Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 23, 2014

WENGI WAPE-MAONI KWA BUNGE LA KATIBA



KATIBA ni kitu muhimu sana katika nchi, ni kitu ambacho kila mmoja alitakiwa akifahamu na ikiwezekana, kwa vile tumepata furusa hii, basi kila mmoja alitakiwa achangie kwa namna moja au nyingine kwani huo ni mkataba wake na nchi yake. Mimi sio mtaalamu sana wa sheria, lakini nina maoni yangu kidogo tu.

Kulumbana kwa hoja ni muhimu, hilo halikwepeki, hatuwezi kukubali kila hoja kwa kauli za ndio ndio,..hapana,  ni muhimu watu waelezane na kukosoa pale panapoonekana kuna uwalakini, kwani katiba hutungwa na watu, na watu sio wakamilifu kwa kila jambo. 

Kulumbana kutasaidia kukiweka kila kipengele kwenye stahiki yake na kuleta tija ya mshikamano kama taifa na utaifa wetu. Tusione ajabu kwa hayo wanayoyafanya wenzetu, cha muhimu ni hoja zenye msingi wa kujenga, kuboresha  na sio kubomoa na kuharibu.

Kila mmoja ana mtizamo wake na maoni yake,ni muhimu, basi ni vyema kila mmoja apewe nafasi hiyo, kwa ajili ya katiba yake hiyo, lakini kwa vile Watanzania tupo wengi, itakuwa ni vigumu kwa kila mmoja kusema lake na lisikilizwe, ndio maana wakachaguliwa hao wawakilishi, wakiwa na kianzio cha rasimu ambayo imetokana na maoni ya wananchi, ...hicho ni kianzio, na ni msingi mnzuri wa kuboresha katiba yetu.

Sasa swali la kuuliza hapo, hao wawakilishi walioteuliwa wanawakilisha vyama vyao au wananchi? Jibu lipo wazi kuwa wanawakilisha wananchi, sasa vyama na itikadi za vyama zinatoka wapi?

Kama wao ni wawakilisha wa wananchi basi tunawaomba wavue magamba yao ya uwakilishi wa vyama, na hilo lingelifanyika mapema kwa kula kiapo kuwa hapo sio sehemu ya misimamo ya vyama vyao, au itikiadi zao binafsi hapo ni sehemu ya kutengeneza kitu kwa ajili ya masilahi ya taifa. Leo wapo kwenye chama hicho wanachokitikadia, kesho wanaweza wakawa kwenye chama kingine, lakini taifa lipo pale pale, katiba ipo pale pale...

Sasa kwa maoni yangu, ni kweli kuna mambo magumu sana katika kuiboresha hiyo katiba, hilo tulielewe wote, na maamuzi yake ni magumu pia, yanagusa mambo nyeti. Kwa mfano hilo la Muungano, ni nyeti kwani linagusa utaifa , najua kuna maswala mengine nyeti yanakuja kama ya imani za kidini nk, haya ni mambo yanayotakiwa umakini na busara ya hali ya juu ikiwemo kuvumiliana, ili tukwepe manung'uniko, migongano isiyo na tija. Ili iwe sehemu ya chachu za maendeleo, amani na mshikamano. 

Kwa hayo mimi niliona kama inafikia mahali kunakuwa na ugumu kupitiliza na ili kuokoa muda, hayo maswala magumu kwanza yawekwe pembeni, tuendelee na vipengele vingine, ambavyo havina ubishani wa makundi. Nina imani, kwa vile wote waliochaguliwa hapo wana busara zao na hekima, baada ya kuendelea mbele kwa mjadala wa vipengele vingine, wajumbe watakuwa wamejenga uzoefu fulani, wa kuvumiliana, na kujiona wao ni kitu kimoja, na hapo watakuwa wameweka utaifa wao mbele, hata wakivirudia vile vipengele vigumu, huenda kukawa na suluhu fulani la pamoja.

Mimi nina wasiwasi kuwa tunaweza tukapoteza muda kwa mambo machache na huenda yakakimbilia kutugawa mapema na hata kujenga chuki, ...japokuwa mjadaal kama huo ni  muhimu sana, lakini tuangalie mbali zaidi, tuangalie muda, gharama, na hamasa za ushawishi kwa wananchi ambao unaanza kujengwa kutoka kwa wanasiasa kwa kuleta mitizamo yao ya makundi tofauti, hatuoni kuwa hii ni hatari kwa  utaifa. Taifa hujengwa na makabila dini, rangi na watu tofauti tofauti, ndio maana tunaishi pamoja, tunavumilia,sasa hizo hisia nyingine za nyoyoni tusizitoe kwa sasa, hazina mantiki ya kitaifa...

Jamani wanasiasa, tusianze kutoa hoja za kuonyesha hisia zetu za ndani, zenye chuki, tuwe makini kwa hilo. Nashangaa  kama viongozi wa siasa wanarudi kwenye makundi yao mbali mbali kujenga hadhira, na hamasa fulani, ili hoja zao zionekane zina msingi, hatuoni tunaanza kuwagawa wananchi. Kwa hivi sasa kwa nia njema ya katiba, itikadi zetu tuzipumzishe, tuwe na wimbo mmoja wa utaifa.

Mpaka hapo najiuliza, kama wanasiasa wanataka kuliinglia bunge la katiba, hao wawakilishi wetu wana maana gani, je hiyo ndio katiba ya pamoja tunayoitaka au ni utashi wetu ..tuwaache wawikilishi wajadili, watoe hoja, wakatae, ili kuondoa mapungufu yaliyonekana katika katiba tuliyokuwa nayo...ila ni muhimu sana, mabo ya itikadi za kivyama yaondolewe, hapo sio sehemu ya kampeni za kisiasa...uongozi huo una muda wake, lakini utaifa upo pale pale....

Mimi naona hivi kama tulishakubali kuwa hao wajumbe waliopo bungeni ni wawakilishi wetu, hebu tuwaachie nafasi hiyo hao wawakilishi wetu, wajadili kwa mapana yao walumbane wanavyoweza, hata kusigishana ili tuone uzuri na ubaya wa kila kipengele, sisi wananchi tuliowatuma  yetu yawe ni macho na masikio, na hata ikiwezekana kuwaongezea hoja, tufanye hivyo kwa nia njema...

Mimi nina imani baada ya hapo kwa kuwa hao wajumbe wetu ni watu wenye ufahamu hekima na akili, watakaa pamoja na kuyaangalia hayo walioshindwana kihekima zaidi, waone mapungufu yake na kuona jinsi gani ya kuyaweka sawa. Tusibezane, tusikubali kutengana, hapo kama viongozi onyesheni uhodari wenu wa kusuluhishana, kuvumiliana na kujenga hoja zenye tija.

Kama itashindikiana zaidi, basi hivyo vipengele vigumu, virudishwe kwa wananchi, wananchi watavipigia kura, ili kila mmoja awajibike navyo, na hilo litaleta uzito zaidi kuwa kila mmoja kashiriki kikamlifu kwenye katiba yake, hakuna kulaumiana  tena,  kwani wengi wape.

Ni maoni yangu tu

2 comments :

Anonymous said...

Mambo ya siasa na mimi mbali mbali kabisa..tuendelee na kisa chetu m3

Anonymous said...

Awesome! Its in fact remarkable piece of writing, I have
got much clear idea regarding from this article.