Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, September 26, 2014

DUNIA YANGU-37


 Inspecta Maneno aliitwa kwenye jopo maamulumu, jopo hilo ni la maadili na uwakajibikaji, humo kuna wanasheria, na wakuu mbali mbali wenye dhamana. Inspecta aliambiwa aseme ukweli wake, kuhusiana na kadhia ya kundi haramu, lakini hakuweza kusema ukweli huo…..

Kama wakuu na watendaji wanaojua kazi yao vyema, waliona ni vyema kujisafisha na kusafisha idara yao, kwa kashifa zilizokuwa zinaendelea, kwani ili uwe sahihi kwa jambo lolote, kwanza jichunguze kwanza wewe mwenyewe, chunguza familia yako, chunguza watu wako unaofanya kazi nao kwanza….

Ndio maana mku huyo akasema;

‘Ndio maana nimekuita ndani ya chumba hiki, maalumu kwa kazi hiyo, mimi kama mkuu  wakitengo hiki, nina mamlaka ya kusikiliza kesi zote, na mwanzoni nilikutaka useme ukweli ili tujue jinsi gani ya kulitatua hili tatizo, na kwa vile hukutaka kutoa ushirikiano, basi inabidi tupate maelezo sahihi kutoka kwako, kwa utanguzi wa kesi, na hili linatakiwa lifanyike sasa hivi…’akasema.

‘Lakini sikujiandaa kwa hilo….’akajitetea.

‘Wewe ni askari, askari popote anatakiwa awe tayari, kwa hilo huwezi kujitetea, ndio najua hayo ni mambo ya kitaalamu zaidi, lakini kwa kuanza, ni lazima leo tusikilize ukweli , …tunahitaji kusikia ukweli wote ili kuhakikisha kitengo hiki kinaondokana na dhana ya kuwa hamfanyi kazi zenu vyema, na kama hilo lipo, …..’akasema na Maneno akakatiza na kusema

‘Lakini mkuu unataka ukweli gani kutoka kwangu, ina maana huamini taarifa yangu niliyokupa?’ akauliza
I
nspecta akachukua simu na kumpigia mtendaji mwingine, akasema;

‘Mlete….’

*************
Inspecta maneno akawa kaduwaa, hakujua ni nani aliyeitwa, na mara mlango ukafunguliwa, kwa pale alipokaa manen asingeliweza kumuona moja kwa moja huyo aliyeingia, hadi pale alipofika mbele ya meza ya huyo mkuu, alikuwa ni binti mmoja, akiwa kavalia mawani, akayavua yale mawani, na wigi kubwa alilokuwa kalivaa kichwani

Akawa sawa na usawa wa Maneno kumuona, na Inspecta Maneno akabakia mdomo wazi, na hakuweza kuficha mshanga wake, akisema;

‘Mrembo Jembe, umefuata nini hapa?’ akauliza kwa mshangao, na mrembo Jembe akatabasamu kidogo, huku akiwa kasimama kiaskari…yule binti akasema;

‘Mkuu nimekuja…’akasema kwa ule ukakamavu wa kiaskari, na kuendelea kumfanya Maneno kushangaa zaidi, maana ile ishara na ule ukakamavu aliouonyesha huyo binti unaonyesha wazi huyo binti hakuwa anaigiza ni kweli upo kwenye damu.

Detective Jembe, karibu ndani ya kikao,….nakutambulisha kwa jopo kwa mara ya kwanza, sikupenda utambulike mapema, lakini kwa vile unahitajika kwenda masomoni na ukirudi najua utakuwa mtu mwingine nimeona nikuweke wazi kwa watendaji wengine…’akasema mkuu huyo.

‘Haiwezekani….’akasema Maneno, na mkuu hakujali huo mshangao wake, akawa amemuangalia huyo binti, akiendelea kusema;

‘Pole sana kwa majukumu mazito, najua ni kazi ngumu na yenye kujitoa mhanga, na wakati mwingine ilibidi ujizalilishe, ili mwisho wa siku tuweze kupata kile kinachostahili…hilo mungu atakulipa, na serikali imethamini juhudi yako hiyo ndio maana imeona ikupeleke ukasome zaidi, ili ukija uwe mkuu kama sisi…’akasema.

‘Ni kweli kazi zetu hizi zina mitihani mingi, …mwanzoni kama isingelikuwa kipaji hiki alichonipa mungu, ningewachukulia nyie wote, kuwa makosa mliyoyafanya ni kutokana na utendaji wenu wa kazi, ni sehemu ile ya kujitoa mhanga,…ndio maana nilitangulia kumsisitiza Maneno aseme ukweli wake,..wenyewe mumesikia nikimsisitiza, lakini akakataa..nilijua hataweza kusema ukweli…’akasema.

‘Sasa Inspecta Maneno unapewa nafasi ya mwisho, ya kuongea ukweli ulivyo…’akasema na Maneno akainama chini akiwa hana la kuongea. Mkuu akageuka kuwaangalia waliopo humo ndani, halafu akageuka tena kumuangalia Maneno na kusema;

‘Maneno unajua katika kazi zetu hizi tunatakiwa tuwe waangalifu kila hatua, nilipowatuma wewe na mwenzako kwenda kwenye hicho kituo niliwaamini sana, na ni kweli mwanzoni ulikuwa mtendaji mzuri sana wa kazi, kwahiyo hakuna aliyeweza kukutilia mashaka…ila mimi sikuwa nimekuamini kihivyo..’akatulia

‘Kutokana na uzoefu na kipaji alichonipa mungu, cha kuwagundua watu walivyo, mimi niliwahi kutamka kwa mkubwa wangu wa kazi kuwa wewe sio mwaminifu kama unavyojionyesha, ni kama fisi ndani ya ngozi ya kondoo…’akasema.

‘Mkubwa wangu huyo hakunikubalia kauli yangu hiyo, akijua wewe umeweza hata kwenda kusoma nje, na kupata ujuzi, elimu iliyo bora, kwahiyo utakuwa ni hazina ya serikali,..na kiukweli ulifaulu vizuri na kazi yako unaijua, una taaluma nzuri elimu ya hali ya juu, lakini kuna udhaifu ulio nao, ambao ni tamaa, tamaa imekuzidi…hilo unalijua mwenyewe ndani ya nafsi yako….’akasema.

‘Ni kweli wakati mwingine kwenye kazi zetu hizi, unategeka inafikia hatua unasema potelea mbali ngoja nifanye wanavyotaka wao, lakini mwisho wa siku unatakiw ujirudi, ujue wajibu wako ni nini…nilitarajia na wewe utafanya hivyo, tumekupa muda wa kutosha kufanya hivyo, lakini hata kama tungekupa miaka mia, hadi unaingia kaburini, usingelibadilika….’akasema.

‘Na sasa hivi ulikuwa mbioni kuandika barua ya kuacha kazi…ili upate muda wa kufanya mambo yako vyema, hayo yote tunayajua, ..au unabisha hukuwa umeshaandaa baru ya kuacha kazi?’ akaulizwa.

‘Mkuu…..’akataka kusema lakini mkuu wake akaendelea kuongea;

‘Maneno, hata hivyo kwa vile wewe ni mfanyakazi wetu, kiubinadamu tuliona bora tukupe nafasi nyingine mbele ya jopo hili, ujirudi, kwani huenda, umetegeka, sana, unaogopa ahadi uliyotoa kwa mabosi wako wa utajiri,ndio maana nimekupa nafasi a kusema ukweli na kujitetea hapa, sisi kama watendaji , viongozi tuliopewa dhamana tungejua ni nini cha kufanya..lakini hukuweza kufanya hivyo…je unaweza kujitetea kivipi kwa hilo…’akasema

‘Labda kwa muhutasari tu, ningelipenda, kuelezea kwa kifupi, kuhusu hili kundi haramu, kutokana na utafiti uliofanyika hadi sasa, ni kuwa kweli kundi hilo lipo, na limeweza kuwateka sehemu kubwa ya watendaji wazuri kutoka kwenye idara nyeti, na nia yao ilikuwa hivyo, kuwapata wale watendaji wazuri, hasa wale wenye akili ya ziada katika utendaji wako, ni kipaji chao….’akatulia

‘Kwahiyo utaona kwa jinsi gani walivyokuwa wamejipanga, kila sehemu kila idara na kila mahali ambao walijua kuna umuhimu kwako waliweza kuwapata watu wao, kutoka humo au kuwapandikiza wengine kwa kuajiriwa sehemu hizi…’akatulia.

‘Tulihitajia muda zaidi wa kulikamata hili kundi, kwani ni hatari na wamejipanga kikamlifu, wameenea kila sehemu, na sio humu nchini tu, kundi hilo ni la kimataifa, hili lililopo hapa nchini ni kundi dogo tu, ukilinganisha na mtandao wao ulioendea dunia nzima…’akasema

‘Wameweza kupenyeza watu wao kila mahali, na kila vurugu inayotokea ujue ni wao wameichochea kupitia kwa watu wao waliowapandikiza, na wanafanya hivyo wakiwa na malengo, kuhakikisha kuwa wanawavunja nguvu wale wanaoona ni maadui zao, na pia ili waweze kupenyeza mambo yao….ni wajanja sana.

‘Maneno angeweza kuthibitisha haya, kama angekuwa mkali, lakini naona aliona huko ni bora kuliko nchi yake, ni bora kuliko wananchi wake, maana yanayotokea hapa ni madhara kwa nani, ni madhara kwa raia, kwa wanachi ambao wanalipa kodi zao, ili tuweze kupata mishahara yetu, ina maana wao ndio wametuajiri, sasa leo unawageuka…ni dhambi kubwa sana…’akasema.

‘Utajiri ni kitu cha muda, huwezi kuishi nao milele, utatumia, itafika muda utakufa utauacha, lakini wema, uadilifu, haki na uwajibikaji kwa ajili ya dhamana uliyopewa ndio hazina pekee utakayoondoka nayo, hiyo ni taji kwako, hata ukifa bado utabakia nayo milele…..’akasema.

‘Katika kazi zetu hizi, asilimia kubwa ni kujitolea muhanga, unakuwa tayari kufa kwa ajili ya wenzako, na ni kweli hakuna  utakachoweza kulipwa kitosheleze hayo tunayofanya, kujitolea nafsi kuwa mbele ya risasi kwa ajili ya kulilinda taifa lako, ni kazi kubwa sana…’akasema na kugeuka kumuangalia yule binti.

‘Hebu angalia binti mdogo kama huyu, aliwekwa mbele ya hatari, kujitolea kufanya hata yale yasiyofaa, kwa ajili ya taifa lake,….anashida gani huyu binti, ni mzuri, ana vipaji vingi tu, angetulia na kujifanyia shughuli zake na, angelikuwa mbali sana, lakini kwa uzalendo wa nchi yake, utashi, wa taifa lake, aliamua kujitolea, kufanya hata yale yasiyofaa ili kuhakikisha taifa lake linakuwa katika amani,…hivi kweli mtamlipa nini huyu binti, kinacholingana na hiyo kazi aliyofanya….’akatulia.

‘Eti Maneno, hivi kweli wewe ungelikuwa ni mkuu, ungelimpa nini huyu binti kwa hayo aliyoyafanya kwa ajli ya taifa lake, ambayo wewe umeshindwa kuyafanya, hakuna thamani itakayolingana na hayo aliyoyatenda ni kujitoa mhanga tu kwa ajili ya taifa lako….’akatulia

‘Jembe najua upo kwenye maandalizi ya safari yako, lakini tutakuhitajia kutoa ushahidi muhimu kwenye kesi yetu hii, ikibidi,….hata hivyo, najua kwa sasa Maneno ana mengi ya kusema, na yeye, atahitajika kulikabili hilo kundi lake, hadi mtu wa mwisho…huo ni wajibu wake….’akasema.

‘Pamoja kuwa yeye ni mhalifu lakini kwa dhamana aliyopewa, ajue kuwa ni deni, na hilo deni ni lazima alilipe, na kwa kazi yetu hii, huwezi kusema naacha kazi, hili halipo, wewe ni mtu wa usalama katika maisha yako yote…sasa basi…tunahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu kuanzia sasa…’akatulia.

‘Maneno tunakupa nafasi nyingine ya mwisho, kuliweka wazi hili jambo, tunahitaji kusikia kila kitu unachojua kuhusu hili kundi, na unajau ni nini kitakacho kupata ukisaliti nchi yako…’akaambiwa na Maneno akabakia kimiya akiwa hana nguvu kabisa.

‘Pamoja na wewe pia tuna nguvu nyingine ya kutosha, wapo watu wengii mtashirikiana nao, kuhakikisha kundi hili linafyweka, na kila anayehusika, kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, kila kitu kipo tayari, cha muhimu ni mambo machache ambayo tunayahitajia kutoka kwako …’akasema akimuangalia Maneno

‘Maneno upo tayari kutoa ukweli wote….?’ Akaulizwa

‘Mkuu, kwa hali kama hii unataka mimi niseme nini,….najua hamtanielewa, kwasababu mumeshaniweka kwenye kundi hilo, lakini hamjui mitihani gani niliyokutana nayo hadi kuweza kuingia huko…..ni vyema, ikabakia hivyo, na kama ulivyosema, nahitajika kulipa deni la wananchi, ..nitafanya hivyo, na kiukweli sikuwa nafurahia hayo yaliyotokea, ili kulihakikisha hilo nitafanya yote niwezayo kuhakikisha hilo kundi linapatikana….’akasema

‘Kabla ya hayo, tunahitaji ukweli wako, tunahitaji yote unayoyajua, na uliyoyafanya, kuanzia kwa kifo cha muheshimiwa, hadi kifo cha mke wa Inspecta….maana hata kauli yako bado ina mashaka, unakuwa kama huamini kuwa kundi hilo lipo…unaposema linapatikana una maana gani…’akasema mkuu.

‘Mkuu hayo si yanajulikana, …mimi sioni kwanini nioyaongee tena, …na kuhusu kundi siwezi kukiri moja kwa moja kuwa lipo….’akasema

‘Nakuelewa sana Maneno, najua ulivyo, lakini kumbuka utajiri sio mali kitu, na natumai umenielewa vyema niliotaka kujua kutoka kwako, kama mkuu wako nahitaji uyaongee yote ukweli wote….’akasema.

‘Sawa mkuu nitafanya hivyo….’akasema

‘Kabla hujaanza kusema ukweli, kiutaratibu wa kesi, kwanza heu tuambie, je ni kweli mke wa Inspecta alijiua mwenyewe…?’ akaulizwa

‘Ni kweli alijiua mwenyewe…’akasema kwa kujiamini

‘Je Inspecta Moto yupo wapi…?’ akaulizwa

‘Hilo mimi sijui, ndio tulikuwa tunamtafuta..’akasema

‘Kwa ajili ya kumuaa au sio…?’ akaulizwa

‘Hayo ni yao wao, lakini mimi nilikuwa na mbinu yangu ya kumuokoa, kama nigetaka kufanya wanavyotaka wao, angelishakufa, ..lakini sikupenda itokee hivyo, na nimefanya juhudi kadri ya uwezo wangu kumuokoa, hata yeye mwenyewe anajua hilo…’akasema

‘Hebu tuambie ukweli kuhusu urafiki wako wewe na mke wa Inspecta…’akaambiwa

‘Hivi hilo ni muhimu kuliongea hapa kwa sasa, hamuoni kuwa linapandikiza chuki,..na mnajua fika hayo yalitokea kwa dhamira ya kunitega mimi ili niingie kwenye hilo kundi…’akasema.

‘Hata kabla ya hayo, hamkuwa na urafiki huo wa siri…?’ akaulizwa

‘Hakuna kitu kama hicho, mimi nilimchukulia yeye kama shemeji yangu, na tulikuwa na utaratibu mnzuri tu, mimi na Moto, hata Moto alikuwa akitoka na mke wangu nilimuamini…’akasema.

‘Wewe ulimuamini mwenzako na kiukweli yeye alikuwa muaminifu kwa mke wako, ila wewe sio mwaminifu..sema ukweli wako, maana hapa ni sehemu ya kujitakasa…’akaambiwa

‘Hilo halipo, sio kweli, tuliheshimiana sana na shemeji yangu,…hata kama mwenyewe Inspecta Moto angelikuwepo angalibainisha hilo…’akasema

‘Sawa labda tusipoteze muda, sasa naona ni bora tuianze hii kesi, kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa wazi, ukweli ubainike, na uwajibikaji uwepo, kisheria na nidhamu za kijesho ziwepo, naona tufanye hivi…’akasema na kuchukua simu kupiga sehemu nyingine akasema

‘Waambie wote waingie chumba cha mashahidi na tutawaita mmoja mmoja….’akasema

WAZO LA LEO: Mara nyingi kwenye ukweli uwongo hujitenga.

Kuna watu wana tabia ya kuwa ndumilakuwili, wakifika kwa huyu wanasema hivi wakifika kwa mwingine wanasema vile, nia na lengo ni kuchonganisha, watu hawa ni wabaya sana, kwa tabia zao hizo, kwani mwisho wa siku ni kuleta uhasama. Ukiona tabia ya namna hiyo ni vyema ukawaita wote wawili, mtoa taarifa na msemwa, ili ukweli ubainike, na hapo uwongo utajitenga, na tabia hiyo itakoma.
Ni mimi: emu-three

No comments :