Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, June 16, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-77



‘Jibu maswali yangu kama wewe ni wakili unayejiamni, ...kama huna hatia mbona unaogopa,kuyajibu maswali yangu ...’akasema mpelelezi

‘Nimeshakujibu maswali yako yote muhimu kwa sasa, hasa yale ninayostahili kukujibu kwa hapa, kama kuna maswali zaidi ya hayo nione ofisini kwangu, au kama unaona nina kosa nishitaki, mimi nitakuja kujieleza huko kituoni, lakini hayo uyafanye kwa kufuata utaratibu, sio kihuni huni tu,...’akasema na kuanza kuondoka, na mpelelezi akamuendea na kumshika begani

Yule wakili akatulia na taratibu akageuza kichwa kukabiliana na huyo mpelelezi, na nilijua kitakachofuata hapo ni ngumi,...

‘Usiondoke mimi sijamalizana na wewe...mu-he-shi-miwa, ’akasema mpelelezi na yule wakili akageuka mzima mzima huku akiusogeza mkono wa mpelelezi pembeni na kusema;

‘Naona sasa unataka kunipanda kichwani, nimeshakuambia kuwa kama unataka kuongea na mimi kisheria, fuata utaratibu, mimi ni mtu nineyeheshimika, mimi ni wakili, na ninajua sheria ni nini, ...usitake tuharibiane....’akasema

‘Nakufahamu sana, na ndio maana nyafanya hayo..na kama unakubaliana na mimi kuwa na mimi ni mpelelezi ninayefahamu kazi yangu vyema, tulia uyajibu maswali yangu....’akasema mpelelezi.

‘Nimeshakuambia fuata utaratibu, ili nijibu maswali yako kisheria, njoo ofisini kwangu au nifungulieni mashitaka, na mimi nitafika kituoni, na kuja kuyajibu maswali yenu ambayo mnataka kuniuliza, lakini kwa utartibu uliokubalika kisheria, lakini hapa tunaongea kama wapiti njia tu...’akasema

‘Sasa mimi ninakushika kwa kosa la kuhusika na mauaji ya mlinzi, ninakushuku wewe kuwa unahusika, na nataka nifanye uchunguzi wa kina bila kuingiliwa, kwahiyo ili niweze kufanya hayo ni lazima ushikiliwe ...’akasema na mara nikamuona mpelelezi akitoa pingu aliyokuwa kaiweka nyuma,...

‘Eti nini.....’akasema wakili sasa akibadilika na kuwa mkali na muda huo mkuu wa hapo gerezani akawa anawasogelea akijua sasa hali sio shwari tena...

Tuendelee ni kisa chetu

***********

Mkuu wa kituo hicho cha magereza alipoona hali inataka kuwa mbaya, akawasogeela wale watu wawili ambao kila mmoja aliashaanza kutunisha misuli tayari kwa mapambano, na kabla yule mkuu hajawafikia  mara wakaingia askari polisi wawili wakiwa wameshikilia pingu mikononi, wakasimama kusubiri amri , na yule mkuu wa gereza alipowaona  akasema

‘Mpelelei hebu kwanza tuongee ofisini, na wewe wakili tulia hapo hapo….’akasema na kuwaangalia wale askari polisi, alitaka kusema neno lakini akaghairi, akamshika mkono mpelelezi na kuondoka naye

‘Askari hakikisha huyu mtu hasogezi mguu, na hapigi simu , huyu mtu anatakiwa kushikiliwa, tukimuachia ataharibu ushahidi kama ilivyo kawaida yake, mapaka anafika hapa hakujua kuwa mimi nafahamu mipango yake yote, kwahiyo ukimpa nafasi akatoka humu atakwenda kuharibu kilakitu…’akasema mpelelezi

‘Hizo ni hasira zako, mimi sihusiki na lolote, siwezi kufanya kama unavyosema wewe,mimi naijua vyema sheria na wote wanajua nipo sahihi wakati wote,….huyu mkuu wa hapa anafahamu kuwa sijui lolote, nimeshaongea naye, na yeye akanihoji kwa utaalamu wake amegundua kabisa kuwa mimi sihusiki na lolote…wewe na mihasira yako unashindwa kutumia akili…’akasema huyo wakili

‘Basi, basi….hebu tukaongee kwanza ofisini kwangu, nataka uniweke sawa...’akasema na wakaondoka kuelekea ofisini kwa  huyo mkuu, ilipita muda, baadaye wakarudi na mkuu huyo alikuwa na mfuko wa plastiki sikujua ni wa nini kwa wakati ule.

‘Mkuu kama nilivyokuambia  huyu mtu hawezi kuachiliwa, huyu ni mtu hatari kuliko unavyofikiria wewe mkuu, huyu sasa hivi anawekwa pingu tunaondoka naye hadi kituo cha polisi, au wewe umshikilie hapa hadi tukamlishe uchunguzi wetu….’akasema mpelelezi,

‘Mkuu lakini huyu ni wakili hawezi kukimbia mimi naona tumuachie halafu yeye mwenyewe atakuja huko kituoni, mimi namfahamu sana…’akasema askari mmoja,nampelelezi akamuangalia yule askari kwa makini, halafu akasema;

‘Huyu haachliwi,ni kama mkuu wa kituo hiki yupo tayari kubeba dhamana hiyo, sawa anaweza kushikiliwa hapa hapa gerezani, maana hatujui huko mbele kuna watu gani wa kumsaidia, najua huyu mtu ana watu kila mahali,hata ndani ya vijana wetu wa kipolisi….’akasema mpelelezi.

‘Sawa mimi nakubali kubeba hiyo dhamana ,nitamshikilia hapa kituoni, lakini kwa masaa ysiyozidi 24,…’akasema yule mkuu akiangalia saa yake.

‘Unafanya makosa makubwa sana mpelelezi, siamini kuwa ni wewe, mimi nilikuwa nakuheshimu sana, lakini kwa hili, tutafikishana mbali nitahakikisha nitakushitaki kwa kunidhalilisha, na kunisingizia uwongo  huwezi kunishutumu kwa jambo ambalo sijalifanya, na kilakitu kipo wazi , huu sio utaratibu wa kikazi, na kwahili ni lazima likomeshwe na watu kama nyie hamfai kwenye kazi kama hizo.....’akasema

‘Wewe ndio unafaa, eeh,...usipoteze pumzi yako kwa vitisho, fanya unalotaka, lakini ni lazima uwajibike, ili haki itendeke...’akasema mpelelezi.

‘Nakuonya, hizo hasira zako zitakupeleka kubaya, na nakuhakikishia hili jambo litafika mbali…’akasema yule wakili

‘Usijali,…nimeshajiandaa kwa hilo, tutakutana huko huko mbali unapopaamini wewe….’akasema mpelelezi kwa kujiamini na yule mkuu akasema;

‘Naona tumelewana, sawa wakili, wewe utabakia hapa , ili watu wa usalama wafanye uchunguzi wao, na kama watamaliza mapema, basi wewe utaruhusiwa kuondoka, wao wanatimiza wajibu wao wa kikazi , sio kwa nia ya kukomoana….’akasema yule mkuu na mara mpelelezi akamsogelea yule wakili, na kumuambia;

‘Nipe simu yako…’akasema mpelelezi

‘Siwezi kukupa simu yangu…kwanini nikupe simu yangu?’akasema huyo wakili kwa hasira na mpelelezi akamgeukia mkuu wa kituo

‘Chukua simu yake hatutaki mawasiliano yoyote kutoka kwake kuanzia sasa hivi, najua ana watu wake watafanya hiyo kazi, lakini kwa hivi sasa ni vyema kuchukua vitu vyake vyote alivyo navyo vyenye kutilia mashaka, hasa vya mawasiliani..,hii ni  amri ya polisi….’akasema mpelelezi na yulemkuu akamuangalia wakili , na kusema;

‘Bora utii sheria, natumai unalielewa hilo muheshimiwa wakili, mtu ukishikiliwa unatakiwa utoe vitu vyote kwa polisi, ikiwemo simu…na ukiondoka utakabidhiwa vitu vyako.’akasema huyo mkuu, na wakili akatulia kwa muda akionyesha hasira, halafu akaitoa simu yake na ilionekana kama anataka kufanya kitu kwenye simu yake,lakini mpelelezi akmuwahi na kusema

‘Acha ujanja wako…..’akasema mpelelezi akiwa keshamfikia akitaka kuichukua ile simu mikononi mwa huyo wakili , na yule wakili akasema;

‘Nilikuwa naizima simu yangu na kuangalia muda wa tukio hili, sina wasiwasi na lolote lile, mnaweza kuchukua kila kitu,lakini nataka kila jambo lililofanyika hapa liwekwe kwenye kumbukumbu....’akasema

‘Hiyo ni kazi ya mkuu wa hapa, anajua kazi yake hatuwezi kumfundidha ila ninachotaka mimi ni wewe kukabakia hapa, bila kuleta ujanja wa kuwasiliana na watu wako, ambao wanaweza kuharibu ushahidi...’akasema

‘Hata hivyo kwa vile umenishuku, ni lazima nimpata wakili , kwani mimi siwezi kujiwakili mwenyewe,...hiyo ni haki yangu kisheria...’akasema

‘Utafanya hilo kwa wakati muafaka, kila kitu utapewa kwa mujibu wa sheria, sasa hivi tunakushikilia ili tuweze kupata ushahidi ...’akasema mpelelezi

‘Sawa, nakusikiliza wewe bosi....’akasema wakili huyo akikunja uso wa hasira, na kutulia akimuangalia yule mkuu wa hicho kituo cha magereza, na yule mkuu, akamsogelea na kuichukua ile simu, akampekua na kutoa kifaa kingine kidogo, nahisi ni cha kuchukulia mawasiliano...akakiangalia na mpelelezi akasogea na kukiangalia

‘Na hiki ulikuja nacho kwa kazi gani?’ akauliza

‘Hayo maswali nitayajibu nikiwa na wakili wangu....’akasema, na mpelelezi akakiangalia na kutafuta sehemu ya kuzimia, kwani ilionekana chombo hicho kilikuwa kikichukua sauti ya maongezi yote yaliyotokea hapo, akamwambia mkuu,

‘Mkuu, samahani sio kwamba nakupa amri, lakini kwa vile huyu mtu haniamini, basi nataka wewe ufanye hiyo kazi, hivyo vitu vyote ni ushahidi, ni vyema ukaviweka kwenye chombo maalumu, na hakikisha havigusi tena...’akasema na yule mkuu akageuka kumuagalia askari wake mmoja aliyekuwepo hapo, akasema;

‘Fanya hiyo kazi, mpekue na toa kila kitu alicho nacho uweke kwenye huu mfuko...’akasema huyo mkuu, na yule askari wake, akafanya hiyo kazi,

 ‘Huwezi kunifanyia hivyo, ..sio haki kabisa,na mkuu unaona alichokifanya huyu mtu, ametumia nguvu kuninyang’anya mali yangu,na hiyo simu yangu  ina mambo yangu ya kikazi, natakiwa niwasiliane nao muda wowote, hivi  ikitokea mteja wangu ananihitaji kwa haraka atajuaje kuwa nipo sehemu nisiyoweza kumfikia, hamjui umuhimu wangu ehe…’akasema akitaka kumsogelea huyo mpelelezi,na wale askari wakawa wamemuwahi na kusimama kati kati yao..

‘Huna ujanja wakili,….ni lazima safari hii upambane na nguvu ya dola, niliwahi kukuambia kuwa siku za mwizi ni arubaini,usijifanye kutumia sheria kwa masilahi yako…hakuna aliye juu ya sheria,wewe na wenzako mjue mwisho wenu umefika, na bora mtubu madhambi yenu, ili tuokeo muda, kwani sasa hivi, ni lazima haki ipatikane….’akasema

‘Haki, ni nani hajui hiyo haki, hiyo ndio kazi yangu ya kuitafuta haki kwa watu , kwa jamii,leo hii unanituhumu,…sitakubali hili lililotokea hapa na mkuu wa hiki kituo ni shahidi, ni lazima lifike kwa vyombo vya sheria, mkuu  umeona yote yaliyotokea hapa, hili ni lazima litafika mahakamani….’akasema wakili, na mkuu akamshika mkono huyo wakili na kusema;

‘Twende …..tuwaache hawa watu wakatimize wajibu wao...usiwe na shaka, ni tarataibu za kawaida tu, kama huna tatizo hakuna shaka, .....’akasema, na huyo mpelelezi akawaangalia wakiondoka, na yeye akawageukia wale maaskari na kusema

‘Mimi sipaamini mahali hapa….chukueni zamu,kuhakikisha  huyu mtu hatoki, ….’akasema na kuchukua simu yake, na akawa anaongea na mtu akasema;

‘Upo leo zamu, ..okey safi kabisa,kuna vijana wangu wawili mtasaidiana nao, kama utahitajia huo msaada, vinginevyo ni kuwa kuna jamaa ,yule wakili aliyekuwa akimtetea mlinzi, ndio…yes, ameuwawa, ...'akasikiliza halafu akasema

'Mhh, oooh, na wewe ulimuona eeh, jana usiku eeh, okey, usijali yote hayo nimeshaambiwa....sasa kama upo zamu leo, hakikisha huyu wakili akiingizwa sehemu atakayokaa, muhakikishe hana kitu mfukoni,...’akasema na kusogea mabli kidogo ili tusikia anachoongea, na mimi nikajisogeza sikutaak kitu kinipite.

‘Hakikisheni analala usiku kucha….ndio, msijali,fanyeni muwezavyo, anaweza kutumia mbinu nyingine....nafahamu kuna watu wake watakuwa wameshahisi hilo,  na hata hawa watu wetu wanaweza wakafanya hiyo kazi kumsaidia, kila mahali ana watu...’akasema na kusikiliza simu kwa makini, halafu akasema;

‘Okey, hilo nakuachia wewe…’akasema halafu akawageukia,maaskari, akatulia akiwaangalia, akamgeukia yule aaskari aliyemtetea huyo wakili na kutaka kumuambia kitu lakini akaghairi na kunigeukia mimi akasema;

 ‘Tunaweza kuondoka, nina kazi nyingi sana leo,….’akasema na mimi nikamfuatilia nyuma na tulipofika kwenye magari yetu, akawa anawasiliana na watu wake, alikuwa akitoa amri;

‘Wale watu wote, washikiliwe, ...ndio wafikishwe kituoni, waambiwe kuna maswali wanahitajika kuulizwa basi, msiwape nafasi hiyo , kama ni wakili wao atakuja huko huko kituoni, msiwape nafasi ya kujitetea, hiyo ni amri....’akasema halafu akatulia na baadaye akapiga simu sehemu nyingine.

‘Hao watu wakichukuliwa fanyeni upekuzi wa haraka, kila kitu chenye ushahidi, kama tulivyoongea hakikisheni mnakiwakilisha kwenye chumba chetu, yaah, nimeshapata hicho kibali, msijali,....’akasema.

Baadaye wakati anaingia kwenye gari lake nikamuuliza

‘Mkuu una uhakika na unachokifanya, huyu wakili nasikia ni mkorofi  sana, ukimchezea, ni lazima akuweke ndani, nasikia hakubali kushindwa kirahisi,nina uhakika akitoka hapa atakuchukulia hatua…’nikamwambia mpelelezi

‘Usiwe na shaka na maamuzi yangu,ninamfahamu sanahuyu jamaa lakini ni vyema tukafanya hivyo ili niweze kukamlisha uchunguzi wangu,huyu jamaa amekuwa kikwazo kwangu kila ninapotaka habari fulani kwa watu, ninajikuta napambana naye, yeye wateja wake wengi ni watu ninaowashuku,…na ili nifanikiwe kwa uchunguzi wangu ni lazima hili lifanyike….’akasema

‘Lakini huna uhakikakuwa yeye anahusika na kifo cha mlinzi?’ nikamuuliza

‘Uhakika nitaupata tu, kuna vigezo vingi vinamshuku, na mimi sitaki kupoteza hiyo nafasi, kuna kitu nataka kuthibitisha,usiwe na wasiwasi,ninachohitajia ni huyu mtu asiachiwe, vinginevyo kazi yangu itakuwa ngumu sana, hawa watu wana mbinu za kila namna…sasa hivi watu wake watakuwa wakimtafuta hawajui kuwa na yeye yupo kituoni, lakini watakuwa kwenye vituo tofauti tofauti..hakuna mawasiliano hapo’akasema mpelelezi

‘Lakini huna uhakika kuwa huyo wakili anahusika na mauaji ya mlinzi…?’nikamuuliza

‘Niwe na uhakika nisiwe na uhakika,lakini jamaa huyu anahusika na kifo cha mlinzi, kuna jambo nataka kulicheza, ni swala la muda, nina imani hadi kesho nitakuwa nimeshafanikiwa, na itabakia kazi ya kuwakilisha ushahidi wote mahakamani, kama mdada angelikuwepo, isingelisumbua hivi, hata hivyo hakijaharibika kitu….’akasema mpelelezi na kuanza kuondoka,na yulemkuu akasema

‘Mdada angesaidia nini?’ nikamuuliza

‘Yeye ana ushahid muhimu sana, zikiwemo hizo nyaraka za siri, na uchunguzi wote aliokuwa nao mzee, kauchukua yeye, sijui anampelekea nani, au ana ajenda gani ya siri na kundi hili. Hii inanifanya nimshuku sana huyu, japokuwa mzee anasema huyo dada hahusiki...lakini kwa nini mzee anamtetea....’akawa anasema.

‘Labda mdada alikwua akimfanyia kazi zake...’nikasema

‘Hapana, mdada na mzee hawaelewani kabisa, hasa kipindi hiki cha nyuma, mzee anamshuku mdada kuwa anatumiwa na watu ambao wanamshuku mzee vibaya, lakini hawajulikani hao watu ni akina nani, na wana masilahi gani....’akasema mpelelezi

‘Inawezekana wewe na mzee mnamshuku mdada kuwa yupo kwenye hilo kundi kisiri au?’ nikauliza

‘Hapo sijui...inawezekana, uwezekano ni mkubwa sana, na wewe unatakiwa unisaidie kwa hilo, tukifika kwako nataka uniambie kila kitu unachokijua kuhusu mdada, vinginevyo na wewe utashikirishwa kwenye washukiwa, sasa hivi sina urafiki na mtu, sasa hivi ni kazi tu...’akasema mpelelezi akiniangalia kuwa uso wa kiaskari.

‘Mhh, hata mimi mkuu...!’ nikasema huku nikijua sasa mambo yameiva, na mdada hayupo tena, ina maana nisiposhirikiana na mpelelezi, nitaweza kuyabeba madhambi ya mdada, lakini mdada amekwenda wapi, mbona ameamua kunisaliti...

‘Kama mdada kafanya hivyo sitamsamehe, ni lazima nimtafute, sijui yupo wapi, huenda huko alipo anachekelea kuwa kaniweza, mmh, lakini hata hivyo ooh ....kweli moyo wangu hautakuwa na raha bila ya kumuona mdada,...’nikasema na huku moyoni nikikiri kuwa kweli nampenda mdada, na sijui nitawezaje tena kuficha madhambi yake. 

Na mara nilisikia honi ikipigwa kuashiria kuwa mpelelezi  ananisubiri ili tuongezane na yeye ili nikamuambia ukweli wote kuhusu mdada...

NB: Haya haya umekucha,

WAZO LA LEO:Muda ni kitu muhimu sana, wengi wetu tunakipuuzia, muda ni mtaji aliotujalia mwenyezimungu, na tulitakiwa tuhakikishe kuwa kila sehemu ya muda inaleta tija, na hasa kwa matendo mema.


Hebu angalia watu wanavyopteza muda kwa maongezi kijiweni, au kwa kufanya yale yasiyonufaisha jamiii. Tukumbuke kuwa muda kamwe haurudi nyuma, kila mlio wa sekunde, ni kuashiria kuwa muda unasonga mbele, uhai unapungua, na kama hakuna faida ujue ni hasara inaingia,

Jiulize, je wewe unakwenda na huo muda, je wewe umafanyia nini  na mtaji huo muda, jiulize sana , maana kazi ya mtaji ni kuzalisha, tena kwa faida, kama sio faida ni hasara. Kumbuka kuwa muda kamwe hautakusubiri wewe, ufanyie kazi huo mtaji ili usije ukajuta wakati huna muda tena wa kuishi hapa duniani.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Hello, yοu useԀ to compoose amazing articles, Ƅut the
immeԀiate paѕt feԝ posts haѵe alreaԁy been sorta lackluster...
I miss уour incrediblpe writing. Ƥast ɑ few posts arе
only a little from ϲourse!

Feel free to surf to myy blog - healthy cat r7 weight diagram; ,

Anonymous said...

Hi! I understand this is somewhat off-topic
however I had to ask. Does running a well-established website like yours take a massive amount work?

I'm completely new to operating a blog however I do write in my journal on a daily basis.
I'd like to start a blog so I can easily share my own experience and
feelings online. Please let me know if you have any suggestions
or tips for new aspiring bloggers. Appreciate it!


Feel free to surf to my website :: senior moving assistance