Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 6, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-72



‘Hata huyo mhasibu umemtumia kwa njia hiyo hiyo,  ulimchukua picha mbaya ili aweze kuingia kwenye anga zako, kama ulivyowahi kuwafanyia watu wengine, nia ni ili akubali kufanya kila unachokitaka, ukiongozwa na shetani wako....' Akawa anasema kwa hasira na kwa jaziba

‘Sasa muda umefika wa wewe kuachana na huyo shetani wako, shetani ashindwe, shetani shindwa, ....ili haki itendeke usitake, unasikia wewe mdada...’akasema akimnyoshea mdada kidoke, na watu sasa wakawa kimiya hata hakimu akawa kama kaduwaa,...na huyo wakili akaendelea kusema

‘Kutokana na huyo shetani wako, umefikia kumsingizia mlinzi wako kwa kosa ambalo hakulifanya yeye, wewe ndiye uliyeua, bila kujitambua ukiwa umebadilia, ukiamrishwa na shetani wako,...kubali kuwa wewe ndiye uliyeua, ili shetani wako asiwe na nguvu ya kukufanya wewe mtumwa wake, kubalia,...kubali ili huyo mdudu asikufanye mtumwa....shetani toka ...achana na huyo shetani kubali kubali...’akawa anamsogelea mdada huku kamnyoshea kidole na akiongea kwa jaziba

Mdada alikuwa katulia akimuangalia huyo wakili, hakuonyesha dalili yoyote ya kukasirika, nikaona akiinua mkono na kushika sehemu ya kichwa,...nahisi kichwa kilishaanza kumuuma, nilkajiuliza kwanini hawamzuii huyu wakili, hajui kuwa analikoroga, nilimuonea mdada huruma maana ndani kwa ndani mdada alikuwa akiumia, mimi nilijua kwa uhakika mdada hajaua, lakini huwezi jua....

‘Mdada kubali ili damu uliyoimwanga isifukiwe hivi hivi, kubali haki itendeke, kubali kubali kuwa wewe ndiye uliyemuua mtoza ushuru, ili kuficha machafu yako...’akaendelea kuongea kama wahubiri wanavyofanya bila kujali pingamizi la hakimu,huku akimnyoshea mdada idole na kupandisha mkono juu chini...

‘Stop...’sauti ikatoka kwa mdada, sauti nzito yenye mikwaruzo, na sura yam dada ikaanza kubadilia...

Mimi hapo nikajua hali ya hatari imeshatangazwa

Tuendelee na kisa chetu...

*******

Sauti ile iliyofanya chumba kizima cha mahakama kuwa kimiya, na wakili mtetezi naye akatulia ghafla kumuangalia mdada, huku akionyesha wasiwasi na mkono uliokuwa hewani ukaanza kushuka, lakini ukafika mahali ukaganda ukiwa bado hewani...

Wakili yule akiwa na wasiwasi akamuangalai mdada,...walipokutanisha macho yao, wakili huyo akaanza kurudi kinyume nyume,...

Mimi kwa haraka nikamtupia macho mdada, nikamuona akianza kutikiswa, mwili ulikwua ukitikiswa kwa nguvu,na kwa haraka, na mara uso wa kupendeza ukabadilika na kujaa makunyazi ya hasira,..macho yakabadilika na kuwa meupe yenye sura ya kutisha, mdomo ukabakia wazi na ulimi kutoka nje..na mara sauti ikatoka mdomoni kwa mdada....

Sauti iliyotoka kwenye mdomo kwa mdada ilikuwa nzito na ilikuwa kama ya mikwaruzo kwaruzo hivi uliweza kuhisi kama inatetemesha paa la jengo hilo.., na moyoni kwenye akili yangu niliifananisha sauti ile kama sauti ya simba dume...


Hali ya hatari ikatawala.....

Mimi pale nilipokuwa  nimekaa nilihisi mwili mzima ukizizima kwa woga, na hata kuhisi shinikizo la moyo likipanda na kushuka, na nilipoona ile hali inaelekea kubaya, niligeuka kumuangalia askari aliyekuwa nyuma yangu eti akinilinda kama mmoja wa watuhumiwa, lakini nilimuona akiwa kakodoa macho kuangalia kule mbele kwa woga  nahisi na kutokuamini kile kinachotokea, ..

‘Oh…siamini,yaani mdada mnzuri kama huyu…oh’,akawa anasema mwenyewe

‘Inabidi kumuita dakitari wake haraka iwezekanavyo….’nikasema nikumshauri askari niliyekua naye,lakini ilikuwa kama naongea na mti,kwani askari yule alikuwa kakodoa macho akiangalia kule mbele, na ghafla niliona mtu akidondoka pembeni yangu, ni kama mtu aliyedondoka toka juu, kumbe alikuwa yule wakili mtetezi, aligugumia kwa maumivu na mara akawa kimiya, nikasema;

‘Mdada keshaaua…’ na yule askari aliyekuwa nyuma yangu, nilimuona kama anataka kukimbia wakati wenzake wanakwenda kule alipo mdada ili wamshike, na hapohapo nikaona watu wakigombea  kule  mlangoni kutaka kutoka nje, mlago ulionekana mdogo, nikageuka kumuangalia yuleaskari niliyekuwa naye kuona jinsi gani anaweza kwenda kusaidia…yeye bado alikuwa kaduwaa.

Haikupita muda, askari wawili waliokwenda kumkamata mdada, nao walirushwa na kudondokea  kwenye viti wanavyokalia watu,wale watu waliokuwa wamebakia humo ndani walipoona hilo tukio kila mmoja alitafuta njia yake…

‘Mkamateni….’ilikuwa ni amari ya hakimu ambaye muda mwingi naye alibakia mdomo wazi akiwa haamini kinachotokea, akiwa katoa macho kama walivyokuwa wamefanya watu wengine, na ni aheri asingelitoa ile amri kwani sauti yake ilimfanya mdada ageuke na kuelekea palealipokuwa amekaa huyo muheshimiwa hakimu,na hapo ikawa ni hatari... askari majasiri walijaribu kumkbili mdada, ili kumzui asiende huko kwa muheshimiwa laini kila aliyemfikia alishikwa , akainuliwa juu, na kurushiwa mbali.

Nilichoona cha ajabu ni kuwa mdada hakuwa akipiga, japokuwa maaskari wengine walijaribu kumpiga na virungu vyao, lakini yeye kile aliyemkamata, alichofanya ni kumuinua juu na kumtupia mbali...sasa inategemea huyo mtu kaanguka vipi....kama wakili mtetezi, nahisi alikuwa kapoteza fahamu kwani pale alipolala sakafuni alikuwa kimiya...

Mimi nilipoona ile hali itakuwa mbaya zaidi,  nikageuka kumuangalia askari aliyekuwa nyuma yangu,lakini sikuona mtu, nilikuwa nimebakia peke yangu eneo lile, hakuna cha walinzi au watu wengine wa usalama ambao walikuwa sehemu ile niliyowekwa...

Nikageuka kuangalia sehemu  wanapokaa watu, kwa muda ule sehemu kubwa ya eneo wanapokaa watu ilikuwa wazi,waliibakia watu wachache tu ambao nao walikwa wameshikwa na butwaa, wakijaribu kuangalia, lakini hapo hapo wakiwa wameshikwa na kigugumizi cha miguu, wengine wakipambana na shinikizo la damu, na niliona wengine wakikimbilia mlangoni kutoka nje..

Pale mbele alipokuwepo hakimu na wazee wa baraka,na watu wa usalama kulianza kupungua watu walinzi waliokuwepo ambao waliteremka upande wa chini kuja kusaidia wenzao, walikuwa wamelala sakafuni, wengine wakigugumia maumivi na wengine fahamu zimewatoka, wazee wa mahakama, walikuwa wakihema wakiombea mdada asije akawakabili, nahisi kama kungelikuwa na silaha humo ndani, mdada sasa hivi angelikuwa keshapigwa risasi...maana alishakuwa mbogo aliyejeruhiwa...

Wakili muendesha mashitaka alikuwa hayupo, nahisi ndio watu wa mwanzo kukimbia,nikajikuta nikicheka kimoyo moyo, japokuwa hali iliyokuwepo humo ndani ilikuwa ni hatari,....sikuweza kukimbia maana mimi ni mtuhumiwa, siruhusiwi kutoka hapo bila ridhaa ya askari wangu.

Hata hivyo niliona ni lazima nifanye kitu, ningelikuwa na simu ningempigia dakitari wa mdada, lakini nilijua ni lazima kuna mtu keshampigia, ...nikasimama, huku nikiogopa nisije nikala kirungu, lakini ni nani angenipiga hicho kirungu wakati asari wangu hayupo, nikainua hatu amoja mbele, hakuna kilichotokea, , nikasema;

‘Mdada tafadhali…wahurumie hawajui walichokifanya....’nikasema lakini pale hapakuwepo mdada, kilichokuwepo ni mwili tu wa mdada, ndani yake kulikuwa na hisia nyingine siyotambulikana,mdada au umbile la mdada likawa sasa linakaribia mezani kwa muheshimiwa hakimu, na muheshimiwa hakimu alikuwa mdomo wazi,akiona kifo kinamnyemelea, ni nani angemsaidia kwa wakati huo...

Nilipoona ile hali nikaanza kutembea pole pole kumfuata mdada kwa nyuma,huku naogopa kitakachonipata, nikikumbuka wenzangu walivyoinuliwa hewani na kutupwa mbali, lakini moyoni nikasema ngoja tu nifanya la kufanya,nikamkaribia nikasema.

‘Mdada ni mimi mhasibu, mpenzi wako, nakuomba uwasamehe hao watu, hawajui walichokifanya….’nikasema

‘Mimi sijajua, kwanini wananisingizia kuwa nimeua...haki itatendeka vipi hapa...nyie waandamu mnajifanya mnajua sana haki kumbe ni wanafiki , wanafiki wakubwa, waliofanya hayo mauaji ndio hao hao wanaojitia kuitafuta haki, toka lini kesi ya ngedere ukampelekea tumbili...’sauto nzito yenye mikwaruzo ilisikika ikitokea mdomono mwa mdada.

‘Wamekusikia, wahurumie...’nikasema.

‘Kwanza wewe ni nani, unayeniambia hivyo....’akasema na kunigeukia, na haraka nikatoa ishara kuwa muheshimiwa atoke pale mezani, na ilikuwa kama nimetoa amri kuwa watu pale mbele wakimbie, kilichofuata hapo ni muheshimiwa na wazee wa baraza waigongana kila mmoja akitafuta usawa wake wa kukimbilia.

Mdada aliiona ile hali , lakini cha ajabu hakugeuka kuwakabili, akawa ananiangalia mimi, akasema;

‘Wewe ndiye unayejifanya mjanja...ooh, wewe ndiye unayekataa kumchukua kiti wangu, nimekupa awe na wewe lakini unakaidi, ..unataka kuishi na mtu asiyekuthamini, ...sasa nitakuchukua na wewe mkaishi huo kuzimu, na kiti wangu....’akasema na kunishika, akaniinua hewani akanizungusha,..nikiwa hewani kichwa kilianza kuuma..lakini sikuacha kumuomba mungu wangu anisaidie...

Wakati nikiwa hewani , mdada alinizungusha mara mbili, ni kitedndo cha sekunde, alivyoniinua na kuniweka hewani akawa ananizungusha ili kunitupia mbali, nilimuona dakitari wa mdada akija kwa kasi pale tulipokuwepo, lakini nikajua keshachelewa, ...nikahisi nikipaa hewani....

NB: Haya walichokitaka wamekipata, walitaka ushaidi wa dhahiri kuwa kweli mdada alikuwa ana matatizo kama hayo, matatizo ya akili, mahakama imeshuhudia, nay eye kakana kuwa hajaua, je ataaminika,? Kama sio yeye, ni nani kamuua mtoza ushuru, ni mlinzi, ni mdada, au ni...? hebu toa na wewe mawazo yako mpendwa

Lakini hata hivyo, huo ni ushahidi mmojawapo kwenye kesi hii, tutaona ushahidi mwingine kwenye sehemu ijayo...tuwe pamoja

WAZO LA LEO: Unapopewa dhamana ya kuhukumu, unapopewa dhamana ya kuwa mtu kati, unapopewa dhamana ya uongozi, ambapo unahitajika kuangalia kuwa haki ipo wapi ni muhimu sana, ukajitoa kabisa kwenye upande wowote, kinafsi na kimatendo, ni kweli kama kibinadamu kila mtu ana mapendeleo yake, lakini kwenye haki, hakikisha haki inatendeka,kwa wakati huo, hapo hutakiwi kuwa na upendeleo wa sehemu yoyote, hata kama ni ndugu yao, unachotakiwa kufanya ni kuwasikilize wote, na uangalie haki na sheria inasemaje.

Tatizo sasa, haki na sheria inakuwa na makengeza pale inapomgusa mwenzetu, inapowagusa wenye uwezo na wasio na uwezo, inapowagusa wao na nyie, inapogusa masilahi yetu, jamani huo sio uungwana, huo sio uadilifu,timizeni wajibu wenu kwa kuhukumu kwa haki na ukweli ili mpate baraka kutoka kwa mwenyezimungu.

Ni mimi: emu-three

No comments :