Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, February 13, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-12


   Bosi aliporudi, kwanza alituita mimi na mdada kutaka kujua maelezo ya hizo hundi na majina ya hao wateja ambalo walilipwa hizo hundi bila vielelezo vya kutambulikana , na mimi nikatakiwa kuleta kumbukumbu zote, za hawo wateja, viambatishi vyake, ikiwemo ankara ya kuomba malipo na mkataba na hati nyinginezo.

Nilikwenda kwenye file la kuhifadhia stakabadhi za malipo, nikazitafuta hizo nyaraka lakini hazikuwepo, nihakikisha tena na tena, sikuziona na nilikuwa na uhakika kuwa niliziweka kwenye hilo file,...baada ya kutafuta tena na tena, nikakata tamaa, nikarudi kwa bosi na kumwambia;

‘Hizo kumbukumbu hazipo, stakabadhi za malipo na nyaraka zake...kwenye file, ...’nikasema nikiwa na wasiwasi.

‘Una maana gani kusema hazipo, ina maana zimechukulia na mtu, anazitumia labda, au ..mbona sikuelewi, kwanini hazipo kwenye file lake?’ akauliza bosi akiwa kanitolea macho ya mshangao.

‘Mimi nia uhakika niliziweka zote kweye file la malipo na jana tu, niliziona wakati uliponiambia nijaribu kuangalia ni watu gani hao tuliowalipa malipo bila ukamilifu wa viambatishi vyake..., lakini hivi sasa zisizioni, ina maana kuna mtu kazitoa kwenye file,....’nikasema

‘Anayehusika na hilo file ni nani?’ akaniuliza kama vile hajui, kwana anafahamu fika kuwa mimi ndiye mwenye dhamana na hilo file.

‘Ni mimi, ila watu wakihitajia rejea, huja kulichukua,na mara nyingi wanaangalia hapo hapo na kulirudisha hilo file, hawachukui nyaraka,  na sana sana anayelitumia mara nyingi ni Mdada...’nikasema nikikwepa kumuangalia. Mdada akakohoa kama kunipa onyo.

‘Kwa maana hiyo wenye mamlaka na hilo file, ni wewe kama mwenye lilihifadhi, hata hivyo mdada, anaweza kulitumia na kuchukua nyaraka hata bila yaw ewe kufahamu, na akazitumia na kuzirejesha, kama ilivyo mimi, mimi pia naweza kulichukua hilo file, kama nalihitaji, lakini ni lazima nikupe taarifa....kwahiyo mnaowajibika kwa hilo ni wewe na mdada?’ akauliza tena kama vile hafahamu huo utaratibu.

‘Ndio bosi....’nikasema lakini mdada alikaa kimiya.

‘Basi nyie wawili nitafutieni hizo kumbukumbu, nazihitajia haraka iwezakavyo...’akasema bosi na mimi nikamwangalia mdada, ambaye alikuwa kimiya, nikamuuliza;

‘Mdada umezichukua hizo nyaraka kwenye file?’ nikamuuliza na yeye akaniangalia kwa macho makali na kusema.

‘Kama ningezichukua ningelisema, na toka lini nikachukua file lako bila kukuambia,...’akasema na kuniangalia kwa macho makali, na mimi nikasema;

‘Bosi, mimi naona ajabu kabisa, maana jana tu zilikuwepo, na nilihakikisha kuwa zipo, kabla sijalirudisha hilo file sehemu yake, ...ni lazima kuna mtu kazichukua,...’nikasema.

‘Sasa ni nani....mtafuteni, mniletee hizo kumbukumbu, ni muhimu sana, maana kama wenyewe wakija kudai malipo yao, tutasemaje, kuwa tumezipoteza, na wakati hundi zilishakwenda kwao, wakazipeleka benki, lakini kukapatikana na hitilafu...’akasema bosi.

Sikujua kabisa nikamuulize nani, maana haijatokea mtu kuchukua file, bila kuniarifu, na kama mtu anahitaji kitu kwenye hilo file, ananiambia mimi nakitoa na kumtolea nakala, huwezi kuchukua nyaraka yoyote humo...sasa ni nani kachukua hizo nyaraka za malipo, ....nikawa najiuliza kichwani bila kupata jibu.

 Tukatoka kwenye ofisi ya bosi na kurudi ofisini kwangu na mdada, na mdada, akawa kimiya akiniangalia kwa makini, aliponiona nahangaika kuzitafuta akasema;

‘Hivi unaweza kutafuta shilingi iliyozama chooni...’akasema kama ananiuliza, nikageuka kumuangalia na yeye akageuka na kuanza kuondoka.

‘Mdada hebu niambie ukweli, umezichukua hizo nyaraka?’ nikamuuliza

‘Jibu unalo mwenyewe, na haina haja ya kuumiza kichwa, tumia akili yako, ...wewe ni mhasibu bwana, au ?’ akaniuliza akiniangalia kwa dharau.

‘Sijakuelewa...’nikasema na kumwangalia kwa macho yaliyojaa hasira.

‘Jamani, ...mhasibu unatia huruma....’akasema huku kashika shavu, na mwingina kama anashika kichwa, kama vile ananionea huruma, na aliponiona namwangalia wa hasira akaondoka, nikabakia nimeduwaa, 

Nilibaki peke yangu nikitafakari, nikijaribu kujiuliza ni nani kachukua hizo nyaraka, inawezekana kweli mdada,  sasa sijui kwa madhumuni gani, na wakati natafakari huku nikiendelea kutafuta, mara bosi akatokea,..akaniangalia kwa makini halafu akasema;

‘Una uhakika hizo nyaraka zipo huko unapozitafuta?’ akaniuliza

‘Kwakweli hapa nimechanganyikiwa , kwasababu mimi mwenyewe niliziweka, na nina uhakika zilikuwepo, ukiangalia katika mfululizo wa namba wa mpangilio, inaonekana kabisa  kuna mtu kaja kazitoa, na hakutoa kwa utaratibu, alivuta, unaona mabaki ya  karatasi, ya kuonyesha kuwa wakati anavuta zilichanika...’nikasema na bosi akaangalia na kugeuka, akasema;

‘Hilo ndilo lililofanya nikawafukuza wahasibu waliopita, sitaki lirudie tena, nimesimamisha malipo yoyote yanayokwenda benki ambayo hayana uhakiki wangu, ina maana kila hundi ikienda huko ni lazima wanipigie simu nihakiki, kuwa kweli anayelipwa ndiye mlengwa, na jana tu, nimepigiwa simu, kuwa kuna hundi imekwenda huko....’akatulia kidogo.

‘Hundi gani tena hiyo...?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Je zile hundi nilizosaini zikiwa hazina mlipwaji kwa ajili ay dharura, ulizitumia?’ akaniuliza na kunifanya nishituke, maana ile hundi aliyochukua mdada, hakunirudishia, nikasema;

‘Hapana..ila, kuna hundi alichukua mdada,alisema kuna malipo ya haraka yanatakiwa, nikamwambia kabla ya kulipa, ni lazima nipate hizo kumbukumbu zake, ...sizani kama kaipeleka benki...’nikasema

‘Sikuelewi hapo, ina maana alichukua hiyo hundi, ikiwa haijaandikiwa mlipwaji, nay eye ndiye aliyeandika ni nani anatakiwa kulipwa, au sio...nifafanulie vyema, ...?’ akauliza.

‘Ndio hivyo, kwani huyu muhusika, sikuwa namtambua, yeye ndiye anayemfahamu..’nikasema.

‘Hapana, hapo unaniambia kitu ambacho hakiingii akilini, toka lini mdada akaandika hundi yeye, ....je akiandika gharama ambazo sio kweli, je akiandika mtu ambaye hahusiki,...hilo ni kosa kubwa, sitaki kuliangalia kwa nia mbaya, lakini nataka wewe mwenyewe ulihakiki, na uniambie ukweli kwanini haya yametokea, kwani nahisi yana maingiliano na kupotea kwa hizo kumbukumbu, sina uhakika na hao watu waliotakiwa kulipwa...ila nahisi kuna kitu kisocho cha kawaida kimefanyika...’akasema akiniangalia kwa makini.

‘Bosi kwani mdada hatumuamini?’ nikamuuliza na yeye akaniangalia kwa makini na kusema.

‘Sitaki nikufundishe uwajibikaji wa kazi yako,...nafahamu unafahamu taratibu na kanuni za kazi zako, je hilo lililofanyika ndio utaratibu wa kazi zako?’ akaniuliza.

‘Kwakweli, hilo limetokea bila kutarajia, niseme ukweli bosi, mdada alikuja na mambo mengi yaliyonichanganya kichwa, na hata sijui aliichukua vipi hiyo hundi, nilikuja kugundua haipo, na nilipomuuliza ndio akanipa maelezo hayo....’nikasema na bosi akaniangalia kwa mshangao.

‘Mhasibu, upo makini na kazi yako kweli, je kama nikiondoka ndivyo utakavyokuwa unafanya kazi hivyo, huoni utaleta hasara kubwa kwenye kampuni, sitaki nichukue hatua yoyote kabla sijalifanyia hili swala uchunguzi....’akasema huku akiniangalia machoni.

‘Sitaki hayo yaliyotokea huko nyuma yajirudie tena, ....sasa nakuambia hivi nataka wewe mwenyewe, ufanye utafiti, kama kweli hujui ukweli wa hayo yote, ni nani hao watu waliotakiwa kulipwa, pili hizo kumbukumbu zimeenda wapi, na hiyo hundi iliyokwenda hivi karibuni alitakiwa kulipwa nani, na uje na maelezo yanayojitosheleza kama mhasibu wa kampuni, maana mimi nafanya uchunguzi wangu pia..kesho wewe na mdada tutakuwa na kikao.’akasema.

‘Sawa bosi....’nikasema huku nikihisi kichwa kikianza kuuma, hadi nikakishika, nikainama kwenye meza na kutulia kwa muda, sikujua kuwa bosi bado yupo mlangoni ananitizama, nilipoinua kichwa nikamuona ananiangalia, yeye hakusema kitu akaondoka.

*********
 ‘Nimekuita tuendelee na kisa chetu, natumai unalifanyia kazi hilo swala la malipo na hizo kumbukumbu zilizopotea...hilo ni jukumu lako na ni dhamana yako, ukumbuke kuwa dhamana ni deni, ...’akasema na mimi nikawa kimiya

‘Ama kama kuna kitu kinachoendelea hapa, na unahitajia msaada wangu, nieleze, ili isije nikagundua mwenyewe, halafu ndio ukaanza kujitetea, sitakusikiliza, na sitasita kuchukua hatua za kisheria, ...sasa hivi nataka kampuni hii ilewe vyema taratibu za kazi, na kanuni za kazi, na kila mmoja awajibike kwenye nafasi yake....’akasema.

‘Wewe ni mhasibu, hutakiwi mtu akuingilie kwenye kazi yako, unaona hata mimi sipendi kukuingilia kwenye mamlaka yako, japokuwa mimi ni bosi wako, sijawahi kuja kukushurutisha jambo ulifanye, huwa nakuuliza na tunashauriana, sasa iweje, mtu mwingine aje akushurutishe, au achukua majukumu yako, bila ya rizaa yako, ni nani huyo yupo juu ya sheria na kanuni za kampuni,....’akawa ananiuliza.
‘Wewe na mdada, mna lenu jambo, na usipokuwa makini na huyo msichana, utajikuta, unaingia matatizoni, ...nakuona sasa hivi unahangaika na maumivu ya kichwa, je ulishafanay utafiti ni kwanini sasa hivi unaumwa sana na kichwa...huoni kuwa hayo maumivi ni kutokana na msongo wa mawazo, je hayo mawazo yanasababishwa na nini hasa..’akasema kama ananiuliza.

‘Sikiliza mhasibu, usipende kabisa mtu akakuingilia katika maisha yako,na hasa hasa aktika fani yako, akawa ndiye usukani wa maisha yako, na fani yako, maana kila mtu anafanya jambo kwa masilahi yake, na wengina wanachojali ni masilahi bila kujali atahari zake kwa upande wako, ...’akasema

‘Usiwe kama bendera fuata upepo, utajikuta mwenzako ananeemeka wewe unaumia, usikubali kabisa kuwa hivyo...’akazidi kunisisitizia kama vila anafahamu kuwa mdada ndiye nyuma ya hayo yote.

‘Nina muda kidogo, ngoja nikusimulie kisa cha maisha yangu, ili upate muda wa kuendelea na kazi yako, kwani kesho ni muhimu sana, nipate taarifa kamili ya hilo tukio , na nataka uniambie ukweli...ukweli na kutenda haki, ndio njia pekee itakayokusaidia katika maisha yako...’akasema.

******
Katika kisa cha maisha yangu tuliishia pale tulipofika kwa shemeji, ndugu wa mume wangu, na hapo tukapata taarifa kuwa mama mkwe hanitaki, na haitambui ndoa yangu na mtoto wake,..... je kiliendelea nini, hebu tuanzie hapo...

‘Kwani kuna nini kinachoendelea kwanini mama hanitaki mimi?’ niamuuliza mume wangu na mume wangu alionekana hataki kunieleza ukweli akasema;

‘Usiwe na wasiwasi ni maswala madogo tu tutayamaliza...’akasema, lakini kwa tetezi nilizozisikia, wakiongea, ni kuwa mama mkwe alikuwa hanitaki, eti yeye hakutaka mimi niolewe kabisa na mtoto wake,sikuelewa ni kwanini! 

Niliposikia wakiongea watu humo ndani japokuwa haikuwa rasimi nilihisi kama vile damu yangu ina mkosi. Moyoni niliumia sana, pale nilipokuwa peke yangu, niliinama na bila kujijua nikaona machozi yakinitoka kwa mfulululizo. Nilijuta kwanini sikutilia mkazo ule msimamo wangu wa kukataa kuolewa, lakini hilo lilishapita siwezi kujilaumu tena.

Nikajikuta nawaza huku nalia, kwanini mimi maisha yangu yawe hivi, na hata siku muhimu ya ndoa naianza kwa mkosi, ina maana mimi nina makosa gani, katika hii dunia, ina maana hata huko nilipokuwa nikiona ndio matumaini yangu mapya, haitakuwa hivyo tena, kama mama mkwe hanitaki mimi nitakuwa mgeni wa nani.

‘Mume wangu ina maana tunakwenda kuishi na mama huyo ambaye hanitaki?’ nikamuuliza.

‘Tunaenda kuishi huko, huko, ..usijali...ngoja tuongee na wanandugu tuone tutaklifanya vipi hili jambo..’akasema. Na mimi niligundua jambo, mume wangu sio muongeaji sana kama alivyo ndugu yake, na anaonyesha kuwa hataweza kuwa na msimamo wake kama alivyo ndugu yake. Ndugu yake, alionekana muongeaji na mwenye msimamo.
‘Kama ni hivi nitakwenda kuishije huko?’ nikajiuliza bila kupata jibu.

Baadaye wanandugu wakaitana tena, kwani muda ulikuwa unakwenda na taarifa kutoka huko nyumbani kwako, zinasema mama mkwe hataki kabisa kusikia lolote , kashikilia msiamamo wake. Kwa vile tulitakiwa kuondoka hapo siku hiyo, wanandugu wakaona wakutane walijadili ili kutafutwe njia ya kulimaliza, kwani mume wangu, anaishi na familia yao, akiwemo huyo mama mkwe asiyenitaka.

Wakati wanaongea, japokuwa sikuwemo kwenye hicho kikao, lakini niliweza kusikia sauti zao, wakijadiliana, kuna mmoja akatoa hoja, kuwa kwa vile mama mkwe hanitaki, basi kwa muda, nitafutiwe sehemu nyingine ya kukaa, hadi hapo watakapolimaliza hilo tatizo,

‘Mhh, haiwezekani....’nikajikuta naguna na kulikata hilo wazo kimoyo moyo.

‘Ina maana kweli mtu ndio umeolewa, unatengana naye, kila mmoja akikaa sehemu tofauti, kwasababu ya mama mkwe...’nikajiuliza

Wazo la huyo likajadiliwa kukawa na wengi wanalipinga, na muwakilishi wangu akaingia ndani pale nilipo, kwani kuna mtu alinisindikiza ambaye atarudia hapo na kunifahamisha jinsi kikao kinavyoendelea, akasema anawasiliana na wazazi wangu, kama inawezekan nirudi na yeye

‘Kweli hilo ni wazo zuri, kama hawa watu hawajajipanga nikakae nyumbani, wakiwa tayari ndio waje kunichukua...’nikasema

‘Sawa ngoja niongee na wazazi wako...’akasema na kuwapigia simu wazazi wangulakini

Wazazi wangu wakalipinga hilo wazo, wakasema, mimi sasa sio mtu wao, nahitajika kuwa pamoja na familia ya mume wangu, na hilo la kusema mimi nikaishi sehemu nyingine, wao hawaliafiki, hata hivyo, wao hawawezi kuingilia mambo ya huko, hayo ni mambo yangu na mume wangu, yule muwakilishi wangu akasema;

‘Mimi niliona wazo jema, mimi nirudi na bibi harusi huko nyumbani, tuwaache hawa watu wakamalizane na mama yao, wakiwa tayari ndio wamchukue mke wao...’ akasema

‘Haiwezekani hilo halipo, na usije ukalitoa hilo wazo kwenye kikao chao, wao wanajua ni jinsi gani ya kulitatua, hawajatuomba msaada, huyo ni mtu wao....’wakasema wazazi wangu.

‘Hamuoni kuwa mtoto wetu ataenda kuishi maisha mugumu huko anapokwenda?’ akauliza huyo msindikizaji wangu.

‘Hayo ni kawaida tu, na ni maswala ya muda, yatakwishi, yeye anatakiwa kumtii mume wake, na familia hiyo....’wakasema wazazi wangu, na huyo msindikizaji akawa ahana jinsi,akaniambia jinsi wazazi wangu walivyosema, na mimi nikasema;

‘Ina maana kweli wazazi wangu hawanitaki tena, ni kama walinitupa, wameniozesha kwa nguvu kwa mume ambaye sikuwa na mapenzi ya yeye, na haya yanatokea, bado ahwataki kunisaidia...’nikasema kumueleza huyo jamaa yetu aliyenisindikiza.

‘Sio hivyo, sio kwamba hawakutaki, hayo ni maswala ya ndoa, yana taratibu zake ukishaolewa, unakuwa sio mtu wa familia yenu tena, wewe ni mtu wa familia ya mume wako,...wazazi wako hawatakiwi kuingilia mambo yenu,mpaka waombwe kufanya hivyo...’akasema.

‘Sasa mimi wananiweka katika hali gani?’ nikauliza

‘Cha muhimu wewe ni kusubiria tu, watakubaliano jinsi gani ya kufanya na wewe huna hiari, watakavyosema wao, ndivyo utakavyofuata...’akaniambia.

Kwa hali kama hiyo mimi nikajiona sina raha, nikajiona mpweke, wazazi wangu hawataki kunipokea, huku kwa mume mama mkwe hanitaki. Nikawa sina jinsi ila kusubiria yatakavyoamuliwa. Baada ya majadiliano marefu wakamua kuwa twende huko huko kwa mama mkwe.

‘Atakubali tu, maana ndoa imeshafanyika, hana uwezo wa kuivunja...’akasema shemeji.

‘Je kama akikataa kabisa tutafanya nini,...?’ akauliza mume wangu.

‘Hawezi kukataa, ni hasira tu, mama ni mama tu, atafikia muda atakubaliana tu, unachotakiwa wewe ni kuwa na msimamo na ndoa yako...’akasema shemeji.

 Mimi nikiwa ndani, nikawa namkabidhi mungu, maana sikuwa na la kufanya, kama nyumbani hawanitaki nitakwenda wapi, na kama huko kwa mume sitakiwi, ina maana mimi ni mtu wa kusubiria tu, ni kama mkiwa sina la kufanya,...nikatulia, na mara mume wangu akaja, na kuniambia;

‘Tunaondoka usiku wa leo, jiandae...’akasema

‘Na mama mkwe keshakubali....?’ nikauliza.

‘Atakubali tu, ni hasira za muda, ....mambo yote tutayajua huko tukifika...’akasema.

‘Kama hanitaki kwanini ulikimbilia kunioa?’ nikamuuliza na yeye akaniangalia kwa muda baadaye akasema;

‘Kwani yeye ndiye aliyekuoa au ni mimi...unachotakiwa kunisikiliza ni mimi, ....’akasema.

‘Sawa lakini mama ni mama, unatakiwa umsikilize mama yako...’nikasema

‘Kwahiyo nikuache, ndivyo unavyotaka...?’ akaniuliza

‘Mimi ninachojiuliza ni kwanini, kama mama yako alikuwa hanitaki ukakimbila kuja kushinikiza unioe?’ nikamuuliza

‘Nimeshakuambia kuwa mama sio anayekuoa, mimi ndiye niliyekuoa, hilo linatosha mengina tuachie sisi wenyewe, tutajua jinsi gani ya kuongea na mama...’akasema na kuonyesha kukerwa na kauli yangu hiyo.

Tukajiandaa kwa safari hiyo ambayo ilifanyika usiku, na ilipofika usiku tukaondoka kwenda kukutana na mama mkwe asiyenitaka.


WAZO LA LEO: Tusikate tamaa na maisha pale tunapokutana na mitihani mbali mbali, cha muhimu ni kuangalia kuwa tumesimamia kwenye ukweli na haki.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Outcomes will certainly differ depending upon the individual.
Lots of see results within the very first week, and most will find their garments fitting better by the end of the first month.



Also visit my website: garcinia cambogia extract (imobileface.com)