Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 20, 2014

DUNIA YANGU-51

 
‘Huyu mtu hafanani kuwa mvuvi….kwa jinsi anavyoonekana japokuwa kavalia hayo mavazi, lakini wavuvi tunawafahamu hali zao bwana,..huyu bwana hata, hafanani hivyo….labda ndio hao wavuvi matajiri,...
'Hata jana tu, nilimuona akiwa katika hiyo hali, kavalia koti,akionekana na wasiwasi, akaingia humo ndani  na sijamuona akitoka, kama kawaida yake, unamuona akiingia lakini akitoka humuoni,…’akasema huyo mtu


Inspecta aliposikia hivyo, akawa na hamasa ya kuonana na huyo mtu, hata hivyo, hali ya hiyo nyumba ilionekana kuwa hatarini, kulikuwa na kila dalili kuwa kuna moto ndani ya hiy nyumba na usipodhibitiwa unaweza kuwa mkubwa ukanguza hiyo nyumba na nyumba za jirani...
Amri ikatolewa...,
'Tuvunje tuingie....'
Moto akiwa na kikosi chake wao walibaki nyuma, wakawaachia wahusika wa moto na milipuko kama mabomu watangulie mbele, mlango mkubwa wa kwanza ukavunjwa, na watu wakaingia ndani.
Mwanzoni watu walihisi labda ni lile bomu la makaburini ndilo limeleta athari hadi hapo, labda kuna kipande cha mabaki ya bomu kilidondokea humo ndani na kuleta moshi, na ukumbuke watu wengi walikuwa wamelikimbia hilo eneo, na wachache sasa ndio walikuwa wakirudi rudi, kuona kama kuna amani.
Wakaingia kikosi cha Zima moto na askari wa mabomu, na Inspecta Moto akawafuatia kwa nyuma....

Mlango ulipovunjwa, tu, watu wakakaribishwa na harufu mbaya, ilikuwa ni harufu ya gesi, na haikupita muda ghafla mlipuko mkubwa ukasikika…….

Tuendelee na kisa chetu

**********

Tulia utazidi kujiumiza….’

Inspecta Moto alifungua macho  huku akihema kama mtu aliyekuwa akikimbizwa, na alipofungua macho alionyesha kuwa mwingi wa wasiwasi,  akainua mkono, akitaka kushika kichwa lakini hakuweza ,mkono ulikuwa mnzito kuinuka, akakunja sura kuashiria maumivu, halafu  akainua mkono mwingine, huo mkono ukawezekana kuinuka,na ndipo akaweza kushika kichwa , lakini badala ya kugusa kichwa akaguswa kitu kingine, mmh, kichwa changu kina nini,mbona kimefungwa...

Akafunua macho na kuangaza huku na kule hakujua yupo wapi, akawa anahangaika, akahisi kuna kitu kinamkandamiza miguuni,  akakumbuka ile ndoto, ndani ya ndoto hiyo alikuwa yeye na wakewe, alikuwa kaumia mguu, mkono, na kichwa, majeraha hayo aliyapata kutoka kwa jitu moja la kutisha, linalomomonyoka uso na kuwa na sura mbaya, …

Alipofika kwa mke wake hakawa hajiwezi, mkewew akawa anamtibia hayo majereha na alikuwa akitumia maji ya moto, yaliyokuwa yakiunguza sana, lakini kwa ajilii ya mumivu, akawa anakataa kukandwa, akijua yatamzidishia...

Na wakati mkewe akiwa anaendelea na hayo matibabu, kwa kupitia dirishani akaliona hilo jitu, jitu lile sasa limezidi kuwa kubwa, linatoa cheche mdomoni, uso umekuwa mpana, na sura ya kutisha,  sasa linataka kumuumiza hata mke wake, na kwa vile mkewe alikuwa kalipa mgongo hilo jitu, alikuwa hajui ni nini kinachoendelea.
 Inspecta Moto akawa anajaribu kumuonyesha mke wake kwa ishara lakini mkewe  akawa haelewi, yeye akawa anaendelea kumkanda na maji ya moto, na katika purukushani za kukataa kuendelea kuumizwa na maji ya moto, na kutaka kumuokoa mkewe ndipo hapo akazindukana na kujiona yupo eneo ambalo hakujua yupo wapi..

Akawa anahema kwa wasiwasi, na sasa akawa anajitutumua kuinuka, na mara sauti ikasema

‘Tulia, utazidi kujiumuza.....?’ ilikuwa sauti ya kike ooh ni sauti ya mke wake, kumbe ni kweli,sio ndoto , kumbe ni  kweli ni mke wake  anamkanda, akajaribu kuinua kichwa ili kumuangalia vyema, ...mmmh, kumbe sio ndoto, kumbe ni kweli, mke wangu yupo name,  akili ikawa inamuambia hivyo, akatabasamu,....lakini macho mbona kazidi kuwa msichana, akawa anajiuliza, …akatabasamu tena

Muda ukawa unapita na macho yakaanza kuzoea,na  ule ukungu wa giza, na uzito wa kukumbuka ukaanza kuondoka,  macho yakaanza kuona vyema,  na akili ikaanza kujua kinachoendelea mbele yake, akagundua kuwa sura iliyopo mbele yake sio ile ya mke wake...

‘Oh, kumbe ni wewe tena, ..nilijua wewe ni mke wangu’akajikuta akisema

‘Mhh, mke wako, jamanii `but’nakumbuka uliwahi kunambia kuwa mke wako auwawa jamani,kwani mimi nafanana na mke wako....?’ huyo binti akauliza

‘Huafanani na yeye moja kwa moja, lakini kisifa mnafanana sana....unanikumbusha enzi nilipokutana na mke wangu kwa mara ya kwanza, alikuwa kama wewe,binti mdogo mdogo mrembo, .....’akasema na Yule binti akatabasamu na kusema;

‘Mhh, natamani ningelimuona huyo mke wako,..ana bahati sana,..’akasema

‘Kwanini?’ akauliza

‘Kumpata mume kama wewe, ila mimi sipenzi kuolewa na askari...’akasema kwa haraka na kuonyesha aibu, kama alilotamka halikufaa kutamkwa.

‘Kwanini?’ Moto akamuuliza kwa sauti kama ya ukali vile.

‘Nitaishi maisha ya mashaka mashaka, angalia hali yenyewe ndio kama hii, kila mara upo taabani,na kwa mfano ukichelewa kurudi kazini, unafikiri nitakuwa na amani moyoni, nitakuwa naishi maisha ya mashaka mashaka, ...’akasema

‘Basi ukiolewa na askari ndio maisha yako yatakuwa salama, maana mume wako anajua jinsi ya gani ya  kujilinda na kukulinda, na kulinda  taifa lako, na raia wake wema unaona eeh, huyo ndiye mume anayekufaa unaonaje hilo...’akasema kama anauliza na mara akahisi kichwa kama kinaanza kuuma tena, lakini akajikausha

‘Pole sana, unajisikiaje, nakuona kama unakunja uso, kichwa inazidi kuuma?’ Yule binti akamuuliza

‘Hata sijui, kichwa kilikuwa kinauma sana, lakini cha ajabu nilipoanza kuongea na wewe maumivu yamepotea, ni kama vile umenipa dawa, na ghafla tena kuna amumivi kwa mbali...’akasema

‘Mhh, jamani mbona sijakupa dawa….ngoja nikupe dawa, nimesahau kabia, kuna dawa niliambiwa nikupe ukizindukana.’akasema.

‘Hapana , usinipe dawa yoyote, hakuna maumivu tena….alisema hivyo akiwa anaogopa dawa, kwani hakuamini  dawa, alihisi zisije zikawa zimetoka kwa hao jamaa .

Akili ya Inspecta Moto ikawa anafunguka na kumbukumbu zikawa zinaanza kumrejea vyema,  akasema;

‘Najiuliza nimekuwaje..nimefikaje hapa, hapa ni hospitali, nimefikaje hapa.., kwanini mmmh, hata sikumbukia, ilikuwaje…kichwa sasa kinaanza kuleta matatizo, je watu wote waliokolewa, na wale waliokuwa humo ndani....?’akajiuliza huku akijaribu kutuliza akili, na mara kumbukumbu ndio zikaanzaa kujirudi kichwani kwake na kuanza kukumbuka yaliyotokea,

************

Ilikuwa wakati wamevunja mlango kuingia, na mlango ulipofunguka, kwanza waliweza kuingia  wataalamu wa moto na na silaha zao tayari, Inspecta Moto, akawa nyuma yao akijua hilo sio jukumu lake kwa muda huo,akawa anawaangalia  wale watalaamu wakitoa ishara kwa mikono, wakionyesheana ishara kuwa moto huo upo  kwenye chumba cha pembeni kinachoangaliana na ukuta unaozunguka eneo la makaburini ndipo moshi ulikuwa ukitokea na ufukutoa ulikuwa mkali, na kila mmoja akageuka kuelekea huko

‘Lakini nahisi kuna harufu ni ya gesi tusifungue huo mlango kwanza,  hakikisheni kila mmoja kavaa kinga, vaeni vifaaa vya kinga hiyo ya gesi, hiyo ni  harufu ya gesi, rudini nyuma..’akawa anaonya  kiongozi wao,  na mmojawapo aliyekuwa mbele alikuwa tayari keshaukaribia mlango, akawa ameugusa mlango kwa silaha yake, kabla onyo hilo halijatoka, kumbe ule mlango ulishaathirikia kutokana na moto uliokuwa ukitokea ndani, kwahiyo alipougusa tu, ukamong’onyoka na hapo hapo ndio kukatoka hicho kizaa zaa.....

Loooh….., Iilikuwa kama upepo mkali wa kupuliza, hewa kali upepo mkali uliwazoa zoa watu wote waliokwemo humo ndani na kutupiwa nje, na hiyo ndio ilikuwa salama yao, kwani kama wangedondokea humo ndani, wote wangelikuwa ni maiti

Inspecta Moto yeye wakati wataalamu hao wanakagua sehemu hizo, wakivaa vifaa vya kinga, yeye, alikuwa nyuma yao, akiwaachia wafanye kazi yao. Yeye akawa anakagua upande wa pili, kwani ule mlango ukifunguka unajikuta kati kati ya njia panda,  kuna sehemu mbili mbele, moja ya kuelekea huko moto unapotokea na sehemu ya pili, ni kwa upande ambapo hakukuwa na moto, na huko ndipo harufu ya gesi ilikuwa inatokea sana

Ule upande wa pili, akaona kama kuna mtu kwa kupitia kwenye upenyo wa mlango, na wakati huo alishahisi hiyo harufu, akakumbuka taarifa ya kundi hilo kuwa kuna wataalamu wa kila aina  ambao wanaweza kutengeneza silaha za ina mbalimbali, ikiwemo wa mabomu ya hewa, ...akajua hiyo inaweza ikawa ni hewa ya bomu, sio hewa ile ya gesi inayjulikana, ni gesi maalumu ambayo ikigusana na hewa hugeuka kuwa bomu, akashika pua kujihami, lakini kule kwenye chumba cha pili alijua kabisa kuna mtu,...

Akakisogelea kile chumba na hayo yalifanyika kwa haraka sana,, aliona kabisa kuna  kitu kikitembea, akakisogelea kile  chumba cha pili, akashika kiuononi, kuhakikisha kama  silaha yake ipo tayari, mkono mwingine umeshikilia puani, akasogea hatua mbili za haraka, hadi pale kwenye chumba akanyonga mlango, ..

Alimuona  jamaa akiwa kavalia vifaa mdomoni vifaa vya kujizuia asizurike na alikuwa kasimama akiwa kampa mgongo mkononi alikuwa na silaha, ya aina yake, hajawahi kuiona,  huyo mtu alionekana kama anataka kuruka kwa kupitia dirishani na kwa chini pembeni yake kulikuwa na miili ya watu imelala sakafuni..

 Inspecta Mot akajua asipomuwahi huyo mtu atakimbia, haraka akatoa bastola, lakini ndio muda huo mlipuko ulipotokea, hata hivyo aliweza kufyatua risasi, ambayo alikuwa na uhakika ilimjeruhi huyo jamaa sehemu ya mkononi, na muda huo huo ndio nay eye akajikuta akirushwa hewani, na kutupwa nje

Na kipindi anarushwa hewani, ndio hapo akamuona jamaa akiruka kwa kupitia dirishani kati kati ya moto, na usoni akaonekana akiwa kama anaungua ngozi ya usoni, na huyo jamaa akaibandua  hiyo ngozi, lakini hakuweza kumuona vyema  usoni , jamaa akatupa kitu kwenye moto na kuanza kukimbia, na Inspecta Moto aligonga kichwa, pale alipodondokea, na kuhisi moto ukimpamab mwilini.

‘Wamwagieni maji, sogea…..waondoeni hapo haraka moto unazidi…..’ni sauti za mwisho kuzisikia kabla hajazama kwenye giza nene, maana, hewa ilikuwa nzito, na hata alipojaribu kusimama hakuweza, akapoteza  fahamu......

 

********

 Inspecta alipokumbuka hivyo, akajitutumua kuinuka, na akitaka kuondoka,akijua kuwa kuna kazi nzito anahitajika kwenda kukabiliana nayo, na inatakiwa kufanyika kwa haraka, je yule mtu ni nani, na je wale watu waliokuwepo mle ndani waliweza kuokolewa, au ndio waliteketea na huo moto, ndio maana akauliza hilo swali, na yule binti akasema;

‘Nasikia watu wengi wamejeruhiwa sana, ila cha ajabu wanasema kuna upepo mkali ulitupoa watu nje, kila mtu alijua hakuna aliyepona...mimi huko sikufika, nimeambiwa tu, nikuulize, hivi kwanini hao watu wanafanya hivyo, kuna nini wanataka,?’ akauliza huyo binti

‘Na hilo jengo limekuwaje, na je watu waliokuwepo ndani walitolewa?’ akauliza tena hilo swali

‘Mimi sijui,...sijasikia kama kulikuwa na watu ndani ya hilo jengo....’akasema huyo binti

‘Simu yangu ipo wapi?’ akauliza

‘Lakini nimeambiwa ukizindukana unywe dawa, na usifanye kitu chochote….’akasema huyo binti.

‘ni muhimu sana nijue kinachoendelea la sivyo, itabidi nitoke humu niende huko nithibitishe mwenyewe…’akasema na Yule binti alipoona hivyo akasogea pembeni ambapo kulikuwa na nguo za huyo askari, akapekua na kuona simu.

‘Ndio hii?’ akauliza

‘Yah, nipe….’akasema , na alipoishika mkononi, akaanza kutafuta namba anayoihitajia na kuanza kupiga kuwasiliana na watu wake, lakini kila aliyempigia simu hakuweza kumpata, akajikuta akiguna.

‘Mhhh...’

‘Mhh, vipi tena hawapatikani?’ akauliza

‘Hawapatikani, au kuna baya limewakumba….mmh, sijui nimpigie nani, ngoja nimpigie mkuu….’akasema na kuanza kuitafuta namba ya mkuu wake wa kazi….


************

WAZO LA LEO: Je hawa watu wanaoua wenzao kwa madhumuni ya kupata utajiri, hawana utu wa kibinadamu..?’ ni swali kutoka kwa mtoto mdogo tu, na sijui wewe utalijibuje.

Vyovyote iwavyo, watu kama hao,utu, ubinadamu umeshawavuka,na watu kama hao wapo wa aina nyingi, wapo wanaotumia silaha, lakini wapo wengine, hawatumii silaha za moto, lakini ni wauwaji, watu wanaodhulumu haki za wenzao, wakijua haki hiyo ni rasilimali ya wanyonge, rasilimali ambayo ingelinunulia hata dawa kuokoa maisha ya watu, wagonjwa…kusomesha watoto ili waje kuwa madakitari, walimu, nk na kufanya mambo mengi  kwa masilahi ya wengi, na kuokoa maisha ya wenza wao, wao wanaifisidi, na watu wanateseka, wanaumia, na wanakufa hawa ni wauwaji wabaya sana, sawa na hao wanaotumia silaha za moto kupata utajiri,….


Ni mimi: emu-three

No comments :