Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 8, 2014

DUNIA YANGU-45


‘Mama samahani sana kwa usumbufu, lakini nikuulize swali mtoto wako alizikwa sehemu gani, maana tumeuliza sana , hatujaweza kuonyesha kaburi la mtoto wako?’

‘Mnataka niwapeleke ehe, huko anatakiwa kwenda maiti, kwanza mfe ndio niwapeleke

‘Aaah subirini, hatujamalizana na nyie bado, msije kusema mama ni mkorofi, …mlichotaka mtakipata, lakini masharti yake ndio hayo, toka alipofariki mwanangu nimekuwa nikiwauliza watu kama kuna mtu anataka kuliona kaburi la mwanangu, na wakisema sawa, nawapa hayo masharti, lakini wanaogopa..hivi kwanini mnaogopa kufa, wakati ni lazima kila mtu atakufa….

************

‘Nimekumbuka nina ahadi ya kuonana na mtu muhimu hoteli ya Paradise unaonaje tukaongozana, nataka uhakikishe mwenyewe kuwa mimi sihusiki, nawajibika tu, ukaonane na huyo mtu niliyekuwa nikiongea naye …’

‘Janja yako…’

‘Ndio nafasi peke yake ya kuhakiki shutuma zako, twende au uje kinamna, ili tuyamalize haya..’

‘Wewe endelea na shughuli zako, mimi sishirikiani na wewe, …’

‘Uwe makini na hayo unayoyafanya…wewe ni rafiki yangu , kuna mbinu za kukumaliza kabisa,..usije ukasema sikukuonya,…’

‘Umejuaje hayo kama huhusiki…?’

‘Dunia hii haina siri, kama ulivyojua ya kwangu ujue nafahamu mengi ya kwako….lakini mwisho wa siku ni ujanja kupata…’

***********

Tuendelee na kisa chetu

Inspecta Moto, aliendesha pikipiki yake taratibu huku akiwasiliana na jamaa zake ambao walikuwa wakimpa taarifa mbalimbali, akawa anaendesha pikipiki yake akijaribu kuwa makini, kwani alishaumwa na nyoka, na mtu akiumwa na nyoka, huogopa hata unyasi

‘Makaburi ya Msasani, kuna mazishi huko?’ akauliza na akaambiwa hakuna mazishi yoyote siku hiyo, akapiga simu kwa mtu mwingine kazini kwake kumuuliza kama kuna tukio lolote la mauji, ambalo kuna watu wametumwa makaburi ya msasani kuchunguza, akaambiwa hakuna.

Akaona ngoja tu afike huko ajionee mwenyewe, hakuwasiliana na waku wake wa kazi kuwa anakwenda wapi, hakutaka mtu afahamu hilo,japokuwa alijua ni hatari, kama atakutana na jambo, anaweza asipate msaada.

Alifika eneo aliloelekezwa, ilikuwa ni eneo la makaburini, karibu na bahari, kwanza kilichompa mshangao ni kuona boti moja kubwa, boti za mwendo kasi ikiwa imesimama karibu na eneo hilo, boti hili lilikuwa na muundo wa kipekee, hapo liliposimama lilikuwa kama gari,lina magurudumu na kila kitu, ila likiingia ndani ya maji sehemu ya gari haifanyi kazi.

‘Mhh, ndio mambo ya dunia hayo…’akasikia mtu akisema, na Inspecta akajichanganya kwenye kundi la watu waliokuwa wamesimama wakishangaa

‘Hili boti-gari linafika hapa mara kwa mara?’ akauliza

‘Mhh, sio mara kwa mara hii sijui ni mara ya pili au ya tatu, ..mimi mara nyingi nipo hapa sijaliona mara kwa mara, na mara nyingi linafika usiku, leo nashangaa limefika mchana, nahisi kuna mizigo wameleta…’akasema

‘Kwahiyo likifika hapa kuna magari yanakuja kuchukua mizigo?’ akaulizwa

‘Unafikiri mizigo yenyewe mingi, …sio mingi sana ya kuleta lori, linaweza kuja gari dogo, wakatoka na mabegi haya ya kisasa mawili matatu wakaingia kwenye gari wakaondoka zao…’akasema

Mara kukaja gari dogo kwenye muelekeo wa barabara, likafika eneo lile la makaburini na kusimama karibu na nyumba za watu, akatoka jamaa mmoja akawa anatembea kuelekea kwenye eneo kulipokuwepo na kibanda, akaingia ndani ya kile kibanda, hakutoka, na likaja garii jingine, na mtu akatoka akafanya hivyo hivyo, walifika kama watu kumi na magari tofauti, na wote waliingia kwenye kile kibanda na hakuna aliyetoka

‘Wale watu wanafanya nini ndani ya kile kibanda?’ akauliza Moto

‘Hata mimi nashangaa, nahisi kuna maiti inatakiwa kufanyiwa mazishi, maana mmojawapo pale ni dakitari, huenda kuna kitu kimetokea kwa maiti yao, wanataka kuifanyia uchunguzi kabla ya kumzika…’akasema huyo jamaa

‘Kwani pale kuna sehemu ya kuhifadhi maiti, au kufanyia uchunguzi?’ akaulizwa

‘Kile kibanda kilijengwa kwa ufadhili, walipoona kuna watu wanafariki ovyo, hawana ndugu, hawana watu wa kusaidia, wakaona wajenge, ili wakileta miili yao hapo ifanyiwe taratibu zote za kibinadamu,..na pia kama kuna hitajika uchunguzi wowote kwa hiyo maiti, basi dakitari huitwa hapo na kufanya hiyo kazi….’akasema

‘Lakini sijaona maiti ikiletwa hapo…’akasema Inspecta , na mara wakaona jeneza likiletwa, kutoka kwenye gari lililofika baadaye, na lile jeneza likaingizwa humo kwenye kibanda,

‘Unaona…..kuna maiti imeokotwa au maiti inatakiwa kufanyiwa uchunguzi….ndio maana hao watu wapo hapo, na huenda mwenye hiyo boti ana mahusiano na hiyo maiti…’akasema huyo mtu.

Inspecta hakuwa na amani alihisi kuna jambo lisilo la kawaida,…akakumbuka kilichomleta hapo, akageuka huku na kule kulitafuta gari alilolifuata, na kwa mbali akaliona likiwa limeegeshwa pembeni ya nyumba, akaanza kulisogelea lile gari

Alipofika pale akakuta hakuna mtu, ila aliona simu kwa ndani imeachwa, akasema kwa kimoyo moyo

‘Huyu jamaa bwana, kakurupuka kwa haraka na kuacha simu yake humu ndani, hajui wezi wakiona hivi wanaweza kuvunja na kuingia kwa ajili tu ya hiyo simu.

Taratibu akatoa funguo wake Malaya na kufungua mlango wa hilo gari, akaichukua ile simu na kulifunga lile gari, kama kawaida akasimama pembeni kuangalia huku na kule kama atamuona mwenye hilo gari, lakini hakutokea,

Akiwa amesimama pale mara akasikia ujumbe wa simu ukiingia kwenye simu, akagundua ujumbe huo umeingia kwenye simu aliyoichukua kwenye lile gari, akaingiwa na hamasa ya kuusoma,

Akaichukua ile simu na kusoma ule ujumbe;

‘Usiende kwenye hicho kikao ni mtego wa kuwamaliza wote,…’ujumbe ukaishia hivyo

‘Kikao, kikao gani,..akajiuliza, na hapo akaingiwa na hamasa ya kusoma ujumbe za nyuma

‘Mnahitajika kwenye kikao maalumu , fike eneo la makaburini, alipozikwa kiongozi wetu, hakikisha una kila kitu chako, ni muhimu usikose…’ujumbe ukaishia hivyo

Mhh, ….alipozikiwa kiongozi wetu….mmh, usiende kwenye hicho kikao ni mtego wa kuwamaliza…..


WAZO LA LEO: Huwezi kujua ndani ya nafsi ya mwanadamu kuna nini, kapanga nini, kama hali hiyo ingelikuwa wazi, kila mtu akaona ni nini mtu mwingine anawaza, anapanga,basi  tungelikimbiana maana wengine wana inda, chuki, husuda ….visasi, na kama wangelijaliwa kufanya hayo waliyonayo moyoni,wangelifanya ubaya uliopindukia. kumbuka kuwa nafsi ya mwanadamu ni kichaka cha giza kilichojaa mambo mengi mazuri na mabaya.

Ni mimi: emu-three


Ni mimi: emu-three

No comments :