Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, August 18, 2014

DUNIA YANGU-18Inspekta Majuto aliangalia ule ujumbe toka kwa mkewe wa msisitizo kuhusu ahadi aliyotoa kwenye kikao cha harusi, ...na tarehe kama hizo hakujua wapi azipate hizo pesa,na mkewe kasisitiza afanye akope wapi lakini hizo pesa zitumwe haraka iwezekanavyo...

Mkewe leo ni siku ya tatu hajaonekana nyumbani, na kila anapompigia simu mkewe anadai yupo kwenye vikao vya kifamilia atarudi kihakikisha mambo yamekwenda sawa kwani yeye kachaguliwa kama msimamizi wa shughuli yote na shughuli ya mdogo wake, kwahiyo hawezi kuondoka haraka,...

Lakini akaongezea kusema;

Hata hivyo  pia kesho kuna kingine,  kikao cha harusi kwa mjomba, hii ni shughuli tofauti na hii ninayosimamia mimi, hiyo ni shughuli ya mjomba mkwe wako, haswaah, hapo kwa vile na mimi nina shughuli, nimeahidi kutoa laki saba, kwahiyo zitafute haraka unitumie....’akasema mke wake kwa sauti ya amri.

‘Laki saba, kirahisi hivyo,kwanini ukaahidi pesa nyingi kiasi hicho..?’ akauliza Inspecta

‘Kwani hizo pesa nyingi, wewe ni Inspecta, mtu mkubwa, ulitaka niahidi nini, wanzako wameahidi milioni,mimi nimeahidi hizo tu kwa vile wewe haupo, ukumbuke sisi ni ndugu wa karibu, wewe ni mkwe wao, kwanini niahidi pesa ndogo, nitumie hizo pesa haraka iwezekanavyo, kama hutaki  kuabikia, uanjua zangu....’akaambiwa

‘Mke wangu mambo yapo mengi kwenye familia hutaweza kuyashika yote, mengine yafumbie macho, unajua mwenyewe tarahe kama hizi mshahara bado ni tarehe mbaya , mtu unakuwa umeshatumia mshahara wote, ukumbuke tunahitajika pesa kwa ajili ya ada za watoto, elimu kwa watoto ni muhimu sana, kuna mambo mengi ya muhimu kama tutakimbilia kwenye mambo hayo hatutajijenga...’akalalamika mumewe.

‘Kwanini unaongea sana, hayo yapo na haya yapo vile vile, kwani hili nalo unaona sio la muhimu eeh, kwa vile sio ndugu zako eeh, mimi sipendi maneno mengi, nimeshaahidi hivyo, nimefanya hivyo kwa ajili yako ili uonekanae mkwe anayejali, sasa kama unaona mimi nimefanya makosa, niambie nikafute hiyo ahadi yangu, na nitawaambia ni wewe umekataa,....’akasema na kukata simu.

Inspecta akaiangalia ile karatasi iliyopo mezani yake inayotoka shule anaposoma mtoto wao, waliamua kumpeleka shule ya kimataifa ili mtoto wao awe kwenye nafasi nzuri huko mbele, na mlolongo wa ada haupungi millionimbili na nusu kwa mwaka na anatakiuwa kilipia kianzia nusu ya gharama, bado vifaa....

Akasimama na kushika kichwa, .....

Wakati anatafakari hayo,mara ujumbe wa maneno ukaingia, Inspecta, akaufungua na kuanza kuusoma, uliokuwa ujumbe kutoka kwa mdogo wa mke wake ambaye anasoma chuo na akakumbuka kuwa alimuahidi kumsaidia baadhi ya malipo, alikuwa hakutaja kiasi, alimwambia amtumie gharama aone na yeye atachangia kiasi gani na mkewe akasema;

‘Sio kuchanga huyu ni mtu wetu, tumsaidia, ujue ukikwama huyu ndiye atabeba dhamana ya watoto, mjomba wa watoto wako ni sawa na mimi mama yao, akausoma huo ujumbe ulisema;

‘Shemeji kama ulivyoahidi kwa dada, mimi nadaiwa milioni na nusu, na dada ksema wewe utachangua angalau nusu ya gharama, au laki saba kwa mambo mbali mbali, pia nahitaji lako tatu kununulia ile simu niliyokuambia...’ujumbe ukakatika na baadaye ukaingia mwingine kutoka kwake huyo shemeji yake.

‘Simu hiyo ni muhimu sana shemeji, si mwenyewe unafahamu mambo ya kisasa, inasaidia sana kupata mtandao kwa ajili ya masomo yangu, natumai utanitumia shemeji yangu nawategemea sana nyie mzee, alishanikatalia hii kozi na hataki kunisaidia kwa lolote lile....’akaiweka simu chini na hakutamani kusoma zaidi

Hata kabla hajatulia akapiga simu mdogo wa kike wa mke wake, ni shemeji yake na wamezoeana sana kutaniana mpaka mke wake akafikia kuchukia, hakutaka kumuangusha shemeji yake huyu, naye akaja na ambo yake mengi, akashindwa hata kusikiliza,...

‘Sawa shemeji yangu ngoja nijipange mambo yapo mengi kweli...’akasema
‘Shemeji ujipange vipi wakati dada kasema siku hizi huna shida ya pesa, kuna sehemu ukihitaji pesa unapewa tu, nitashindwa kukuamini tena shemeji yangu,..unakumbuka ile siri yaetu nitamwambia dada halafu utaona chungu yake....’akasena

‘Ok, umeanza tena, hayo situlishayamaliza, ....na wewe bwana, usifanye hivyo,..ok, nitakupigia nikiwa tayari sasa hivi nipo kwenye kikao....’akakata simu akihisi mwili ukimtetemeka, hakutaka hata kufikiri, akakuna kichwa na kutaka kumpigia simu tena huyo shemeji yake, lakini akaona aache tu;

‘Hawezi kusema, ....’akajipa moyo, huku akikumbuka siku alipofanya hayo aliloyafanya na shemeji yake, na akawa anamsihi sije kusema kwa dada yake na hapo ikawa kila anachotaka shemeji yake huyo ni lazima ampe kwa kila hali.....

‘Hivi hawa watu, mbona baba yao ana uwezo, mbona wananiandama mimi tu, hili sasa ni janga, wadogo zangu wenyewe nimewatolea nje kuwa sina pesa, wanahangaika kupata ada za masomo, wapo nyumbani, wazee wangu wanahitaji matumizi, sasa haya yanayokuja kila siku ni mzigo kwangu sijui kama nitauweza, hii sasa ni kero, lakini nitafanya nini mimi....’akasema na mara mke wake akapia simu akaipokea haraka

‘Gari limegongwa, shemeji yako alichukua bila idhini yangu kaingia barabarani akagongwa, halitamaniki.....’akasema mkewe

‘Eti nini.....?’ akauliza kwa hasira na mara simu ya bosi yake ikaita kwenye simu nyingine, ikabidi akate simu ya mkewe, na kuanza kumsikiliza bosi wake;

‘Kuna kikao cha dharura ufika makao makuu haraka..’siku haikuendelea ana anajua bosi wake wa kikazi alivyo, hii inaashiria kuna tatizo, akashika kichwa na kabla hajafikiri sana  akakumbuka, jambo, na hapoa kachukua simu yake ya namba maalumu, akaipiga;

‘Bosi bosi, nakumbuka uliniambia una ujumbe maalumu kwangu, ulisema leo  au kesho?’ akauliza

‘Leo, kesho sio mbaya, tumeshakamilisha sehemu yake ambayo ni muhimu sana, iliyobakia ni ya kwako, ni kazi ndogo ndogo tu....’akaambiwa

‘Kazi gani bosi na wewe una wafanyakazi kibao, mimi nitafanya nini kwako...?’ akauliza akihisi kuna jambo hapo, na mara kwa mara akipokea simu kwa huyo mtu anahisi mwili ukiishiwa nguvu, lakini safari hii yeye ndiye kampigia simu

‘Nataka tuonane kwenye simu kuna majungu tunataka kuyatengeneza....’akaambiwa

‘Nitakuja lakini nahitaji mkopo kidogo wa milioni kama tatu, nne hivi...kama yawezekana.’akasema

‘Mimi nitakupa tano kabisa, usijali, muhimu ufanya kazi yangu....’akaambiwa

‘Umesema milioni tano eeh?’ akauliza kwa mshangao

‘Sasa hivi nakutumia kwenye simu, ....’akaambiwa na haikupita muda akapokea ujumbe kuwa kwenye akaunti yake kaingiziwa shilingi milioni  tano na lakini tano mbele....akatabasamu na kuchekelea, akasema

‘Mambo sio ndio hayo, sasa nataka nini tena, japokuwa mmh, hiyo kazi inawezekana ikawa ni kazi chafu, lakini nitafanya nini, kama kuna namna kwanini nisifanye namna...’akasema na baadaye akapokea ujumbe mwingine ukisema;

‘Mwenzako anapata fundisho kidogo, usihangaike naye, mpaka tutakapokupa taarifa nyingine...fanya uwezavyo usiwe karibu naye, na huko kazini sema hujui lolote.....’ujumbe usio na namba ukaingia akajua umetoka wapi.

‘Mwenzangu eeh, keshaingia kwenye mkenge huyo, anajifanya mjanja sio....’ akasema akikunja uso kama mtu anasikia maumivu, na ndipo baadaye akapokea ujumbe wa hatari kutoka kwa Inspecta mwenzake akajua ndio hayo aliyopewa onyo, sasa afanye nini...

Alijaribu kukumbuka enzi zake na mwenzake huyu , kila akipokea ujumbe kama huo anajua mwenzake yupo matatizoni, haraka anachukua pikipiki anakwenda kumuokoa, walifanya akzi hiyo wakawa kama ndugu, lakini leo hii kashindwa...


‘Oh, sasa huuni mtihani,..hata hivyo kajitakia mwenyewe ngoja apate fundishi huenda atakuja kujiunga na mimi, ...lakini hapana sijui ni tatizo gani huenda sio hilo analozungumzia huyu aitwaye bosi,....’akasema, na hapo akachukua simu yake na kumpigia msaidizi wake wa chini na kumwambia;

‘Naona Insepcta Moto yupo kwenye matatizo..’akasema

‘Matatizo gani?’ akauliza mwenzake akionyesha kuchoka, inaonekana alikuwa bado kalala.

‘Hata sijui, mimi nilishamwambia aachane na haya mambo, kuingilia mambo mengine amabayo hayana tija na hayapo katika mtirirko wa kazi zetu, lakini anajifanya shujaa, sijui, hebu kuna tatizo gani, wewe fanya hivi, fuatilia huo ujumbe  niliokutumia uone umetoka wapi, na jitahidi kutoa msaada kama ni muhimu kama sio muhimu achana naye, atajua mwenyewe la kufanya..’akasema

‘Na wewe bwana siku hizi umemgeuka mwenzako tena....maana mara nyingi wewe ndiye msaada wake mkukubwa, mnajuana kwenye kazi zenu, nyie ndio matelingi, nilihskuambia hayo yana mwisho, umeonaeeh...’akasema mwezake kwa kebehi,

‘Nina mambo yangu mengi, karibu yananishinda nilishamueleza kuwa Majuto wa sasa sio yule wa awali, akili imepevuka sasa ni chukua chako mapema, ukizubaa unaachwa kwenye mataa, kesho wenzako wanakucheka kwenye kiyoyozi huku ukipiga lapa kudai mafao....’akasema na kutkata simu.
Alipoangalia saa akaona muda umekwenda, akakumbuka mkewe alivyosema, kwa haraka ofisini na kuingia kwenye gari  lake kwenda kuchukua pesa alizotumiwa na moyoni akijua kuwa hizo hazitoshi kabisa kama gari nalo limeharibiwa basi anahitajia pesa nyingine, lakini hataweza kuzipta nyingine mpaka amfurahishe bosi wake wa uficho, na kumfurahisha ni kwenda kumfanyia kazi atakayopewa, je ni kazi gani.

‘Nitajua mbele kwa mbele, hakuna kazi inayoshindikana kama kuna pesa,.....’akasema na sehemu nyingine ya akaili ikawa inamuwa rafiki yake, inspecta mwenzake, akahisi kujilaumu kinamna nyingine na akawa anawaza mazungumzo yake na Inspecta mwenzake siku mbili nyuma;

Yeye kwa ujumla alikubaliana na taarifa kuwa kifo cha muheshimiwa ni cha kawaida, kwahiyo hakuna haja ya kuhangaika kufanya uchunguzi wa kina na hakupenda taarifa za kifo cha muheshimiwa huyo ziende hivyo, kuwa inawezekana kuna hujuma, alipenda ziseme ni kifo cha kawaida.

‘Mimi sijaridhika kabisa ya kuwa mheshimiwa amepatwa na umauti bila sababu ya msingi, kama inavyoonyesha mheshimiwa hakuwa na tatizo la shinikizo la damu au tatizo la moyo kabla, hili tatizo limekuja hivi karibuni tu. Hii inaonyehs kuna kitu kilimsonga, kitu hicho kilikuwa kikubwa sana mpaka akashindwa kuhimili...’alisema Inspecta mwenzake.

‘Ina maana kila atakayezongwa na mawazo akafa, tunahitajika sisi kama polisi kutafuta ni mazongo gani, huoni tutakuwa tunajivika majukumu yasiyo yetu....’akasema mwenzake

‘Kama inavyoonekana, kiafya mtu huyu alikuwa imara, mtu wa mazoezi, ghfla anapata mshituko, anafika kutibiwa anaonekana ana shinikizo la damu,  na kitu cha ajabu zaidi mbona vifo vya namna hii vinakuwa vingi, huoni kuna umuhimu wa kwenda mbali zaidi kulichunguza hili swala...tusikwepe majukumu, hilo pia ni moja ya majukumu yetu, huoni kuna jambo lipo nyuma yah ii sinmtofahamu,....’akasema mwenzake

‘Hiyo sio kweli,ni kweli kuwa kuna majukumu yanastahiki kufanyiwa uchunguzi, lakini sio hili, kwani kihali halisi, ukichunguza kila mtu ana mazongo ya kimaisha, mimi mwenyewe hapa nina matatizo kibao, je ni nani atanisaidia, je utamchunguza nani uache nani, ..hayo ni mambo ya mtu binafsi na familia husika....sioni sababu ya kuumiza kichwa hapo ’akasema

‘Hapa duniani kuna watu wajanja sana, wanaweza kuona kuna hiyo hali, wakaamua kutumia udhaifu huo kupandikiza mambo yao, kwa vile tu tatizo hilo linafunganishwa na mienendo ya kibinadamu, na kwa kutumia mwanya huo, watu wakaumizwa huku wengine wananufaika....’akasema

‘Sasa wewe unataka tufanye nini?’ akauliza

‘Ni vyema tukaifanya uchunguzi wa kina, tukianzia kwa huyu muheshimiwa, tuone ni kwanini watu wengi wanakufa kwa mashinikizo ya moyo hasa hawa wenye majukumu ya serikali, ni kweli kuna magonjwa na misiba inatokea, lakini hili la muheshimiwa linatia mashaka, mimi nahisi kuna jambo...naona kifo chake kina sababu ya msingi ya kuchunguzwa.....’ ulikuwa mjadala wa maispekta hawa wawili wakati wamerejea ofisini.

‘Ni kweli unavyosema, ...ni wajibu wetu kuchunguza, lakini hebu angalia tatizo lilivyo, ni nani wakutusaidia kutupatia hizo taarifa, mimi naona hapo tunajitafutia kazi, zisizo na malipo, tutapoteza muda bure, maana watu muhimu wa kutusaidia ni madakitari, unaone taarifa zao, zinasema wazi, marehemu kafa kwa shinikizo la damu, unataka kuchunguza nini hapa.

Haya ukirudi kifamilia, wao wamerizika kuwa mtu wao kafa kwa kifo cha kawaida, hakuna anayedai uchunguzi , wewe unataka kujianzishia malalamiko yako ili upate kazi ya kufanya...tutapoteza muda wetu bure, na mshahara wenyewe ndio huo huo, mimi naona tuliache kama lilivyo, kama tutapata fununu nyingine, au malalamiko kutoka kwa familia huska, then, tutalifanyia kazi...’akasema mwenzake

‘Unapenda sana kulalamika kuhusu mshahara, hivi unafikiri serikali itapataia wapi mishahara mikubwa ya kutulipa kama watendaji wake wanafanyakazi katika mazingira hatarishi, wazalishaji wanakuwa hawana amani, jukumu letu nikuhakikisha amani yao ili waweze kuzalisha kwa bidiii , wakizalisha kwa wingi na ndio sisi moja kwa moja kipato kitapanda....’akasema

‘Usijifanye mchumi bwana, kwanini nyanja nyingine wanajaliwa kupita kiasi, kukaa na kuongea tu kwenye vikao wanalipwa marupurupu, sisi na walimu kwanini hatuonekani watu wa maana, tunahatarisha amisha yetu, lakini hiyo inachukuliwa kama kujitolea,..hivi kweli kuna mtu hapendi maisha yake, hivi kweli kuna mtu hapendi maisha bora....’akasema

Ilionakena mjadala huo hautafikia ufumbuzi, na kwa vile inspecta mwenzake alishamfahamu kuhusu msimamo wake, wa kulalamika, kwa kuhitaji kupata masilaha zaidi, akamuona mwenzake akianza kumpuuzia kwa kuanzisha mjadala mwingine kupoteza muda, na alipoona hivyo akamwambia

‘Unajua mimi sasa nawaza kuachana na hii kazi nikatafuta shughuli nyingine ya kufanya...’akasema akimtupia jicho inspecta mwenzake aone atasema nini

‘Shughuli gani  ya kufanya, wakati wewe ulikubali kuingia huku ukatoa kiapo, kuwa upo tayari kuitumikia taifa lako, kulinda raia, na ukachagulia kwa kuziba nafasi hiyo, kama ungeliona haikufai ungewaachia wengine waishie hiyo nafasi, huo sasa ni ufisadi.....

‘Nikuambie ukweli mimi sasa natamani kuwa mfanyabiashara au nijiunge na isiasa na ikibidi nitakuwa mpelelezi wa kujitegemea, ...’akasema

‘Sasa hapo utakuwa umeacha nini, na kufanya nini?’ akauliza mwenzake

‘Kujiajiri, unakuwa na uhuru wa kufanya upendavyo, na kazi nyingine unaweza kupata pesa nyingi tu, wapo watu wana mambo yao, ukiyaweka sawa, ...kama ni kesi ikafutika, unalipwa vizuri tu...ukiwa mwanasiasa ukatumia mdomo wako vyema, unaweza kutajirika, ni uwongo kidogo, maneno mengi, watu wanakuamini...’akasema

‘Wewe sasa unakiuka wito, kiapo cha kazi, ....’akasema

‘Wewe endelea na hicho kiapo chako, mimi nimeshafikia huo uamuzi wangu, ngoja mwaka huu uishe vyema, utanionea wivu...’akasema.

‘Wivu, wivu wa nini bwana, mimi natimiza wajibu wangu wa kitafifa, sitarudi nyuma, nitahakikisha naupata ukweli....’akasema

‘Kila la heri. Tatizo lako hujui unapambana na  nani,...nakuonea huruma, ipo siku utanikumbuka....’akasema na Inspecta Moto akainuka kuondoka, na hawawakuwasiliana tena mpaka hapo alipopata ujumbe huo wa hatari

‘Sijui kapatwa na nini huyu mtu, mmh, nilishamkanya, hakusikia, ngoja afundishwe adabu aijue dunia ilivyo, hajui kuna watu wengine wana dunia yako, sasa ukijifanya mjanja utajikuta unaumia huku wenzako wanachekelea na ukifa wanakuja kutoa maua na zawadi huku moyoni wanajipongeza kuwa hatimaye kikwazo kimeondoka, .....mimi hawanipti tena,....’akasema na mra simu yake ikalia, alipoangalia akaona ni namba ya mke wa Inspecta Moto.

‘Mkewe, ....anapiga toka kwa au kaja yupo hapa Dar..mmmh, nahisi sasa kuna tatizo...’akasema kabla hajaipokea hiyo simu na kichwani akakumbuka kauli ya anayeitwa bosi wake;

‘Usihangaike na lolote kwa huyo mwenzako, sisi tunataka kumfunza adabu...’

NB: Haya hiyo ndio dunia ya bwana Diamu, tuone itakuwaje kwa Inspecta Diamu, atakubali kujiunga na hiyo dunia au ndio kichwa moto?

WAZO LA LEO: Mnapotoa ahadi yoyote iwe ahadi ya biashara,  ahadi za makazini,ahadi za utawala, uongozi, au ahadi zozote zenye kuhusisha mtoa ahadi na mwingine, ahadi za ndoa, nk mjue mungu yupo kati yenu, na pindi mkija kuzihidi hizo ahadi zenu kwa makusudi, mjue hiyo ni dhuluma, na kile kiapo kitakuja kuwaandama hadi hapo mtakapozitimiza.


Mjue kwenye ahadi kuna atakayeumia , hasa yule aliyedhulumia, je utawezaje kuja kulipa hayo maumivu anayoyapata mdhulumiwa. Jamani tukumbuke ahadi ni deni na deni ni laima lilipwe.
Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

What i don't realize is actually how you are now not really a lot more smartly-preferred than you may be right now.

You're very intelligent. You understand thus significantly in terms of this matter,
produced me in my view believe it from a lot of varied angles.
Its like men and women are not involved except it is something to do with Lady
gaga! Your individual stuffs nice. All the time maintain it up!


Also visit my site; ro เถื่อน

Anonymous said...

Aw, this was an extremely nice post. Taking a few minutes and actual effort to generate a top notch article… but what
can I say… I hesitate a whole lot and don't seem to get anything done.


My web blog; adana escort bayan

Rachel siwa Isaac said...

Mhhh ndugu wa mimi..Hongera sana sana..Asante kwa Wazo la Leo pia..Kweli kabisa..

Ni mimi nduguyo.

Anonymous said...

Great work! This is the kind of information that should be shared across the net.
Shame on Google for not positioning this put up upper! Come on over and visit my website .
Thank you =)

My web blog Bernadette Hardacre