Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 11, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-24


Nilipogeuka tu nilikutana na mdomo wa bastola ukinitizama, ...bastola ni ndogo na mdomo wake ni mdogo tu, lakini kwa muda huo niliona kama natizama bomba..au mtutu wa bunduki,

Macho yakanitoka pima kwa woga, na nilitaka kupanua mdomo nipige ukelele, lakini sura ya yule jamaa ambaye kwa muda huo alikuwa akinitizama kwa uso uliojaa makunyazi, ya hasira chuki, macho yakiwa yamemuiva alipanua mdomo wake na kusema;

‘Nataka twende nikaonane na huyo malaya wako,,....’akasema

‘Ma-la-ya, wa-wa-ngu ni nani?’ nikauliza na mara yule jamaa akainua ila bastola kama anataka kunilenga akasema;

‘Tusitaniane....uninielewa namtaja nani, kwanza mbona wewe mtu mwenyewe ni kiozo, unaogopa kama vile hukuzoea hii kazi, wakati wewe ni jambazi, tapeli...mablackmailer..?’ akaniuliza.

‘Mi...mi nakuapia, sijawahi mimi io jambazi,.....na tafadhali ondoa hiyo batola mbele yangu, inaweza kunifyatukia....’nikasema huku nikiwa nimeshapiga magoti.

‘Inuka haraka twende huko ndani nimekuambia nakataka kuonana na huyo malaya wako, ...siamini kuwa huu mzigo alionipa umekamilika namfahamu sana huyo mwanamke, na kama asiponipa kila kitu, kinachonihusu mimi , naona ni bora nikafungwe kwa maujaji,...’akawa anaichezesha ile bastola nikamuona anatupia jicho kule getini, nahisi alikuwa na wasiwasi na huyo mlinzi asije akamuona.

‘Tusipoteze muda hapa, unafahamu nimehachoka na nyie, nimepoteza pesa nyingi kwa kuwapa nyie, kwa kazi gani mlionifanyia, ...sina raha na familia yangu ...siamini haijawahi kutokea hivi kabla, yaani huyu mwanamke ananizalilisha hivi, ...anataka nimpe shilingiu ngapi ndio anipe uhuru wangu ungelijua ni kiasi gani alivyoniumiza usingelidirriki kuwa naye...’akasema

‘Hata mimi sitaki....sipendi, lakini ...’nikasita.

‘Hata wewe hutaki nini..., wewe hujawahi kutumia pesa yangu kutoka kwa huyo mdada, anakulipa kwa kazi hii chafu, .....mimi sijui kama hupendi, hiyo lakini yako itakutokea puani, njaa zako zitakutokea puani, inuka twende...’akasema huku akiinua ile bastola kama anataka kuifyatua.

‘Sikiliza...tafadhali, mdada ni mgonjwa, ukiingia hivi ...utamtibua, ana matatizo ya akili, utampandisha hasira zake na ...na...atakuua..’nikasema nikijaribu karata nyingine, kwani nilijua kabisa kama ataingia hivi, mdada atabadilika, na sijui kama kutakuwa na usalama hapo....

‘Hahaha..unasema ataniua, hahaha, unafahamu mimi sasa siogopi kufa, ni heri kufa kuliko kuzalilika hivi, nimeshaamua kuwa leo iwe mwisho wa haya yote, nipo tayari kwa lolote lile...’akasema na mara simu yake ikaingia ujumbe, lakini hakutaka kuiangalai akasema;

‘Haya, inuka haraka twende ndani...’akanigonga kichwani na ule mtutu wa bastola na akilini nilijua ndio risasi imeshafyatuka na kugonga kichwa kwangu nikadondoka chini, jamaa akaniangalia huku katoa macho ya hasira, na mimi kwa haraka nikawa nimepitisha mkono wangu na kushika simu yangu, nikabonyeza kwa hisia, nikijua hapo nabonyeza namba mbili, namba mbili ni kwa bosi, ...ndivyo nilivyoegesha nikajua sasa ipo hewani.

‘Unafanya nini, hebu ....’akanishika, na kutoa mkono wangu mfukoni, akanikagua na kuiona ile simu, akaitoa na kubamiza chini..

‘Unataka kufanya nini.....’akanigonga na kitako cha ile bastola kichwani hadi nikahisi kichwa kinataka kupasuka,...

‘Nitakuua,..sina utani leo...’akasema na kuangalia getini, mlinzi sijui alikuwa wapi, maana kama angelikuwa makini angeliona hayo yanayotokea.

Jamaa akanishika shati kwa nyuma na kunisukuma nitembee mbele...

‘Haya twende huko ndani..’akasema.

Kwa haraka sasa nikiwa na wasiwasi kuwa jamaa anaweza kweli kuniua, nikasimama nikishika kichwa, kama kuna damu zinatoka, nikaona hakuna kitu, huku natetemeka, nikaanza kueleka ndani...

‘Usifikiri natania, ...leo ndio mwisho wa haya yote, kama huyo malaya anaumwa wazimu mimi ni wazimu zaidi yake, haya twende,...haraka....’akasema na mimi nikaanza kutembea kuelekea ndani huku bastola ikinigusa kichwani kwa nyuma.

******
Nyumbani kwa muheshimiwa, ikiwa ni asubuhi na mapema, mke wa mpokea ushuru wa magari, alikuwa kasimama huku akawa anangalia dirishani, akiongea na simu na ilionekana anaongelea jambo kubwa sana kwani alikuwa akiongea kwa jaziba na hata kiti alikiona ni cha moto, mara ake mara asimame, akasema;

‘Mna uhakika na hilo kuwa mume wangu kaonekana asubuhi na mapema akiingia kwenye nyumba , unasema anaishi mdada, msichana, mrembo,..mungu wangu, mna uhakika ni mwanamke gani huyo?’ akauliza.

‘Ohooo, ni kile kisichana,nakifahamu, ...mmh, nimeshamuelewa, nitaonana naye uso kwa uso, leo hii-hii, tena sasa hivi naeleekea huko...ataniambia ukweli ulivyo, ana nini huyu mume, kakosa nini kwangu, hapana haiwezekani,...sizani, nahisi kuna kitu,...’akawa anaongea huku kasimama dirishani mkono mmoja umeshika kichwa.

‘Ninachotaka hakikisheni mnakuwa hapo kuhakikisha akitoka mnamuona, na hakuna uwezekano wa mtu kuingia ndani,...vyovyote lakini hakikisheni hafahamu mtu mwingine yoyote, maana sitaki kashifa nyingine’ akasema.

‘ Ni mara ngapi kafika hapo, .....unasema ni zaidi ya mara mbili, ana kazi gani na huyo mwanamke...gari, ...kwanini mazungumzo hayo yafanyikie kwake...kwanini isiwe ofisini, huyo mwanamke ana mume, hana...ana mchumba, hawara....nataka kujua yote hayo..leo hii  ndio,..’akasema

‘Ok, nitakwenda huko huko, maana jinsi mume wangu alivyoondoka leo inaonekana kuna jambo kubwa anafuatilia, na hizo pesa nyingi hivyo anazipeleka wapi,...alkuambia ukamchukulie jana, na una uhakika anazo mkononi,....’akatulia kidogo.

‘Una uhakika gani, bahasha,..anyway,yeye ana pesa zake nyingi za kuchezea, hilo sina uhakika nalo, ila cha kujua kafuata nini kwa huyo mwanamke, kaondoka asubuhi sana, hata kabla sijaamuka....alipotoka hapa kwangu hakupitia sehemu nyingine, mna uhakika, ok,...?’ akawa anauliza na kuandika jambo kwenye kumbukumbu zake.

‘ Nahisi kuna jambo, ok, waambieni hao vijana wahakikishe wanapata ushahidi wa kutosha, sitaki uzushi, na kama hakuna kitu kama hicho, manafahamu ni kitu nitakachokifanya, mimi namwamimi sana mume wangu....ok, naelekea huko huko....’akasema na akatulia kusikiliza

‘Hapana hili swala haliwahusu polisi, kwanini polisi, ....kama tutawahusisha polisi itakuwa ni kashifa, hatuna uhakika kafuata jambo gani,na ni kitu gani kimefanyika...kutembea na bastola sio mara ya kwanza, hilo sio ajabu kwangu, huwa anajihamu kutokana na kazi yake...’akasema

‘Polisi wa nini....achana na mawazo hayo,...’akasema kwa hasira.

‘Basi nitayafahamu huko huko nikifika,....mimi mwenyewe ni polisi , najiamini...’akasema na kuanza kujiandaa kuondoka kuelekea huko alipoambiwa mume wake yupo

********
Wakati hayo yanaendelea nyumbani kwa muheshimiwa, baba mkwe, alikuwa mjini, alifika kwa shughuli zake, na alipomaliza akawa na hamu ya kwenda kwa mkwewe, lakini hakupata nafasi hiyo, hadi asubuhi ambapo alitakiwa kurudi nyumbani kwake,  akiwa usingizini asubuhi, akapigiwa simu;

‘Mhh, ni kitu gani asubuhi hii, ...unasema, hajaonekana nyumbani kwake, toka jana, yupo wapi, ...kwa mdada, oooh,...una maana yule msichana anayeitwa mdada, ...kweli anaumwa...., kama anaumwa ndio yeye akalale huko,..haiwezekani, ...’ akawa anajindaa huku kashika simu.

‘Yawezekana kwa vile ni mfanyakazi mwenzao, sawa,...lakini...ok, leo siwezi kuonana naye, maana naondoka asubuhi hii, ila.....nitapitia kwa huyo mdada kama anaumwa, sitakaa sana....sasa hivi naondoka...’akasema

 Akachukua viatu vyake na kuanza kuvaa...na mara simu ikalia tena, alipoangalia akaona ni mke wake...akasalimiana naye, halafu akasema;

‘Mimi ni mwanajeshi bwana, muda wote nimejiandaa, sasa hivi navaa viatu, kuoga, usitie shaka,...chai nitakunywa huko mbele kwa mbele, muda hautoshi, ....natakiwa kufika huko kabla ya saa nne, kukutana na wale watu...’akasema

‘Kuonana na huyo mkwe wenu...sijapata muda, kabisa...na hata hivyo, mimi kwa nafasi yangu sio mtu wa kuonana naye,....hajakuwa mkwe, japokuwa kafanya hayo aliyoyafanya, kuna watu wanamfuatilia, hilo ondoa shaka, kama ni kweli nitajua ...hawezi , akifanya hivyo nitahakikisha anaozea jela,..’akasema

‘Sawa baadaye...’akasema na kukata simu, na kabla hajachukua mkoba wake, simu yake ikaita tena, akaipokea, ....

‘Nani , mtoza ushuru wa magari, na yeye kaingia hapo, asubuhi hii, kuna nini, kazi za asubuhi hivi,...kuna jambo gani hapo, au huyo msichana kazidiwa, au ni mpenzi wake wa siri, ....unasema ni kawaida yake,...mmmh haiwezekani...’akatikisa kichwa kama kutokukubaliana.

‘Mke wake si yule muheshimiwa, ok, ok, ...sina haja na mambo yao, ..hayanihusu,...kwanini, ina maana kuna mgongano, una uhakika, ok, nimeanza kukupata kuwa mtoza ushuru, anamtaka mdada, na mkwe wangu pia inawezekana na yeye anamtaka au anatumiwa kwa jambo fulani,...’akatulia kusikiliza.

‘Hilo haliwezekani, tafuteni ushahidi sio majungu,..sitaki udaku, mimi ni mtu wa heshima zangu,...haiwezekani, lakini mimi umuhimu wangu ni huyo mkwe wangu anafanya nini hapo, kwanini alale usiku kucha hapo,...yah, ndio hivyo nataka kujua hilo hayo mengine hayanihusu, sitaki kuingilia kazi za watu...’akasema.

‘Ok, nitapitia hapo nihakikishe mwenyewe...mdada nilimpa kazi hiyo, ya kuangalia nyendo za huyo mkwe wangu, sizani kama anaweza kufanya hivyo, una uhakika...mbona hamkuniambia kwenye taarifa zenu, ushahidi, sasa mnao...?’ akauliza

‘Unasema mara nyingi wapo naye, huyo mkwe wngu na mdada,  labda mdada anafanya hivyo katika kumchunguza huyo mkwe wangu, namuaminia sana huyo msichana, ...una uhakika, analewa kupindukia, toka lini akawa mlevi..haiwezekani, ...kama ni hivyo..ooh, ni lazima nionane naye. ....’akatulia akisikiliza

‘Akifanya hivyo,nitamfunga, hawezi kuniharibia binti yangu afanye uchafu huo...unasema...ok, ok, naelekea huko huko....’akasema na kukata simu kwa hasira

‘Haiwezekani...tutaona huko huko...’akasema akijiandaa kuondoka.....

*******

Katika kituo kidogo cha polisi, mpelelezi maarufu anayefuatilia maswala ya biashara ya madawa ya kulevya na makosa ya jinai, alifika ofisini kwake asubuhi sana, na alifika hapo baada ya kuwasiliana na vijana wake wanaofuatilia kazi maalumu, akachukua faili la kesi hiyo, inayofanyiwa uchunguzi, na akawa analipitia, mara simu ikaita;

‘Ndio niambie,....asubuhi hii?, ...yupo kwa mdada!, ok, vijana wapo hapo tayari au sio?, ok, sitaki ajue.....je kijana wetu anaweza kuingia ndani,...hapana asifanye hivyo..., vitu vingine ni kinyume na kazi yetu, ila kama ni dharura, fanya uonavyo, ...ok, ok, kama mnahisi hivyo, kuwa inawezekana kukawa na biashara hiyo,...ajanye iwezekanavyo, ila awe muangalifu....ok....’akatulia akisikiliza

‘Unasema hii ni mara ya pili, ...ni pesa nyingi eeh,...kwani lile gari lilitokaje...kwahiyo hakuna uhakika wa moja kwa moja, je kumbukumbu za kazini zinonyesha vipi..kila kitu kipo sahihi, kwahiyo hizo ni dhana za kuzua, huenda hata kama kuna ukweli, lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja, ndio hivyo?,...unasema kuna mengine kama yapi, ...shinikizo!!?...ok, ?’ akauliza kwa mshangao

‘Nimekuelewa....hayo yanaanza kuja huku kwetu, na yanaweza kuleta athari kubwa,..inabidi hilo tulifanyie kazi, nitalifikisha kwa wahusika...’akasema

‘Hilo ....linawezekana, kuwa analazimishwa kutoa hizo pesa, kuziba kashifa, lakini kashifa kama ipi,..usaliti wa ndoa,...ok, ok,... unauhakika na hilo, ...udaku,...gazeti lipi hilo,achana nao hao, fanyeni yanayotuhusu,hayo mengine, nitawaambia wahusika... basi,yah, kama kweli hilo lipo, tunahitajika kupata ushahidi,...’akatulia halafu akasema

‘Hayo ya usaliti wa ndoa, kuwa yametumiwa kama chambo, mmmh, hayo ni maswala binafsi , hayana kigezo, ninaweza kusema kwa sisi hayatuhusu,yatatumika kama kweli yanaambatana na kesi yetu, unakwenda huko, ok, tutakutana, kwani hata mimi mwenyewe naelekea huko nitaonana nao, ....ok, and over...’akakata simu.

NB: Kazi imeanza, fichua fichua,...kashfa, udaku na rushwa. Je hilo litawezekana, kuna nini kipo nyuma ya haya yote, tukutane sehemu ijayo...


WAZO LA LEO: Mara nyingi aliyezoea kudhulumu, kutenda ubaya kwa watu ni jambo la kawaida, anaona ni ujanja, ni bahati yake...nk, ila yeye hapendi kufanyiwa hivyo,kudhulumiwa kwake inauma sana, atalia sana, kuwa anaonewa, vyovyote iwavyo tukumbuke kuwa ubaya hauna mwisho mwema, tenda utendavyo, lakini dhuluma itakurudia wewe mwenyewe, ipo siku itafika na wewe utapata jaza yake.

Ni mimi: emu-three

No comments :