Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, September 25, 2014

DUNIA YANGU-36


‘Mkuu unahitajika makao makuu haraka….’akasema huyo msaidizi wake

‘Kuna nini tena…?’ akauliza inspecta Maneno kwa mashaka huku akifunga mlango wa nyumba ya Inspecta kwa nyuma yake.

‘Inspecta Moto kapatikana….’akasema Inspecta mwenzake, ambaye kaletwa hivi karibuni kwenye kituo chao


‘Eti nini….!’
 
Tuendelee na kisa chetu

*********

Lilikuwa ni jopo la watu wa usalama, miongoni mwao alikuwepo Inspecta Maneno aliyefika muda mfupi kutoka kituo chake cha utendaji, na alipofika, alikaribishwa kwenye ofisi maalumu.

Kwanza alitakiwa kutoa maelezo kuhusu kituo chake, na kuhusu tetesi zilioenea kuwa eneo lao limeingiliwa na kundi haramu…kwanza alianza kwa kusema yeye alipoitwa hapo hakuwa amearifiwa ni nini anachoitiwa kwahiyo hakuwa amejiandaa kihivyo, ila kwa vile yeye ni askari, wakati wote yupo tayari, basi ataweza kutoa maelezo hayo na kwa ushahidi, kwani kila kitu kipo kwenye mtandao wao wa usalama, …akaanza kutoa maelezo yake na ushahidi

Maelezo yake yalipokwisha ilionekana kama hayatoshelezi, hasa aliposema kuwa maneno au tetesi zilizozagaa kuwa kuna hujuma ndani ya kitengo chao ni mambo ya kisiasa na hayana ukweli  wowote.

Jopo hilo lilikuwa na mambo mengi ya kiutendaji, na yalihitajika kusikilizwa, kwahiyo likaamua kuliweka hilo tatizo la pemneni kwanza, wakawa wanajishughulisha na mambo mengine.

Kwa hali ile ilimfanya Inspecta Maneno kujisikia vibaya, kwani hakujua ni kwanini wanamfania hivyo, lakini kwa vile waliopo hapo ni wakuu wake, ikabidi atulie hadi ikafika hata tena ya yeye kusikilizwa, na sasa akawa anahojiwa na mkuu wake wa kazi.

‘Inspecta Maneno tumekuita hapa ili utuambie ukweli ni nini kinachoendelea katika kituo chako’ akaambiwa.

‘Nimeshaeleza ukweli wote mkuu….’akasema

‘Hatujarizika na maelezo yako, wewe kama kiongozi kuna zaidi ya hayo tunahitajika kuyafahamu, maana hili hapa ni jopo, na linahitaji kuona kuwa kila kitu kipo sahihi na maelezo yote yanafika kwao, …wamaone kuwa leo wapate taarifa moja kwa moja kutoka kwako, je huo ndio ukweli wote….?’ akaulizwa

‘Sijaelewa mkuu msingi wa swali lako, maana juzi tu uliniagiza nikupe maelezo ya uchunguzi wangu na kazi kwa ujumla nikakupa, sasa hili swali ni kuhusu hiyo taarifa nilitoa sasa hivi au jpo linahitaji nini zaidi…?’ akauliza.

‘Ni kutokana na taarifa yako uliyonipa, ambayo inagongana na taarifa nyingine tulizozipokea hivi karibuni kutoka kwa watendaji wenzako…’akasema.

‘Wenzangu ni akina nani ambao wanaokiuka utaratibu wa kiutendaji, kwani wao walitakiwa kufikisha hizo taarifa kwangu kwanza, ili nizifanyie kazi kabla hazijafika kwako…’akasema.

‘Wamefanya hivyo, baada ya kuona kuwa taarifa zao hazipewei kipaumbele, ni kama vile wewe unazizarau taarifa zao, na wakati wao wamesema wana uhakika na hicho walichokifanyia kazi,na wamewahi kukuambia ukasema hazina uzito, sio kweli, ni siasa tu…’akaambiwa

‘Kwanza hao watu ni akina nani,..kweli kiutendaji hilo lipo sahihi, wamekosea sana, hata nyie mnajua hivyo, walitakiwa wanithibitishie, nipata uhakika, mimi kama kiongozi wao siwezi kuleta taarifa zenye walakini…mnalifahamu hilo vyema kama ningelifanya hivyo, nyie wenyewe mngekuwa wa kwanza kunilaumu…’akasema

‘Sikiliza Maneno, kuna kundi haramu lipo katika maeneo yenu, kundi hili sio kundi dogo, ni kundi la kimataifa, inavyosadikiwa ni kuwa kundi hili limeshaingiza hata watu wa usalama, wanasisasa, wafanyabiashara na watu wa kila idara nyeti, kutokana na mbinu zao za ushawishi, mimi nilikuamini sana wewe, ndio maana nikawa nakutumia wewe kupata ukweli, je huo ndio ukweli wote….’akatulia

‘Ndio, huo ndio ukweli wote, nimeshawafikishia kila kitu kutokana na uchunguzi wetu mkuu…’akasema

‘Maneno, hili jopo hapa ni la wataalamu mbali mbali wakiwepo wanasheria, mimi kama mkuu wako wa kitengo, nakupa nafasi ya mwisho nataka kujua ukweli wa hicho kinachoendelea huko, na ukweli huo nautaka sasa hivi...’akasema

‘Mkuu, ukifanya hivyo, unaniweka katika mahali pabaya, maana kila kitu kina utaratibu wake, kama ni taarifa ya hizo tetesi na mnahisi kuna zaidi ya hayo, basi labda mnipe muda tena nilifania kazi…’akasema

‘Kwa hali hiyo ya kuomba muda, ina  maana unakubali kuwa ukweli wote hujatupatia au sio?’ akaulizwa

‘Ukweli wa tatizo ambalo tumekamlisha uchunguzi wake, ndio huo, kuna matatizo mengi kwenye vitengo vyetu nab ado tunaufanyia kazi…sasa kuhusu kuwepo kwa kundi hilo hararamu na kuwa kuna watendaji nyeti wameingizwa, mimi hilo sina ushahdi nao ndio maana nahitaji muda, niweze kuandaa taarifa kitaalamu sizani kama hilo litakuwa sahihi nikiongea tu.

‘Nataka uongee hivyo hivyo, tupata maelezo yako….’akaambiwa.

‘Mkuu lakini hivyo nitakuwa sitimizi wajibu wangu kitaalamu, wewe ni mkuu wangu sawa, ukinilazimisha nikupe maneno tu, ninaweza,  hata bila vielelezo lakini je itasaidia nini,…mimi ni mtendaji na mtaalamu, sitakiwi kufanya hivyo…’akasema kwa kujiamini

‘Nafahamu wewe ni mmoja wa watu wetu tuliowafunza na kuwapeleka nje kusomea kazi hizi,lakini utaalamu wako hauwezi kunifanya mimi nishindwe kutimiza wajibu wangu, kwani hli ninalokuambia lina uthibitisho kuwa kuna walakini katika taarifa zenu, kuna mgongano wa taarifa zenu,….kwahiyo kuanzia sasa nataka uniambie ukweli ulivyo..’akasema huyo mkuu

‘Ukweli upi mkuu, zaidi ya huo niliokuambia…?’ akauliza Inspecta Maneno

‘Inspecta Moto yupo wapi?’ akaulizwa swali.

‘Ndio tuliokuwa tunamtafuta mkuu, hadi napigiwa simu kuja huku, tulikuwa kwenye hizo harakati, siwezi kuja kuongea maelezo yasiyojitosheleza dhidi yake, na  kama ulivyosema, kuwa kuna tetesi kuwa kuna kundi haramua, tena la kimataifa, tulihitaji uangalifu wa hali ya juu, kumtafuta mwenzetu huyo ikizingatiwa kuwa karibuni alimpoteza mkewe, kwahiyo ilibid tuwe makini sana, kwa usalama wake pia …’akasema

‘Mpaka hapo mlipofikia mlishagundua nini?’ akaulizwa

‘Tulikuwa hatujahitimisha, ukumbuke huyu mtu nilimdhamini mimi, kwenye kesi ya kifo cha mkewe, kabla hatujagundua kuwa kweli mkewe alijiua mwenyewe, na kesi yake ilitakiwa kesho au keshokutwa isikilizwe huko uraiani, mara akapotea, iliniweka mimi sehemu mbaya,..kama mdhamini wake…lakini hilo lipo chini ya uwezi wetu tutalitatua tu mkuu….’akatulia

‘Kwanini ulimdhamini ukijua kuwa ana kosa, ..?’ akuliza

‘Mwanzoni ilionekana hivyo, kuwa ana kosa, kuwa huenda ni yeye aliyemuua mkewe, lakini baada ya uchunguzi wangu nikagundua tofauti, na kwa vile naamini kutokana na upelelezi wangu kuwa yeye hakumuua mkewe, mkewe alijiua mwenyewe, nikaona kwanini nisimdhamini mfanyakazi mwenzetu…’akasema.

‘Kutokana na taarifa zako za nyuma, ilionekana kupishana sana na taarifa za mwenzako huyo, ilikuwa kama mnashindana, je hiyo haiwezi kuwa sababu ya matatizo yanayotokea ndani ya kitengo chenu…?’akaulizwa

‘Kitengo chetu hakina matatizo, huo ulikuwa mtindo wetu wa kazi, pamoja na ushirikiano, lakini pia tulitaka tufanye kazi kwa mashindano, ili kukuza utendaji wetu, na kama mlivyoona, kazi zilikuwa zinakwenda haraka na kwa ufanisi….’akasema

‘Kundi hili haramu, linasadikiwa kuea limeweza kuwaingiza watu wa usalama, na hilo lina ushahidi, ni hatari kwa usalama na kashifa kwetu, wewe ni mmoja wa viongozi wa ngazi nyeti katika idara zetu, una taarifa gani kuhusiana na hili….?’ Akaulizwa

‘Kivipi, kuwa ni kweli au si kweli…?’ akauliza swali hili akijua kuna mtego ndani yake.

‘Umenielewa vizuri sana swali langu Maneno, wewe ni mtendaji , mtaalamu nijibu swali langu…’akasema huyo mkuu.

‘Tetesi hizo zipo, lakini mimi kama mmoja wa viongozi , siwezi kulithibitisha tu kwa maneno ya kusikia , mpaka nilifanyie kazi, nilishawahi kusikia hivyo kabla, nikafanya uchunguzi, lakini nilikuja kugundua kuwa ni mambo ya kisiasa tu, hayana ukweli….’akasema.

‘Maneno, hili ni tatizo kubwa sana, na usiponipa maelezo ya kutosha sitasita kuchukua hatua za kinidhamu, ..unajua utendaji wetu ulivyo, na kiongozi kama wewe ulitakiwa unifahamishe hilo mapema, ili tuhakikishe idara yetu haina kashifa zozote…’akasema mkuu

‘Lakini mkuu unaposema hivyo, unakuwa kama unatuhuma dhidi ya utendaji wetu,….je kwanza nielewe, nipo kama kama mtuhumiwa au kutoa taarifa…?’ akauliza

‘Yote mawili,…..nikuambie ukweli, kuwa, kwa hatua iliyofikia, na kwa maeelzo niliyoyapata, mimi kama kiongozi wetu, siwezi kuvumilia tena, kwahiyo kuanzia sasa wewe utafanya kazi huku makaoni, kituo cheni kwa hivi sasa kitaongozwa na Inspecta tuliyemtuma huko hivi karibuni….’akasema

‘Kwanini mkuu…?’ akauliza

‘Uchunguzi bado unaendelea, ulitakiwa urudi kituoni kwako kakabidhi kila kitu kwa mwenzako, lakini kwa vile bado kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi, wewe kwa hivi sasa utabakia hapo hadi taarifa nyingine zitakapotolewa…natumai umenielewa, mengine yatafuata baadaye…’akaambiwa

‘Lakini mkuu bado nilikuwa sijamaliza kazi yangu, na bado tunamtafuta mwenzetu hatujui yupo wapi,…’akasema

‘Hili linafanyiwa kazi, kama kawaida, hapa tunataka kuimaliza hii kesi…’akasema

‘Kesi ya nani?’ akauliza kwa mshangao.

‘Kesi ya mauaji ya mke wa Inspecta, hiyo ni kesi ndani ya idara zetu za usalama, japokuwa uraiani imethibitishwa hivyo, kuwa kajiua mwenyewe, lakini ndani ya idara zetu hilo halijathibitishwa hivyo, ..’akaambiwa

‘Kama ni kesi huo ndio utaratibu wa kesi…?’ akauliza kwa mshangao.

‘Tunachotaka kutoka kwako ni maelezo, kama kweli kajiua au hajajiua na kwanini akajiua, …hilo ni lazima lifanyiwe kazi, kwani ni muhimu kusafisha kitengo chetu haraka iwezekanavyo, na kama ni kuwajibishwa, hatutasita kufanya hivyo…’akasema

‘Na kutokana na unyeti wa kesi hiyo, tumeona kesi hiyo ianze mara moja,kwa kupata maelezo yako binafsi ….’akasema

‘Una maana gani mkuu?’ akauliza

‘Ndio maana nimekuita ndani ya chumba hiki, maalumu kwa kazi hiyo, mimi kama mkuu  wakitengo hiki, nina mamlaka ya kusikiliza kesi zote, na mwanzoni nilikutaka useme ukweli ili tujue jinsi gani ya kulitatua hili tatizo, na kwa vile hukutaka kutoa ushirikiano, basi inabidi tupate maelezo sahihi kutoka kwako, kwa utanguzi wa kesi, na hili linatakiwa lifanyike sasa hivi…’akasema

‘Lakini sikujiandaa kwa hilo….’akajitetea

‘Wewe ni askari, askari popote anatakiwa awe tayari, kwa hilo huwezi kujitetea, ndio najua hayo ni mambo ya kitaalamu zaidi, lakini kwa kuanza, ni lazima leo tusikilize ukweli , …

‘Ukweli upi tena mkuu?’ akauliza

Inspecta akachukua simu na kumpigia mtendaji mwingine, akasema;

‘Mleteni….’

NB: Ni mambo ndani ua kitengo maalumu, tunagusia kidogo tu ilivyookea, lakini wenzetu wamejipanga wao wana kila kitu ndani ya utendaji wao, tutaona baadaye itakavyokuwa.


WAZO LA LEO: Kiongozi wa kweli ni yule anayetafutwa na watu kuwa awe kiongozi wao, kutokana na sifa zake. Na sio yule anayeutafuta uongozi kwa watu kwa kuwaomba watu kuwa yeye anafaa kuwa kiongozi wao. Hatua iliyofikia kwa sasa ,kwa uongozi hasa wa kisiasa umekuwa ni kuwa uongozi sasa ni uwekezaji, kwahiyo ule utashi, ari, na wito  wa uongozi unakuwa haupo tena.
Ni mimi: emu-three

No comments :