Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 14, 2014

Gharama iliyo bora kwa mtoto ni kumsomeshaNimeona leo tutete kidogo, huku kisa chetu cha 'Baada ya Dhiki ni Faraja', kikiendelea . 

Ni muhimu tukaliongelea hili kama utangulizi, kwani huenda kisa hiki kikiisha tunaweza kuanza kisa kingine chenye mtizamo huo, japokuwa mengi mengine yatakuwepo. Ni swala zima la ndoa, mahusiano na mitihani yake.

‘Kwanini mnapenda kuongelea maswala haya ya mapenzi, na ndoa,...hakuna mengine ya kuongelea?’ nikaulizwa hili swali, na jibu lake ni rahisi tu kama tutakuwa na nia njema, na kuitizama asili ya jamii.

‘Je katika maisha yetu, swala la mapenzi na ndoa halipo? Ukweli ni kuwa lipo, na pamoja na mengine utaona hili linachukua nusu ya mambo yetu, kwani huko ndipo tulipotoka, na ndipo tunapoishi na ni maisha yetu ya kila siku, upende usipende, na mungu akijalia, huko ndipo tunapopata matunda yake.

‘Haya Matunda yake’ Ni muhimu sana katika jamii, katika taifa na dunia kwa ujumla ...na haya matunda yake yanategemeana na nyie wawili mlivyoweza kupata kizazi na kukilea vyema, nyie ndio mliosababisha au mtakaosababisha amani na upendo katika hii dunia, na kinyume chake pia, ndio maana umuhimu wa hili swala unapokuja.

‘Ulezi wa watoto’, ndio ngao , ndio nguo, ndio...swala muhimu, kwa ajili ya kujenga jamii yenye upendo na amani wa hii dunia, lakini ulezi huu utakuja vipi kama hakuna upendo kati ya wawili walioweza kupata hawa watoto, utakuta unarudi kule kule, kwenye swala zima la kujadili mapenzi na ndoa.

‘Ili taifa liendelee ‘linahitaj watendaji wazuri, wenye sifa zote, kielimu, kimaadili na kiafya, hawa watendaji hawaji hivi hivi, ila wanatokana na familia, wanatokana na baba na mama, wanatokana na familia iliyojengwa kwa upendo na amani, je upendo na amani vinatoka wapi, kama sio kwenye mahusiano mema...Mnapoishi wawili mlijue hili, kuwa kama hampendani, kama mnanuniana, kama mnagombana, mnakuwa chanzo cha jamii mbaya.

Tusijidanganye kuwa hatuwezi kukaa bila kulijadili hili, ni kweli yapo mambo mengi ya kujadili ambayo ni changamoto za kimaisha, lakini haya mambo mengine, yawe ya kisiasa, kiuchumi, au kiutamaduni, ya kuleta maendeleo, yasingelikuwa ni tatizo, kama tungeliangalia hili, la msingi wa familia, wapi familia hii ilipotokea, inapotokea, na inatakiwa itokee, ili kujenga jamii iliyo bora.

Ni kwamba kama tungekuwa na msingi mzuri, wa jinsi gani kwanza ya kuchagua mume na mke bora, pili, watu hawa waishi vipi basi...na hapa unaweza kuchungulia nyuma, walivyofanya wazee wetu, utaona kuwa haya mengine yasingelikuwa ni tatizo...leo hii jamii, ambayo haijui misingi hii, inakaa na kujadili haki za kuona jinsia moja,hivi hii kweli ni haki ya binadamu, huo sio ugonjwa jamani, mbona tunamzihaki, bin-adamu...tunakwenda wapi. Haya ndio matokea yake, wa kulaumiwa ni nani...

Hapa kwa wenye hekima wataona kosa limetoka wapi, ni kuwa, nyanja hii ya chimbuko la familia kama msingi wa jamii, imeachwa kama ilivyo ijiendeshe yenyewe tu, kwani kama wanavyosema wengi ambao hawalioni hilo kwa mapana yake, eti ni swala la asili kwahiyo linajileta lenyewe,... na kwa msimamo huo ndio maana tumefika hapa tulipo,...Hatuangalii visa vya maadiko matakatifu, kuwa kwa hiyo kulitokea, gharika, hatujiuliza hii gharika ilitokana na nini,...hayo sasa tunayaona kama visa vya kitabuni. Tunajidanganya.

Mzazi bora ambaye anafahamu wajibu wake atamuelimisha mtoto wake, kwa gharama yoyote ile, kwani gharama kubwa iliyo njema kwa mtoto ni kumsomesha. Usipomgharamikia mtoto wako leo, ili aje kuwa na maisha bora ili aje kuwa kiongozi bora, unategemea nini, na gharama ya kumsomesha huanzia ndani kwenu, wewe na mwenzako, mnaishi vipi, vinginevyo, tuache iwe ya asili tu, ..ndio haya yanayotokea hii leo katika dunia yetu, kuwa tumeona gharama kubwa kwa mtoto ni kumnunulia gari, kumjenga jumba la kifahari,...kumnunulia laptop, sherehe za kuzaliwa za anasa kwa kushindana..

Sawa kwa wenye uwezo hatuwakatazi, ila tufanye kwa tahadhari, kwani vyote hivyo vina mitihani yake, kama huyu mtoto hajajengeka kielimu kimaadili, na kiitikadi, kwani mwisho wa siku hizo gharama za hivyo vitu vya anasa, haitakuwa na manufaa kwake, huyo mtoto atavitumia hivyo vitu kwa kuja kumuangamiza yeye mwenyewe huko baadaye na jamii haitakuwa na amani tena.

Swala la kujiuliza ni hapa ni hili, huyu mzazi bora anatoka wapi? Haya maadili mema yanatoka wapi, hiki kizazi bora kinatoka wapi, utajikuta unarudi kule kule kule kwenye asili, kwenye msingi wa familia, ambao unatokana na familia yenye upendo na amani. Na huo upendo na amani unatokana na wazazi walioishi kwa mapenzi na mahusiano mema ambayo yametokana na mume na mke mwema, waliolelewa na kuijua ndoa na muhusiano yake.

Kwa wazo hili la leo, blog yenu inawapa pole wale wote walikumbwa na mitihani ya kimaisha kama kuugua au kuuguliwa, kufiwa,kupoteza ajira, na mengineyo, na wale wote waliopo kwenye mitihani ya kindoa, kuitafuta ndoa, na kuipata lakini bado hakuna upendo ndani yake, na pia swala zima la miitihani ya maisha magumu. Yote haya ni sehemu ya maisha yetu, tusikate tamaa, tuzidi kuwajibika huku tukimuomba mungu, kwa kila mtu na imani yake,Imani ya dini ndio sabuni ya kuzisafisha nyoyo zetu ili ziwe na huruma na upendo.

Ahsanteni sana


Ni mimi: emu-three

No comments :