Inspecta
alishituka kutoka kwenye usingizi mnzito ulioandamana na ndoto za kutisha,
alipofungua macho alihisi kuchoka sana na akili hakiuwa sawa, hakujitambua kwa
mara moja kuwa yupo wapi…akahisi kichwa kinamuuma…
Akashikilia
kichwa na kupiga miayo, halafu akajitutumua na kukaa, akageuka kutafuta wapi
maji yapo, mara nyingi akiwa nyumbani kwake ni lazima anakuwa na jagi la maji
kwenye kimeza cha kitanda, kwahiyo kwa vile akili haikuwa sawa,a akujua maji
yapo, akanyosha mkono kupapasa, lakini kulikuwa hakuna jagi la maji
Akainuka
ili kutafuta maji, mara akahisi mkono laini ukimpapasa mgongoni, kwanza akajua
ni mke wake, akageuka kumuangalia na sauti ya kutoka usingizini ikasema;
‘Baby
wataka kwenda wapi saa hizi…..’sauti hiyo ilimfanya ashituka na usingizi wote na
machomvi, yakaisha, akakurupuka na kutoka kitandani, akasimama haraka na kuangalia huku na kule,
alijikuta yupo uchi…oh, kumbe hakuwa nyumbani kwake, na alipogundua hivyo,
akaanza kuhangaika kutafuta nguo zake.
‘Baby
unafanya nini, mimi nasikia baridi…njoo bwana bado mapem.’sauti ile ikaendela
kusema;
‘What,
ooh, my God, hivi tumefanya nini…mungu wangu…’akasema na hakuweza kuona nguo
zake, akasimama bila kujua la kufanya baadaye akauliza;
‘Nguo
zangu zipo wapi?’ akauliza
‘Nguo
za nini bwana, mbona hivi,..unajua saa hizi saa ngapi?’ akauliza huyo mrembo, na
kujiinua pale alipokuwa amelala, akakaa kitandani, akiwa kama alivyozaliwa.
‘Siamini…’akasema
Inspecta akimtupia macho kwa aibu, sasa akawa haulii, akawa anahangaika huku na
kule kutafuta nguo zake, na wakati huu akawa anamuwaza mke wake, akijua atakuwa
sehemu…
‘Hahaha
heeya,..njoo, nipo kwenye vyumba maalumu vya starehe, najua na wewe upo kwenye chumba
cha starehe na mwenzako, kwani kuna tatizo gani, siku moja moja sio mbaya,
hahaha, kama wewe umeshatosheka, nitakukuta nyumbani….
Alipokumbuka
hayo maneno akashika kichwa, akageuka kumuangalia huyo mwanamke kitandani na
jinsi alivyokaa mkao wa kihasara, akageuza kichwa haraka na kuanza kuendelea
kutafuta nguo zake.
‘Huamini
nini tena, …wewe sio mtoto mdogo, kama ni mke wako usiwe na wasiwasi yupo na
mpenzi wake wanakula raha, kumbe mke wako ni mkali kiasi hicho, …’akasema na
aliposikia hivyo akashituka na kugeuka kumuangalia huyo binti, na kusema
‘Unasema
nini?’ akauliza na sasa akiwa katulia akijaribu kusikiliza sauti, kama vile
anatafuta sauti ya mkewe itatokea wapi, na yule binti akalala kitumbo tumbo, na
huku akisema;
‘Mhh,
siamini..unajua hawa wanawake wengine bwana huwa wanajifanya wacha mungu kweli,
lakini moyoni sio hivyo, wanakuwa hivyo pale wakiwa kwenye matatizo, lakini wakipata mwanya mdogo tu, wanakuwa kama ngombe
aliyekuwa zizini,… unajua kilichotokea…’akawa anajichezesha chezesha makalio
yake na kumfanya Inspecta akeguke kuangalia kwingine.
‘Mkeo
bwana, anakunywa, hivi ni mnywaji wa pombe hivyo, mimi nilijua ni mcha mungu wa
kweli…, alikunywa sana, ikafika muda hata kusimama hawezi, mwenzake akaona hiyo
imezidi kiasi, akamshauri waondoke,..lakini wapi, akawa anadai mengine…’akasema
‘Anadai
mengine ana anadai nini….mwenzake nani huyo…?’ akauliza Inspecta kwa hamaki.
‘Alikuja
na mwenzake mmoja, na walipoanza kunywa wakaja jamaa wawili watanashati,
wakajiunga nao, ikawa kila mmoja na mwenzake, unaona hapo, kukawa hakutulii,
kila mmoja anataka kumuonyesha mwenzake anajua ….’akakatiza.
‘Anajua
nini…una maana gani, sio kweli,…haki ya mungu , nitaua mtu,…nguo zangu zipo
wapi…’ akasema kwa hasira
‘Mkeo
alipoulizwa na mwenzake kuwa kweli ana nia ya kufanya anachotaka kukifanya,
maana alishavuka mpaka, na alikuwa akimtaka huyo mwenzake watoke, waende vyumba
maalumu, akasema na yeye anafanya kama unavyofanya wewe…’akasema
‘Kama
ninavyofanya mimi, kwani mimi nimefanya nini?’ akauliza kwa mshangao, na kabla
hajajibiwa akaongeza
‘Kwani
mimi nilifanya nini…?’ akauliza huku akijiangalia na mrembo akacheka na kusema;
‘Hahahaha
, wanaume bwana, kwani wewe umefanya nini, hukumbuki eeh, haha eti kwani wewe
ulifanya nini, …, hahaha, nyie wanaume bwana, mbona mna ubinafsi sana, wewe
ulichofanya hukioni, unaona cha mke wako tu,…ningelikuwa mimi wewe, wala
nisingelijali,..’akasema
‘Tatizo
lako hujaolewa kwahiyo huna hisia za kindoa, ukiolewa utaona uchungu wa kuibiwa…
nikimuona huyo mwanamke atanitambua, nitamuua, atajuta kuolewa na mimi, wewe
utasikia hanijui mimi eeeh, na ole wako iwe ni uwongo,..ngoja, nguo zangu zipo
wapi, niambie haraka, .’akasema
‘Unasema
utamuua, acha mihasira hiyo…utafungwa…’akasema
‘Nitamuua,
…yaani yeye kaamua kuwa kahaba,..hajui yeye ni mke wa mtu, anafanya kama nyie
wanawake wahuni msioolewa, ….ngoja,..labda iwe sio kweli, nitamfanya kitu mbaya
, hatakisahau maishani, nitamuulia mbali…’akasema kwa hasira.
‘Hahaha,
niolewe mara ngapi wewe…tatizo lako unajifanya huelewi, anyway, tuongee kibiashara, maana naona unataka kuondoka….’akasema na
kujigeuza akalala chali, hakuhangaika kujifunika, na hapo akamuona Inspecta
akifungua kabati, na kuona nguo zake, akajua mtu wake sasa anaondoka.
‘Tuongee
nini , kibiashara , biashara gani…?’ akauliza Inspecta akivaa nguo zake, na huku
akikosea kufunga vifungo
‘Nakumbuka
nilishakuambia kuhusu kuacha kufuatilia mambo yasiyokuhusu…’akasema
‘Mambo
gani yasiyonihusu, kama yapi….?’ Akauliza Inspecta akitulia kumuangalia huyo
mwanamke, kwa ule mlalo…na ibilisi akawa anafanya kazi yake…hasira ,mara tama kidogo,
na akili ya ulevi ulevi, vikamchanganya mzee mzima…
‘Wewe
huwa unajifanya unachunguza sana mambo ya watu, kiasi kwamba unawakera watu,
unajua hii nchi yetu kila mtu ana mipangilio yake ya kupata riziki, na mingine
ni ya kimabumashi, ….unaonaeeh, sasa kunaweza kutokea kutokuelewana, hapa na
pale, …hapo nyie mnaingiza pua zenu bila kujua chanzo ni nini…’akasema
‘Bado
sijakuelewa, ongea unachotaka kuongea mimi ninataka kuwahi nyumbani,…sijui
kumetokea nini huko, sijihisi vyema…’akasema akipitisha ulimi kulainisha mdomo,
akageuka kuangalia mlangoni.
‘Kwani
kumetokea nini bwana, wasiwasi wako tu…mbona jana usiku hukuliona hilo…ulikuwa
umeniganda kama ruba, hahaha mwanaume wewe, halafu wajifanya kumuonea wivu
mwenzako, ukila vya wenzako na vya kwako ni lazima viliwe, titi for tati…au sio…hahahaheeeya…njoo baby, tuondoe hizo hasira….’akasema
na kucheka huku akijichezesha kitandani.
Inspecta
akageuka kumuangalia, halafu akageuka kuangalia mlangoni, na akilini akasikia
sauti aliyosikia kwa mkewe akiwa kwenye ndoto, na kwenye ndoto hiyo alimuona
mkewe kwa mbali akiwa kasimama , kachanganyikiwa, analia kwa kujuta huku akisema;
‘Mume wangu kwa lolote litakalotokea ujue
nakupenda sana, ujua haya yote umeyataka wewe mwenyewe,usimlaumu mtu kwa lolote
litakalotokea ujilaumu wewe mwenyewe…kwaheri….’ Sauti hiyo ikamfanya aanza
kutembea kuelekea mlangoni na Yule msichana akasema;
‘Ukiondoka
na kuniacha hivi, utakutana na uchafu wako kwa mkeo, na mwingine nautuma kwa
baba ya mke wako……na unajua nini kitafuta baadaye,…’
Inspecta
akasimama,na huki kichwani anasikia sauti ya mkewe akitoa maneno yale yale..
`Lolote litakalotokea
ujilaumu wewe mwenyewe….’
Aliposikia
sauti hiyo ya mkewe, hakusubiri, akatoka mle ndani na huku nyuma mdada akawa
anatoa lugha ya kulaani na kuapiza kuwa atamfanya kitu mbaya, kwa kumtekeleza,
hakujali, akatoka mle hadi sehemu ya mapokezi, akajaribu kumuuliza Yule mtu wa
mapokezi ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka , kumpisha mtu mwingine
‘Samhani
ndugu yangu naomba masaada wako.’akasema
‘Msaada
gani bosi, mimi nimeshamaliza muda wangu ndio naondoka hivyo…’akasema
‘Jana
kulikuwa na mwanamke, alikuwa sehemu hizi,…akalewa na kuanza kuleta fujo,
unamkumbuka….’akasema
‘Oh,
Yule anaonekana ni mgeni sana, na sijui aliwezake kuingia, ..huku hakutakiwi
mambo kama yale,…lakini hakuleta fujo, ila alilewa sana, na mwenzake akataka
waondoke, lakini akawa hakubali, akawa anamlazimisha mwanamke aliyekuwa naye
waingie kwenye vyumba vya wageni, wakati yeye ni mualikwa tu..’akasema
‘Alialikwa
nani?’ akaulizwa
‘Na
huyo rafiki yake…’akasema
‘Rafiki
yake yupi?’ akauliza
‘Siwezi
kukuambia, siruhusiwi….’akasema
‘Sasa
huyo mwanamke yupo wapi?’ akauliza
‘Unajua
bosi mimi kutoa siri haza za mwanachama, ila kama ni huyo mwanamke ameshaondoka
kwenda nyumbani….’akasema
‘Kaondoka
na nani,…saa ngapi?’ akauliza
‘Ni
usiku huo huo, alikuja jamaa, tukasikia huyo mwanamke akisema;…’
‘Shemeji,
shemeji…sasa .sijui ni shemeji yake kwa vipi....’akasema
‘Oh,
nahisi ni Inspecta eeeh, yupoje, na alikuja baadaye au alikuwepo muda wote?’
akauliza akionyesha kutaka kuondoka.
‘Huyo
shemeji yake ….aah, unajua siruhusiwei kuongea zaidi, ila ndio alikuja baadaye,
na alipoona hiyo hali, akamshawishi huyo mwanamke, na baadaye akakubali
wakaondoka naye…’akasema
‘Mke
wangu muda huo alikuwa wapii chumbani au hapo nje…?’ akauliza
‘Tafadhali
bosi,..nimekuambia vya kutosha…ukiwa hapa na ukiwa na mwanachama, kila sehemu
ni hiari yako,….kama huna zaidi naomba uondoke…’akasema akigeuka kuangalia huku
na kule, ilionyesha huyo mtu wa mapokezi alikuwa na wasiwasi kuongea zaidi.
‘Oh…sijui
….sijui…hii sasa ni kashfa, siwezi, haki ya mungu, nitaua mtu, huyu mwanamke
atanitambua,….na huyu rafiki yangu nikikutana naye ama zangu ama zake, ina
maana hata yeye ananifanyia hivyo…’akasema
‘Huyo
aliyekuja baadaye ni rafiki yako, ehe, lakini, mbona yeye, hakuwepo,…alikuja
badaye.’akasema
‘Hakuwepo
alijuaje kuwa mke wangu yupo hapo..ina maana aliitwa na mtu , na huyo
aliyemuita ni nani, huo ni ujanja wao…kwanini wasingeniita mimi, wakati mimi ni
mume wake…’akasema kwa hasira
‘Mimi
haya sijui zaidi,…..kwaheri, ’akasema huyo muhudumu na mara Yule muhudumu
akasikia simu yake ikiingiza ujumbe, akawa anausome, halafu akamtupia jicho
Inspecta, akasema;
‘Tafadhali
uondoke…….hutakiwi humu ndani, vinginevyo urudi kwa mwenyeji wako…’akasema
‘Naondoka……lakini
kabla ya yote nataka kuonana na muhusika wa humu ndani…’akasema
‘Unatakiwa
uondoke, au urudi kwa mwenyeji wako…’ilikuwa sauti kali kutoka nyuma, alikuwa
mlinzi akiwa na silaha yake,…akawa anamsogelea Inspecta, na Inspecta alipoona
hivyo, akageuka kuondoka.
Inspecta
alifika nyumbani kwake, ilikua ni alifajiri sana, kulikuwa kumeulia, akaingia
na gari lake, na kulisimamisha, haraka akatoka na kukimbilia ndani, akazungusha
kitasa cha mlango, mlango haukuwa umefungwa na ufunguo, akafungua na kuingia
ndani
Mwili
ukawa unamsisimuka, sio kwa hasira, sasa alihisi uwoga, alihisi hali isiyo ya
kawaida,…akawa anaomba mungu kusiwe na tatizo, akaelekea moja kwa moja
chumbani, akafungua mlango..
Kitandani
kulikuwa hakuna mtu, ila shuka, lilikuwa limetupwa chini , kuonyesha kuwa kuna mtu alikua kalala hapo, akasogea hadi pale kitandani na kukaa huku akilini akitafakari yote yaliyotokea, alijua , na alijipa moyo huo kuwa mkewe atakuwa bafuni, au
chooni,akasubiri, akaona kimia, akashindwa kuvumilia, akatoka taratibu hadi bafuni…
Macho
yake yakatua kwenye beseni al kuogea,…mkewe alikuwa kalala ndani ya maji,,
upande, kaegemea, mdomo upo wazi, macho yamemtoka….maji yamebadilika rangi, wekendu ..damu....
NB:
Hicho kipande kidogo, japokuwa nimeandika kihivyo, tuwiane radhi kwa hilo
WAZO LA LEO: Katika maisha yetu
magumu, tunahitajika kuhurumiana, na kusameheana, hasa mmoja anapokosea, kwani
kuna kukosea kwingine kwa bahati mbaya, au kumetokea kwa kuzidiwa na
mafungamano ya kimaisha,..hakuna kitu kibaya kama ufukara, ufukara unaweza
kumtuma mtu akafanya mambo mabaya sana, ibilisi hapo hachezi mbali,..Lakini
yote ni maisha cha muhimu sana ni kujitahidi kuwa na subira na kutenda mema…tukumbuke,mungu
ni mja wa wote.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment