Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, August 21, 2014

DUNIA YANGU-20
‘Unaona hapa nimetumiwa huu ujumbe na majaribio ya mtaalamu wako, wanasema wao wameshafanikiwa kupandikiza vimelea vya ukimwi na magonjwa mbali mbali kwenye mtandao...unaona huu ujumbe wao....’akasema akisogea pembeni kumpa nafasi Inspecta kusoma, Inspecta alisoma kidogo, akataka kusogea zaidi lakini jamaa akasema;

‘Mkuu jiandae, wakishindwa kukushawishi kwa hizo skendo zao, utakuwa majaribio ya hivi virusi, wameshaviingiza kwenye mtandao, nakuonea huruma mkuu, kama hutafanya watakavyo watakupandikizia hivi virusi na utakufa kifo ambacho kitaonekana ni kawaida tu....

‘Usiniulize kwa vipi, ....ninachojua ni kuwa wanakuwekea kama shoti ya umeme, na au kwenye chombo chochote utakachoshika kwenye maji, kwenye aina yoyote ya kitu kinachoweza kukusambazia hivyo virusi,..wao wana mbinu za kila namna, ila hii ya mtandao ni kubwa yake, ....wanakutumia ujumbe, na kwa vile siku hizi tunatumia sana vidole, ukijaribu kuufungua huo ujumbe inakuja kitu kama shoti ya umeme kwenye kidole....papu,...vimelea vimeshapenya mwilini.....’

‘Unaona na hapa, vingine wataviweka kwenye  vyakula, kwenye madawa, na ukumbuke huko kwenye madawa wana watu wao, watakuwa wanadhibiti wao. wenyewe...mmh,

‘Mmmh, unaona na hapa...eeh, hata haya madawa ya kurutubisha mimea, kuna vitu vyao wameweka ili kuharibu mfumo wa binadamu,...wanahisi watu weusi wanazaa sana, na watu wa rangi, unaonaeeh, kama wachina na wahindi, unaonaeeh, ...kwahiyo kwa kupitia hivyo vimelea wataharibu uzazi, nguza za kiume na kike,....

‘Unaona hapa na pia wamebuni jinsi gani binadamu mume anaweza kupadilika katika maumbile na hisia zake, mke awe kama mume na mume awe kama mke kihisia, wanataka kuleta dunia isiyo na utofauti...hahahaha, wanasema wanataka hizo haki za kila mtu kuwa sawa ziwe za kiukweli mke asiwe tofauto na mume kimaumbile wawe na maumbile yao tu, lakini....haya soma mwenyewe hapa...

‘Wanadai wao wanapigania haki za binadamu vimelea hivi ni silaha yao, wanachotaka wao eti ni kujenga usawa, dunia hii isiwe na tofauti ya mume au mke...no..no...hapana this now is too much...’akawa anaendelea kusoma....

Hii ndio dunia inaliyojengwa na huyu jamaa,...je hayo hayapo au bado... tuendelee na kisa chetu....

 ************
Inspecta alifika nyumbani kwake muda wa saa sita na kumkuta mkewe hayupo, akaingia ndani na kupumzika kwenye sofa, mara simu yake ikaita, alikuwa ni Inpecta mwenzake;

‘Vipi hali yako,...?’ akauliza Inspecta mwenzake

‘Sijambo, nipo sawa hakuna shaka.....’akasema

‘Nafahamu kuwa kweli hujambo...dawa na tiba uliyopata ni lazima utapona tu, pumzika tu.  je kuna lolote umepata hadi sasa, najaua kuumwa kwako sio bure kuna jambo ulikuwa unafukuzia..?’ akauliza inspecta mwenzake

Kauli za mwezake zikawa zinamchnganya, lakini hakutaka kumuuliza zaidi, hakutaka kuongeza msongo wa mawazo zaidi maana hapo alipo alikuwa ameshazidiwa, pale alipo alitamani kwenda kuoga na kuondoa uchafu wote uliopo mwilini na kwenye akili, lakini alijua hata aoge vipi hataweza kuondoa huo uchafu, hasa ulioganda akilini. Akamjibu Inspecta wake kifupi fupi.

‘So far, hakuna, ..ni yale yale ya mzunguko tu wa hapa na pale.....’akasema

‘Yah, nilijua tu, ...je kesho utaweza kuja kazini, maana kuna kikao kwa wakubwa huko, ulisikia eeh?’ akauliza mwenzake

‘Utaniwakilisha tu, siwezi kufika...’akasema akipiga miayo,na akaangalia saa yake, huku akijiuliza mkewe kaenda wapi, hakutaka kumpigia simu, akaona asubiri tu.

‘Sawa nimeona Sick sheet yako, ugua pole...’akasema na kukata simu, Inspecta akashikwa na mshanga maana hakuwahi kupeleke hiyo sick sheet, akakumbuka wakati aanongea na yule binti alimuelezea kitu kama hicho.

Pale alipokaa alijikuta akimuwaza sana huyo binti na hata pale alipojaribu kufikiria mambo mengine, alijikuta akitawaliwa na sura iya huyo binti, akili ikawa hautulii ni huyo binti tu, ilikuwa kama kapewa kitu kipiya kwenye ubongo ambacho hakikuwepo, uzoefu mpya ambao hajawahi kuupata, ...akasimama na kukimbilia bafuni, akaoga na kujisikia afadhali kidogo.

Mara mlango ukafunguliwa na mkewe akaingia, akiwa na mfuko wenye vifaa vya nyumbani, akasalimiana naye, na mkewe akasema;

‘Vipi kulikoni, maana nimesikia unaumwa, lakini nyumbani huonekani, ulikuwa wapi?’ akaulizwa.

‘Aaah, haya mambo yetu yaache kama yalivyo, unaweza ukaumwa nab ado ukawa kazini, na kazi zetu zilivyo, unaweza ukajikuta kwenye matatizo, ukashindwa hata kurudi nyumbani, muhimu nione nipo salama....’akasema

‘Mimi ndio maana nilishakuambia achana na hizi kazi, kwanini unang’ang’ania hizi kazi, ona mwenzako sasa ana mipango ya kuacha kazi, na kaanzisha miradi mingi tu...’akasema.

‘Mwenzangu yupo?’ akauliza.

‘Huyo unayefanya kazi naye, mwenzako mjanja anauma huku anakupiliza, mkewe anamuendesha puta, lakini kwa manufaa ya familia, umeshaona miradi yao?’ akaulizwa

‘Miradi gani hiyo?’ akaulizwa

‘Wewe endelea kulala, endelea kujituma tu ni utaifa wako uone utafikia wapi, ...’akasema

‘Huyo mke wake ulionana naye wapi?’ akauliza

‘Kanipigia simu tukaongea kwa marefu, na mara mume wake akaja kuniarifu kuwa anaumea, nikamwambia nataka kununu vifaa vya ndani maana naona kumekauka, hakuna vyukala hakuna chochote akasema atanipeleka, na ndipo akanipeleka kwenye miradi yao....mmh, wenzako wapo mbali....’akasema

‘Kwahiyo muda wote ulikuwa na huyo unaiyemuita mwenzangu?’ akauliza Inspecta kwa sauti ya wivu.

‘Hahaha, ndio waona wivu sio, umesahau kuwa wewe ulilala nje, na huko nje ulilala na nani, au nyie wanaume ndio wakuona wivu tu....’akasema

‘Sasa una maana gani kusema hivyo, kuwa kwa vile nililala nje na wewe unalipiza, au?’ akauliza

‘Mimi sijasema hivyo, na hata siku moja siwezi kufanya uchafu huo, ..ni wewe umeanza kwa kusema kauli zenye utata wa wivu....haya niambie hizo picha ulizosema utanitumia zipo wapi?’ akauliza

‘Picha gani?’ akauliza Inspecta kwa mshangao na mara mkewe akaenda kwenye kabati na kutafuta kitu, ..lakini hakukiona, akauliza kwa sauti ya ukali

‘Ile karatasi yenye ujumbe wako kuwa haupo na chini yake kulikuwa na maelezo ukasema kuna picha zako...mbona siioni, na mimi niliweka hapa, ilikuwa juu juu, na sizani huyu mfanyakazi wa ndani kaingia na kupekua huku kabatoni, hawezi kufanya hivyo ni wewe meichukua,?’ akauliza

‘Mbona mimi sikuelewi, sijaweka ujumbe wowote humu ndani na wala sijui chochote kuhusu hizo picha, naona huyo mwenzangu kakulewesha mpaka unaongea mambo ambao hayapo ...’akasema kama mdhaha, alishamjulia mkewe akikasirika ujaribu kumtania.

Inspecta kichwani akakumbuka kuwa wakati alipokuwa anaagana na yule binti , yule binti alimwambia;

‘Mpenzi kwa vile sasa tupo pamoja na umekubali kuwa sambamba na mimi kila kitu kitakuwa shwari, nitahakikisha kila aina ya fitina inaondolewa, ili mradi na wewe utimize wajibu,...hakuna kufuatana fuatana ..achana na mambo ya watu, usichunguze chunguze saaana, huu ni muda wako wa kujijenga...angalia wenzakoo wanavyoneemeka...’akasema.

‘Sawa akaitikia kwa shingo upande...’akiwa kama hayupo, alikuwepo kimwili lakini kiroho alikuwa akiwaza mbali, na kujiuliza je alichofanya ni sahihi, na kama si sahihi angelifanya nini, akawa anajijutia.....

‘Na ukumbuke mimi ni mpenzi wako, ili mambo yaende sawa, na hao jamaa waone kuwa upo kweli sambamba na wao, ni lazima niwe mke wako...unaelewa....’akaambiwa na hapo akashituka na kusema

‘Itakuwaje wewe uwe mke wangu, wakati nina mke wangu...huko sasa mnakwenda mbali...’akasema na kusimama kuonyesha kuwa anataka kuondoka.

‘Mmm una mke wako tayari, eeh, naona mke wako ni kikwazo, au tufanye hivi, wao wamuondoe huyo mke wako kabisa, ndivyo unavyotaka, au...., ?’ akauliza na Inspecta akamuangalia huyo binti kwa mshangao

‘Unasema nini?’ akauliza

‘Hebu niambie wewe unataka nini...ungelijua haya ni kwa faida yako, usingelikataa kabisa muhimu ni kufanya wanavyotaka wao, toa ushirikiano...unajua nyie watu mnajifanya wachapa kazi, lakini moyoni mnaumia....’akasema

‘Sisi tunatimiza wajibu wetu kwasababu tuna kiapo cha uaminifu,pia tunamuogopa mungu, haya yanayoendelea hapa ni ushetani....’akasema

‘Hahaha eti ni ushetani, mbona ulikuwa unafurahia, hebu nambie hayo tuliyofanya wanafanya akina nani, wewe si mcha mungu au sivyo mnavyojiita kinafiki, kuwa nyie ni wacha mungu,...’akasema kwa dharau

‘Hivi kweli mcha mungu anaweza kutembea na mwanamke ambaye sio mke wake, hapa tumefanya nini, bado unajiita mcha mungu hahaha...hahaha, kwahiyo ili kwelu uwepo ucha mungu wako, kuanzia sasa mimi ni nani kwako..?’ akamuuliza akimkazia macho, na Inspecta akageuka kutaka kuondoka na yule bint akamsogelea na kumzuia akasimama mbele yake, kwa kujiamini.

‘Kwanini unanifanyia hivyo, hivi kama wewe ungelikuwa mke wangu akaja mwanamke mwingine akafanya kama unavyonifanyia ungelijisikiaje?’ akauliza

‘Ni mimi nimekufanyia au wewe ndiye uliyenifanyia, ni nani alitoka nyumbani kwake akamfuata mwenzake,..ushahidi upo wazi, kila ulipopita umeacha ushahidi, au unataka nikuonyeshe, kila kitu kipo wazi, huwezi kumdanganya yoyote, ..kwa kauli yako mwenyewe umetamka unanitaka..nikuonyeshe ushahidi....’akasema akiangalia zile CD mezani...

‘Ok, niambie mnataka nini, au umetumwa kufanya hivyo kwa madhumuni gani?’ akauliza na yule binti akashika kichwa na kugeuka, akasema;

‘Sijatumwa, ..ondoa huo usemi, nimekuuliza ni nani aliyemfuata mwenzake,...kama ningelitumwa ningelikuja kwako,...umekuja hapa kwa hiari yako mwenyewe kunitaka, kwahiyo hiyo kauli yako sio kweli, na huenda umebadili mawazo, kinafiki, kwa vile mke wako amekuja..nimekuuliza je mke wako ni kikwazo, kama ni kikwazo niambie , wenyewe watajua jinsi gani ya kufanya, ila...usije ukalalamika....’akasema na kugeuka kumuangalia Inspecta

‘Acheni familia yangu, kama mnataka vita na mimi ingilieni familia yangu, kama mna shida na mimi nifanyeni mtakavyo, ....mke wangu anawahusu nini, kwanini kila mara unamtaja mke wangu....?’ akauliza

‘Hahaha, mke wako, ukumbuke hata mimi ni mchumba wa mtu, au nilikuwa sijakuambia, lakini wewe ukaanza kunitafuta, au hujanitafuta...sema mwenyewe , hujanitafuta, ...hapo ulipo mwenyewe akili yote ipo kwangu, ..umekipata kile ambacho hujawahi kukipata kwa mke-,o ni kweli si kweli?’ akauliza akimsogelea na kuanza kumshiak shika.

‘Tafadhali narudia tena kama unataka tuelewane, mke wangu asihusike kwa lolote lile, acheni kumsumbua, vinginevyo, sitajali cha kashifa au nini, nitachukua hatua mikononi mwangu, nitawatafuta chini hadi juu, na nawahakikishia nitawapata mmoja mmoja, na mnajua nini kitakachofuata...’akasema akikunja uso wa hasira hadi yule binti akaogopa, akarudi nyuma na kusema

‘Usinitishe,..hahaha, tatizo ni kuwa nyie watu mna hasira, mna miguvu, lakini hamtumii akili, ...sisi tunatumia akili na zana za kisasa, kwahiyo unajisumbua,....cha muhimu ni mapenzi tu, ...mimi na wewe,..huku ukiwa mbali na mambo ya watu,ni hilo mpenzi, usijali, ....mimi nitatimiza wajibu wangu, nitahakikisha mkeo haguswi, ila ......na wewe utimize wajibu, kila nikikutaka uwepo,....sawa?’ akauliza
‘Huwezi kuniambia hivyo, maana ujue kuwa mke wangu yupo, na yeye anastahiki haki zake, ...huwezi kuniambia nije kwako kwa muda utakao, ....hilo ulifahamu....’akasema

‘Nalijua hilo sana, na nitahakikisha nachukua tahadhari,...kwa vile nakupenda, amini hilo, sijui kwanini nimetokea kukupenda hivyo, .....i love you...’akasema na kumsogelea kumbusu...Inspecta akajaribu kumkwepa, lakini akawa keshawahiwa, kilichofuata hapo, kilimfanya aishiwe na nguvu.

‘Unaona eeh, mkeo anaweza kufanya hivyo....hahaha hiyo ni salamu tu, na mengine yapo pale kwenye CD, utachukua nakala yako, utaangalia ukiwa peke yako ....hakikisha ukiwa peke yako, sisi tutahakikisha hakuna anayeipata hiyo kazi, ni mimi na wewe tu...nimehakikisha hakuna udurufu, ni live...utaona mwenyewe, ..hahaha ni ya hali juu, nimeipenda sijawahi ....mmmh, baby, usiondoke....’akasema pale alipoona Inspecta anaondoka.

‘Nakuapia, ...i will finish this myself, ..mtaona....’akasema

‘Mhh, baby, ukumbuke mimi ni mpenzi wako, hilo likukakae kichwani vinginevyo.. hiyo CD ikifika kwa mke, nakuapia, atajiua...si unampenda sana mkeo, sasa chunga hicho kitu asikione, achilia mbali baba mkwe au kazini kwako...kumejaa raha za dunia humo, hahaha, mke hawezi, ooh, samahani nafuta usemi, ulishasema tusimuhusishe mkeo, ..’akaweka mkono kuziba mdomo.

Inspecta alijikuta akitetemeka kwa hasira, akasogea pale kwenye zile CD, akaziweka sakafuni na kuzikanyaga kwa hasira kuhakikisha zimepasuka vipande vipande....’halafu akageuka kumuangalia yule binti, akuwa kabadilika sura kwa hasira, na yule binti akatabsamu, kwa dharau na kuanza kucheka,....

‘Unaona eeh, hivyo ndivyo nataka,yaani mwanaume akiwa hivyo, nahisi mwili mzima unasisimuka..mmh...mpenzi usijali haya yote yatakwisha, kuna watu walikuwa hivyo, huwezi amini, sasa wana majumba yao, miradi yao, wanakuja kunishukuru, wananitaka tena, wengine wapo tayari kuwaacha wake zao,...lakini nishamaliza kazi nao, ..na sasa nakupenda wewe tu, sitaki mwingine.....’akasema

‘Narudia tena, haya hayataisha hivi hivi, na kama mnataka vita visivyo isha, gueni familia yangu, ..mtaona kama mimi ni nani, msione nipo kimia, msione nafanya hivi kama mjinga, lakini hamnijui...waambie wenzako hapa wamechozea moto...hili jina sio bure, mtaona...’akasema akianza kuondoka na yule binti akaanza kucheke kwa dharau akisema...

‘Hahaha, unalo hilo.....hiyo ni onja onja tu, kazi bado kabisa...nisalimie mke mwenzangu, kwa nia njema, na ni bora ukifika jaribu kutabasamu maana ulivyobadilika na hizo hasira unatisha, tupo pamoja well come to our world bby.


WAZO LEO: Fitina ni mbaya sana, mfitinishaji anakuwa ni wakala wa shetani, ambaye kazi yake kubwa ni kufarakanisha kati ya ndugu na ndugu yake mke na mumewe, jamii kwa jamii. Dunia sasa hivi imegubikwa na fitina, kinachoendelea sasa hivi ni propaganda za kufitinisha watu, jamii , nchi zifarakane, zipigane, ziuane, kwa manufaa ya matajiri...


Hao ni mawakala wa mashetani wanaofanya kazi hiyo, hawa ni wachawi wa kisasa, na kazi ya wachawi ndiyo hiyo ya kumuwakilisha shetani. Jamani tutafakari tuangalie mambo kihekima zaidi, tujaribu kuwa makini kwa kila tukio linalotokea, kwani hicho kinachoendelea duniani hivi sasa, sivyo kilivyo, bali ni mipango ya ubeberu na ukoloni mamboleo, mwenye macho aone, mwenye masikio asikie na mwenye akili atafakari.

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

Lakini kumbuka pia mengi Mungu huangalia na kulipa haha hapa duniani. Kazi nzuri tupo pamoja.