Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 28, 2014

IDD MUBARAKA


BLOG YENU YA DIARY YANGU, INAWATAKIA HERI NA BARAKA ZA SIKUKUU YA IDD- EL -FITRY:

Muhimu kwa kukumbushana, Nia kubwa ya funga ilikuwa kutujenga imani zetu ili ziweze kumcha mungu ipasavyo, kumcha mungu ni neno lenye maana pana. Kila tendo jema tunalofanya huwa tunamcha mungu, kufanya kazi, kuongea kula kwa nama itakiwavyo nk ni kumcha mungu, na tunasalimiana naye muumba wetu au kumuomba kwenye ibada zetu ambazo nazo zina muda wake maalumu(swala tano)

Katika funga tumejifunza mengi lakini zaidi ni uvumilivu, jinsi gani unavyoweza kusubiri, jinsi gani unavyoweza kuihisi njaa, ili hata ukimuona mwenzako ana njaa ujua jinsi gani njaa inavyouma. Viongozi , wakubwa, matajiri, mumeliona hili, ni wajibu wenu kujenga usawa, kuwahurumia wafanyakazi wenu, na kuwapa haki zao stahiki.

Katika hali ya maisha,wapo wasiojiweza, masikini wanakufa kwa njaa, sasa wewe umeiona njaa inavyouma, maisha yalivyo, hutashindwa kumsaidia mwenzako, mfanyakazi wako , jirani yako nk.

Pia tumejifunza upendo na mshikamano, ni ajabu siku ya mwisho watu wanaanza kunyosheana kidole, na kusutana kuwa wale walitangulia kufungulia au kuanza kufunga, au walichelewa wana makosa hili sio muhimu kwetu, ilikuwa ni sehemu ya kupeana pongezi wale waliotangulia na hao watakaofuatia kesho kuwa TUNAKUSHUKURU MWENYEZIMUNGU TUKASHIKANA MIKONO YA HERI, KUWA kila mmoja katimiza nguzo hii muhimu kati ya nguzo tano, hilo la kuswali Iddi ni sehemu ya kusherehekea, lisitufanye tunyosheane vidole.

Hii ni dhima ya viongozi wa dini, wao watakuja kuulizwa  kwa hili,...

Blog yenu inawatakia idd njema na tunasema;

IDD MUBARAA


Ni mimi: emu-three