Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 1, 2014

DUNIA YANGU-40




‘Bosi, kwasasa haitawezekana......

‘Ok, kama haitawezekana kwako wewe, nitampa kazi huyo uliyemtaja, …naona nyote wawili kwasasa ni tatizo kwa kundi, hata hivyo kazi mliyohitajiwa kwenye kundi mumeshamaliza, kubakia kwenu kwangu naona hakuna maana mnakuwa ni mzigo tu,…

'Na kwa vile umemuota huyo mtu anayeitwa Kifo kuwa kakujia basi kwanini hiyo ndoto yako iswe kweli kwa sasa ,…basi jiandae, kifo atakuja kukutembelea hilo nimelithibitisha rasmi, kazi kwako...

..... na kabla hajasema neno, akahisi kitu kikipenya mkono wa kushoto, ….akajua hiyo ndio ile, sindano ya umauti. Kifo keshafanya kazi yake…..

Tuendelee na kisa chetu




Kilikuwa chumba maalumu, ambapo mtaalamu alikuwa akifanya kazi, na alikuwa akiliondoa lile jiwe jeusi kutoka kwa mgonjwa wake, na ilivyo, lile jiwe haliondoki mwilini, pale lilipowekwa, kwenye jeraha, mpaka lihakikishe limenyonya sumu yote iliyoingia kupita kwenye damu, na likidondoka ujue sumu imeshakwisha.

 Mtaalamu alipokwisha kumaliza kazi hiyo, iliendelea na kazi nyingine ya kumpaka paka madawa ya miti shamba mgonjwa wake, zilikuwa dawa zene harufu kali ya kukereketa puani ilichukua muda kuhakikisha kazi hiyo imekwisha, baadaye akasema;

‘Mhh, hii sumu ya safari hii ni mbaya zaidi, huyu aliyefanya hivi, alijua kuwa kuna dawa imepatikana ya kutoa sumu kwahiyo ameongeza nguvu yake....hata hivyo, naona imekwisha, tusubiri mgonjwa azindukane….’akasema bado akionyesha wasi wasi

‘Lakini mtaalamu, sisi tunahitaji akizindukana asijua kilichotokea, maana bado anahitajika kuwajibika, na usije kumuambia kuwa mimi ndiye niliyemleta hapa…’ Jamaa mmoja aliyekuwa akianalia hayo yakiendelea akasema.

‘Hamna shida, nikiona yupo tayari, basi watu wenu wamchukue na kumpeleka sehemu salama…’akasema.

‘Nitaangalia hilo, mimi nakwenda kuna kazi naenda kumalizia …..’sauti ikasema na huyo mtu akaondoka na mgonjwa akawa anahangaika, alionekana kutapatapa huku na kule,na mtaalamu akahisi huenda ni maumivu na kwahiyo alihitajika kumpa dawa ya namna hiyo.

‘Mmmh mbona huyu mgonjwa ananitia wasiwasi,…’akasema na binti yake aliyekuwa karibu yake akauliza.

‘Lakini baba kawaida sumu ikitoka, mara nyingi, mgonjwa hahangaiki sana, lakini huyu inaonyesha ana maumivu ya ndani kwa ndani…’akasema.

‘Halafu jana nimeota ndoto mbaya, mizimu haikutaka nimtibie huyu mtu, inadai ni mtu mbaya..’akasema.

‘Baba nawe bwana, kwani hiyo mizimu haikubali mtu mbaya kutibiwa, huenda akipona akajirekebisha….’akasema.

‘Kuna watu wabaya wametenda mabaya sana, hata akipewa muda wa kujirekebisha, hawezi kufanya hivyo, roho zao zimeshajaa chuki, …ngoja tuone titafanya nini..’akasema na kujaribu kumpa huyo mgonjwa, kwa kumpanua mdomo, na alipomeza, akatulia na kusema;

‘Hiyo itafanya kazi yake, wewe subiria hapa akiinuka kama kawaida mpe ile dawa, na awe karibu na choo, maana hiyo niliyompa yenyewe, inakwenda kusafisha uchafu wote tumboni…’akasema na kuondoka.

Baada ya muda yule mgonjwa aliinua uso, na mara akashituka, akawa anahangaika kuangalia huku na kule, na mwishoni akatuliza kichwa na uso wake ukakutana na sura ya binti mrembo, haraka akajaribu kujiinua…

‘Mhhh…’akaguna.

‘Hutakiwi kiunuka, kuna dawa natakiwa nikupe kwanza, ukishainywa, unatakiwa uende sehemu ya chooni,…ina nguvu sana…kazi yake kubwa ni kusafisha sumu na uchafu uliopita hadi tumboni..’akasema huyo binti.

‘Mhh, nikiwa na binti kama wewe karibu , ninakuwa nimeshapona, ….wewe ni nani, ni nesi, au, lakini mbona hapa sio hospitalini, kunanuka madawa yam ii shamba, hapa nipo wapi…?’ akauliza.

‘Sihitajiki kutaja jina langu,muhimu ni wewe kupona, unajisikiaje …?’akasema.

‘Kwanza kwani hapa nipo wapi maana nahisi ‘Kifo’ atakuja hapa muda wowote kunimaliza, nipo wapi hapa binti?’ akauliza akitaka kuinuka.

‘Kwa mganga, wa tiba mbadala….usiwe na wasiwasi upo kwenye usalama…’akasema

‘Kanileta nani hapa?’ akauliza

‘Mimi sijui…’akasema huyo binti

‘Ninakumbuka kuna mtu alitaka kunichukua kwenye pikipiki, na mara nikapigwa sindani ya sumu, yupo wapi huyu mtu wa pikipiki…?’ akauliza

‘Mimi ninavyokumbuka wewe hapa hukuletwa na pikipiki, umeletwa na taksi…’akaambiwa

‘Oh, ina maana ndio yeye….’akasema

‘Nani?’ akauliza

‘Kifo…’akasema

‘Kifo ndio nani…?’ akauliza

‘Mhh, usiombe kukutana na mtu kama huyu, akija kwako ujue anakuja kukumaliza, na kama bado nipo hai basi safari hii kafanya makosa, na ole wake nikutane naye tena…’akasema

‘Muhimu ni wewe upone kwanza….’akaambiwa na huyo binti.

‘Mmmh, ina maana baba yako ni mtaalam wa tiba mbadala anaweza kuondoa sumu mwilini..mmh, basi baba yako ni tajiri sana….’akasema

‘Ndio anaweza kawasaidia watu wengi sana, hata hivyo yeye hana utajiri wowote, kazi zake nyingi anafanya kwa kujitolea, analipwa pesa kdogo tu…’akasema

‘Mimi nitamfanya awe tajiri, kama kaweza kuokoa maisha yangu..japokuwa siamini, maana sumu iliyopachikwa mwilini mwanagu natakiwa kufa,ile sumu ikiingia mwili, inaua kiajabu, inapandisha shinikizo la damu, ukidondoka, unahesbu masaa….’akasema

‘Huwezi kufa kwa hiyo sumu , labda ufe kwa kitu kingine, sumu imeshaondolewa mwilini mwako na dawa za baba….’akasema huyo binti

‘Una uhakika gani wewe, mimi naifahamu sana hiyo sumu inavyofanya kazi yake, hakuna dawa ya kuweza kuiondoa hiyo sumu, na huwezi kujua ni sumu ya aina gani ukipimwa hospitalin, wataishia kusema umepatwa na shinikizo la damu…’akasema

‘Hahaha, ina maana huamini, sasa kama huamini subiri uone miujiza ya dawa ya baba, mwenzako mbona keshapona..na kama ni kufa si ungelishakufa basi, masaa karibu kumi na tano, baba alikuwa akikuhangaikia,….’akasema

‘Umesema mwenzangu alishapona ni mwenzangu gani huyo?’ akauliza

‘Kuna wagonjwa wengi wanaletwa hapa kwa baba wakiwa na sumu mbaya zaidi ya hiyo wanapona, ..umeshapona hakuna sumu tena mwilini mwako…’akaambiwa na huyo binti alipokumbuka kuwa aliambia asimtaje mgonjwa ambaye aliwahi kutibiwa na baba yake kwa tatizo kama hilo

‘Una uhakika gani wewe, umesomea wapi kujua hilo, na huyo mwenzangu ni yupi huyo…?’ akawa anauliza

‘Chukua dawa hii unywe, halafu unatakiwa kukaa karibu na choo, kwani inamalizia sumu iliyopo tumboni…tunapoteza muda kwa kuongea…..’akaambiwa, na akainywa ila dawa, baadaye akatoka kuelekea huko chooni, na aliporudi akakuta chumba kina watu wengine yule binti hayupo, alikuwepo mkuu wake wa kazi na mzee moja ambaye kwa jinsi alivyomuona alitambua kuwa ndiye huyo mtaalamu wa kutoa sumu.

‘Pole sana, natumai sasa wewe ni marehemu, kama walivyotaka hao watu wako, na kuanzia sasa hatutaki ujulikane kuwa upo hai, tunataka tuimalize hii kazi mara moja, utashirikiana na mwenzako

‘Mwenzangu gani?’ akauliza

‘Rafiki yako…’akaambiwa

‘Ni nani huyo rafiki yangu, maana nijuavyo anayetambulikana kama rafiki yangu ni marehemu….?’ Akauliza
Mara mlango ukafunguliwa akaingia jamaaa akiwa na mindevu mingi, akasema

‘Ni mimi rafiki yako, najua ulishajua kuwa umemaliza kazi uliyokuwa umetumwa na bosi wako ya kunimaliza, lakini haikufanikiwa na maana mungu ndiye anayejua lini mja wake ataejea kwake, ….’ile sauti aliyoisikia kule chumbani kwa moto ikatanda hewani, akaiduwaa, na kuuliza

‘Ina maana ni wewe uliyefika kule…..’akasema, lakini akiwa na wasiwasi asije akawa yule mwendesha pikipiki ambaye alishahisi wana mahusiano na kundi, na alifanya vile ili kumpa nafasi kifo afanye kazi yake.

‘Usijali.....mimi nina mengi nataka kuyasikia kutoka kwako, kwani nina uhakika wewe ndiye uliyemuua mke wangu, lakini kwasasa hilo halina umuhimu au sio mkuu….’akasema akimgeukia mkuu wake.

‘Sio kweli,mimi sijamuua mke wako, mke wako alijiua mwenyewe mbona hamnielewi nyie watu, hilo nawahakikishieni, kajiua mwenyewe kwa kuogopa kashifa….’akasema akionyesha wasiwasi

‘Hata kama alijiua mwenyewe lakini sababu kubwa ni wewe uliyehusika kuzitengeneza hizo kashfa…hayo utakuja kuniambai vyema baadaye ni lazima hilo lifanyiwe kazi, siwezi kukubali hata siku moja mke wake afe, na aliyefanya hivyo asiwajibike, jino kwa jino….hilo ukumbuke...’akaambiwa.

'Ina maana kama mrembo Jembe angeamua kujiua kwa kashfa mlizohusika naye, wewe ungekuwa umemuua,...hizo ni mbinu za kundi hilo....'akasema kwa kujitetea.

'Tutaona...ukweli wake...sijaamini hayo unayoyasema....'akasema huyo mtu

Mkuu ikabidi aingilie kati na kusema;

‘Kuanzia sasa nyie hamtakiwa kuwa maadui, tunahijai kazi moja ya kulimaliza hili kundi, hayo yaliyopita yaacheni kwanza, mnanielewa…’akasema huyo mkuu

‘Sawa mkuu….’akasema Maneno, lakini huyo mtu mwingine mwenye madevu alikuwa akimuangalia Maneno kwa macho yaliyojaa hasira….


WAZO LA LEO: Kumtendea mwenzako ubaya ni rahisi sana, na kwa vile hujui uchungu wa ubaya huo, kwako itakuwa rahisi kusema, yaishe,samahani,….. kama utakuwa na angalau na chembe ya busara, lakini ngoja siku utendewe wewe uone jinsi gani kelele zitakavyopigwa, dunia nzima itafahamu hilo…hata hakimu hatahitajika kuhukumu, rungu la hasira litashushwa kwako, hata kwa asiyehusika anaweza kuathirika. Hiyo ndio dunia ya bwana Di-amu.
Ni mimi: emu-three


Ni mimi: emu-three

No comments :