Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 6, 2014

DUNIA YANGU-43


Inspecta Maneno alikuwa akiongea na mkuu wake wa kazi, akitoa taarifa ya safari yao ya kwenda kumuona mama wa huyo anayemiliki hoteli ya Paradise, na akaanza kuelekezea;

‘Mkuu yule mama ni kiboko, pamoja na kuchanganyikiwa kwake, lakini mama yule anaonekana ni jasiri kweli, hutaamini kuwa ni mzee, ana amri, vitisho, ….’akasema.

‘Kwani imekuwaje, mumepata nini cha kusaidia kujua ukweli wa hilo kundi?’ akaulizwa

‘Yule mama sizani kama anaweza kutusaidia lolote, yeye kasema kweli mtoto wake amekufa, na yupo huko kaburini kwake, na tukamuuliza hilo kaburi lipo wapi..’akatulia

‘Kwani kaburi lake halijulikani lipo wapi?’ akauliza huyo mkuu

‘Kiukweli hakuna anayefahamu wapi alizikiwa japokuwa kwenye taarifa za dakitari aliyethibitisha kufa kwa huyo mtu zinaonyesha kweli, huyo mtu alishafariki, sasa alipofariki alizikiwa wapi, imekuwa ni kitendawili kingine..’akasema

‘Hakuna ndugu au jamaa yoyote wa familia hiyo anaefahamu, au wawekezaji wake , ina maana alipokufa hakuna watu waliohudhuria mazishi yake?’ akaulizwa

‘Kwa taarifa za juu juu tu, wanasema kifo cha mtoto huyo kinahusiana na mambo ya kishirikina, alipokufa hakuna mtu aliyeruhisiwa kufika kwenye huo msiba, walikuwepo ni wazee wachache kutoka huko kijijini kwao, na kundi la vijaba kutoka hko huko kijijini kwao, ambao walikuja na hao wazee kusaidia mazishi, na kilichoendelea hapo hakuna anayejua…’akasema

‘Lakini walizikia hapa hapa mjini?’ akaulizwa

‘Ndivyo inavyoaminika hivyo, …ni jambo lililofanyika kisiri sana, na baadaye wanasema hao ndio pekee walitakiwa kufanya hivyo, na kaburi lake halitakiwi kulitembelea, ukitaka kwenda huko kuna msharti yake…..’akasema

‘Masharti gani?’ akauliza

‘Huyo mama anasema ni mpaka ufe…’akasema na mkuu huyo akacheka kidogo, na kusema

‘Msilete mzaha kwenye kazi, ina maana mlishindwa kumshawishi huyo mama kujua wapi kaburi hilo lipo..mumeogopa hayo masharti, hamuoani kuwa alikuwa akiwaogopesha tu….’akasema kwa sauti ya ukali.

‘Mama huyo kachanganyikiwa, hatuwezi kupata msaada wowote kwake,…’akasema Maneno.

‘Tutaliona hilo baadaye, ni lazima ukweli wote ujulikane, nahisi kuna jambo limejificha hapo,…’akasema

**********

‘Mkuu mimi naona hilo halitatusaidia sana kuupata ukweli, inabidi tutumie njia nyingine, na kuhusu hilo kundi, huenda ni wahuni tu walijifanya kuanzisha kitu kama hicho kikakuzwa na midomo ya watu,…sio uhalisia wake….’akasema

`Cha muhimu kwa sasa ni kuwa kesi ya mauaji ya mke wa Inspecta Moto , kesho yake inafikia mwisho wake, na mujibu wa ushahidi ulipelekwa mahakamani ni kuwa  rafiki yako hana hatia na huenda kesi ikafutwa kabisa.

‘Nilishamuambia kuwa hana hatia, na mimi nitajitahidi kumsaidia kuhakikisha haki inapatikana, akawa mkaidi, matokea yake ni ndio anapambana na watu wasijulikana, hivi huyu mtu yupo sawa kweli,…?’ akauliza

‘Hilo ni swala jingine, cha muhimu ni kuwa kesi dhidi yake haipo tena, ila kuna utata katika hilo, inavyoelekea ni kuwa kweli mke wake aliuwawa, hata kama sio yeye, lakini kuna mtu alihusika katika mauji yake, kwahiyo kwasasa kinachotakiwa kufanyika ni kumtafuta muuaji wake ni nani…?’ akaambiwa

‘Haiwezekani, ni nani katoa maneno hayo, mimi mwenyewe nimeongoza upelelezi wake na kuhakikisha kuwa kweli mke huyo alijiua mwenyewe, mnataka nini tena,…mbona mnataka kuharibu mambo, ina maana mnataka kesi hiyo ifufuliwe upya, wakati tumeshaimaliza?’ akauliza.

‘Kwa ushahidi mpya uliopatikana mke huyo aliuliwa,..’akaambiwa

‘Ushahidi mpya, una maana gani kusema ushahidi mpya, na ni nani aliyemuua,…?’ akauliza

‘Inavyooneka aliyepo nyuma ya hayo yote ni hilo kundi haramu…’akaambiwa

‘Haiwezekani, ina maana hamuniamini mimi, hamuamini upelelezi wangu nilioufanya?’ akauliza

‘Sio swala la kukuamini wewe na upelelezi wako, hili ni swala la ushahidi, ambao inavoonekana kulikuwa na njama za kuufisidi, kama ulivyosema awali, unakumbuka ulisema mwenyewe awali kuwa kundi hili lina mbinu nyingi, na moja ya mbinu zao ni kugeuza ushahidi, kugeuza mambo kwa masilahi yao, na kwa vile wana watu wao kila idara hilo kwao inakuwa ni kazi rahisi tu…’akaambiwa

‘Ni nani aliongoza upelelezi huo hadi akafikia kupata huo mnaosema ni ushahidi?’ akauliza, na kabla hajajibiwa mara mlango ukafnguliwa kwa kasi;

‘Ni mimi hapa bwana Maneno….’sauti ikatokea mlangoni na jamaa mwenye midevu akiwa na mawani makubwa machoni akaingia na kukabiliana uso kwa uso na Maneno.

************

Ni siku ya mahakama ambapo kesi ya kuhitimisha kesi ya  kifo cha mke wa Inspecta ilikuwa ikisikilizwa, japokuwa kulikuwa na fununu kuwa kesi hiyo inaweza kuanza tena upya, kutoka na baadhi ya wanafamilia kuja juu na kutoa madai kuwa binti huyo aliuwawa, na hakujiua mwenyewe, na wao wanataka haki itendeke

Cha ajabu kilichotokea ni kuwa hakimu aliyekuwa akiendelea na kesi hiyo toka awali aliamua kujitoa kwasababu ambazo hazikutajwa, na baadaye akawekwa hakimu mwingine, na huyo hakimu mpya, na siku ya kesi hiyo huyo hakimu mpya akaanza kuelekezea kesi hiyo ilipofia na kusema hatua iliyofikia ni kwa wahusika kutoa ushahidi wao kuwa kweli mke huyo alijiua mwenyewe kinyume na ilivyoletwa awali.

Kesi hii imekuwa na utata mwingi, na sisi kama mahakama, tumeliona hilo ndio maana hatukukimbilia kutoa hukumu, na kama tulivyowaagiza waendesha mshitaka kuwa waje na ushahidi unaothibitisha maamuzi yao, tunawahitajia leo watoe ushahidi wao kamili…’akasema hakimu.

Muendesha mashitaka akaanza kuelezea na kuanza kutoa vidhibiti mbali mbali vikielezea tukio zima lilivyokuwa na hadi mke huyo akafikia kujiua.
Upande uliokuwa unatetea ambao kwasasa umewashangaza wengi kuona unashinikiza kuwa mshitakiwa afikishwe mbele ya mahakama ili waweze kumtetea na kuhakikisha kuwa kweli hakuhusika;

‘Inavyoonekana wote sasa mnamtetea mshitakiwa lakini kwa njia tofauti, …’akasema hakimu

‘Sisi muheshimiwa hakimu tunachohitajia ni wao wamleta mtu wetu mbele ya mahakama, maana hatumuoni, na tuna uhakika kashikiliwa na hao waendesha mashitaka kwa nia ya kuharibu uhalisia…’wakasema watetezi.

‘Kuharibu uhalisia gani, kama kesi ipo hapa mbele ya mahakama, sheri itaangalia uhalisia na ukweli wa jambo hilo, hiyo ni kazi ya mahakama sio wewe….’akasema hakimu.

‘Huyu mtu yupo lakini tumemuhifadhi kwa usalama, …’wakasema waendesha mashitaka

‘Sisi ndio watetezi wake na ndio tuliobeba dhamana yake, inakuwaje waendesha mashitaka wageuke kuwa wao ndio watetezi wake, je hii sheria gani muheshimiwa halimu.?’ wakahoji

‘Kwasababu nia yenu sio kumtetea mlifanya hivyo kwa masilahi binafsi, na tuna ushahidi kuwa kuna watu walitaka kumuua, ili kupoteza ushahidi…’wakasema waendesha mashitaka

‘Shutuma hiyo ni nzito sana, je waliotaka kumuua ndio hao watetezi wake?’ akauliza hakimu

‘Hatujasema ni hao watetezi wake, ila kuna watu ambao walitaka kumuua kwa sumu, je kama wao ndio watetezi wake mbona hawakuweza kumlinda kwa hilo, na alipotoweka walianya juhudi gani za kumtafuta, ndio maana tukachukua jukumu hilo la kumlinda hadi hapo haki itakapopatikana na waliohusika wakafikishwa mbele ya mahakama hii tukufu…’wakasema

‘Ushahidi wenu umeishia hapo?’ wakaulizwa na hakimu

‘Ndio muheshimiwa hakimu, kutokana na ushahidi huo na vielelezo tulivyotoa, tumejirizisha kuwa kweli mshitakiwa hana hatia, na mke wa Inspecta alijiua mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo kuwa mume wake alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine, lakini kumbe mume wake alikuwa katika harakati za kufanya kazi yake…’wakasema

 Hakimu akageuka kuteta na wasaidizi, na wakati wanateta, mara mlango wa kuingia mahakamani kukaonekana kama kuna msogomano, ilionekana kama kuna watu anataka kuingia na kwa vile nafasi ilikuwa n indigo kukawa na kusukama, na hakimu akauliza;

‘Kuna zogo gani linaendelea huko mlangoni?’ akauliza

Na kabla hajajibiwa mara mtu mmoja mwenye mandevu mengi akaingia na kumsogelea muendesha mashitaka wakateta, na hakimu akasema

‘Ni nani wewe unayengilia mahakama yangu bila mpangilio…?’ akauliza
Muendesha mashitaka akasema;

‘Samahani muheshimiwa hakimu, huyu aliyeingia sasa hivi ndiye mshitakiwa waliyekuwa wakimuulizia wenzetu, na kaja rasmi,…’akasema na watu wakawa wanashangaa kwa kutoa sauti ya mguno

‘Kiutaratibu anatakiwa kukaa sehemu ya mshitakiwa, na kwa vile maamuzi yameshafikiwa huku mbele kuwa hana hatia, hatuoni kama kuna haja ya yeye kuja kukaa hapa mbele tena…kuanzia sasa yeye ni mtu huru , hana hatia…’akasema hakimu

‘Muheshimiwa hakimu, mimi nimefika kwa lengo moja, kuwa mke wangu hakujiua mwenyewe, amuuwawa….’akasema huyo mtu mwenye ndevu.

Watu wakaanza kuguna na kila mmoja akawa anongea lake.

‘Kwanini unasema kuwa hakujiua mwenyewe wakati ushahidi upo wa kutosha kuwa amejiua mwenyewe?’ akaulizwa

‘Ushahidi huo ni wa kutengenezwa,……’akasema

‘Una uhakika na hilo unalolisema, maana wewe ndiye uliyekuwa ukishukuwa na mauaji hayo, na wewe ndiye uliyekuwepo hapo siku hiyo, hakuna mtu mwingine aliyewahi kuingia humo kabla , kwa namna hiyo unataka kusema nini, kuwa wewe sasa unakiri kuwa kweli ndio wewe uliyemuua mke wako...?’ akaulizwa


WAZO LA LEO: Hata siku moja huwezi kufuta haki na ukweli kwa hadaa, kwa kufanya hivyo ni kujenga jamii isiyo aminiana, na matokeo yake ni jamii hiyo kuishi maisha ya ujanja ujanja, utapeli ulaghai na rushwa. Usitegemee amani kuwepo katika jamii ya namna hiyo. 

Ni mimi: emu-three

No comments :