Inspecta Moto akasogea mbele ya muendesha mashitaka na kumnong’oneza jambo.

Muendesha mashitaka akiwa na furaha akasema;

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kama nilivyokuelekezea awali ni kuwa katika ushahidi wetu kuna wagonjwa tutakaowaleta hapa mbele, ili kuonyesha madhila ya hili kundi, na mtu aliyekuwa akitumiwa kuwadhuru wanadamu wengine kwa nia ya msilahi yao yupo hapa mbele, …

'Ni huyu docta Chize, na hao walioingizwa sasa hivi ni watu waliopingwa masindano na huyu docta…hatujui ni aina ya dawa gani aliyowadunga mwilini hawa watu, maana watabibu wetu wameshindwa kuyagundua ili kuwasaidia hawa mashahidi wetu…..’akasema

Aliposema hivyo watu wakazomea, wengine wakawa wanamtukuna huyo docta, hakimu akagonga kirungu chake mara tatu, na watu wakawa kimia

‘Je ni kweli docta?’ akauliza hakimu

‘Ni kweli docta….’akasema na watu wakapandisha sauti kwa hasira

‘Nataka mtulie la sivyo wote mtatoka nje…’akasema hakimu kwa ukali

‘Kwanini umefanya hivyo..?’ akauliza hakimu

‘Kabla sijajibu hilo swali naomba unipe muda, niweze kuwasaidia hawa watu , maana imebakia muda mchache wa kuweza kuwasaidia,….’akasema docta na muendesha mashitaka akasema;

‘Ndugu muhehimiwa hakimu madawa waliyodungwa yana muda maalumu, ukizidi huo muda hatutaweza kuwasaidia tena hawa watu, na hapa tunawakilisha ushahidi wetu wa kuonyesha jinsi gani kundi hili lilivyokuwa na unyama wa kupitliza..na tunaomba kibali chako ili huyu docta aweze kufanya kazi yake, na ukiwa pia kama ushahidi wetu ….’akasema

‘Ok,..docta hakikisha hao watu wanarudi katika hali yao, na ukimaliza hapo tunataka utuambie ni kwanini uliwafanyia hivyo hao watu, natoa dakika kumi za mapumziko, si zinatosha wewe docta….?’akasema hakimu, na docta akasema zinatosha,

Hakimu akionyesha kukerwa na hiyo ahali akatoka,akiwaita mawakili wa pande zote kuwa anataka kuteta nao, huku akipangusa uso kuonyesha kuwa jasho linamtoka, japokuwa kulikuwa na kipoza hali ya hewa

Docta akatoa sindami kwenye mkoba wake na kuanza kuwapitia wale watu watano, na kila aliyepigwa hiyo sindano alishituka, na kutetemeka mwili mzima, halafu akatulia kama vile kapoteza fahamu, na alipomaliza hilo zoezi, haikupita muda wale watu wakazindukana, na kuonyesha hali ya uhai….

Baadaye hakimu alirudi , walitangulia kwanza wale mawakili wa pande zote, na kila mmoja akarudi sehemu yake, na hakimu akakaa kwenye kiti chake na kupiga kirungu chake akasema;

‘Haya tuendelee….’akasema hakimu.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, docta kamaliza kazi yake, na hao watu kama unavyoona sasa wanaweza hata kusimama, lakini bado hatuna uhakika wa fya zao,  kuanzia sasa tumwambie docta kuwa hao  ni wagonjwa wake, tunahitajia afya zao zirejee kama kawaida, na hili tunaliwakilisha kwao muheshimiwa, ili haki itendeke kwa hao watu..’akasema muendesha mashitaka

‘Docta, ni kwanini umewafanyia hao watu hivyo?’ akauliza hakimu kwa sauti ya ukali

‘Muheshimiwa hakimu hilo sio kusudio langu, sikufany ahayo kwa ridhaa yangu mwenyewe, na wala sio fani yangu kuwafanyia hao watu hivyo, nimefanya hivyo kwa kulazimishwa….’akasema

‘Na nani, ina maana wewe kama docta unaweza kulazimishwa kuua watu na ukakiuka mujibu wa kazi yako ya udakitari, je ina maana fani yako ya udakitar ni kuwatesa watu, ndio masomo uliyokwenda kusomea huo nje..?’ akalizwa

‘Muheshimiwa hakimu, najua wengi mtanichukia, na kuniona mimi ni mtu mbaya sana,…lakini hamjui ni kwanini nilifikia kufanya hivyo, na kama ningelifuata yote niliyokuwa nikiambiwa nifanye, huenda hata hawa watu wasingelikuwepo hii leo hapa…’akasema

‘Nakupa muda wa kijielezea, elezea mahakama hii ni kwanini ulifanya hivyo…..’akaambiwa

‘Kwanza nataka kujua uhakika wa uslama wangu, nataka kujua je huyo mtu niliyewaambia wamkamate kwanza, wameshafanya hivyo…?’ akauliza

‘Nani unayemuogopa, upo ndani ya mahakama, hakuna aliye juu zaidi ya sheria,…ina maana huamini serikali yako, huamini mahakama yako?’ akaulizwa

‘Kama hayo yangelifanika vyema, kama unavyodai muheshimiw a hakimu, yoye haya yasingelikuwepo, mimi nimefanya haya baada ya kuona hakuna msaada wowote niliopata toka awali, niliwahi kutoa  taarifa ya haya mamboi kwa wahusika mapema wa usalama,, nikiomba msaada, kumbe huko nilikopeleka taarifa ndio watu wale wale, nilichokipata sitakisahau…’akasema na hakimu akamuangalia muendesha mashitaka kutaka aendelee na mtu wake.

‘Docta tunakuhakikishia kuwa sasa upo salama, na hakuna mtu atakayekuhduru kwa hivi sasa, kwani kama unavyoona wahusika karibu wote wamekamatwa, na huyo mtu  unayemuogopa yupo mikononi mwa polisi…’akaambiwa

‘Mumemkamata huyo mtu, haiwezekani, …Nithibitishieni, maana nyie hamjui mnachopambana nacho…’akasema kwa mshangao.

Inspecta Moto, akamsogelea pale alipo akamuonyesha simu, na yule docta akaangalia, kwenye ile simu kulikuwa na picha akaiangalia , halafu akasema;

‘Ni bora huyo mtu  akaletwa mbele ya mahakama, ili haki itendeke, ili kuwa na uhakia wa maisha yetu, mimi simuamini kabisa huyo mtu, ..’akasema.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, tunaiomba mahakama yako ikubali ombi la huyu mtu, kwani hawa watu wamepitia maisha ya hatari, mateso vitisho na hata wengine kuuwawa…kwahiyo wanajua jinsi gani kundi hili lilivyokuwa na nguvu, tunaomba tumlete huyo mtu anayemuogopa, awepo hapa mbele, ili awe na uhakika wa usalama wake, kama anavyodai, na ili kila kitu sasa kiwe wazi, kundi hili sasa tunalimaliza…’akasema muendesha mashitaka na watu wakashangilia

‘Mbona mimi siwaelewi, ina maana nyie watu wa usalama mumeshindwa kidhibiti hiyo hali, kuwadhibiti wahalafu , mpaka mfanyiwe kazi yenu,hii sio kazi ya mahakama kutoa ulinzi na usalama, sisi kazi yetu ni kutoa amri kutokana na sheria, siwaelewi….?’ Akauliza hakimu

‘Muheshimiwa hakimu, kundi hili lina watu kila idara, kama tulivyokwisha kuelezea toka awali, na imefikia hatua raia hawaamini tena idara yao ya usalama, na ndio maana hata huyu docta anaogopa kujieleza, akijua wote ni wale wale…tunaomba tulifanye hilo…’akasema

‘Huyu mtu anayeogopewa hivyo ni nani,kwanini hamkumkamata, maana huyo ni mhalafu, natoa amri huyu mtu akamatwe haraka iwezekanavyo..?’ akauliza hakimu na kutoa amari ya kukamatwa kwa huyo anayeogopewa


WAZO LA LEO: Kiburi cha pesa, kipuri cha utawala, kiburi cha uwezo ulio nao sio mali kitu, vyote hivyo ni mapito tu,w alikuwepo wenye viburi kama hivyo kabla, lakini leo wapo wapi. Hakuna aliye juu ya sheria, hakuna mwenye mamlaka ya kujihakikishia kuwa yeye ni zaidi ya wengine na anaweza kufanya apendavyo, hakuna, wote viburi vyetu itafika siku vitakwisha tu….mwenye mamlaka hayo ni mungu peke yake, na ndiye wa kuogopewa.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel Siwa said...

Mmmhhhh....Hongera sana ndugu wa mimi..kazi kazini,kazi hii ni yako..Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako..

Wazo La Leo...linagusaaaaa.

Pamoja Daima.

emuthree said...

NASHUKURU SANA NDUGU WA MIMI TUPO PAMOJA