Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, July 2, 2014

KISA KIPYA KINAKUJA


                                Kisa kipya kinakuja

Ndugu wapenzi wa diary yangu, huu ni mwezi ambao mtandao huu wa kijamii uliwekwa hewani, japokuwa tarehe rasmi haijafika, tumeweza kumaliza kisa kilichokuwa kikiendelea, kisa cha ‘Baada ya Dhiki Faraja’, kisa hicho kimegusia kuni moja haramu, lililotaka kuweka mitandao yake kil mahali, ni mbinu za kibinafsi, je hili kundi lilianzishwaje, swali hili linatufanya turudie kisa kilichowahi kuandikwa kabla lakini hatukuweza kukimalizia kwasababu za nje ya uwezoo wetu, kisa hicho kilijulikana kama `dunia yangu..

Hali tunayokwenda nayo sasa, inahitaji kukiweka hicho kisa tena, kwa namna ya kipekee inayoendana na wakati, wakati ambao una changamoto nyingi, changamoto za kimaisha, changamoto za kisiasa, changamoto za kimaadili...tunahitaji kukumbushana na kuelekezana kihekima

Dunia yangu’ ni ndoto walizo nazo wengi, hasa vijana wanapoibukia kuyatafuta maisha, na maisha yanaanzia utotoni kwenye malezi, na yanakuja kupata maelekezo kwenye elimu, elimu inakuwa ni dira na nuru ya kutuongoza, lakini  changamoto za elimu ni usahihi wa jinsi ya kuifikisha kwa mlengwa, na jinsi atakavyoipkea na kuifanyia kazi, wakati mwingine elimu inaweza kuwa chanzo cha chachu ya kufanya yale yasiyofaa..

Kisa chetu kitajaribu kuyamulika hayo kwa mawazo yetu, na kuona jinsi gani tunaweza kusaidiana kuelemisha jamii kwa mtizamo wa kisa hiki, mimi  kama mwanadamu naweza nisiwe sahihi, lakini kwa nia moja au nyingine kila mmoja anahitajika kutoa mawazo yake, huenda yakasaidia na kuleta tija, na wewe uwe mwenza wa kuyafanikisha kwa kutoa maoni yako, tkumbuke umoja ni nguvu na pia kidole kimoja katu hakivunji chawa....


Kuna kisa kingine cha simulizi la bosi,...tutaangalia jinsi gani ya kuweka simulizi hili kwani  lina mafunzo mengi sana, bado tunakusanya hizo simulizi zikiwa tayari, hatutachelewa kuziwakilisha. 

TUPO PAMOJA WAPENDWA

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Iddi said...

Pamoja big up,tunasubiri kisa kipya kwa hamu.Unaonaje kama ukiandika kitabu cha kisa kilichopita BAADA YA DHIKI FARAJA,

Yasinta Ngonyani said...

Twasubiri kwa hamu mno...

emu-three said...

Ndio nia yangu kuwa na vitabu vya visa ninavyotunga hapa, lakini yote ni gharama, tuombeane heri tu, ipo siku tutaweza

Nawashukuruni sana kuwa pamoja nami , kunitia moyo, na kuchangia pia, mungu awabariki sana