Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, August 20, 2014

DUNIA YANGU-19Inspecta Moto, akashika kitasa na kutaka kufungua, mara akasikia kama mtu anakuja kwenye muelekeo wa varanda, akageuka kuangalia, akaona ni mlinzi alikuwa kwenye mizunguko yake, na yule mlinzi alipomuona akasema;

‘Oh bosi, nilikuwa nafanya doria, mambo yanakwendaje?’ akauliza

‘Hamna shida, ...’akasema Inspecta

‘Samahani nikuuliza, nahisi nimewahi kukuona mahali...’akasema

‘Yawezekana maana dunia siku hzi ni kijiji, unafikiri uliwahi kuniona wapi?’ akauliza Inspecta

‘Sikumbuki, lakini sura yako sio ngeni kwangu, wewe haupo kweney safu ya wakubwa wa polisi?’ akauliza

‘Mhh, usijali, ...’akasema Inspecta na kuzungusha kitasa, na mlango ukafunguka, akamuacha yule mlinzi akibakia kuwaza, hakutaka kumueleza lolote, na mawazo yake sasa yakawa ni nani hao wanaongea huko ndani.
Kilikuwa chumba kikuwa kama studio ya picha, na komputa na dhana za kisasa zilionekana mezani, na pembeni kabisa akamuona mtu kakaa, akiwa kaangalia kwenye runinga iliyokuwa ikionyesha picha ya video, na jamaa huyo alikuwa katulia kimiya hakugeuka.

Inspecta akatulia akichelea kusema neno maana aliingia kwenye ofisi ya mtu bila kupiga hodi, akajiuliza arudi, au amuongeleshe huyo mtu, na akaamua ageuke odnoke zaie lakini kabla hajachukua hatua huyo jamaa akasema;

‘Usipoteze muda, kwani muda ni mali, sogea hapa nikuonyeshe kitu....’huyo jamaa akasema kwa sauti ya kilevi, na inspecta akajiuliza huyu mtu anataka kunionyesha nini, na kwanini kalewa mapema hii.

Akasogea hadi pale alipokaa na macho yake yakawa yanaangalia kwenye runinga, na alichokiona alitamani kuvunja vunja kiyoo kile lakini akasubiri, na kusema;

‘Hiyo ndio kazi yenu sio, kwani wewe ni nani?’ akauliza akitafuta njia ya kuona sura ya huyo mtu,

‘Usifikiri mimi napenda kuyafanya haya, na nijuavyo hukutakiwa kuona, au kuniona, mimi sitakiwi kuonekana na watu wasiostahiki, na sijui kwanini umeingia hapa, ila nimekuamini... na nahisi unaweza kunisaidia jambo, je unanikumbuka mimi?’ akauliza na kugeuka, aligeuza kiti ambacho kilikuwa kinazunguka.

‘Mimi siwezi kuwajua watu kama nyie, manachokfanya kitawatokea puani...’akasema Inspecta .

‘Nakumbuka kama uliongea na ndugu yangu akakuambia nimepotea kimaajabu, na y a kuwa wamapeleka taarifa polisi lakini hawajapata msaada wowote...’akasema

‘Ni nani kakuambia maneno hayo?’ akauliza inspecta kwa mshangao

‘Tatizo lenu ni kuwa hamtaki kujifunza, hii dunia kuna watu wameiweka mkononi, kila kinachotokea, wanakijua kama kima masilahi kwao,....hebu angalia angalia hapa, toka umetoka nyumbani kwako hadi umefika hapa, wenzako wanakuona...’akasema na kumuonyeshea alivyotoka nyumbani hadi akafika hapo

‘Kwanini mnanifuatilia?’ akauliza

‘Kwasababu wewe ni tishio, wenzako wote wamekwa mkononi, lakini wewe unajifanya hamnazo, lakini sasa huna ujanja , nakusihi, ni bora ufanye watakavyo vinginevyo, ...’akatulia na sasa akawa anaonyesha yale yaliyotokea kati yake na huyo msichana, na inspecta akataka kwenda kuzima ile kopmuta jamaa akazunguka na kitu kama ngao kikaziba na Inspecta akajikuta akisukumwa na hiyo ngao hadi akaanguka chini.

‘Usithubutu kufanya hivyo, watakuua hao jamaa,...mimi nakusaidia kukupa taarifa ili uweze kujipanga, ...haina faida kwangu, ni kwa ajili yako tu...’akasema

‘Kwani wewe ni nani?’ akauliza Inspecta

‘Kama hujanifahamu haina haja kukuambia, ila nataka usije kusema uliniona, ni muhimu sana, mimi nakusaidia kukupa taarifa na wewe unisaidie kunilinda,.....’akasema

‘Kwa vipi, mimi ni kulinde wakati wewe inaonyesha una ulinzi wa kutosha...’akasema

‘Maana yangu ni hii, kwa hali niliyo nayo sitaki kuonekana na ndugu zangu, kama unavyoniona madawa yameniharibu nipo kama sipo, na hapa nikikosa madawa nakuwa kama goigio sijiwezi, hawa watu wameniharibia maisha yangu,....’akasema

‘Sasa kwanini ukakubali kujiunga na kufanya hayo wanayotaka wao, huoni umejiingiza wewe mwenyewe, kwanini usitoe taarifa polisi...?’ kaulizwa

‘Swali hilo utakuja kupaat jibu lako pindi...hakuna aliyetaka kujiunga na hawa jamaa ila wao wakitaka ujiunge na wao utajiunga tu, na mimi walichofanya ni kunidunga haya madawa,....nikawa kama zezeta, na sasa siwezi kuishi bila haya madawa...’akasema

‘Ina maana walikulazimisha..?’ akaulizwa

‘Nahisi ndugu yangu aliwahi kukuelezea jinsi ilivyotokea, ...au?’ akauliza na Inspecta akamuangalia tena kwa makini , akauliza;

‘Ina maana wewe ndiye.....ooh, nimekukumbuka, nimekumbuka sura yako, kweli alinionyesha picha yako, japokuwa nakuona kama umebadilika sana....’akasema Inspecta akimuangalia kwa makini.

‘Ndio lengo lao hilo, nibadilike kabisa hata nikitoka hapa, biwe sio yule waliyekuwa wakimfahamu na hapo wameshaniosha kichwa na kuchukua kila kilichokuwa kichwani mwangu, wanataka hata ndugu zangu wakiniona wasinitambue,...wanadai watanisaidia baadaye nirejee kwenye hali yangu maana wana huyo mtaalamu wao, dakitari bingwa....’akasema

‘Ni nani huyo...?’ akauliza

‘Simjui...’akasema

‘Kwahiyo mimi nitakusaidiaje ...?’ akauliza.

‘Cha kunisaidia kwa hivi sasa hakuna,hakuna...hakuna...hakuna anayeweza kunisaidia mpaka wenyewe wapende...ninachokuomba kama unajijali, kubali hayo watakayokuambia...kubali ndugu yangu, yasije kukupata yaliyonipata mimi,...’akatulia akikunja uso kama akihisi maumivu

‘Hebu nikuulize tangu nipotee kumefanyika, hata ndugu wameshakata tamaa, huku naumia, sio kwamba nimekaa tu,..unaona hapo, ina maana utatekwa, utafanya lolote baya, wenzako watajaribu kukutafuta au kukusaidia siku ya kwanza ya pili ya taatu wanaanza kukusahau....,mimi nilijaribu kuwa mbishi , walichonifanyia ndio hivi, najuta kwanini sikukubali nikaenda nao taratibu... kama una mipango yako ni bora ukaisimamisha kwa muda hadi wakati muafaka, najua kabisa dhuluma haidumu, ipo siku haki itakuja kuishinda dhuluma...’akatulia kidogo.

‘Hebu fikiri hawa watu walivyo na mtandao mkubwa, walikuwa wakikuchunguza nyendo zako kila siku, wanakufuatilia hatua ka hatua, wanakuona, wanaweka kumbukumbu zako, unaona huo utaalamu, sasa utashindana na watu hawa, wanaojua hata kile unachokula, ukiingia chooni wanakuona, hebu fikiria hapo...kuwa makini...’akasema

‘Lakini kwanini tushirikiane , wewe umeliona hili na ni kweli ni tatizo kubwa, lakini tukisaidiana mimi na wewe,tutawashinda, kwa mfano wewe hapo unao ushahidi wa kutosha au sio,...hayo mambo unayofanya hapo yote ni ushahidi wa kuwakamata hao wote wanashiriki kufanya uchafu huu...’akasema Inspecta.

‘Nakuomba tena sana, na nakutahdharisha, hili jambo kwa hivi sasa uliache kama lilivyo, hawa watu wamejipanga, kila kona wana watu wao, na watu walionao sio watu wadogo, ndio wanashikilia maidara yote nyeti, hebu niambie kwa hali hiyo utaenda wapi,...ok, tusema umeupta huo ushahidi halafu ....’akatulia kwa makini kama anafikiri jambo

‘Hatua ya kwanza najua utakwenda kwa wakubwa zako, au ...wapi mahakamani moja kwa moja, huwezi kwenda mahakamani moja kwa moja kuna taratibu zake, sasa hizo ngazi za kupanda hadi kufikia mahakamani kuna watu wao katikati, ushahidi unageuzwa, na itakuwa wewe unashitakiwa....hayo ynafanyika itaalamu kabisa, na propaganda nyingi tu...wangapiw anasota rumande kwasababu ya propaganda...

‘Sikiliza ndugu yangu, wewe kwa hivi sasa kula bata, kubali, fanya watakalo, kama utapata mwanya, na uhakika, basi fanya hilo unalokusudia, lakini natumai siku ukionja asali mwenyewe utachonga mzinga, wangapi nimewaona..hahaha...mimi nakuambia ukweli ni mzalendo haswa,..lakini mmmh, nimesalimu amri, japokuwa kiukweli wamefanya jitihada hadi za kunifanya hivi, ...sasa hivi aaah, nimechoka....’akasema na ujumbe ukaingia kwenye mitandao yake.

‘Jiandae ...mtu wako anakuja....’akasema

‘Angalizo, ni kuwa wenzako walishafikiria kila hatu, kuwa kwa mfano wamekufanyia hivyo, wana uchafu wako mwingi tu, kwanza ni kukuharibia jina, hilo linafanyika kitaalmu kwa propaganda ya hali ya juu, pili wanaharibu ajira yako, tatu wanaharibu afya yako, hapo utafanya nini...na nikuulize unajua ni nani na yupo kwenye huo mtandao...’akawa kama anauliza huku akifanya vitu kwenye komputa baada ya kupokea huo ujumbe.

‘Nikuembie ukweli hawa watu ni wajanja sana,...yeye alifanya uchunguzi wa kina, akagundua kuwa viongozi wengi walijisahau wakawa wanakula wanastarehe, wanafanya ufisadi...unaona hili, kumbe jamaa anawanakili, akahifadhi shutuma zao...na pia wengine wameingizwa kimtego tu kama mimi, na wengine wakategewa skendo...unaona alivyoijenga dunia yake huyu mtu....’akasema

‘Dunia yake..?’ akauliza Inspecta akikumbua kuona hayo maandishi

‘Sikiliza mtu wangu,sitaki kusema mengi kwa sasa, ...naona mtu wako anakaribia, sio vyema akakukuta humu,....’akasema.

‘Mimi bado nakushauri, hujachelewa, shirikiana na mimi, tulimalize hili tatizo, ili haki ipatikane, hawa watu waondolewe, sheria ichukue mkondo wake....’akasema Inspecta

‘Ka hali ilivyo, na ndivyo ilivyo,haki dunia hii sasa haipo, kila mtu anatafuta kwa juhudi zake, ubinafsi, ....ufisadi..ndio asili ya mwanadamu au sio ndio maana wewe waitwa jina hili, wewe upo hivi, unaona, hakuna jina moja kwa wote, hata vidole unavionaje....eeh, sasa kama hakuna haki,ni ubinafsi kwa kwenda mbele, dhuluma inakuwa ni ujanja, ndio shule...unaonaeeh,..unafikiri nini kitaendelea

‘Angali hali ilivyo, wengine sasa hivi wananeemeka kwa visingizio mbali mbali, wengine wanadhulumiwa, mifano ipo hai ndugu yangu, hakuna haki hapa duniani, hata hao viongozi wa dini, wanatumia dini kujitajirisha tu,...kama si hivyo, ni kwanini kiongozi wa dini awe na majumba ya kifahari, magari, wakati waumini wake ni masikini...hebu fungua akili hapo...dunia hii hakuna haki..kila mtu akipata mwanya na yeye hata bila kupenda atafanya mabaya, na yanaweza yakawa mabaya zaidi ya hayo ya waliotangulia, nenda ndugu yangu...’akatulia

‘Sasa nitakupataje..?’ akauliza Inspecta, na huyo jamaa akawa anafanya kitu kwenye mtandao, akasema bila kujali swali la Inspecta

‘Hebu niambie ni nani hataki kuendelea kuwa madarakani, kuingiza kipato, kuendelea kuneemeka,eeh, wewe si una watoto, je wewe hutaki watoto wako wasome nje, au kwenye shule nzuri, angalia hao watoto wanaosifika kuwa wamefaulu, wanatoka wapi,...ni kwenye shule za bei mbaya, sasa ni nani hapendi watoto wake wasome huko,..kila mtu anapenda au sio, ni kwanini, ni ili baadaye wawe kama yule au yule waweze kuendeleza mrija wa neema.....hahaha amuka ndugu yangu

‘Hakuna aliyejipangia kuwa apate zaidi zaidi ya mwingine watu wote wanayi haki ya kupata asu sio, sasa kwanini wengine wapate haki hiyo kuliko wengine,...elimu mpo sawa, kazini unafanya zaidi yao, unalima, unafanya biashara, lakini wengine wanakuwa juu, juu zaidi, ukiangalia kiukweli hawajapitia njia ya haki,...hao ndio wanaonekana watukufu,...unaona hapo,.. hicho ndicho chanzo cha watu kama hawa kuibuka...’akasema na Inspecta akakunja uso akiwaza.

‘Makundi mabaya yanatokana na kukithiri kwa dhuluma,haki ikipotea, ni lazima watu wengine watabuni mbinu, hata zikiwa chafu, lakini na wao wanaona ndio haki yao...bila hivyo, usemi wa aliyenacho atapata zaidi na atapata zaidi kutoka wapi, ni kutoka kwenye kile chako kidogo ulicho nacho...unafikiri kwa nini wanaunadi huo usemi, na je kweli huo usemi ulikuwa na maana hiyo, ...sio kweli, wanacheza na maandiko na kujenga propaganda wapendavyo wao....natumai imenielewa, kama hujanielewa, subiri watakufundisha wenyewe....’akasema, akionyesha wasiwasi, nahisi alishahisi jambo.

‘Unaona hapa, mtaalamu wao ameshafanikiwa kupandikiza vimelea vya ukimwi na magonjwa mbali mbali kwenye mtandao...wamenitumia niweke tayari kwa majaribio, sasa sijui wanataka kujaribia kwako.....hahaha..hawa watu balaa....’akawa kama anasoma jambo kwenye komuta

‘No..no, ...mkuu jiandae, wakishindwa kukushawishi kwa hizo skendo zao, utakuwa majaribio ya hivi virusi, wameshaviingiza kwenye mtandao, nakuonea huruma mkuu, kama hutafanya watakavyo watakupandikizia hivi virusi na utakufa kifo ambacho kitaonekana ni kawaida tu....’akasema

‘Kwa vipi, kwenye mtandao..?’ akauliza Inspecta.

‘Usiniulize kwa vipi, ....ninachojua ni kuwa wanakuwekea kama shoti ya umeme, na au kwenye chombo chochote utakachoshika kwenye maji, kwenye aina yoyote ya kitu kinachoweza kukusambazia hivyo virusi,..wao wana mbinu za kila namna, ila hii ya mtandao ni kubwa yake, ....’akatulia akawa anasoma maelezo.

‘Unaona na hapa, vyakula, madawa, watakuwa wanadhibiti wao....mmh, unaona na hapa...eeh, hata haya mavukula ya kupandikiza, mime ya kupandikiza, yanawekwa vitu, vya wenda kuharibu mfumo wa binadamu,...wanahisi watu weusi wanazaa sana, na watu wa rangi, unaonaeeh, na wamebuni jinsi gani binadamu mume anaweza kupata vimelea, awe kama mke, wanachotaka wao eti ni kujenga usawa, dunia hii isiwe na tofauti ya mume au mke...no..no...hapana this now is too much...’akawa anaendelea kusoma.

Inspecta akasogelea akitaka kusoma, lakini jamaa akasogeza pembeni na kusema,;

‘Wao..wenyewe watakuonyesha mfano halisi, mkuu, kubali tu,...yaishe, hivi wewe kwenu una akili zako utakataa kufanya watakavyo ili upate sifa tu, shujaa, sijui nani,..huku unakufa taratibu kwa magonjwa yasiyotibika..unajua naanza kuamini kuwa haya magonjwa mabaya chanzo chake ni watu kama hawa, nikuambie ukweli, hawa watu ni mashetani...i don’t know wanataka nini katika hii dunia, nahisi wanahitaji dunia yao....’akasema

‘Hebu nikuulize hao watu ni akina nani...?’ akauliza Inspecta sasa akianza kuhisi hatari inayomkabili.

‘Kwa hivi sasa mimi sijui, nimeshikwa, nimefungwa na nipo hivi kama nilivyo, kazi yangu ni kuambiwa fanya hiki, fanya hiki,nikikataa napata adhabu isiyovumilika....siwezi kuilezea, lakini wanajua kuumiza, sasa mimi nimeamua kufanya watakavyo, kwanza nitakosa nini, kama wanaostahiki kunisaidia wameshindwa, mimi nifanye nini, nifa wanililie, kama shujaa, hahaha, eti alikuwa mtu mzuri, shujaa, hakuna kitu hapo wewe umeshakuwa mzoga, huna maana tena....’akasema

Inspecta akawa hajakata tamaa akasema;

‘Lakini kwa vile wewe upo kwenye huo mtandao inamaana utakuwa unawafahamu wote au sio, na yote wanayofanya unayo kwenye kumbukumbu zako, huoni ndio wakati muafaka wa kujitoa , mimi nitakusaidia, tulimalize hili tatizo,...ukumbuke familia yako wanakutafuta...nilitaka kujua kuhusu familia yako ....’akasema Inspecta na kabla hajamaliza huyo jamaa akageuka na kumuangalia akasema

‘Jamaa wajanja kweli, mimi ni mtaalamu wa mitandao, naweza kubuni namba yako ya siri kwa ujanja ujanja, lakini hawa watu ni zaidi,....nashindwa kujua ni nani anawasaidia,..wameniwekea mipaka ambayo siwezi kuona zaidi...wamenificha mambo yao mengi, lakini nitawashika,....hilo naahidi, ila sijui lini na kwa vipi....unajua, nimejaribu kwa uwezo wangu lakini sijaweza kuwafahamu ni nani wahusika wote...’akasema

‘Ama kuhusu familia yangu, tafadhali sana, usije kunitaja kuwa umeniona, mimi nimeshakufa, sitaki kabisa familia yangu waje kuniona katika hii hali, ...’akasema na kushika kichwa kama anawaza jambo, halafu akasema;

‘Wakati mwingine akili ikinijia naumia sana nikijiona hivi nilivyo, nilikuwa mtu wa maana nina kazi yangu, lakini utaalamu wangu , kipaji changu ndio kimenipoza, sijui kama nitaweza kurudi hivyo, ,....unaona walichonifanya madawa yakiisha mwilinini nahisi vibaya, ....unaona oooh, imeanza taabu, ooh, balaa, dawa yangu ipo wapi....’akaanza kama kujikuna, na hapo hapo akachukua kitu kama kiko na kuvuta puani, akatulia kimiya kama kalala

Inspecta alipoona hivyo, akataka kusogea pale kwenye hivyo vifaa vilivyopo mbele yake, ili ajaribu kuona kama anaweza kupata chochote, lakini mara akasikia sauti nje ya gari lipikipiga honi, akajua  hao jamaa wameshaingia, na sasa anatakiwa kujiandaa kupambana nao, akatoka nje ya kile chumba kwa haraka.


WAZO LA LEO : Kila siku maisha yanazidi kuwa magumu, na jinsi hali inavyozidi kuwa mbaya ndivyo watu wanavyozidi kubuni njia mbali mbali za kupata kipato, na mara nyingi kipato kikubwa hupatikana kwenye njia mbaya. Tusipoangalia yale yaliyosemwa kwenye vitabu vitakatifu sisi tutafanya mara dufu yake, sisi tunafanya mabaya zaidi yao, na yote haya ni sababu ya kutojali haki za watu, dhuluma imekuwa ndio rasimali. Tujirudi, tuangalia haki inatendeka, tuache dhuluma...
Ni mimi: emu-three

No comments :